3 John
3 John 1
3 John 1:1-4
Kwa cheo gani mwandishi Yohana anajitambulisha mwenyewe katika barua hii?
Yohana anajitambulisha mwenyewe kama mzee.
Ni uhusiano gano gani aliokuwa nao Yohana kwa Gayo, anayepokea barua hii?
Yohana anampenda Gayo katika kweli.
Kwa ajili ipi Yohana anaomba kumhusu Gayo?
Yohana anaomba kwamba Gayo afanikiwe katika mambo yote na kuwa na afya, kama vile roho yake ifanikiwavyo.
Nini furaha kuu ya Yohana?
Furaha kuu ya Yohana ni kusikia kwamba watoto wake wanatembea katika kweli.
3 John 1:5-8
Nani aliyekaribishwa na Gayo na kisha kumtuma katika safari yake?
Gayo alimkaribisha na kisha kumtuma katika safari ya baadhi ya wale waliokuwa wakienda kwa ajili ya Jina.
Kwanini Yohana anawaambia waumini kuwakaribisha ndugu kama vile hawa?
Yohana anasema waumini waweza kuwakaribishaili waweze kuwa watendakazi wenzao kwa ajili ya kweli.
3 John 1:9-10
Diotrofe anapenda nini?
Diotrofe anapenda kuwa wa kwanza miongoni mwa kusanyiko.
Mtazamo wa Diotrofe kwa Yohana ukoje?
Diotrofe hakumpokea Yohana
Yohana atafanya nini akimtembelea Gayo na kanisa lake?
Yohana akija atakumbuka matendo yake maovu.
Diotrofe anafanya nini kwa ndugu wanaoendelea na Jina?
Diotrofe hataki kuwapokea hao ndugu.
Diotrofe anafanya nini kwa wale wanaowapokea ndugu wanaoendelea na Jina?
Diotrofe anawakataza wasiwapokee hao ndugu, na anawafukuza watoke kwenye kusanyiko.
3 John 1:11-12
Yohana anamwambia Gayo jambo la kuiga?
Yohana anamwambia Gayo aige wema.
3 John 1:13-15
Yohana anatumaini kufanya kini wakati ujao?
Yohana anatumaini kuja na kuzungumza na Gayo uso kwa uso.