Kiswahili: translationQuestions

Updated ? hours ago # views See on DCS Draft Material

Job

Job 1

Job 1:1-3

Jinsi gani tabia za Ayubu zimeelezewa?

Yeye alikuwa mwenye haki na mkamilifu, na aliyemcha Mungu na kuachana na uovu.

Job 1:4-5

Je, baada ya wana wa kiume wa Ayubu kufanya karamu na kaka zao na dada zao katika nyumba zao, Ayubu alifanya nini?

Ayubu aliwaweka wakfu kwa Mungu, na kutoa sadaka ya kuteketezwa, na kuwaombea.

Job 1:6-8

Kwa nini BWANA alimuuliza Shetani umemwangalia Ayubu?

Kwa kuwa hapana mmoja aliye kama Ayubu duniani, mtu mwenye haki na mkamilifu, mmoja aliye na hofu ya Mungu, na kuepukana na uovu.

Job 1:9-12

Shetani anasema jinsi gani BWANA amemkinga Ayubu?

Yeye amemzungushia Ayubu uzio, kuzunguka nyumba yake, na kuzunguka vitu vyote alivyo navyo kila upande.

Je, Shetani anafikiri nini kita sababisha Ayubu amkane Mungu?

Akamwambia Ayubu tafadhali mkane Mungu ni Mungu aliyeangamiza mali yako yote.

Je, BWANA alimpa Shetani ruhusa ya kufanya nini?

BWANA alimpa Shetani ruhusa ya kuchukua vyote alivyonavyo Ayubu, isipokuwa uhai wake.

Job 1:13-15

Mjumbe alimwambia nini Ayubu walichomfanyia Waseba?

Wamewaua watumishi wote wa Ayubu shambani na kuwachukua maksai na punda wote.

Job 1:16-17

Mjumbe wa pili alimwambia nini Ayubu kilichotokea kwa kondoo zake?

Moto wa Mungu umeanguka toka mbinguni na kuwateketeza wao pamoja na watumishi.

Mjumbe wa tatu alimwambia nini Ayubu kilichotendeka kwa ngamia zake?

Makundi matatu ya wanyang'anyi yamekuja na kuwashambulia wao. Wamewaiba ngamia wote na kuwaua wanaume wote ambao walikuwa wakiwatunza.

Job 1:18-19

Habari ipi ambayo mjumbe wa nne alimletea Ayubu?

Watoto wa kiume na binti za Ayubu walikuwa wakisherehekea nyumbani mwa ndugu yao ambapo upepo mkubwa ulitokea na kuipiga nyumba, ambayo imewaangukia na kuwaua.

Job 1:20-22

Ayubu alifanya nini baada ya kupata taarifa hizi?

Ayubu alirarua joho lake, akanyoa kichwa chake, akalala chini kifudifudi, na kumwabudu Mungu.

Ayubu alisema nini kuhusu hali yake baada ya matukio haya?

Alisema yeye alitoka uchi tumboni mwa mama yake, na atarudi akiwa uchi.

Je ni nini anachosema Ayubu kwamba BWANA amefanya kwake?

BWANA alitoa, na BWANA ametwaa.

Jinsi gani Ayubu alionesha kuwa yeye hakuwa mtu mpumbavu?

Ayubu hakutenda dhambi, wala hakumwazia Mungu kwa uovu.

Job 2

Job 2:1-2

Nani alikuja pamoja na wana wa Mungu wakati walipo jihudhurisha mbele za BWANA?

Shetani pia alikuja na kujihudhurisha yeye mwenyewe.

Nini Shetani alimwambia BWANA kile alichokuwa akikifanya?

Yeye alisema alikuwa akizunguka zunguka duniani, na kutembea huku na huko humo.

Job 2:3

Jinsi gani BWANA anasema kwamba Ayubu anaendelea kufanya baada ya mashambulizi ya Shetani?

Ayubu anashikamana na utimilifu wake.

Job 2:4-6

Shetani anataka kufanya nini sasa kwa Ayubu ili kwamba Ayubu amtukane Mungu?

Shetani anataka kuigusa mifupa ya Ayubu na mwili wake ili amdhuru.

Job 2:7-8

Jinsi gani Shetani ameudhuru mwili wa Ayubu?

Yeye amemdhuru Ayubu na majipu mabaya toka wayo wa mguu hadi utosini mwa kichwa chake.

Ayubu alifanya nini kuyakabiri maumivu ya mateso yake?

Yeye alichukua kipande cha kigae na kujikunia yeye mwenyewe akiwa ameketi chini majivuni.

Job 2:9-10

Mke wa Ayubu alitaka nini yeye afanye?

Mke wa Ayubu alitaka yeye amtukane Mungu nakufa.

Ni lawama gani Ayubu alizitoa kwa mke wake?

Yeye alimlaumu kwa kufikiri wao wagepata mema toka kwa Mungu lakini si mabaya.

Job 2:11

Rafiki watatu wa Ayubu walifanya nini waliposikia kilichomfika Ayubu?

Wao walifika kuomboleza naye na kumfariji.

Job 2:12-13

Jinsi gani marafiki watatu wa Ayubu walionesha huzuni yao walipomuona yeye?

Wao walipaza sauti zao na kulia, wakararua majoho yao, wakarusha mavumbi juu ya vichwa vyao, na kuketi chini kimya kwa siku saba usiku na mchana.

Job 3

Job 3:1-3

Ayubu anasema nini kuhusiana na siku aliyozaliwa?

Yeye anaichukia siku aliyozaliwa na kuomba kwamba ingepotea.

Job 3:4-5

Je, ni nini haja ya Ayubu juu ya siku aliyozalia?

Yeye anataka siku hiyo ishikwe na giza na kivuli cha mauti.

Job 3:6-10

Je, Ayubu anataka usiku alioshikiwa mimba ukamatwe na nini?

Ayubu anataka usiku huo ukamatwe na giza nene.

Job 3:11-12

Je, Ayubu alitamani nini kigelitokea wakati alipotoka kwenye tumbo la uzazi?

Yeye alitamani angelikufa na kuitoa roho yake.

Job 3:13-16

Je, nini Ayubu anasema angelikuwa anafanya sasa kama angelikufa wakati wa kuzaliwa?

Yeye angelikuwa amelala usingizi na kupumzika pamoja na wafalme na washauri wa dunia.

Job 3:17-19

Kutoka kwenye nini wafungwa na watumishi wamewekwa huru na kifo?

Mfungwa amewekwa huru kutoka kwa sauti ya msimamizi wa watumwa, na mtumishi kutoka kwa bwana wake.

Job 3:20-22

Kwa nani Ayubu anasema kwamba kifo hakitakuwepo?

Hakiwezi kumpata yule atamaniye kufa, na ambaye hukitafuta sana zaidi ya wale ambao hutafuta hazina iliyofichika.

Job 3:23-24

Jinsi gani Ayubu anaelezea kuugua kwake?

Kuugua kwake kumemiminika kama maji.

Job 3:25-26

Je, ni mambo gani ambayo Ayubu yalimtia hofu ambayo yamemfika?

Yeye haoni raha au utulivu, na hapati pumziko.

Job 4

Job 4:1-3

Je, ni mambo gani mema Elifazi anasema Ayubu aliyafanya kwa wengine?

Ayubu amewafunza wengi, na ameipa nguvu mikono dhaifu.

Job 4:4-6

Je, Elifazi anasema nini kuhusiana na imani ya Ayubu na tumaini wakati wa taabu?

Hofu ya Ayubu kwa Mungu ndiyo imani yake, na ukamilifu wa njia zake ni tumaini lake.

Job 4:7-9

Je, ni nani aliyeangamizwa na kuteketezwa kwa pumzi ya Mungu na hasira zake?

Wale walimao uovu na kupanda taabu hupotea na kuteketezwa.

Job 4:10-11

Jinsi gani Elifazi anazungumzia kuvunjika moyo?

Sauti ya simba mkali na meno ya simba wadogo yamevunjika.

Job 4:12-13

Jinsi gani Elifazi alipokea ujumbe fulani kisiri?

Alisikia mnong'ono sikioni mwake na kuona maono wakati wa usiku.

Job 4:14-15

Nini kilimpata Elifazi wakati alipopokea ujumbe?

Hofu na kutetemeka kilimpata.

Job 4:16-17

Je sauti ilisema nini kuhusu mtu wa kufa?

Iliuliza kama mtu wa kufa anaweza kuwa mwenye haki kuliko Mungu, na msafi zaidi kuliko muumba wake?

Job 4:18-21

Jinsi gani Elifazi amemuelezea watu wa kufa?

Wanaishi katika nyumba za udongo, ambazo msingi wake ni vumbi, na ambao husagika mapema kuliko nondo.

Job 5

Job 5:1-3

Je, ni nini Elifazi anasema kitatokea kwa mpumbavu na mtu mjinga?

Hasira huua mtu mpumbavu, na wivu huua mjinga.

Job 5:4-5

Je, nini kinatokea kwa watoto wa mtu mpumbavu katika lango la mji?

Wameangamia langoni mwa mji.

Job 5:6-7

Kwa kweli taabu inatoka wapi?

Mwanadamu hutengeneza taabu yake mwenyewe.

Job 5:8-10

Je Mungu hutoa nini juu ya nchi na mashambani?

Yeye hutoa mvua juu ya nchi na hupeleka maji mashambani.

Job 5:11-13

Je, Mungu huifanya nini mipango ya watu wenye hila?

Yeye huzuia mipango yao ili kwamba mikono yao isiweze kuendeleza njama zao.

Job 5:14-16

Je, Mungu humuokoa mhitaji na mtu masikini kutoka wapi?

Yeye huwaokoa watu masikini kutoka kwa makali ya upanga, na humuokoa mhitaji kutoka kwa mkono wa mtu mwenye nguvu.

Job 5:17-19

Kwa sababu gani mtu anafuraha ambaye hutiwa adabu na Mungu na kuongozwa?

Yeye anafuraha kwa sababu Mungu baada ya kumjeruhi, yeye huyafunga majeraha, na mikono yake huponya.

Job 5:20-22

Je ni wakati gani mtu ambaye ametiwa adabu na Mungu atafurahi?

Yeye atafurahi wakati wa uharibifu na njaa.

Job 5:23-25

Je, mtu ambaye amemtiwa adabu na Mungu ataona nini wakati atakapotembelea zizi la kondoo wake?

Yeye atakuta kwamba hakuna chochote kinachopungua.

Job 5:26-27

Je itachukua muda gani mtu ambaye ametiwa adabu na Mungu kuishi?

Yeye atafika kaburini kwake akiwa na umri mkubwa.

Job 6

Job 6:1-3

Jinsi gani Ayubu ameelezea maumivu yake makubwa na msiba wake mkubwa?

Maumivu yake makubwa na msiba wake mkubwa yangepimwa kwenye mizani, yangekuwa mazito kuliko mchanga wa baharini.

Job 6:4-6

Je Mwenyezi kwa mishale yake alimfanyia nini Ayubu?

Mishale yake ipo ndani ya Ayubu, na moyo wa Ayubu umelewa sumu

Je ni chakula gani Ayubu anasema hakina radha?

Yeye anasema ute mweupe wa yai hauna radha yoyote.

Job 6:7-9

Je ni ombi gani moja Ayubu ametamani sana kuruhusiwa na Mungu?

Yeye anataka Mungu amwangamize na kuyakata maisha yake.

Job 6:10-11

Je faraja ya Ayubu ni nini?

Faraja yake ni kwamba yeye hajayakana maneno yake Mtakatifu.

Job 6:12-13

Je, nini kimeondolewa toka kwa Ayubu?

Hekima imeondolewa mbali naye.

Job 6:14-17

Je, rafiki anatakiwa kuonyesha uaminifu kwa nani?

Rafiki anatakiwa kuonyesha uaminifu kwa mtu ambaye yu karibu kuzirai.

Jinsi gani Ayubu anawalinganisha ndugu zake na mkondo wa maji jangwani?

inapita mpaka pasipo kitu, wakati ikiyeyuka hutoweka, na kukiwa na joto huyeyuka..

Job 6:18-20

Je, nini hutokea kwenye misafara wakati wakitafuta maji katika mikondo hii?

Wao huzurura jangwani na kisha huangamia. Wao hudanganywa na kuvunjika moyo.

Job 6:21-23

Kwa nini rafiki zake Ayubu si kitu kwake?

Wao wameona hali yake ya kutisha na wakaogopa.

Job 6:24-25

Je Ayubu anasema yeye atafanya nini iwapo rafiki zake watamfundisha yeye?

Yeye ataishika amani yake.

Job 6:26-27

Je Ayubu anasema nini rafiki zake wanapanga kuyafanyia maneno yake?

Wanapanga kuyakataa maneno yake, na kuyachukulia kama upepo.

Job 6:28-30

Kwa nini Ayubu anasema rafiki zake wanatakiwa kurudi katika shutuma zao juu yake?

Sababu za Ayubu ni za haki.

Job 7

Job 7:1-3

Je Ayubu analinganisha na nini miezi yake ya mateso na taabu-zilizoujaza usiku?

Yeye anailinganisha na mtumwa atamaniye jioni, au mwajiriwa atafutaye ujira wake.

Job 7:4-5

Je mwili wa Ayubu umefunikwa na nini?

Minyoo na madonda yenye vumbi yameufunika mwili wake.

Job 7:6-7

Je ni picha gani Ayubu anaitumia kuelezea kasi ya siku zake?

Siku zake zinakimbia kuliko chombo cha kufumia.

Job 7:8-10

Je, Ayubu anamlinganisha na nini mtu ambaye anaelekea Sheoli?

Yeye ni kama wingu liishavyo na kutoweka.

Job 7:11-12

Je, ni kwa namna gani Ayubu ataongea na kunung'unika?

Yeye atasema juu ya maumivu makubwa ya roho yake na kunung'unika juu ya uchungu wa nafsi yake.

Job 7:13-15

Je, ni nini Ayubu alichofanyiwa yeye na Mungu wakati akiwa amelala kitandani?

Alitishwa na Mungu kwa ndoto na kutiwa hofu kwa maono.

Job 7:16-18

Kwa nini Ayubu anataka Mungu amuache peke yake?

Ayubu alisema siku zake hazifai.

Job 7:19-20

Je Ayubu ana muomba nini Mungu kutokumsumbua kiasi cha kuweza kutenda?

Yeye anaomba kuachwa peke yake kiasi cha kutosha kumeza mate yake mwenyewe.

Job 7:21

Je nini Ayubu anafikiri Mungu hatafanya?

Ayubu anafikiri Mungu hatamsamehe makosa yake na kumuondolea uovu wake.

Job 8

Job 8:1-3

Je Bildadi aliyalinganisha na nini maneno ya kinywa cha Ayubu?

Aliyalinganisha na upepo wenye nguvu.

Job 8:4-5

Jinsi gani Bildadi anasema anafahamu kwamba watoto wa Ayubu wametenda dhambi?

Anasema analifahamu hili kwa sababu Mungu amewatia mkononi watoto wa Ayubu kwa makosa yao.

Job 8:6-7

Jinsi gani Bildadi alisema kwamba Mungu atambariki Ayubu kama atakuwa msafi na mkamilifu?

Atampa Ayubu zawadi ya makazi ambayo ni haki yake kweli.

Job 8:8-10

Je Bildadi analinganisha na nini siku zetu duniani?

Anasema ni kivuli.

Job 8:11-12

Je mafunjo na matete yanahitaji nini ili yaweze kumea?

Mafunjo yanahitaji matope, na matete yanahitaji maji kumea.

Job 8:13-15

Je Bildadi analinganisha na nini matumaini ya atu waovu?

Matumaini yao ni kama utando wa buibui.

Job 8:16-18

Je mizizi inafanya nini hata iwe mfano wa mtu ambaye humsahau Mungu?

Mizizi yake hujifunga funga katika rundo la mawe na kutafuta sehemu nzuri miongoni mwa mawe.

Job 8:19-20

Jinsi gani Mungu humtendea tofauti mtu asiye na kosa na mtenda maovu?

Yeye hatamtupa mtu asiye na kosa, lakini hatashika mkono wa mtenda maovu.

Job 8:21-22

Je, kwa kutumia nini Mungu atakijaza kinywa na mdomo wa mtu asiye na kosa?

Yeye atakijaza kinywa chake na kicheko na mdomo wake na shangwe.

Job 9

Job 9:1-3

Je, nini kitatokea mtu akijaribu kuhojiana na Mungu?

Mtu hatamjibu Mungu mara moja katika elfu zaidi.

Job 9:4-6

Je, Mungu ataifanyia nini milima wakati akiwa na hasira?

Yeye huiondoa milima bila onyo na kuipindua.

Job 9:7-9

Je, Mungu hutuliza nini?

Yeye kupunguza nguvu na kutuliza mawimbi ya bahari.

Job 9:10-12

Je, Ayubu anamuona Mungu wakati akipita?

Mungu yupamoja naye na Ayubu hawezi kumuona au kumtambua.

Job 9:13-15

Hata kama Ayubu alikuwa mwenye haki, jinsi gani anatakiwa kumwambia Mungu?

Ayubu asingeweza kumjibu, lakini angeweza kuomba msamaha tu.

Job 9:16-18

Kwa nini Ayubu ana amini Mungu ameyaongeza majeraha yake?

Ayubu anaamini Mungu ameyaongeza majeraha yake pasipo sababu.

Job 9:19-20

Je inawezekana Ayubu kuwa mwenye haki na mkamilifu?

Hapana, hata kama, kinywa chake kitamhukumu na kumshuhudia kuwa ni muovu.

Job 9:21-24

Je Ayubu anafikiri Mungu atawatendea wenye haki na watu waovu tofauti?

Anasema Mungu huwaangamiza wote pamoja watu wakamilifu na watu waovu.

Job 9:25-26

Je, ni mambo gani matatu Ayubu anayalinganisha na kasi ya siku zake?

Zinapita haraka kuliko mjumbe akimbiae, zina kasi kama mashua zilizotengenezwa kwa mafunjo, na zina kasi kama tai ashukae chini kwa kasi.

Job 9:27-31

Kwa nini Ayubu anasema itakuwa kazi bure kusahau manung'uniko yake?

Mungu hata mhesabu kuwa hana hatia, lakini Ayubu atahukumiwa.

Job 9:32-33

Je, Ayubu ana maanisha nini anaposema kwamba hakuna hakimu atakayeweza kuufanya?

Hakuna hakimu awezaye kuweka mkono wake juu ya Ayubu na Mungu.

Job 9:34-35

Je Ayubu ana maanisha nini anaposema hakuna hakimu mwingine awezaye kufanya?

Hakuna hakimu mwingine ambaye anaweza kuchukua fimbo ya Mungu toka kwa Ayubu, au kuzuia kitisho cha Mungu kisimtishe Ayubu.

Job 10

Job 10:1-3

Kwa nini Ayubu anataka Mungu amuonyeshe, badala ya kumhukumu yeye tu?

Anataka Mungu amuonyeshe Ayubu sababu za yeye kumshutumu.

Job 10:4-7

Je ni macho ya aina gani Ayubu anamuuliza Mungu kama anayo?

Ayubu anamuuliza yeye kama ana macho ya mwili na anaona kama mtu aonavyo.

Je Ayubu anasema nini kwamba Mungu anadadisi na kuchunguza tena?

Mungu anadadisi tena uovu wa Ayubu na kuchunguza tena dhambi zake.

Job 10:8-9

Je mikono ya Mungu imefanya nini kwa Ayubu?

Imemfinyanga na kumuumba Ayubu, kwa wakati mmoja ikimzunguka.

Job 10:10-11

Je, Mungu amemvika Ayubu na nini?

Yeye amemvika Ayubu na ngozi na nyama.

Job 10:12-14

Je Mungu amemzawadia nini Ayubu?

Mungu amemzawadia yeye uhai na ahadi ya uaminifu.

Je Mungu atafanya nini kama Ayubu atatenda dhambi?

Mungu ataizingatia dhambi yake, na hatamuachia yeye kwa uovu wake.

Job 10:15-16

Je Mungu atafanya nini kwa Ayubu kama atatembea kichwa juu?

Mungu atamwinda kama simba.

Job 10:17

Je Mungu amemleta nani dhidi ya Ayubu kuelezea kile kilichotokea kwake?

Mungu ameleta mashahidi wapya dhidi yake.

Job 10:18-19

Je Ayubu anatamani nini kitokee kwake?

Anatamani angelikata roho na kwamba jicho lolote lisimuone milele.

Job 10:20-22

Je, Ayubu anakwenda wapi, ambako yeye hatarudi tena?

Yeye anakwenda kwenye nchi ya giza na kivuli cha mauti.

Job 11

Job 11:1-3

Sofari alifikiri Ayubu amefanya nini kwa mafundisho yao?

Yeye alifikiri Ayuba ameyadharau mafundisho ya rafiki zake.

Job 11:4-6

Sofari anasema nini ambacho Mungu amekidai kwa Ayubu?

Yeye alisema Mungu amedai kidogo kutoka kwa Ayubu kuliko uovu wake yeye ulivyostahili.

Job 11:7-9

Je, Sofari anaweza kufikiri kwamba Ayubu ingewezekana kumfahamu Mungu?

Sofari anafikiri kwamba haiwezekani kwa sababu Mungu yuko juu kama mawingu, kina kuliko kuzimu, mrefu kuliko nchi na mpana kulio bahari.

Job 11:10-14

Je, sofari anafikiri kuwa inawezekana kwa mtu yeyote kumzuia Mungu?

haiwezekani kumzuia Mungu kwa sababu yeye anawajua watu waongo na huukumbuka udhalimu.

Ni wakati gani sofari anasema watu wapumbavu watamfahamu Mungu?

Wao watakuwa na ufahamu wakati punda mwitu atakapozaa mtu.

Job 11:15-17

Je, Sofari anasema kitatokea nini kwa aibu ya Ayubu ikiwa kweli atauweka mbali uovu wake?

Ayubu angeisahau aibu yake na kuikumbuka tu kama maji ambayo yametiririka mbali.

Job 11:18-19

Je, kwa nini Ayubu angekuwa salama ikiwa ataweka mbali uovu wake yeye?

Yeye angekuwa salama kwa sababu kungekuwa na tumaini pale.

Job 11:20

Je, Sofari anasema ni kitu gani ambacho pekee ni tumaini la watu waovu?

Tumaini lao litakuwa pumzi ya mwisho ya uhai wao.

Job 12

Job 12:1-3

Jinsi gani Ayubu anajilinganisha yeye mwenyewe na rafiki zake?

Yeye anasema yeye pia ana ufahamu na siyo dhaifu kwao.

Job 12:4-6

Jirani za Ayubu wanafikiri nini juu yake sasa?

Wao wanamcheka.

Job 12:7-8

Je, nini Ayubu anafikiri angewafundisha rafiki zake?

Wanyama wakali wa porini, ndege, nchi, na samaki wa bahariniwangeweza kuwafundisha rafiki zake.

Job 12:9-10

Je, wanyama wote wanafahamu nini?

Wanafahamu kwamba mkono wa Yahwe umewapa wao uhai.

Job 12:11-12

Je, Ayubuanasema nini kuhusu watu wazee na wenye ufahamu?

Watu wazee wana hekima, na katika wingi wa siku mna ufahamu.

Job 12:13-15

Je, Mungu anafanya nini na maji?

Yeye pamoja huyashikilia na yana kauka, na yeye huyapeleka nje na yanaitaabisha nchi.

Job 12:16-18

Mungu huchukua nini kutoka kwa wafalme?

yeye huwandolea mkufu wa mamlaka.

Job 12:19-21

Je, Ayubu anasema nini kuhusu kile ambacho Mungu amefanya kwa watu wenye kuaminiwa na wazee?

Yeye anaondoa hotuba za watu wanaoaminiwa, na anaondolea mbali ufahamu wa wazee.

Job 12:22-23

Ayubu anasema nini kuhusu alichofanya Mungukwa mataifa?

Yeye huwafanya wao wawe na nguvu au huwaharibuwao,na na kuwakuza wao au kuwaongoza mbali kama watumwa.

Job 12:24-25

nini kilichotokea kwa viongozi wa watu wa nchi wakati Mungu anapowaondolea mbali ufahamu wao?

yeye huwafanya wao kutangatanga katika pori mahali pasipo na njia.

Job 13

Job 13:1-2

Ayubu anasemaje maarifa yake kulinganishwa na yale ya rafiki zake?

Ayubu anasema kwamba kile ambacho yeye anakifahamu, ndicho hichohicho wanachokijua wao na yeye siyo duni kwao.

Job 13:3-5

Ayubu angependa kuongea na nani badala ya rafiki zake na kwa nini?

Yeye angependa kuzungumza na aliye mkuu kwa sababu Ayubu anataka kuhojiana na Mungu.

Je, Ayubu anasema rafiki zake hufanya nini na ukweli?

Wanauficha ukweli kwa uongo.

Job 13:6-8

Je, Ayubu anataka rafiki zake wasikie nini?

yeye anawataka wao kusikiliza kuomba kwa midomo yake.

Job 13:9-10

Mungu angekubali ikiwa rafiki za Ayubu walionyesha upendeleo kwa Mungu?

Hapana, wangejitathimini wao, ikiwa walionyesha upendeleo kwake yeye.

Job 13:11-12

Je, Ayubu anafikiri nini kuhusu maneno ya rafiki zake na utetezi?

Yeye anasema maneno yao ni simulizi zilizotengenezwa kwa majivu, na utetezi wao umetengenezwa kwa udongo wa mfinyanzi.

Job 13:13-15

Je, Ayubu anawaambia rafiki zake kufanya nini ili kwamba yeye waweze kuzungumza?

Ayubu anawaambia kuishikilia amani yao na kumwache yeye peke yake.

Job 13:16-17

kwa nini Ayubu anafikiri kwamba yeye hatahesabiwa hatia?

Yeye hakuja mbele za Mungu kama mtu asiyemcha Mungu.

Job 13:18-19

Ni kitu gani ambacho Ayubu amekiweka katika mpangilio?

Yeye ameuweka utetezi wake katika mpangilio.

Job 13:20-22

Je, ni kitu gani ambacho Ayubu anamtaka Mungu kukitoa kutoka kwake?

Ayubu anamtaka Mungu kuondoa kutoka kwa Ayubu mkono wake unaotesa.

Job 13:23-25

Je, Mungu anamtendea Ayubu hivi kama nani?

Yeye anamtendea Ayubu kama adui yake.

Job 13:26-28

Je, vitu gani visivyo na faida ambavyo Ayubu amelinganishwa navyo?

yeye ni kama kitu kilichooza, ambacho chatupiliwa mbali kama kanzu ambayo nondo wamelila.

Job 14

Job 14:1-3

Ni kwa jinsi gani Ayubu anamsema mtu ambaye ni kama ua?

Mtu huchipuka kutoka chini kama ua na hukatwa chini.

Job 14:4-6

Ni nani anayepanga muda wa mtu kuishi?

Mungu amezipanga siku zake na idadi ya miezi yake?

Job 14:7-9

Je, Ayubu anasema nini kuhusu mti ambao umekatwa chini?

Kutakuwa na tumaini kwa mti ambao umekatwa chini, kwa maana unaweza kuchipua tena.

Job 14:10-12

Je, Ayubu anasema mtu anaweza kuishi tena?

yeye anasema kwamba watu hawafufuliwi tena, na hawataamshwa kutoka katika usingizi wao.

Job 14:13-14

Ni wapi ambapo Ayubu anatamani Mungu angemficha yeye?

Ayubu anamtaka Mungu kumfiche yeye mbali katika kuzimu mbali kutoka katka mahangaiko.

Job 14:15-17

Je, Mungu angeutendea vipi uovu na udhalimu wa Ayubu ikiwa ghadhabu ya Mungu ilikuwa imemalizika?

Mungu angeutia muhuri uovu na udhalimu wa Ayubu katika mkoba,na kuufunika udhalimu wake.

Job 14:18-19

Je, ni kitu gani cha kusisimua maji yanaweza kufanya juu ya muda?

yanaweza kuyaangusha mawe chini.

Job 14:20-22

Je, ni kwa jinsi gani hii humwathiri mtu aliyekufa kama watoto wake wa kiume wameheshimiwa au wameshushwa?

Ikiwa wataheshimiwa, yeye hajui , na kama wakishushwa yeye haoni hicho kutokea.

Job 15

Job 15:1-3

Je, mtu mwenye hekima hapaswi kujazwa na nini?

Yeye hapaswi kujijaza na upepo wa mashariki.

Job 15:4-6

Je, kwa jinsi gani Elifazi anafikiri maneno ya Ayubu yanamvunjia heshima Mungu?

Yeye anafikiri Ayubu anafifisha heshima kwa Mungu, na kuzuia sifa kwake yeye.

Job 15:7-9

Je, Elifazi anafikiri kwamba Ayubu anafahamu kitu chochote ambacho rafiki wengine hawakifahamu?

Yeye hafikiri kwamba Ayubu anafahamu kle ambacho hawakifahamu, au kwamba yeye anafahamu pia kile kisichokuwa katika wao.

Job 15:10-11

Ni akina nani ambao Elifazi anasema wanakubaliana na rafiki za Ayubu?

Ni watu wenye mvi na waliozeeka sana ambao ni wazee kuliko baba wa Ayubu wako pamoja na Elifazi na marafiki zake.

Job 15:12-14

je, ni kitu gani Elifazi anafikiri roho ya Ayubu imefanya?

Yeye anafikiri roho yake Ayubu imemgeuza mbali na Mungu.

Job 15:15-16

Je, Mungu anamtathimini vipi mtakatifu wake aliye mmoja na mbingu?

Yeye haweki tumaini hata katika mmoja wake aliy mtakatifu, na mbingu haziko safi machoni pake.

Job 15:17-18

Ni kutoka kwa nani Elifazi alipata vitu ambavyo yeye atavitangaza kwa Ayubu?

Vitu ambavyo yeye ameviona ni vitu ambavyo watu wenye heshima walipita chini ya baba zao, na vitu ambavyo mababu hawakuvificha

Job 15:19-21

Ni lini hao waharibifu huja juu ya mtu mwovu?

Mharibu atakuja juu yake pindi yeye akiwa katika kufanikiwa kwake.

Job 15:22-24

nini kinamgojea mtu mwovu?

Upanga unamngojea mtu mwovu.

Job 15:25-26

Mtu mwovu alikimbia dhidi ya Mungu na kitu gani?

yeye alikimbia kwa Mungu na shingo ngumu vishindo vya ngao.

Job 15:27-28

Je, nini kitatokea kwa miji na nyumba za mtu mwovu?

Viko tayari kuwa magofu.

Job 15:29-30

Je, ni kitu gani kitamfanya mtu mwovu kwenda mbali?

Yeye atakwenda mbali katika pumzi ya mdomo wa Mungu.

Job 15:31-33

Ni tuzo gani mtu mwovu atapokea kwa kutumaini katika vitu visivyo na faida?

vitu visivyo na faida vitakuwa faida yake yeye.

Job 15:34-35

Je nini kitatokea kwa kundi la watu wasio mcha Mungu?

Litakuwa tasa, na moto utameza hema zake za rushwa.

Job 16

Job 16:1-5

Je, Ayubu alisema nini juu ya faraja ya rafiki zake?

Ayubu alisema wao ni wafariji wanaohuzunisha wakitumia maneno yasiyokuwa na maana.

Job 16:6-8

Ni kwa jinsi gani maneno ya Ayubu kunaathiri kuhuzunika kwake?

kama akisema, kuhuzunika kwake hakusikilizwi, na kama akiendelea kusema, yeye hapati msaada.

Job 16:9-10

Je, ni kwa jinsi gani watu wengine wanamtendea Ayubu kama Mungu anamshambulia yeye?

Wao wanamcheka na midomo iliyo wazi, kumpiga kwa kejeli katika mashavu yake, na kukusanyika pamoja kinyume chake.

Job 16:11-12

Je, Mungu amemtoa Ayubu kwa nani?

mungu amemtoa yeye kwa watu waiomcha Mungu, na kumtupa yeye ndani ya mikono ya watu waovu.

Job 16:13-14

J Mungu amemtia jeraha Ayubu kwa namna gani?

Yeye ameichoma figo ya Ayubu na kuimwaga nyongo yake chini ya ardhi.

Job 16:15-17

Je, Ayubu amefanya nini kwa ngozi yake kuonyesha kwamba yuko katika kuomboleza?

Yeye ameshona nguo ya magunia juu ya ngozi yake.

Job 16:18-19

Je, ni nani shahidi wa Ayubu anayeweza kumshuhudia yeye?

Ushuhuda wa Ayubu uko mbinguni, na mmoja aliyeko kwa ajili yake yuko juu.

Job 16:20-22

Je, Ayubu aligeuka nani kama vile rafiki zake walivyomcheka?

Ayubu alimwaga machozi yake kwa Mungu

Job 17

Job 17:1-3

Ni kitu gani Ayubu lazima akione daima?

Yeye lazima daima aone kukasirisha kwa wenye mzaha ambao wako pamoja naye.

Job 17:4-5

Ni matendo ya nani maovu ambayo yatasababisha macho ya watoto wake kutoona?

Mmoja ambaye rafiki zake kwa tuzo watayasababisha macho ya watoto wake yeye kutoona.

Job 17:6-8

Nini kimetokea kwa macho ya Ayubu na kwa mwili wake kwa sababu ya huzuni?

Macho yake yeye hayaoni vizuri na sehemu za mwili wake wote ni nyembamba kama kivuli.

Job 17:9-10

Je, Ayubu anafikiri kwamba anaweza kupata mtu mwenye hekima miongoni mwa rafiki zake.

Ayubu anafahamu kwamba yeye hatapata mtu mwenye hekima miongoni mwao.

Job 17:11-12

Je, Ayubu ana mipango ya baadaye?

mipango ya Ayubu imekwisha, kama matamanio ya moyo wake.

Job 17:13-16

Je, nini kimekuwa baba wa Ayubu, mama na dada?

Shimo limekuwa baba yake yeye, na funza amekuwa mama na dada yake.

Job 18

Job 18:3-4

Jinsi gani Bildadi alifikiri Ayubu alivyowafikiria rafiki zake?

Bildadi alimfikiria Ayubu aliwahesabu wao kama wanyama wakali wa porini na alifikiri walikuwa wapumbavu.

Job 18:5-6

nini kitatokea kwa taa ya mtu mwovu?

Taa yake yeye itawekwa nje, na na mwali wa mwanga wake hautanga'ra.

Job 18:7-8

Ni kitu gani kitamtupa mtu mwovu katika mtego?

Yeye atatupwa ndani ya mtego kwa miguu yake mwenyewe, na atatembea ndani ya shimo.

Job 18:9-11

Je, nini kitamkamata mtu mwovu?

Yeye atanaswa na tanzi, mtego, na mtego wa kamba.

Job 18:12-13

nini kitatokea kwa mali ya mtu mwovu?

Utajiri wake kugeuka hasira.

Job 18:14-15

Ni wapi mtu mwovu hataweza kuishi?

Yeye atafukuzwa kutoka katika hema yake, nyumbani kwake ambako sasa anatumainia.

Job 18:16-17

Je, Bildadi anatumia picha gani kuelezea kile ambacho kitatokeakwa mtu mwovu?

Yeye anamwelezea mtu mwovu kama mti ambao mizizi yake itanyauka katika ardhi, na ambao matawi yake yatakatwa juu.

Job 18:18-21

Je, mtu mwovu atakuwa na uzao?

yeye hatakuwa na watoto au wajukuu miongoni mwa watu wake, wala vizazi mahali alipokuwa amekaa.

Jinsi gani watu huitikia kwa yale yanayotokea kwa mtu mwovu?

Watu wanoishi upande wa magharibi watashtushwa na watu waishio upande wa mashariki watafadhaishwa.

Job 19

Job 19:1-2

Ni katika nini Ayubu anasema rafiki zake wamemvunja?

Ayubu anasema wao wamemvunja yeye katka vipande vipande vya mti.

Job 19:3-4

Je, ni mara ngapi rafiki za Ayubu wamemkejeli?

Wao wamemkejeli yeye mara kumi.

Ni shauri ya nani kiwa Ayubu amekosa?

Ayubu anasema makosa lazima yawe juu yake.

Job 19:5-6

Jinsi gani Ayubu anasema Mungu alivyomtendea?

Ayubu anasema Mungu amefanya mabaya kwa Ayubu na amemnasa yeye katika mtego wa Mungu.

Job 19:7-9

Nini kinatokea wakati Ayubu anapopasa sauti kwa ajili ya msaada kwasababu amefanya makosa

Yeye hasikiwi na hakuna haki.

Job 19:10-12

Je, Mungu amemtambua vipi Ayubu?

Yeye amemtambua Ayubu kama mmoja wa adui zake.

Job 19:13-14

Je, nini kilikuwa kimetokea kwa familia yote ya Ayubu na rafiki?

Mungu amewaweka mbali naye kaka zake, watu wake wa karibu wamemtelekeza, uzao wake unamwangusha yeye, na rafiki zake wa karibu wamemsahau yeye.

Job 19:15-16

Je, ni kwa namna gani mtumishi wa Ayubu anaitikia kwa Ayubu wakati yeye anapomwita yeye?

Mtumishi wake yeye hanijibu mimi ingawa anamtendea hivyo kwa mdomo wake.

Job 19:17-19

Je, wale ambao Ayubu aliwapenda walimjibu yeye?

Wale ambao aliwapenda wamegeuka kinyume chake.

Job 19:20-22

Je, ni kwa jinsi gani Ayubu alipata kuishi?

Yeye aliishi tu kwa ngozi ya meno yake.

Job 19:23-24

Je, ni kitu gani Ayubu alitaka kitokee kwa maneno yake ?

Yeye anataka yaandikwe chini na kutunzwa katika kitabu, au kuachorwa kwa kalamu na risasi katika mwamba.

Job 19:25-27

Je, Ayubu anasema anafahamu nini yeye?

Yeye anafahamu kuwa mkombozi wake anaishi, na kwamba mwisho mkombozi wake atasimama katika nchi.

Je, Ayubu anasema nini kitatokea wakati mwili wake una umeharibiwa?

Ayubu katika mwili wake atamwona Mungu.

Job 19:28-29

Ghadhabu huleta nini?

Ghadhabu huleta adhabu ya upanga.

Job 20

Job 20:1-3

Kwa nini Sofari alimjibu Ayubu kwa haraka?

Yeye alimjibu Ayubu kwa haraka kwa sababu ya hofu yake na kwamba kulikuwa na roho mbali na ufahamu kuwa anamjibu yeye. Yeye amesikia kukemewa kwa Ayubu na anasema humweka yeye katika aibu.

Job 20:4-5

Ni kwa muda gani furaha ya mtu asiyemcha Mungu hdumu?

Furaha ya mtu asiye mcha Mungu hudumu kwa kitambo tu.

Job 20:6-7

jinsi gani mtu mwovu ataangamia?

Yeye ataangamia siku zote kama mavi yake mwenyewe.

Job 20:8-9

Ni kwa namna gani mtu mwovu ataenda zake?

Yeye atapaa mbali kama ndoto, na kufukuzwa mbali kama ono la usiku.

Job 20:10-11

Je, watoto wa mtu mwovu watafanya nini?

Watoto wake yeye wataomba kwa watu maskini.

Job 20:12-14

Je, nini hutokea kwa uovu ndani ya mtu mwovu?

utasababisha chakula katika kaakaa kuwa chungu, na itakuwa kama sumu ya swira ndani yake yeye.

Job 20:15-16

Je, nini kitatokea kwa utajiri ambao mtu mwovu huumeza chini?

Yeye atautapika tena.

Job 20:17-19

Je, ni kitu gani mtu mwovu hataishi na kukifurahia?

Yeye hataishi kufurahia kutazama juu ya mito na vijito vya asali na siagi vinavyotirirka.

Je, kwa nini mtu mwovu hufurahi?

Yeye amewanyanyasa na kuwapuuza watu maskini, na kwa unyanyasaji amechukulia mbali nyumba ambayo hakuijenga.

Job 20:20-22

Kwa nini kufanikiwa kwa mtu mwovu hakutadumu?

Hakutadumu kwa sababu hakuna chochote kilichobakia ambacho hakukimeza.

Job 20:23-25

Je, Mungu atafanya nini kwa mtu mwovu ambaye yuko katika kulijaza tumbo lake?

Mungu atainyeshea chini hasira ya ghadhabu yake juu yake yeye wakati akiwa anakula.

Nini kitatokea wakati mtu mwovu hukimbia kutoka kwenye silaha ya ya chuma?

Upinde wa shaba utampiga yeye.

Job 20:26-27

Je, mbingu na nchi zitafanya nini dhidi ya mtu mwovu?

Mbingu zitaufunua udhalimu wake, na nchi itakuwa shahidi dhidi yake.

Job 20:28-29

Je, nini kitakachotokea kwa mtu mwovu siku ya ghadhabu ya Mungu?

Utajiri wa nyumba yake utapotea na bidhaa zake zitapotelea mbali.

Job 21

Job 21:1-3

Ayubu anafikiri rafiki zake watafanya nini baada ya maongezi yake?

Anafikiri wataendelea kumfanyia dhihaka.

Job 21:4-6

Mwitikio wa watu utakuwa wa namna gani wanapomtazama Ayubu?

Watashangaa na kuweka mikono yao juu ya vinywa vyao.

Kitu gani kinatokea kwa Ayubu anapofikiri kuhusu mateso yake?

Anafadhaika na kitisho kinaushika mwili wake.

Job 21:7-9

Ayubu anauliza nini kuhusu watu waovu?

Ayubu anauliza kwa nini waovu wanaendelea kuishi, kuwa wazee, na kuongezeka kuwa na nguvu?

Job 21:10-12

Nini hutokea kwa fahari na ng'ombe jike wa waovu?

Fahari haachi kuzalisha na ng'ombe jike hapotezi ndama wake kabla ya kukomaa.

Job 21:13-15

Watu waovu humwambiaje Mungu?

Wanamwambia Mungu aondoke kwao, maana hawahitaji maarifa yoyote ya njia zake.

Job 21:16-18

Mwitikio wa Ayubu ukoje kwenye ushauri wa watu waovu?

Hana cha kufanya katika ushauri wao.

Job 21:19-21

Ayubu anataka nani alipe kwa ajili ya hatia ya mtu mwovu?

Ayubu anataka mtu mwovu alipe kwa ajili ya hatia yake mwenyewe, na watoto wake, ili kwamba aijue hatia yake.

Job 21:22-24

Je mtu yeyote anaweza kumfundisha Mungu maarifa?

Hapana, maana Yeye huwahukumu hata wale wakuu.

Job 21:25-26

Jambo gani hutokea kwa watu wote ambao hufa katika nguvu zao kamilifu na wale wanaokufa katika uchungu wa nafsi zao?

Wote hulala mavumbini vilevile na minyoo huwafunika wote.

Job 21:27-28

Ayubu anajua nini kuhusu mawazo na njia za rafiki zake?

Anayajua mawazo yao na njia ambazo wameazimia kumpotosha.

Job 21:29-30

Watu wanaosafiri wameona jambo gani likitokea kwa mtu mwovu?

Wameona kwamba mtu mwovu hutunzwa kwa siku ya msiba, na kwamba hupelekwa mbali kwa siku ya ghadhabu.

Job 21:31-33

Watu watafanya nini kwa ajili ya kaburi la mtu mwovu?

Watu watalinda juu ya kaburi lake.

Job 21:34

Ayubu anasema Sofari alijaribu kumfariji kwa namna gani?

Ayubu anasema Sofari alikuwa akimfariji kwa upuuzi.

Job 22

Job 22:1-3

Elifazi anamuuliza Ayubu kwamba anaweza kufanya nini kwa Mwenyezi kama ni mwenye haki?

Anamuuliza kama inaleta furaha yoyote kwa Mwenyezi kama Ayubu ni mwenye haki.

Job 22:4-5

Ni jinsi gani Elifazi anaudhihaki ucha Mungu wa Ayubu?

Kwa kudhihaki anasema kuwa Ayubu anakemewa kwa kuwa yeye alimcha Mungu.

Job 22:6-8

Elifazi anamlaumu Ayubu kwa jambo gani alilokuwa akifanya kwa waliouchi?

Anasema kwamba Ayubu amewavua nguo zao waliouchu.

Job 22:9-11

Elifazi anamlaumu Ayubu kwa jambo gani alilokuwa akifanya kwa wajane?

Anasema Ayubu amewawaondoa wajane bila kitu?

Elifazi anasema giza limekuwaje kwa Ayubu?

Anasema kuwa kuna giza, hivyo Ayubu hawezi kuona.

Job 22:12-14

Elifazi anadi Ayubu anasema nini kuwa Mungu hawaoni watu?

Ayubu asema, " Mawingu mazito yanamfunika Mungu, hivyo hawaoni watu."

Job 22:15-17

Ni jambo gani hutokea kwenye misingi ya watu waovu?

Misingi ya watu waovu imetoweka kama mto.

Job 22:18-20

Jinsi gani wenye haki hutenda wanapotazama maangamizi ya waovu?

Wenye haki huyaona maangamizi yao na kufurahi.

Job 22:21-22

Nini kitatokea kama Ayubu akiwa na amani kwa Mungu?

Kama Ayubu akiwe na amani kwa Mungu, mazuri yatamjia.

Job 22:23-25

Elifazi anasema nini kitatokea kama Ayubu atamrudia mwenyezi?

Kama Ayubu atamrudia mwenyezi atajengwa.

Job 22:26-28

Nini kitatokea Ayubu atakapomfurahia Mwenyezi?

Ayubu atakapomfurahia Mwenyezi, atainua uso wake kwa Mungu.

Job 22:29-30

Mungu hufanya nini kwa wenye kiburi?

Mungu huwanyenyekesha wenye kiburi.

Job 23

Job 23:1-2

Ayubu anasema kitu gani ni kizito zaidi ya kuugua kwake?

Ayubu anasema mateso yake ni mazito zaidi ya kuugua kwake.

Job 23:3-5

Ayubu angefanya nini mbele za Mungu kama angeweza kukutana naye?

Angeweka shitaka lake mbele za Mungu na kukijaza kinywa chake kwa hoja.

Job 23:6-7

Je Ayubu anafikiri Mungu atakuwa kinyume dhidi yake kwa ukuu wake ikiwa atasimama mbele zake?

Hapana, anafikiri Mungu angeweza kumsikiliza.

Job 23:8-9

Ayubu anasema Mungu anafanya jambo gani huko kusini?

Ayubu anasema huko kusini, Mungu hujificha hivyo Ayubu hawezi kumwona.

Job 23:10-12

Ayubu ategemea matokeo gani kutokana na kujaribiwa na Mungu?

Mungu atakapokuwa amemjaribu Ayubu, atakuwa kama dhahabu.

Job 23:13-14

Mungu anaamuru nini kwa Ayubu?

Mungu anaamuru sheria zake kwa Ayubu.

Job 23:15-17

Ayubu anajisikiaje anapofikiri juu ya Mungu?

Ayubu apofikiri kuhusu Mungu anamwogopa.

Nini kinaufunika uso wa Ayubu?

Giza kuu linaufunuka uso wa Ayubu.

Job 24

Job 24:1

Ayubu anafikiri ni nyakati gani hazijawekwa na Mwenyezi?

Ayubu anauliza kwa nini nyakati za kuwahukumu waovu hazijawekwa na Mwenyezi.

Job 24:2-4

Waovu hufanya nini kwa punda wa yatima?

Huswaga punda wa yatima.

Job 24:5-7

Masiki wanatumaini Araba itawapatia nini?

Wanatumaini Araba itawapatia chakula kwa ajili ya watoto wao.

Masiki wanapungukiwa na nini kwenye mvua?

Hawana cha kujifunika kwenye baridi.

Job 24:8-10

Masikini hukumbatia kwa kukosa malazi?

Wanakumbatia mwamba kwa kukosa malazi.

Ingawa masikini huenda zao na njaa huwatendea nini watu wengine?

Ingawa huenda zao na njaa, hubeba miganda ya nafaka kwa watu wengine.

Job 24:11-12

Ingawa masikini hupatwa kiu je hufanya nini kwa ajili ya wengine?

Hukanyaga mashinikizo ya divai ya watu waovu, lakini wao huteseka kwa kiu.

Job 24:13-14

Mwuaji yupo namna gani wakati wa usiku?

Wakati wa usiku, mwuaji ni kama mwizi.

Job 24:15-17

Kwa nini waovu hujifungia ndani wakati wa mchana?

Waovu hawajali kwa ajili ya mwanga.

Waovu wanafarijika kwa vitisho vya aina gani?

Wanafarijika kwa vitisho vya giza nene.

Job 24:18-19

Kuzimu humla nani?

Kuzimu huwala wale ambao wametenda dhambi

Job 24:20-21

Waovu humteketeza nani?

Waovu huwateketeza wanawake tasa ambao huwajazaa watoto.

Job 24:22-23

Mungu huwaburuta kina nani?

Mungu huwaburuta wenye uwezo kwa nguvu zake.

Job 24:24-25

Kutatokea nini kwa watu wenye nguvu kwa muda mchache?

Kwa muda mchache tu, wenye nguvu watatoweka.

Job 25

Job 25:1-3

Mungu hufanya amri wapi?

Mungu hufanya amri kwenye maeneo yake ya juu mbinguni.

Job 25:4-6

Bildadi anauliza ni akina nani wanaweza kuwa wasafi na kukubalika kwa Mungu?

Anauliza kama mtu aliyezaliwa na mwanamke anaweza kuwa msafi na kukubalika kwa Mungu.

Bildadi anamlinganisha na nini mwana wa mtu?

Anasema mwana wa mtu ni mnyoo

Job 26

Job 26:1-4

Ayubu anafikiri Bildadi aliongea maneno yake kwa namna gani?

Hapana, Ayubu anataka kujua ni nani aliyemsaidia Bildadi kuongea maneno yake.

Job 26:5-6

Ni nini hakina kifuniko mbele za Mungu?

Uharibifu hauna kifuniko dhidi ya Mungu.

Job 26:7-8

Mungu huyakusanya maji wapi?

Huyakusanya maji kwenye mawingu mazito.

Job 26:9-10

Mungu hutandaza juu ya uso wa mwezi?

Huuzungushia uso wa mwezi na kuutandazia mawingu yake juu.

Job 26:11-12

Mungu alituliza nini kwa nguvu zake?

Alituliza bahari kwa nguvu zake.

Job 26:13-14

Mungu alisafisha dhoruba ya mbingu kwa kitu gani?

Kwa pumzi yake, alisafisha mbingu kwenye dhoruba.

Huwa tunasikia kipimo gani cha sauti ya Mungu?

Huwa tunasikia lakini ni mnong'ono wake mdogo.

Job 27

Job 27:1-3

Ayubu anasema Mungu amendolewa kitu gani kwake?

Mungu ameondoa haki yake.

Job 27:4-5

Ayubu anaweka nadhiri kuwa midomo yake haitaongea kitu gani?

Ayubu anaweka nadhiri kwamba kwa hakika midomo yake haitaongea udhalimu.

Job 27:6-7

Ni kwa muda gani mawazo yake Ayubu yataacha kumsuta?

Mawazo yake hayatamsuta tena kwa kadri atakavyoishi.

Job 27:8-10

Ayubu anasema Mungu hufanya nini wakati anapokatilia mbali maisha ya mtu kafiri?

Wakati Mungu anapokatia mbali maisha yake, Mungu humwondolea roho yake.

Job 27:11-12

Ayubu anasema hataficha nini kwa Mwenyezi?

Ayubu anasema kwamba hataficha mawazo ya Mwenyezi.

Job 27:13-14

Uzao wa mtu mwovu hapati kitu gani kwa utosheleza?

Uzao wake hautapata chakula cha kutosheleza.

Job 27:15-17

Mjane wa mtu mwovu hatafanya nini kwake?

Mjane wake hataomboleza kwa ajili yake.

Fedha ya mtu mwovu itakuwaje?

Wenye haki wataigawana fedha yake miongoni mwao.

Job 27:18-19

Mtu mwovu huona nini wakati afumbuapo macho yake baada ya kulala akiwa tajiri?

Hufumbua macho yake, na kila kitu huwa kimeondoka.

Job 27:20-21

Upepo wa mashariki hufanya nini upomchukua mtu mwovu ?

Upepo wa mashariki humchukua na kumpeleka mbali na humzoa kutokakwenye mahali pake.

Job 27:22-23

Mtu mwovu hujaribu kufanya nini wakati upepo wa mashariki usipo koma?

Hujaribu kukimbia mbali na mkono wa upepo.

Job 28

Job 28:1-2

Shaba huyeyushwa kutoka wapi?

Shaba huyeyushwa kutika kwenye mawe.

Job 28:3-4

Binadamu futafiti nini hadi kwenye mipaka ya mbali zaidi?

Binadamu hutafiti, mawe katika uvunguvungu na giza nene hadi kwenye mipaka ya mbali zaidi.

Ni wapi binadamu huvunja na kubomoa shimo?

Huvunja na kubomoa shimo mbali na sehemu wanapoishi watu.

Job 28:5-6

Vumbi la ardhi limechanganyika na nini?

Vumbi la ardhi limechanganyika na dhahabu.

Job 28:7-8

Nini hakijapitia katika njia ya shimo la wadamu?

Wanyama wenye kiburi hawajapita kwenye njia kama hiyo, wala simba mwenye hasira hajapita pale.

Job 28:9-11

Binadamu huona nini katika mifereji anayoichonga kwenye miamba?

Macho yake huona kila kitu chenye thamani mahali pale.

Job 28:12-14

Ni wapi ambapo maarifa na hekima havipatikani?

Vyote hivi havipatikani kwenye nchi ya waliohai.

Job 28:15-17

Nini hakiwezi kulingana na thamani ya hekima na maarifa?

Dhahabu na vito vyote hivi haviwezi kulinganishwa kwa thamani yake.

Job 28:18-19

Gharama ya hekima ni zaidi kuliko marijani ipi?

Gharama ya hekima ni zaidi kuliko rubi.

Job 28:20-22

Nani amefichwa hekima kwenye macho yake?

Hekima imefichwa kutoka kwenye macho ya viumbe hai vyote.

Job 28:23-25

Nani anajua mahali pa hekima?

Mungu anaijua njia ya kuelekea kwenye hekima na anapajua mahali pake.

Job 28:26-28

Mungu alifanya amri kwa ajili ya kitu gani?

Alifanya amri kwa aji;i ya mvua.

Job 29

Job 29:1-3

Je Ayubu anakumbuka wakati ambapo Mungu alipomlinda?

Ayubu anakumbuka kwamba katika miezi iliyopita Mungu alimlinda.

Job 29:4-6

Nini kilikuwepo kwenye hema ya Ayubu katika siku zake za kukomaa?

Ayubu anakumbuka siku zake za kukomaa, wakati urafiki wake na Mungu ulipokuwa hemani mwake.

Mwamba ulimwaga nini kwa Ayubu nyakati zilizopita?

Wakati mwenyezi alipokuwa pamoja na Ayubu, mwamba ulimwaga mafuta kwa ajili yake.

Job 29:7-8

Jinsi gani vijana walionyesha hesima kwa Ayubu kwenye viunga vya mji.

Walimwona Ayubu na kukaa mbali naye kwa heshima.

Job 29:9-10

Mfalme walifanya nini hapo zamani Ayubu alipowaendea?

Walikuwa wakijizuia wasinene alipokuja kwao

Nini kilitokea kwenye ulimi wa waungwana wakati Ayubu alipowaendea?

Ndimi zao ziligandamana kwenye makaakaa ya midomo yao.

Job 29:11-13

Waungwana waliweza kufanya nini baada ya macho yao kumwona Ayubu?

Waliweza kumshuhudia Ayubu na kumthibitisha.

Ayubu alisababisha moyo wa mjane kufanya nini?

Alisababisha moyo wa mjane kuimba kwa furaha.

Job 29:14-16

Ayubu alifanya nini hata kwa mtu asiyemfahamu?

Aliweza kuchunguza shitaka hata la yule ambaye hakumfahamu?

Job 29:17-19

Ayubu aliweza kumuopoa nani katika meno ya wadhalimu?

Aliwaopoa wahanga kutoka katikati ya meno ya wadhalimu.

Job 29:20-22

Ayubu anasema ni kitu gani mara nyingi huwa ni kipya katika mkono wake?

Upinde wa nguvu zake huwa mara nyingi ni mpya mkononi mwake.

Job 29:23-24

Watu walisubiri kunywa kitu gani kama mvua kutoka kwa Ayubu?

Walifumbua sana kinywa chao kunywa katika maneno yake kama walivyofanya kwenye mvua ya masika.

Job 29:25

Ayubu anajifananisha na nini kwenye mazishi?

Anasema kwamba yeye ni kama mwenye kufariji waombolezaji kwenye mazishi.

Job 30

Job 30:1-3

Nani ambaye hana lolote lakini dhihaka kwa ajili ya Ayubu?

Wale ambao ni vijana zaidi kuliko Ayubu hawana lolote isipokuwa dhihaka kwa ajili yake.

Nini kiliwakondesha baba zao vijana?

Walikuwa wamekonda kutokana na umasikini na njaa.

Job 30:4-6

Baba zao vijana waliondolewa kutoka wapi?

Baba zao walitolewa nje miongoni mwa watu.

Job 30:7-8

Ayubu anasema baba zao vijana ni uzao wa nani?

Ayubu anasema walikuwa uzao wa wapumbavu kabisa, watu wasiofaa.

Job 30:9-11

Ayubu alikuwa namna gani kwa wana wa watu wasiofaa?

Ayubu alikuwa mada yao kwenye wimbo wa dhihaka .

Sasa watu wanakosa kitu gani kutoka kwa Ayubu?

Watu hawa wanakosa kiasi mbele za Ayubu.

Job 30:12-13

Kwa nini watu wanaweza kusukuma mbele uharibifu kwa ajili ya Ayubu?

Wanasukuma uharibifu kwa ajili ya Ayubu, maana hawana mtu wa kuwazuia.

Job 30:14-15

Ayubu anasema ni nini kimeondolewa kwa upepo?

Heshima yake imeondolewa kama kwa upepo.

Job 30:16-17

Nini kinamshika Ayubu pale maisha yake yanapomwagika kutoka ndani yake?

Siku nyingi za mateso zimeshikilia juu yake.

Job 30:18-19

Ayubu anasema ni nini kishika mavazi yake?

Nguvu kuu ya Mungu imekamata mavazi yangu.

Job 30:20-21

Ayubu anasema Mungu anamtesa kwa namna gani kana kwamba amebadilika na kuwa mkali?

Mungu amebadilika na kuwa mkali kwa Ayubu; kwa nguvu za mkono wake anamtesa.

Job 30:22-23

Ayubu anajua ni nini hatima ya viumbe hai vyote?

Anajua kwamba Mungu atamleta katika mauti, kwenye nyumba ya hatima ya viumbe hai vyote.

Job 30:24-26

Nini kilimjia Ayubu wakati alipongoja kwa ajili ya nuru?

Alipongoja nuru, badala yake lilikuja giza.

Job 30:27-29

Ayubu alisimama wapi ili kuomba msaada?

Alisimama katika kusanyiko na kulia kwa ajili ya msaada.

Job 30:30-31

Ayubu anasema kinubi chake kimetayarishwa kwa mziki wa namna gani?

Ayubu anasema kwamba kinubi chake kimatayarishwa kwa nyimbo za maombolezo.

Job 31

Job 31:1-2

Ni gani ambayo Ayubu inaisema ilitiishwa na agano pamoja na macho yake?

Ayubu alikuwa amefanya agano na macho yake kutomwangalia mwana mwali kwa tamaa.

Job 31:3-4

Ayubu alikuwa akidhania kuwa majanga yamehifahdiwa kwa akina nani?

Ayubu alikuwa akidhani kwamba majanga yalikuwa ni kwa watu wasio haki.

Job 31:5-6

Ayubu aliomba kitu gani kifanyike ili kwamba Mungu ajue uadilifu wake?

Aliomba upimwaji katika mizani sawa, ili kwamba Mungu ajue uadilifu wake.

Job 31:7-8

Ni kitu gani ambacho Ayubu alikiomba kitokee kwa mavuno, kama amegeuka na kuiacha njia ya kweli?

Alisema mavuno na yang'olewe katika shamba.

Job 31:9-10

Ayubu alisema hukumu ingekuwa ni ya namna gani kama angevutiwa na mwanamke mwingine?

Ayubu alisema mke wake asage nafaka kwa mwanaume mwingine.

Job 31:11-12

Ni aina gani ya moto ambao Ayubu alisema ulikuwa umefanana na uovu huu?

Ayubu alisema kwamba ni moto ambao unateketeza kila kitu kwa uharibifu

Job 31:13-15

Je Mungu alifanya nini kwa mtumishi na kwa Ayubu?

Mungu aliwafanya na kuwaumba wote katika tumbo.

Job 31:16-18

Ayubu alisema nini juu ya jinsi alivyowajali yatima tangu ujana wake?

Alisema tangu ujana wangu yatima walikua pamoja nami kama kuwa na baba,

Job 31:19-21

Ni kitu gani anchotakiwa apewe muhitaji asiye na nguo ili kumtia joto?

Wanatakiwa watie joto na sufu za kondoo.

Job 31:22-23

Ni sehemu gani ya mwili ambayo Ayubu aliisema kuwa ingemtoka kama asingekuwa na huruma?

Ayubu alisema bega lake lianguake kutoka katika sehemu yake,

Job 31:24-25

Watu wangeweza kusema nini juu ya dhahabu safi?

Wangeweza kuiambia dhahabu safi, ''wewe ni tumaini langu'"

Job 31:26-28

Ni nani ambaye Ayubu angekuwa anamkataa kama angeabudu jua au mwezi?

Kama angeviabudu angekuwa anamkataa Mungu aliye juu.

Job 31:29-30

Ni kwa namna gani Ayubu hajautese ulimi wake kwa dhambi?

Ayubu hajauruhusu hata mdomo wake utende dhambi kwa kuuomba uhai wa wale wanaomchukia kwa laana.

Job 31:31-32

Ayubu alikuwa akifanya nini mara kwa mara kwa wasafiri?

Alikuwa mara kwa mara akizifungua milango yake kwa ajili ya wasafiri.

Job 31:33-34

Ayubu alisema ni kwa namna gani mtu huzificha dhambi zake?

Huzificha dhambi zake kwa kuificha hatia zake ndani ya kanzu yake.

Job 31:35-37

Ni kitu gani ambacho Ayubu anataka awe nacho ambacho adui yake alikuwa amekiandika?

Ayubu alitamani kuwa na shitaka ambalo adui yake alikuwa ameliandika.

Ni kwa namna gani Ayubu angeweza kupanda kwa adui zake kama angekuwa na mashitaka yao?

Angepanda kwake kama mwana wa mfalme anayejiamini.

Job 31:38-40

Ni vitu gani ambayo Ayubu alitaka viote badala ya mazao kama Ayubu alikuwa amewafanya wamili wa mashaka kupoteza maisha yao?

Ayubu alisema angeruhusu miiba badala ya ngano na magugu badala ya shayiri.

Job 32

Job 32:1-2

Je marafiki watatu wa Ayubu walifanya nini wakati waliposhindwa kumshawishi kwamba yeye alikuwa ametenda kitu kibaya?

Waliacha kumjibu Ayubu.

Ni hisia gani zilikuwa zinawaka kwa Elihu wakati Ayubu alipokuwa akiendelea kujihesabia haki kuliko Mungu?

Hasira ya Elihu iliwaka dhidi ya Ayubu.

Job 32:3-5

Kwannini hasira ya Elihu iliwaka kinyume cha marafiki watatu wa Ayubu?

Hasira ya Elihu iliwaka pia kinyume cha marafiki zake watatu kwasababu hawakupata jibu kwa ajili ya Ayubu, na bado walimhukumu Ayubu.

Job 32:6-7

Kwanini Elihu alikuwa mwoga na mwenye hofu kumwambia Ayubu na marafiki zake kile alichokuwa akikifikiri?

Elihu alikuwa ni mdogo na wengine wote walikuwa ni wakubwa na walipaswa kuwa na uwezo wa kufundisha hekima.

Job 32:8-10

Elihu anamsema nani kuwa ndiye hutoa ufahamu kwa mtu?

Pumzi ya Mwenye nguvu humpa mtu ufahamu.

Kwanini Elihu anasema wengine lazima wamsikilize yeye na kumruhusu aseme yale anayoyajua?

Si tu watu wakubwa ndio wenye hekima, wala watu wazee pekee ambao hufahamu haki.

Job 32:11-12

Ni kitu gani ambachho marafiki zake Ayubu wahawakuweza kukifanya ingawa Elihu aliwasubiria waseme, na kuweka umakini mkubwa?

Marafiki zake Ayubu hawakuweza kumshawishi Ayubu au kujibu maneno yake.

Job 32:13-16

Ni nani ambaye Elihu anamsema lazima ampinge Ayubu wakati marafiki watatu waliofikiri kuwa walikuwa ni wenye hekima, hawakuwa na uwezo wa kufanya hivyo?

Ni Mungu lazima ampinge Ayubu

Job 32:17-19

Ni kitu gani kinachomsukuma Elihu kumshirikisha Ayubu ufahamu wake?

roho ndani yake inanisukuma kushirikisha ufahamu wake.

Ni kitu gani Elihu alikisema alikuwa akikisikia kifuani kwake?

Alisema kwamba kifua chake ni kama divai yenye chachu ambayo haina tundu; kama viriba vipya, kiko tayari kupasuka.

Job 32:20-22

Ni kitu gani Elihu alisema juu ya Muumbaji wake angekifanya kama angesema na kutoa sifa za majina kwa mtu fulani?

Elihu alisema kwamba Muumbaji wake angemkatilia mbali.

Job 33

Job 33:1-3

Kwanini Elihu alimwomba Ayubu asikilize maneno atakayoyasema?

Elihu alimwomba Ayubu asikilize kwasababu atasema unyofu wa moyo wake.

Job 33:4-5

Nani alimwumba Elihu na ni nini kilichompa uhai?

Roho ya Mungu imemuumba na pumzi ya Mwenye nguvu imempatia uhai

Ni kitu gani ambacho Elihu anamwomba Ayubu akifanye kama Ayubu ataweza kumjibu Elihu?

Anamwomba Ayubu ayaweka maneno yake katika mpangilio na kisha usimame mbele yake.

Job 33:6-7

Ni sababu gani ambayo Elihu anaitoa ambayo Ayubu alipaswa kutomwogopa au kusikia msukumo kwa Elihu?

Elihu alimwambia Ayubu kwamba wako sawa machoni pa Mungu na wote walikuwa wameumbwa kutokana na udongo.

Job 33:8-9

Elihu alikuwa amemsikia Ayubu akisema nini?

Elikuwa alimsika Ayubu akisema kwamba alikuwa safi bila uovu, asiye na hatia na hapakuwa na dhambi ndani yake.

Job 33:10-12

Ni nani ambaye Ayubu anamlaumu kwa kupata fursa ya kumshambulia, na kwa kumwona kana kwamba ni adui?

Ayubu anamlaumu Mungu kwa kufanya vitu hivi.

Job 33:13-15

Kwanini Elihu alisema kwamba ni bure kushindana na Mungu?

Mungu huwa hahesabu matendo yake yoyote.

Elihu alisema ni kwa namna gani Mungu huzungumza na mtu?

Mungu huzungumza katika ndoto, katika maono ya usiku, wakati usingizi mzito unapowapata watu, katika usingizi kitandani

Job 33:16-18

Kwanini Mungu hufungua masikio ya watu na kuwatisha kwa vitisho?

Mungu hufanya hivi kwa kusudi la kumvuta mtu atoke katika makusudio yake maovu, na kuyaweka majivuno mbali naye.

Job 33:19-20

Ni kitu gani Elihu alikisema ambacho kilikuwa ni sababu ya mtu kuwa na maumivu kitandani mwae, maumivu makali katika mifupa yake na kukoswa hamu ya chakula au starehe?

Elihu alisema kwamba hii ni kwasababu mtu amekwisha kuhukumiwa.

Job 33:21-22

Elihu alisema kitatokea nini kwa mtu aliyehukumiwa na Mungu?

Nyama yake imeharibiwa ili kwamba usionekane; mifupa yake, mara moja isionekane, sasa basi ng'ang'ania na roho yake inasogea shimoni.

Job 33:23-24

Je malaika mpatanishi angeweza kusema nini kwa Mungu ili kumwokoa mtu anayetumbukia shimoni?

Malaika angemwambia Mungu, 'Mwokoe mtu huyu ili asishuke chini shimoni; nimepata fidia kwa ajili yake

Job 33:25-26

Ni kitu gani kingetokea kwa mwili wa mtu aliyeokolewa kutoka katika shimo?

mwili wake utakuwa mororo kuliko mwili wa mtoto

Job 33:27-28

Kutatokea nini katika maisha ya mtu anayekubali dhambi zake na ameokolewa na Mungu kutoka katika shimo?

Maisha ya mtu huyo yataendele kuiona nuru.

Job 33:29-30

Kwanini Elihu alisema kwamba Mungu humwokoa mtu kutoka katika shimo?

Mungu hufanya mambo haya yote ili kwamba mtu aweze kumlikwa na mwanga wa maisha.

Job 33:31-33

Elihu alitaka kumfundisha nini Ayubu kama angeweka umakini na kumsikiliza na kukaa kimya?

Elihu alitaka kumfundisha hekima.

Job 34

Job 34:1-3

Ni akina nani ambao Elihu anawataka wamsikilize maneno yake na kumsikia?

Elihu anawataka watu wenye hekima na wale wenye maarifa wamsikilize yeye.

Job 34:4-6

Ni kitu gani Elihu anawataka watu wengine wachague na kukigundua wao wenyewe?

Elihu anawataka wachague mambo ya adili na kugundua yale yaliyo mazuri.

Ayubu alisema kitu gani ambacho kimechukuliwa kwake ingawa yeye hana dhambi na ni kitu gani hakitibiki?

Ayubu anasema kwamba Mungu amemwondolea haki zake.

Job 34:7-9

Ni katika ushirika watu gani ambao Elihu anausema kuwa Ayubu hushirikiana nao?

Anasema kuwa Ayubu huzunguka katika ushirika wa watu wanaofanya uovu.

Job 34:10-12

Elihu aliwaambia nini watu wenye ufahamu ambacho Mungu huwa hakifanyi?

hakika, Mungu hatendi uovu, wala Mwenye nguvu hajaipotosha haki.

Job 34:13-15

Ni gani Elihu alikisema kuwa kingetokea kama Mungu hataizulia mwenyewe roho yake na pumzi yake?

miili yote itateketea pamoja; mwanadamu angerudi mavumbini tena.

Job 34:16-17

Swali la Elihu linaonesha ni nani ambaye Ayubu alikuwa akimhukumu?

Anamaanisha kuwa Ayubu alikuwa akimhukumu Mungu ambaye ni mwenye haki na mwenye nguvu.

Job 34:18-20

Ni akina nani ambao Elihu anawasema kuwa walikuwa ni kazi ya mikono ya Mungu?

Viongozi, matajiri na masikini, wote ni kazi ya mikono ya Mungu.

Job 34:21-23

Elihu anasema ni kitu gani ambacho Mungu hukiona?

Elihu anasema kwamba Mungu huziona njia za watu na hatua zake zote.

Job 34:24-25

Mungu hufanya nini wakati wa usiku kwa watu wenye nguvu ambao anazijua njia zao na matendo yao?

huwatupa watu hawa wakati wa usiku; nao wameangamizwa.

Job 34:26-28

Je Mungu atafanya nini kwa wale wanaofanya matendo maovu kama wakosaji dhahiri na kukifanya kilio chao masikini kimfikie?

Mungu atawaua katika sehemu ya uwazi mbele za watu wengine.

Job 34:29-30

Je Mungu hutawala juu ya nani?

Mungu anatawala sawa sawa juu ya taifa na mtu pia,

Job 34:31-33

Ni kitu gani Elihu anakipendekeza ambacho Ayubu anapaswa akikubali kwa Mungu?

Elihu anapendekeza kwamba Ayubu alitakiwa kukubali kwamba yeye ni mwenye hatia na ya kwamba ametenda dhambi, lakini hataendelea kuifanya zaidi.

Job 34:34-35

Je watu wenye ufahumu watasema nini juu ya Ayubu?

Watasema kwamba Ayubu anazungumza bila maarifa na hekima

Job 34:36-37

Elihu anasema nini ambacho Ayubu anakiongeza kwa dhambi yake kwasababu ya kuongea kwake kama watu waovu?

Anasema kuwa Ayubu anaongeza uasi juu ya dhambi yake.

Job 35

Job 35:1-3

Ni kwa namna gani Elihu anamaanisha kwa Ayubu kujilinganisha na Mungu?

Elihu anamaanisha kwamba Ayubu anadhani kuwa hana hatia na ya kwamba yeye ni mwenye haki kuliko Mungu.

Job 35:4-5

Elihu anamwambia Ayubu na rafiki zake waangalie na kuona nini?

Elihu anawambia watazame na kuona anga

Job 35:6-8

Kuna athari gani za uovu wa Ayubu au haki yake kwa mtu mwingine?

Uovu wa Ayubu unaweza kumuumiza mtu na haki yake inaweza kumnufaisha mwana mwingine wa mtu.

Job 35:9-11

Kwanini watu wanalilia msaada kutoka katika mikono ya watu wenye nguvu?

Wanalilia msaada kwasababu ya matendo mengi ya uonevu.

Ni vitu gani ambavyo Elihu anavisema kwamba Mungu angevifanya kwa ajili ya watu ingawa hakuna hata mmoja anayeridhia?

Mungu hutoa nyimbo wakati wa usiku, ambaye hutufundisha sisi kuwa wenye hekima

Job 35:12-14

Kwanini Elihu alisema kwamba Mungu hatoi jibu wakati wanapomlilia kuomba msaada?

Elihu anasema kwamba Mungu hatia jibu wakati watu wanapomlilia kuomba msaada kwasababu ya kiburi cha watu waovu.

Job 35:15-16

Ni kitu gani Elihu anamshitakia Ayubu kukifanya anapofumbua kinywa chake.

Anasema Ayubu hufumbua kinywa chake kusema upumbavu na huongeza maneno bila maarifa

Job 36

Job 36:1-5

Elihu anakubali kuwa haki ni miliki ya nani?

Elihu anakubali kuwa haki ni mali ya Yeye aliyeifanya.

Job 36:6-7

Je Mungu hufanya nini kwao hao wanaoteswa?

Mungu hufanya yaliyo haki kwa wale wanaoteseka.

Mungu hufanya nini kwa wenye haki?

huwaweka juu ya viti vya enzi kama wafalme milele, nao wameinuliwa juu

Job 36:8-9

Je Mungu hufunua nini kwa hao waliofungwa minyororo na kunaswa katika kamba za mateso?

Huwafunuliwa yale waliyoyafanya, uovu wao na jinsi walivyoenenda kwa kiburi.

Job 36:10-12

Ni kitu gani kitatokea kwa kumsikiliza na kumwabudu Mungu?

wataishi katika mafanikio katika siku zao, na miaka yao katika hali ya kuridhika.

Kutatokea nini kwa watu wale wasiomsikiliza Mungu?

wataangamia kwa upanga; watakufa kwasababu hawana maarifa.

Job 36:13-14

Je watu wasiomjua Mungu ambao hutunza hasiria zao katika mioyo wala hawaombi msaada kwa Mungu?

Hawa hufa katika ujana wao; na maisha yao hukoma katika aibu.

Job 36:15-16

Elihu alisemaje juu ya Mungu kutumia uonevu na mateso?

Mungu huwainua watu walioonewa kwa njia ya mateso yao; hufungua masikio yao kwa njia ya uonevu wao

Je Elihu alisema nini kwamba Mungu angependa kufanya kwa ajli ya Ayubu?

Mungu angependa kumtoa Ayubu katika mateso na kumweka katika sehemu pana ambapo hakuna masumbufu

Job 36:17-18

Ni nini kilikuwa kimemjaa Ayubu?

Amejaa hukumu juu ya watu waovu

Ni vitu gani vinaweza kumpeleka Ayubu katika udanganyifu na kumgeuze atoke katika haki?

utajiri unaweza kumpeleka Ayubu katika udanganyifu na rushwa inaweza kumgeuza kutoka katika haki.

Job 36:19-21

Ni vitu gani ambavyo visingeweza kumsaidia Ayubu atoke katika taabu?

Utajiri wa Ayubu na nguvu zake haziwezi kumsaidia atoke katika mateso.

kwanini Elihu anasema kwamba Ayubu anajaribiwa kwa mateso?

Ayubu anajaribiwa kwa mateso ili kwamba akae mbali na dhambi.

Job 36:22-24

Ni kitu gani ambacho mtu yeyote hawezi kukisema kumhusu Mungu?

Hakuna yeyote anayeweza kusema kwamba Mungu ametenda mambo yasiyo ya haki.

Job 36:25-26

Ni kitu gani kuhusu Mungu ambacho hatuwezi kukihesabu?

Sisi hatuwezi kuhesabu namba ya miaka yake.

Job 36:27-29

Ni kwa namna gani Mungu huifanya mvua inyeshe?

Yeye huvuta matone ya maji ili kuyachuja kama mvua katka mvuke wake, ambayo mawingu yake huyamwaga chini na kuyandondosha kwa wingi kwa mwanadamu.

Job 36:30-31

Kwanini Elihu anasema kwamba Mungu hueneza mwanga na kufunika baharika kwa giza?

hueneza mwanga wake kumzunguka na kufunika mizizi ya bahari ili kuwapa chakula kwa wingi.

Job 36:32-33

Ni kitu gani kitachowaambia watu na mifugo juu ya dhoruba ijayo?

Muungurumo wa mwanga wa radi ukigonga shabaha yake huwaambia watu na wanyama juu ya dhoruba inayokuja.

Job 37

Job 37:1-3

Ni gani kinachoufanya moyo wa Elihu utetemeke?

Kelele za sauti ya Mungu na sauti kutoka katika mdomo wake huufanya moyo wa Elihu utetemeke.

Job 37:4-6

Mungu aliiambia barafu na mvua ifanye nini?

huiambia theluji, 'Angukeni juu ya dunia'; hali kadhalika kwa manyunyu ya mvua, 'Iweni manyunyu makubwa ya mvua.'

Job 37:7-9

kwanini Mungu huuzuia kila mkono wa kila mtu usifanye kazi?

Huuzuia mkono wa kila mtu usifanye kazi, ili kwamba watu wote aliowaumba wataona matendo yake

Ni kwa ajili ya sababu gani hayawani hujificha na kukaa katika mapango?

hayawani huenda na kujificha na kukaa katika mapango yao kwasababu ya dhoruba itakayokuja.

Job 37:10-11

Pumzi ya Mungu hutoa nini?

Pumzi ya Mungu hutoa barafu.

Job 37:12-13

Ni kwasababu gani Mungu hutoa mwongozo kwa mawingu na kuyafanya yafanye chochote anayoyaagiza?

Huyafanya haya yote yatokee; wakati mwingine hutokea kwa ajili ya kusahihisha, wakati mwingine kwa ajili ya nchi yake, na wakati mwingine ni kwa matendo ya agano la uaminifu.

Job 37:14-17

Elihu alitaka Ayubu aache na kufikiri juu ya mambo gani?

Alitaka Ayubu aache na kufikir juu ya matendo ya Mungu ya kushangaza.

Ni kitu gani hutokea wakati Mungu anaposhurutisha mapenzi yake katika mawingu?

Mungu hushurutisha mawingu na kuufanya mwanga wa radi ung'ae ndani yake

Job 37:18-22

Ni mfano/sura gani ambayo Elihu anaitumia kulielezea anga?

Anasema anga lina nguvu kama kioo cha chuma kigumu

Kwanini Elihu alisema kuwa yeye na wengine hawawezi kuweka hoja zao mbele za Mungu?

Hawawezi kuweka hoja zao mbele za Mungu kwasababu ya giza katika akili zao.

Job 37:23-24

Ni kitu gani ambacho Elihu anakisema kuwa Mwenye enzi hakifanyi kwa watu wake?

Mwenye enzi hawatesi watu.

Ni akina nani ambao Elihu alikuwa anasema kuwa Mwenye enzi hawaangalii?

Mwenye enzi huwa hawajali wale ambao ni wenye hekima katika akili zao wenyewe."

Job 38

Job 38:1-5

Yahweh alikuwa akiongea na Ayubu kutoka katika nini?

Yahweh aliongea na Ayubu kutoka katika dhoruba kali.

Ni kwa njia gani mtu huleta giza katika mipango ya Yahweh?

Ayubu alileta giza katika mipango ya Yahweh kwa njia ya maneno pasipo maarifa.

Yahweh alimwambia nini Ayubu wakati ule alipomwuliza maswalli?

Ayubu lazima ajifunge kiunoni mwake kama mwanaume na Yahweh atamwuliza maswali

Job 38:6-7

Ni vitu gani viliimba kwa pamoja na nani alipiga kelele za furaha wakati jiwe la pembeni lilipowekwa?

nyota za asubuhi ziliimba kwa pamoja na wana wote wa Mungu walipopiga kelele kwa furaha wakati jiwe la pembeni lilipowekwa.

Job 38:8-9

Yahweh analinganisha na nini kupasuka kwa bahari baada ya kuwa imefungu kwa milango?

Mungu analinganisha kupasuka kwa milango na kutoka katika tumbo.

Job 38:10-13

Ni kitu gani Yahweh alikiweka ili kuwa alama ya mpaka wa bahari ili kwamba inapotoka mbali na isiende zaidi?

Yahweh aliweka baharini makomeo yake na milango kuonesha mpaka wa bahari.

Job 38:14-18

Ni kwa namna gani dunia imebadilishwa katika mwonekano kama udongo unavyobadilika chini ya muhur?

Mwanga wa mapambazuko huibadili dunia ili kwamba vitu vyote juu yake visimame dhahiri kama kibindi cha nguo.

Job 38:19-21

Yahweh alisema nini katika kumkejeli Ayubu juu ya kukoswa kwake maarifa kuhusu njia ya kupumzika kwa mwanga na giza?

Yahweh alimkejeli kwa kusema bila shaka Ayubu anapaswa kujua hili kwasababu hesabu ya siku zake ni kubwa sana!

Job 38:22-24

Ni kwa sababu gani Yahweh anasema ametunza ghala kwa ajili ya barafu na mawe ya mvua?

Yahweh ametunza maghala haya kwa ajili ya siku za mateso na kwa ajili ya mapigano na vita.

Job 38:25-30

Kwanini Yahweh huifanya inyeshe katika jangwa pasipo na mtu?

Huifanya mvua inyeshe juu ya nchi kwa kusudi la kutimiza mahitaji ya mikoa iliyo kame na yenye ukiwa, na kuyastawisha majani mororo

Job 38:31-35

Ni kitu gani Yahweh alimwomba Ayubu kama anaweza kufanya kwa Kilimia na Orioni?

Anamwomba Ayubu kama anaweza kuzifunga minyororo Kilimia au kuvifungua vifundo vya Orioni.

Job 38:36-38

Ni kitu gan hutokea kwa mavumbi na mabonge ya nchi wakati Yahweh anapomwaga maji juu yake?

Mavumbi anapoungana kuwa kitu kigumu na mabonge ya dunia yanaposhikama kwa pamoja

Job 38:39-40

Ni sehemu gani ambayo wana wa simba hukaa na kulala katika hali ya kusubiria?

Hukwaruza kwaruza katika pango lao na kukaa katika kificho ili kulala katika hali ya kuvizia

Job 38:41

Kwanini watoto wa kunguru hutangatanga?

Wanatanga tanga kwa ya kukoswa chakula.

Job 39

Job 39:3-4

Ni kitu gani hutokea kwa watoto wa paa baada ya kukua katika uwanda?

Watoto wao huwa na nguvu na kukua katika uwanda wa wazi; hutoka nje na hawarudi tena

Job 39:5-6

Ni wapi Yahweh amefainya nyumba ya punda?

Ameifanya nyumba yake katika Araba, na nyumba yake katika nchi ya chumvi.

Job 39:7-8

Punda mwitu hupata chakula wapi?

Hutembeatembea juu ya milima kama malisho yake; huko hutafuta kila mmea ulio wa kijani kwa ajili ya kula.

Job 39:9-12

Ni kitu gani Yahweh anachomwomba Ayubu amfanye nyati wafanye kwa kamba?

Anamwomba Ayubu kama kwa kamba anaweza kumfanya nyati alime mtaro au kuchimba bonde kwa ajili yake.

Job 39:13-15

Ni kwa kitu gani Mbuni hupunga kwa majivuno?

Mbawa za mbuni hupunga kwa majivuno.

Mbuni hufanya nini kwa miguu yake?

Huyaacha mayai yake katika nchi na huyaacha yapate joto katika mavumbi.

Job 39:16-18

Kwanini mbuni hawaogopi kwamba kazi yao inaweza kuwa ni bure?

Mungu amemnyima hekima na hajampa ufahamu wowote.

Yahweh anasema nini juu ya kile mbuni anachokifanya wakati anapokimbia?

huwacheka kwa dharau farasi na mpanda farasi wake.

Job 39:19-20

Ni kitu gani huvika shingo ya farasi?

Manyoya yanayoshuka shingoni huvika shingo yake.

Job 39:21-23

Ni kwa namna gani farasi hutikia kwa upanga?

Hageuki nyuma kutoka katika upanga.

Job 39:24-26

Farasi hataweza kufanya nini katika sauti za tarumbeta?

Hawezi kusimama katika sehemu moja.

Job 39:27-30

Ni sehemu gani tai hufanya kiota chake na nyumba yake?

Hufanya kiota katika sehemu za juu, na nyumba yake katika vilele vya majabali, na ngomeni.

Job 40

Job 40:3-5

Ayubu alifanyaje kuonesha kwamba alikuwa mtu ambaye hakuwa na umuhimu katika kumjibu Yahweh?

Ayubu aliuweka mkono wake juu ya mdomo wake

Job 40:6-7

Yahweh alimjibu Ayubu kutoka katika kitu gani?

Yahweh akamjibu Ayubu kutoka katika dhoruba kali

Yahweh alimwambia Ayubu afanye nini ili kujiandaa amjibu Yahweh?

Alimwambia ajifunge sasa mkanda kiunoni mwako kama mwanaume

Job 40:8-9

Kwanini Yahweh alisema kwamba Ayubu alikuwa akimhukumu Yahweh?

Alisema kuwa Ayubu alimhukumu Yahweh ili kwamba Ayubu aweze kusema alikuwa yuko sawa.

Job 40:10-11

Yahweh alimtia changamoto ajivike mwenyewe kwa kitu gani?

Alimtia changamoto Ayubu katika kujivika mwenye kwa utukufu, utu, heshima na enzi.

Job 40:12-14

Yahweh alimwambia nini Ayubu afanye kwa watu waovu?

Yahweh alimwambia Ayubu awakanyage chini watu waovu mahali wanaposimama

Job 40:15-16

Kiboko anakula nini?

Kiboko hula majani kama ng'ombe

Job 40:17-18

Mkia wa kiboko unafanana na nini?

Mkia wake ni kama mti wa mwerezi

Job 40:19-21

Ni nani aweza kumshinda kiboko?

Ni Mungu tu anaweza kumshinda kiboko.

Kiboko hulala wapi?

Hujilaza chini ya mimiea ya kivuli katika makao ya mianzi, na katika bwawa la matope.

Job 40:22-24

Kiboko hufikiri nini wakati mto unapofurika na Yordani inapojaa?

Hatikisiki na ni mwenye kujiamini.

Job 41

Job 41:1-3

Yahweh anamwomba Ayubu atuumie kitu gani kama anaweza kumvua mamba?

Yahweh anamwomba Ayubu kama anaweza kumvua mamba kwa ndoano ya samaki

Job 41:4-6

Ni kitu gani Yahweh anamwomba Ayubu kama wavuvi wangefanya pamoja na Mamba?

Anamwomba Ayubu kama wavuvi wangeweza kumfanyia biashara mamba na kumgawanya ili kufanya biashara miongoni mwa wafanya biashara

Job 41:7-9

Kutatokea nini kama mtu ataweka mkono wake juu ya mamba?

Kama mtu ataweka mkono wake juu yake mara moja, ataikumbuka vita na hataendelea kufanya hivyo tena

Job 41:10-12

Kwa kuwa hakuna mtu mkali ambaye anawea kuthubutu kumtikisa mamba, Ni nani basi awezaye kusimama mbele ya Yahweh?

Hakuna aliye mkali ambaye aweza kuthubutu kumtikisa mamba, na hivyo basi hakuna awezaye kusimama mbele ya Yahweh.

Job 41:13-15

Ni kwa namna gani zaidi Yahweh anauelezea mdomo wa mamba?

Anasema kuwa milango ya uso wake imezungukwa na meno yake ambayo ni ya kutisha.

Job 41:16-18

Je ni ukaribu gani magamba katika mgongo wa mamba yamesogeleana?

Moja li karibu na jingine na ya kuwa hakuna hewa inaweza kupita katikati yake.

Yahweh anasema macho ya mamba yanafananaje?

macho yake ni kama kope za mapambazuko ya asubuhi

Job 41:19-21

Katika mdomo wa mamba hutoka nini?

Ndani ya mdomo wake hutoka miali ya mwanga, chembe za moto huruka nje

Moshi utokao ndani ya pua za mamba unafananaje?

Katika pua zake hutoka moshi kama chungu kinachotokota juu ya moto ambao umechochewa ili uwe na joto sana.

Job 41:22-24

Je moyo wa mamba unafanana na nini?

Moyo wake ni mgumu kama jiwe la chini la kusagia.

Job 41:25-27

Je miungu hufanya nin wakati mamba anaposimama mwenyewe juu?

miungu huogopa na hurudi nyuma

Hutokea nini wakati upanga, mkuki au silaha iliyochongoka inapompiga mamba?

Haziwezi kufanya lolote kwake.

Je mamba hufikiri nini juu ya chuma na shaba?

Yeye hufikiri juu ya chuma kana kwamba ni majani makavu na hufikiri juu ya fedha kana kwamba ni ubao uliooza

Job 41:28-30

Je mamba huacha alama za aina gani?

huacha alama zilizosambaa katika udongo kana kwamba alikuwa ni chombo cha kusagia.

Job 41:31-32

Je kilindi hukifanya kifanye nini?

Yeye hukifanya kilindi kichemke kama chungu cha maji ya moto

Job 41:33-34

kwanini mamba hana kitu cha kulinganisha hapa duniani?

yeye ameumbwa kuishi pasipo hofu

Job 42

Job 42:1-3

Ayubu alikubali nini kwamba alikuwa amekwisha kusema?

Alikuwa amekwisha kuzungumza mambo ambayo alikuwa hayajui, mambo magumu sana kwake kuyaelewa, ambayo hakuyajua.

Job 42:4-6

Ni kwa namna gani Ayubu alimjibu Yahweh baada ya kumwona kwa macho yake?

Ayubu alijidharau mwenyewe na kutubu kwa mavumbi na majivu

Job 42:7-9

Yahweh alisema nini juu ya Elifazi na rafiki zake wawili kwamba walikuwa wamefanya mabaya?

Walikuwa hawajasema mambo ya kweli kumhusu Yahweh kama Ayubu alikuwa amefanya.

Yahweh alimwambia nini Elifazi kutoa kama sadaka?

Alimwambia Elifazi kuchukua mahafari saba na mabeberu saba ili atoe kwa ajili yao wenyewe kama sadaka za kuteketezwa.

Ni maombi ya nani amnayo Yahweh alisema kuwa atayapokea?

Yahweh alisema angeyapokea maombi ya Ayubu.

Job 42:10-11

Ni nini kilitokea baada ya Ayubu kuwaombea marafiki zake?

Yahweh alirejeza bahati yake, na alimjalia mara mbili ya kile alichokimiliki hapo awali.

Job 42:12-14

Ni kwa namna gani Yahweh alimbariki Ayubu katika siku zake za maisha yake?

Yahweh alimbariki Ayubu zaidi kuliko sehemu ya kwanza ya maisha ya Ayubu.

Ni watoto wangapi wa kiume na wa kike ambao Yahweh alimpa Ayubu?

Alikuwa na wana saba na mabinti watatu.

Job 42:15-17

Ni kitu gani cha tofauti kilikuwa kwa mabinti zake Ayubu?

Katika nchi yote hawakupatikana wanawake wazuri kama mabinti wa Ayubu. Baba yao aliwapa urithi miongoni mwa kaka zao