Kiswahili: translationQuestions

Updated ? hours ago # views See on DCS Draft Material

Daniel

Daniel 1

Daniel 1:1-2

Ni lini Nebukadneza mfalme wa Babeli alienda Yerusalemu ili kuuzunguka mji na kuuzuia mahitaji yake?

Nebukadneza alienda Yerusalme katika mwaka wa tatu wa utawala wa Yehoyakimu mfalme wa Yuda.

Ni nani alimpa Nebukadneza ushindi dhidi ya Yehoyakimu?

Bwana ndiye aliyempa Nebukadneza ushindi dhidi ya Yehoyakimu.

Daniel 1:3-5

Mfalme alimwambia Ashipenazi afanye nini?

Mfalme alimwambia Ashipenazi kuwaingiza baadhi ya watu wa Israeli, watu kutoka familia ya kifalme na za kiungwana.

Ni aina gani ya vijana ambao mfalme aliwataka waletwe Babeli?

Mfalme aliwataka vijana wasio na waa, wenye mwonekano wa kuvutia, wenye maarifa katika hekima yote , wakijawa na ufahamu na weledi, wenye sifa ili kutumika katika ikulu ya mfalme.

Vijana hawa walitakiwa kulishwa nini?

Walitakiwa kulishwa fungu la vyakula vizuri vya wafalme vya kila siku pamoja na divai ya mfalme.

Daniel 1:6-7

Ni majina gani waliyokuwa nayo Vijana kutoka Israeli na ni majina gani waliyopewa na Afisa mkuu?

Majina ya baadhi ya vijana hawa na majina waliopewa na Afisa mkuu. Danieli aliitwa Belteshaza, Hanania akaitwa Shadraka, Mishaeli akaitwa Meshaka, na Azaria aliitwa Abedinego.

Daniel 1:8-10

Danieli alikusudia nini akilini mwake?

Danieli alikusudia katika akili yake kwamba asingejitia unajisi yeye mwenyewe kwa chakula cha mfalme au kwa divai ya mfalme.

Je Afisa mkuu alimjibuje Daniel baada ya kumwomba ruhusa kwamba asijitie unajisi kkwa chakula na divai ya mfalme?

Afisa Mkuu alimwambia Danieli kwamba alikuwa anamwogopa mfalme, maana mfalme alikuwa ameagiza aina ya chakula na vinywaji ambavyo Danieli alitakiwa kula na ya kwamba mfalme angekitwaa kichwa cha Afisa mkuu kama angemwona Danieli akionekana vibaya kuliko vijana wengine wa rika la Danieli.

Daniel 1:11-13

Danieli alimwomba nini msimamizi aliyekuwa amewekwa juu ya Danieli, Hanania, Mishaeli na Azaria?

Danieli alimwomba msimamizi awajaribu kwa siku kumi kwa kuwalisha mboga tu na maji ya kunywa na mwishoni mwa siku kumi awalinganishe na vijana wengine ambao walikuwa vyakula vya mfalme na kisha awahudumia kwa kufuata kile alichokiona.

Daniel 1:14-16

Baada ya kukubali kuwajaribu, msimamizi aligundua nini baada ya siku kumi wakati alipowalinganisha akina Danieli, Hanania, Mishaeli na Azaria na vijana wengine?

Msimamizi aligundua kwamba mwonekano wa Danieli, Hanania, Mishaeli na Azaria ulikuwa mzuri na wenye afya, na ya kwamba walikuwa wazuri walionawili kuliko vijana wengine wote waliokula chakula cha mfalme.

Daniel 1:17-18

Mungu aliwapa nini akina Danieli, Hanania, Mishaeli na Azaria?

Mungu aliwapa uelewa, ufahamu katika maandiko na hekima, na Danieli angeweza kufahamu aina zote za maono na ndoto.

Daniel 1:19-21

Mfalme aligundua nini wakati alipoongea na kundi la vijana?

Mfalme aligundua kwamba hapakuwa na mtu wa kumlinganisha na Danieli, Hanania, Mishaeli na Azaria. Katika kila swali la hekima ambalo mfalme aliwauliza, aligundua kwamba walikuwa vizuri mara kumi kuliko waganga wote na wale waliojidai kusema na wafu, waliokuwa katika ufalme wake wote.

Danieli alikuwa Babeli kwa muda gani?

Danieli alikuwa huko hadi mwaka wa kwanza wa Mfalme Koreshi.

Daniel 2

Daniel 2:1-4

Ni wakati gani Nebukadneza aliota ndoto ambazo zilimsumbua akili zake na hivyo hakuweza kulala?

Hii ilitokea wakati wa mwaka wa pili wa utawala wake.

Kwanini mfalme aliwaita waganga, wachawi na wale wenye kuongea na wafu?

Mfalme aliwataka watu hawa ili awaambia juu ya ndoto yake.

Daniel 2:5-9

Ni kitu gani halisi ambacho mfalme aliwataka watu wenye hekima wakifanye?

Mfalme aliwataka watu wenye hekima kumfunulia ndoto na pia kumtafsiria mfalme ndoto.

Mfalme alisema kungetokea nini kwa watu wenye hekima kama watashindwa kumwambia mfalme ndoto yake na kumtafsiria?

Mfalme alisema kama watashindwa, miili ya watu wenye hekima ingekatwa vipande na nyumba zao zingefanywa vichuguu vya uchafu.

Mfalme alisema angefanya nini kwa mtu au watu ambao wangeifunua ndoto na kuitafsiri kwa ajili yake?

Mfalme alisema angempa mtu au watu zawadi, thawabu, na heshima kubwa.

Daniel 2:10-11

Ni nani ambaye wenye hekima walimsema kwamba angeweza kufanya kile alichokitaka mfalme kuhusu ndoto yake?

Watu wenye hekima walisema kwamba hakuna mtu juu ya nchi ambaye anaweza kutimiza matakwa ya mfalme, isipokuwa miungu inaweza kufanya hivyo.

Daniel 2:12-13

Mfalme aliagiza nini baada ya watu wenye hekima kumjibu Nebukadneza?

Mfalme aliagiza kwamba wale wote waliojulikana kwa hekima zaowauawe.

Daniel 2:14-18

Arioki ni nani?

Alikuwa ni Kamanda wa walinzi wa mfalme, ambaye mfalme alimweka ili kumwua kila mtu aliyekuwa na hekima katika Babeli.

Ni kwa namna gani Danielli aliweza kuongea na Arioki, wakati alipomwendea Danieli?

Danieli alimjibu Arioki kwa adabu na hadhari. na pia alimwambia Arioki kwanini amri ya mfalme ni ya haraka sana.

Danieli aliomba nini baada ya kuongea na Arioki?

Danielli aliingia ndani na aliomba muda wa kuonana na mfalme ili kwamba aweze kuwasilisha tafsiri kwa mfalme.

Daniel 2:19-22

Je Danieli alifanya nini baada ya siri kufunuliwa kwake?

Danieli alimsifu Mungu wa mbinguni.

Daniel 2:23

Danieli alimshukuru Mungu wa baba zake kwa ajili ya kitu gani?

Danieli alimshukuru Mungu wa baba zake kwa ajili ya hekima na nguvu za baba zake alizokuwa amepewa.

Daniel 2:24-26

Danieli alienda kumwona nani baada ya siri kufunuliwa kwake?

Danieli alienda ndani kumwona Arioki.

Danieli alimwambia nini Arioki?

Danieli alimwambia Arioki asiwaue watu wenye hekima katika Babeli. Danieli alimwambia Arioki amsindikize mbele za Mfalme ili Danieli aweze kumwambia mfalme maana ya ndoto yake.

Daniel 2:27-28

Baada ya Danieli kufikishwa kwa mfalme, Danieli alisema ni nani angeweza kuifunua siri ambayo Mfalme aliihitaji?

Danieli alisema kuwa kuna Mungu ambaye anaishi mbinguni, yeye hufunua siri.

kwa ujumla Danieli alisema ndoto ya mfalme ilihusu nini ?

Danieli alisema kuwa ndoto ya mfalme ilihusu kile ambacho kingetokea katika siku zijazo.

Daniel 2:29-30

Kwanini ndoto ilifunuliwa kwa Danieli?

Ndoto ilifunuliwa kwa Danieli ili kwamba Mfalme aweze kufahamu maana na kujua mawazo yaliyo ndani yake mwenyewe.

Daniel 2:31-33

Sanamu ambayo mfalme aliiona ilikuwa inaonekanaje?

Sanamu ilikuwa ni kubwa na ilikuwa na kichwa cha dhahabu, kifua na mikono ya fedha, sehemu za kati na mapaja yalikuwa ya shaba, miguu yake ya chuma na sehemu za chini za miguu yake ilikuwa kwa sehemu chuma na sehemu udongo.

Daniel 2:34-35

Ni kitu gani kilitokea kwa sanamu ambayo mfalme aliiona?

Mfalme aliona jiwe lililokatwa, lakini si kwa mikono ya watu. Jiwe liliipiga miguu ya sanamu na sanamu yote ilivunjika vipande vipande ambavyo vilichukuliwa mbali na upepo.

Ni nini kilitokea kwa jiwe ambalo liliipiga sanamu?

Jiwe ambalo liliipiga sanamu lilikuwa mlima mkubwa na ambao ulijaza dunia yote.

Daniel 2:36-43

Kichwa cha dhahabu alikuwa ni nani?

Mfalme Nebukadneza alikuwa ndiye kichwa cha dhahabu.

Daniel 2:44-45

Mungu wa mbinguni atafanya nini kaika siku za ufalme ambao kwa nusu ni chuma na nusu ni udongo?

Katika siku hizo Mungu wa mbinguni atauweka ufame ambao hautaangamizwa au kushindwa na mtu mwingine.

Daniel 2:46-47

Nebukadneza aliagiza Danieli afanyiwe nini baada ya kumaliza kumwambia Mfalme ndoto na maana yake?

Mfalme aliagiza sadaka na manukato yatolewe kwa ajili ya Danieli.

Nebukadneza alisema nini juu ya Mungu wa Danieli?

Danieli alisema kwamba Mungu wa Danieli ni Mungu wa miungu, Bwana wa wafalme na ambaye hufunua mafumbo.

Daniel 2:48-49

Nebukadneza alifanya nini baada ya Danieli kutoa ombi lake kwa mfalme?

Mfalme aliwateua akina Shadraka, Meshaki na Abedinego kuwa watawala juu ya jimbo la Babeli.

Daniel 3

Daniel 3:1-2

Je sanamu ile iliyosimamishwa na Nebukadneza katika uwanda wa Dura ilikuwa na ukubwa gani?

Sanamu ilikuwa na urefu wa dhiraa sitini na upana dhiraa sita

Daniel 3:3-5

Ni akina nani walihudhuria katika uwekaji wakfu wa sanamu ambayo Nebukadneza alikuwa ameiweka?

Magavana wa majimbo, magavana wa mikoa, na magavana wa vijiji, pamoja na washauri, wahasibu, waamuzi, mahakimu, na maafisa wa juu wa majimbo walikusanyika kwa pamoja katika uzinduzi wa sanamu ambayo Nebukadneza aliyokuwa ameiweka

Je Nebukadneza aliwataka watu waliohudhuria wafanye nini?

Aliwataka wale waliohudhuria kuanguka chini na kuisujudia sanamu ya dhahabu baada ya kusikia sauti ya pembe, filimbi, ala za muziki, zeze, vinubi na zumari na aina zote za muziki.

Daniel 3:6-7

Mfalme aliagiza kitu gani kitokee kwa wale ambao hawakuanguka na kuiabudu sanamu baada ya kusikia ala zote za muziki?

Mfalme alisema kwamba wale wote ambao wasingeanguka chini na kuabudu, kwa wakati huo huo wangetupwa katika tanuru liwakalo moto.

Daniel 3:8-10

Ni nani alileta mashitaka kinyume na akina Shadraka, Meshaki na Abedinego?

Baadhi ya Wakaldayo walikuja na kuleta mashitaka dhidi yao.

Daniel 3:11-15

Ni nani hakuanguka chini na kuibudu sanamu?

Baadi ya Wayahudi ambao majina yao ni Shadraka, Meshaki, na Abednego, hawataiabudu, kuitumikia wala kuisujudia wenyewe sanamu ya dhahabu ambayo umeiweka

Daniel 3:16-18

Je ni jibu gani ambalo wakina Shadraka, Meshaki na Abedinego walimwambia mfalme baada ya mfalme kulirudia agizo la kuanguka chini na kuiabudu sanamu, na matokeo yake kama mtu hataitii amri ya mfalme?

Shadraka, Meshaki na Abedinego walimjibu kwa kusema kwamba Mungu wao angeweza kuwalinda salama na kuwaokoa kutoka katika tanuru liwakalo moto. Bali kama sivyo, wasingeweza kuiabudu miungu ya Nebukadneza au kuisujudia sanamu.

Daniel 3:19-20

Nebukadneza aliamuru nini kuwahusu akina Shadraka, Meshaki na Abedinego?

Aliagiza kuwa tanuru lichochewe ukali mara saba zaidi kuliko lilivyokuwa kawaida. 20Kisha aliwaamuru baadhi ya watu wenye nguvu katika jeshi lake kuwafunga Shadraka, Meshaki na Abednego na kuwatupa katika tanuru liwakalo moto

Daniel 3:21-23

Ni kitu gani kilitokea kwa Shadraka, Meshaki na Abedinego na kwa watu wale waliowatupa katika tanuru?

Miali ya moto iliwaua watu waliowatupa Shadraka, Meshaki, na Abedinego. 23Hawa wanaume watatu, Shadraka, Meshaki, na Abednego, waliangukia katika tanuru liwakalo moto wakali wamefungwa.

Daniel 3:24-25

Ni kitu gani kilichomshangaza Nebukadneza na kumfanya asimame haraka?

Nebukadneza mfalme alishangazwa na alisimama haraka kwasababu aliwaona watu wanne, ambao hawajafungwa, wakitembea katika moto, na walikuwa hawajadhurika na mng'ao wa mtu wa nne ulikuwa kama mwana wa miungu.

Daniel 3:26-28

Ni kitu gani ambacho watu walikuwa hapo walikiona kuhusu akina Shadraka, Meshaki na Abedinego baada ya kutolewa kutoka katika moto?

Watu waliokuwa hapo waligundua kwamba moto ulikuwa haujadhuru miili yao, nywele katika vichwa vyao hazikuungua; mavazi yao yalikuwa hayajaharibiwa; na hawakuwa na harufu ya moto.

Daniel 3:29-30

Ni agizo gani ambalo Nebukadneza alilipitisha baada ya tukio la Shadraka, Meshaki na Abedinego na tanuru la moto?

Nebukadneza aliagiza kwamba kila mtu, taifa au lugha watakaosema neno lolote kinyume na Mungu wa Shadraka, Meshaki na Abedinego wangekatwa vipande, na nyumba zao zingefanywa kuwa vichuguu vya uchafu kwasababu hakuna mungu mwingine anayeweza kuokoa kama yeye.

Mfalme aliwafanyia nini akina Shadraka, Meshaki na Abedinego?

Nebukadneza, Mfalme, aliwapandisha cheo akina Shadraka, Meshaki na Abedineg katika jimbo la Babeli.

Daniel 4

Daniel 4:1-3

Nebukadneza aliituma amri yake kwa nani?

Mfalme Nebukadneza aliituma amri hii kwa watu wote, mataifa, na lugha walioishi katika nchi.

Je Nebukadneza alisema nini kuhusu Mungu aliye juu?

Nebukadneza alisema hivi juu ya Mungu aliye juu, "Ni kwa namna gani Ishara zake ni kubwa, na ni kwa namna gani maajabu yake yana nguvu! Ufalme wake ni ufalme unaodumu milele, na utawala wake hudumu kizazi hadi kizazi."

Daniel 4:4-6

Ni kitu gani kilichomfanya Nebukadneza aogope?

Ndoto ilimfanya Nebukadneza kuwa mwoga.

Kwanini Nebukadneza aliwaita waletwe mbele yake watu wote wenye hekima katika Babeli?

Nebukadneza aliwataka watu wenye hekimma katika Babeli waje na kumtafsiria ndoto yake.

Daniel 4:7-9

Danieli alipewa jina gani la Kibabeli na ni nafasi gani Danieli alikuwa nayo katika ufalme wa Nebukadneza?

Jina la Danieli la Kibabeli lilikuwa ni Belteshaza na alishika nafasi ya "mkuu wa wachawi"

Ni nani ambaye Nebukadneza alimwamini kuwa alikuwa na uwezo wa kutafsiri ndoto yake?

Nebukadneza alimwamini Danieli kuwa angeweza kumtafsiria ndoto yake, kwa kuwa Nebukadneza alisema kuwa katika Danieli ..."roho ya miungu mitakatifu iko ndai yako na hakuna siri ngumu kwako."

Daniel 4:10-12

Ni kitu gani ambacho Nebukadneza alikiona katika sehemu ya kwanza ya ndoto yake?

Nebukadneza aliona mti mkubwa, wenye nguvu, na mzuri ambao ulifika mbinguni, uliweza kuonekana kutoka miisho ya dunia yote. Majani yake yalikuwa mazuri, matunda yake yalikuwa ni mengi, na juu yake kulikuwa na chakula kwa ajili ya wote. Wanyama wa mwituni walipata kivuli chini yake, na ndege wa angani waliisha katika matawi yake. Viumbe vyote hai vililishwa katika mti huo.

Daniel 4:13-14

Ni kitu gani ambacho mjumbe mtakatifu kutoka mbinguni alisema juu ya kitu cha kufanya kwa mti?

Mjumbe mtakatifu alisema kuukata mti, kuyakata matawi yake, kuyapukutisha majani na kuyasambaza matunda yake.

Daniel 4:15-16

Ni kitu gani kilipaswa kufanyika kwa kisiki cha mti?

Kisiki kilitakiwa kubaki katika nchi kikiwa kimefungwa na fungu la chuma na shaba. Kilowanisheni kwa umande. Kiacheni kiishi pamoja na wanyama. Akili yake na ibadilishwe kutoka akili ya kibinadamu, na apewe akili ya mnyama mpaka ipite miaka saba

Daniel 4:17-19

Kusudi la kufanya hivi kwa mti lilikuwa ni nini katika ndoto ya Nebukadneza?

Kusudi lilikuwa ni kwamba wale ambao wako hai wangejua kwamba Mungu aliyejuu hutawala juu ya falme za watu na huwapa kila mtu amtakaye na kumweka juu yake.

Daniel 4:20-23

Danieli alisemaje kuwa mti huu alikuwa ni nani kulingana na ndoto ya Nebukadneza?

Danieli alisema kuwa mti ule alikuwa ni Nebukadneza.

Daniel 4:24-25

Je ni kitu gani kingetoka kwa Nebukadneza mpaka akubali kuwa Mungu aliye juu anatawala juu ya falme zote na ya kwamba humpa yeyote amtakaye?

Nebukadneza alifukuzwa kutoka miongoni mwa watu . Angeishi porini na wanyama wa porini na kula majani kama ng'ombe , na kulowanishwa kwa umande utokao mbinguni.

Je hii ingechukua muda gani kabla ya Nebukadneza hajakubali kwamba Yeye aliye juu anatawala juu ya falme za watu naye humpa yeyote amtakaye ili azitawale?

Miaika saba ilitakiwa kupita ndipo Nebukadneza atakubali kwamba Yeye aliyejuu anatawala juu ya falme zote za watu na ya kwamba Yeye humpa kila mtu amtakaye.

Daniel 4:26-27

Danieli alimpa ushauri gani Nebukadneza baada ya kumtafsiria ndoto?

Danieli alimwambia Nebukadneza aache kutenda dhambi kufanya yale yaliyo ya haki. Alimwambia pia Nebukadneza ageuke na kuacha dhambi zake kwa kuonesha rehema kwa walioonewa.

Daniel 4:28-34

Ilichukua muda gani kabla ya tafsiri ya ndoto ya Nebukadneza haijaanza kutokea?

Mambo haya yote yalianza kutokea miezi kumi na miwili baada ndoto yake.

Daniel 4:35

Nebukadneza alifanya nini baada ya kurejeshewa utimamu wake?

Nebukadneza alimsifu Yeye aliye juu, alikubali utawala wake wa milele na kukiri kwamba Yeye aliye juu hufanya chochote kinachopendeza matakwa ya Yeye aliye juu.

Daniel 4:36-37

Ni kitu gani kilitokea katika ufalme wa Nebukaneza?

Ufalme ulirudishwa tena kwake.

Ni maelezo gani ya mwisho ambayo Nebukadneza aliyatoa kuhusus Mfalme wa mbinguni?

Maelezo yake yalikuwa: "mimi Nebukadneza, ninamsifu, ninamtukuza na kumheshimu mfalme wa mbinguni, kwa kuwa matendo yake yote ni ya haki, na njia zake ni za adili. Anaweza kuwashusha wale wanaotembea katika kiburi chao wenyewe."

Daniel 5

Daniel 5:1-2

Ni nani ambao mfalme Belshaza aliwafanyia sherehe kubwa?

Alifanya sherehe kubwa kwa ajili ya maelefu ya wakuu wake wa kuheshimiwa.

Belshaza alikuwa ni nani?

Alikuwa ni mwana wa Nebukadneza.

Daniel 5:3-4

Walitumia vyombo gani katika kunywea divai katika sherehe hii?

Walitumia vyombo dhahabu vilivyokuwa vimechukulia katika hekalu, nyumba ya Mungu huko Yerusalemu.

Watu katika sherehe walikuwa wakifanya nini wakati walipokuwa wanakunywa divai?

Waliisifu miungu yao iliyofanywa kwa dhahabu na fedha, shaba, chuma, mbao na mawe.

Daniel 5:5-6

Kilitokea nini wakati watu walipokuwa wanakunywa divai na kuisifu miungu yao?

Vidole vya mkono wa mtu vilitokea mbele ya kinara cha taa na kuandika ukutani katika ikulu ya mfalme

Mfalme aliitikiaje mara baada ya kuuona mkono?

Uso wa mfalme ulibadilika na mawazo yake yalimtisha, miguu yake haikuweza kumfanya asimame, na magoti yake yalikuwa yakigongana kwa pamoja

Daniel 5:7-12

Mfalme aliahidi nini kwa mtu ambaye angeweza kuyaeleza maandishi yaliyo ukutani na maana yake?

Mfalme aliahidi kwamba yeyote atakayeyaeleza maandishi haya na maana yake atavikwa nguo za zambarau na atavikwa na mkufu wa dhahabu shingoni mwake. Naye atakuwa mtawala wa tatu wa juu kwa mamlaka katika ufalme

Daniel 5:13-16

Danieli alikuwa na sifa gani kutokana na kile ambacho mfalme alikuwa amekisikia kumhusu Danieli?

Mfalme alimwambia mfalme kuwa alikua amesikia habari kumhusu yeye, kwamba roho ya miungu iko ndani yake, na ya kwamba mwanga na ufahamu na hekima bora inapatikana ndani yake.

Daniel 5:17-19

Danieli alijibuje baada ya kuwa ameambiwa juu ya thawabu ambazo angepokea kwa kusoma maandishi na kueleza maana yake?

Danieli alimweleza mfalme, " Zawadi yako na iwe kwa ajili yako mwenyewe, na thawabu yako na umpe mtu mwingine. Hata hivyo, mfalme, nitakusomea maandishi na nitakwaambia maana."

Daniel 5:20-21

Kwanini Nebukadneza alishushwa chini kutoka katika kiti chake cha kifalme na kwanini enzi iliondolewa kutoka kwake?

Nebukadneza alipoteza enzi yake na kiti cha enzi cha kifalme kwasababu alikuwa na kiburi na roho yake ilifanywa kuwa mgumu na kwasababu hiyo alitenda kwa kiburi, alishushwa kutoka kiti chake cha enzi cha kifalme, na waliiondoa enzi yake.

Daniel 5:22-24

Ni yapi yalikuwa ni mashitaka ya Danieli kwa Belshaza?

Danieli alisema "Belshaza, haujaunyenyekeza moyo wako, ingawa aliyajua haya yote. Umejiinua mwenyewe kinyume cha Bwana wa mbinguni ambaye anashikilia pumzi yake katika mkono wake na ambaye alijua njia zake zote."

Daniel 5:25-28

Maana ya maandishi hayo juu ya ukuta ilikuwa ni nini?

Maana ilikuwa kama ifuatavyo: Mungu ameshauhesabu ufalme wa Belshaza na kuufikisha mwishoni. Belshaza amepimwa katika skeli na akakutwa kuwa hana vitu, Ufalme Belshaza uligawanyika na wamepewa

Daniel 5:29-31

Kilitokea nini usiku huo baada ya Danieli kumaliza kutoa maana za maandishi kwa Nebukadneza?

Usiku huo Belshaza, Mfalme wa Babeli, aliuawa, na Dario Mmedi aliuchukua ufalme.

Je Dario Mmede alikuwa na umri gani wakati alipouchukua ufalme?

DarioMmede alikuwa na umri wa miaka sitini na mbili wakati alipoutwaa ufalme.

Daniel 6

Daniel 6:1-3

Ni akina nani ambao Dario aliwaweka juu ya ufalme?

Aliweka magavana wa majimbo 120 pamoja na watawala wakuu watatu juu yao.

Ni nani alikuwa miongoni mwa watawala wakuu watatu?

Daniel alikuwa mmoja wao.

Kwanini watawala wakuu watatu walichaguliwa?

Hawa watawala waliwekwa ili waweze kuwasimamia magavana wa majimbo, ili kwamba mfalme asipate hasara

Mfalme alikuwa amepanga kumweka nani juu ya ufalme wote?

Mfalme alikuwa akipanga kumweka juu ya ufalme wote

Daniel 6:4-5

Kwanini watawala wengine wakuu na magaana wa majimbo hakuweza kuona ufisadi au kushindwa katika majukumu yake katika ufalme wala hakuna kosa au uzembe uliopatikana ndani yake?

Hatukuweza kupata sababu yoyote ya kumshitaki huyu Danieli kwasababu alikuwa mtakatifu.

Ni sehemu gani nyingine katika maisha yake ambayo watawala wengine wakuu na magavana wa majimbo walidhani wangeweza kupata kitu cha kumshitaki Danieli?

Walifikiri kwamba wangetafuta kitu fulani dhidi yake kuhusiana na sheria za Mungu wake

Daniel 6:6-9

Magavana wa majimbo na watawala wengine walimshauri mfalme afanye nini?

Walimshauri Dario kupitisha amri na kuitekeleza, ili kwamba mtu yeyote anayefanya dua kwa mungu yeyote au mtu kwa siku thelathini, isipokuwa wewe mfalme, mtu huyo lazima atupwe katika tundu la simba.

Daniel 6:10-12

Je Danieli alifanya nini baada ya kujua kuwa amri imekwisha kusainiwa na nyaraka zimesainiwa kuwa sheria?

Danieli alipojua kuwa nyaraka imekwisha kusainiwa kuwa sheria, alienda ndani ya nyumba yake (madirisha yake katika chumba cha juu yalikuwa wazi kuelekea Yerusalemu), na alipiga magoti yake, kama alivyokuwa akifanya mara tatu kwa siku, na aliomba na kushukuru mbele ya Mungu wake, kama alivyofanya hapo kabla

Daniel 6:13-16

Watu waliofanya njama kinyume na Danieli walifanya nini baada ya kumwona Danieli akiomba na kutafuta msaada kwa Mungu?

Wale watu walienda kwa mfalme na kumwambia kwamba Danieli hamtii mfalme wala amri na kwamba Danieli humwomba Mungu mara tatu kwa siku.

Mfalme alifanya nini baad ya kusikia kwamba Danieli alikuwa ameiasi amri ya mfalme?

Mfalme aliposikia haya, alisikitishwa sana, alitumia akili jinsi ya kumwokoa kutoka katika utawala huu.

Daniel 6:17-18

Mfalme alifanya nini baada ya Danieli kutupwa katika tundu la simba?

Mfalme alilitia muhuri wa pete yake mwenyewe na pamoja na muhuri wa wakuu wake ili kwamba chochote kisiweze kubadilishwa kuhusiana na Danieli. Basi mfalme alienda kwenye ikulu yake na usiku ule alikuwa na mfungo. Hakuna starehe yoyote iliyoletwa mbele yake, nao usingizi ulimkimbia.

Daniel 6:19-20

Katika siku iliyofuata baada ya kuwa Danieli ametupwa katika tundu la simba, Mfalme alimwuliza nini Danieli baada ya kuwa ameenda katika tundu?

Mfalme alimwuliza Danieli kama Mungu ambaye anamtumkia daima ameweza kukuokoa kutoka katika simba

Daniel 6:21-22

Je Danieli alimjibuje mfalme?

Danieli akamwambia mfalme, "Mfalme, uishi milele! Mungu wangu amemtuma mjumbe na amevifunga vinywa vya simba, na hazijaweza kunidhuru. Kwa kuwa sikuwa na hatia yoyote mbele yake na pia mbele yako, ewe mfalme, na sijakufanyia jambo lolote la kukudhuru

Daniel 6:23

Agizo la kwanza la Mfalme lilikuwa ni lipi baada ya kumkuta Danieli alikwa hai katika tundu la simba?

Agizo la kwanza lilikuwa ni kwamba wanatakiwa wamtoe Danieli nje ya tundu

Daniel 6:24-25

Agizo la pili la Mfalme lilikuwa ni lipi baada ya kumkuta Danieli alikwa hai katika tundu la simba?

Mfalme alitoa agizo la pili, waletwe wale watu waliomshitaki Danieli na kisha akawatupa wao katika tundu la simba - wao, na watoto wao, na wake zao.

Daniel 6:26-27

Mfalme Dario alisema nini kuhusu amri yake juu ya Mungu wa Danieli?

Dario alisema kwamba juu ya Mungu wa Danieli, "...Mungu aliye hai na huishi milele, na ufalme wake hauwezi kuharibiwa; utawala wake utakuwepo hadi mwisho. Yeye anatuhifadhi salama na kutuokoa, na anafanya ishara na maajabu mbinguni na duniani; amemhifadhi Danieli salama dhidi ya uwezo wa simba.

Daniel 6:28

Danieli alifanikiwa katika utawala wa nani?

Danieli alifanikiwa katika utawala wa Dario na katika utawala wa Koreshi Mwajemi

Daniel 7

Daniel 7:1-3

NI wakati gani ambao Danieli alipata ndoto na maono katika akili yake?

Danieli alikuwa na ndoto na maono katika akili zake wakati alipokuwa amelala kitandani kwake, katika mwaka wa kwanza wa Belshaza mfalme wa Babeli.

Katika maono yake Danieli, ni kitu gani kilikuwa kinaitikisa bahari kuu?

"Usiku katika ndoto zake aliona pepo nne za mbinguni zilikuwa zinaitikisa bahari kuu.

Ni kitu gani kilitoka katika bahari?

Wanyama wakubwa wanne, kila mmoja alikuwa tofauti na mwenzake, walitoka katika bahari.

Daniel 7:4-5

Mnyama aliyekuwa kama simba alipewa nini?

Na alipewa akili za kibinadamu.

Mnyama aliyekuwa kama dutu aliambiwa kufanya nini?

Aliambiwa, 'Inuka na umeze watu wengi.

Daniel 7:6-7

Mnyama aliye kama chui alipewa nini?

Alipewa mamlaka ya kutawala.

Mnyama wa nne alifanya nini?

Mnyama wa nne aliteketeza, na kuvunja vunja katika vipande, na kusaga saga katika miguuni pake kile kilichosalia

Daniel 7:8

Danieli aliona nini kinatokea kwa mnyama wa nne alipokuwa akitafakari juu ya pembe zake?

Danieli aliona pembe nyingine ndogo ilichipuka katikati ya pembe zingine. Mizizi ya pembe tatu kati ya pembe za mwanzo iling'olewa. Niliona katika pembe hii macho kama macho ya mtu na mdomo ambao ulikuwa ukijivuna kwa mambo makubwa.

Daniel 7:9

Ni nani aliyekaa juu ya viti vya enzi vilivyokuwa vimewekwa?

Mtu wa siku za kale alikaa juu ya kiti kimoja kati ya viti vya enzi vilivyokuwa vimewekwa

Daniel 7:10

Ni kazi gani ilikuwa inafanywa na Mzee wa Siku?

Mahakama iliitishwa, na vitabu vilifunguliwa.

Daniel 7:11-12

Ni kitu gani kilitokea kwa mnyama wa nne?

Mnyama mwenye pembe ambayo ilisema maneno ya kiburi aliuliwa, na mwili wake uliharibiwa, na ulitolewa kwa ajili ya kuchomwa moto. Na kwa wale wanyama wengine watatu waliosalia, mamlaka yao yalitwaliwa mbali, lakini maisha yao yaliendelezea kwa kipindi fulani cha muda.

Daniel 7:13-16

Katika ndoto yake Danieli, ni nani aliwasilishwa mbele za Mzee wa Siku?

Mmoja anakuja katika mawingu ya mbinguni alikuwa kama mwana wa mtu; alikuja kwa Mzee wa Siku na aliletwa mbele zake.

Ni kitu gani alichopewa yeye aliye kama "mwana wa mtu"?

Naye alipewa mamlaka ya kiutawala na utukufu na mamlaka ya kifalme ili kwamba watu wote, na mataifa na lugha ziweze kumtumikia yeye. Mamlaka yake ya kutawala ni mamlaka ya milele ambayo hayatapita, na ufalme wake ni ule ambao hautaangamizwa.

Daniel 7:17-22

Danieli aliambiwa wanyama hawa wanne wanawakilisha nini?

Danieli aliambiwa kwamba hawa wanyama nne wakubwa ni wafalme wanne ambao watatoa katika nchi.

Ni nani ataupokea ufalme na kuumiliki milele?

watu watakatifu wa Mungu aliyejuu wataupokea ufalme na wataumiliki milele na milele

Daniel 7:23-24

Wakati Danieli alipomwuliza yeye aliyekuwa amesimama kuhusu mnyama wa nne, ni kitu gani ambacho alikisema kuwa mnyama wa nne alikuwa na angekifanya katika dunia?

Mtu yule alisema mnyama wa nne ulikuwa ni ufalme wa nne juu ya dunia ambao utakuwa tofauti na falme zingine zote. Utaimeza dunia yote, na utaikanyaga yote chini na kuivunja vunja vipande vipande

Ni kitu gani alichokisema yeye aliyesimama hapo kuhusu pembe kumi?

Yeye aliyesimama pale alisema kwamba kutoka katika ufalme huu wa nne, wafalme kumi watainuka.

Daniel 7:25-26

Je yeye anayezungumza maneno kinyume na Yeye aliye juu atafanya nini na upi utakuwa mwisho wake?

Atawatesa watu watakatifu wa Mungu Aliye Juu. Atajaribu kuzibadili sikukuu na sheria. Mambo haya atapewa mikononi mwake kwa mwaka mmoja, miaka miwili na nusu mwaka. 26Lakini kikao cha mahakama kitaitishwa, na watazichukua nguvu zake za kifalme ili mwisho aweza kuharibiwa na kuteketezwa.

Daniel 7:27-28

Je ni akina nani watapewa ufalme na utawala chini ya mbingu yote?

Ufalme na utawala, ukubwa wa falme chini ya mbingu yote, watapewa watu walio wa watu watakatifu wa Yeye Aliye juu Sana

Ni lipi lilikuwa ni jibu la Danieli kwa maono haya?

Danieli alihuzunisha sana mimi na mwonekano wa uso wangu ulibadilika. Lakini maono haya aliyahifadhi mwenyewe.

Daniel 8

Daniel 8:1-2

Ni lini Danieli alipata maono yake ya pili?

Danieli aliona maono yake ya pili katika mwaka wa tatu wa utawala wa mfalme Belshaza,

Danieli alikuwa wapi katika ndoto yake?

Danieli alikuwa katika mji wa Shushani wenye ngome katika jimbo la Elamu karibu na mfereji wa Ulai.

Daniel 8:3-4

Walikuwa ni wanyama gani wawili ambao Danieli aliwaona katika maono haya?

Danieli alimwona kondoo dume na beberu katika ndoto yake.

Mapembe mawili ya kondoo dume yalifanana na nini?

Pembe moja lilikuwa refu kuliko jingine, lakini pembe ndefu ilikuwa inakua pole pole kuliko ile fupi na pembe fupi ilirefuka na kuizidi nyingine.

Je kondo huyu mme alikuwa a nguvu kiasi gani?

Hakuna mnyama mwingine aliyeweza kusimama mbele yake. Hakuna yeyote aliyeweza kumwokoa yeyote katika mkono wake. Alifanya chochote kile alichokitaka, na alikuwa mtu mkubwa sana

Daniel 8:5-6

Mbuzi allikuwa na mapembe ya aina gani?

Mbuzi huyo alikuwa na pembe kubwa katikati ya macho yake.

Daniel 8:7-8

Mbuzi alifanya kitu gani kwa kondoo dume?

Mbuzi alimpiga kondoo na alizivunja pembe zake mbili. Mbuzi alimgonga kondoo akaanguka chini na akamkanyaga

Baada ya kuvunjika kwa pembe kubwa ya mbuzi, ni kitu gani kilichipuka katika sehemu yake?

Katika sehemu yake zilichipuka na kukua pembe nne kubwa zilizochomoza kuelekea pepo nne za mbingu.

Daniel 8:9-10

Ni kitu gani kilitokea kwa moja kati ya pembe nne za mbuzi?

Kutoka katika pembe moja ilichipuka pembe nyingine, ilikuwa ndogo hapo awali, lakini baadaye ilikuwa pembe kubwa upande wa kusini, na mashariki, na katika nchi ya uzuri ya Israeli.

Pembe hii ilifanya nini baada ya kuwa pembe kubwa?

Pembe ilikuwa kubwa na matokeo yake iliinua vita dhidi ya jeshi la mbinguni

Daniel 8:11-12

Kwanini pembe ya mbuzi ilipewa jeshi na sadaka za kuteketezwa zilikomeshwa?

Haya yatatokea kwasababu ya uasi.

Daniel 8:13-14

Mambo haya yatadumu kwa muda gani, maono haya ya sadaka ya kuteketezwa, dhambi ile iletayo uharibifu, ukabidhiajia wa sehemu takatifu, na jeshi la mbinguni kukanyagwa?

Itadumu kwa Itadumu kwa jioni na asubuhi zipatazo 2,300

Ni kitu gani kitatokea baada ya jioni na asubuhi zipatazo 2,300?

Baada ya hapo, mahali patakatifu patawekwa sawa.

Daniel 8:15-17

Ni nani aliambiwa kumsaidia Danieli kufahamu maono?

Gabrieli aliambiwa kumsaidia Danieli kufahamu maono.

Daniel 8:18-19

Maono yalikuwa kwa ajili wa wakati gani? Ilihusu muda gani?

Maono haya yalikuwa ni kwa ajili ya kipindi cha ghadhabu, kwasababu maono haya yanahusu wakati wa mwisho uliopangwa.

Daniel 8:20-21

Je pembe mbili za kondoo dume na beberu ziliwakilisha nini katika maono ya Danieli?

kondoo mme uliyemwona, yule mwenye pembe mbili - ni wafalme wawili wa Umedi na Uajemi. 21Mbuzi dume ni mfalme wa Ugiriki.

Daniel 8:22-23

Pembe nne zinawakilisha nini, pembe ambazo zilitokeza katika pembe iliyokuwa imevunjika?

pembe nne zilizochipuka hizi ni falme nne zitakazoinuka kutoka katika taifa lake zinawakilishwa na pembe ambayo ilivunjika.

Daniel 8:24-26

Huyu mfalme mwenye akili na uso wa kikatili atafanya nini?

Atakuwa wa kustaajabisha kwa kile atakachokuwa anakiharibu; atafanya na kufanikiwa. Atawaangamiza watu wenye nguvu, watu miongoni wa watakatifu. Ataufanya udanganyifu usitawi chini ya mkono wake kwasababu ya ujanja wake. Atawaangamiza watu wengi bila kutegemea. Atainuka pia hata kinyume cha Mfalme wa wafalme,

Ni kitu gani kitakachotokea mwishoni kwa mfalme huyu mwenye ujanja na uso wa kikatili?

atavunjwa, lakini si kwa mkono wowote wa binadamu

Daniel 8:27

Maono haya yalimwathiri vipi Danieli?

Danieli nilichoka sana na akalala akiwa dhaifu kwa siku kadhaa na alitishwa sana na maono

Daniel 9

Daniel 9:1-2

Ahasuero alikuwa ni mfalme juu ya ufalme gani?

Alikuwa ni mfalme juu ya ufalme wa watu wa Babeli.

Danieli aligundua nini kwa kujifunza neno la Yahweh kutoka kwa Yeremia?

Aligundua kwamba kungekuwa na miaka sabini hadi kufikia mwisho wa kuachwa kwa Yerusalemu ungefika.

Daniel 9:3-4

Danieli alimtafutaje Bwana Mungu?

Danieli alimtafuta Bwana Mungu kwa sala na maombi, kwa kufunga, na kuvaa nguo za magunia na kukaa katika majivu.

Ni jambo gani la kwanza ambalo Danieli alilifanya baada ya kwenda mbele za Bwana kwa Maombi?

Danieli aliungama dhambi za Waisraeli.

Daniel 9:5-6

Manabii waliongea na nani kwa jina la Mungu?

Manabii walizungumza na wafalme , viongozi, baba, na kwa watu wote wa nchi kwa jina Mungu.

Daniel 9:7-8

Kwanini watu wa Israeli walikuwa na aibu usoni mwao?

Aibu ilikuwa usoni mwao kwasababu walikuwa wametenda dhambi kinyume na Bwana.

Daniel 9:9-11

Ni kitu gani kilikuwa kimemwagwa juu ya Israeli kwasababu ya dhambi zao?

Laana na viapo vilivyoandikwa katika sheria ya Musa, mtumishi wa Mungu, zimemwagwa juu yetu kwa kuwa tummetenda dhambi

Daniel 9:12-14

Ni kwa muda gani Yahweh alihakiki maneno aliyoyasema kinyume na Israeli na watawala wake?

Yahweh ameyathibitisha maneno ambayo aliyasema kinyume na sisi na kinyume na viongozi wetu juu yetu, kwa kuleta juu yetu janga kubwa.

Ni kitu gani Danieli alichokisema kwamba Israeli ilikuwa haijakifanya ili kumwomba Mungu rehema?

Danieli alisema bado hawajageuka na kuacha maovu yao na hawajaufuata ukweli wa Mungu.

Daniel 9:15-19

Danieli alisema kuwa ilikuwa ni sababu gani ya Mungu kuwasamehe Israeli?

Danieli alisema kwamba Bwana anatakiwa kuwasamehe Israeli kwasababu ya matendo ya Bwana ya haki.

Daniel 9:20-21

Ni wakati gani Gabrieli alienda kwa Danieli?

Gabrieli alienda kwa Danieli katika wakati wa sadaka ya jioni wakati Danieli alipokuwa anaomba.

Daniel 9:22-23

Kwanini Gabrieli alienda kwa Danieli?

Gabrieli alienda kwa Danieli kumpa utambuzi na ufahamu.

Daniel 9:24-25

Kwanini Miaka sabini na saba zilikuwa zimeamriwa kwa ajili ya watu w Danieli na mji wake mtakatifu?

Miaka sabini na saba ilikuwa imeamriwa ili kukomesha hatia, na kumaliza dhambi, na kuleta haki ya milele, na kutimiza maono na unabii, na kupaweka wakfu mahali patakatifu san

Ni muda gani utapita kati ya kupitishwa kwa amri ya kurud na kuijenga upya Yerusalemu hadi kuja kwake mpakwa mafuta?

kutakuwa na majuma saba na majuma sitini na mbili yatapita kati ya matukio hayo mawili.

Daniel 9:26

Mpakwa mafuta ataharibiwa wakati gani?

Mtiwa mafuta ataharibiwa baada ya miaka ya majuma sitini na mbili.

Daniel 9:27

Mtawala ajaye atafanya nini?

Atalithibitisha agano pamoja na watu wengi kwa miaka saba. Katikati ya miaka saba atakomesha dhabihu na sadaka.

Ni kitu gani kitatokea kwa yeye atakayeleta ukiwa?

Mwisho kamili na uharibifu umeamriwa kutokea kwa yeye aliyesababisha ukiwa.

Daniel 10

Daniel 10:1-3

Ni ujumbe gani uliofunuliwa kwa Danieli katika mwaka wa tatu wa Koreshi mfalme wa Uajemi?

Ujumbe ulihusu vita kuu.

Ni kwa namna gani Danieli aliufahamu ujumbe huo?

Danieli alilfahamu ujumbe kwasababu alikuwa na ufumbuzi wa maono.

Daniel 10:4-6

Danieli alimwona nani katika maono yake?

alimwona mtu aliyevaa kitani, akiwa na mkanda kiunoni mwake uliotengenezwa kwa dhahabu safi kutoka Ufazi.

katika ndoto yake Danieli mtu huyo alifanana na nini?

Mwili wake ulikuwa kama kito, na sura yake ilikuwa kama radi. Macho yake yalikuwa kama miali ya tochi, na mikono yake na miguu yake ilikuwa kama shaba iliyosafishwa. Sauti ya maneno yake ilikuwa kama sauti ya umati mkubwa wa watu.

Daniel 10:7-11

Danieli alijibu nini baada ya kuona maono makubwa na kusikia sauti ya mtu?

Hakuna nguvu iliyobakia ndani yangu; mwonekano wangu wa kung'aa ulibadilika na kuwa mwonekano wa uharibifu, na hazikubakia nguvu ndani yangu. 9Kisha nikasikia maneno yake, na nilipoyasikia, nilianguka kifudifudi na kupata usingizi mzito.

Daniel 10:12-13

Malaika alitumwa lini kwenda kwa Danieli?

Malaika alitumwa katika siku ya kwanza ambayo Danieli aliweka akili yake ili kufahamu na kujinyenyekeza mbele za Mungu.

Kwanini malaika alichukua muda wa siku ishirini na moja kufika kwa Danieli?

Malaika alizuiliwa na mwana wa mfalme of ufalme wa Uajemi ambaye alimpinga.

Daniel 10:14-15

Matukio ya ndoto yatatokea lini?

Maono ni kwa ajili siku za mwisho ambazo hazijatokea bado.

Daniel 10:16-17

Danieli alisema nini juu ya kile ambacho maono haya yalikuwa yamemfanyia?

Danieli alisema kuwa kwasababu ya maono hana nguvu ndani yake iliyosalia na hana nguvu, na hakuna pumzi iliyosalia ndani yake.

Daniel 10:18-19

Yeye mwenye sura kama ya mtu alifanya nini ili kumtia nguvu Danieli?

Tena yule mwenye mwonekano wa mtu alinigusa na kunitia nguvu

Daniel 10:20-21

Yeye mwenye mwonekano kama mtu alisema atafanya nini baada ya kumwacha Danieli?

Alisema atarudi hivi karibuni kupigana na mkuu wa Uajemi.

Je yeye mwenye mwonekano kama wa mtu alisema atamwambia nini Danieli?

Alisema kwamba atamwambia kile kilichoandikwa katika Kitabu cha Ukweli.

Daniel 11

Daniel 11:1-2

Ni kwa jinsi gani mfalme wa nne wa Uajemi alipata nguvu zake?

Atapata nguvu kupitia utajiri wake

Daniel 11:3-4

Ni nani ambaye hatapewa ufalme wa mfalme mwenye nguvu?

Wazawa wa mfalme mwenye nguvu hawatapewa ufalme.

Daniel 11:5-6

Ni akina nani watafanya ushirika/muungano?

Mfalme wa Kusini atakuwa na nguvu nai mmoja kati ya maamiri jeshi wake atakuwa mfalme wa Kaskazini watafanya mwungano.

Ni nani atakuja kuimarisha muungano kati ya mfalme wa Kusini na mfalme wa Kaskazini?

Binti wa mfalme wa Kusini atakuja kwa mfalme wa Kaskazini kuyathibitisha makubaliano yao.

Daniel 11:7-9

Je tawi la binti wa mfalme wa Kusuini atafanya nini kwa mfalme wa Kaskazini?

Atalishambulia jeshi na kuingia ngome ya mfalme wa Kaskazini. Atapigana nao, na atawashinda.

Daniel 11:10

Wana wa mfalme wa Kaskazini watafanya nini?

Watapigana na kuunganisha jeshi kubwa. Litaendelea kukua na litagharikisha kila kitu, litapita katikati hadi kwenye ngome yake

Daniel 11:11-12

Mfalme wa kusini atafanya nini katika kujibu mashambulizi ya wana wa mfalme wa Kaskazini?

Mfalme wa Kusini atakasirika na kisha ataenda na kupigana naye, mfalme wa Kaskazini

Nani alishinda katika vita hii kati ya Kaskazini na Kusini?

Mfalme wa Kusini atashinda vita.

Daniel 11:13

Mfalme wa Kaskazini atafanya nini baada ya miaka kadhaa?

Baada ya miaka kadhaa, mfalme wa Kaskazini atakuja na jeshi kubwa likiwa na vifaa vingi.

Daniel 11:14

Ni nani zaidi atainuka kinyume na mfalme wa Kusini katika siku hizo?

Katika siku hizo wengi watainuka kinyume na mfalmea wa Kusini kujumuisha Wana wa vurugu miongoni mwa watu wa Danieli.

Daniel 11:15-16

Ni kitu gani kitatokea katika muda ule mfalme wa Kaskazini atakapomshambulia mfalme wa kusini?

Majeshi ya Kusini hayataweza kusimama, hata wanajeshi wake bora. Mfalme wa Kaskazini atafanya kila akitakacho dhidi ya mfalme wa Kusini.

Daniel 11:17-19

Kwanini mfalme wa Kaskazini alimtoa binti yake katika ndoa kwa mfalme wa Kusini?

Mfalmw wa Kaskazini atafanya haya ili kuuharibu mfalme wa Kusini.

Kutatokea nini kwa mfalme wa Kaskazini?

amiri jeshi atakikomesha kiburi chake na atakisababisha kiburi chake kiishe. Atajikwaa na kuanguka; na hatapatikana tena.

Daniel 11:20-22

Je yeye atakayeinuka katika sehemu ya mfalme wa Kaskazini atafanya nini?

Atalazimisha kodi ilipwe ili kuleta ufahari wa ufalme.

Ni nini kitatokea kwa yeye anayelazimisha ulipaji wa kodi?

Baada ya siku chache atakatiliwa mbali, lakini si kwa hasira wala si katika vita.

Ni kwa jinsi gani mtu aliyedharauliwa ambaye hakupewa heshima ya ufalme ataingia madarakani?

Atakuja kimya kimya na atautwaa ufalme kwa ulaghai.

Daniel 11:23-24

Je mfalme aliyedharauliwa atafanya nini baada ya kuundwa kwa muungano pamoja naye?

Tangu katika kipindi kile ambacho makubaliano yalifanywa pamoja naye, ataenenda kwa kwa hila.

Daniel 11:25-27

Ni nini kitatokea katika kiipindi ambacho mfalme mwongo atakapopigana vita dhidi ya mfalme wa Kusini?

Mfalme wa Kusini atapigana vita akiwa na jeshi kubwa lenye nguvu, lakini hataweza kusimama kwa kuwa wengine watafanya njama dhidi yake.

Kwanini mfalme wa Kaskazini na mfalme wa Kusini watakaa meza moja na kudanganyana?

Wafalme wote hawa wawili watakaa katika meza moja na kudanganyana kwasababu mioyo yao imejawa na uovu kinyume na mwenzake.

Daniel 11:28

Moyo wa mfalme wa Kaskazini utaweka kuwa kinyume na kitu gani?

Moyo wake utapinga vikali agano takatifu.

Daniel 11:29-32

Ni kwa namna gani hasira ya mfalme Kaskazini itadhihirishwa kinyume na agano takatifu?

Mfalme wa Kaskazini ataonesha hasira yake dhidi ya agano takatifu kwa kuwaonyesha mema wale watakaoliacha agano takatifu.

Daniel 11:33-35

Ni kitu gani kitatokea kwa wenye hekima?

Watu wenye hekima wataanguka kwa upanga na kwa miali ya moto; watatiwa mateka na kunyang'anywa kwa siku. Katika siku za kujikwaa kwao, watasaidiwa kwa msaada kidogo.

Kwanini baadhi ya watu wenye hekima watajikwaa?

Baadhi ya watu wenye hekima watajikwaa ili kujisafisha kutokee kwao, na kujiosha, na kujitakasa, mpaka wakati wa mwisho.

Daniel 11:36-37

Mfalme wa Kaskazini anayelaghai atajiinua juu ya nani?

Atajiinua mwenyewe na kujifanya mkubwa kuliko kila mungu. Kinyume cha Mungu wa miungu, na mungu anayependwa na wanawake.

Daniel 11:38-39

Mfalme wa Kaskazini anayelaghai atafanya nini kwa wale wanaomkubali?

Atawapa heshima wale wanaomkubali. Atawafanya wawe watawala juu ya watu wengi.

Daniel 11:40-41

Ni kitu gani kitatokea wakati mfalme wa Kaskazini atakapoingia katika nchi ya utukufu katika siku za mwisho?

Katika siku hizo makumi elfu wa Israeli watajikwaa na kuanguka.

Nani atatoroka kutoka katika mkono wa mfalme wa Kaskazini?

Watu hawa watatoroka kutoka katika mkono wake: Waedomu, Wamoabu, na mabaki ya watu wa Amoni

Daniel 11:42-43

Mfalme wa Kaskazini ataueneza utawala wake mpaka katika nchi gani?

Mfalme wa Kaskazini ataueneza utawala wake juu ya Misri; watu wa Libya na watu wa Ethiopia.

Daniel 11:44-45

Mfalme wa Kaskazini atafanya nini baada ya kupata taarifa kutoka mashariki na Kaskazini?

Atatoka akiwa mwenye hasira nyingi kuwa ili kuwaharibu kabisa na kuwahifadhi kwa ajili ya uharibifu.

Mfalme wa Kaskazini ataziweka wapi hema zake kwa ajili ya sehemu yake?

Naye ataisimamisha hema ya makao yake ya kifalme kati ya bahari na milima ya uzuri wa utakatifu.

Ni nani atamsaidia mfalme wa Kaskazini mwishoni?

Mfalme wa Kaskazini ataufikia mwisho wake na hapatakuwa na mtu wa kumsadia.

Daniel 12

Daniel 12:1-2

Ni nani huyu ambaye huwalinda watu wa Danieli?

Mikaeli, jemedari mkuu ambaye huwalinda watu wake.

Nyakati za mateso zilizoandikwa hapa zitakuwa za namna gani?

Kutakuwa na wakati wa mateso ambao haujawahi kutokea tangu mwanzo wa taifa lolote mpaka kipindi hicho.

Katika kipindi hicho ni nani ataokolewa?

Katika muda huo watu wako wataokolewa, yeyote ambaye jina lake litapatikana katika kitabu.

Ni kitu gani kitatokea kwa wale wengi waliolala katika mavumbi ya dunia?

Na baadhi ya wale waliolala katika mavumbi ya dunia watainuka. baadhi kwa uzima wa milele na baadhi kwa ajili ya fedheha na matwezo ya milele.

Daniel 12:3-6

Ni kitu gani kitatokea kwa wale wenye hekima na wale wanaowageuza wengi katika haki?

Wale wenye hekima watang'ara kama mng'ao wa anga la juu, na wale wenye kuwaelekeza wengine katika haki, watakuwa kama nyota milele na milele.

Ni kwa muda gani Danieli aliambiwa akitunze kitabu kikiwa kimefungwa?

Aliambia kukihifadhi kitabu kikiwa kimetiwa chapa mpaka nyakati za mwisho.

Daniel 12:7

Je Mtu aliyevaa nguo za kitani alisema ingechukua muda gani hadi mwisho wa matukio haya ya kushangaza?

mtu yule aliyevaa nguo za kitani, alisema itakuwa kwa wakati, nyakati, na nusu wakati. Na wakati nguvu za watu watakatifu zitakapokuwa zimeshaharibiwa, mambo haya yote yatakuwa yamemalizika.

Daniel 12:8-9

Ni sababu gani aliyoitoa mtu aliyevaa nguo za kitani juu ya kwanini Danieli hakuelewa kile ambacho mtu aliyevaa nguo za kitani alikuwa akimwambia?

Mtu aliyevaa nguo za kitani alimwambia Danieli "Nenda zako Danieli, kwa kuwa maneno yamefungwa na kutiwa chapa mpaka wakati wa mwisho."

Daniel 12:10-11

katika nyakati za mwisho ni akina ambao wataelewa na akina nani ambao hawataelewa maneno ya unabii?

Hakuna hata mmoja katika watu waovu atakayefahamu, lakini wenye hekima watafahamu.

Ni muda gani utapita kati ya wakati ambo sadaka za kawaida zitaondolewa na kipindi cha kuwekwa kwa chukizo la uharibifu ambalo litasababisha ukiwa?

kutakuwa na siku zipatazo 1,290

Daniel 12:12-13

Mtu aliyevaa nguo za kitani alisema ni nani atabarikiwa katika kipindi hicho?

Mtu aliyevaa nguo za kitani alisema, "Ana heri mtu yule anayengojea mpaka mwisho wa siku 1,335."

Mtu aliyevaa nguo za kitani alisema kingetokea nini kwa Danieli?

Mtu aliyevaa nguo za kitani alisema kwamba Danieli angepumzika na atainuka katika sehemu uliyopewa, mwishoni mwa siku."