Colossians
Colossians 1
Colossians 1:1-3
Kwa namna gani Paulo alikuwa mtume wa Yesu Kristo?
Paulo alikuwa mtume wa Yesu Kristo kwa mapenziyaMungu
Paulo aliandika hii barua kwa nani?
Paulo aliwaandikia wale waliotengwa kwa ajili ya Mungu na ndugu waaminifu katika Kolosai.
Colossians 1:4-6
Wakolosai walisikia kutoka wapi kuhusu taraja ambalo wanalo?
Wakolosai walisikia kuhusu taraja lao la ujasiri katika neno la ujasiri, la injili.
Paulo anasema injili imekuwa ikifanya nini katika dunia?
Paulo anasema injili imekuwa ikizaa tunda na kukua katika dunia yote.
Colossians 1:7-8
Nani alifikisha injili kwa Wakolosai?
Epafra, mtumishi mwaminifu wa Kristo, alifikisha injili kwa Wakolosai
Colossians 1:9-10
Pamoja na nini Paulo anaomba kwamba Wakolosai wajazwe?
Paulo anaomba kwamba Wakolosai wawe wamejazwa na ujuzi wa Mapenzi ya Mungu katika hekima yote na ufahamu wa kiroho.
Paulo anaombea kwamba Wakolosai waenende vipi katika maisha yao?
Paulo anasema kwamba Wakolosai waendelee kutembea kwa ustahivu wa Bwana, wakizaa tunda pamoja na matendo mazuri, kukua katika ujuzi wa Mungu.
Colossians 1:11-12
Kwa namna gani wale waliotengwa kwa ajili ya Mungu wamestahilishwa?
Wale waliotengwa na Mungu wamestahilishwa kwa kuwa na sehemu katika urithi wa nuru.
Colossians 1:13-14
Kutoka wapi Baba amewaokoa wale ambao wametenga kwa ajili yake?
Amewaokoa wao kutoka katika utawala wa giza na kuwahamisha kwa ufalme wa mwana wake.
Katika Kristo tunaukombozi, ambao ni wa nini?
Katika Kristo tunao ukombozi, ambao ni msamaha wa dhambi.
Colossians 1:15-17
Mwana ni mfano wa nani?
Mwana ni mfano waMungu asiyeonekana.
Nini kiliumbwa kupitia Yesu Kristo na kwa ajili yake?
Vitu vyote viliumbwa kupitia Yesu Kristo na kwa ajili yake.
Colossians 1:18-20
Ni kwa jinsi gani Mungu amevipatanisha vitu vyote kwake?
Mungu alivipatanisha vitu vyote kwake wakati alipotengeneza amani kupitia damu ya mwanaye.
Colossians 1:21-23
Uhusiano gani Wakolosai walikuwa nao na Mungu kabla hawajaamini Injili?
Kabla ya kuamini Injili, Wakolosai walikuwa wageni kwa Mungu na walikuwa maadui zake.
Ni kipi Wakolosai wanalazimika kukifanya?
Wakolosai wanalazimika waendelee kuishi katika imani na ujasiri wa injili.
Colossians 1:24-27
Ni kwa ajili ya nani Paulo anateseka, na nini nia yake?
Paulo anateseka kwa ajili ya Kanisa, na anafurahia katika hilo.
Ni siri gani ilyokuwa imefichwa kwa miaka mingi lakini sasa imefunuliwa?
Siri iliyokuwa imefichwa kwa miaka mingi lakini sasa imefunuliwa ni Krsito ndani yenu, ujasiri wa heshima
Colossians 1:28-29
Ni nini lengo la Paulo katika maonyo na mafundisho?
Lengo la Paulo ni kuwafikisha kila mmoja mkamilifu katka Kristo.
Colossians 2
Colossians 2:1-3
Siri ya Mungu ni nini?
Siri ya Mungu ni Kristo.
Nini kimefichwa katika Kristo?
Yote yamefichwa hazina ya hekima na ufahamu yamefichwa katika Kristo.
Colossians 2:4-5
Ni jambo gani ambalo Paulo anahofu kuwa laweza kutokea kwa Wakolosai?
Paulo anahofu kuwa Wakolosai wanaweza kuharibiwa na hotuba zenye mvuto.
Colossians 2:6-7
Ni jambo gani ambalo Paulo anawataka Wakolosai wafanye kwa kuwa wamempokea Kristo?
Paulo anawataka Wakolosai watembee ndani ya Kristo Yesu kama ambavyo wamempokea.
Colossians 2:8-9
Ni katika mambo yapi ambapo Paulo anasema kuna maneno matupu ya udanganyifu?
Maneno matupu ya udanganyifu yapo katika tamaduni za watu na katika mifumo ya dhambi ya ulimwengu.
Nini kinaishi katika Kristo?
ukamilifu wote wa asili ya Mungu unaishi katika Kristo.
Colossians 2:10-12
Nani ni kichwa cha utawala wote na mamlaka?
Kichwa cha utawala wote na mamlaka ni Kristo.
Nini kimetolewa kupitia tohara ya Kristo?
Dhambi ya mwili wa nyama imetolewa kupitia tohara ya Kristo.
Nini kinatokea katika ubatizo?
Mtu huzikwa pamoja na Kristo katika ubatizo.
Colossians 2:13-15
Hali ya mtu ikoje kabla Kristo hajamfanya kuwa hai?
Mtu anakuwa amekufa katika dhambi zake kabla Kristo hajamfanya kuwa hai.
Nini Kristo alifanya juu ya kumbukumba ya madeni tulikuwa tunadaiwa?
Kristo alitoa kumbukumbu ya madeni na kuyagongomea msalabani.
Kristoalifanya nini juu ya nguvu na mamlaka?
Kristo alitoa nguvu na mamlaka, kwa uwazi kuwaonyesha, na kuwaongoza katika ushindi wa kumiliki.
Colossians 2:16-17
Ni kitu gani Paulo anasema ni ni kivuli cha mambo yajayo?
Paulo anasema chakula, kinywaji, siku ya sikukuu, na Sabato ni kivuli cha mambo yajayo.
Ni katika uhalisia gani unafanya kiini cha kivuli?
Kiini cha kivuli ni kwa uhalisia wa Kristo.
Colossians 2:18-19
Ni jinsi gani mwili wote ulisambaa na kuponya wote?
Mwili wote ulisambaa na kuponya wote kwa kichwa, Krsito.
Colossians 2:20-23
Ni aina gani za amri ambazo Paulo anasema ni sehemu ya imani za kidunia?
Amri za kutoshika, kuonja, na kutokugusa ni sehemu ya imani za kidunia.
Ni sheria zipi zilizotengenezwa za kinyume na dini ziwe hazina thamani?
Sheria zilizotengenezwa kidini hazina thamani kinyume kuendeleza mateso ya mwili.
Colossians 3
Colossians 3:1-4
Kristo amefufuka wapi?
Krisro amefufuka kukaa katika mkono wa kuume wa Mungu
Ni kipi waumini wanapaswa kukitafuta na kipi hawapaswi kukitafuta?
Waumini wanapaswa kutafuta mambo yaliyo juu,
na sio mambo ya duniani.
Ni wapi Mungu ameweka maisha ya waamini?
Mungu ameficha maisha ya waamini katika Kristo.
Nini kitatokea kwa muumini wakati Kristo atakapoonekana?
Wakati Kristo atakapoonekana, waamini wataonekana pamoja naye katika utukufu.
Colossians 3:5-8
Ni kitu gani waumini wanatakiwa kufisha?
Waumini wanatakiwa kufisha hamu ya dhambi ya ulimwengu.
Nini kitatokea kwa wale ambao hawamtii Mungu?
Hasira ya Mungu itakuwa juu yao wale ambao hawamtii Mungu.
Ni vitu gani ambavyo Paulo anasema kwa waamini wayaondoe, ni sehemu ya utu wa zamani?
Waamini lazima waondokane na ghadhabu, hasira, nia mbaya, matusi, na maneno machafu.
Colossians 3:9-11
Ni mambo gani ambayo Paulo anasema waumini lazima wayaondoe, ambayo ni sehemu ya utu wa kale?
Waumini lazima waondoe gadhabu, hasira, nia mbaya, matusi, lugha chafu, na udanganyifu.
Colossians 3:12-14
Ni baadhi mabo gani ambayo Paulo anasema waumini lazima wayavae, ambayo ni sehemu ya utu mpya?
Waumini lazima wavae moyo wa huruma, ukarimu, unyenyekevu, upole, na uvumilivu.
Ni kwa njia gani mwamini anaweza kusamehe?
Mwamini anawezakusamehe katika njia ile ile ambayo Mungu amemsamehe.
Kigezo cha ukamilifu miongoni mwa Mkristo ni kipi?
Upendo ni kigezo cha ukamilifu.
Colossians 3:15-17
Kipi kinapaswa kutawala katika moyo wa muumini?
Amani ya Kristo lazima itawale katika moyo wa muumini.
Ni nini anachopaswa muumini kutoa kwa Mungu katika mtazamo wake, nyimbo, neno, na matendo?
Katika mtazamo wake, nyimbo, neno, na matendo muumini lazima ampe Mungu shukurani.
Ni kipi kinatakiwa kukaa kwa mwamini kwa utajiri?
Neno la Kristo likae kwa mwamini kwa utajiri.
Colossians 3:18-21
Ni jinsi gani mke amjibu mme wake?
Mke lazima anyenyekee kwa mme wake.
Ni jinsi gani mume anatakiwa kumtenda mke wake?
Mume anatakiwa ampende mke wake na sio kuwa wakali kwake.
Ni jinsi gani mtoto anatakiwa kutenda kwa wazazi wake?
Mtoto anatakiwa awatii wazazi wake katika yote.
Ni kipi ambacho baba hatakiwi kufanya kwa watoto?
Baba hatakiwi kuwachokoza watoto wao.
Colossians 3:22-25
Waamini wafanye kazi kwa nani kwa kila wafanyacho?
Waamini wafanye kazi kwa Bwana katika kila jambo wafanyalo.
Watapokea nini wale ambao wanamtumikia Mungu katika chochote wafanyacho?
Wale ambao wanaomtumikia Mungu kwa vyovyote watapokea zawadi ya kurithi.
Watapokea nini wale ambao watendao yasiyo haki?
Wale ambao watendao yasiyo haki watapokea hukumu kwa yale waliyoyafanya.
Colossians 4
Colossians 4:1
Paulo anawakumbusha nini mabwana wa duniani kwamba pia wanaye?
Paulo anawakumbusha mabwana wa duniani kwamba wana Bwana pia mbinguni.
Colossians 4:2-4
Paulo anataka Wakolosai waendelee kuwa na subira katika nini?
Paulo alitaka Wakolosai waendelee kuwa na subira katika maombi.
Paulo aliwataka wakolosai waombee nini?
Paulo aliwataka wakolosai waombe kwamba apate na mlango wa kuongea neno, siri ya Kristo.
Colossians 4:5-6
Jinsi gani Paulo anawaelekeza Wakolosai waweje kati yao walio nje?
Paulo anawaelekeza wao waishi kwa hekima, na neema katika maneno kwa hao walio nje.
Colossians 4:7-9
Kazi gani ngumu Paulo aliwapa Tikiko na Onesmo?
Paulo aliwapa kazi ya kuamua kila jambo linalomhusu yeye kwa Wakolosai.
Colossians 4:10-11
Ni maelekezo gani aliyotoa Paulo kuhusu Marko, binamu yake Barnaba?
Paulo aliwaambia Wakolosai wampokee Marko atakapofika kwao.
Colossians 4:12-14
Epafra aliwaombea nini Wakolosai?
Aliomba kwamba Wakolosai wasimame kikamilifu na uhakika katika mapenzi yote ya Mungu.
Jina la tabibu aliyekuwa na Paulo lilikuwa nani?
Jina la tabibu ni Luka.
Colossians 4:15-17
Ni sehemu gani tofauti waliokutania kanisa la Laodekia?
Kanisa la Laodekia walikuwa wakikutana ndani ya nyumba.
Ni kwa kanisa gani Paulo aliandika barua?
Paulo aliandika pia barua kwa kanisa la Leodekia.
Colossians 4:18
Paulo alionyeshaje kama hii barua ilikuwa yake?
Paulo aliandika jina lake kwa mkono wake mwenyewe mwishoni mwa barua.