Psalms
Psalms 1
Psalms 1:1-2
Mtu aliyebarikiwa hatembei wapi?
Hatembei katika ushauri wa waovu.
Mtu aliyebarikiwa hasimami wapi?
Hasimami katika njia ya watenda dhambi.
Mtu aliyebarikiwa haketi wapi?
Haketika katika kusanyiko la wanaokejeli.
Mtu aliyebarikiwa hufurahia nini?
Anafurahi katika sheria ya Yahwe.
Mtu aliyebarikiwa hutafakari juu ya sheria wakati gani?
Anaitafakari mchana na usiku.
Psalms 1:3
Mtu aliyebarikiwa yukoje?
Ni kama mti uliopandwa katika mikondo ya maji.
NIni kitatokea kwa kila kitu atakachofanya mtu aliyebarikiwa?
Kila anachifanya kitafanikiwa.
Psalms 1:4-5
Watu waovu wakoje?
Ni kama makapi ambayo hupulizwa na upepo.
Nini kitatokea kwa watu waovu katika hukumu?
Hawatasimama katika hukumu.
Psalms 1:6
Nani huthibitisha njia ya mwenye haki?
Yahwe anakubali njia ya mwenye haki.
Nini kitatokea kwa njia ya mwovu?
Njia ya mwovu itapotea.
Psalms 2
Psalms 2:1-3
Watawala wanapanga njama dhidi ya nani?
Wanapanga njama dhidi ya Yahwe na Masihi wake.
Watawala wanataka kubomoa na kutupa nini?
Wanataka kubomoa pingu ambazo Yahwe na Masihi wake walizowawekea na kutupa minyororo yao.
Psalms 2:4-5
Nani hukaa katika mbingu na kukejeli mataifa yanayoasi?
Bwana anawakejeli.
Psalms 2:6-7
Bwana amemtia mafuta nani?
Bwana amemtia mafuta mfalme wake juu ya Sayuni, mlima wa mtakatifu.
Yahwe amempa amri gani mwandishi?
Yahwe anasema, "Wewe ni mwana wangu! Siku hii nimekuwa baba yako."
Psalms 2:8-9
Yahwe atafanya nini na mataifa na sehemu za mbali za dunia?
Yahwe atawapa kama urithi na mali.
Nini kitatokea kwa mataifa?
Yatavunjwa na kupondwa.
Psalms 2:10-11
Wafalme na watawala wanapaswa kuitikiaje amri ya Yahwe?
Wanapaswa kumwabudu Yahwe kwa kumcha na kushangilia kwa kutetemeka.
Psalms 2:12
Kwa nini wafalme wamtii mwana wa Yahwe?
Wanapaswa kumtii ili asikasirike na hawatakufa.
Nini hutokea kwa wale wote wanaoenda kwenye kivuli cha mwana?
Wanabarikiwa.
Psalms 3
Psalms 3:1-2
Adui wa Daudi wamefanya nini kwake?
Wamegeuka na kumshambulia.
Psalms 3:3-4
Daudi anamfananisha Yahwe na nini?
Yahwe ni ngao iliyomzunguka, utukufu wake, na yule anayeinua kichwa chake.
Yahwe anafanya nini wakati Daudi anapoinua sauti yake kwake?
Anajibu kutoka katika kilima chake kitakatifu.
Psalms 3:5-6
Daudi hatamwogopa nani kwa sababu ya ulinzi wa Yahwe?
Daudi hatawaogopa watu waliojiweka dhidi yake.
Psalms 3:7-8
Yahwe atafanya nini kwa adui wa Daudi?
Atawapiga adui zake wote kwa taya; atavunja meno ya waovu.
Wokovu unatokea wapi?
Wokovu unatoka kwa Yahwe.
Psalms 4
Psalms 4:1
Daudi anamwomba nani ajibu anapoita?
Daudi anaomba kwa Mungu wa haki yake kumjibu anapoita.
Psalms 4:2-3
Watu wanafanyia nini heshima ya Daudi?
Wanageuza heshima yake kuwa aibu.
Yahwe amemteua nani pembeni?
Yahwe amemteua mtauwa kwa ajili yake.
Psalms 4:4-5
Daudi anasemaje kutafakari?
Anasema, "Tafakari moyoni mwako kitandani mwako na uwe kimya".'
Ni aina gani za sadaka ambazo Daudi anasema zitolewe?
Anasema kutoa sadaka za haki.
Daudi anasema kumtumaini nani?
Anasema kumtumaini Yahwe.
Psalms 4:6-8
Wengi watasema nini?
Wengi watasema, "Nani atatuonesha chochote kizuri?"
Daudi anamwomba Yahwe kuinua nini?
Anamwomba Yahwe kuinua mwanga wa uso wake juu yao.
Yahwe ameupa nini moyo wa Daudi?
Yahwe ameupa moyo wake furaha zaidi wengine wanapota nafaka yao na divai yao mpya inapojaa.
Nani humfanya Daudi salama anapolala chini katika usingizi wa amani?
Yahwe pekee humweka Daudi salama.
Psalms 5
Psalms 5:1-3
Daudi anamwomba nani kusikiliza kuita kwake na kufikiria kuhusu gumio zake?
Daudi anamwomba Yahwe kusikiliza kuita kwake na kufikiria kuhusu gumio zake.
Daudi anatumia majina gani kwa ajili ya yule anayesikia sauti ya kuita kwake?
Daudi anamwita, "mfalme wangu na Mungu wangu."
Daudi atafanya nini asubuhi?
Ataleta ombi lake kwa Yahwe na kusubiri kwa matarajio.
Psalms 5:4-6
Kwa uhakika Mungu hafanyi nini?
Hakika hakubali uovu, na watu waovu hawatakuwa wageni wake.
Nani hatasimama katika uwepo wa Mungu?
Wenye kiburi hawatasimama katika uwepo wa Mungu.
Mungu humchukia nani?
Mungu huwachukia wote wanaotenda uovu.
Mungu atafanya nini kwa waongo?
Mungu atawaangamiza waongo.
Mungu anawachukia kina nani?
Yahwe anawachukia watu wenye vurugu na waongo.
Psalms 5:7-8
Kwa nini Daudi atakuja katika nyumba ya Yahwe?
Daudi atakuja katika nyumba ya Yahwe kwa sababu wa uaminifu mkuu wa agano wa Yahwe.
Daudi atainamaje kuelekea hekalu takatifu la Yahwe?
Daudi atainama chini kwa heshima kubwa.
Kwa nini Daudi anamwomba Bwana kumwongoza katika haki?
Daudi anamwomba Bwana kumwongoza katika haki ya Bwana kwa sababu ya adui wa Daudi.
Psalms 5:9-10
Daudi anawaelezeaje adui zake?
Daudi anawaelezea adui zake kama wasio na ukweli mdomoni mwao, ndani yao ni uovu, koo yao ni kaburi lililo wazi na wanajipendekeza kwa ulimi wao.
Daudi anamwomba Mungu kufanya nini kwa adui wa Daudi kwa sababu ya makosa yao mengi na kuasi dhidi ya Mungu?
Daudi anamwomba Mungu kutangaza kuwa adui zake wana hatia.
Psalms 5:11-12
Kwa nini wale wote wanaomkimbilia Yahwe wapige kelele ya furaha?
Wanapaswa kupiga kelele ya furaha kwa sababu Mungu anawalinda.
Yahwe atafanya nini kwa ajili ya wenye haki?
Yahwe atawabariki wenye haki na kuwazunguka na fadhila zake kama vile na ngao.
Psalms 6
Psalms 6:1-2
Daudi anamwomba Yahwe asifanye nini?
Anamwomba Yahwe kutomkemea katika hasira yake au kumwadhibu katika gadhabu yake.
Daudi anamwomba Yahwe kufanya nini kwa sababu Daudi ni mdhaifu?
Daudi anamwomba Yahwe kumhurumia na kumponya.
Psalms 6:3-5
Kwa nini Yahwe amkomboe na kumwokoa Daudi?
Kwa sababu ya uaminifu wa agano wa Yahwe.
Nini hakitakumbukwa katika mauti?
Katika mauti hakuna kumbukumbu ya Yahwe.
Psalms 6:6-7
Daudi anafanya nini kitandani pake kwa sababu amechoka na anagumia.
Usiku kucha anakiloanisha kwa machozi yake.
Nini kitatokea kwa jicho la Daudi kwa sababu ya huzuni yake na kwa sababu ya adui zake wote?
Macho yake yanafifia na kudhoofika.
Psalms 6:8-10
Kwa nini wale wote wanaotenda udhalimu waende mbali na Daudi?
Kwa sababu Yahwe alisikia sauti ya kulia kwake na ombi lake la huruma na amekubali ombi lake.
Nini kitatokea kwa adui wa Daudi?
Adui zake wote wataaibika na kutaabika sana na watageuka na kuaibishwa ghafla.
Psalms 7
Psalms 7:1-2
Daudi anamkimbilia nani?
Daudi anamkimbilia Yahwe Mungu wake.
Daudi anamwomba Yahwe kufanya nini?
Daudi anamwomba Yahwe kumwokoa kutoka kwa wale wanaomfukuza, na kumkomboa.
Ni nini ambacho Yahwe pekee anaweza kufanya kwa ajili ya Daudi?
Hakuna mtu bali Yahwe anayeweza kumleta Daudi kwenye usalama.
Psalms 7:3-4
Daudi alisema nini ambacho hakufanya?
Daudi anamwambia Yahwe kuwa hakufanya kile ambacho adui zake wanasema alifanya na hakuna udhalimu mikono mwake.
Daudi anasema hajafanya nini kwa mtu ambaye ana amani naye au ambaye yuko kinyume naye?
Daudi anasema hajawai kufanya ubaya kwa mtu aliye naye amani au kumdhuru mtu ovyo ambaye yuko kinyume naye.
Psalms 7:5
Daudi anasema Yahwe anapaswa kufanya nini kama Daudi hasemi ukweli?
Daudi anasema Yahwe anatakiwa kuwaruhusu adui zake kufuatilia maisha ya Daudi na kumpita, kukanyaga mwili wake ukiwa hai, na kumwacha bila heshima katika mavumbi.
Psalms 7:6-7
Daudi anamwomba Yahwe kufanya nini katika hasira ya Yahwe?
Daudi anamwomba Yahwe kuinuka na kusimama dhidi ya adui wa Daudi.
Daudi anamwomba Yahwe kufanya nini kwa ajili yake?
Daudi anamwomba Yahwe kuamka na kubeba amri za haki ambazo Yahwe aliamuru.
Daudi anamtaka Yahwe kufanya nini kuhusu nchi?
Daudi anamtaka Yahwe kuchukua nafasi yake halali juu ya nchi.
Psalms 7:8-9
Daudi anataka Yahwe ahukumu nini?
Daudi anataka Yahwe ahukumu mataifa.
Daudi anasema Mungu mwenye haki hufanya nini?
Daudi anasema Mungu anachunguza mioyo na akili.
Psalms 7:10-11
Ngao ya Daudi inatoka wapi?
Ngao ya Daudi inatoka kwa Mungu.
Mungu anamwokoa nani?
Mungu humwokoa mnyofu wa moyo.
Daudi anamfafanuaje Mungu?
Daudi anamwelezea Mungu kama mwamuzi mwenye haki ambaye anachukizwa kila siku.
Psalms 7:12-13
Mungu atamfanya nini mtu kama hatatubu?
Mungu atanoa upanga wake na kuandaa upinde wake kwa ajili ya vita.
Psalms 7:14-16
Daudi anafafanuaje uovu ndani ya yule ambaye hatubu?
Daudi anamweleza kama mtu mwenye mimba ya uovu, mtu ambaye ameshika mimba ya mipango ya uharibifu na kuzaa uongo wa kudhuru.
Nini hutokea kwa mtu mwovu anayechimba shimo?
Anaanguka katika shimo alilotengeneza.
Nini hutokea kwa mipango ya uharibifu ya mtu mwovu?
Mipango yake inarudi juu ya kichwa chake mwenyewe na vurugu yake huja chini ya kichwa chake mwenyewe.
Psalms 7:17
Daudi atampa Yahwe shukrani kwa ajili ya nini?
Atampa Yahwe shukrani kwa ajili ya hukumu yake.
Daudi ataimba sifa kwa nani?
Daudi ataimba sifa kwa Yahwe Aliye juu.
Psalms 8
Psalms 8:1-2
Jina la nani tukufu duniani kote?
Jina la Yahwe Bwana wetu ni tukufu.
Yahwe aliumba nini kutoka katika midomo ya watoto wachanga?
Yahwe aliumba sifa.
Kwa nini Yahwe aliumba sifa?
Aliumba sifa ili kumweka kimya adui na anayelipiza kisasi.
Psalms 8:3-5
Daudi aliangalia nini kilicho msababisha kufikiri kuwa wanadamu sio muhimu?
Aliangalia mbingu, mwezi, na nyota.
Wanadamu wanalinganishwaje na viumbe vya mbinguni?
Yahwe aliwaumba wanadamu chini kidogo ya viumbe wa mbinguni.
Yahwe aliwavika nini wanadamu?
Aliwavika taji ya utukufu na heshima.
Psalms 8:6-8
Yahwe alimfanya binadamu kufanya nini?
Yahwe alimfanya kutawala juu ya kazi za mikono ya Yahwe.
Ni vitu gani ambavyo Yahwe aliweka chini ya miguu ya binadamu?
Aliweka kondoo wote na ngome, na hata wanyama wa shambani, ndege wa mbinguni, na samaki wa baharini, na kila kitu kinachopita katika mikondo ya bahari chini ya miguu ya mwanadamu.
Psalms 8:9
Ni jina la nani tukufu duniani kote?
Jina la Yahwe Bwana wetu ni tukufu.
Psalms 9
Psalms 9:1-2
Daudi alitoaje shukrani kwa Mungu na ataeleza nini?
Atatoa shukrani kwa Yahwe kwa moyo wake wote na kueleza kuhusu matendo yake makuu.
Psalms 9:3-4
Nini kinatokea kwa adui wa Daudi wanapogeuka?
Adui anajikwaa na kuangamia mbele ya Yahwe.
Mwamuzi mwenye haki amefanya nini kwa ajili ya Daudi?
Mwamuzi mwenye haki ameketi kwenye kiti chake cha enzi na ametetea haja ya haki ya Daudi.
Psalms 9:5-6
Mwamuzi mwenye haki alifanya nini kwa mataifa na waovu?
Aliyatisha matifa na kilio chake cha vita, akawaangamiza waovu, na kutia doa kumbukumbu yao milele.
Nini kilitokea kwa adui wakati mwamuzi mwenye haki alivyoipindua miji yao?
Adui alianguka kama vitu vya uharibifu na kumbukumbu yao yote ikapoteaa.
Psalms 9:7-8
Nani anabaki milele na kuimarisha kiti chake cha enzi kwa ajili ya haki?
Yahwe anabaki milele na kuimarisha kiti chake cha enzi kwa ajili ya hukumu.
Yahwe anahukumuje dunia na anafanya nini kwa ajili ya mataifa?
Yahwe anahukumu ullimwengu kwa haki na kufanya maamuzi ya haki kwa ajili ya mataifa.
Psalms 9:9-10
Yahwe atakuwa nini kwa ajili ya waliokandamizwa?
Yahwe atakuwa ngime kwa ajili ya wale waliokandamizwa wakati wa taabu.
Daudi anamwomba Yahwe kufanya nini kwa ajili ya wale wanaomtafuta?
Daudi anamwomba Yahwe kutowaacha wale wanaomtafuta.
Psalms 9:11-12
Daudi anasema watu wanapaswa kufanya nini kwa Yahwe, anaye watawala?
Wanapaswa kuimba sifa kwa Yahwe na kuyaambia maataifa ambacho Yahwe amefanya.
Mungu hasahau nini?
Hasau kilio cha walio kanandamizwa.
Psalms 9:13-14
Daudi anamwomba Yahwe amfanyie nini?
Anamuuliza Yahwe awe na huruma juu yake.
Daudi anakandamizwa nani?
Daudi anakandamizwa na wale ambao wanamchukia.
Daudi atafurahi wapi katika wokovu?
Daudi atafurahi katika wokovu wa malango ya binti Sayuni.
Psalms 9:15-16
Nini kilitokea kwa mataifa?
Mataifa yalizama chini katika shimo ambalo walitengeneza na miguu yao ilishikwa katika wavu walioficha.
Nani alijifanya kujulikana na kupitisha hukumu?
Yahwe alifanya ajulikane na kutekeleza hukumu.
Psalms 9:17-18
Waovu wanatumwa wapi?
Wanatumwa kuzimu, ambayo ni hatma ya mataifa yote ambayo yanamsahau Mungu.
Nini kitatokea kwa wahitaji na waliokandamizwa?
Wahitaji hawatasahaulika daima wala matumaini ya waliokandamizwa hayatavunjwa milele.
Psalms 9:19-20
Daudi anamtaka Yahwe amzuie binadamu kufanya nini?
Daudi anamtaka Yahwe kuinuka na kutomruhusu mtu kumshinda.
Daudi anamwomba Yahwe kufanya nini kwa maatifa?
Anamwomba Yahwe kuwatisha na kuwafanya watambue kuwa wao ni watu tu.
Psalms 10
Psalms 10:1-3
Mwandishi anahisije Yahwe anavyomtendea?
Mwandishi anahishi kwamba Yahwe amesimama mbali na amejificha.
Mwandishi anamwomba Yahwe kufanya nini kwa watu waovu?
Mwandishi anamwomba Yahwe kuwaruhusu waovu kutegwa kwa hila zao wenyewe.
Psalms 10:4-5
Kwa mtu mwovu hamtafuti Mungu?
Mtu mwovu hamtafuti Mungu kwa sababu ana kiburi sana.
Psalms 10:6-7
Mtu mwovu husema nini moyoni mwake?
Mtu mwovu anasema, "Sitaanguka kamwe; katika vizazi vyote sitakutakana na taabu."
Nini hujaza mdomo wa mtu mwovu?
Mdomo wake umejaa laana na maneno ya uongo ya kudhuru.
Psalms 10:8-10
Mtu mwovu ni kama mnyama gani?
Yeye ni kama simba anayejificha sehemu ya siri nene na kulala akisubiri waliokandamizwa.
Psalms 10:11-12
Mtu mwovu anasema nini moyoni mwake kumhusu Mungu?
Mtu mwovu anasema, "Mungu amenisahau; anafunika uso wake; hatahangaika kuangalia."
Mwandishi anamtaka Yahwe amwitikiaje mtu mwovu?
Anamtaka Yahwe kuinua juu mkono wake katika hukumu na kutowasahau waliokandamizwa.
Psalms 10:13-14
Mtu mwovu anasema nini moyoni mwake kwa Mungu?
Anasema, "Hautaniwajibisha".
Psalms 10:15-18
Mtu mwovu aliwaza nini kuhusu matendo yake maovu?
Alifikiri kuwa Mungu hatayagundua.
Yahwe anaitikiaje mahitaji ya walio kandamizwa?
Anaimarisha mioyo yao, anasikiliza maombi yao, na anawatetea.
Psalms 11
Psalms 11:1-2
Daudi anamkimbilia nani?
Daudi anamkimbilia Yahwe.
Watu watasema nini kwa Daudi kuhusu nafsi yake?
Watamwambia kukimbia kama ndege kwenye mlima.
Waovu wanajiandaaje kumshambuli mnyofu moyoni?
Wanaandaa pinde zao kuweka tayari mishale yao.
Psalms 11:3-4
Yahwe anafanya nini katika hekalu lake takatifu?
Macho yake yanatazama na kuchunguza watoto wa wanadamu.
Psalms 11:5-7
Yahwe anachunguza nini?
Anawachunguza wenye haki na waovu.
Yahwe anachukia nini?
Anawachukia wale wanaopenda kufanya vurugu.
Yahwe anafanya nini kwa waovu?
Anawanyeshea makaa na kibiriti juu yao na kumwaga upepo wa kuchoma kutoka katika kikombe chake.
Yahwe anafikiria nini juu ya wenye haki?
Anapenda haki.
Nini kitatokea kwa wanyofu?
Wanyofu wataona uso wa Yahwe.
Psalms 12
Psalms 12:1
Kwa nini Daudi anaomba msaada wa Yahwe?
Daudi anamwomba Yahwe kumsaidia kwa sababu watauwa na waaminifu wamepotelea.
Psalms 12:2-4
Kila mmoja anazungumzaje na jirani yae?
Kila mtu anasema maneno yenye utupu kwa jirani yake, na kuzungumza kwa midomo ya kujipendekeza na moyo uliogawanyika.
Daudi anamtaka Yahwe afanye nini kwa midomo inayojipendekeza?
Daudi anamtaka Yahwe kuikata midomo yote ya kujipendekeza na kila ulimi unaotangaza vitu vikubwa.
Ni vitu gani vya kujipendekeza ambavyo baadhi wamesema?
Baadhi wamesema, "Kwa ndimi zetu tutashinda. Midomo yetu inapozungumza, nani anaweza kuwa bwana juu yetu?
Psalms 12:5
Yahwe atafanya nini kwa masikini na wahitaji?
Yahwe atainuka na kutoa usalama ambao wanashauku nayo.
Psalms 12:6-8
Maneno ya Yahwe yakoje?
Maneno ya Yahwe ni masafi kama fedha na yamesafishwa katika tanuu na kusafishwa mara saba.
Daudi anamwomba Yahwe kufanya nini kwa ajili ya watu watauwa
Anamwomba Yahwe kuwaweka na kuwatunza kutoka katika kizazi kiovu.
Nini husababisha waovu kutembea kila upande?
Waovu wanatembea kila upande wakati uovu unatukuzwa miongoni mwa wana wa watu.
Psalms 13
Psalms 13:3-4
Daudi anaombaje Yahwe ajibu ombi lake?
Anamwomba Yahwe kumtazama, kumjibu, na kufungua macho yake.
Daudi anaogopa nini kitatokea kama Yahwe asipojibu?
Daudi anahofu kuwa atalala katika kifo.
Daudi hataki adui zake wasema nini juu yake?
Hataki wasema kuwa wamemshinda adui yao.
Nini kitatokea kama Daudi akishindwa?
Adui zake watashangilia akiletwa chini.
Psalms 13:5-6
Daudi ametumaini katika nini?
Daudi amemtumaini katika agano la uaminifu wa Yahwe.
Moyo wa Daudi unafurahi katika nini?
Moyo wake unashangilia katika wokovu wa Yahwe.
Kwa nini Daudi ataimba kwa Yahwe?
Daudi ataimba kwa sababu Yahwe amemtendea kwa ukarimu sana.
Psalms 14
Psalms 14:1
Mpumbavu anasema nini moyoni mwake?
Mpumbavu anasema, "Hakuna Mungu."
Psalms 14:2-3
Kwa nini Yahwe anatazama chini kwa wanadamu?
Anatazama chini kuona kama kuna mtu anyeelewa, anayemtafuta yeye.
Nani amegeuka na kuwa mchafu?
Kila mtu amegeuka pembeni na wote wamekuwa wachafu.
Psalms 14:4
Nani hamwiti Yahwe?
Wale wanaotenda udhalimu na kuwala watu wa Daudi kama wanavyokula mkate, na hawamwitii Yahwe.
Psalms 14:5-6
Kwa nini wale ambao hawamwiti Yahwe wanatetemeka na kuogopa?
Wanatetemeka kwa uoga kwa sababu Mungu yuko pamoja na kusanyiko la wenye haki.
Ni nani kimbilio la mtu masikini?
Yahwe ni kimbilio lake.
Psalms 14:7
Daudi anataka nini kije kutoka Sayuni?
Daudi anataka wokovu wa Israeli utoke Sayuni.
Yakobo itashangilia lini na Israeli kufurahi?
Wakati Yahwe atakapowarudisha watu wake kutoka katika mateka.
Psalms 15
Psalms 15:1-2
Ni aina gani ya mtu anaweza kukaa katika hema takatifu la Yahwe na kuishi katika kilima chake kitakatifu?
Mtu anayetembea bila lawama, anayetenda cha haki, na kuzungumza ukweli kutoka moyoni mwake anaweza kubaki katika hema lake takatifu na kuishi katika kilima chake kitakatifu.
Psalms 15:3
Mtu huyu ambaye hana lawama hafanyi nini na ulimi wake?
Hakashifu kwa ulimi wake.
Psalms 15:4-5
Mtu huyu ambaye hana lawama anachukia nini?
Huchukia mtu asiyefaa.
Mtu huyu ambaye hana lawama anaheshimu nini?
Anawaheshimu wale wanaomcha Yahwe.
Wakati mtu huyu anapoapa katika hasra yake, huwa hafanyi nini?
Harudishi ahadi zake.
Mtu huyu ambaye hana hatia anapokopesha fedha, huwa hafanyi nini?
Hatozi riba.
Mtu huyu ambaye hana lawama hachukui rushwa kwa ajili ipi?
Hachukui rushwa kushuhudia dhidi ya wasio na hatia.
Nini hakitawahi kutokea kwa mtu asiye na lawama ambaye hufanya hivi vitu?
Hatatikisika.
Psalms 16
Psalms 16:1-3
Daudi anamwomba Mungu kumfanyia nini?
Daudi anamtaka Mungu amlinda kwa sababu anamkimbilia.
Daudi anagundua nini kuhusu uhusiano wake kwa Yahwe?
Daudi anatambua kwamba Yahwe ni Bwana wake, na wema wa Daudi ni bure nje ya Yahwe.
Ni nani watakatifu wa duniani?
Ni watu wenye heshima ambao Daudi anawafurahia.
Psalms 16:4
Nini kitatokea kwa wale wanaotafuta miungu yao?
Taabu itaongezeka kwa wale wanaotafuta miungu mingine.
Daudi hataabudu miungu mingine kwa njia gani?
Hatamwaga vimiminiko vya sadaka ya damu kwa miungu yao, au kuinua majina yao kwa midomo yake.
Psalms 16:5-6
Daudi anagundua nini ambacho Yahwe humtendea?
Yahwe anashikilia hatima ya Daudi, humpa sehemu nzuri, na urithi mzuri.
Psalms 16:7-8
Kwa nini Daudi anambariki Yahwe?
Daudi anambariki Yahwe kwa sababu Yahwe anamshauri.
Psalms 16:9-10
Kwa nini moyo wa Daudi unaitika kwa Yahwe?
Moyo wa Daudi unafuraha, na unamtukuza Yahwe.
Yahwe hataruhusu nini kitokea kwa yule ambaye ana agano la uaminifu?
Yahwe hatamwacha kuona shimo.
Psalms 16:11
Daudi anapata faida gani kutoka kwa Yahwe?
Yahwe humfundisha Daudi njia ya uzima, humpa furaha, na furaha zinazotokana na kuwa katika mkono wa kuume wa Yahwe milele.
Psalms 17
Psalms 17:1-2
Daudi anamwomba Mungu amfanyie nini?
Daudi anamwomba Yahwe kumtetea kwa ajili ya haki, kusikiliza kwa usikivu wito wake wa msaada, na kusikiliza ombi lake.
Daudi anaomba nini kiju kutoka katika uwepo wa Yahwe?
Daudi anaomba kuwa uthibitisho wake utoke katika uwepo wa Yahwe.
Psalms 17:3
Nini kitatokea kwa Daudi kama Yahwe atakuja kwake usiku?
Yahwe atamtakasa na hatapata mipango yoyote ya uovu au dhambi mdomoni mwake.
Psalms 17:4-5
Daudi amejiewkaje kutoka katika njia ya wahalifu?
Ni katika neno la midomo ya Yahwe ambamo Daudi amejiepusha na njia za uhalifu.
Psalms 17:6-7
Kwa nini Daudi anamwita Mungu?
Daudi anamwita Mungu kwa sababu Mungu humjibu.
Daudi anamwomba Mungu amwoneshe nini?
Anamwomba Mungu kuonesha uaminifu wake wa agano kwa namna ya ajabu.
Mungu anamwokoa nani kwa mkono wake wa kuume?
Anawaokoa wale wanaomkimbilia kutoka kwa adui zao.
Psalms 17:8-10
Daudi anaelezaje njia ambayo Mungu anamlinda kutoka kwa adui waovu wanaomshambulia?
Mungu atamlinda Daudi kama mboni la jicho la Mungu kwa kumficha chini ya kivuli cha mabawa ya Mungu.
Daudi anawaelezeaje adui zake?
Anasema adui zake hawana huruma kwa yeyote, na midomo yao inazungumza kwa majivuno.
Psalms 17:11-12
Adui wa Daudi wamefanya nini kwake?
Wamesunguka hatua zao na kuweka macho yao kwake kumwangusha ardhini.
Psalms 17:13-14
Daudi anamwomba Yahwe kuwafanya nini adui zake?
Anamwomba Yahwe kuinuka, kushambulia adui azke, na kuwatupa chini katika nyuso zao.
Daudi anamwomba Yahwe kumwokoa kutoka katika mkono wa nani?
Anamwomba Yahwe kumwokoa kutoka kwa watu wa dunia hii ambao mafanikio yao yako katika maisha haya tu.
Yahwe atawahudumieaje hazina yake?
Yahwe atayajaza matumbo yao kwa utajiri ili wawe na watoto wengi ambao watawaachia utajiri wao.
Psalms 17:15
Daudi anategemea nin ikitokee anapoana uso wa Yahwe katika haki?
Ataridhika kwa kumwona Yahwe.
Psalms 18
Psalms 18:1
Daudi anaonesha hisia gani mbele ya Yahwe?
Anasema, "Nakupenda."
Psalms 18:2-5
Nini kitatokea Daudi akimwita Yahwe?
Daudi atakombolewa kutoka kwa adui zake.
Psalms 18:6
Yahwe alikuwa wapi aliposikia sauti ya Daudi?
Yahwe alisikia sauti ya Daudi kutoka katika hekalu lake.
Psalms 18:7-8
Kwa nini misingi ya dunia ilitikisika?
Ilitikisika kwa sababu Mungu alikasirika.
Psalms 18:9-12
Yahwe alishukaje kutoka mbinguni?
Aliendesha juu ya kerubi na kupaa; aliteleza juu ya mabawa ya upepo.
Psalms 18:13-14
Yahwe aliwatawanyishaje adui zake?
Alipiga mishale yake na kuwatawanya.
Psalms 18:15
Nini kilionesha misingi ya dunia?
Kilio cha vita cha Yahwe na mlipuko wa pumzi wa kutoka katika tundu za pua.
Psalms 18:16-17
Yahwe alimvuta Daudi kutoka kwenye nini?
Alimvuta Daudi kutoka kwenye maji yanayoenda mbele.
Psalms 18:18-26
Kwa Yahwe alimwokoa Daudi?
Yahwe alimwokoa Daudi kwa sababu Yahwe alipendezwa naye.
Psalms 18:27-29
Yahwe anafanya nini watu walioteswa?
Huwaokoa watu walioteswa.
Yahwe anawafanya nini wale wenye macho ya kiburi na yaliyoinuka?
Huwaleta chini wale wenye macho ya kiburi yaliyoinuka.
Psalms 18:30-36
Daudi anaielezeaje njia ya Yahwe?
Anasema njia ya Yahwe ni kamili.
Psalms 18:37-39
Daudi anawafanyia nini adui zake?
Daudi aliwafuatilia adui zake na kuwashika.
Psalms 18:40-42
Nini kilitokea wakati adui wa Daudi walipomwita Yahwe?
Yahwe hakuwajibu.
Psalms 18:43-47
Yahwe amemweka Daudi kichwa juu ya nini?
Yahwe amemfanya Daudi mkuu juu ya mataifa.
Psalms 18:48-49
Daudi anawekwa huru kutoka kwa nani?
Anawekwa huru kutoka kwa adui zake.
Psalms 18:50
Yahwe anaonesha uaminifu wake wa agano kwa nani?
Anaonesha uaminifu wake wa agano kwa mtiwa mafuta wake, Daudi na uzao wake milele.
Psalms 19
Psalms 19:1-3
Mbingu zinatangaza nini na anga zinaweka nini wazi?
Mbingu zinatangaza utukufu wa Mungu na anga zinaweka wazi kazi ya mikono yake.
Maneno yanayomwagwa yanaonesha nini?
Maneno yanayomwagwa yanaonesha maarifa.
Psalms 19:4-6
Maneno ya mbingu na anga yanaenda wapi?
Maneno yao yanaenda juu ya dunia yote, hadi mwisho wa dunia.
Jua ni kama nini?
Jua ni kama bwana arusi, na kama mtu mwenye nguvu.
Psalms 19:7-8
Sheria ya Yahwe inafanya nini?
Sheria ya Yahwe hurejesha nafsi.
Hukumu za Yahwe zinafanya nini?
Hukumu za Yahwe humpa hekima asiye na uzoefu.
Maagizo ya Yahwe yanafanya nini?
Huufanya moyo kuwa wenye furaha.
Amri za Yahwe zinafanya nini?
Hutoa utambuzi kwa macho
Psalms 19:9-10
Hukumu za haki za Yahwe zinalinganishwaje na dhahabu?
Zina thamani zaidi ya dhahabu, hata zaidi ya dhahabu safi.
Psalms 19:11-12
Hukumu za haki za Yahwe humfanya nini mtumishi wa Yahwe?
Kwa hayo anaonywa, zilimsababisha kutii na kupokea dhawabu kuu.
Daudi anaomba kusafishwa nini?
Anaomba kusafishwa na makosa yaliyojificha.
Psalms 19:13-14
Nini hutokea wakati mtumishi asiporuhusu dhambi zake senye kiburi kumtawala?
Atakuwa kamili na bila hatia kwa makosa mengi.
Daudi anataka nini kikubalike machoni pa Yahwe?
Daudi anataka maneno ya mdomo wake na mawazo ya moyo wake kukubalika machoni pa Yahwe.
Psalms 20
Psalms 20:1-2
Daudi anataka Mungu atume msaada kutoka wapi?
Anamwomba yahwe kutuma msaada kutoka katika mahali pake patakatifu na kumsaidia kutoka Sayuni.
Psalms 20:3-4
Daudi anataka Yahwe akumbuke na kukubali nini?
Daudi anamwomba Yahwe kukumbuka sadaka zake zote na kukubali sadaka za kuteketeza kwa moto.
Psalms 20:5-6
Daudi anasema atafurahi katika nini?
Daudi anasema kuwa atashangilia katika wokovu wa Yahwe.
Daudi anasema Yahwe ataokoa nini?
Daudi anajua kuwa Yahwe atamwokoa mtiwa mafuta wake.
Psalms 20:7-9
Watu wengine wanatumaini nini?
Wengine wanatumaini vibandawazi na wengine katika farasi.
Daudi na watu wake wanafanya nini ili kupata ushindi?
Wanamwita Yahwe Mungu wao.
Psalms 21
Psalms 21:1-2
Mfalme anashangilia nini?
Anashangilia katika nguvu ya Yahwe na katika wokovu amabao Yahwe anatoa.
Yahwe amefanya nini kwa ajili ya mfalme?
Yahwe amempa mfalme hamu zake za moyoni na hajakataa ombi la midomo yake.
Psalms 21:3-4
Yahwe ameleta nini kwa mfalme na ameweka nini katika kichwa chake?
Alimletea mfalme baraka nyingi na kuweka taji la dhahabu safi zaidi kichwani pake.
Yahwe alimpa nini mfalme baada ya mfalme kukiomba?
Yahwe alimpa mfalme maisha na siku nyingi milele na milele.
Psalms 21:5-6
Kwa nini utukufu wa mfalme ni mkuu?
Utukufu wake ni mkuu kwa sababu ya ushindi wa Yahwe.
Yahwe ameweka nini juu ya mfalme?
Yahwe ameweka fahari na utukufu.
Psalms 21:7-8
Kwa nini mfalme hatasogezwa?
Hatasogezwa kwa sababu anatumaini Yahwe katika uaminifu wa agano wa Aliye juu.
Mkono wa Yahwe utamkamata nani?
Mkono wake utawakamata adui zake wanaomchukia Yahwe.
Psalms 21:9-10
Yahwe atafanya nini kwa adui zake?
Atawachoma, na watamezwa katika gadhabu yake.
Yahwe atafanya nini kwa kizazi cha adui zake?
Ataangamiza watoto wake na uzao wake.
Psalms 21:11-12
Kwa nini Yahwe ataangamiza adui zake?
Atawaangamiza kwa sababu walikusudia uovu dhidi yake.
Kwa nini njama za adui wa Yahwe hawatafanikiwa?
Haitafanikiwa kwa sababu Yahwe atawageuza na kuvuta upinde wake dhidi yao.
Psalms 21:13
Watu watamtukuzaje Yahwe?
Wataimba na kusifu nguvu zake.
Psalms 22
Psalms 22:1-2
Daudi anaomba nini?
Daudi anauliza kwa nini amemwacha, kwa nini yuko mbali kutoka kwa Daudi.
Daudi anafanya nini wakati wa mchana na usiku?
Daudi analia mchana na usiku na hayuko kimya.
Psalms 22:3-5
Daudi anamtambuaje Mungu?
Daudi anamtambua Mungu kama Mtakatifu, kukaa kama mfalme na sifa ya Israeli.
Uzao wa Daudi ulifanya nini na Mungu aliitikiaje?
Walimtumani Mungu, akawaokoa, na hawakunjwa tegemeo.
Psalms 22:6-8
Daudi anajielezaje?
Daudi anasema yeye ni mnyoo na sio mtu, aibu kwa binadamu na anachukiwa na watu.
Watu wanaomsuta na kumkejeli Daudi wanasema nini kwake?
Wanasema, "Anamtumaini Yahwe; acha Yahwe amwokoe."
Psalms 22:9-10
Daudi amemtumani Mungu kwa muda gani?
Daudi alimtumaini Mungu wakati yuko katika maziwa ya mama yake na tangu yuko kwenye tumbo la mama yake.
Psalms 22:11-13
Daudi anamwomba Mungu kumfanyia nini?
Anamwomba Mungu kutokuwa mbali na yeye kwa sababu taabu iko karibu na hakuna mtu wa kumsaidia.
NIni kinamzunguka Daudi kama simba anaye unguruma?
Mafahali wengi wa Bashani wamemzunguka na midomo ikiwa wazi dhidi yake.
Psalms 22:14-15
Daudi anajielezaje?
Anasema anamwagwa kama maji, mifupa yake yote imeteguka, moyo wake ni kama nta, nguvu yake imekauka, ulimi wake unachomoza hadi kwenye paa ya mdomo wake.
Psalms 22:16-17
Nini kimemzunguka Daudi na kumzingira?
Mbwa walimzunguka na kundi la watenda maovu walimzingira, wakiwa wamemchoma mikono na miguu yake.
Psalms 22:18-19
Nini kilifanyika kwa mavazi na nguo?
Mavazi yaligawanywa na kura kupigwa kwa ajili ya nguo.
Daudi anamwomba nini Yahwe?
Anamwomba Yahwe kutokuwa mbali.
Psalms 22:20-21
Daudi anataka kuokolewa na nini?
Anataka nafsi yake iokolewa kutoka katika upanga, maisha yake ya thamani kutoka katika nyao za mbwa, pembe za nyati, na uokolewe kutoka katika mdomo wa simba.
Psalms 22:22-23
Daudi atatangaza nini kwa ndugu zake na atamsifu Yahwe wapi?
Atatangaza jina la Yahwe kwa ndugu zake na kumsifu katikati ya kusanyiko.
Nani anapaswa kumsifu Yahwe, kumheshimu, na kusima kwa kumtaajabu Yahwe?
Wote wanaomcha Yahwe, uzao wote wa Yakobo, na uzao wote wa Israeli unapaswa kumsifu, kumheshimu, na kusimama kwa kumstaajabu.
Psalms 22:24-25
Yahwe alimsikia lini aliyeteswa?
Alimsikia aliyeteswa alipoaanza kulia kwake.
Daudi alisifu wapi na kukamilisha viapo vyake?
Atamsifu Yahwe katika kusanyiko kuu na kutimiza viapo vyake mbele yao wanaomcha Yahwe.
Psalms 22:26-27
Nani atakula, kuridhika, na kumsifu Yahwe?
Waliokanadamizwa watakula, wataridhika na wale wanaomtafuta Yahwe watamsifu.
Watu wote wa duniani na familia za mataifa zitafanya nini?
Watu wa dunia watakumbuka na kugeuka kwa Yahwe na familia za mataifa zitainama mbele zake.
Psalms 22:28-29
Yahwe anatawala juu ya nini?
Yahwe anatawala juu ya mataifa.
Nani atainama mbele ya Yahwe?
Wale wote wanaoshuka kwenye mavumbi, ambao hawawezi kutunza nafsi zao, watainama mbele zake.
Psalms 22:30-31
Vizazi vya mbele vitafanyaje?
Watakuja na kuwaambia watu ambao bado hawajazaliwa alichokifanya.
Psalms 23
Psalms 23:1-2
Mchungaji wa Daudi ni nani?
Mchungaji wa Daudi ni Yahwe.
Yahwe anamfanya Daudi kulala chini wapi?
Yahwe anamfanya Daudi kulala chini katika malisho ya kijani.
Yahwe anamwongoza wapi Daudi?
Yahwe anamwongoza Daudi kando ya maji yaliyotulia.
Psalms 23:3
Yahwe anarejesha nini?
Yahwe anarejesha nafsi ya Daudi.
Yahwe anamwongoza wapi Daudi?
Yahwe anamwongoza Daudi katika njia sahihi.
Psalms 23:4
Nani yuko pamoja na Daudi anapotembea katika kivuli cha giza?
Yahwe yuko pamoja na Daudi.
Psalms 23:5
Yahwe anaandaa nini mbele ya Daudi?
Yahwe anaandaa meza katika uwepo wa adui wa Daudi.
Yahwe anatia nini mafuta?
Yahwe anakitia mafuta kichwa cha Daudi.
Psalms 23:6
Nini kitamfuata Daudi siku zote za maisha yake?
Wema na uaminifu wa agano utamfuata Daudi.
Psalms 24
Psalms 24:1-2
Nani alianzisha dunia?
Yahwe alianzisha dunia juu ya bahari na kuiimarisha juu ya mito.
Psalms 24:3-4
Nani atapanda mlima wa Yahwe na kusimama katika sehemu takatifu ya Yahwe?
Wale walio na mikono misafi na mioyo misafi; ambao hawajainua nafsi zao kwa kile ambacho ni uongo, na ambao hawajaapa kwa uongo watapanda mlima wa Yahwe na kusimama katika sehemu yake takatifu.
Psalms 24:5-6
Nani atapokea baraka kutoka kwa Yahwe?
Kizazi cha wale ambao watamtafuta, wale wanaotafuta uso wa Mungu wa Yakobo, watapokea baraka.
Psalms 24:7-10
Kwa nini malango yanapaswa kuinuliwa?
Ili kwamba mfalme wa utukufu aingie ndani.
Psalms 25
Psalms 25:1-3
Daudi anamwomba nini Mungu?
Daudi anamwomba Mungu kutomuacha kuaibika, na kutowaacha adui zake kushangilia juu yake.
Psalms 25:4-5
Daudi anamwomba Yahwe kufanya nini kujulikana kwake?
Daudi anamwomba Yahwe kufanya njia za Yahwe zijulikane kwake.
Psalms 25:6-7
Daudi anamwomba Mungu akumbuke nini?
Daudi anamwomba Mungu kukumbuka matendo yake ya huruma na uaminifu wa agano, lakini kutokuwaza kuhusu dhambi za ujana wa Daudi au ukaidi wake.
Psalms 25:8-9
Yahwe anafanya nini kwa sababu ni mwema na mwenye haki?
Huwafundisha watenda dhambi njia, kuwaongoza wanyenyekevu kwa haki, na kuwafundisha wanyenyekevu njia yake.
Psalms 25:10-11
Njia za Yahwe zinatengenezwa na nini?
Zimetengenezwa na uaminifu wa agano na uaminifu.
Kwa nini Yahwe anapaswa kusamehe dhambi za Daudi?
Anapaswa kumsamehe Daudi kwa ajili ya jina la Yahwe.
Psalms 25:12-13
Yahwe atafanya nini kwa mtu anayemcha Yahwe?
Bwana atamwongoza katika njia anayopaswa kuchagua.
Psalms 25:14-16
Yahwe anafanya nini kwa ajili ya wale wanaomheshimu?
Huwapa urafiki wake na kufanya agano lake kujulikana kwao.
Kwa Daudi huweka macho yake kwa Yahwe?
Kwa sababu Yahwe ataokoa miguu ya Daudi kutoka kwenye wavu.
Daudi anaomba nini kwa Yahwe anapokuwa mwenyewe na kuteseka?
Daudi anamwomba Yahwe kumgeukia na kuwa na huruma kwake.
Psalms 25:17-19
Wakati moyo wa Daudi unataabika huwa anamwomba nini Yahwe?
Daudi anamwomba Yahwe kuona mateso yake na kazi zake, kusamehe dhambi zake, na kuwaona adui zake wanaomchukia na kuwa wakatili kwake.
Psalms 25:20-21
Kwa nini Daudi hataaibishwa?
Kwa sababu anamkimbilia Yahwe.
Psalms 25:22
Daudi anamwomba Mungu kumwokoa kutoka kwa kitu gani?
Anamwomba Mungu kuokoa Israeli katika taabu zake.
Psalms 26
Psalms 26:1-3
Daudi anasema alitembeaje?
Daudi anasema ametembea kwa uadilifu na amemtumaini Yahwe bila kuwa na mashaka.
Daudi anamwomba Yahwe kuchunguza na kujaribu nini?
Anamwomba Yahwe kupima usafi wa ndani yake na moyo wake.
Nini kiko mbele ya macho ya Daudi?
Uaminifu wa agano wa Yahwe uko mbele ya macho ya Daudi.
Psalms 26:4-5
Daudi hajihusishi au kujichanganya na nani?
Daudi hajihusishi na watu waongo au kujichanganya na watu wasio wakweli.
Daudi anachukia nini?
Daudi anachukia kusanyiko la watenda maovu.
Daudi haishi na nani?
Haishi na waovu.
Psalms 26:6-8
Daudi anafanya nini anapozunguka madhabahu ya Yahwe?
Anaimba wimbo wa sifa na kutoa taarifa ya matendo yote ya ajabu ya Yahwe.
Daudi anajisikiaje kuhusu nyumba ambayo Yahwe anaishi?
Anaipenda nyumba ambayo Yahwe anaishi.
Psalms 26:9-10
Daudi anamwomba Yahwe kutofanya nini?
Daudi anamwomba Yahwe kutofagia nafsi yake pamoja na watenda dhambi, au maisha yake na watu wenye kiu ya damu.
Psalms 26:11-12
Daudi anasema atatembeaje?
Daudi anasema atatembea katika uadilifu.
Mguu wa Daudi unasimama wapi na atambariki Yahwe wapi?
Miguu yake inasimama katika ardhi ambayo iko sawasawa na atambariki Yahwe katika makusanyiko.
Psalms 27
Psalms 27:1
Kwa nini Daudi hakumwogopa mtu?
Daudi hapaswi kumwogopa yeyote kwa kuwa Yahwe ni nuru yake, wokovu wake, na kimbilio la maisha yake.
Psalms 27:2-3
Nini kitatokea wakati watenda maovu watakaposgea karibu na Daudi?
Adui zake walijikwaa na kuanguka.
Daudi hataogopa hali gani bali kuwa mjasiri?
Moyo wake hautaogopa hata kama jeshi likiweka kambi dhidi yake na vita kuinuka dhidi yake.
Psalms 27:4
Daudi amemwomba nini Yahwe?
Daudi ameomba kwamba aishi katika nyumba ya Yahwe siku zake zote za maisha yake, ili aone uzuri wa Yahwe, na kutafakari katika hekalu lake.
Psalms 27:5-6
Yahwe atamfanyia nini Daudi katika siku ya taabu?
Yahwe atamlinda katika kibanda chake, kumficha katika mfuniko wa hema lake, na kumwinua juu ya mwamba.
Daudi atamwabuduje Yahwe?
Daudi atatoa sadaka za furaha, ataimba, na kutengeneza nyimbo kwa Yahwe.
Psalms 27:7-8
Daudi anamwomba Yahwe kufanya nini?
Daudi anamwomba Yahwe kusikia sauti yake, kuwa na huruma kwake, na kumjibu.
Moyo wa Daudi unasema nini kumhusu Yahwe?
Moyo wa Daudi unasema, "Tafuta uso wake!"
Psalms 27:9-10
Daudi anamwomba Yahwe kutofanya nini?
Daudi anamwomba Yahwe asifiche uso wake kutoka kwake, kutompiga mtumishi wake katika hasira yake, wala kumtelekeza.
Yahwe atamweka Daudi katika hali gani?
Yahwe atamchukua Daudi hata kama baba yake na mama yake watamtelekeza.
Psalms 27:11-12
Daudi anamwomba Yahwe kufanya kwa sababu ya adui wa Daudi?
Daudi anamwomba Yahwe kumfundisha njia za Yahwe na kumwongoza katika njia iliyo sawasawa kwa sababu ya adui zake.
Kwa nini Daudi anamwomba Yahwe kutotoa nafsi yake kwa adui zake?
Daudi anamwomba Yahwe kutowapa adui zake nafsi yake kwa sababu mashahidi waongo wameinuka juu dhidi yake, na wanapumua vurugu.
Psalms 27:13-14
Daudi aliamini nini kilichomsaidia?
Aliamini kuwa ataona uzuri wa Yahwe katika nchi ya walio hai.
Daudi anawatia moyo watu kufanya nini?
Daudi anawatia moyo watu kumsubiri Yahwe, kuwa imara, na kuacha mioyo yao iwe na ujasiri.
Psalms 28
Psalms 28:1-2
Daudi analia kwa nani?
Daudi analia kwa Yahwe, mwamba wake.
Nini kitatokea kwa Daudi kama Yahwe asipomwitikia?
Daudi ataungana na wale wanaokwenda chini kaburini.
Daudi anataka nani asikie sauti ya maombi yake?
Daudi anamtaka Yahwe kusikia sauti ya kuomba kwake.
Psalms 28:3-5
Daudi anamwomba Yahwe kutofanya nini?
Daudi anamwomba Yahwe kutomburuza pamoja na waovu.
Daudi anamwomba Yahwe kuwapa nini waovu?
Daudi anamwomba Yahwe kuwapa kile ambacho matendo yao wanastahili na kuwalipa kwa ajili ya madai yao ya uovu.
Mtu mwovu haelewi nini?
Mwovu haelewi njia za Yahwe au kazi ya mikono yake.
Psalms 28:6-8
Yahwe amesikia nini?
Yahwe amesikia sauti ya ombi la Daudi.
Ni nani nguvu na ngao ya Daudi?
Yahwe ni nguvu ya Daudi na ngao yake.
Moyo wa Daudi unamtumaini nani?
Moyo wa Daudi unamtumaini Yahwe na kushangilia sana.
Ni nani nguvu ya watu wake?
Yahwe ni nguvu ya watu wake.
Ni nani kimbilio la wokovu la mtiwa mafuta wake?
Yahwe ni kimbilio la wokovu la mtiwa mafuta wake.
Psalms 28:9
Daudi anamtaka Yahwe kumwokoa na kumbariki?
Daudi anamtaka Yahwe awaokoe watu wake na kubariki urithi wake.
Psalms 29
Psalms 29:1-2
Daudi anasema nani akiri kuwa Yahwe ana utukufu na nguvu?
Daudi anasema kuwa wana wa wenye nguvu wanapaswa kukiri utukufu na nguvu ya Yahwe.
Jina la Yahwe linastahili nini?
Jina la Yahwe linastahili heshima.
Psalms 29:3-5
Daudi analinganisha sauti ya Yahwe na nini?
Analinganisha sauti ya Yahwe na radi.
Yahwe anavunja nini katika vipande?
Yahwe anavunja seda za Lebanoni katika vipande.
Psalms 29:6-8
Yahwe anatikisa nini?
Yahwe anatikisa nyika za Kadeshi.
Psalms 29:9-10
Watu wote katika hekalu la Yahwe wanasema nini?
Watu wote katika hekalu lake wanasema, "Utukufu!"
Yahwe ataketi kama mfalme hadi lini?
Yahwe ameketi kama mfalme milele.
Psalms 29:11
Ni mambo gani mawili ambayoYahwe anawapa watu wake?
Yahwe anawapa nguvu watu wake na kuwabariki watu wake kwa amani.
Psalms 30
Psalms 30:1-3
Kwa nini Daudi anamtukuza yahwe?
Anamtukuza Yahwe kwa sababu Yahwe amemwinua Daudi na hawaruhusu adui wa Daudi kushangilia juu yake.
Yahwe alifanya nini Daudi alipokuja akilia kwa ajili ya msaada?
Yahwe alimponya Daudi.
Yahwe aliinua nafsi ya Daudi kutoka wapi?
Yahwe aliinua nafsi ya Daudi kutoka kuzimu.
Psalms 30:4-5
Waaminifu wanaambiwa kufanya nini kwa ajili ya kumbukumbu ya utakatifu wa Yahwe?
Waaminifu wanaambiwa kuimba sifa kwa Yahwe na kumpa shukrani.
Hasira na fadhila za Yahwe zinadumu hadi lini?
Hasira ya Yahwe ni kwa muda tu, lakini fadhila yake ni ya maisha yote.
Nini hutokea baada ya kulia kuja kwa usiku mmoja?
Furaha huja asubuhi.
Psalms 30:6-8
Daudi alisema nini kwa ujasriri?
Daudi alisema, "Sitatikiswa kamwe."
Nini kilitokea kwa Daudi Yahwe alipoficha uso wake?
Yahwe alipoficha uso wake, Daudi alitaabika.
Daudi alitafuta nini kutoka kwa Bwana?
Daudi alitafuta fadhila kutoka kwa Bwana.
Psalms 30:9-10
Daudi anamwomba Yahwe kumfanyia nini?
Daudi anamwomba Yahwe kumsikia, kuwa na huruma kwake, na kuwa msaidizi wake.
Psalms 30:11-12
Yahwe amefanya nini kwa ajili Daudi?
Yahwe amegeuza maombolezo ya Daudi kuwa kucheza, ameondoa gunia na kumvika na furaha.
Moyo ulioheshimiwa wa Daudi utafanya nini?
Moyo wa Daudi utaimba sifa kwa Yahwe na hautakuwa kimya. Atatoa shukrani kwa Yahwe Mungu wake milele.
Psalms 31
Psalms 31:1-2
Daudi anamkimbilia nani?
Daudi anamkimbilia Yahwe.
Daudi anamwomba Yahwe kuwa nini kwa ajili yake?
Anamwomba Yahwe kuwa mwamba wake wa kimbilio na ngome ya kumwokoa.
Psalms 31:3-4
Kwa nini Daudi anamwomba Mungu kumwongoza?
Daudi anamwomba Mungu kumwongoza kwa ajili ya jina la Yahwe.
Kwa nini Daudi anaamini kuwa Yahwe atamnyakua kutoka katika wavu ambao adui zake wameficha kwa ajili yake?
Yahwe atamnyakua kutoka katika wavu kwa sababu Yahwe ni kimbilio lake.
Psalms 31:5-7
Daudi anakabidhi roho yake wapi?
Daudi anakabidhi roho katika mikono ya Yahwe.
Daudi anawachukia kina nani?
Anawachukia wale wanaotumikia sanamu zisizofaa.
Kwa nini Daudi atafurahi na kushangilia katika uaminifu wa agano wa Yahwe?
Daudi atafurahi na kushangilia kwa sababu Yahwe ameona mateso yake na kufahamu dhiki za nafsi yake.
Psalms 31:8-9
Yahwe ameweka wapi miguu ya Daudi?
Yahwe ameweka miguu ya Daudi kataika sehemu pana ya wazi.
Kwa nini Daudi anamtaka Yahwe kuwa na huruma kwake?
Anamtaka Yahwe kuwa na huruma juu yake kwa sababu yuko katika dhiki na macho yake yamechoka kwa huzuni.
Psalms 31:10-11
Kwa nini nguvu ya Daudi inafifia na mifupa yake kupotea?
Nguvu yake inafifia na mifupa yake kupotea kwa sababu ya dhambi yake.
Watu waliitikiaje hali ya Daudi?
Watu wanamdharau, jirani zake wanatishwa na kushtuliwa na hali yake, na wale wanaomwona mtaani wanamkimbia.
Psalms 31:12-13
Daudi anajifananisha na nini?
Daudi anasema kuwa amesahaulika kama mtu aliyekufa amabye hakuna mtu anayemfikiria, na kwamba ni kama chungu kilichovunjika.
Kwa nini Daudi ametaabika?
Amesikia manong'onezo ya wengi, taarifa za kutisha kutoka kila upande wakati wanapanga njama pamoja za kuchukua maisha yake.
Psalms 31:14-16
Daudi anamwomba Mungu kumwokoa kutoka kwa nani?
Anamwomba Mungu kumwokoa kutoka kwa adui zake na kwa wale wanaomfuatilia.
Daudi anamwomba Mungu kufanya nini kwa ajili ya mtumishi wake?
Daudi anamwomba Mungu kufanya uso wake ung'ae juu ya Daudi, na kumwokoa katika uaminifu wa agano wa Yahwe.
Psalms 31:17-18
Daudi anamwomba Yahwe asiruhusu nini kitokee kwa Daudi?
Daudi anamwomba Yahwe kutomwacha aaibike.
Kwa nini midomo midanganyifu inapaswa kunyamazishwa?
Wanazungumza dhidi ya wenye haki kwa ukaidi na kwa kiburi na chuki.
Psalms 31:19-20
Uzuri wa Yahwe umetunzwa kwa ajili ya nani?
Uzuri wa Yahwe umetunzwa kwa ajili ya wale wanao mheshimu sana.
Yahwe anawaficha nini wale wanomheshimu sana?
Anawaficha hila za watu na vurugu za ndimi.
Psalms 31:21-22
Kwa nini Yahwe anapaswa kubarikiwa?
Yahwe alimwonesha Daudi uaminifu wake wa ajabu wa agano wakati Daudi alipokuwa katika mji uliotekwa.
Yahwe alifanya nini kwa ajili ya Daudi licha ya kwamba Daudi alisema kuwa amekatwa katika macho ya Mungu?
Yahwe alisikia ombi lake kwa ajili ya msaada wakati Daudi alipolia kwake.
Psalms 31:23-24
Yahwe anafanya nini kwa ajili ya wafuasi wake waaminifu?
Yahwe anawalinda waaminifu lakini anawalipa wenye kiburi kwa ukamilifu.
Daudi anatoa ushauri gani kwa wale wanaomtumaini Yahwe?
Anawaambia kuwa imara na ujasiri.
Psalms 32
Psalms 32:1-2
Yahwe anawabarikije watu?
Yahwe anawabariki watu kwa kuwasamehe makosa na kufunika dhambi zao.
Psalms 32:3-4
Nini kilitokea kwa Daudi alipobaki kimya?
Mifupa yake ilipotea na akagumia siku nzima. Mkono wa Mungu ulikuwa mzito juu ya Daudi na nguvu yake ikanyauka.
Psalms 32:5-6
Mungu alifanya nini Daudi alipokiri dhambi yake na kuacha kuficha udhalimu wake?
Mungu alisamehe hatia ya dhambi ya Daudi.
Watu watauwa wanapaswa kufanya nini?
Wanapaswa kuomba kwa Yahwe katika wakati wa dhiki.
Nini kitatokea kwa watauwa wanaoomba kwa Yahwe wakati wa dhiki kuu?
Wakati maji yanayokimbia yakitiririka, hayatawafikia hao watu.
Psalms 32:7-8
Mungu anamzunguka Daudi na nini?
Mungu anamzunguka Daudi na nyimbo za ushindi.
Psalms 32:9-10
Nini kitatokea kwa yule anayemtumaini Yahwe?
Uaminifu wa agano wa Yahwe utamzunguka.
Psalms 32:11
Wenye haki na wanyofu wa moyo wanapaswa kufanya nini kwa ajili ya Yahwe?
Wanyofu wa moyo wanapaswa kushangilia na kupiga kelele ya furaha.
Psalms 33
Psalms 33:1-3
Mwandishi anasema wenye haki wanapaswa kushangili katika nani?
Wenye haki wanapaswa kushangilia katika Yahwe.
Mwandishi anasema Yahwe apewe shukrani kwa kutumia vyombo vipi?
Mwandishi anasema kumpa Yahwe shukrani kwa kinubi.
Psalms 33:4-6
Mwandishi anaelezeaje maneno na matendo ya Yahwe?
Neno la Yahwe ni adili na kila kitu anachofanya ni sawa.
Yahwe anapenda nini?
Yahwe anapenda haki na hukumu.
Nini kiliumbwa kwa neno la Yahwe?
Mbingu ziliumbwa kwa neno la Yahwe.
Nini kilitengenezwa kwa pumzi ya mdomo wa Yahwe?
Nyota zote zilitengenezwa kwa pumzi ya mdomo wa Yahwe.
Psalms 33:7-9
Mwandishi anasema Yahwe hufanya nini kwa maji ya bahari?
Hukusanya maji ya bahari pamoja kama rundo.
Mwandishi anasema wakazi wote wa duniani wanapaswa kufanya nini?
Wakazi wote wa duniani wanapaswa kusimama kwa kumstaajabu Yahwe.
Psalms 33:10-12
Mipango ya Yahwe itasimama hadi lini?
Mipango ya Yahwe itasimama milele, mipango ya moyo wake kwa vizazi vyote.
Psalms 33:13-17
Yahwe humtazama nani kutoka juu anapoishi?
Yahwe huwatazama watu wote, wote wanaoishi duniani.
Psalms 33:18-19
Jicho liko kwa nani?
Jicho la Yahwe liko kwa wale wanaomcha.
Psalms 33:20-22
Kwa nini mioyo yetu inapaswa kushangilia katika Yahwe?
Mioyo yetu inapaswa kushangilia katika yeye, kwa kuwa tunatumaini katika jina lake takatifu.
Psalms 34
Psalms 34:1
Daudi atamsifu Yahwe mara ngapi?
Daudi atamsifu Yahwe muda wote.
Psalms 34:2-3
Daudi anataka kumsikia nani anapomsifu Yahwe?
Daudi anataka waliokandamizwa kusikia na kushangilia.
Daudi anawaomba watu kufanya nini naye?
Daudi anawaomba wamsifu Yahwe na kuinua jina lake kwa pamoja.
Psalms 34:4-6
Nini kilitokea Daudi alipomtafuta Yahwe?
Yahwe alimjibu Daudi na kumpa ushindi juu ya hofu zake zote.
Nini hutokea kwa wale wanaomtafuta Yahwe?
Wanang'aa na nyuso zao hazina aibu.
Yahwe alifanya nini alipomsikia mtu huyu aliyekandamizwa akilia?
Yahwe alimwokoa katika taabu zake zote.
Psalms 34:7-9
Malaika wa Yahwe hufanya nini anapoweka kambi kwa wale wanaomcha yeye?
Malaika wa Bwana huwaokoa.
Ni nani mtu aliyebarikiwa?
Mtu amebarikiwa anayemkimbilia Yahwe.
Watu waliochaguliwa na Yahwe na kumcha wamepungukiwa nini?
Hawajapungukiwa kitu wale wanaomcha Yahwe.
Psalms 34:10-11
Daudi alisema nini kuhusu wale wanaomtafuta Yahwe?
Wale wanaomtafuta Yahwe hawatapungukiwa chochote kizuri.
Daudi anasema nini kwa watoto wake?
Daudi anasema, "Njooni, msikilize na nitawafundisha hofu ya Yahwe."
Psalms 34:12-14
Daudi anasema mtu anayetamani maisha anapaswa kufanya nini?
Daudi anasema anapaswa kuepuka kuzungumza uovu, kuepuka kuzungumza uongo, kuugeuka uovu, kufanya mema na kutafuta amani na kuitangaza.
Psalms 34:15-17
Yahwe anaitikiaje kilio cha wenye haki?
Macho yake yako kwa wenye haki na masikio yake yanasikiliza kilio chao.
Yahwe atawafanya nini watenda maovu, ambao yuko kinyume nao?
Atafuta kumbukumbu yao ktuoka duniani.
Yahwe hufanya nini wenye haki wanapomlilia?
Huwasikia na kuwaokoa kutoka katika taabu zao zote.
Psalms 34:18-20
Yahwe yuko karibu na nani?
Yuko karibu na walio vunjika moyo.
Yahwe humwokoa nani?
Yahwe anawaokoa wale walipondeka roho.
Nini hutokea kwa wenye haki ambao wana taabu nyingi?
Yahwe anawapa ushindi juu yao wote na kulinda mifupa yake yote.
Psalms 34:21-22
Nini kitatokea kwa waovu?
Uovu utawaua waovu.
Nini kitatokea kwa wale wanaowachukia wenye haki?
Watahukumiwa.
Yahwe hufanya nini kwa ajili ya watumishi wake wanaomkimbilia?
Hukomboa nafsi zao na hawatahukumiwa.
Psalms 35
Psalms 35:1-3
Daudi anamwomba Yahwe amfanyie nini?
Daudi anamwomba Yahwe kutenda kinyume ya wale wanaotenda dhidi yake, na kupigana dhidi ya wale wanopigana dhidi yake.
Daudi anamwomba Yahwe atumie silaha gani kumsaidia?
Anamwomba Yahwe kutumia ngao yake ndogo na kubwa, mkuki wake, na shoka yake ya vita.
Psalms 35:4-6
Daudi anataka nini kitokea kwa wale wanaopanga kumdhuru?
Daudi anataka wageuzwe na kustaajabishwa.
Daudi anataka nani awafukuze adui zake?
Anata malaika wa Yahwe awafukuze.
Psalms 35:7-8
Adui wa Daudi walifanya nini bila sababu?
Waliandaa wavu na kuchimba shimo kwa ajili ya Daudi.
Daudi anataka nini kitokee kwa adui zake?
Daudi anataka uharibifu kuwapita na kuwashangaza, kwa wao kushikwa katika nyavu zao wenyewe, na kwa wao kuanguka katika uharibifu wao.
Psalms 35:9-10
Daudi atashangilia katika nini?
Atashangilia katika wokovu wa Yahwe.
Psalms 35:11-12
Kwa nini Daudi anahuzuni?
Anahuzuni kwa sababu mashahidi wasio na haki wameinuka kumshtaki kwa uongo, na kumlipa uovu kwa mema.
Psalms 35:13-14
Daudi aliitikiaje taabu za adui zake?
Daudi alivaa gunia, akafunga kwa ajili yao, akaenda kwa huzuni na kuinama katika maombolezo kwa ajili yao.
Psalms 35:15-16
Adui waliitikiaje taabu za Daudi?
Walifurahi, wakakusnayika dhidi yake, wakamrarua, wakamdhihaki, na wakamsagia meno.
Psalms 35:17-18
Daudi atamshukuru Yahwe lini katika kusanyiko?
Atamshukuru Yahwe nafsi yake itakapookolewa kutoka katika mashambulizi yao ya uharibifu.
Psalms 35:19-20
Adui wa Daudi wanafanya nini badala ya kuzungumza amani?
Wanapanga maneno ya uongo dhidi ya wale wanaoishi katika amani.
Psalms 35:21-23
Daudi anamtaka Yahwe afanye nini kwa kuwa ameona taabu za Daudi?
Anamtaka Yahwe asiwe kimya, asiwe mbali naye, na kuamka kwa ajili ya utetezi wake.
Psalms 35:24-28
Kwa nini Daudi anasema kuwa Yahwe anapaswa kumtetea?
Anasema kuwa Yahwe anapaswa kumtetea kwa sababu ya haki ya Yahwe.
Psalms 36
Psalms 36:1-2
Dhambi inazungumzaje ndani ya moyo wa mtu mwovu?
Dhambi huzungumza kama mwaguzi ndani ya moyo wa mtu mwovu.
Mtu mwovu anajifarije?
Anafikiri kuwa dhambi yake haitagundulika na kuchukiwa.
Psalms 36:3-4
Maneno ya mtu mwovu yakoje?
Maneno yake ni ya dhambi na ya udanganyifu.
Mtu mwovu hataki kuwa nini?
Hataki kuwa na hekima na kufanya mema.
Mtu mwovu hufanya nini anapolala kitandani kwake?
Hupanga njia za kufanya dhambi wakati amelala kitandani kwake.
Psalms 36:5-6
Nini hufika mbinguni na kwenye mawingu?
Uaminifu wa agano wa Yahwe ulifika mbinguni, na uaminifu wake hufika mawinguni.
Hukumu ya Yahwe ikoje?
Hukumu yake ni kama mlima wa juu zaidi na bahari lenye kina kirefu zaidi.
Yahwe hutunza nini?
Yahwe huwatunza binadamu na wanyama.
Psalms 36:7-9
Nani hukimbilia chini ya kivuli cha mabawa ya Mungu?
Wanadamu hukimbilia chini ya kivuli cha mabawa ya Mungu.
Nini kitawaridhisha kwa wingi wanadamu?
Utajiri wa chakula cha nyumba ya Mungu kitawaridhisha wanadamu.
Psalms 36:10-12
Daudi anamwomba Mungu kunyosha uaminifu wake wa agano kwa nani?
Daudi anamwomba Mungu kunyosha uaminifu wa agano wa Mungu kikamilifu kwa wale wanaomjua Mungu.
Daudi anamwomba Mungu asiruhusu nini kitokee?
Daudi anamwomba Mungu kutoruhusu mguu wa mtu mwenye kiburi kuja karibu naye, na mkono wa mwovu kumwondoa.
Nini kitatokea kwa watenda maovu walioanguka?
Wanaangushwa chini na hawawezi kuinuka.
Psalms 37
Psalms 37:1-2
Kwa nini Daudi anasema kutoudhika kwa sababu ya watenda waovu?
Anasema kutoudhika kwa sababu ya watenda maovu kwa sababu watakauka punde kama nyasi zinavyonyauka kama mimea ya kijani.
Psalms 37:3-4
Kwa nini Daudi anasema kufurahi katika Yahwe?
Anasema kufurahi katika Yahwe ili akupe hamu za moyo wako.
Psalms 37:5-6
Kwa nini Daudi anasema kumtumaini Yahwe?
Anasema kumtumaini Yahwe ili atende kwa niaba yako, kuonesha haki yako kama mchana, na kutokuwa na hatia kwako kama siku wakati wa mchana.
Psalms 37:7
Daudi anasema tufanye nini mbele ya Yahwe?
Anasema tutulie mbele yake na kusubiri kwa uvumilivu, kutokuwa na wasiwasi kama mtu akijaribu kufanikisha njia zake za uovu.
Psalms 37:8-10
Kwa nini Daudi anasema kutokuwa na hasira au kukatishwa tamaa au kuwa na wasiwasi juu ya watenda maovu?
Watakatwa na kupotea, lakini wale wanaomsubiri Yahwe watarithi nchi.
Psalms 37:11-13
Nini kitatokea kwa wapole?
Watarithi nchi na kufurahi katika mafanikio makubwa.
Psalms 37:14-15
Nini kitatokea kwa waovu waliojaribu kuwaua wale walio wanyofu?
Panga za waovu zitaichoma mioyo yao wenyewe na pinde zao zitavunjika.
Psalms 37:16-17
Kwa nini kidogo walichonacho wenye haki ni bora kuliko kingi cha watu waovu?
Kidogo walichonacho wenye haki ni bora zaidi kwa sababu mikono ya watu waovu itavunjwa, lakini Yahwe atawashikilia watu wenye haki.
Psalms 37:18-19
Yahwe atawahudumiaje wasio na hatia?
Wasio na hatia hawataaibika nyakati mbaya zikija, watakuwa na chakutosha cha kula, na urithi wao utakuwa wa milele.
Psalms 37:20-21
Nini kitatokea kwa adui wa Yahwe?
Adui zake watakuwa kama utukufu wa malisho ambayo yatamezwa na kupotea katika moshi.
Psalms 37:22-24
Kuna faida gani ya Yahwe kuthibitisha hatua za mtu?
Hata kama atajikwaa, hataanguka chini kwa kuwa Yahwe anamshika kwa mkono wake.
Psalms 37:25-27
Daudi hajaoni nini kikitokea kwa mtu mwenye haki?
Hajaona mtu mwenye haki akiwa ametelekezwa au watoto wake wakiomba omba mkate.
Mtu mwenye haki ana mwenendo gani?
Ni mwenye neema siku nzima na anakopesha.
Watu wanapaswa kufanya nini kuwa salama milele?
Wanapaswa kugeuka maovu na kufanya kilicho sawa.
Psalms 37:28-30
Wenye haki watarithi nini?
Watarithi nchi na kuishi hapo milele.
Mdomo wa mwenye haki utazungumza nini?
Mdomo wa mtu mwenye haki huzungumza hekima na kuzidisha haki.
Psalms 37:31-33
Nini kitatokea kwa mtu mwenye haki ambaye mtu mwovu anamtafuta kumuua?
Yahwe hatamwacha katika mkono wa mtu mwovu au kumshutumu anapohukumiwa.
Psalms 37:34
Nini kitatokea kwa wale wanaomsubiri Yahwe?
Yahwe atawainua kuimiliki nchi.
Psalms 37:35-38
Nini kitatokea kwa mtu mwovu na anayetisha?
Atasambaa kama mti wa kijani katika udongo wake wa asili, lakini baadaye hatapatikana.
Psalms 37:39-40
Yahwe anawafanyia nini wenye haki?
Yahwe anawalinda wakati wa taabu, na kuwasaidia na kuwaokoa.
Psalms 38
Psalms 38:1-2
Daudi anamwomba Yahwe asifanye nini katika hasira yake?
Anamwomba Yahwe kutomkemea katika hasira yake, au kumwadhibu katika gadhabu yake.
Psalms 38:3-4
Kwa nini Daudi anasema, "Hakuna afya katika mifupa yangu?"
Anasema hakuna afya kwenye mifupa yake kwa sababu ya dhambi yake.
Nini kimemlemea Daudi?
Udhalimu wake umemlemea.
Psalms 38:5-6
Daudi anafanya nini siku nzima?
Anaomboleza siku nzima.
Psalms 38:7-8
Daudi analemewa na nini?
Analemewa aibu.
Psalms 38:9-10
Daudi anasema Bwana anaelewa nini?
Anasema Bwana anaelewa shauku yake ya ndani ya moyo.
Psalms 38:11-14
Kwa nini marafiki wa Daudi na wenzake wanamwepuka?
Marafiki wa Daudi na wenzake wanamwepuka kwa sababu ya hali yake.
Psalms 38:15-18
Daudi anaogopa adui zake watafanya nini kama mguu wake ukiteleza?
Kama mguu wa Daudi utateleza, adui zake watafanya vitu vibaya kwake.
Psalms 38:19-20
Adui zake wanalipaje wema alioufanya?
Wanamlipa Daudi uovu kwa uzuri na wanamtupia shutuma.
Psalms 38:21-22
Daudi anatumia majina gani anapomwomba Yahwe msaada?
Anamwita, "Yahwe", "Mungu", "Bwana", na "wokovu wangu."
Psalms 39
Psalms 39:1
Daudi aliamuwa atafanya nini?
Daudi aliamuwa kuchunga anachokisema na kufunga mdomo wake wakati yuko kwenye uwepo wa mtu mwovu.
Psalms 39:2-3
Nini kilitokea Daudi alipobaki kimya na kuzuia maneno yake kusema chochote kizuri?
Maumivu ya Daudi yalikuwa zaidi na moyo wake ukawa wa moto kama moto.
Psalms 39:4-5
Daudi anataka kujua nini kuhusu maisha yake?
Daudi anataka kujua maisha yake yataisha lini, urefu wa siku zake, na jinsi alivyo wakupita.
Daudi anasema maisha yake ni kama nini mbele ya Yahwe?
Urefu wa maisha ya Daudi ni kama bure mbele za Yahwe.
Psalms 39:6-7
Kila mmoja anaharakisha kufanya nini?
Kila mmoja anaharakisha kukusanya utajiri.
Ni nini tumaini pekee la Daudi?
Bwana ndiye tumaini pekee la Daudi.
Psalms 39:8-9
Daudi anamwomba Yahwe kumpa ushindi gani?
Daudi anamwomba Yahwe kumpa ushindi juu ya dhambi zake zote.
Daudi hataki kuwa chombo cha nini?
Daudi hataki kuwa kifaa cha matusi ya wapumbavu.
Daudi anaitikiaje kile amabacho Bwana alifanya?
Daudi yuko kimya na hafungui mdomo wake.
Psalms 39:10-11
Daudi amelemewa na nini?
Daudi amelemewa kwa kipigo cha mkono wa Bwana.
NIni hutokea wakati Bwana anapowaadhibu watu kwa ajili ya dhambi?
Bwana anameza nguvu yao kama nondo na sio kitu bali mvuke.
Psalms 39:12-13
Kwa nini Daudi anamwomab Yahwe kusikiliza kulia kwake na kutokuwa kiziwi kwake?
Anamwombwa Yahwe kumsikiliza kwa sababu Daudi ni kama mgeni kwake na mkimbizi kama baba zake walivyokuwa.
Daudi anamwomba Yahwe kufanya nini kabla Daudi hajafa?
Anamwomba Yahwe kuondoa macho yake kwake ili atabasamu tena.
Psalms 40
Psalms 40:1-2
Yahwe alifanya nini baada ya Daudi kumsubiri kwa uvumilivu?
Yahwe alimsikiliza Daudi na kusikia kilio chake.
Yahwe alifanya nini kingine kwa ajili ya Daudi?
Yahwe alimtoa Daudi kutoka kwenye shimo baya, kutoka kwenye udongo wa tope, na kuweka miguu yake juu ya mwamba.
Psalms 40:3-4
Wengi watafanya nini kwa sababu Mungu ameweka wimbo mpya wa sifa mdomoni mwa Daudi?
Wengi watauona na kumpa heshima Yahwe na kumtumaini Yahwe.
Nani amebarikiwa?
Mtu amfanyaye Yahwe tumaini lake na hawapi heshima wenye kiburi au wale wanaomgeuka Mungu ndiye aliyebarikiwa.
Psalms 40:5-6
Daudi anaelezeaje matendo na mawazo ya Mungu?
Matendo ya ajabu ya Mungu ni mengi na mawazo yake juu yetu hayawezi kuhesabiwa.
Psalms 40:7-9
Nini kimeandikwa kumhusu Daudi katika hati ya nyaraka
Imeandikwa kuwa anafurahi kufanya mapenzi ya Mungu na kwamba sheria za Mungu ziko moyoni mwake.
Daudi ametangaza nini katika kusanyiko kuu?
Ametangaza habari njema za haki ya Mungu katika kusanyiko kuu.
Psalms 40:10-11
Daudi hajaficha nini?
Hajaficha haki ya Mungu moyoni mwake wala uaminifu wa agano wa Mungu au uaminifu wake kwa kusanyiko kuu.
Daudi ameomba nini ambacho anataka Yahwe amtendee?
Daudi anaomba kwamba Yahwe asizuie matendo yake ya huruma kutoka kwa Daudi bali aruhusu uaminifu wa agano wa Yahwe na uaminifu wake daima umtunze Daudi.
Psalms 40:12-13
Kwa nini Daudi anaogopa?
Anaogopa kwa sababu ya taabu ambazo haziwezi kuhesabiwa zimemzunguka na udhalimu wake umempita. Moyo wake umemwangusha.
Anaomba nini ambacho Yahwe atafurahi kufanya?
Anaomba kwamba Yahwe afurahi kumwokoa.
Psalms 40:14-15
Daudi anaomba nini kitokee kwa wale wanaotafuta maisha yake?
Anaomba kuwa waaibishwe na kuchanganyikiwa, wageuzwe na kukosa heshima.
Psalms 40:16-17
Daudi anawaombea nini wale wanaomtafuta Mungu na kupenda wokovu wake?
Anaomba kwamba washangilie na kuwa na furaha katika Mungu, na kwamba wasema kila wakati, "Yahwe asifiwe."
Daudi anamwelezaje Bwana?
Bwana humfikiria, ni msaada wake, na huja kumsaidia Daudi.
Psalms 41
Psalms 41:1-3
Daudi anasema ni nani aliyebarikiwa?
Yule anayewajali wanyonge amebarikiwa.
Yahwe atafanya nini kwa ajili ya mtu aliyebarikiwa?
Yahwe atamwokoa, atamtunza na kumweka hai, na atabarikiwa duniani.
Yahwe hatafanya nini kwa mtu aliyebarikiwa?
Yahwe hatampa kwa mapenzi ya adui zake.
Yahwe atafanya nini kwa mtu aliyebarikiwa katika kitanda cha mateso?
Yahwe atamshikili katika kitanda cha mateso na kufanya kitanda cha ugonjwa kuwa kitanda cha uponyaji.
Psalms 41:4-6
Kwa nini Daudi alimwomba Yahwe kuwa na huruma juu yake?
Alimwomba Yahwe kuwa na huruma juu yake kwa sababu alitenda dhambi dhidi ya Yahwe.
Adui wa Daudi wanazungumza uovu gani dhidi yake?
Wanauliza atakufa lini na jina lake kupotea.
Adui wa Daudi anasema nini kwake?
Adui wake anasema vitu visivyofaa.
Psalms 41:7-9
Wale wanaomchukia Daudi wanong'onezana ni na kutamani nini?
Wale wanaomchukia Daudi wananong'onezana pamoja dhidi yake na kutamani apate madhara.
Rafiki wa karibu wa Daudi ambaye alimwamini amefanya nini?
Rafiki yake wa karibu ameinua kisigino chake dhidi yake.
Psalms 41:10-12
Yahwe amefanya nini kwa ajili ya Daudi?
Yahwe alikuwa na huruma juu yake na kumwinua juu ili kwamba awalipe wale wanaomchukia.
Daudi anajuaje kuwa Yahwe amemfurahia?
Daudi anajua hili kwa sababu adui yake hajamshinda.
Yahwe anambebaje Daudi?
Yahwe anambeba katika uadilifu wake na atamtunza mbele ya uso wa Yahwe milele.
Psalms 41:13
Yahwe anaweza kusifiwa wakati gani?
Yahwe anaweza kusifiwa tangu milele hadi milele.
Psalms 42
Psalms 42:1-2
Nafsi ya mwandishi inatweta vikoje kwa ajili ya Mungu?
Nafsi yake inatweta kwa ajili ya Mungu kama mbawala anavyotweta baada ya mikondo ya maji.
Mwandishi anasema nini kuhusu nafsi yake?
Nafsi yake ina kiu kwa ajili ya Mungu, kwa ajili ya Mungu aliye hai.
Psalms 42:3-4
Machozi ya mwandishi yamekuwa nini kwake?
Machozi yake yamekuwa chakula chake mchana na usiku.
Mwandishi anakumbuka vitu gani?
Anakumbuka jinsi alivyokwenda na umati na kuwaongoza kwenye nyumba ya Mugnu kwa sauti ya furaha na ya kusifu.
Psalms 42:5-6
Mwandishi anaiambia nafsi yake kufanya nini?
Anaiambia nafsi yake kutumaini katika Mungu, kwa kuwa atamsifu Mungu kwa msaada wa uwepo wa Mungu.
Psalms 42:7-8
Nini kimeenda juu ya mwandishi?
Mawimbi madogo na makubwa yote yameenda juu ya mwandishi.
Yahew ataamuru nini mchana?
Yahwe ataamuru uaminifu wake wa agano wakati wa mchana.
Nini kitatokea usiku?
Usiku wimbo wa Mungu utakuwa na mwandishi, ombi kwa Mungu wa maisha yake.
Psalms 42:9-10
Mwandishi atamuuliza nini Mungu, mwamba wake?
Atauliza kwa nini Mungu amemsahau, na kwa nini anapaswa kuomboleza kwa sababu ya adui.
Mwandishi analinganisha nini lawama za adui zake?
Anasema ni kama vidonda vinavyovunjavunja mifupa yake.
Psalms 42:11
Mwandishi atatarajia Mungu afanye nini?
Atatarajia Mungu ambariki.
Psalms 43
Psalms 43:1-2
Mwandishi anamwomba Mungu amfanyie nini?
Anamwomba Mungu kumhukumu na kutetea haja yake dhidi ya taifa lisilo la utauwa.
Kwa nini Mungu amhukumu na kutetea haja yake?
Mungu anapaswa kumhukumu kwa sababu yeye ndiye Mungu wa nguvu yake.
Psalms 43:3-4
Mwandishi anamwomba Mungu kuacha nuru yake na ukweli ufanye nini?
Anamwomba Mungu kuacha nuru yake na ukweli kumwongoza na kumleta katika kilima kitakatifu cha Mungu na hema lake takatifu.
Mwandishi ataenda wapi Mungu atakapomleta katika hema lake takatifu?
Ataenda katika madhabahu ya Mungu.
Mwandishi atafanya nini kwenye kinubi chake?
Atamsifu Mungu kwenye kinubi chake.
Psalms 43:5
Kwa nini nafsi ya mwandishi haipaswi kukata tamaa wala kunyamaza ndani yake?
Nafsi yake inapaswa kumtumaini Mungu kwa kuwa atamsifu Mungu, ambaye ni msaada wake na Mungu wake.
Psalms 44
Psalms 44:1-2
Waandishi wamesikia nini kwa masikio yao?
Wamesikia kazi ambayo Mungu alifanya katika siku zao, katika siku za kale.
Mungu alifanya nini kwa mkono wake?
Mungu aliyaondoa mataifa kwa mkono wake na kuwapanda watu wa Israeli.
Psalms 44:3-4
Waisraeli walipataje nchi na kujiokoa?
Hawakupata nchi kuwa mali yao kwa nguvu ya upanga wao au mkono wao wenyewe, bali kwa mkono wa kuume wa Mungu kwa sababu alikuwa na fadhila kwao.
Psalms 44:5-6
Waisraeli watafanya nini kupitia kwa Mungu?
Watawasukuma chini adui zao na kwa kupitia jina la Mungu watawakanyaga chini.
Mwandishi hatatumaini nini?
Hatatumaini katika upinde wake, wala upanga wake hautamwokoa.
Psalms 44:7-8
Mungu amewaokoa na nini?
Mungu amewaokoa na adui zao na kuwaaibisha wale wanaowachukia.
Psalms 44:9-11
Mungu amefanya nini sasa?
Mungu amewatupa na kuwanyima heshima, na haendi na majeshi yao.
Mungu anawafanya Waisraeli kufanya nini?
Mungu anawafanya wageuka kutoka kwa adui zao.
Wale wanaowachukia Waisraeli wanafanya nini?
Wale wanaowachukia wanajichukulia mateka.
Mungu amewafanya Waisraeli kama nini?
Mungu amewafanya kama kondoo ambao hatima yao ni kuwa chakula na kuwatawanya miongoni mwa mataifa.
Psalms 44:12-14
Mungu anawafanya Waisraeli kuwa nini kwa jirani zao?
Mungu anawafanya kuwa lawama kwa jirani zao, dhihaki na kejeli kwa wale wanaomzunguka.
Psalms 44:15-17
Kwa nini fedheha ya mwandishi ikko mbele yake siku nzima?
Fedheha yake iko mbele yake, na aibu ya uso wake umemfunika kwa sababu ya sauti ya yule anayemlaumu na kumtukana, kwa sababu ya adui na mlipiza kisasi.
Waisraeli hawajafanya nini?
Hawajamsahau Mungu wala kutenda kwa udanganyifu na agano la Mungu.
Psalms 44:18-24
Mioyo ya Waisraeli na hatua zao hazijafanya nini?
Moyo wao haujageuka wala hatua kutoka katika njia ya Mungu.
Mungu amefanya nini hata hivyo?
Mungu amewavunja sana katika sehemu ya mbweha na kuwafunika na kivuli cha mauti.
Hakika Mungu atatafuta nini?
Mungu atawatafuta kama wamesahau jina la Mungu wao au kunyosha mikono yao kwa mungu mgeni.
Waisraeli wanachukuliwa kuwa nini kwa ajiliya Mungu?
Wanachukuliwa kuwa kondoo kwa ajili ya kuchinjwa.
Psalms 44:25-26
Nafsi za Waisraeli zimefanya nini?
Nafsi zao zimeyeyuka kwenye mavumbi na miili na kung'ang'ania dunia.
Mwandishi anaomba Mungu afanye nini?
Anaomba kwamba Mungu ainuke kwa ajili ya msaada wao na kuwakomboa kwa ajili ya uaminifu wa agano la Mungu.
Psalms 45
Psalms 45:1-2
Mwandishi atasoma nini kwa sauti?
Atasoma kwa sauti maneno aliyotunga kumhusu mfalme.
Mwandishi anamwelezeaje mfalme?
Mfalme ni mzuri kuliko watoto wa watu, neema imemwagwa katika midomo yake, na Mungu amembariki milele.
Psalms 45:3-4
Kwa nini mfalma anapaswa kuendesha kwa ushindi?
Mfalme anapaswa kuendesha kwa ushindi kwa sababu ya uaminifu , upole, na haki.
Psalms 45:5-7
Mishale ya mfalme inaelezwaje?
Mishale yake ina ukali na iko kwenye mioyo ya adui wa mfalme.
Kiti cha enzi cha Mungu na fimbo yake ya hukumu inafafanuliwaje?
Kiti chake cha enzi ni milele, na fimbo yake ya hukumu ni fimbo ya ufalme wa Mungu.
Mfalme amependa nini na kuchukia nini?
Amependa haki na kuchukia uovu.
Psalms 45:8-11
Mavazi yote ya mfalme yana harufu ya nini?
Mavazi yake yote yana harufu ya manemane, mishubiri, na mdalasini.
Mabinti wa mfalme na malikia wako wapi?
Mabinti wa mfalme wako miongoni mwa wanawake wa heshima na katika mkono wa kuume wa Mungu anasimama malikia akiwa amevikwa Ofiri.
Psalms 45:12-13
Matajiri watafanya nini?
Matajiri miongoni mwa watu wataomba fadhila.
Psalms 45:14-15
Binti wa kifalme ataongozwa wapi?
Ataongozwa kwa mfalme akiwa na nguo ya tarizi.
Mabikra waliongozwaje na wapi?
Wataongozwa kwa furaha na kwa kushangilia; wataiingia kwenye hekalu la mfalme.
Psalms 45:16-17
Nani atakuwa kwenye nafasi ya baba wa mfalme?
Katika nafasi ya baba zako watakuwa watoto wako, ambao utawafanya wakuu duniani kote.
NIni kitafanyika kwa jina la mfalme?
Litakuwa jina la kukumbukwa katika vizazi vyote.
Psalms 46
Psalms 46:1-3
Mwandishi anamwelezeaje Mungu?
Mungu ni kimbilio letu, msaada wa sasa katika shida.
Waisraeli hawatafanya nini, hata kama dunia itabadilika na milima itatikiswa kwenye moyo wa bahari?
Kwa hiyo, hawataogopa.
Psalms 46:4-5
Nini huufanya mji wa Mungu kuwa na furaha?
Kuna mto, mikondo ambayo hufurahisha mji.
Mji wa Mungu hautafanya nini?
Mji hautasogezwa.
Psalms 46:6-7
NIni kilitokea kwa dunia Mungu alipoinua sauti yake baada ya mataifa kukasirika na falme kutikiswa?
Dunia iliyeyuka.
Yahwe wa majeshi ni nani na yuko wapi Mungu wa Yakobo?
Yahwe wa majeshi yuko na Israeli, na Mungu wa Yakobo ni kimbilio lao.
Psalms 46:8-9
Yahwe hufanya nini vita?
Hufanya vita kukoma hadi mwisho wa dunia, na huvunja upinde, hukata mkuki vipande vipande, na kuchoma ngao.
Psalms 46:10-11
Mungu anawaambia watu kufanya nini?
Kuwa kimya na kujua kuwa yeye ni Mungu.
Nini kitatokea kwa Mungu katikati ya mataifa?
Atatukuzwa katikakati ya mataifa na duniani.
Mungu wa Yakobo ni nini kwa Israeli?
Yeye ni kimbilio lao.
Psalms 47
Psalms 47:1-2
Kwa nini kila mtu anapaswa kupiga makofi yao na kupiga kelele kwa Mungu kwa sauti ya ushindi?
Wanapaswa kupiga makofi na kupiga kelele kwa sababu Yahwe Aliye Juu Zaidi anatisha na Mfalme mkuu juu ya dunia nzima.
Psalms 47:3-5
Yahwe anafanya nini kwa watu na mataifa?
Huwashinda watu chini ya Waisraeli na mataifa chini ya miguu yao.
Mungu amekwendaje juu?
Mungu amekwenda juu kwa kelele na sauti ya tarumbeta.
Psalms 47:6-7
Kwa nini kila mtu anapaswa kuimba sifa kwa Mungu?
Wanapaswa kuimba sifa kwa sababu Mungu ni Mfalme juu ya dunia yote.
Psalms 47:8-9
Mungu anatawala wapi?
Mungu anatawala juu ya mataifa.
Mungu anakaa wapi?
Mungu anakaa juu ya kiti chake kitakatifu cha enzi.
Wakuu wa watu wamekusanyika pamoja wapi?
Wamekusanyika pamoja kwa watu wa Mungu wa Abrahamu.
Kwa nini wakuu wamekusanyika kwa watu wa Abrahamu?
Wamekusanyika kwa watu wa Abrahamu kwa sabbau anainuliwa sana.
Psalms 48
Psalms 48:1-3
Mwandishi anamwelezaje Yahwe?
Yahwe ni Mkuu na anasifiwa kwa ukuu.
Mlima Sayuni unaelezwaje?
Mlima Sayuni ni mzuri kwa kimo, furaha ya dunia nzima.
Mungu amejifanyaje kujulikana?
Mungu amejifanya kujulikana kama mkimbizi.
Psalms 48:4-6
Nini kilitokea wafalme walipokusanyika pamoja na kuona Mlima Sayuni?
Walishangazwa, kuvunjika moyo, na kuharakisha mbali; kutetemeka kukawashika kule.
Psalms 48:7-8
Mungu atafanya nini kwa ajili ya mji wa Yahwe wa Majeshi?
Mungu atauimarisha milele.
Psalms 48:9-10
Waisraeli waliwaza nini katikati ya hekalu la Mungu?
Walifikiri juu ya agano la Mungu la uaminifu.
Mwandishi anafafanuaje mkono wa kuume wa Mungu?
Mkono wake wa kuume umejaa haki.
Psalms 48:11
Kwa nini Mlima Sayuni unapaswa kufurahi na binti wa Yuda kushangilia?
Inatakiwa kufurahi na wanapaswa kushangilia kwa sababu ya amri za haki za Mungu.
Psalms 48:12-13
Kwa nini Waisraeli wanatakiwa kutembea kuzunguka Mlima Sayuni walihesabu minara yake, na kuangalia kasri zake?
Wanapaswa kufanya vitu hivi ili waweze kuisema kwa kizazi kinachofuata.
Psalms 48:14
Mungu atafanya nini kwa Waisraeli?
Atakuwa kiongozi wao mpaka kifo.
Psalms 49
Psalms 49:1-2
Mwandishi anamwambia nani kusikia na kutega sikio?
Anawaambia watu wote kutega sikio, na wakazi wote wa dunia, wote wa chini na juu, tajiri na maskini pamoja, kutega sikio.
Psalms 49:3-5
Mdomo wa mwandishi utazungumza nini?
Mdomo wake utazungumza hekima.
Taamuli ya moyo wa mwandishi itakuwa nini?
Taamuli ya moyo wake itakuwa ya kuelewa.
Mwandishi atainamisha sikio lake kwa kitu gani na ataanzaje?
Atainamisha sikio lake kwa mfano ambao ataanza kwa kinubi.
Psalms 49:6-8
Wale ambao wanatumaini katika utajiri wao hawatafanya nini?
Hakuna kati yao kwa njia yoyote ile anaweza kukomboa ndugu yake wala kumpa Mungu malipo kwa ajili yake.
Mwandishi anafafanua ukombozi wa maisha ya mtu kwa namna gani?
Ukombozi wa maisha ya mtu ni wa gharama na daima hugharimu sana.
Psalms 49:9-11
Nani ataishi milele?
Hakuna awezaye kuishi milele ili kwamba mwili wake usiweze kuoza.
Nini hutokea kwa wenye hekima, mpumbavu, na katili?
Wenye hekima wanakufa; mpumbavu na katili wote hutoweka na kuacha utajiri wao kwa wengine.
Psalms 49:12-13
Nini hutokea kwa binadamu?
Mtu, kuwa na utajiri, habaki hai.
Psalms 49:14-15
Nani atakuwa mchungaji wa binadamu?
Kifo kitakuwa mchungaji wake.
Nini kitatokea kwa binadamu asubuhi?
Mnyoofu atakuwa na nguvu juu yao asubuhi.
Mungu atafanya nini kwa mwandishi?
Mungu atawakomboa nafsi yake kutoka kwa nguvu ya kuzimu; atampokea.
Psalms 49:16-17
Mwandishi anasema kutoogopa kitu gani?
Watu wanapaswa kutoogopa pale mtu anapokuwa tajiri, pale uwezo wa nyumba yake inapokua.
Kwa nini mwandishi anasema kutoogopa?
Anasema kutoogopa kwa sababu ya tajiri anapokufa, hataondoka na chochote, na nguvu yake haitashuka pamoja naye.
Psalms 49:18-20
Wanamume wanasifu watu wengine wakati gani?
Wanamume husifu watu wengine ambao huishi kwa ajili yao wenyewe.
Matajiri watakwenda kwa nani?
Atakwenda kwa vizazi vya baba zake.
Matajiri na baba zake hawataona nini?
Hawataona mwanga tena.
Mtu ambaye ana utajiri lakini hana uelewa ni kama nini?
Yeye ni kama mnyama, ambaye hutoweka.
Psalms 50
Psalms 50:1-2
Asafu anatumia majina yapi matatu ya Mungu kumaanisha Mungu?
Anatumia majina "Mwenye Uwezo", "Mungu", na "Yahwe"
Psalms 50:3-6
Kwa nini Mungu anaita mbingu za juu na kwa dunia?
Anaita mbingu za juu na kwa dunia ili kwamba aweze kuhukumu watu wake.
Psalms 50:7-8
Mungu anawaambia nini watu wake ya kwamba hatalaumu?
Mungu anawaambia ya kwamba hatawashutumu kwa ajili ya sadaka zao.
Psalms 50:9-13
Kwa nini Mungu anasema hatachukua ng'ombe dume au mbuzi kutoka kwa watu wake?
Mungu anasema ya kuwa kila mnyama wa msitu ni wake, na ng'ombe juu ya vilima elfu moja.
Psalms 50:14-15
Asafu anasema kila mtu anapaswa kutoa nini na kumlipa Mungu?
Kila mtu anapaswa kutoa kwa Mungu sadaka ya shukrani na kulipa viapo vyao kwa Aliye Juu.
Psalms 50:16-20
Mungu anasema waovu wanachukia nini na kutupa mbali?
Mungu anasema ya kwamba waovu huchukia maelekezo na kutupa mbali maneno yake.
Psalms 50:21-22
Mungu anasema waovu wanafikiri nini juu yake wakati Mungu anapokuwa kimya?
Walifikiri ya kwamba alikuwa mtu kama wao.
Nani atawasaidia waovu Mungu anapowachana katika vipande?
Hapatakuwa na mtu kuja kuwasaidia.
Psalms 50:23
Mungu ataonyesha wokovu wake kwa nani?
Mungu ataonyesha wokovu wake kwa yeyote ambaye hutoa sadaka ya shukrani na kupanga njia yake katika njia sahihi.
Psalms 51
Psalms 51:1-2
Kwa nini Daudi anasema ya kwamba Mungu anatakiwa kuwa na huruma juu yake?
Anasema Mungu anatakiwa kuwa na huruma kwa sababu ya agano lake aminifu.
Psalms 51:3-4
Daudi amesema ametenda dhambi dhidi ya nani?
Anasema ametenda dhambi dhidi ya Mungu, na dhidi ya Mungu pekee.
Psalms 51:5-6
Daudi anasema dhambi yake ilianza lini?
Anasema alizaliwa katika udhalimu, na mara tu mama yake alipotunga mimba yake, alikuwa katika dhambi.
Psalms 51:7-9
Daudi anamuuliza Mungu kufanya nini ili kwamba aweze kutakaswa?
Anamuuliza Mungu kumtakasa kwa hisopo ili aweze kuwa safi, na kumwosha ili aweze kuwa mweupe kuliko theluji.
Psalms 51:10-13
Daudi anamuuliza Mungu kuumba na kufanya upya ndani yake?
Anamuuliza Mungu kuumba ndani yake moyo safi, na kufanya upya roho sahihi ndani yake.
Daudi anamuuliza nini Mungu kutofanya kwake?
Anamuuliza Mungu kutomfukuza katika uwepo wake, na kutochukua Roho wake mtakatifu kutoka kwake.
Psalms 51:14-16
Daudi anamuuliza Mungu kumsamehe dhambi gani?
Anamuuliza Mungu kumsamehe kwa kumwaga damu.
Psalms 51:17-19
Sadaka za Mungu ni zipi?
Sadaka za Mungu ni roho iliyovunjika. Hataudharau moyo uliovunjika na kupondeka.
Psalms 52
Psalms 52:1-2
Nini hutoka kwa Mungu kila siku?
Agano la uaminifu la Mungu huja kila siku.
Psalms 52:3
Mwenye uwezo anapenda nini zaidi ya mazuri?
Anapenda uovu kuliko mazuri.
Psalms 52:4-5
Ni maneno gani mtu mwenye uwezo hupenda?
Anapenda maneno yote ambayo humeza wengine.
Mungu atafanya nini kwa mtu mwenye uwezo?
Mungu atamuangamiza milele
Psalms 52:6-7
Mtu aliamini katika nini?
Aliamini katika wingi wa utajiri wake.
Psalms 52:8-9
Daudi ataweka imani yake juu ya nini?
Ataamini katika agano aminifu la Mungu milele na milele.
Psalms 53
Psalms 53:1-3
Mpumbavu anasema nini moyoni mwake?
Anasema, "Hakuna Mungu".
Mungu anapotazama chini juu ya wana wa binadamu, je! anakuta yeyote ambaye huelewa na kumtafuta yeye?
Hapana, wote wamekuwa wachafu, na hakuna mtu anayefanya mema.
Psalms 53:4-5
Kwa nini watu ambao hawamwiti Mungu hawataaibishwa?
Wataaibishwa kwa Mungu amewakataa.
Psalms 53:6
Daudi alikuwa na matumaini ya kwamba wokovu wa Israeli utatoka wapi?
Alikuwa na matumaini wokovu wa Israeli utatoka kutoka Sayuni!
Psalms 54
Psalms 54:1-3
Daudi alimwomba Mungu amuokoea na nini?
Alimuuliza Mungu kumwokoa kwa jina la Mungu.
Ni nani ameinuka na kutafuta nafsi ya Daudi?
Wageni wameinuka dhidi yake, na wanamume wasio na huruma wametafuta nafsi yake.
Psalms 54:4-5
Ni nani hushikilia nafsi ya Daudi?
Bwana ndiye ambaye hushikilia nafsi yake.
Mungu atawalipa nini maadui wa Daudi?
Atawalipa maovu kwao.
Psalms 54:6-7
Kwa nini Daudi hutoa shukrani kwa jina la Yahwe?
Atatoa shukrani kwa jina kake kwa wema wake.
Daudi ametazamaje juu ya adui zake?
Jicho lake limetazama kwa ushindi juu ya adui zake.
Psalms 55
Psalms 55:1-3
Kwa nini Daudi hana pumziko katika shida zake?
Hana pumziko kwa sababu ya sauti ya adui zake, na kwa sababu ya mateso ya waovu.
Psalms 55:4-5
Aina gani ya hofu imeanguka juu ya Daudi?
Hofu za kifo imeanguka juu yake.
Psalms 55:6-7
Daudi alisema atafanya nini kama angekuwa na mabawa kama njiwa?
Kama angekuwa na mabawa kama njiwa, angepaa na kuwa mapumzikoni.
Psalms 55:8-9
Daudi anamwomba Bwana kufanya nini kwa adui zake?
Anamuuliza Bwana kuwaangamiza, na kuchanganya lugha zao.
Psalms 55:10-11
Nini kinapatikana katikati mwa mji?
Udhalimu, vurugu na uovu zipo katikati ya mji.
Psalms 55:12-14
Nani alimkaripia Daudi na kujiinua juu dhidi yake?
Mwenzake Daudi na rafiki wa karibu alimkaripia Daudi na kujiinua juu dhidi yake.
Psalms 55:15
Daudi anataka nini kuja ghafla juu ya adui zake?
Anataka kifo kuja ghafla juu yao, na kwao kwenda chini wakiwa hai kuzimu.
Psalms 55:16-18
Daudi anafanya nini jioni, asubuhi na mchana?
Analalamika na kunung'unika kwa Mungu.
Psalms 55:19
Kwa nini Mungu atasikia na kujibu adui za Daudi?
Atasikia na kujibu kwa sababu hawabadiliki, na hawamuogopi Mungu.
Psalms 55:20-21
Rafiki wa Daudi alifanya kwa agano alilolifanya?
Hajaheshimu agano ambalo alilifanya.
Psalms 55:22-23
Mungu atawaleta chini waovu sehemu gani?
Atawaleta chini waovu katika shimo la uharibifu.
Psalms 56
Psalms 56:1-2
Kwa nini Daudi anamuuliza Mungu kuwa na huruma kwake?
Anamuuliza Mungu kuwa na huruma kwa sababu mtu hutamani kummeza yeye.
Maadui wa Daudi wanatamani kummeza wakati gani?
Maadui wa Daudi wanatamani kummeza siku nzima.
Psalms 56:3-4
Daudi anaapa kufanya nini anapoogopa?
Daudi anapokuwa na hofu, ataweka tumaini lake kwa Mungu.
Nini matokeo ya tumaini la Daudi kwa Mungu?
Daudi aliweka tumaini lake kwa Mungu ili kwamba asiogope.
Psalms 56:5-6
Maadui wa Daudi wanafanya nini maneno ya Daudi?
Wanageuza maneno ya Daudi.
Maadui wa Daudi wanawaza nini juu ya Daudi?
Mawazo yao yote yapo kinyume na Daudi kwa ajili ya uovu.
Psalms 56:7-8
Daudi anamuulizaje Mungu kuweka chini adui za Daudi?
Daudi anamuuliza Mungu kuwaleta chini katika hasira ya Mungu.
Daudi anamuuliza Mungu kufanya nini na machozi yake?
Daudi anamuuliza Mungu kuyaweka machozi ya Daudi katika chupa ya Mungu.
Psalms 56:9-11
Maadui wa Daudi watageuka wakati gani?
Maadui wa Daudi watageuka katika siku ambayo atamwita Mungu.
Psalms 56:12-13
Daudi anaapa kumpa nini Mungu?
Daudi anaapa ya kwamba atatoa sadaka ya shukrani kwa Mungu.
Daudi anatembea wapi mbele za Mungu?
Daudi anatembea mbele za Mungu katika mwanga wa walio hai.
Psalms 57
Psalms 57:1
Kwa nini Daudi anamwomba Mungu awe na huruma kwake?
Anamuuliza Mungu kuwa na hururma kwake, kwa maana nafsi yake hujificha ndani ya Mungu.
Daudi anafanya kimbilio kwa Mungu kwa muda gani?
Daudi hukimbilia kwa Mungu hadi shida hizi zitakapokamilika.
Psalms 57:2-3
Daudi anasema Mungu anafanya nini kwake?
Daudi anasema Mungu hufanya vitu hivi vyote kwake.
Daudi anasema Mungu atatuma nini kwake?
Daudi anasema ya kuwa Mungu atatuma kwake agano aminifu la Mungu na uaminifu wake.
Psalms 57:4-5
Daudi analala katikati ya kina nani?
Analala kati ya wale ambao wamewashwa moto.
Daudi anamwomba Mungu aruhusu utukufu wake uweje?
Daudi anamuuliza Mungu kuruhusu utukufu wa Mungu kuwa juu ya dunia yote.
Psalms 57:6
Nini kilitokea kwa wale waliochimba shimo mbele ya Daudi?
Wao wenyewe wameanguka katikati yake.
Psalms 57:7-8
Vyombo gani vya muziki Daudi anaviita kuamka?
Daudi anaviita kinanda na kinubi kumwamsha.
Psalms 57:9-11
Daudi atampa Bwana shukrani wapi?
Daudi atampa Bwana shukrani miongoni mwa watu.
Daudi ataimba sifa kwa Bwana wapi?
Daudi ataimba sifa kwa Bwana miongoni mwa mataifa.
Daudi anaomba utukufu wa Mungu utukuzwe wapi?
Daudi anaomba utukufu wa Mungu kutukuzwa duniani kote.
Psalms 58
Psalms 58:1-2
Daudi anasema wana wa watu wanasambaza nchini?
Wanasambaza vurugu nchini kwa mikono yao.
Psalms 58:3-5
Daudi anasema waovu wanapotoka wakati gani?
Wanapotoka mara tu wanapozaliwa.
Psalms 58:6-8
Daudi anamwomba Mungu kufanya nini waovu wanapopiga mishale?
Daudi anamwomba Mungu kufanya mishale iwe kana kwamba haina ncha.
Psalms 58:9-11
Wenye haki watashangilia lini?
Wenye haki watashangilia watakapoona kisasi cha Mungu.
Psalms 59
Psalms 59:1-2
Daudi anamwombaje Mungu kumwokoa kutoka kwa adui zake?
Anmwomba Mungu kumweka juu mbali na wale wanaoinuka dhidi yake.
Psalms 59:3-4
Kina nani wanajikusanya pamoja dhidi ya Daudi?
Watenda maovu wenye uwezo wanakusanyika pamoja dhidi ya Daudi.
Psalms 59:5-9
Daudi anamwomba Yahwe asiwe na huruma na nani?
Anamwomba Yahwe asiwe na huruma kwa mtu yeyote mtenda maovu.
Psalms 59:10-11
Daudi anategemea kukutana na Mungu wake vikoje?
Mungu atakutana naye kwa uaminifu wake wa agano.
Psalms 59:12-15
Daudi anamwombaje Mungu kuwameza adui zake?
Anmwomba Mungu kuwameza katika gadhabu yake, na kuwameza ili wasiwepo tena.
Psalms 59:16-17
Daudi anaimbaje kuhusu nguvu ya Mungu?
Anasema Mungu amekuwa mnara wake wa juu na kimbilio lake katika siku ya dhiki yake.
Psalms 60
Psalms 60:1
Mungu amewafanyia nini Waisraeli?
Amewatupa, amewavunja, na amekasirishwa nao.
Psalms 60:2-3
Mungu amefanya nini kwa nchi?
Ameifanya nchi itetemeka na kuirarua.
Mungu amewaonesha nini watu wake na kuwafanya wanywe nini?
Amewaonesha vitu vikubwa na kuwafanya wanywe divai ya kupepesuka.
Psalms 60:4-5
Mungu amempa nani bendera?
Aliwapa bendera wale wanomheshimu.
Psalms 60:6-7
Mungu ataifanya nini Shekemu na bonde la Sukothi?
Ataigawanya Shekemu na sehemu kutoka katika bonde la Sukothi.
Psalms 60:8-9
Mungu atafanya nini kwa Edomu?
Atarusha kiatu chake Edomu.
Psalms 60:10-12
Mungu hakufanya nini kwa ajili ya jeshi?
Hakwenda vitani nao.
Waisraeli watawezaje kushinda?
Watashinda kwa msaada wa Mungu, kwa kuwa atawakanyaga adui.
Psalms 61
Psalms 61:1-3
Daudi anamwomba Mungu afanye nini kwa ajili yake?
Daudi anamwomba Mungu kusikia kilio chake, na kushughulikia ombi lake.
Mungu amekuwa kama nani kwa Daudi?
Mungu amekuwa kimbilia na mnara wenye nguvu kutoka kwa adui kwa ajili ya Daudi.
Psalms 61:4-5
Daudi ataishi wapi na kufanya kimbilio?
Daudi ataishi katika tabenakulo la Mungu milele na kufany kimbilio katika sehemu ya maficho chini ya mabawa ya Mungu.
Mungu alifanya nini kwa ajili ya Daudi aliposikia viapo vyake?
Mungu alimpatia urithi wa wale ambao wanaheshimu jina la Mungu.
Psalms 61:6-7
Mungu atafanya nini kwa ajili ya maisha ya mfalme?
Mungu atarefusha maisha ya mfalme ili kwamba miaka yake iwe kama vizazi vingi.
Psalms 61:8
Kwa nini Daudi ataimba sifa kwa jina la Mungu milele?
Daudi ataimba sifa kwa jina la Mungu milele ili kwamba aweze kutekeleza viapo vyake kila siku.
Psalms 62
Psalms 62:1-2
Kwa nini Daudi anasubiri kimya kwa ajili ya Mungu pekee?
Daudi anasubiri kimya kwa ajili ya Mungukwa sababu wokovu wake huja kutoka kwa Mungu.
Daudi anasema Mungu ni nani kwake?
Daudi anasema Mungu pekee ni mwamba wake na wokovu na mnara wake wa juu.
Psalms 62:3-6
Wanamtendeaje mtu katika nafasi yake ya juu?
Wanashauriana naye pekee kumleta chini, wanapenda kusema uongo, na wanambariki kwa midomo yao, lakini ndani ya mioyo yao wanamlaani.
Psalms 62:7-8
Daudi anawaambia watu wafanye nini?
Anawambia watu kumwamini Mungu wakati wote na kumwaga mioyo yao mbele za Mungu.
Psalms 62:9-10
Daudi anafafanuaje wanamume wa msimamo wa chini na juu?
Wanamume wa msimamo wa chini ni batili, na wanamume wa msimamo wa juu ni uongo, wakipimwa pamoja ni wepesi kuliko chochote.
Daudi anasema watu wasiweke mioyo yao juu nini?
Anasema hawatakiwi kuweka matumaini katika mateso au uporaji na kutotumaini bure katika utajiri, kwa sababu hawatazaa tunda.
Psalms 62:11-12
Daudi alisikia nini Mungu alipozungumza?
Daudi amesikia ya kwamba uwezo ni mali ya Mungu.
Agano la uaminifu ni mali ya nani?
Agano la uaminifu ni mali ya Bwana kwa sababu Bwana hulipiza kila mtu kwa kile alichofanya.
Psalms 63
Psalms 63:1-2
Daudi anamtafutaje Mungu?
Anamtafuta Mungu kwa dhati, nafsi yake ina kiu kwa ajili yake, na mwili wake una shauka kwa ajili ya Mungu.
Daudi anaona nini anapomtafuta Mungu katika mahali pake patakatifu?
Anaona uwezo na utukufu wa Mungu.
Psalms 63:3-4
Daudi atafanya nini kwa sababu ya uaminifu wa agano wa Mungu.
Midomo ya Daudi itamsifu Mungu, atambariki Mungu wakati anaishi, na atinua juu mikono yake katika jina la Mungu.
Psalms 63:5-6
Nini kinaridhisha nafsi ya Daudi na kumsababisha amsifu Mungu?
Anridhika na kusifu anapowaza juu ya Mungu kitandani kwake na kutafakari juu yake usiku.
Psalms 63:7-8
Daudi anashangilia wapi?
Anashangilia katika kivuli cha mabawa ya Mungu.
Nini kinamshikilia Daudi?
Mkono wa kuume wa Daudi unamshikilia.
Psalms 63:9-10
Nini kitatokea kwa wale wanaotafuta kuangamiza nafsi ya Daudi?
Watakwenda katika sehemu ya chini ya dunia, watakabidhiwa kwa nguvu ya upanga, na kupewa kwa mbweha.
Psalms 63:11
Nini kitatokea kwa wale wanaoapa kwa Mungu?
Wale wanaoapa kwake watajivunia Mungu.
Nini kitatokea kwa wale wanaozungumza uongo?
Wale wanaozungumza uongo watazuiliwa midomo yao.
Psalms 64
Psalms 64:1-2
Daudi anamwuliza Mungu kusikia nini?
Anamtaka Mungu kusikia sauti yake na kusikiliza lalamiko lake.
Daudi anamwuliza Mungu kumficha na nini?
Anamwuliza Mungu kumficha kutoka kwa mipango ya siri ya waovu na kutoka kwa ghasia ya watendaji wa udhalimu
Psalms 64:3-4
Maadui wa Daudi wamefanya nini kwa ndimi zao?
Wamenoa ndimi zao kama panga.
Maadui wa Daudi wanampiga nani?
Wanampiga mtu ambaye hana hatia.
Psalms 64:5-6
Maadui wa Daudi wanasema nini wanapojadiliana kwa siri pamoja kupanga uovu na kuandaa mitego?
Wanasema, "Ni nani atatuona?"
Psalms 64:7-9
Mungu ataikiaje kwa maadui wa Daudi?
Mungu atawapiga na ghafla watadhuriwa kwa mishale yake.
Nini kitatokea kwa adui kwa sababu ya matendo ya Mungu?
Adui atafanywa kujikwaa na wote watakaowaona watakunja mikia yao.
Watu wote wataitikiaje Mungu atakapohukumu maudui wa Daudi?
Watu wote wataogopa, kutamka matendo ya Mungu, na kufikiri kwa hekima juu ya kile Mungu amefanya.
Psalms 64:10
Wenye haki na wote wanyoofu mioyoni watafanya nini?
Wenye haki watafurahi juu ya Yahwe na watakimbilia ndani yake; wote wanyoofu wa mioyo watajivunia ndani yake.
Psalms 65
Psalms 65:1-3
Daudi anasema viapo vyao vitachukuliwa na nani?
Viapo vyao vitachukuliwa kwa Mungu Sayuni.
Daudi anasema Mungu atafanya nini kuhusu makosa yao?
Anasema Mungu atasamehe makosa yao.
Psalms 65:4
Daudi anasema mtu aliyebarikiwa ni yupi?
Amebarikiwa mtu ambaye Mungu amemchagua kumleta karibu na kuishi ndani ya mabaraza yake; atatosheka na wema wa nyumba ya Mungu.
Psalms 65:5
Mungu wa wokovu wao atajibuje maombi yao?
Mungu atajibu kwa haki kwa kufanya mambo ya ajabu.
Psalms 65:6-7
Mungu ananyamazisha nini?
Ananyamazisha ngurumo za bahari, ngurumo za mawimbi, na vurugu za watu.
Psalms 65:8-9
Ni nani anaogopa ushahidi wa matendo ya Mungu?
Wale ambao huishi katika sehemu za juu za dunia wanaogopa ushahidi wa matendo ya Mungu.
Daudi anasema Mungu anasaidiaje dunia?
Mungu humwagilia, kurutubisha, na kuandaa dunia kuwapa binadamu nafaka.
Psalms 65:10-12
Nini hutokea kwa dunia nyuma ya kibandawazi cha Mungu?
Alama za magurudumu nyuma ya kibandawazi hudondosha unene chini ardhini.
Psalms 65:13
Malisho yamevishwa na nini, na mabonde yamefunikwa na nini?
Malisho yamevishwa na makundi, na mabonde yamefunikwa na nafaka.
Psalms 66
Psalms 66:1-2
Mwandishi anawaambia dunia yote kufanya nini?
Huwaambia kila mtu kufanya kelele za furaha kwa Mungu, kuimba utukufu wa jina lake, na kufanya sifa yake kutukuka.
Psalms 66:3-4
Nini kitasababisha maadui wa Mungu kujiweka chini yake?
Ukubwa wa uwezo wa Mungu utasabisha maadui wake kujiweka chini yake.
Psalms 66:5-7
Tendo gani la muujiza Mungu alifanya kwa watoto wa watu?
Aligeuza bahari kuwa nchi kavu ili kwamba watu wapite katika mto kwa mguu.
Psalms 66:8-9
Mungu anafanya nini kwa watu wake katika maisha?
Hutunza nafsi zao na haruhusu miguu yao kusogezwa.
Psalms 66:10-12
Mungu amewajaribuje watu wake na amewaleta wapi?
Mungu aliwajaribu kama fedha inapojaribiwa.
Mungu aliwaleta watu wapi?
Aliwaleta nje katika mahali penye nafasi kubwa.
Psalms 66:13-15
Mwandishi atakuja katika nyumba ya Mungu na nini?
Atakuja katika nyumba ya Mungu na sadaka za kuteketeza.
Mwandishi atatoa nini kwa Mungu?
Atatoa sadaka za kuteketeza ya wanyama wanene, harufu nzuri ya kondoo, na ng'ombe dume na mbuzi.
Psalms 66:16-18
Mwandishi atatamka nini kwa wote ambao humwogopa Mungu?
Atatamka kile Mungu alichofanya kwa ajili ya nafsi yake.
Bwana atafanya nini kama mwandishi atautazama udhalimu moyoni mwake?
Bwana hatamsikia kama mwandishi atazama udhalimu wake wa moyoni.
Psalms 66:19-20
Mungu hajageuka kutoka kwa nini?
Hajageuka kutoka kwa maombi ya mwandishi na kutoka kwa agano lake la uaminifu.
Psalms 67
Psalms 67:1-2
Ni kwa nini Mungu anapaswa kuwa na hururma kwa watu wake na kuwabariki?
Anatakiwa kuwabariki ili kwamba njia zake ziweze kujulikana juu ya dunia, na wokovu wake katika mataifa yote.
Psalms 67:3-4
Nani anapaswa kumsifu Mungu?
Watu wote wanapaswa kumsifu Mungu.
Kwa nini mataifa yanapaswa kuwa na furaha na kuimba?
Mataifa yanapaswa kuwa na furaha na kuimba kwa sababu Mungu atawahukumu watu kwa haki na kuwaongoza mataifa juu ya dunia.
Psalms 67:5-6
Kwa nini dunia imezaa mavuno yake?
Dunia imezaa mavuno yake kwa sababu Mungu aliwabariki watu.
Psalms 67:7
Nini kinatakiwa kutokea kwa sababu Mungu amebariki watu?
Mwisho wote wa dunia wanapaswa kumheshimu yeye.
Psalms 68
Psalms 68:1-3
Daudi anataka nini kitokee kwa adui wa Mungu na kwa wale wanaomchukia Mungu?
Anataka adui wa Mungu kutawanywa, na wale wanaomchukia Mungu kukimbia mbele yake.
Wenye haki wanapaswa kufanya nini?
Wenye haki wanapaswa kushangilia, kuimba na kufurahi mbele ya Yahwe.
Psalms 68:4-6
Mungu anafanya nini kwa ajili ya wapweke na wafungwa?
Anawaweka wapweke katika familia, na huwatoa nje wafungwa kwa kuimba.
Psalms 68:7-8
Dunia na mbingu zilifanya nini Mungu alipotoka nje mbele ya watu wake?
Dunia ilitetemeka na mbingu zikashusha mvua katika uwepo wa Mungu.
Psalms 68:9-10
Mungu aliwatumia nini watu wake?
Mungu alituma mvua ya kutosha kuimarisha urithi wake ulipokuwa umechoka.
Psalms 68:11-13
Jeshi kubwa lilitanganza nini?
Jeshi lilitangaza maagizo ya Bwana.
Wanawake wanaosubiri nyumbani wanafanya nini baada ya wafalme wa majeshi kutoroka?
Wanagawanya mapato ya fedha na njiwa wa dhahabu.
Psalms 68:14-16
Kilima cha nchi kinatazama nini kwa kutamani?
Kilima cha nchi kinatazama kwa kutamani mlima ambao Mungu anatamani aishi milele.
Psalms 68:17-18
Kuna vibandawazi vingapi vya Mungu?
Vibandawazi vya Mungu elfu ishirini, maelfu juu ya maelfu.
Psalms 68:19-21
Bwana huwafanyia nini watu wake kila siku?
Bwana hubeba mizigo yao kila siku.
Psalms 68:22-23
Bwana atawarudisha watu wake kutoka wapi?
Bwana atawarudisha watu wake kutoka Bashani na kutoka kwenye vilindi vya bahari.
Psalms 68:24-25
Maandamano ya Mungu yalifuata mpangilio gani kwenda mahali patakatifu?
Waimbaji walikwenda kwanza, wapiga vinanda wakafuata, na katikati walikuwepo wasichana ambao hawajaolewa wakicheza ngoma ndogo.
Psalms 68:26-27
Nani anapaswa kumbariki na kumsifu Mungu katika kusanyiko?
Uzao wa kweli wa Israeli unapaswa kumbariki na kumsifu Mungu.
Nani kabila dogo zaidi?
Benyamini ndio kabila dogo zaidi.
Psalms 68:28-29
Daudi anamwomba Mungu kufunua nini kwa watu wake?
Anamwomba Mungu kufunua kwao nguvu ya Mungu kama nyakati za zamani.
Psalms 68:30-31
Daudi anasema nini kikemewe?
Daudi anasema kukemea nyati wa kwenye matete na mafahali na ndama wa watu.
Nani atatoka Misri?
Wakuu watatoka kutoka Misri.
Psalms 68:32-33
Nani anapaswa kuimba kwa Mungu?
Falme za dunia zinapaswa kuimba sifa kwa Yahwe.
Psalms 68:34-35
Daudi anasema nguvu ya Mungu inapaswa kutambuliwa kuwa ya nani?
Daudi anasema kutambua sababu ya nguvu kuwa Mungu.
Mungu anawapa nini watu wake?
Anawapa nguvu na uwezo watu wake.
Psalms 69
Psalms 69:1-2
Daudi anamwomba Mungu kumwokoa na nini?
Anamwomba Mungu kumwokoa na vilindi vya maji vilivyokuja kwenye nafsi yake.
Psalms 69:3-4
Nini kinatokea kwa Daudi anapomsubiri Mungu wake?
Amechoka kulia, koo lake limekauka, na macho yake yamechoka.
Audi wanaomchukia Daudi ni wangapi?
Adui zake ni zaidi ya nywele za kichwani kwake.
Psalms 69:5-6
Mungu anajua nini kumhusu Daudi?
Mungu anajua kuhusu upumbavu wa Daudi na dhambi zake hazijafichwa kwa Mungu.
Daudi hataki nini kitokee kwa wale wanaomsubiri na kumtafuta Mungu?
Daudi anaomba kwamba wasiaibishwe au kukosa heshima kwa sababu ya Daudi.
Psalms 69:7-9
Nini kimemla Daudi?
Ari kwa ajili ya Mungu imemla.
Psalms 69:10-12
Daudi alifanya nini kujikemea?
Alilia na kuadhibu nafsi yake kwa kufunga.
Ni lini Daudi alikuwa chombo cha mithali?
Alitengeneza magunia kwa nguo zake.
Psalms 69:13-15
Daudi anataka Yahwe amjibuje ombi lake?
Anamwomba Yahwe kumjibu katika uaminifu wa wokovu wa Yahwe.
Psalms 69:16-17
Kwa nini Yahwe anapaswa kumgeukia Daudi?
Anapaswa kumgeukia Daudi kwa sababu ya huruma za Yahwe kwa ajili ya Daudi ni nyingi.
Psalms 69:18-19
Daudi anataka Yahwe afanye nini kwa sababu ya adui zake?
Anamtaka YAhwe asogee karibu na nafsi yake na kuikomboa.
Psalms 69:20-21
Adui wa Daudi walimpa nini kula na kunywa?
Walimpa sumu kwa ajili ya chakula na siki kunywa.
Psalms 69:22-23
Daudi anataka meza ya adui zake kuwa nini?
Anataka meza ya adui zake iwe kitanzi na mtego kwa ajili yao.
Psalms 69:24-25
Daudi anataka nini kitokee katika sehemu ya adui zake?
Anataka sehemu yao iwe ya ukiwa, na mtu asiishi katika hema zao.
Psalms 69:26-29
Daudi anataka Yahwe awashtaki nini adui zake?
Anamtaka Yahwe kuwashtaki kwa kutenda uadhalimu baada ya udhalimu.
Psalms 69:30-31
Nini kitampendeza Mungu zaidi ya ngombe na fahali?
Sifa za Daudi kwa jina lake na wimbo na shukrani zake zitampendeza Yahwe.
Psalms 69:32-33
Yahwe anaitikiaje wahitaji na wafungwa wake?
Yahwe huwasikia wahitaji na hawachuki wafungwa wake.
Psalms 69:34-36
Daudi anasema nini kinapaswa kumsifu Mungu?
Mbingu, dunia, bahari, na kila kitu kinachosogea kinapaswa kumsifu Mungu.
Mungu ataifanya nini Sayuni na miji ya Yuda?
Mungu ataiokoa Sayuni na kuijenga tena miji ya Yuda, na watu wataishi huko na kuwa nayo kama mali yao.
Psalms 70
Psalms 70:1-3
Daudi anamwomba Mungu kufanya nini?
Daudi anamwomba Mungu kumwokoa na kuja upesi kumsaidia.
Daudi anamtaka Mungu kufanya nini kwa wanaotafuta nafsi yake?
Daudi anamtaka Mungu kuwaaibisha na kuwafadhaisha, kuwageuza na kuwanyima heshima.
Psalms 70:4-5
Daudi anataka wote wanaomtafuta Yahwe kufanya nini?
Anataka washangilie na kuwa na furaha na kusema, "Mungu asifiwe."
Daudi anahitaji nini kutoka kwa Mungu kwa sababu ni masikini na mhitaji?
Daudi anamhitaji Mungu aharakishe na kumwokoa.
Psalms 71
Psalms 71:1-3
Mwandishi anamwambia Yahwe kuwa anamtaka afanye nini?
Mwandishi anamtaka amkomboe, amfanye salama, ageuze sikio lake kwake na amwokoe.
Mwandishi anamtaka Yahwe awe nini kwake?
Mwandishi anamtaka Yahwe awe mwamba wake na ngome yake.
Psalms 71:4-5
Mwandishi anataka kukombolewa kutoka katika mkono wa nani?
Anataka akombolewe kutoka katika mkono wa mwovu, na kutoka kwa mtu asiye mwenye haki na mkatili.
Mwandishi amemtumaini Yahwe kwa muda gani?
Alimtumaini Yahwe tangu utoto wake.
Psalms 71:6-7
Mwandishi amekuwa nini kwa ajili ya watu wengi?
Amekuwa mfano kwa ajili ya watu wengi.
Psalms 71:8-9
Mwandishi anafanya nini na mdomo wake ziku nzima?
Anajaza mdomo wake na sifa na heshima siku nzima.
Mwandishi anamwomba Mungu asifanye nini wakati mwandishi atapozeeka na nguvu yake kuisha?
Anamwomba Yahwe kutomtupa au kumwacha.
Psalms 71:10-11
Adui wa mwandisih wanasema wanapanga njama ipi dhidi yake?
Wanasema, "Mungu amemwacha; mfutilieni na mmchukue, kwa kuwa hakuna mtu wa kumwokoa."
Psalms 71:12-13
Mwandishi anataka nini kitokee kwa wale walio na uhasama na maisha yake?
Anataka waaibishwe na kumezwa, na kufunikwa kwa lawama na kukosa heshima.
Psalms 71:14-16
Mwandishi atatangaza nini kwa mdomo wake kumhusu Yahwe?
Mdomo wake utaelezea haki ya Yahwe na wokovu wake.
Psalms 71:17-18
Kwa nini Yahwe hapaswi kumwacha mwandishi?
Yahwe hapaswi kumwacha kwa sababu mwandishi anatangaza nguvu ya Yahwe kwa kizazi kijacho, na uwezo wake kwa kila mtu atakayekuja.
Psalms 71:19-20
Mwandishi anasema nini kiko juu sana?
Haki ya Mungu iko juu sana.
Psalms 71:21-22
Mwandishi anatoa shukrani kwa ajili gani na kinubi?
Anatoa shukrani kwa Mungu kwa ajili ya uaminifu wa Mungu.
Psalms 71:23-24
Ulimi wa mwandishi unafanya nini siku nzima?
Unazungumza kuhusu haki ya Mungu siku nzima.
Psalms 72
Psalms 72:1-3
Sulemani anamwomba Mungu ampe nini mfalme na mwanaye?
Sulemani anamwomba Mungu kumpa mfalme amri zake za haki, na kumpa mwana wake haki za Mungu.
Psalms 72:4-5
Sulemani anataka watu wampe heshima Mungu kwa muda gani?
Anataka watu wampe heshima Mungu wakati jua lipo na mwezi unavyokuwa katika vizazi vyote.
Psalms 72:6-7
Sulemani anataka siku za mfalme ziweje?
Anataka ziwe kama mvua kwenye nyasi zilizofyekwa, na mvua zinazomwagilia dunia.
Psalms 72:8-10
Utawala wa mfalme utafika hadi wapi?
Utawala wake utafika kutoka bahari hadi bahari, kutoka mto hadi mwisho wa dunia.
Psalms 72:11-12
Wafalme wote na mataifa watafanya nini mbele ya mfalme?
Wafalme wote wataanguka chini mbele yake na kumtumikia.
Psalms 72:13-14
Mfalme anawatendaje masikini na wahitaji?
Anawahurumia masikini na wahitaji, na huziokoa nafsi za wahitaji.
Psalms 72:15-16
Ni nini ishara za baraka za Mungu kwa mfalme?
Ishara za baraka ni wingi wa nafaka, na watu katika miji watafanikiwa.
Psalms 72:17
Sulemani anaomba jina la mfalme lidumu hadi lini?
Anaomba jina la mfalme lidumu milele, na liendelee kama jua.
Psalms 72:18-20
Yahwe pekee anafanya nini?
Yeye pekee anafanya mambo ya ajabu.
Psalms 73
Psalms 73:1-3
Mungu ni mwema kwa nani?
Mungu ni mwema kwa Israeli, kwa wale wenye mioyo safi.
Kwa nini miguu ya Asafu kidogo iteleze.
Kidogo ateleze kwa sababu aliwaonea wivu wenye kiburi alipoona mafanikio ya waovu.
Psalms 73:4-5
Asafu aliwaelezeaje wenye kiburi na waovu?
Alisema hawana maumivu, wako na nguvu na wamekula vizuri, wako huru na mizigo, na hawateseki kama watu wengine.
Psalms 73:6-7
Kiburi na vurugu ni kama nini kwa waovu?
Kiburi na kama mkufu kwenye shingo zao, na vurugu inawavika kama joho.
Ni nini matokeo ya upofu wa waovu?
Kutoka katika upofu huja dhambi na mawazo maovu.
Psalms 73:8-9
Waovu wanasema vitu gani?
Wanamkejeli, wanasema vitu viovu, wanatishia vurugu, na kuongea dhidi ya mbinguni.
Psalms 73:10-12
Waovu wanasema nini kumhusu Mungu?
Wanasema, "Mungu anajuaje? Je! Mungu anajua kinachoendelea?"
Psalms 73:13-15
Kwa nini Asafu anahisi kuwa aliulinda moyo wake bure?
Asafu ameteswa kila siku na kuadhibiwa kila asubuhi.
Nini kitatokea kama Asafu akisema hivi vitu?
Atasaliti kizazi hiki cha watoto wa Mungu.
Psalms 73:16-17
Asafu alikwenda wapi kupata uelewa wa vitu hivi?
Asafu alikwenda mahali patakatifu pa Mungu.
Psalms 73:18-20
Waovu watakuwa nini punde?
Watakuwa nyika punde.
Psalms 73:21-22
Asafu alisema yeye ni kama nini mbele za Mungu?
Alikuwa kama mnyama mbele za Mungu.
Psalms 73:23-24
Mungu atafanya nini kwa ajili ya Asafu atakapomwongoza kwa ushauri wake?
Baadaye, Mungu atampokea Asafu katika utukufu wake.
Psalms 73:25-26
Ni nini hamu pekee ya Asafu duniani?
Mungu wa mbinguni ndiye pekee anayemtamani.
Psalms 73:27-28
Nani ataangamia?
Wale walio mbali na Mungu wataangamia, na atawaangamiza wote wasio waaminifu kwake.
Asafu anahitaji kufanya kitu gani?
Anahitaji kusogea karibu kwa Mungu.
Psalms 74
Psalms 74:1-2
Asafu anamwomba Mungu akumbuke nini alichowafanyia watu wake nyakati za kale?
Mungu aliwakomboa nyakati za kale, na kuwanunua kuwa urithi wake mwenyewe.
Psalms 74:3-6
Adui alifanya uharibifu gani mahali patakatifu?
Waliweka bendera za vita, wakakata kwa shoka, waliponda na kuvunja sanaa za utiaji nakshi
Psalms 74:7-8
Walifanya nini kingine mahali patakatifu?
Walipawasha moto, na kupatia najisi kwa kupabomoa chini.
Adui alifanyia nini sehemu za mikutano?
Walichoma sehemu zote za mikutano katika nchi.
Psalms 74:9-11
Watu wa Mungu hawakuona nini tena?
Hawakuona ishara za miujiza tena, hakuna nabii tena.
Psalms 74:12-13
Ni nini ishara kwamba Mungu alikuwa mfalme wa Asafu tangu nyakati za milele?
Mungu alitawanya bahari na kuponda vichwa vya wanyama wakubwa wa baharini.
Psalms 74:14-15
Mungu aliifanya nini lewiathani?
Aliponda vichwa vya lewiathani, na kuwalisha naye wale walio nyikani.
Psalms 74:16-17
Mungu aliweka nini sehemu yake?
Aliweka jua na mwezi shemu zake, na kuweka mipaka yote wa dunia.
Psalms 74:18-19
Adui anafanya nini ambacho anataka Yahwe akumbuke?
Adui alitupa matusi kwa Yahwe na kukufuru jina lake.
Psalms 74:20-21
Kwa nini Asafu anamwomba Mungu kukumbuka agano lake?
Anamtaka Yahwe akumbuke agano lake kwa sababu dunia imejaa vurugu.
Psalms 74:22-23
Asafu anamtaka Yahwe atetee nini?
Asafu anamtaka Mungu ainuke na kutetea heshima yake mwenyewe.
Psalms 75
Psalms 75:1-3
Watu wanatoa shukrani kwa sababu gani?
Wanatoa shukrani kwa sababu Mungu anaonesha uwepo wake.
Mungu atafanya nini katika wakati uliopangwa?
Atahukumu kwa haki na kuimarisha nguzo za dunia.
Psalms 75:4-6
Asafu anawaambia wasifanye nini wenye kiburi na waovu?
Anawaambia wasiwe na kiburi au kujiamini juu ya ushindi, na kutozungumza huku vichwa vyao vikiwa juu.
Psalms 75:7-8
Asafu anasema nini kumhusu Mungu?
Mungu ni mwamuzi na humleta mmoja chini na kumwinua mwingine.
Waovu watafanya nini na kikombe cha divai ya povu katika mkono wa Yahwe?
Watainywa hadi tone la mwisho.
Psalms 75:9-10
Asafu atamsifuje Mungu wa Yakobo?
Ataendelea kusema kile ambacho Mungu amefanya na kumwimbia sifa.
Mungu anasema atafanya nini kwa pembe za waovu na za wenye haki?
Atakata pembe za waovu na kuinua pembe za wenye haki.
Psalms 76
Psalms 76:1-3
Wapi mahali pa kuishi pa Mungu wa Yuda?
Sehemu yake ya kuishi iko Sayuni.
Psalms 76:4-5
Mungu anaonekanaje anaposhuka kutoka milimani?
Mungu anag'aa kwa nguvu na kuonesha utukufu wake.
Psalms 76:6-7
Nini kilitokea wakati Mungu wa Yakobo alipowakemea adui zake?
Farasi na mpanda farasi wote walikufa.
Psalms 76:8-9
Nini kilitokea hukumu ya Mungu ilipotoka mbinguni?
Hukumu yake ilipokuja, dunia iliogopa na kuwa kimya.
Psalms 76:10
Hukumu ya hasira ya Mungu kwa adui zake itamletea nini?
Hukumu yake ya hasira ya adui zake itamletea sifa.
Psalms 76:11-12
Watu wanapaswa kufanya nini kuhusu viapo wanavyofanya kwa Yahwe Mungu wao?
Wanapaswa kutunza viapo vyao.
Wakuu na wafalme wanaitikiaje kwa Yahwe?
Hunyenyekesha roho za wakuu, na anaogopwa na wafalme.
Psalms 77
Psalms 77:2-3
Asafu alifanya nini katika siku ya taabu yake?
Alimtafuta Bwana, akaomba usiku wote, na kunyosha mikono yake.
Psalms 77:4-5
Asafu aliwaza nini aliposhindwa kulala usiku?
Aliwaza kuhusu siku za kale, kuhusu nyakati za zamani.
Psalms 77:6-9
Asafu alikumbuka nini usiku?
Alikumbuka wimbo aliowahi kuimba.
Psalms 77:10
Huzuni ya Asafu ni nini?
Huzuni yake ni kubadilika kwa mkono wa kuume wa Mwenyezi kwake na watu wake.
Psalms 77:11-12
Asafu anawaza juu ya matendo gani ya Yahwe?
Anafikiria juu ya matendo ya ajabu ya Yahwe ya zamani.
Psalms 77:13-15
Mungu yukoje tofauti na miungu mingine yote?
Mungu ni wa ajabu, hufanya maajabu, huonesha nguvu yake, na huwapa watu wake ushindi.
Psalms 77:16-17
Ulimwengu uliitikiaje kwa Mungu?
Maji yaliogopa na kutetemeka. Mawingu yalimwaga maji na anga kupiga radi.
Psalms 77:18-20
Njia ya Mungu ilikwenda wapi?
Njia yake ilipita baharini, na njia yake katika maji yanayotiririka, lakini hatua zake hazikuonekana.
Psalms 78
Psalms 78:1-2
Asafu atawafundishaje watu wake?
Asafu atafungua mdomo wake kwa mafumbo na kuimba kuhusu vitu vilivyojificha kuhusu siku za zamani.
Psalms 78:3-4
Asafu atapitisha nini katika kizazi kijacho?
Asafu atakiambia kizazi kijacho kuhusu matendo yanayostahili sifa ya Yahwe, nguvu yake, na maajabu aliyotenda.
Psalms 78:5-6
Kwa nini Yahwe aliwaamuru mababu wa Asafu kuwafundisha watoto wao amri za Yahwe?
Yahwe aliamuru hivi ili kizazi kijacho kiweze kujua kuhusu amri zake ili watoto ambao bado hawajazaliwa waweze kuwaambia watoto wao pia.
Psalms 78:7-8
Kwa nini ilikuwa muhimu ka mababu wa Asafu kuawfundisha watoto wao amri za Yahwe?
Ilikuwa muhimu kwao kufundisha juu ya amri za Yahwe kwa watoto wao ili watoto wao wasiwe kama mababu zao waliokuwa wasumbufu na kizazi cha ukaidi.
Psalms 78:9-11
Israeli walifanyaje makosa machoni pa Mungu?
Hawakutunza agano na Mungu, na kukataa kutii sheria yake.
Psalms 78:12-16
Mungu aliwaongozaje Israeli?
Aliwaongoza mchana kwa wingu na usiku kwa nuru ya moto.
Psalms 78:17-18
Israeli walimjaribuje Mungu?
Walimjaribu Mungu kwa mioyo yao kwa kuomba chakula cha kuridhisha hamu zao.
Psalms 78:19-20
Israeli waliongea nini dhidi ya Mungu?
Walizungumza dhidi ya Mungu kwa kusema, "Mungu anaweza kweli kuweka meza kwa ajili yetu nyikani?"
Psalms 78:21-22
Kwa nini Yahwe alikasirika na kuwashambulia Israeli katika hasira yake?
Yahwe alikasirishwa na Israeli kwa sababu hawakumwamini na kutumaini katika wokovu wake.
Psalms 78:23-30
Mungu aliwahudumiaje Israeli ingawa hawakumwamini?
Mungu aliwahudumia kwa kuwanyeshea mana na nyama kwa wingi kwa ajili yao hadi wakashiba.
Psalms 78:31-32
Mungu aliwafanya nini Israeli katika hasira yake?
Aliwashambulia wenye nguvu zaidi na kuwaleta chini vijana.
Psalms 78:33-34
Watu wa Israeli waliitikiaje wakati Mungu alipowatesa?
Walianza kumtafuta, na wakamrudia na kumtafuta kwa dhati.
Psalms 78:35-37
Hali ya mioyo ya Isralei ilikuwaje mbele za Mungu?
Mioyo yao haikuwa imewekwa thabiti kwa Mungu, na hawakuwa waaminifu kwa agano lake.
Psalms 78:38-43
Mungu alioneshaje huruma kwa watu wa Israeli?
Alisamehe udhalimu wao na hakuwaangamiza kwa sababu alikumbuka kuwa wameumbwa kwa nyama.
Psalms 78:44-49
Mungu alifanya nini mito ya Wamisri?
Aligeuza mito ya Wamisri kuwa damu, ili washindwe kunya kutoka katika mikondo yao.
Psalms 78:50-51
Mungu aliwafanya nini wazaliwa wa kwanza wa Misri?
Aliwaua wazaliwa wote wa kwanza wa Misri, wazaliwa wa kwanza wa nguvu yao.
Psalms 78:52-53
Mungu aliwaongozaje watu wake mwenyewe?
Aliwaongoza kama kondoo, na kuwaongoza nyikani kama kundi.
Psalms 78:54-55
Mungu aliwafanya nini mataifa?
Aliyaondoa mataifa mbele ya Waisraeli na kuwapa urithi Israeli.
Psalms 78:56-57
Watu wa Israeli walitendaje kama baba zao?
Hawakuwa waaminifu na walitenda kwa udanganyifu kama baba zao.
Psalms 78:58-61
Israeli walimkasirisha Mungu kwa kutumia nini?
Walimkasirisha kwa madhabahu yao ya kipagani na kumchokoza awe na wivu wa hasira na sanamu zao.
Psalms 78:62-66
Mungu aliwakabidhi watu wake kwa kitu gani?
Aliwakabidhi kwa upanga, na moto uliwameza vijana wao.
Psalms 78:67-69
Mungu alichagua kabila kutoka Israeli?
Mungu alichagua kabila la Yuda na mlima Sayuni alioupenda.
Psalms 78:70-72
Mungu alimchagua nani kuwa mchungaji juu ya Israeli?
Alimchagua Daudi, mtumishi wake, na kumchukua kutoka katika zizi la kondoo.
Psalms 79
Psalms 79:1-3
Nini kilitokea mataifa mageni yalipokuja Israeli?
Watia najisi hekalu, waligeuza Yerusalemu kuwa rundo la uharibifu.
Psalms 79:4-5
Israeli imekuwa nini kwa jirani zake?
Wamekuwa chukizo kwa jirani zao, na dhihaka kwa wale waliowazunguka.
Psalms 79:6-7
Asafu anamwomba Mungu kumwaga gadhabu yake juu ya nani?
Anamwomba Mungu kumwaga gadhabu yake juu ya mataifa ambayo hayamjui Mungu na juu ya falme ambazo haziliiti jina la Mungu.
Psalms 79:8-9
Asafu hataki Mungu asikumbuke ni dhidi ya Israeli?
Anataka Mungu asikumbuke dhambi za baba zao dhidi yao.
Psalms 79:10-11
Asafu hataki mataifa yaseme nini?
Hataki mataifa yaseme, "Yuko wapi Mungu wao?"
Psalms 79:12-13
Asafu anasema Israeli ni nini kwa Mungu?
Anasema wao ni watu wa Mungu na kondoo wa malisho yake.
Psalms 80
Psalms 80:1-3
Mwandishi anamwomba mchungaji wa Israeli kufanya nini?
Mwandishi anamwomba kuvutia nadhari na kung'aa juu yao.
Mwandishi anamwomba mchungaji wa Israeli kufanya nini machoni pa Efraimu na Benyamini na Manase?
Anamwomba mchungaji wa Israeli kutikisika uwezo wake na kuja kuwaokoa.
Mwandishi anmwomba Mungu kufanya nini?
Anamwomba Mungu kuwarejesha, kuung'arisha uso wake kwao na wataokolewa.
Psalms 80:4-6
Mwitikio wa Yahwe ni upi watu wake wanapoomba?
Alikuwa na hasira na watu wake walipoomba.
Yahwe amewapa wale nini na kula?
Amewalisha machozi na kuwapa machozi kunywa.
Jirani wa israeli na adui zao wanawafanya nini?
Jirani zao wanabishana juu yao na adui zao wanawacheka.
Psalms 80:7-8
Nini kitatokea Mungu wa majeshi atakapowarejesha na kung'aarisha uso wake kwao?
Wataokolewa.
Mungu wa majeshi ataufanya nini mzabibu alioutoa kutoka Misri?
Aliwaondoa mataifa na kuupanda tena.
Psalms 80:9-11
Mungu alifanya nini kwa ajili ya kuandaa kupanda mzabibu?
Mungu alisafisha nchi kwa ajili yake.
Matawi ya mizabibu ilifunika nini?
Mzabibu ulifunika milima na seda za juu zaidi.
Mzabibu ulisambaza matawi yake na vichipukizi vyake umbali gani?
Mzabibu uliweka matawi yake mbali hadi baharini na kuweka vichipukizi vyake katika mto Frati.
Psalms 80:12-13
Nini kitatokea kwa kuwa kuta za mzabibu zimebomolewa?
Wote wanaopita watachuma matunda yake.
Ngiri na wanyama wataufanya nini mzabibu?
Ngiri watauharibu na wanyama kuula.
Psalms 80:14-16
Mwandishi anamwomba Mungu wa majeshi aufanye nini mzabibu?
Anamwomba Mungu wa majeshi kugeuka, kuutazama kutoka mbinguni, kutambua na kuujali mzabibu wake.
Nani aliupanda mzizi wa mzabibu na kuufanya mche uote?
Mkono wa kuume wa Mungu wa majeshi uliupanda mzizi na kuufanya mche kuota.
Nini kinatokea kwa mzabibu?
Mzabibu umechomwa na kukatwa chini.
Mwandishi anataka nini kitokee kwa adui wa Mungu wa majeshi?
Mwandishi anataka adui wa Mungu wa majeshi kuangamia kwa sababu ya kukemea kwake.
Psalms 80:17-18
Mwandishi anataka Mungu amfanye nini mtu aliye mkono wa kuume wa Mungu?
Mwandishi anataka mkono wa Mungu kuwa juu ya huyo mtu.
Mungu alifanya nini kwa ajili ya mwana wa binadamu?
Mungu alimwimarisha kwa ajili yake mwenyewe.
Watu watafanya nini kama Mungu akiwarudisha?
Wataliita jina la Mungu.
Psalms 80:19
Nini kitatokea kama Yahwe, Mungu wa majeshi, aking'aa juu ya watu wake?
Yahwe aking'aa juu yao, wataokoka.
Psalms 81
Psalms 81:1-3
Mwandishi anawaambia watu wote kufanya nini kwa Mungu?
Anawaambia kuimba kwa sauti na kupiga kelele kwa furaha.
Mwandishi anawaambia watu kucheza vyombo gani wanapoimba wimbo?
Watu wanapaswa kucheza tari na kinubi na kinanda.
Watu wanapaswa kupuliza pembe la kondoo dume wakati gani?
Wanapaswa kupuliza katika siku ya mwandamano wa mwezi, wakati siku kuu zao zinapoanza.
Psalms 81:4-5
Nani alitoa sheria na amri kwa ajili ya Israeli?
Mungu wa Yakobo alizitoa kwa ajili ya Israeli.
Kwa nini Mungu wa Yakobo alitoa sheria na amri kwa ajili ya Israeli?
Aliitoa kama kanuni katika Yusufu.
Psalms 81:6-7
Mungu aliondoa nini kwenye mabega ya watu?
Mungu aliondoa mzigo wao.
Nini kilitokea watu walipoita katika dhiki yao?
Mungu aliwasaidia, na akawajibu na kuwajaribu.
Psalms 81:8-10
Mungu alisema nini kuhusu miungu ya kigeni?
Mungu alisema hapatakiwi kuwa na miungu ya kigeni katikati ya Israeli na hawapaswi kuabudu mungu yeyote ya kigeni.
Yahwe anasemaamefanya nini kwa ajili ya Israeli?
Aliwatoa Misri.
Kwa nini Mungu aliwaambia Waisraeli kufungua wazi midomo yao?
Alisema kuifungua ili aijaze.
Psalms 81:11-12
Watu wa Yahwe, Israeli. hawakufanya nini?
Hawakusikiliza maneno ya Yahwe au kumtii.
Kwa nini Yahwe aliwaruhusu watu wafuate njia yao ya usumbufu?
Aliwaruhusu ili wafanye kile walichoona ni sawa kwao.
Psalms 81:13-14
Yahwe anatamani watu wake wafanye nini?
Yahwe anataka watu wake kumsikiliza na kutembea katika njia zake.
Yahwe atafanya nini kama watu wake hawatamsikiliza nakutembea katika njia yake?
Atawatuliza adui zao upesi na kugeuza mkono wake dhidi ya wakandamizaji wao.
Psalms 81:15-16
Mwandishi anataka nini kitokee kwa wale wanaomchukia Yahwe?
Anataka wanywee kwa hofu na kuaibika milele.
Yahwe anasema atafanya nini kwa ajili ya Israeli?
Yahwe atawalisha na ngano safi zaidi na kuwaridhisha kwa asali kutoka katika mwamba.
Psalms 82
Psalms 82:1-2
Mungu anaanza kutoa hukumu wapi?
Anasimama katika kusanyiko takatifu na miongoni ya miungu.
Asafu anamwuliza nini Mungu?
Anamwuliza Mungu atahukumu bila haki na kuonesha upendeleo kwa waovu hadi lini?
Psalms 82:3-4
Asafu anamwomba Mungu awafanyie nini masikini na wasio na baba na walioteseka na fukara?
Anamwomba Mungu kuwatetea na kutunza haki zao.
Asafu anamwomba Mungu kufanya nini kwa ajili ya masikini na wahitaji?
Anamwomba Mungu kuwaokoa na kuwatoa katika mkono wa mwovu.
Psalms 82:5
Wale ambao hawajui walakuelewa huzurura wapi?
Huwa wanazurura gizani.
Psalms 82:6-7
Asafu anasema wana wa Aliye juu watakufaje?
Watakufa kama watu na kuanguka kama mmoja wa wakuu.
Psalms 82:8
Kwa nini Asafu anamwomba Mungu kuinuka na kuihukumu dunia?
Anamwomba Mungu kuhukumu kwa sababu atarithi mataifa yote.
Psalms 83
Psalms 83:1-2
Maadui wa Mungu wanafanya nini?
Wanafanya vurugu, na wameinua vichwa vyao.
Psalms 83:3-8
Maadui wa Mungu wanapanga njama dhidi ya nani?
Wanapanga njama dhidi ya watu wa Mungu na kupanga hila dhidi ya wanaolindwa wa Mungu.
Maadui wa Israeli wanasema watafanya nini kwa Israeli?
Walisema, "Na tuwaangamize kama taifa"
Nini kingetokea kwa jina la Israeli kama maadui wa Mungu wangewaangamiza?
Israeli hatakumbukwa tena.
Maadui wa Mungu wamepanga hila dhidi ya nani?
Walipanga hila dhidi ya Mungu na kuunda ushirikiano.
Psalms 83:9-10
Asafu anamuuliza nini Mungu kufanya kwa adui zake, kama alivyofanya kwa Midiani, Sisera na Yabini?
Anaomba ya kwamba watoweke kule Endori na kuwa kama mbolea kwa ajili ya nchi.
Psalms 83:11-12
Waadilifu na wakuu wa maadui walisema nini juu ya Israeli?
Walisema, "Na tujichukulie kwa ajili yetu malisho ya Mungu"
Psalms 83:13-15
Asafu anataka vitu gani Mungu awafanye adui zake?
Anataka Mungu kuwafanya kama vumbi linalovuma, makapi mbele ya upepo, moto ambao huchoma msitu, na mwale ambao huwasha milima motoni.
Asafau anataka Mungu afukuze na kuwatisha adui zake kwa njia ipi?
Anamtaka Mungu kuwafukuza na upepo wa nguvu wa Mungu an kuwatishakwa dhoruba ya Mungu.
Psalms 83:16-17
Kwa nini Asafu anamuuliza Yahwe kuwajaza nyuso za maadui na aibu?
Anamuuliza Mungu kujaza maadui zake na aibu ili kwamba waweze kutafuta jina la Yahwe.
Asafu anataka nini kutokea kwa adui za Mungu?
Anatamani ya kwamba waweze kuaibishwa, kutishwa milele na kutoweka kwa aibu.
Psalms 83:18
Maadui wa Mungu watajua nini kuhusu Yahwe?
Watajua ya kwamba Yahwe pekee ndiye aliye Juu Zaidi juu ya dunia nzima.
Psalms 84
Psalms 84:1-2
Mwandishi anasema nini kuhusu sehemu ambayo Yahwe wa majeshi huishi?
Anasema sehemu ambapo Yahwe wa majeshi huishi ni nzuri.
Mwandishi anashauku ya nini?
Anatamani nyua za Yahwe.
Moyo na mwili wote wa mwandishi unamwita nani?
Moyo wake na mwili wake wote unamwita Mungu aliye hai.
Psalms 84:3-4
Shomoro amepata wapi nyumba yake na mbayuwayu kiota ambapo anaweza kutaga makinda yake.
Wamepata nyumba yao na kiota chao karibu na madhabahu ya Yahwe wa majeshi.
Mwandishi anatumia jina gani jingine kwa ajili ya Yahwe wa majeshi?
Anatumia majina ya Mfalme wangu na Mungu wangu.
Nini hutokea kwa wale wanaoishi katika nyumba ya Yahwe?
Wamebarikiwa na wanamsifu Yahwe kila wakati.
Psalms 84:5-6
Nini hutokea kwa mtu amabye nguvu yake iko katika Yahwe?
Mtu ambaye nguvu yake iko katika Yahwe amebarikiwa.
Waliobarikiwa hupata wapi chechemi za maji ya kunywa?
Wanapata chemchemi za maji ya kunywa wanapopita katika bonde la Vilio.
Psalms 84:7-10
Watu waliobarikiwa wanatokea wapi?
Wanatokea mbele za Mungu Sayuni.
Mwandishi anataka nani asikie ombi lake?
Anamtaka Yahwe Mungu wa majeshi kusikia ombi lake.
Mwandishi anataka nani asikie anachosema?
Anamtaka Mungu wa Yakobo kusikia kile anachosema.
Mwandishi anataka Mungu aangalie nini na anataka Mungu amjali nani?
Anataka Mungu kuangalia juu ya ngao yao na kuwajali watiwa mafuta wa Mungu.
Siku moja katika mabaraza ya Yahwe ni bora zaidi ya nini?
Siku katika mabaraza ya Yahwe ni bora zaidi miaka elfu sehemu nyingine.
Kwa nini mwandishi anaona ni bora kuwa katika nyumba ya Mungu wake kuliko kuishi katika hema za waovu?
Ni bora awe bawabu katika nyumba ya Mungu wake.
Psalms 84:11-12
Yahwe Mungu ni nini kwa mwandishi?
Yahwe Mungu ni jua letu na ngao.
Yahwe atatoa nini?
Yahwe atatoa neema na utukufu.
Yahwe hazui nini kwa wale wanaotembea katika uadilifu?
Yahwe hazui kitu chochote kizuri kwa wale wanaotembea katika uadilifu.
Nini hutokea kwa mtu anayemtumaini Yahwe wa majeshi?
Mtu anayemtumaini Yahwe atabarikiwa.
Psalms 85
Psalms 85:1-2
Yahwe amefanya nini kwa ajili ya ustawi wa Yakobo?
Yahwe ameonesha fadhila katika nchi yao na kurejesha ustawi wa Yakobo.
Yahwe amefanya nini kuhusu dhambi za watu wake?
Amewasamehe watu wake na kufunika dhambi zao.
Psalms 85:3-5
Yahwe amefanya nini na gadhabu yake na hasira ya moto?
Ameondoa gadhabu yake yote na kugeuka kutoka katika hasira yake ya moto.
Mwandishi anamwomba Mungu kuacha nini?
Anamwomba Mungu kuachia hasira yake na watu wake.
Psalms 85:6-7
Watu wa Mungu watafanya nini kama Mungu akiwarudisha tena?
Watu wa Mungu watashangilia katika Mungu.
Mwandishi anamwomba Mungu kuonesha na kuwapa watu wake nini?
Anamwomba Yahwe kuonesha uaminifu wake wa agano na kuwapa wokovu wake.
Psalms 85:8-9
Mwandishi anasema nini kitatokea atakaposikiliza kwa kile ambacho Yahwe Mungu anasema?
Mungu atafanya amani na watu wake, wafuasi wake waaminifu.
Watu wanapaswa kufanya nini kuwa na amani na Mungu?
Watu wa Mungu hawapaswi kugeukia tena njia za kipumbavu.
Nini kitabaki nchini wakati wokovu wa Mungu utakapokuwa karibu ya wale wanaomcha?
Mungu atabaki katika nchi.
Psalms 85:10-11
Nini zimekutana pamoja na kupigana busu?
Uaminifu wa agano na uaminifu zimekutanapamoja na haki na amani zimepigana busu.
Nini kitachipuka kutoka ardhini na nini kitaangilia kutoka angani?
Uaminifu utachipuka na ushindi utaangalia chini.
Psalms 85:12-13
Nini kitatokea Yahwe akitoa baraka yake njema?
Nchi yao itatoa mazao yake.
Nini kitatangulia mbele ya YAhwe na kufanya njia kwa ajili ya hatua zake?
Haki itatangulia mbele ya Yahwe.
Psalms 86
Psalms 86:1-2
Kwa nini Daudi anamwomba Yahwe kumsikiliza na kumjibu?
Anamwomba Yahwe kumjibu kwa sababu Daudi ni masikni na amekandamizwa.
Daudi anamwomba Mungu kumfanyia nini anapokuwa mwaminifu na kumtumaini Mungu?
Daudi anamwomba Mungu kumlinda na kumwokoa.
Psalms 86:3-4
Daudi anaomba nini anapolia kwa Bwana?
Daudi anamwomba Bwana kuwa na huruma kwake.
Daudi anamwomba nini Bwana anapoinua nafsi yake kwake?
Daudi anamwomba Bwana kumfanya mtumishi wake kuwa na furaha.
Psalms 86:5-7
Nini hutokea kwa wale wote wanaolia kwa Bwana ambaye ni mwema?
Bwana yuko tayari kusamehe na kuwaonesha huruma kuu.
Daudi anamwomba nani asikie ombi lake na asikie madai yake?
Daudi anamwomba Yahwe amsikilize.
Yahwe atafanya nini Daudi atakapomwita katika siku yake ya taabu?
Yahwe atamjibu Daudi.
Psalms 86:8-9
Nani anafananishwa na Bwana miongoni mwa miungu?
Hakuna mtu anayefananishwa na Bwana.
Mataifa yote yatafanya nini mbele za Bwana?
Mataifa yote yatakuja na kuinama mbele za Bwana na kulipa heshima jina la Bwana.
Psalms 86:10-12
Nani peke yake hufanya mambo makuu na ya ajabu?
Mungu peke yake hufanya mambo makuu na ya ajabu.
Daudi anamwomba Yahwe amfundishe nini?
Daudi anamwomba Yahwe kumfundisha njia za Yahwe.
Nini kitatokea Yahwe akimfundisha Daudi?
Daudi atatembea katika ukweli wa Yahwe.
Daudi anamwambia Mungu atafanya nini?
Daudi atamsifu Mungu na kulitukuza jina la Mungu milele.
Psalms 86:13-14
Daudi anasema uaminifu wa agano wa Mungu kwake umemfanya nini?
Mungu ameokoa nafsi ya Daudi kutoka katika vilindi vya kuzimu.
Daudi anasema watu enye kiburi na vurugu wamefanya nini?
Wameinuka dhidi ya Daudi, wakitafuta masiha yake na hawamjali Mungu.
Psalms 86:15-17
Daudi anamwelezeaje Bwana?
Daudi anamwelezea Bwana kama Mungu mwenye huruma na neema, wa polepole kukasirika, na mwingi wa uaminifu wa agano na uaminifu.
Daudi anamwomba Bwana kumfanyia nini?
Daudi anawmomba Bwana kumgeukia, kuwa na huruma juu yake, kumpa nguvu na kumwokoa.
Nini kitatokea Yahwe atakapomwonesha Daudi ishara ya fadhila yake?
Wale wanomchukia Daudi wataonda fadhila ya Mungu na kuaibishwa.
Daudi anasema Yahwe amefanya nini kwa ajili yake?
Yahwe amemsaidia Daudi na kumfariji.
Psalms 87
Psalms 87:1-3
Mji wa Bwana umewekwa wapi?
Imewekwa katika milima mitakatifu.
Yahwe anapenda malango ya Sayuni kiasi gani?
Inaipenda kulikoa hema zote za Yakobo.
Vitu gani vinasemwa kuhusu mji wa Mungu?
Vitu va utukufu vinasemwa kuhusu mji wa Mungu.
Psalms 87:4
Mwandishi alitaja Rahabu na Babeli kwa nani?
Alitaja kwa wafuasi wake.
Psalms 87:5-6
Aliye juu atafanya nini kwa ajili ya Sayuni?
Aliye juu atamthibitisha mwenyewe.
Yahwe anatambua nini anapowaandika watu?
Anatambua, "Huyu hapa alizaliwa hapo."
Psalms 87:7
Waimbaji na wachezaji wanasema nini?
Wansema, "Chemchemi zangu zote za maji ziko ndani yako."
Psalms 88
Psalms 88:1-2
Mwandishi analia wakati gani kwa Yahwe, Mungu wa wokovu?
Mwandishi analia machana na usiku mbele za Yahwe.
Mwandishi anamwomba Yahwe amfanyie nini?
Anamwomba Yahwe kumsikiliza ombi lake na kuvuta nadhari kwa kilio chake.
Psalms 88:3-4
Nafis ya maisha ya mwandishi yana shida gani?
Nafsi yake imejaa taabu na maisha yake yamekaribia kuzimu.
Mwandishi anajielezeaje wakati watu wanapomtenda kama wale wanaoshuka shimoni?
Anajielezea kama mtu asiye na nguvu.
Psalms 88:5-6
Mwandishi anasema nini hutokea kwake akiwa kama wafu waliolala kaburini?
Anasema Yahwe hawajali wafu tena kwa sababu wamekatwa kutoka katika nguvu ya Yahwe.
Mwandishi anasema Yahwe amemweka wapi?
Ansema amemweka katika sehemu ya chini zaidi shimoni.
Psalms 88:7
Nini kinamkandamiza mwandishi?
Gadhabu ya Yahwe inamkandamiza mwandishi.
Psalms 88:8
Yahwe amefanya nini kuwafanye wenzake na mwandishi wamkwepe?
Yahwe amemfanya mwandishi kuwa kitu cha kushangaza machoni pa wenzake.
Psalms 88:9-10
Macho ya mwandishi yanachoka kwa sababu ya nini?
Macho yake yamechoka kwa sababu ya taabu.
Mwandishi anamwuliza Yahwe maswali gani kuhusu wafu?
Anamwuliza Yahwe kama atafanya maajabu kwa ajili ya wafu, na kama watainuka na kumsifu Yahwe.
Psalms 88:11-12
Mwandishi anamwuliza nini Yahwe kuhusu uaminifu wake wa agano, uaminifu, matendo ya ajabu na haki?
Mwandishi anamwuliza Yahwe kama hivi vyote vitatangazwa kaburini, katika sehemu ya wafu, gizani na katika sehemu ya usahaulifu.
Psalms 88:13-14
Ombi la mwandishi linafika kwa Yahwe wakati gani?
Ombi lake linafika mbele za Yahwe asubuhi.
Yahwe amefanya nini kwa mwandishi?
Yahwe amemkataa mwandishi na kuficha uso wake kwake.
Psalms 88:15-16
Mwandishi ameteseka kwa muda gani na kuwa karibu na mauti?
Mwandishi ameteseka na kuwa karibu na mauti tangu ujana wake.
Mwandishi anasema matendo ya hasira na ya kutisha ya Yahwe yamefanya nini?
Matendo ya Yahwe yamepita juu na kumwangamiza mwandishi.
Psalms 88:17-18
Matendo ya Yahwe yamemfanya nini mwandishi siku nzima?
Yanamzunguka mwandishi kama maji yanvyomzunguka.
Mwandishi anasema anafahamiana na nini pekee?
Anasema mwenzake ni giza pekee.
Psalms 89
Psalms 89:1-2
Mwandishi ataimba kuhusu nini milele?
Ataimba kuhusu matendo ya Yahwe ya uaminifu wa agano.
Mwandishi atatangaza nini kwa vizazi vya baadaye?
Atatangaza ukweli wa Yahwe.
Ukweli wa Yahwe umeimarishwa wapi?
Umeimarishwa mbinguni.
Psalms 89:3-4
Agano na kiapo vimefanywa na nani?
Agano limefanywa na aliye chaguliwa na kiapo kimefanywa kwa Daudi.
Uzao na kiti cha enzi kitaimarishwa hadi lini?
Uzao utaimarishwa milele na kiti cha enzi katika vizazi vyote.
Psalms 89:5-6
Mbingu zitamsifu Yahwe kwa sababu gani?
Mbingu zitamsifu Yahwe kwa maajabu yake.
Mkusanyiko wa watakatifu utamsifu Yahwe kwa sababu gani?
Watamsifu Yahwe kwa ukweli wake.
Psalms 89:7-8
Mungu analinganishwaje na wale wanaomzunguka?
Ni wa ajabu zaidi ya wote wanaomzunguka.
Mwandishi anasema nini kuhusu ukweli wa Yahwe?
Unamzunguka Yahwe.
Psalms 89:9-10
Mwandishi anasema nini kuhusu utawala wa Yahwe juu ya bahari lenye hasira?
Anasema kwamba wakati mawimbi yanapotapakaa, Yahwe huyatuliza.
Yahwe alifanya nini kwa Rahabu?
Alimponda kama mtu ambaye ameuawa.
Yahwe alitumia nini kuwatawanya adui zake?
Alitumia mkono wake wenye nguvu.
Psalms 89:11-12
Nini ni mali ya Yahwe ambaye aliumba dunia na kila kitu kilichomo?
Mbingu na nchi ni mali za Mungu.
Yahwe aliumba nini?
Yahwe aliumba kaskazini na kusini.
Psalms 89:13-14
Mwandishi anasema nini kuhusu mkono wa Yahwe?
Yahwe ana mkono wa nguvu na mkono wake wa kuume uko juu.
Msingi wa kiti cha enzi cha Yahwe ni nini?
Haki na hukumu ni msingi wa kiti cha enzi cha Yahwe.
Nini huja mbele ya Yahwe?
Uaminifu wa agano na uaminifu huja mbele za Yahwe.
Psalms 89:15-16
Nini hutokea kwa watu wanaomwabudu Yahwe?
Wamebarikiwa na hutembea katika nuru ya uso wa Yahwe, wanashangilia katika jina la Yahwe, na kutukuza katika haki ya Yahwe.
Psalms 89:17-18
Nguvu ya kifahari ya Yahwe na fadhila zake zinawanufaishaje watu?
Watu ni washindi.
Ni nini mali ya Yahwe na jina lake ni nini?
Ngao ya watu ni mali ya Yahwe na inaitwa Mtakatifu wa Israeli.
Psalms 89:19-23
Yahwe alisema nini katika maono yake kwa watakatifu wake?
Alisema kuwa aliweka taji juu ya mtu hodari na kumwinua mmoja kutoka miongoni mwa watu.
Yahwe alisema atafanya nini kwa ajili ya mtumishi wake Daudi aliyemchagua?
Alisema kuwa alimtia mafuta, atamshikilia, na kumtia nguvu.
Psalms 89:24-26
Nini kitakuwa na Daudi na atakuwaje mshindi?
Ukweli wa Yahwe na uaminifu wa agano utakuwa na Daudi na kwa jina la Yahwe Daudi atashinda.
Daudi ataita nini kwa Yahwe?
Atamwita Yahwe baba yake, Mungu wake, na mwamba wa wokovu wake.
Psalms 89:27-29
Yahwe atafanya nini kwa ajili ya Daudi ambaye amemfanya kuwa mzaliwa wake wa kwanza na aliyetukuzwa kwa wafalme wa duniani?
Yahwe atanyosha na kuimarisha uaminifu wake wa agano kwa Daudi milele.
Uzao wa Daudi na kiti chake cha enzi kitadumu kwa muda gani?
Uzao wake utadumu milele na kiti chiki cha enzi kitadumu kama anga za juu.
Psalms 89:30-32
Yahwe atawafanya nini watoto wa Daudi kama wakiacha sheria ya yahwe, kukaidi amri zake, kuvunja sheria zake na kutokutunza amri zake?
Yahwe ataadhibu ukaidi wao kwa fimbo na udhalimu wao kwa mapigo.
Psalms 89:33-34
Yahwe anampa Daudi ahadi gani?
Yahwe anaahidi kutoondoa uaminifu wake wa agano au kukoma kuwa mwaminifu kwa ahadi yake. Hatavunja agano lake au kubadili maneno ya midomo yake.
Psalms 89:35-37
Yahwe anaapa kwa nini?
Yahwe anaapa kwa utakatifu wake.
Psalms 89:38-40
Mwandishi anasemaje sasa kuhusu jinsi Daudi anavyotendewa na Yahwe?
Mwandishi anasema kuwa yahwe amemkataa na ana hasira na mfalme aliyetiwa mafuta.
Psalms 89:41-43
Mwandishi anasema nini kinatokea kwa mfalme aliyetiwa mafuta?
Anaibiwa na amekuwa chombo cha kuudhi kwa jirani zake.
Adui wa mfalme aliyetiwa mafuta wamefanya nini?
Wameinua mkono wao wa kuume na wamefanywa kushangilia.
Nini kilitokea wakati mfalme aliyetiwa mafuta alipokwenda vitani?
Makali ya upanga wa mfalme umegeuka na ulifanywa kushindwa kusimama vitani.
Psalms 89:44-45
Nini kimetokea kwa fahari ya mfalme na kiti chake cha enzi?
Fahari yake imefikishwa mwisho na kiti chake cha enzi kimeletwa chini hadi ardhini.
Nini kimetokea kwa siku za mfalme aliyetiwa mafuta?
Siku zake zimefupishwa na amefunikwa na aibu.
Psalms 89:46-48
Mwandishi anamwuliza nini Yahwe kuhusu hasira yake?
Anamwuliza Yahwe atajificha hadi lini na hasira yake kuwaka kama moto.
Mwandishi anamwomba Yahwe kuwaza kuhusu nini?
Anamwomba Yahwe kuwaza kuhusu jinsi muda wake ulivyo mfupi kwa ubatili ambao Yahwe amewaumba wanadamu.
Psalms 89:49-51
Mwandishi anamwuliza nini Bwana kuhusu matendo yake ya nyuma ya uaminifu wa agano?
Mwandishi anamwuliza Bwana, "Yako wapi matendo yake ya nyuma ya uaminifu wa agano?"
Mwandishi anamwambia Bwana akumbuke nini?
Anamwambia Bwana kuwa adui wa Yahwe wanamtupia matusi na kukejeli hatua za mtiwa mafuta wa Yahwe.
Psalms 89:52
Mwandishi anasema Yahwe atabarikiwa kwa muda gani?
Yahwe atabarikiwa milele.
Psalms 90
Psalms 90:1-2
Bwana amekuwa kimbilio kwa ajili ya Musa na watu kwa muda gani?
Bwana amekuwa kimbilio katika vizazi vyote.
Psalms 90:3-4
Bwana anamrudisha mtu kuwa nini?
Hurudi mavumbini.
Miaka elfu ni kama nini machoni pa Bwana?
Ni kama jana inapopita, na kama mkesha usiku.
Psalms 90:5-6
Uzao wa mwanadamu ni kama nini?
Wako kama nyasi zinazochipuka, chanuka na kuota, na kisha kusinyaa na kukauka.
Psalms 90:7-8
Kwa nini mwanadamu anamezwa katika hasira ya Bwana na kuogopa gadhabu yake?
Wanamezwa na kuogopa kwa sababu Bwana ameweka udhalimu wao mbele yake, na kuficha dhambi zao katika nuru ya uwepo wake.
Psalms 90:9-10
Binadamu kama ana afya huwa ana miaka mingapi?
Miaka yao ni themanini kama wana afya.
Psalms 90:11-13
Musa anamwomba Bwana kuwafundisha nini wanadamu?
Anamwomba Bwana kuwafundisha wanadamu kuzingatia maisha yao, ili waishi kwa hekima.
Psalms 90:14-16
Musa anamtaka Bwana amridhishe na nini mwanadamu asubuhi?
Anamtaka Bwana amridhishe mwanadamu kwa uaminifu wa agano wa Bwana, ili kwamba washangilie na kufurahi siku zao zote.
Musa anamtaka Bwana awaoneshe nini watumishi wake?
Anamtaka Bwana kuwaruhusu watumishi wake waone kazi yake na watoto wao waone utukufu wake.
Psalms 90:17
Bwana anaoneshaje fadhila kwa wanadamu?
Anafanikisha kazi ya mikono yao.
Psalms 91
Psalms 91:1-2
Mwandishi anasema nini kumhusu Yahwe?
Mwandishi anasema, "Yeye ni kivuli changu na ngome yangu, Mungu wangu, ambaye ninayemtumaini."
Psalms 91:3-4
Yahwe atafanya nini kwa ajili ya yule anaye mtumaini?
Yahwe atamwokoa kutoka katika mtego wa mwindaji na kutoka katika pigo kali na kumfunika kwa mabawa.
Psalms 91:5-7
Yule anaye mtumaini Yahwe haitaji kuogopa nini?
Yule anaye mtumaini Yahwe haitaji kuogopa hofu ya usiku, au mshale unaopaa mchana, mapigo yanayozururazurura gizani, na magonjwa yanayokuja mchana.
Psalms 91:8-9
Yahwe ni nini kwa mwandishi?
Yahwe ni kimbilio la mwandishi.
Psalms 91:10-11
Kwa nini hakuna uovu utakaompita au mateso yatakayokuja karibu na nyumba ya yule anayemtumaini Yahwe?
Hakuna uovu utakaompita wala mateso kuja karibu ya yule anayemtumaini Yahwe kwa sababu Yahwe atawaongoza malaika wake kumlinda na kumchunga katika njia zake zote.
Psalms 91:12-13
Malaika watamlindaje na kumchunga yule anayetumaini katika Yahwe?
Malaika watamwinua kwa mkono wao ili asiteleze na kuanguka juu ya jiwe.
Psalms 91:14-16
Yahwe hufanya nini kwa yule aliyejitolea kwake?
Yahwe atamwokoa, atamlinda, atamjibu anapoita, atampa ushindi na heshima wakati yuko kwenye taabu, atamridhisha kwa maisha marefu, na kumwonesha wokovu wa Yahwe.
Psalms 92
Psalms 92:1-3
Mwandishi anaona kitu gani kuwa chema?
Ni kitu chema kutoa shukrani na kuimba sifa kwa jina la Yahwe.
Mwandishi anasema uaminifu wa agano wa Yahwe na ukweli wake utangazwe wakati gani?
Ansema kutangaza uaminifu wa agano wa Yahwe asubuhi na ukweli wake kila usiku.
Psalms 92:4-5
Mwandishi ameitikiaje matendo makuu ya Yahwe?
Matendo makuu ya Yahwe yamemfanya kuwa na furaha hadi ataimba kwa furaha.
Psalms 92:6-7
Ni aina gani ya mtu hajui na kuelewa furahi hii?
Furaha hii haijulikani na mtu mkatili wala mpumbavu.
Hatima ya waovu wanaochipuka kama nyasi na watenda maovu wanaofanikiwa ni nini?
Waovu wanaochipuka kama nyasi na watenda maovu wanaofanikiwa bado wamehukumiwa uharibifu wa milele.
Psalms 92:8-9
Kwa nini watenda waovu wote wanatawanyika ambao ni adui wa Yahwe?
Watenda maovu wote wanatawanyika kwa sababu Yahwe atatawala milele.
Psalms 92:10-11
Yahwe ametukuzaje pembe la mwandishi na kumtia mafuta mapya?
Yahwe amemtukuza na kumtia mafuta mwandishi kwa kumruhusu kuona anguko la adui zake na kusikia maangamizi ya adui zake waovu.
Psalms 92:12-13
Wenye haki wamepandwa wapi?
Wamepandwa katika nyumba ya Yahwe.
Psalms 92:14-15
Wenye haki wanafanya nini kutangaza kwamba Yahwe ni mwenye haki?
Wenye haki wanatoa matunda wanapozeeka na kubaki wapya na kijani.
Kwa nini Yahwe ni mwamba wa mwandishi?
Yahwe ni mwamba kwa sababu hakuna upungufu wa haki katika Yahwe.
Psalms 93
Psalms 93:1-2
Yahwe amevaa kanzu ya nini na vazi gani?
Yahwe amevaa kanzu ya utukufu na kuvaa vazi la nguvu ambalo huvaa kama mshipi.
Psalms 93:3-4
Bahari imeinuaje juu sauti yake?
Bahari huinuka na mawimbi yake huporomoka na kuunguruma.
Ni nani yupo juu ya mawimbi mengi yanayoporomoka na wavunja bahari?
Yahwe aliye juu ana uwezo na juu ya mawimbi mengi yanayoporomka na wavunjaji wenye uwezo wa bahari.
Psalms 93:5
Mwandishi anaelezaje amri na utakatifu wa Yahwe?
Mwandishi anasema ya kwamba amri za Yahwe zinaaminika sana na utakatifu hupamba nyumba ya Yahwe milele.
Psalms 94
Psalms 94:1-2
Mwandishi anamuuliza Yahwe Mungu kufanya nini?
Mwandishi anamuuliza Yahwe Mungu kung'aa juu ya watu wake na kutoa kwa wenye kiburi kile wanachostahili.
Psalms 94:3-4
Waovu wanashangiliaje kwa kile wanachosema?
Waovu wanashangilia kwa kumwaga maneno ya ufidhuli, ya dharau na kujivuna.
Psalms 94:5-7
Tabia ya waovu ni ipi?
waovu huponda watu wa Yahwe na wanaua mjane, mgeni na asiye na baba.
Waovu wanasema kitu gani?
Waovu wanasema ya kwamba Yahwe hataona wala hatatambua kile wanachofanya.
Psalms 94:8-9
Swali gani mwandishi anauliza kwa wapumbavu?
Anawauliza, "Mtajifunza lini?"
Psalms 94:10-11
Yahwe anajua nini kuhusu mawazo ya watu?
Yahwe anajua ya kwamba mawazo ya watu yamepotoka.
Psalms 94:12-13
Yahwe anafanya nini kwa yule ambaye amebarikiwa?
Yahwe anafundisha sheria yake na kutoa pumziko katika nyakati za shida kwa yule ambaye amebarikiwa.
Psalms 94:14-16
Mwandishi anatoa ahadi gani kwa watu wa Yahwe?
Mwandishi anasema ya kwamba Yahwe hatawaacha watu wake wala kuacha urithi wake.
Matokeo ya ahadi ya Yahwe ni ipi?
Matokeo ya ahadi ya Yahwe ni kwamba haki itatawala na wanyoofu wote wataifuata.
Psalms 94:17-19
Utoaji gani kutoka kwa Yahwe ulikuwa msaada kwa mwandishi?
Utoaji ulikuwa agano la Yahwe la uaminifu ambalo lilimshika mwandishi aliposema, "mguu wangu unatereza".
Psalms 94:20-21
Watawala waovu wanatengenezaje udhalimu kwa sheria?
Watawala waovu wanatengeneza udhalimu kwa kupanga njama dhidi ya wenye haki na kuhukumu wasio na hatia kwa kifo.
Psalms 94:22-23
Yahwe amemtiaje moyo mwandishi?
Yahwe amemtia moyo mwandishi kwa kuwa mnara wake wa juu na mwamba wa kimbilio lake.
Yahwe atafanya nini kwa watawala waovu?
Yahwe ataleta juu yao udhalimu wao wenyewe na kuwakata katika uovu wao wenyewe.
Psalms 95
Psalms 95:1-3
Mwandishi anawasihi kila mmoja kuingia kwa namna gani?
Mwandishi anawasihi watu wote kuingia katika uwepo wa Yahwe kwa shukrani.
Yahwe analinganishwaje kwa miungu wengine?
Yahwe ni Mungu mkuu na Mfalme mkuu ambaye ni mkuu kwa miungu yote.
Psalms 95:4-5
Ni kwa namna gani Yahwe ni mkuu kwa miungu yote?
Yahwe ni mkuu kwa miungu yote kwa kuwa vilele vya milima na bahari ambavyo alivitengeneza ni vyake na mikono yake iliumba nchi kavu.
Psalms 95:6-7
Kwa nini kila mtu anapaswa kuabudu kwa kuinama chini na kupiga magoti mbele za Yahwe?
Kila mtu anapaswa kumwabudu Yahwe kwa sababu ni Mungu wao na wao ni watu wa malisho yake na kondoo wa nchi yake.
Psalms 95:8-9
Mababu wa Israeli walijibuje kwa Yahwe?
Walishindana na mamlaka yake na kujaribu uvumilivu wake, ingawa waliona matendo yake.
Psalms 95:10-11
Yahwe alielezaje watu ambao walishindana na mamlaka yake?
Yahwe alisema, "Hawa ni watu ambao mioyo yao hutangatanga kwa kupotoka; hawajajua njia zangu".
Yahwe aliapa nini katika hasira yake?
Yahwe aliapa katika hasira yake ya kwamba watu walioshindana na mamlaka ayke hawataingia katika sehemu ya kupumzika ya Yahwe.
Psalms 96
Psalms 96:1-2
Mwandishi anawatia moyo watu wote kutanganza nini?
Mwandishi anawatia moyo watu wote kutangaza wokovu wa Yahwe siku baada ya siku.
Psalms 96:3-4
Kwa nini kila mtu anapaswa kutamka utukufu wa Yahwe na matendo yake ya ajabu miongoni mwa mataifa?
Kila mtu anapaswa kutamka utukufu wa Yahwe na matendo yake ya ajabu kwa sababu Yahwe ni mkuu, na anatakiwa kusifiwa sana, na kugopwa juu ya miungu wengine wote.
Psalms 96:5-6
Sifa gani zipo katika uwepo wa Yahwe?
Sifa zilizopo katika uwepo wa Yahwe ni ufahari, utukufu, nguvu na uzuri.
Psalms 96:7-8
Kila mtu anapaswa kufanya nini kumpatia Yahwe utukufu anaostahili kwa jina lake?
Kila mtu anatakiwa kuleta sadaka na kuja katika mabaraza yake.
Psalms 96:9-10
Mwandishi aliwasihi watu kusema nini miongoni mwa mataifa?
Mwandishi anawasihi kila mtu kusema, "Yahwe anatawala".
Yahwe anahukumuje watu?
Yahwe anahukumu watu kwa usawa.
Psalms 96:11-13
Kwa nini mbingu zinatakiwa kuwa na furaha na dunia kushangilia?
Mbingu inatakiwa kuwa na furaha na dunia kushangilia kwa sababu Yahwe anakuja.
Yahwe atafanya nini atakaporudi?
Yahwe atakaporudi atahukumu dunia, ulimwengu kwa haki, na watu kwa uaminifu wake.
Psalms 97
Psalms 97:1-2
Msingi wa kiti cha enzi cha Yahwe ni upi?
Msingi wa kiti cha enzi cha Yahwe ni haki na hukumu.
Psalms 97:3-5
Nini ni matokeo ya moto unakwenda mbele ya Yahwe?
Moto ambao hukwenda mbele ya Yahwe huteketeza wapinzani wake katika kila upande.
Nini kinatokea katika uwepo wa Yahwe?
Mwale wa radi wa Yahwe hutoa mwanga kwa dunia, dunia huona na kutetemeka, na milima huyeyuka kama nta katika uwepo wa Yahwe.
Psalms 97:6-8
Nini hutamka haki na utukufu wa Yahwe?
Anga zinatamka haki ya Yahwe na mataifa yote wanaona utukufu wake.
Nani ataaibishwa na Yahwe?
Wale wote wanaoabudu mifano ya kuchonga na kujivunia katika sanamu zisizo na maana wataaibishwa na Yahwe.
Kwa nini Sayuni walisikia na miji ya Yuda kusgangilia?
Sayuni alisikia na miji ya Yuda ilishangilia kwa sababu ya amri za haki za Yahwe.
Psalms 97:9-11
Mwandishi anasema nini kuhusu Yahwe?
Mwandishi anasema ya kwamba Yahwe yupo juu sana ya dunia yote na ameinuliwa juu ya miungu wote.
Yahwe anafanya nini kwa watakatifu wake?
Yahwe hulinda maisha ya watakatifu wake na kuwaondoa katika mikono ya waovu.
Psalms 97:12
Mwandishi anawasihi wenye haki kufanya nini?
Mwandishi anawasihi wenye haki kuwa na furaha katika Yahwe na kutoa shukrani kwa jina lake takatifu.
Psalms 98
Psalms 98:1-2
Nini kimetoa ushindi kwa watu wa Yahwe?
Mkono wa kuume wa Yahwe na mkono mtakatifu umewapa watu wake ushindi.
Yahwe ameonyesha nini wazi kwa mataifa yote?
Ameonyesha kwa wazi haki yake kwa mataifa yote.
Psalms 98:3-4
Yahwe anakumbuka nini?
Yahwe anakumbuka agano lake aminifu kwa ajili ya nyumba ya Israeli.
Nani ataona ushindi wa Mungu wa Israeli?
Mwisho wote wa dunia utaona ushindi wa Mungu wa Israeli.
Nini linapaswa kuwa jibu la kila mtu kwa utoaji wa Yahwe?
Kila mtu anapaswa kupiga kelele za furaha na kulia kwa wimbo, kuimba sifa za Yahwe.
Psalms 98:5-6
Nyumba ya Israeli inatakiwa kutumia vyombo gani kuimba sifa na kufanya kelele za furaha mbele ya Yahwe?
Nyumba ya Israeli inapaswa kutumia kinubi, tarumbeta, na sauti ya pembe.
Psalms 98:7-9
Mwandishi anamtiaje moyo uumbaji wa Yahwe kujibu kwa ujio wake?
Mwandishi anasema bahari na kila kitu ndani yake na dunia na wale wanaoishi ndani yake wanapaswa kupiga kelele, na mito inapaswa kupiga makofi mikono yao na milima inapaswa kupiga kelele za shangwe.
Yahwe atahukumuje ulimwengu?
Yahwe atahukumu dunia kwa haki na mataifa kwa usawa.
Psalms 99
Psalms 99:1-3
Mataifa yanapaswa kujibu kwa namna gani utawala wa Yahwe?
Mataifa yanapaswa kutetemeka kama jibu la utawala wa Yahwe.
Kwa nini dunia inatetemeka?
Dunia hutetemeka kwa sababu Yahwe hukaa katika kiti cha enzi juu ya makerubi.
Kwa nini Yahwe anainuliwa juu ya mataifa yote?
Yahwe anainuliwa kwa sababu ni mkuu Sayuni.
Kwa nini mataifa yanapaswa kusifu jina kuu na la ajabu la Yahwe?
Mataifa yanapaswa kusifu jina la Yahwe kwa sababu ni takatifu.
Psalms 99:4-5
Mwandishi anamwelezaje mfalme?
Mwandishi anasema mfalme ana nguvu na anapenda haki.
Mwandishi anasemaje ya kwamba mataifa wanapaswa kumjibu Yahwe?
Mwandishi anasema ya kwamba mataifa wanapaswa kumsifu Yahwe na kuabudu katika kigoda chake cha mguuni kwa sababu ni mtakatifu.
Psalms 99:6-7
Baadhi ya wanamume walioomba kwa Yahwe na akawajibu ni kina nani?
Baadhi ya hao wanamume walioomba kwa Yahwe na akawajibu walikuwa Musa, Haruni, na Samueli.
Wanamume walioomba kwa Yahwe walijibu kwa namna gani kwa kile alichosema?
Wanamume walioomba walishika kwa makini amri na sheria za Yahwe alizowapatia.
Psalms 99:8-9
Yahwe alifanya nini kwa wanamume walioomba kwake?
Yahwe alisamehe ingawa aliadhibu matendo yao ya dhambi.
Mwandishi anawatia moyo watu kufanya nini?
Mwandishi anasema kumsifu Yahwe na kumwabudu mkilima chake kitakatifu kwa sababu yeye ni mtakatifu.
Psalms 100
Psalms 100:1-2
Mwandishi anamkaribisha nani kushangilia kwa furaha kwa Yahwe?
Anakaribisha dunia yote kupiga kelele kwa furaha kwa Yahwe.
Watu wanapaswa kuja katika uwepo wa Yahwe kwa namna gani?
Wanapaswa kuja mbele ya uwepo wake kwa nyimbo za furaha.
Psalms 100:3
Picha gani mwandishi anatumia kuonyesha jinsi watu ni wa Yahwe?
Anasema wao ni watu wa Yahwe na kondoo wa malisho yake.
Psalms 100:4-5
Watu wanatakiwa kuingia kwa namna gani katika malango na mabaraza ya Yahwe?
Wanapaswa kuingia katika malango yake kwa shukrani na katika mabaraza yake kwa sifa.
Mwandishi anasema nini hudumu milele?
Anasema ya kwamba agano aminifu la Yahwe hudumu milele.
Psalms 101
Psalms 101:1
Daudi ataimba juu ya sifa gani mbili?
Ataimba juu ya agano aminifu na haki.
Psalms 101:2-3
Daudi hajaweka nini mbele ya macho yake?
Hajaweka matendo mabaya mbele ya macho yake.
Psalms 101:4-6
Daudi atamwangamiza nani?
Ataangamiza yeyote anayekashifu kwa siri jirani yake.
Daudi anataka watu wa aina gani wakae katika upande wake na kumtumikia?
Daudi anataka waaminifu wa nchi kukaa katika upande wake, na wale ambao hutembea kwa uadilifu kumtumikia.
Psalms 101:7-8
Daudi hatamruhusu nani kubaki katika nyumba yake?
Hataruhusu watu wadanganyifu kubaki katika nyumba yake.
Daudi anasema mara ngapi ya kuwa ataangamiza waovu wote kutoka katika nchi?
Asubuhi kwa asubuhi, ataangamiza waovu wote.
Psalms 102
Psalms 102:1-2
Aliyeteswa anaomba kwa Yahwe asifanye nini katika kipindi cha shida yake?
Aliyeteswa anamwomba Yahwe kutoficha uso wake kwake katika kipindi cha shida.
Psalms 102:3-4
Aliteswa analinganisha moyo wake uliopondwa na kitu gani?
Aliyeteswa anasema ya kwamba yeye ni kama nyasi ambayo imenyauka.
Psalms 102:5-6
Nini kimetokea kwa sababu ya malalamishi yanayoendelea ya aliyeteswa?
Kwa mingung'uniko inayoendelea ya walioteswa, amekuwa mwembamba sana.
Psalms 102:7-8
Wale wanaodhihaki walioteswa wanatumiaje jina lake?
Wale ambao hudhihaki walioteswa wanatumia jina lake kwa kulaani.
Psalms 102:9-10
Yule aliyeteswa anasema ametendewaje na hasira ya Yahwe?
Aliyeteswa anasema ya kwamba Mungu amemwinua juu kumtupa chini.
Psalms 102:11-12
Umaarufu wa Yahwe utadumu kwa muda gani?
Mwandishi anasema ya kwamba umaarufu wa Yahwe ni kwa vizazi vyote.
Psalms 102:13-16
Watumishi wa Yahwe wanahisi huruma kwa ajili ya nini?
Watumishi wa Yahwe watahisi huruma kwa ajili ya vumbi la uharibifu wa Sayuni.
Wafalme wa dunia wataonyesha heshima kwa Yahwe kwa namna gani?
Wafalme wote wa dunia wataheshimu utukufu wa Yahwe.
Psalms 102:17-18
Yahwe atajibu nini kwa tendo gani la mkiwa?
Yahwe atajibu maombi ya mkiwa.
Mwandishi anaonyeshaje umbali wa siku za usoni sifa za Yahwe zitaendelea?
Anaandika ya kwamba watu ambao hawajazaliwa watamsifu Yahwe.
Psalms 102:19-20
Yahwe anaona nini kutoka mbinguni?
Kutoka mbinguni Yahwe ameiona dunia.
Psalms 102:21-22
Watu na falme wamekusanyika pamoja kwa ajili ya tukio gani?
Watu na falme wamekusanyika pamoja kumtumikia Yahwe.
Psalms 102:23-24
Mwandishi aliyeteswa anasihi Mungu asifanye kitu gani?
Mwandishi alisema, "Mungu wangu, usinichukue katikati ya maisha yangu".
Psalms 102:25-27
Mwandishi anasema Yahwe alifanya nini katika nyakati za zamani?
Mwandishi anasema ya kwamba katika nyakati za zamani Yahwe aliweka dunia katika sehemu yake.
Miaka ya Yahwe itadumu kwa muda gani?
Miaka ya Yahwe haitakuwa na mwisho.
Psalms 102:28
Mwandishi anasema vizazi wa watumishi wa Yahwe wataishi wapi?
Vizazi wa watumishi wa Yahwe wataishi katika uwepo wake.
Psalms 103
Psalms 103:1-2
Daudi hataki kutosahau nini?
Hataki kutosahau matendo yote mema ya Yahwe.
Psalms 103:3-5
Daudi anasema Yahwe huvika taji nafsi yake kwa kutumia nini?
Anavika taji nafsi yake kwa agano la uaminifu na matendo ya rehema.
Psalms 103:6-8
Yahwe anafanya nini kwa wale ambao wanateswa?
Yahwe anafanya matendo ya haki kwa wote ambao wanateswa.
Yahwe alifanya nini kujulikana kwa vizazi vya Israeli?
Alifanya matendo yake kujulikana kwa vizazi vya Israeli.
Psalms 103:9-10
Daudi anasema Yahwe hataendelea kufanya nini?
Anasema Yahwe hataendelea kuadhibu, na hana hasira daima.
Daudi anasema Yahwe hafanyi nini na sisi?
Yahwe hafanyi na sisi kama jinsi dhambi zetu zinavyostahili.
Psalms 103:11-16
Yahwe ana huruma kwa wale ambao wanamwinua kwa njia gani maalumu?
Yahwe ana huruma kwa wale ambao wanamheshimu kwa njia sawa na baba ambayo anayo kwa watoto wake.
Psalms 103:17-19
Agano aminifu la Yahwe linadumu kwa muda gani?
Agano la uaminifu la Yahwe ni kutoka milele mpaka milele kwa wale ambao humheshimu.
Yahwe ameimarisha kiti chake cha enzi wapi?
Yahwe ameimarisha kiti chake cha enzi katika mbingu.
Psalms 103:20-22
Ni kina nani wenye nguvu kubwa ambao wameitwa kumbariki Yahwe na kutii neno lake?
Malaika wake wanaitwa kutii neno lake.
Watumishi ambao Daudi anasema hufanya mapenzi ya Yahwe ni kina nani?
Malaika wote wa Yahwe hufanya mapenzi yake.
Psalms 104
Psalms 104:1-3
Mwandishi anasema Yahwe amevikwa kwa namna gani?
Anasema kwamba Yahwe amevaa ufahari na enzi.
Kwa njia gani Yahwe hutandaza mbingu?
Anatandaza nje mbingu kama pazia la hema.
Psalms 104:4-5
Mwandishi anasema nini hakitatokea tena kwa misingi ya dunia ambayo Yahwe aliilaza?
Misingi ya dunia haitasogezwa tena.
Psalms 104:6-7
Mwandishi anasema ni kitu gani kilifanya maji kurudi nyuma?
Onyo la Yahwe lilifanya maji kurudi nyuma.
Psalms 104:8-12
Kwa nini maji hayatafunika dunia tena?
Yahwe aliweka mpaka kwa ajili yao ili wasiweze kuvuka.
Psalms 104:13-18
Mwandishi anasema mambo gani matatu ambayo Yahwe hutoa kwa ajili ya mtu?
Yahwe hutoa divai kumfanya mtu kuwa na furaha, mafuta kung'arisha uso wake, na chakula kushikilia maisha yake.
Psalms 104:19-20
Yahwe aliteua mwezi na jua kuwa alama gani?
Aliteua mwezi kuwa alama ya nyakati na jua kujua wakati wake wa kuzama.
Psalms 104:21-24
Nini hutokea kwa simba wadogo jua linapochomoza?
Jua linapochomoza, wanatoroka na kulala katika mapango yao.
Psalms 104:25-26
Bahari refu na pana linashirikiana na nini?
Bahari inashirikiana na viumbe wengi wote wakubwa na wadogo.
Psalms 104:27-28
Viumbe wote wa baharini wanatazama kwa nani kuwapa chakula chao?
Wote wanatazama kwa Yahwe kuwapa chakula chao kwa wakati.
Psalms 104:29-30
Nini hutokea kwa viumbe kama Yahwe akificha uso wake au kuondoa pumzi yake?
Anapoficha uso wake, wanapata taabu; kama akiondoa pumzi yao, wanakufa na kurudi mavumbini.
Psalms 104:31-32
Mwandishi anataka Yahwe afanye nini kwa uumbaji wake?
Mwandishi anataka Yahwe kufurahia uumbaji wake.
Psalms 104:33-34
Mwandishi anaahidi kuimba nini katika maisha yake yote?
Anaahidi kuimba sifa kwa Mungu wake iwapo bado anaishi.
Psalms 104:35
Mwandishi anatumaini nini kitatokea kwa wenye dhambi na waovu katika dunia?
Anataka wenye dhambi kupotelea kutoka duniani na waovu kutokuwepo.
Psalms 105
Psalms 105:1-3
Mwandishi anasema matendo ya Yahwe yajulikane wapi?
Mwandishi anawaita watu kufanya kujulikana matendo ya Yahwe miongoni mwa mataifa.
Mwandishi anashawishi moyo wa nani kushangilia?
Mwandishi anaita moyo wa wale ambao wanaomtafuta Yahwe kushangilia.
Psalms 105:4-6
Watu wanatakiwa kutafuta uwepo wa Mungu mara ngapi?
Mwandishi anawaita watu kutafuta uwepo wake daima.
Psalms 105:7-8
Kwa muda gani mwandishi anasema Mungu hushikilia neno ambalo ameliamuru?
Mwandishi anasema ya kwamba Mungu hushikilia neno ambalo aliamuru kwa vizazi elfu moja.
Psalms 105:9-11
NI agano gani mwandishi anasema Mungu huweka akilini?
Mungu anaweka akilini agano ambalo alilifanya na Abrahamu na kiapo chake kwa Isaka.
Agano gani la milele Yahwe amefanya na Israeli?
Yahwe alifanya agano la milele na Israeli kuwapa nchi ya Kaanani kama sehemu ya urithi wao.
Psalms 105:12-13
Mwandishi anasema Yahwe alifanya agano na Israeli wakati gani?
Mwandishi anasema ya kwamba Yahwe alisema agano hili wakati Israeli walikuwa wachache kwa idadi.
Psalms 105:14-15
Yahwe aliwaambia wafalme wasiguse nini?
Yahwe aliwaambia kutogusa waliotiwa mafuta wa kwake.
Psalms 105:16-17
Yahwe alimtumaje Yusufu mbele ya Israeli?
Alimtuma Yusufu mbele yao kuuzwa kama mtumishi.
Psalms 105:18-19
Yusufu aliwekwa katika minyororo ya chuma kwa muda gani?
Yusufu aliwekwa katika minyororo ya chuma mpaka kipindi ambacho utabiri wake ulipokuwa kweli.
Psalms 105:20-23
Msemo gani unatumika kuelezea mfalme kumweka Yusufu kusimamia nyumba yake?
Yusufu aliwekwa kusimamia nyumba ya mfalme kama mtawala wa mali zote za mfalme.
Yakobo aliishi wapi alipokuja Misri?
Yakobo aliishi kwa kipindi katika nchi ya Hamu.
Psalms 105:24-27
Mungu alisababisha nani kuchukia watu wake wa Israeli?
Mungu alisababisha maadui wa Israeli kuchukia watu wa Mungu.
Musa na Haruni walifanya ishara za Mungu wapi?
Musa na Haruni walifanya ishara za Mungu miongoni mwa Wamisri.
Psalms 105:28-30
Mungu alifanya nini kwa maji na samaki wa Misri?
Mungu aligeuza maji ya Misri kuwa damu na kuua samaki wao.
Psalms 105:31-33
Mungu alituma nini pamoja na mvua ya mawe na mvua huko Misri?
Mungu alituma mvua ya mawe na mvua, kwa radi na ngurumo, katika nchi yao.
Psalms 105:34-36
Kundi gani la watu Mungu aliwaua Misri?
Mungu aliwaua kila mzaliwa wa kwanza katika nchi yao, malimbuko ya kwanza ya nguvu yao.
Psalms 105:37-39
Kwa nini Misri ilifurahi Israeli walipoondoka?
Misri ilifurahi Waisraeli walipoondoka, kwa maana Wamisri waliwaogopa.
Psalms 105:40-42
Aina gani ya chakula Mungu aliwatosheleza Waisraeli?
Mungu aliwatosheleza kwa mkate kutoka mbinguni.
Ahadi gani takatifu Mungu alikumbuka kuhusu Waisraeli?
Mungu alikumbuka ahadi yake takatifu ambayo alifanya kwa Abrahamu mtumishi wake.
Psalms 105:43-45
Mungu aliruhusu watu wake kumiliki kitu gani?
Watu wake walimiliki utajiri wa watu.
Psalms 106
Psalms 106:1-2
Mwandishi nini kinadumu milele?
Agano aminifu la Yahwe linadumu milele.
Psalms 106:3-5
Ni wakati gani mwandishi anamwomba Yahwe amkumbuke akilini?
Anamuuliza Yahwe kukumbuka akilini pale Yahwe atakapoonyesha fadhila kwa watu wake.
Nini kitasababisha mwandishi kushangilia?
Atashangilia atakapoona mafanikioa ya waliochaguliwa wa Yahwe.
Psalms 106:6-7
Baba wa mwandishi wanajibuje kwa matendo makuu ya Yahwe?
Baba hawakukupokea matendo makuu ya Yahwe huko Misri.
Psalms 106:8-9
Kwa nini Yahwe aliwaokoa mababu wa mwandishi?
Aliwaokoa kwa ajili ya jina lake ili kwamba aweze kufunua uwezo wake.
Psalms 106:10-12
Nini kilitokea kwa wapinzani wa Israeli?
Maji yaliwafunika wapinzani wao; hakuna mmoja wao aliyepona.
Psalms 106:13-15
Watu walifanya nini walipopatwa na tamaa isiyotosheka katika nyika?
Walimjaribu Mungu nyikani.
Psalms 106:16-18
Dunia ilifanya nini kwa Dathani na wafuasi wa Abiramu?
Dunia ilifunguka na kuwameza Dathani na kufunika wafuasi wa Abiramu.
Psalms 106:19-21
Watu waliabudu nini Horebu?
Walitengeneza ndama Horebu na kuabudu kiumbe cha kuchonga cha chuma.
Psalms 106:22-25
Kwa nini Mungu hakuagiza uharibifu wa Waisraeli?
Musa, mteule wake, aliingilia kati naye kwatika uvunjaji kugeuza hasira ya Yahwe mbali na kuwaangamiza.
Psalms 106:26-27
Kwa nini Mungu aliapa angefanya atakapoinua mkono wake?
Mungu aliapa kwao ya kwamba angewaruhusu kufa katika jangwa, na kutawanya vizazi vyao katika mataifa.
Psalms 106:28-29
Nini kilitokea kwa Israeli walipochokoza Yahwe mpaka akakasirika?
Pigo likazuka miongoni mwao.
Psalms 106:30-31
Nini kilitokea Finehasi alipoinuka kuingilia kati kwa ajili ya watu?
Finehasi alipoingilia kati, pigo likatulia.
Psalms 106:32-36
Kwa nini Musa alitenda katika maji ya Meriba?
Watu walimchukiza Musa, na akazungumza kwa ukali.
Psalms 106:37-39
Nini kilitokea kwa watu walipochangamana na mataifa na kuabudu sanamu zao?
Sanamu zao zikawa mtego kwao.
Psalms 106:40-43
Nini kilitokea kwa Israeli Yahwe alipokuwa na hasira na wao na kuwakabidhi kwa mataifa?
Yahwe alipowakabidhi, wale ambao waliwachukia na kutawala juu yao.
Psalms 106:44-46
Kwa nini Yahwe alitulia na kuvuta nadhari kwa Israeli kwa ajili ya shiki yao?
Aliweka akilini agano lake na wao na kutulia kwa sababu ya agano lake aminifu.
Psalms 106:47-48
Yahwe anapaswa kukusanya Israeli kutoka kwa mataifa kwa sababu gani?
Anapaswa kuwakusanya ili kwamba waweze kutoa shukrani kwa jina lake takatifu na utukufu katika sifa zake.
Psalms 107
Psalms 107:1-3
Agano la uaminifu la Yahwe linadumu kwa muda gani?
Agano lake aminifu hudumu milele.
Yahwe amekusanya wakombolewa wake kutoka wapi?
Amewakusanya kutoka nchi za kigeni, kutoka mashariki na kutoka magharibi, kutoka kaskazini na kutoka kusini.
Psalms 107:4-7
Yahwe alifanya nini kwa waliokombolewa wake walipomwita katika dhiki yao?
Aliwaokoa katika shida yao.
Psalms 107:8-10
Watu wanapaswa kumsifu Yahwe kwa ajili gani?
Wanapaswa kumsifu yeye kwa ajili ya agano lake aminifu na kwa ajili ya mambo ya ajabu ambayo amefanya kwa ajili ya wanadamu.
Psalms 107:11-13
Kwa nini Yahwe alishusha mioyo ya watu?
Alishusha mioyo yao katika ugumu.
Psalms 107:14-16
Malango ya aina gani na vyuma Yahwe amevunja kwa ajili ya watu wake?
Amevunja malango ya shaba na kukata katikati ya vyuma.
Psalms 107:17-19
Kwa nini watu waliteswa?
Waliteswa kwa sababu ya dhambi zao.
Psalms 107:20-22
Aina gani ya sadaka watu wanapaswa kutoa kwa Yahwe?
Wanapaswa kutoa sadaka za shukrani.
Psalms 107:23-24
Watu waliosafiri juu ya bahari katika merikebu na kufanya biashara ng'ambo za mabli waliona nini kwa Yahwe?
Waliona matendo ya Yahwe na maajabu yake juu ya bahari.
Psalms 107:25-27
Nini kilitokea kwa wanamume mawimbi yalipowafikia juu mbinguni na wakaanguka chini mpaka kwenye vina?
Ujasiri wa wanamume uliyeyuka kwa sababu ya hatari.
Psalms 107:28-30
Nini kilitokea kwa wanamume walipomwita Yahwe katika shida yao?
Aliwatoa katika shida yao na kutuliza dhoruba.
Psalms 107:31-32
Watu wanapaswa kumwinua na kumsifu Yahwe wapi?
Wanapaswa kumwinua katika kusanyiko la watu na kumsifu katika baraza la wazee.
Psalms 107:33-35
Yahwe alifanya nini kwa nchi inayozaa kwa sababu ya uovu wa watu?
Aligeuza nchi inayozaa kuwa sehemu isiyozaa kwa sababu ya uovu wa watu wake.
Psalms 107:36-38
Watu walipanda nini katikia miji yao?
Walipanda mashamba na mashamba ya mizabibu.
Psalms 107:39-40
Nini kilitokea kwa viongozi Yahwe alipomwaga chuki juu yao?
Alisababisha kutangatanga katika nyika ambapo hakuna barabara.
Psalms 107:41-43
Waovu wote watafanya nini pale wanyoofu watakapoona ulinzi wa Yahwe na kushangilia?
Waovu wote watafunga midomo yao.
Mwandishi anamwita nani kutambua mambo haya?
Mwandishi anamwita yeyote mwenye hekima kutambua mambo haya na kufikiria juu ya matendo ya Yahwe na agano la uaminifu.
Psalms 108
Psalms 108:1-2
Daudi anasema ataimba sifa na nini?
Daudi anasema ya kwamba ataimba sifa pia na moyo wake ulioinuliwa.
Psalms 108:3-4
Daudi anasema agano la uaminifu la Yahwe ni kubwa kiasi gani?
Daudi anasema ya kwamba agano aminifu la Yahwe ni kubwa juu ya mbingu.
Psalms 108:5-6
Daudi anaomba utukufu wa Mungu uinuliwe wapi?
Daudi anaomba utukufu wa Mungu uinuliwe juu ya dunia yote.
Psalms 108:7-8
Mungu amezungumza nini kuhusu Efraimu na Yuda?
Mungu alisema ya kuwa Efraimu pia ni kofia yake ya chuma na Yuda ni fimbo yake.
Psalms 108:9-10
Mungu atapigaje kelele kwa sababu ya Filisti?
Mungu atapiga kelele kwa ushindi kwa sababu yaFilisti.
Psalms 108:11-13
Msaada wa nani ambao Daudi anasema ni bure?
Daudi anaomba msaada wa Mungu kwa sababu ya msaada wa mtu ni bure.
Daudi anaelezaje ushindi wake kwa msaada wa Mungu?
Daudi anasema ya kwamba jeshi lake litashinda kwa msaada wa Mungu, kwa sababu Mungu atakanyaga chini maadui wa Daudi.
Psalms 109
Psalms 109:1-3
Daudi anasema ni nani anamshambulia?
Daudi anasema waovu na wadanganyifu wanamshambulia.
Psalms 109:4-5
Waovu wanatoa nini kama jibu la upendo wa Daudi?
Daudi anasema ya kwamba kama jibu la upendo wake wanamtukana.
Psalms 109:6-7
Daudi anaomba nini kifanyike adui yake atakapohukumiwa?
Daudi anaomba ya kwamba adui yake anapohukumiwa, aweze kukutwa na hatia.
Psalms 109:8-10
Ombi la Daudi ni lipi kwa ajili ya watoto wa adui zake?
Daudi anaomba watoto wa adui zake kutangatanga kote na kuomba omba misaada.
Psalms 109:11-13
Daudi anaomba nini kitokee kwa mapatao ya adui zake?
Daudi anaomba wageni kupora kile maadui walichopata.
Kwa nini Daudi anamwomba Yahwe kumtendea wema kwake?
Daudi anamwomba Yahwe Bwana wake kutenda kwa wema na yeye kwa ajili ya jina la Yahwe.
Psalms 109:14-16
Ombi la Daudi ni lipi kutoka kwa Yahwe kwa ajili ya kumbukumbu ya adui yake?
Daudi anaomba ya kwamba Yahwe akate kumbukumbu ya adui zake kutoka duniani.
Kwa nini Daudi anamwomba Yahwe kukata kumbukumbu yao?
Daudi anaomba ya kwamba Yahwe aweze kufanya hivi kwa sababu mtu huyu hakujishughulisha kuonyesha agano la uaminifu lolote.
Psalms 109:17-18
Daudi anaomba nini kwa kuwa adui zake walichukia baraka?
Daudi anasema ya kwamba kwa kuwa adui yake alichukia baraka, ya kwamba baraka yoyote isifike kwake.
Psalms 109:19-20
Daudi anaomba zawadi kwa ajili ya washtaki wake kutoka kwa nani?
Daudi anaomba kwa hili kuwa zawadi ya washtaki wake kutoka kwa Yahwe.
Psalms 109:21-23
Daudi analinganisha kufifia kwake na nini?
Daudi anasema ya kwamba kufifia kwake ni kama kivuli cha jioni.
Psalms 109:24-25
Washtaki wa Daudi wanafanya nini wanapomwona?
Daudi anasema ya kwamba wanapomwona, washatki wake hutikisa vichwa vyao.
Psalms 109:26-27
Daudi anamwomba Yahwe amwokoea na nini?
Daudi anamwomba Yahwe amwokoe kwa agano aminifu la Yahwe.
Psalms 109:28-29
Daudi anaomba nini kutokea pale washataki wake wakimshambulia?
Daudi anaomba ya kwamba washtaki wake wanapomshambulia, waweze kuaibishwa.
Psalms 109:30-31
Daudi anasema nini kitatokea Yahwe atakaposimama katika mkono wa kuume ya mtu mhitaji?
Yahwe atamwokoa mtu mhitaji kutoka kwa wale wanaomhukumu.
Psalms 110
Psalms 110:1
Yahwe anamwomba bwana wa Daudi aketi wapi, na kwa muda gani?
Yahwe anamwomba aketi katika mkono wake wa kuume hadi atakapofanya maadui zake kigoda chake cha mguu.
Psalms 110:2-3
Watu watavaa nini wanapomfuata bwana wa Daudi?
Watamfuata katika mavazi ya matakatifu.
Psalms 110:4
Yahwe ameapa nini na hatabadilika?
Ameapa kwa bwana wa Daudi ya kwamba, "Wewe ni kuhani milele".
Psalms 110:5-6
Bwana wa Daudi atafanya nini kwa wafalme katika siku ya hasira yake?
Atawaua wafalme katika siku ya hasira yake.
Psalms 110:7
Bwana wa Daudi atafanya nini baada ya kunywa katika kijito kando na barabara?
Atainua kichwa chake juu baada ya ushindi.
Psalms 111
Psalms 111:1-3
Mwandishi anasema atatoa shukrani wapi kwa Yahwe kwa moyo wake wote?
Atatoa shukrani kwa Yahwe katika kusanyiko ya wanyoofu, katika kusanyiko lao.
Haki ya Yahwe itadumu kwa muda gani?
Haki yake itadumu milele.
Psalms 111:4-6
Yahwe atakumbuka nini daima?
Ataendelea kukumbuka agano lake.
Yahwe alionyeshaje kazi zake za uwezo wake kwa watu wake?
Alionyesha kazi zake za uwezo kwa watu kwa kuwapa urithi wa mataifa.
Psalms 111:7-9
Maelekezo ya Yahwe yanatakiwa kufuatwaje?
Maelekezo yake yote yanapaswa kushikwa kwa uaminifu na kwa usahihi.
Mwandishi anaelezaje jina la Yahwe?
Mwandishi anasema, "JIna lake ni takatifu na ajabu"
Psalms 111:10
Ni nini mwanzo wa hekima?
Kumheshimu Yahwe ni mwanzo wa hekima.
Wale wanaobeba maagizo ya Yahwe wana nini?
Wale wanaotimiza maagizo yake wana uelewa mzuri.
Psalms 112
Psalms 112:1-2
Nini hutokea kwa uzao wa mtu anayemtii Yahwe na anayefurahia amri zake?
Uzao wake utakuwa na nguvu duniani na utabarikiwa.
Psalms 112:3-5
Nini kiko kwenye nyumba ya mtu anayemtii Yahwe?
Utajiri uko kwenye nyumba yake.
Mwandishi anasema vitu vitaenda vizuri kwa ajili ya nani?
Itaenda vyema kwa mtu anayefanya wema na kukopesha fedha, na anaye fanya mambo yake kwa uaminifu.
Psalms 112:6-7
Mtu mwenye haki anafanya nini badala ya kuogopa habari mbaya?
Haogopi, lakini anaujasiri, akimtumaini Yahwe.
Psalms 112:8-9
Nini hutokea kwa mtauwa anyetoa kwa ukarimu kwa masikini?
Atatukuzwa kwa heshima?
Psalms 112:10
Nini hutokea kwa mtu mwovu anayeona baraka za mtu mwenye haki na kukasirika?
Mtu mwovu atasaga meno na kuyeyuka.
Psalms 113
Psalms 113:1-2
Jina la Yahwe litabarikiwa lini?
Jina lake litabarikiwa sasa na hata milele.
Psalms 113:3-4
Utukufu wa Yahwe unafika wapi?
utukufu wake unafika juu ya anga.
Psalms 113:5-6
Kiko wapi kiti cha Yahwe?
Kiti chake kiko juu, ambapo anatazama chini anga na dunia.
Psalms 113:7-8
Yahwe anamweka maskini na mtu mhitaji aketi wapi anapomwinua?
Yahwe anawaweka waketi na wakuu, na wakuu wa watu wake.
Psalms 113:9
Yahwe anampa nini mwanamke tasa?
Anampa mwanamke tasa kwenye nyumba kiti kama mama mwenye furaha wa watoto.
Psalms 114
Psalms 114:1-2
Yuda na Israeli zilikuwa nini Israeli ilipoondoka Misri?
Yuda palikuwa mahali pake patakatifu, na Israeli ikawa ufalme wake.
Psalms 114:3-4
Milima na vilima ilifanya nini Waisraeli walipokuja katika nchi?
Milima ilirukaruka kama kondoo madume, na vilima vilirukaruka kama wanakondoo.
Psalms 114:5-7
Mwandishi anasema kwamba dunia inapaswa kutetemeka mbele ya nani?
Dunia inapaswa kutetemeaka mbele ya Bwana, katika uwepo wa Mungu wa Yakobo.
Psalms 114:8
Mwandishi anasema Yahwe aligeuza jiwe na mwamba mgumu kuwa nini?
Aligeuza jiwe kuwa bwawa la maji, na mwamba mgumu kuwa chemchemi ya maji.
Psalms 115
Psalms 115:1-2
Daudi anaomba Yahwe alete heshima kwa jina la Yahwe kwa sababu gani?
Anamwomba Yahwe alete heshima kwa jina lake kwa ajili ya uaminifu wake wa agano na kwa ajili ya uaminifu wake.
Psalms 115:3-4
Daudi anasema sanamu za mataifa ni nini?
Anasema sanamu zao ni fedha na dhahabu, kazi ya mikono ya watu.
Psalms 115:5-8
Sanamu haziwezi kufanya nini?
Haziwezi kuzungumza, au kuona, au kusikia, au kunusa.
Psalms 115:9-11
Kwa nini kila mtu anapaswa kumtumaini Yahwe?
Wanapaswa kumtuamaini Yahwe kwa sababu ni msaada wao na ngao yao.
Psalms 115:12-14
Mtu anapaswa kuwa na umri gani kabala Yahwe hajambariki?
Yahwe atawabariki wale wanaomheshimu, wadogo kwa wakubwa.
Psalms 115:15-16
Mbingu na dunia ni mali ya nani?
Mbingu ni za Yahwe; lakini dunia amewapa binadamu.
Psalms 115:17-18
Daudi anasema watu watambariki Yahwe kwa muda gani?
Anasema watambariki Yahwe sasa na hata milele.
Psalms 116
Psalms 116:1-2
Mwandishi anasema anampenda Yahwe kwa sababu gani?
Anampenda Yahwe kwa sababu Yahwe husikia sauti yake na maombi yake kwa ajili ya huruma.
Psalms 116:3-4
Mwandishi alihisi nini alipozungukwa na kamba za mauti na kukabiliana na mitego ya kuzimu?
Alihisi uchungu na huzuni.
Psalms 116:5-6
Yahwe anamlinda nani?
Yahwe anamlinda asiye na hila.
Psalms 116:7-8
Nafsi ya mwandishi iliokolewa kutoka wapi?
Yahwe aliweka huru nafsi yake na mauti.
Psalms 116:9-11
Mwandishi anasema atamtumikia wapi Yahwe?
Atamtumikia Yahwe katika nchi ya walio hai.
Psalms 116:12-15
Mwandishi anasema atatimizia wapi viapo vyake kwa Yahwe?
Atatimiza viapo vyake katika uwepo wa watu wake wote.
Ni nini cha thamani machoni pa Yahwe?
Ni ya thamani machoni pa Yahwe vifo vya watakatifu wake.
Psalms 116:16-17
Mwandishi anasema atatoa nini kwa Yahwe kwa kutoa vifungo vyake?
Anasema atatoa sadaka za shukrani kwake.
Psalms 116:18-19
Mwandishi atatimiza viapo vyake kwa Mungu mbele ya uwepo wa nani?
Atatimiza viapo vyake katika uwepo wa watu wote wa Yahwe.
Psalms 117
Psalms 117:1-2
Mwandishi anamwita nani kumsifu Yahwe?
Anayaita mataifa yote na watu wote kumsifu Yahwe.
Nini ni kikuu kwa watu wake?
Uaminifu wa agano wa Yahwe ni mkuu kwa watu wake.
Uaminifu wa Yahwe unadamu kwa muda gani?
Uaminifu wa Yahwe unadumu milele.
Psalms 118
Psalms 118:1-4
Ni sababu gani mbili zmbazo mwandishi anasema watu wanapaswa kumpa shukrani Yahwe?
Wanapaswa kumpa Yahwe shukrani kwa sababu ni mwema na kwa sababu uaminifu wake wa agano unadumu milele.
Psalms 118:5-7
Yahwe aliitikiaje mwandishi alipomwita?
Yahwe alimjibu na kumweka huru.
Psalms 118:8-9
Mwandishi anasema ni bora kwenda kwenye kivuli cha Yahwe kuliko nini?
Ni bora kuwa kwenye kivuli cha Yahwe kuliko kuweka matumaini katika mtu.
Psalms 118:10-14
Mwandishi anasema mataifa yote yalikuwa kama nini yalipomzunguka?
Alisema mataifa yote walimzunguka kama nyuki.
Psalms 118:15-16
Ni aina gani ya kelele inasikika kwenye hema za wenye haki?
Kelele ya furaha inasikika kwenye hema za wenye haki.
Psalms 118:17-18
Yahwe hakufanya nini alipomwadhibu mawndishi kwa ukali?
Yahwe hakumkabidhi kwa mauti.
Psalms 118:19-21
Mwandishi atafanya nini Yahwe akifungua malango ya haki kwake?
Mwandishi ataingia malango ya haki na kumpa shukrani Yahwe.
Psalms 118:22-23
Nini kimetokea kwa jiwe ambalo wajenzi walilolikataa?
Jiwe mabalo wajenzi walilolikataa limekuwa jiwe la pembeni.
Psalms 118:24-25
Watu watafanya nini katika siku ambayo Yahwe ametenda?
Watashangilia na kuwa na furaha ndani yake.
Psalms 118:26-29
Mwandishi anasema watu wanapaswa kufanya nini na sadaka?
Wanapaswa kuifunga sadaka kwa kamba kwenye pembe za madhabahu.
Mwandishi anasema atafanya nini kwa sababu Yahwe ni Mungu wake?
Atampa Yahwe shukrani na kumtukuza.
Psalms 119
Psalms 119:1-4
Mwandishi anasema watu wanapaswa kumtafuta Yahwe vikoje?
Wanapaswa kumtafuta Yahwe kwa mioyo yao yote.
Psalms 119:5-6
Mwandishi anasema nini kitatokea kama atafuata kwa thabiti sheria za Yahwe?
Anasema hataaibika akifikiria juu ya amri zote za Yahwe.
Psalms 119:7-8
Mwandishi anampa Yahwe shukrani kwa kutumia nini?
Anatoa shukrana kwa moyo wa unyofu.
Psalms 119:9-10
Mwandishi anasema kijana anawezaje kuweka njia yake iwe safi?
Kijana anaweza kuiweka njia yake iwe safi kwa kutii neno la Yahwe.
Psalms 119:11-12
Kwa nini mwandishi amelitunza neno la Yahwe moyoni mwake?
Amelitunza neno la Yahwe moyoni mwake ili asitende dhambi dhidi ya Yahwe.
Psalms 119:13-14
Mwandishi anafurahia nini zaidi ya utajiri wote?
Anafurahi katika njia ya amri za agano za Yahwe zaidi ya utajiri wote.
Psalms 119:15-16
Mwandishi atafanya nini na maagizo ya Yahwe?
Atatafakari juu ya maagizo ya Yahwe.
Psalms 119:17-18
Mwandishi ataonaje mambo ya ajabu katika sheria ya Yahwe?
Ataona mambo ya ajabu katika sheria ya Yahwe pale Yahwe atakapofungua macho yake.
Psalms 119:19-20
Nini kinatokea kwa nafsi ya mwandishi anapokuwa na shauku la kujua sheria za haki za Yahwe?
Nafsi yake inapondeka kwa shauku ya kujua sheria za haki za Yahwe.
Psalms 119:21-22
Mwandishi anasema nani amelaaniwa na kinazurura kutoka kwenye amri za Yahwe?
Wenye kiburi wamelaaniwa na wanazurura kutoka kwenye amri za Yahwe.
Psalms 119:23-24
Mwandishi anafanya nini ingawa watawala wanapanga njama na kumkashifu?
Anatafakari juu ya sheria za Yahwe.
Psalms 119:25-26
Mwandishi anamwomba Yahwe ampe uhai kwa njia ipi?
Anamwomba Yahwe kumpa uhai kwa neno la Yahwe.
Psalms 119:27-28
Kwa nini mwandishi anataka kuelewa njia za maagizo ya Yahwe?
Anataka kuelewa njia za maagizo ya Yahwe ili aweza kutafakari juu ya mafunzo ya ajabu ya Yahwe.
Psalms 119:29-34
Mwandishi anamwomba Yahwe amgeuza kutoka njia gani?
Anamwomba Yahwe amgeuza kutoka njia ya udanganyifu.
Psalms 119:35-36
Mwandishi anamwomba Yahwe auongoze wapi moyo wake?
Anamwomba Yahwe kuongoza moyo wake kuelekea amri za agano za Yahwe na mbali na ongezeko lisilo la haki.
Psalms 119:37-42
Mwandishi anamwomba Yahwe ageuze macho yake kutoka wapi?
Anamwomba Yahwe kugeuza macho yake kutoka kuangalia vitu visivyofaa.
Psalms 119:43-44
Mwandishi anamwomba Yahwe asichukue nini kutoka mdomoni mwake?
Anamwomab Yahwe asichukue neno la kweli kutoka mdomoni mwake.
Psalms 119:45-46
Kwa nini mwandishi anasema atatembea kwa usalama?
Atatembea kwa usalama kwa sababu anatafuta maagizo ya Yahwe.
Psalms 119:47-48
Mwandishi anasema anapenda nini sana?
Anapenda sana amri za Yahwe.
Psalms 119:49-50
Mwandishi anamwomba Yahwe akumbuke nini?
Anamwomba Yahwe akumbuke ahadi yake kwa mtumishi wake.
Psalms 119:51-52
Ingwa wenye kiburi wamemdhihaki, mwandishi hajafanya nini?
Mwandishi hajageuka kutoka kwenye sheria ya Yahwe.
Psalms 119:53-56
Mwandishi anasema sheria za Yahwe zimekuwa nyimbo zake katika aina gani ya nyumba?
Sheria za Yahwe zimekuwa nyimbo za mwandishi kwenye nyumba anayoishi kwa muda.
Psalms 119:57-60
Mwandishi aliomba fadhila kwa Yahwe kwa kutumia nini?
Aliomba kwa dhati fadhila za Yahwe kwa moyo wake wote.
Psalms 119:61-62
Mwandishi hajasahau nini wakati kamba za mwovu zilivyo mnasa?
Hajasahau sheria ya Yahwe.
Psalms 119:63-64
Mwandishi ana urafiki na aina gani ya watu?
Ni rafiki wa wale wote wanaomheshimu Yahwe, na wale wote wanaofuata maagizo yake.
Psalms 119:65-68
Kwa nini mwandishi anamwomba Yahwe kumfundisha utambuzi sahihi na uelewa?
Anamwomba Yahwe kumfundisha utambuzi sahihi na uelewa kwa sababu ameamini katika amri za Yahwe.
Psalms 119:69-70
Mwandishi alifanya nini wenye majivuno walipompaka uongo?
Alitunza maagizo ya Yahwe kwa moyo wake wote.
Psalms 119:71-72
Kwa nini mwandishi anasema kuwa ni vyema ameteseka?
Ilikuwa vyema kwake kuteseka ili ajifunze sheria za Yahwe.
Mwandishi anasema maagizo kutoka katika mdomo wa Yahwe ni ya thamani zaidi ya nini?
Maagizo kutoka katika mdomo wa Yahwe ni ya thamani zaidi kwake kuliko vipande elfu vya dhahabu na fedha.
Psalms 119:73-74
Kwa nini mwandishi anasema kwamba wale wanomheshimu Yahwe watafurahi watakapomwona mwandishi?
Watafurahi watakapomwona mwandishi kwa sababu amepata matumaini katika neno la Yahwe.
Psalms 119:75-78
Mwandishi anasema Yahwe alimtesaje?
Yahwe alimtesa kwa uaminifu.
Psalms 119:79-80
Mwandishi anaomba kwamba moyo wake usiwe na lawama kwa sheria za Yahwe ili kwamba nini kisitokee?
Anataka moyo wake usiwe na lawama kwa sheria za Yahwe ili kwamba mwandishi asiaibishwe.
Psalms 119:81-84
Mancho ya mwandishi yanashauku ya kuona nini?
Macho yake yanashauku ya kuona ahadi ya Yahwe.
Psalms 119:85-86
Wenye kiburi amekaidije sheria za Yahwe?
Wenye kiburi wamechimba mashimo kwa ajili ya mwandishi, wakikaidi sheria za Yahwe.
Psalms 119:87-88
Mwandishi anamwomba Yahwe kumweka hai ili mwandishi afanye nini?
Anamwomba Yahwe kumweka hai ili kwamba atunze amri za agano ambazo Yahwe amezungumza.
Psalms 119:89-92
Uaminifu wa Yahwe unadumu kwa muda gani?
Uaminifu wa Yahwe unadumu katika vizazi vyote.
Psalms 119:93-94
Kwa nini mwandishi hatasahau maagizo ya Yahwe?
Hatasahau maagizo ya Yahwe, kwa kupitia hayo amewaweka hai.
Psalms 119:95-98
Ni kitu gani ambacho hakina mipaka?
Amri za Yahwe ni pana, zaidi ya mipaka.
Psalms 119:99-102
Kwa nini mwandishi anasema kuwa anauelewa zaidi ya walimu wake wote?
Anauelewa zaidi ya walimu wake wote, kwa kuwa huwa anatafakari amri za agano za Yahwe.
Psalms 119:103-104
Mwandishi anasema maneno ya Yahwe ni matamu zaidi ya nini?
Maneno ya Yahwe ni matamu zaidi ya asali katika mdomo wa mwandishi.
Psalms 119:105-110
Mwandishi ameapa nini na kuthibitisha kitu gani?
Ameapa na kuthibitisha kuwa atafuata amri za Yahwe.
Psalms 119:111-112
Mwandishi anadai nini kama urithi wake milele na furaha ya moyo wake?
Anadai amri za agano za Yahwe kama urithi wake milele, kwa kuwa ni furaha ya moyo wake.
Psalms 119:113-116
Kwa kuwa Yahwe ni sehemu yake ya kujificha na ngao yake, mwandishi anasubiri nini?
Mwandishi anasubiri neno la Yahwe.
Psalms 119:117-118
Kwa nini Yahwe anawakataa wale wote wanaopotoka kutoka kwenye sheria zake?
Anawakataa wale wote wanaopotoka sheria zake, kwa kuwa watu hao ni waongo na sio wa kutegemea.
Psalms 119:119-122
Mwili wa mwandishi unaogopa nini hadi kutetemeka?
Mwili wake unatetemeka kwa kumcha Yahwe.
Psalms 119:123-124
Mwandishi anasubiri nini wakati macho yake yanachoka?
Anasubiri wokovu wa Yahwe na kwa ajili ya neno lake la haki.
Psalms 119:125-126
Kwa nini mwandishi anamwomba Yahwe uelewa?
Anaomba uelewa ili kwamba ajue amri za agano za Yahwe.
Psalms 119:127-128
Mwandishi anachukia nini?
Anachukia kila njia ya uongo.
Psalms 119:129-130
Kufunua kwa maneno ya Yahwe hutoa nini?
Kufunua kwa maneno ya Yahwe hutoa mwanga, na uelewa kwa wale ambao ni wajinga.
Psalms 119:131-132
Yahwe hufanya nini kwa wale wanaolipenda jina lake?
Yahwe huwa anawageukia na kuwaonea huruma.
Psalms 119:133-134
Kwa nini mwandishi anamwomba Yahwe kumkomboa kutoka katika ukandamizaji wa wanadamu?
Anamwomba Yahwe kumkomboa ili kwamba afuate maagizo ya Yahwe.
Psalms 119:135-136
Kwa nini mikondo ya machozi inatiririka kutoka kwenye macho ya mwandishi?
Mikondo ya machozi inatiririka machoni pake kwa sababu watu hawafuati sheria ya Yahwe.
Psalms 119:137-140
Yahwe ametoa amri za agano kwa njia gani?
Yahwe amewapa amri za agano kwa haki na uaminifu.
Psalms 119:141-142
Mwandishi hachukii nini licha ya ukweli kwamba hana maana na anachukiwa?
Hasahau maagizo ya Yahwe.
Psalms 119:143-144
Ni amri gani za Yahwe kwa mwandishi, ingawa dhiki na uchungu zimempata?
Ingawa dhiki na uchungu zimempata, amri za Yahwe bado ni furaha yake.
Psalms 119:145-150
Mwandishi atafanya nini kama Yahwe akimwokoa?
Atafuata amri za agano za Yahwe.
Psalms 119:151-152
Mwandishi alijifunza nini zamani kutoka kwa amri za agano za Yahwe?
Alijifunza kuwa Yahwe aliweka amri zake za agano sehemu yake milele.
Psalms 119:153-154
Kwa nini mwandishi anasema kuwa Yahwe anapaswa kutazama mateso yake na kumsaidia?
Yahwe anapaswa kumsaidia kwa sababu mwandishi hasahau sheria ya Yahwe.
Psalms 119:155-156
Kwa nini wokovu uko mbali na waovu?
Wokovu uko mbali na waovu, kwa kuwa hawapendi sheria za Yahwe.
Psalms 119:157-158
Kwa nini mwandishi anawatazama waongo kwa maudhiu?
Anawatazama waongo kwa maudhi kwa sababu hawazingatii neno la Yahwe.
Psalms 119:159-160
Kila amri ya yahwe inadumu muda gani?
Kila amri ya Yahwe hudumu milele.
Psalms 119:161-162
Mwandishi anaogopa nini wakati wakuu wanamtesa bila sababu?
Anaogopa kukaidi neno la Yahwe.
Psalms 119:163-166
Mwandishi anamsifu Yahwe mara ngapi kwa sababu ya amri zake za haki?
Anamsifu Yahwe mara saba kwa siku.
Psalms 119:167-168
Kwa nini mwandishi anatunza maagizo ya Yahwe na amri zake takatifu?
Anatunza maagizo ya Yahwe na amri zake takatifu kwa sababu Yahwe anafahamu kila kitu amabacho mwandishi hufanya.
Psalms 119:169-170
Yahwe aliahidi kufanya nini katika neno lake?
Yahwe aliahidi kwenye neno lake kumsaidia mwandishi wakati ombi lake likija mbele ya Yahwe.
Psalms 119:171-174
Kwa nini mwandishi anamwomba Yahwe kuruhu ulimi wake kuimba juu ya neno la Yahwe?
Anataka ulimi wake kuimba juu ya neno la Yahwe kwa sababu amri za Yahwe ziko sawa.
Psalms 119:175-176
Mwandishi anamwomba Yahwe kufanya nini wakati anapopotea kama kondoo mpotevu?
Anamwomba Yahwe kumtafuta mtumishi wake, kwa kuwa hajasahau amri za Yahwe.
Psalms 120
Psalms 120:1-2
Yahwe alifanya nini mwandishi alipomwita katika dhiki?
Mwandishi anasema kwamba Yahwe alimjibu.
Mwandishi anamwomba Yahwe kufanya nini kwa ajili ya nfasi yake?
Mwandishi anamwomba Yahwe kuokoa nafsi yake kutoka kwa wale wanaodanganya kwa ndimi zao.
Psalms 120:3-4
Mwandishi anawaambia nini watu ambacho Yahwe atawafanya wale wenye ulimi wa udanganyifu?
Yahwe atawapiga na mishale iliyochongeka na vichwa vya mishale vilivyopashwa na makaa ya moto kutoka kwenye mbao za mti wa ufagio.
Psalms 120:5-7
Mwandishi anasema ameishi wapi kwa muda mfupi na aliwahi kuishi wapi?
Mwandishi anasema aliishi kwa muda mfupi Mesheki na aliwahi kuishi miongoni mwa hema za Kedari.
Mwandishi anasema nini kuhusu amani?
Mwandishi anasema kuwa ameishi kwa muda mrefu sana na wale wanaochukia amani na yeye yuko kwa ajili ya amani.
Psalms 121
Psalms 121:1-2
Mwandishi atainulia nini macho yake?
Mwandishi anasema atainua macho yake milimani.
Mwandishi anasema msaada wake unatoka wapi?
Mwandishi anasema msaada wake unatoka kwa Yahwe.
Psalms 121:3-4
Yahwe atamsaidiaje mwandishi?
Yahwe hataruhu mguu wa mwandishi kuteleza na atamlinda.
Mwandishi anasema kuwa mlinzi wa Israeli huwa hafanyi nini?
Mlinzi wa Israeli huwa hasinzii wala kulala.
Ni nani mlinzi na kivuli cha Israeli?
Yahwe ni mlinzi wa Israeli na kivuli mkono wao wa kuume.
Psalms 121:5-6
Nini hakitaidhuru Israeli?
Jua halitawadhuru mchana wala mwezi usiku.
Psalms 121:7-8
Nani atawalinda Israeli dhidi ya uovu wote, kutunza nafsi zao, na kuwalinda katika yote wanayofanya?
Yahwe atawalinda dhidi ya uovu wote, atatunza nafsi zao na kuwalinda katika yote wanayofanya.
Psalms 122
Psalms 122:1-3
Nini kilisemwa kwa Daudi kumfurahisha?
"Twende kwenye nyumba ya Yahwe" ndicho kilichosemwa kwa Daudi.
Miguu ya watu imesimama wapi?
Miguu yao imesimama ndani ya malango ya Yerusalemu.
Yerusalemu ilijengwa wapi?
Yerusalemu ilijengwa kama mji uliounganishwa pamoja.
Psalms 122:4-5
Kwa nini makabila yalikwenda juu Yerusalemu?
Makabila yanakwenda Yerusalemu kutoa shukrani kwa jina la Yahwe.
Kwa nini viongozi wanaketi kwenye viti vya enzi Yerusalemu?
Viongozi wanaketi kwenye viti vya enzi kwa ajili ya hukumu ya nyumba ya Daudi.
Psalms 122:6-7
Nini kitatokea kwa wale wanaoipenda Yerusalemu?
Wale wanaoipenda Yerusalemu watafanikiwa.
Daudi anataka nini iwe ndani ya kuta na minara ya Yerusalemu?
Anataka iwepo amani ndani ya kuta na mafanikio ndani ya minara.
Psalms 122:8-9
Daudi atasema kwa ajili ya nani, "Na iwepo amani ndani yako."?
Daudi anasema hivi kwa ajili ya ndugu zake na wenzake.
Kwa nini Daudi anasema ataomba kwa ajili ya wema wa Yerusalemu?
Ataomba kwa ajili ya wema wa Yerusalemu kwa ajili ya nyumba ya Yahwe.
Psalms 123
Psalms 123:1-2
Mwandishi anainua macho yake kwa nani?
Mwandishi anainua jicho lake kwa yule aliyetawazwa mbinguni.
Macho ya watu yanamwangalia Yahwe Mungu wao kwa muda gani?
Wanamwangalia Yahwe hadi awaonee huruma.
Psalms 123:3-4
Kwa nini watu wanamowmba Yahwe awahurumie?
Watu wamejaa aibu, wameshiba sana dhihaki wa wenye jeuri na chuki ya wenye kiburi.
Psalms 124
Psalms 124:1-3
Nini kingetokea kama yahwe asingekuwa upande wa Israeli watu walipoinuka dhidi yao?
Kama Yahwe asingekuwa upande wa Israeli, watu walioinuka dhidi yao wangewameza wakiwa hai.
Psalms 124:4-5
Maji, mvo na maji yanayotiririka kwa kasi yangeifanya nini Israeli?
Maji yangewabeba, mvo ungewalemea, na maje ya kasi yangewazamisha.
Psalms 124:6-7
Watu walifanya nini baada ya Yahwe kutowaruhusu wararuriwe na meno ya adui zao?
Watu walimbariki Yahwe.
Kutoroka kwa Waisraeli kukoje?
Kutoroka kwao ni kama ndege anayetoka kwenye mtego wa mwindaji wa ndege.
Psalms 124:8
Daudi anasema msaada wa Waisraeli unatoka wapi?
Msaada wao unatoka kwa Yahwe aliyeumba mbingu na dunia.
Psalms 125
Psalms 125:1-3
Wakoje wale wanaomtumaini Yahwe?
Wako kama mlima Sayuni, hawatikisiki na hudumu milele.
Mwandishi anafananisha na nini jinsi Yahwe anavyowazunguka watu wake?
Mwandishi anafananisha jinsi Yahwe anavyowazunguka watu wake na milima inayoizunguka Yerusalemu, sasa na milele.
Nini hakipaswi kutawala katika nchi ya wenye haki?
Fimbo ya uovu haitakiwa kutawala katika nchi ya wenye haki.
Psalms 125:4-5
Mwandishi anaomba Yahwe amtendee wema nani?
Anaomba kwamba Yahwe afanye wema kwa wale ambao ni wanyofu mioyoni mwao.
Nini kitatokea kwa wale ambao wanageukia njia zao zilizojikunja?
Yahwe atawaongoza na watenda maovu.
Mwandishi anataka nini kiwe juu ya Israeli?
Mwandishi anataka amani iwe juu ya Israeli.
Psalms 126
Psalms 126:1
Ilikuaje Yahwe aliporejesha ustawi kwa Sayuni?
Ilionekana kama wale wanaoota.
Psalms 126:2-3
Nini kiliijaza midomo ya watu Yahwe aliporejesha ustawi kwa Sayuni?
Midomo yao ilijazwa na kicheko na ndimi zetu na kuimba.
Psalms 126:4-6
Mwandishi anamwomba nin Yahwe?
Mwandishi anaomba kwamba Yahwe arejeshe bahati yao.
Nini kitatokea kwa wale wanaopanda kwa machozi?
Watavuna na kelele za furaha.
Nini kitatokea kwa mtu ambaye anaenda akilia na kubeba mbegu za kupanda?
Atarudi kwa kelele za furaha, akileta miganda yake.
Psalms 127
Psalms 127:1-2
Nini hutokea kama Yahwe asipojenga nyumba na asipoulinda mji?
Yahwe asipojenga nyumba wale wanaoijenga wanafanya kazi bure na kama Yahwe asipoulinda mji walinzi wanalinda bure.
Yahwe humpa nini mpendwa wake?
Yahwe humpa mpendwa wake usingizi.
Psalms 127:3-5
Ni nini urithi na thawabu kutoka kwa Yahwe?
Watoto ni urithi na matunda ya tumbo ni thawabu kutoka kwa Yahwe.
Watoto wa ujana wa mtu wako kama nini?
Watoto ni kama mishale mkononi mwa shujaa.
Mtu aliyebarikiwa, mwenye podo lililojaa watoto, hataaibishwa lini?
Hataaibishwa atakapokutana na adui zake katika lango.
Psalms 128
Psalms 128:1-2
NIni hutokea kwa wale wanaomheshimu Yahwe na kutembea katika njia zake?
Kila mtu anayemheshimu Yahwe na kutembea katika njia zake amebarikiwa.
Mwandishi anasema nini kitatokea kwa mtu anayefurahia kile ambacho mikono yake imeleta?
Mtu huyo atabarikiwa na kufanikiwa.
Psalms 128:3-6
Mwandishi anasema mke wa mtu aliyebarikiwa ni kama nini?
Ni kama mzabibu weney matunda.
Mwandishi anasema watoto wa mtu aliyebarikiwa watakuwa kama nini?
Watoto wake watakuwa kama mmea wa mizeituni.
Nini kitatokea kwa mtu anyemheshimu Yahwe?
Mtu anayemheshimu Yahwe atabarikiwa.
Mwandishi anamwomba Yahwe kufanya nini kwa ajili ya mtu aliyebarikiwa kutoka Sayuni?
Mwandishi anaomba kwamba mtu kutoka Sayuni aone mafanikio ya Yerusalemu siku zote za maisha yake na kwamba aone watoto wa watoto wake.
Psalms 129
Psalms 129:1-3
Israeli imeshambuliwa kwa muda gani na haijashindwa?
Israeli ilikuwa ikishambuliwa na kutoshindwa tangu ujana wake.
Wakulima walifanya nini mgongoni mwa Israeli?
Wakulima walilima kwenye mgongo wa Israeli na kufanya mifuo yake kuwa mirefu.
Psalms 129:4-5
Yahwe mwenye haki ameifanyia nini Israel?
Yahwe amekataa kamba za waovu.
Mwandishi anataka nini kitokee kwa wale wanaochukia Sayuni?
Anawataka waaibishwe na kugeuzwa.
Psalms 129:6-8
Mwandishi hataki wale wanaopita waseme nini?
Hataki waseme, "Baraka za Yahwe ziwe juu yako; tunakubariki katika jina la Yahwe."
Psalms 130
Psalms 130:1-2
Mwandishi analia nini kwa Yahwe?
Mwandishi analia kwa Bwana kusikia sauti yake na kuwa msikivu kwa maombi yake.
Psalms 130:3-4
Kwa nini mwandishi anasema kwamba anapaswa kuheshimiwa sana?
Yahwe anapaswa kuheshimiwa sana kwa sababu kuna msamaha kwake.
Psalms 130:5-6
Nafsi ya mwandishi inamsubiri na kumtumaini nani?
Nafsi yake inamsubir Yahwe na inatumaini katika neno lake.
Psalms 130:7-8
Kwa nini mwandishi anaiambia Israeli kumtumaini Yahwe?
Yahwe ana huruma, yuko tayari kusamehe, na ataikomboa israeli kutoka katika dhambi zake zote.
Psalms 131
Psalms 131:1
Daudi anaelezeaje moyo wake na macho?
Moyo wake hauna kiburi na macho yake hayana maringo.
Psalms 131:2-3
Nafsi ya Daudi ni kama nini?
Nafsi yake imetulia na iko kimya kama mtoto aliyeachishwa maziwa.
Daudi anawaambia Israeli wakati gani kumtumaini Yahwe?
Anawaambia kumtumaini Yahwe sasa na milele.
Psalms 132
Psalms 132:1-2
Mwandishi alimwomba Yahwe kukumbuka nini?
Alimwomba Yahwe kukumbuka mateso ya yake, jinsi alivyoapa kwa Yahwe, na jinsi alivyoapa kwa Hodari wa Yakobo.
Psalms 132:3-5
Daudi aliapa kuwa hataingia kwenye nyumba yake wala kulala hadi afanye nini?
Alisema hatalala hadi apate sehemu kwa ajili ya Yahwe, hema takatifu kwa ajili ya Hodari wa Yakobo.
Psalms 132:6-8
Watu watakwenda wapi na watafanya nini watakapofika huko?
Watakwenda katika hema takatifu la Mungu na kuabudu katika kiti chake cha kuwekea miguu.
Psalms 132:9-10
Makuhani wanaweza kuvaaje na nani anaweza kupiga kelele ya furaha?
Makuhani wanaweza kuvikwa na uadilifu na waaminifu wa Mungu wanaweza kupiga kelele ya furaha.
Waaminifu hawapaswi kumgeuka nani?
Hawapaswi kumgeuka mfalme wao aliyetiwa mafuta.
Psalms 132:11-12
Yahwe aliapa kiapo gani kwa Daudi?
Yahwe aliapa kuwa mwaminifu kwa Daudi.
Psalms 132:13-14
Mwandishi anatamani kupumzika wapi na kuishi milele?
Anatamani kupumzika na kuishi katika Sayuni iliyochaguliwa na Yahwe.
Psalms 132:15-16
Yahwe ataifanyia nini Sayuni?
Ataibariki sana, atawaridhisha masikini wake kwa mkate, na kuwavika makuhani wake na wokovu.
Psalms 132:17-18
Yahwe atamvika nani na aibu?
Atawavika adui zake na aibu.
Psalms 133
Psalms 133:1
Daudi anasema nini kuhusu ndugu?
Anasema ni vyema na kupendeza kwa wao kubaki pamoja kwa umoja.
Psalms 133:2-3
Daudi anasema umoja wa ndugu ni kama nini?
Ni kama mafuta ya thamani yaliyotiririka chini ya kichwa, ndevu, na mavazi ya Haruni. Pia ni kama umande wa Hermoni, ambao unakuja chini juu ya milima ya Sayuni.
Yahwe aliamuru wapi baraka ya maisha milele?
Aliamuru maisha milele juu ya milima ya Sayuni.
Psalms 134
Psalms 134:1-2
Watumishi wote wa Yahwe wanapaswa kufanya nini?
Wanapaswa kuja, kumbariki Yahwe, na kuinua mikono yao kwenye sehemu takatifu.
Psalms 134:3
Yahwe, aliyeumba mbingu na nchi, atawabariki wapi watumishi wake?
Atawabariki kutoka Sayuni.
Psalms 135
Psalms 135:1-2
Nani anapaswa kumsifu Yahwe?
Watumishi wa Yahwe, wale wanaosimama katika nyumba ya Yahwe, na wale wa barazani wanapaswa kumsifu Yahwe.
Psalms 135:3-4
Kwa nini watumishi wa Yahwe wanapaswa kumsifu na kumwimbia?
Wanapaswa kumsifu Yahwe kwa kuwa ni mwema, na wanapaswa kuimba kuwa ni jambo la kupendeza kufanya.
Psalms 135:5-6
Mwandishi anajua nini kumhusu Yahwe?
Anajua kuwa Yahwe ni mkuu, yuko juu ya miungu yote, na chochote ambacho Yahwe anatamani hufanya mbinguni, duniani na baharini.
Psalms 135:7
Yahwe anafanya matendo gani kuonesha ukuu wake?
Yahwe huleta mawingu, hufanya radi kuambatana na mvua, na huleta upepo kutoka katika ghala lake.
Psalms 135:8-11
Yahwe aliwafanya nini Wamisri?
Aliwaua wazaliwa wa kwanza wa binadamu na wanyama wa Misri na alituma ishara na maajabu dhidi ya Farao na watumishi wake.
Psalms 135:12-13
Yahwe alifanya nini na nchi ya wageni ambayo Waisraeli walivamia?
Aliwapa watu wake wa Israeli nchi kama urithi.
Psalms 135:14-18
Sanamu za mataifa zikoje?
Zimetengenezwa kwa fedha na dhahabu, zina midomo, macho, na masikio lakini hazizungumzi, hazioni, hazisikii, wala kupumua.
Nani alitengeneza sanamu za mataifa?
Watu walio kama wao na wanaowatumaini walizitengeneza.
Psalms 135:19-21
Nani anapaswa kumbariki Yahwe?
Uzao wa Israeli, Haruni, Lawi, na wale wanaomsheshimu Yahwe wanapaswa kumbariki.
Psalms 136
Psalms 136:1-3
Kwa niniwatu wanapaswa kumpa Yahwe shukrani?
Wanapaswa kumpa shukrani kwa sababu ni mwema, na uaminifu wake wa agano hudumu milele.
Psalms 136:4-9
Yahwe hufanya nini ambacho hakuna mwingine anayeweza?
Yahw pekee hufanya mambo ya ajabu"
Psalms 136:10-12
Yahwe alifanya nin kwa wazaliwa wa kwanza wa Misri?
Aliwaua wazaliwa wa kwanza wa Misri.
Psalms 136:13-15
Yahwe aliwafanyia nini Waisraeli alipogawanya bahari ya Shamu?
Aliwafanya Waisraeli kupita katikati ya bahari ya Shamu.
Psalms 136:16-20
Yahwe alikuwaje mwaminifu kwa watu wake?
Aliwaongoza watu wake nyikani.
Psalms 136:21-23
Yahwe alifanya nini na nchi ya wafalme wakuu?
Alimpa nchi yao kama urithi kwa Israeli mtumishi wake.
Psalms 136:24-26
Kwa nini mwandishi anasema kumpa shukrani Mungu wa mbinguni?
Watu wanapaswa kumpa shukrani kwa sababu ya uaminifu wake.
Psalms 137
Psalms 137:1-2
Wafungwa walikuwa wapi walipoketi chini na kulia?
Walikuwa kando ya mto wa Babeli.
Psalms 137:3-4
Watekaji waliwataka mateka waimbe nini?
Watekaji waliwataka wawe na furaha na kuimba nyimbo za Sayuni.
Psalms 137:5-6
Mwandishi anataka nini kitokee kama akisahua Yerusalemu na kutomfikiria Yahwe tena.
Anataka mkono wake wa kuume usahahu ujuzi wake na ulimi wake ung'ang'anie kwenye paa ya mdomo wake.
Psalms 137:7
Mwandishi alimtaka Yahwe akumbuke nini kuhusu watu wa Edomu?
Anataka Yahwe akumbuke kuwa katika siku ambayo Yerusalemu ilianguka watu wa Edomu walisema, "Ibomoe chini, ibomoe chini hadi kwenye misingi yake."
Psalms 137:8-9
Mwandishi anataka nani abarikiwe?
Anamatka mtu anayeangamiza Babeli kubarikiwa.
Psalms 138
Psalms 138:1-2
Yahwe ametukuza nini juu ya vyote?
Ametukuza neno lake na jina lake juu ya vyote.
Psalms 138:3-4
Yahwe alimfanyia nini Daudi alipomwita?
Yahwe alimjibu, na kumtia moyo na kuimarisha nafsi yake.
Wafalme wa duniani watafanya nini?
Watatoa shukrani kwa ajili ya maneno ya Yahwe.
Psalms 138:5-6
Yahwe anamjali nani?
Anawajali walio chini.
Psalms 138:7-8
Daudi anamwomba Yahwe asimwache nani?
Anamwomba Yahwe asiwaache wale ambao mikono yake imewaumba.
Psalms 139
Psalms 139:1-2
Yahwe anaelewa nini kutoka mbali?
Yahwe anaelewa mawazo ya Daudi kutoka mbali.
Psalms 139:3-6
Daudi anaitikiaje juu ya uelewa kwamba Yahwe amemzunguka kabisa?
Uelewa huo ni mwingi sana kwa Daudi, uko juu sana, na hawezi kuuelewa.
Psalms 139:7-10
Daudi hawezi kutorokea wapi uwepo wa Yahwe, kwa sababu Yahwe yuko huko?
Hawezi kwenda juu mbinguni au kutengeneza kitanda chake kuzimu, kwa kuwa Yahwe yuko huko.
Psalms 139:11-12
Giza na nuru ziko tofauti kwa Yahwe?
Giza na nuru zote ni sawa kwa Yahwe.
Psalms 139:13-14
Yahwe alimuundia wapi Daudi?
Yahwe alimuunda Daudi tumboni mwa mama yake.
Psalms 139:15-16
Yahwe alitunza kumbukumbu lini ya siku za maisha ya Daudi?
Yahwe aliweka kumbukumbu ya siku zote za maisha ya Daudi katika kitabu cha Yahwe hata kabla siku ya kwanza haijatokea.
Psalms 139:17-18
Daudi alielezeaje mawazo ya Mungu?
Ni ya thamani na ni mengi sana kuhesabu.
Psalms 139:19-22
Daudi anataka Mungu awafanye nini waovu na watu wenye vurugu?
Daudi anamtaka Mungu awaue waovu na kuwaondoa watu wenye vurugu kwake.
Psalms 139:23-24
Daudi anamtaka Yahwe amwongoze njia gani?
Daudi anawomba Mungu kumwongoza katika njia ya milele.
Psalms 140
Psalms 140:1-3
Daudi anahitaji Yahwe amwokoe kutoka kwa nani?
Daudi anamhitaji Yahwe amwokoe kutoka kwa waovu na kumtunza kutoka kwa watu wenye vurugu.
Daudi anasema waovu ni kama nini?
Anasema ndimi zao zitakuwa kama nyoka na wana sumu ya kipiribao midomoni mwao.
Psalms 140:4-5
Watu wenye vurugu wanapanga kufanya nini kwa Daudi?
Wamepanga kumpindua.
Wenye kiburi wameandaa nini kwa ajili ya Daudi?
Wameweka mtego kwa ajili yake na kitanzi.
Psalms 140:6-8
Daudi anamwomba Yahwe kusikiliza nini?
Daudi anamwomba Yahwe kusikiliza vilio vyake kwa ajili ya huruma.
Yahwe anamfanyia nini Daudi katika siku ya vita?
Yahwe analinda kichwa cha Daudi katika siku ya vita.
Psalms 140:9-11
Daudi anataka nini kiwalemee wale wanaomzunguka?
Daudi anataka madhara ya midomo yao wenyewe iwalemee.
Daudi anataka nini kitokee kwa wale wanaosema vitu viovu kuhusu wengine?
Daudi anataka wote wanaosema vitu viovu kuhusu wengine wasiwe salama duniani.
Psalms 140:12-13
Yahwe atafanya nini kwa ajili ya wanaoteseka na wahitaji?
Yahwe endeleza haja ya wanaoteseka na kufanya haki kwa ajili ya wahitaji.
Hakika watu wenye haki watafanya nini?
Hakika watu wenye haki watatoa shukrani kwa jina la Yahwe.
Nini kitatokea kwa watu wanyofu?
Wataishi katika uwepo wa Yahwe.
Psalms 141
Psalms 141:1-2
Daudi analia nini kwa Yahwe?
Analia kwa Yahwe ili aje upesi na kumsikiliza anapoita.
Daudi anataka maombi yake na mikono iliyoinuliwa kuwa kama nini kwa Yahwe?
Daudi anataka ombi lake kuwa kama ubani mbele za Yahwe na mikono yake iliyoinuliwa iwe kama sadaka ya jioni.
Psalms 141:3-4
Daudi hataki moyo wake ufanye nini?
Anataka moyo wake usitamani kitu chochote kiovu, au kushiriki katika matendo ya dhambi na watu waovu, na kutokula chakula kizuri chochote cha watu waovu.
Psalms 141:5-7
Daudi anasema itakuwa kama nini kama mtu mwenye haki akimpiga?
Anasema kama mtu mwenye haki akimpiga, itakuwa ni huruma kwake.
Daudi anasema itakuwa kama nini kama mtu mwenye haki akimsahihisha?
Anasema itakuwa kama mafuta kichwani pake.
Daudi huwa anaomba dhidi ya nini?
Daima huwa anaomba dhidi ya matendo ya watu waovu.
NIni kitatokea kwa viongozi wa watu waovu?
Viongozi wao watatupwa chini kutoka juu ya jabali na kusikia kuwa maneno ya Daudi mwenyewe yanapendeza.
Nani itabidi asema, "Kama mtu anavyo lima na kupasua ardhi, hivyo ivyo mifupa yetu imesambaa mdomoni kwa kuzimu."
Watu waovu itabidi waseme, "Kama mtu anavyo lima na kupasua ardhi, hivyo ivyo mifupa yetu imesambaa mdomoni kwa kuzimu."
Psalms 141:8-10
Macho ya Daudi yako kwa nani?
Macho ya Daudi yako kwa Yahwe, Bwana.
Daudi anamtaka Yahwe amlinde na nini?
Daudi anamtaka Yahwe amlinde kutoka katika mitego ambayo imeandaliwa kwa ajili yake, na kutoka katika mitego ya watenda maovu.
Daudi anataka nini kitokee kwa waovu?
Daudi anataka waovu waanguke kwenye nyavu zao wenyewe wakati anatoroka.
Psalms 142
Psalms 142:1-2
Daudi anamwaga nini kwa Yahwe?
Daudi anamwaga maombolezo kumwambia Yahwe shida zake.
Psalms 142:3-5
Yahwe anajua nini wakati roho ya Daudi ni dhaifu?
Yahwe anajua njia ya Daudi wakati roho yake ni dhaifu.
Daudi anaona nini anapotazama kulia?
Daudi anaona kwamba hakuna mtu anayemjali, na hakuna pa kutorokea kwake.
Daudi anasema Yahwe ni nani kwake?
Yahwe alikuwa kimbilio la Daudi na sehemu yake katika nchi ya walio hai.
Psalms 142:6-7
Kwa nini Daudi anamhitajiYahwe amwokoe kutoka kwa watesaji wake?
Daudi anamwomba Yahwe kumwokoa kutoka kwa watesaji wake kwa sababu wana nguvu kumliko Daudi.
Kwa nini wenye haki watakusanyika kwa Daudi?
Wenye haki watakusanyika kwa Daudi kwa sababu Yahwe amekuwa mwema kwake.
Psalms 143
Psalms 143:1-2
Kwa nini Daudi hataki Yahwe amhukumu?
Daudi hataki Yahwe amhukumu kw sababu machoni pa Yahwe hakuna mtu aliye wa haki.
Psalms 143:3-4
Adui amemfanya nini Daudi?
Adui amefuatilia nafsi yake, amemsukuma chini ardhini, na kumfanya aishi gizani.
Adui amesababisha nini kitokea kwa roho na moyo wa Daudi?
Adui anasababisha roho ya Daudi kumlemea na moyo wake kukata tamaa.
Psalms 143:5-6
Daudi anaelezeaje hamu ya nafsi yake kwa ajili ya Yahwe?
Nafsi ya Daudi inakiu kwa ajili ya Yahwe katika nchi iliyokauka.
Psalms 143:7-8
Nini kitamsababisha Daudi kuwa kama wale wanaokwenda chini kwenye shimo?
Daudi atakuwa kama wale wanaokwenda chini shimoni kama Yahwe asipojibu upesi au kama akificha uso wake kwa Daudi?
Daudi anataka kusikia nini asubuhi kwa sababu anamtumaini Yahwe?
Daudi anataka kusikia uaminifu wa agano wa Yahwe.
Daudi anataka Yahwe afanye nini kwa sababu anainua nafsi yake kwa Yahwe?
Daudi anataka Yahwe amwoneshe njia ambayo anapaswa kutembea.
Psalms 143:9-10
Daudi anataka nini kimwongoze katika nchi ya unyofu?
Daudi anataka roho nzuri ya Yahwe imwongoze katika nchi ya unyofu.
Psalms 143:11-12
Daudi anamtaka Yahwe afanye nini kwa adui zake?
Daudi anamwomba Yahwe kuwakata adui zake wote na kuwaangamiza.
Psalms 144
Psalms 144:1-2
Yahwe anafanyisha maoezi mikono ya Daudi na vidole vyake kwa ajili gani?
Yahwe anafanyisha mazoezi mikono ya Daudi kwa ajili ya vita na vidole vyake kwa ajili ya mapambano.
Psalms 144:3-4
Yahwe anamgundua na kumfikiria nani ambayo inamshangaza Daudi?
Daudi anashangaa kwamba Yahwe anamgundua mtu na mwana wa mtu.
Psalms 144:5-6
Milima itafanya nini kama Yahwe akiigusa?
Yahwe atasababisha milima itoe moshi kama akiigusa.
Psalms 144:7-8
Yahwe anamwokoaje Daudi kutoka katika mikono ya wageni?
Yahwe anatoa mkono wake kutoka juu na kumwokoa Daudi kutoka kwenye maji na kutoka kwenye mkono wa wageni.
Psalms 144:9-11
Daudi ataimba wimbo mpya kwa Mungu kwa kutumia chombo gani?
Daudi ataimba wimbo mpya kwa Mungu kwenye kinanda cha nyuzi kumi.
Midomo ya wageni inazungumza nini?
Midomo yao huzungumza uongo na mkono wao wa kulia ni udanganyifu.
Psalms 144:12-13
Daudi anataka wana wa Israeli wawe kama nini?
Anawataka wawe kama mimea inayoota kikamilifu katika ujana wao.
Daudi anataka mabinti wa Israeli wawe kama nini?
Anawataka wawe kama nguzo za pembeni, zenye umbo kama zile za hekalu.
Psalms 144:14-15
Daudi anasema ni watu gani wenye furaha?
Daudi anasema watu wenye furaha ni wale ambao Mungu wao ni Yahwe.
Psalms 145
Psalms 145:1-3
Daudi atamtukuza na kumbariki nani?
Daudi atamtukuza Mungu wake na mfalme, akibariki jina lake milele.
Daudi humbariki Mungu mara ngapi?
Daudi atambariki Mungu kila siku.
Psalms 145:4-5
Kizazi kimoja kitasifu na kutangaza nini kwa kizazi kinachofuata?
Kizazi kimoja kitasifu matendo ya Mungu na kutangaza matendo yake makuu kwa kizazi kinachofuata.
Daudi atatafakari juu ya nini?
Atatafakari juu ya fahari ya utukufu wa Yahwe na matendo yake ya ajabu.
Psalms 145:6-9
Kizazi kimoja kitatangaza na kuimba nini kwa kizazi kinachofuata?
Watatangaza uzuri mwingi wa Yahwe na kuimba kuhusu haki yake.
Psalms 145:10-12
Nini kitamshukuru na kumbariki Yahwe?
Vyote alivyoumba Yahwe vitatoa shukrani kwake na waaminifu wake watambariki.
Nani atazungumza kuhusu ufalme wa Yahwe na kuelezea uwezo wa Yahwe?
Waaminifu wa Yahwe watazungumza kuhusu utukufu wa ufalme wake na kuelezea uwezo wake.
Psalms 145:13
Ufalme wa Yahwe utadumu hadi lini?
Ufalme wa Yahwe ni ufalme wa milele na mamlaka yake wanadumu katika vizazi vyote.
Psalms 145:14-16
Yahwe anamshika na kumwinua nani?
Yahwe huwashika wote wanaoanguka na kuwainua juu wote walioinama.
Macho ya nani yanamsubiri Yahwe na kupewa chakula wakati sahihi?
Macho ya kila mtu yanamsubiri Yahwe na yanapewa chakula kwa wakati sahihi.
Yahwe huridhishaje hamu za kila kiumbe hai?
Yahwe hufungua mkono wake na kuridhisha hamu ya kila kiumbe hai.
Psalms 145:17-19
Yahwe yuko karibu na nani?
Yahwe yuko karibu kwa wale wote wanaomwita na kwa wote wanamwita katika uaminifu.
Psalms 145:20-21
Yahwe huwafanyia nini wale wanompenda?
Yahwe huwaangalia wote wanaompenda.
Yahwe atawafanya nini waovu?
Atawaangamiza waovu wote.
Psalms 146
Psalms 146:1-2
Mwandishi atamsifu Yahwe kwa muda gani?
Atamsifu Yahwe maisha yake yote.
Psalms 146:3-4
Mtu hapaswi kuweka matumaini katika nini?
Watu hawapaswi kuweka matumaini yao katika wakuu au wanadamu, ambapo hakuna wokovu.
Nini hutokea wakati pumzi ya uhai wa mtu ikikoma?
Pumzi ya uhai wa mtu ikikoma, hurudi ardhini, siku hiyo mipango yake hufika mwisho.
Psalms 146:5-6
Ni nani aliyebarikiwa?
Aliyebarikiwa ni yule ambaye ana Mungu wa Yakobo kwa ajili ya msaada wake, ambaye matumaini yake yako katika Yahwe Mungu wake.
Yahwe ameumba nini?
Yahwe ameumba mbingu na dunia, bahari, na vyote vilivyomo.
Psalms 146:7-8
Yahwe hufanya nini kwa ajili ya vipofu na wale walioinama chini?
Yahwe hufungua macho ya vipofu, na huwainua wale walioinama chini.
Psalms 146:9-10
Yahwe anamlinda nani?
Yahwe anawalinda wageni katika nchi.
Yahwe atatawala kwa muda gani?
Yahwe atatawala milele, kwa vizazi vyote.
Psalms 147
Psalms 147:1
Kwa nini Yahwe anapaswa kusifiwa?
Yahwe anapaswa kusifiwa kwa sababu ni vyema, inapendeza na inafaa.
Psalms 147:2-3
Yahwe anawasaidiaje wafuasi wake?
Yahwe anasaidia kujenga tena Yerusalemu, na kukusanya watu waliotawanyika wa Israeli.
Psalms 147:4-5
Yahwe anazifanya nini nyota baada ya kuzihesabu?
Yahwe anahesabu nyota na kuzipa zote majina.
Uelewa wa Bwana ni mkuu vikoje?
Uelewa wake hauwezi kupimwa.
Psalms 147:6-7
Yahwe anawafanya nini waovu?
Yahwe anawaleta waovu chini ardhini.
Psalms 147:8-9
Yahwe anawatunzaje wanyama na kunguru?
Yahwe anawapa chakula wanyama na kunguru wadogo wanapolia.
Psalms 147:10-11
Yahwe hapendezwi na kutokuwa na furaha juu ya kitu gani?
Yahwe hapendezwi na nguvu ya farasi na hafurahii miguu yenye nguvu ya mtu.
Yahwe anafurahishwa na nini?
Yahwe hufurahishwa na wale wanaomheshimu, wanao tumaini katika uaminifu wake wa agano.
Psalms 147:12-14
Yahwe anawaridhisha watu wa Yerusalemu na nini?
Yahwe anawaridhisha na ngano bora zaidi.
Psalms 147:15-16
Amri ya Yahwe ya duniani inafanya nii?
Yahwe anatuma amri yake duniani na amri yake inakimbia kwa kasi sana.
Psalms 147:17-18
Yahwe anagawaje mvua ya mawe?
Yahwe anagawa mvua ya mawe kama chembechembe.
Psalms 147:19-20
Yahwe alitangaza kwa nani neno lake na sheria na amri za haki?
Yahwe alitangaza neno lake kwa Yakobo, na sheria zake na mari za haki kwa Israeli.
Yahwe ametangaza neno lake, sheria na amri kwa taifa gani lingine?
Yahwe hajatangaza neno lake, sheria na amri zake kwa taifa jingine lolote.
Psalms 148
Psalms 148:1-2
Ni nani wa kumsifu Yahwe?
Kila mtu mbinguni, wale walio juu, malaika wote na majeshi ya malaika ni ya kumsifu Yahwe.
Psalms 148:3-4
Ni nani wa kumsifu Yahwe?
Jua, mwezi, nyota zinazong'aa, mbingu ya juu na maji juu ya anga ni ya kumsifu Yahwe.
Psalms 148:5-6
Kwa nini Yahwe anapaswa kusifiwa?
Yahwe anapaswa kusifiwa kwa sabau alitoa amri na kila kitu kikaumbwa.
Amri gani haitabadilika kamwe?
Amri ya Yahwe haitabadilika kamwe.
Psalms 148:7-8
Nani anapaswa kumsifu Yahwe kutoka duniani?
Viumbe wa baharini, bahari lote, moto, mvua ya mawe, theluji, mawingu na upepo ambavyo vinatimiza neno lake vinapaswa kumsifu Yahwe.
Psalms 148:9-12
Nani pia anapaswa kumsifu Yahwe?
Milima, vilima, miti ya matunda, seda, wanyama wa pori na wa kufuga, viumbe vinavyotambaa na ndege wanatakiwa kumsifu Yahwe.
Psalms 148:13-14
Kwa nini Yahwe anapaswa kusifiwa?
Yahwe anapaswa kusifiwa kwa sababu jina lake pekee limetukuzwa na utukufu wake umesambaa juu ya dunia na mbingu.
Watakatifu wa Yahwe ni kinanani?
Waisraeli na watu walio karibu naye ni watakatifu wa Yahwe.
Psalms 149
Psalms 149:1
Watu wote wanatakiwa kumsifu Yahwe vikoje?
Watu wote wanatakiwa kuimba wimbo mpya kwa Yahwe na kuimba sifa yake katika kusanyiko.
Psalms 149:2-3
Israeli wanapaswa kumshangilia nani?
Israeli wanapaswa kumshangilia yule aliyewafanya kuwa taifa, na katika mfalme wao.
Watu wote wanatakiwa kumsifu Yahwe vikoje?
Kila mtu anapaswa kulisifu jina la Yahwe kwa kucheza na kwa kuimba sifa kwake kwa tari na kinubi.
Psalms 149:4-5
Yahwe anamfurahia nani?
Yahwe hufurahi katika watu wake.
Yahwe anamwinua nani?
Huwainua wanyenyekevu kwa wokovu.
Watauwa wanapaswa kufurahi kwa namna gani?
Watauwa wanapaswa kufurahi katiak ushindi na kuimba kwa furaha.
Psalms 149:6-7
Nini kinatakiwa kuwa ndani ya midomo ya watauwa?
Sifa za Mungu zinatakiwa kuwa katika midomo yao.
Upanga wenye makali pande mbili katika mikono ya watauwa una kududi gani?
Upanga katika mikono yao ni kwa ajili ya kutekeleza kisasi juu ya mataifa na matendo ya adhabu juu ya watu.
Psalms 149:8-9
Wanyofu watawafanya nini wafalme na watu wenye vyeo wa mataifa mengine?
Watawafunga wafalme kwa minyororo na wenye vyeo kwa pingu za chuma.
Nani ataheshimiwa hukumu ikipitishwa?
Hii itakuwa heshima kwa ajili ya waaminifu wake wote.
Psalms 150
Psalms 150:1-2
Ni wapi watu wote wanapaswa kumsifu Mungu?
Watu wote wanapaswa kumsifu Mungu katika mahali pake patakatifu na mbingu zake kuu.
Waatu wanapaswa kumsifu Mungu kwa ajili gani?
Watu wote wanapaswa kumsifu Mungu kwa ajili ya matendo yake makuu na ukuu wake unaozidi.
Psalms 150:3-5
Watu wanapaswa kumsifu Mungu kwa kutumia vyombo vipi?
Watu wote wanapaswa kumsifu Mungu kwa pembe, kinanda, kinubi, matari, kucheza, kwa vyombo vya nyuzi na vya upepo, na kwa matoazi.
Psalms 150:6
Nani anapaswa kumsifu Yahwe?
Kila kitu chenye pumzi kinapaswa kumsifu Yahwe.