John
John 1
John 1:1-3
Hapo mwanzo kulikuwa na nini?
Hapo mwanzo kulikuwa na neno.
Neno alikuwa na nani?
Neno alikuwa pamoja na Mungu.
Neno alikuwa na nani?
Neno alikuwa Mungu.
Je kuna chochote kilichofanyika bila Neno?
Vitu vyote vilifanywa kupitia yeye, na bila yeye hakuna hata kitu kimoja kingengefanyika ambacho kimefanyika.
John 1:4-5
Kulikuwa na nini ndani ya neno?
Ndani yake kulikuwa uzima
John 1:6-9
Jina la mtu aliyetumwa kutka kwa Mungu lilikuwa nani?
Jina lake lilikua Yohana
Yohana alikuja Kufanya nini?
Alikuja kuwa shahidi wa kushuhudia kuhusu nuru, ili kwamba wote waweze kuamini kupitia yeye.
John 1:10-11
Je ulimwengu ulijua au kupokea nuru ambayo Yohana alikuja kuishuhudia?
Ulimwengu haukuijua ile nuru ambayo Yohana alikuja kuishuhudia. na kwamba watu wenyewe wa huyo nuru hawakumpokea yeye.
John 1:12-13
Nuru ilifanya nini kwa wale walioamini juu ya jina lake?
Wale walioamini juuwa ya jina lake aliwapahaki ya kuitwa watoto wa Mungu.
Wale walioamini juu ya jina lake wangeweaje kuwa watoto wa Mungu?
Wangeweza kufanyika watoto wa Mungu kwa kuzaliwa na Mungu
John 1:14-15
J e kuna mtu au kumewahi kuwa na mtu yeyote kama neno ambaye alikuja kutoka kwa Mungu?
Hapana! Neno pekee ndiye mtu maalum kutoka kwa Baba.
John 1:16-21
Tumepokea nini kutokana kwa ukamilifu wa yule ambaye Yohana alishuhudia habari zake?
Kutoka katika utimilifu wake, sisi sote tumepokea bure kipawa baada ya kipawa cha bure.
Kutoka katika Yesu Kristo nini kilikuja?
Neema na kweli zilikuja kupitia kwa Yesu Kristo.
Ni nani aliyemwona Mungu wakati wowote?
Hakuna mtu aliyemwaona Mungu wakati wowote.
Ni nani aliyefanya Mungu ajulikane?
Aliye katika kifua cha Baba, amemfanya yeye ajulikane kwetu.
John 1:22-28
Yohana alisema kuwa yye ni nani alipoulizwa na makuhani na Walawi kutoka Yerusallemu?
Alisema, "Mimi ni sauti yake aliaye nyikani: 'Inyosheni njia ya Bwana,' kama tu vile nabii Isaya alivyosema."
John 1:29-31
Yohana alisema nini alipomwona Yesu akija kwake?
Alisema "Tazama Mwana-Kondoo wa Mungu aichukuae dhambi ya ulimwengu!"
Ni kwa nini Yohana alikuja akibatiza kwa maji?
Alikuja akibatiza kwa maji ili kwamba Yesu, Mwana - Kondoo wa Mungu aichukuaye dhambi ya ulimwengu, angeweza kufunuliwa kwa Israeli.
John 1:32-36
Ni ishara gani iliyomdhihirisha Yesu kuwa ni Mwana wa Mungu kwa Yohana?
Ishara ilikuwa kwamba kwa yeyote yule ambaye utaona Roho akishuka na kukaa juu yake, Huyo ndiye abatizaye kwa Roho Mtakatifu.'
John 1:37-39
Wanafunzi wawili wa Yohana walifanya niniwaliposikia Yohana akimwita Yesu "Mwana kondoo wa Mungu"?
Walimfuata Yesu
John 1:40-42
Jina la mmoja wa wawili waliomsikia Yohana akiongea na kisha kumfuata Yesu alikuwa nani?
Jina la mmoja wapo kati ya wale wawili ni Andrea
Andrea alimwambia nini Simoni nduguye kuhusu Yesu?
Andrea alimwambia Simoni, "Tumempata Masihi"
Je! Yesu alisema Simoni angeitwa nani?
Yesu alisema Simoni anegitwa "Kefa," (maana yake 'Petro').
John 1:43-48
Mji wa andrea na Petro uliitwaje?
Mji wa Andrea na Petro ulikuwa Bethsaida
John 1:49-51
Nathanaeli alisema nini kuhusu Yesu?
Nathanaeli akasema, "Rabi, wewe ni mwana wa Mungu! Wewe ni Mfalme wa Iziraeli".
Yesu alisema Nathanieli angeona nini?
Yesu alimwambia Andrea angeziona mbingu zikifunguka, na kuwaona malaika wakipanda na kushuka juu ya Mwana wa Adamu."
John 2
John 2:1-2
Ni nani alikuwa katika harusi huko Kana ya Galilaya?
Yesu, mama yake, na wanafunzi wake walikuwa kwenye harusi katika Kana ya Galilaya.
John 2:3-5
Kwa nini mama wa Yesu alimwambia Yesu, "Hawana divai?."
Alimwambi hivyo kwa sababu alitarajia kuwa angefanya kitu fulani kuhusu mazingira husika
John 2:6-8
Yesu aliwaambia watumishi kufanya mambo gani mawili?
Kwanza aliwambia kuijaza maji mitungi. Kisha aliwambia hao watumishi kupeleka kiasi cha "maji" kwa mhudumu mkuu wa meza.
John 2:9-10
Je! Mhudumu mkuu wa meza alisema nini alipoyaonja maji aliyokuwa yamebadilika kuwa divai?
Mhudumu mkuu wa meza alisema, "Kila mmoja huanza kuwahudumia watu divai nzuri na wakiishalewa huwapa divai isiyo nzuri. Lakini wewe umeitunza divai nzuri mpaka sasa"
John 2:11-12
Mwitikio wa wanafunzi wa Yesu walipoona ishara hii?
Yesu' wanafunzi wanaamini katika Yesu.
John 2:13-14
Yesu aliona nini alipokwenda hekkaluni huko Yerusalemu?
Aliwakuta wabadili fedha na waliokuwa wakiuza ng'ombe, kondoo, na njiwa
John 2:15-16
Yesu alifanya nini kwa wauzaji na wabadilisha fedha?
Akatengeneza mjeledi wa kamba akawafukuza wote waende nje ya Hekalu pamoja na kondoo na ng'ombe. Pia akamwaga fedha za wanavunja fedha, na kupindua meza zao.
Yesu aliwaambia nini wauza njiwa?
Akawambia, "Toeni hapa vitu hivi, acheni kuifanya nyumba ya Baba yangu kuwa mahali pa soko."
John 2:17-19
Je! Wakuu wa Kiyahudi waliitikiaje kwa vitendo vya Yesu hekaluni?
Wakamuuliza Yesu, "Ni ishara ipi utakayoionyesha kwa sababu unayafanya mambo haya?"
Yesu aliwajibuje Wakuu wa Kiyahudi?
Akawajibu, "libomoeni Hekalu hili, na katika siku tatu nitaliinua."
John 2:20-22
Yesu alikuwa akimaanisha hekalu gani?
Yesu alikuwa akiongea hekalu la mwili wake.
John 2:23-25
Kwa nini wengi waliamini katika jina la Yesu?
Wao waliamini kwa sababu waliona dalili zote za miujiza aliyofanya.
Kwanini Yesu asingejiaminisha mwenyewe kwa watu?
Asingejiaminisha mwenyewe kwa watu kwa sababu aliwajua wanadamu wote, na hakuhitaji mtu yeyote kuthibitisha kuhusu walivyo wanadamu.
John 3
John 3:1-2
Nikodemo alikuwa nani?
Nikodemo alikuwa Mfarisayo, mjumbe wa Baraza la Wayahudi.
Nicodemo alishudia nini kwa Yesu?
Nikodemo alimwambia Yesu,"Rabi, tunajua ya kuwa u mwalimu kutoka kwa Mungu, kwa maana hakuna mtu awezaye kutenda ishara hizi zote Mungu asipokuwa pamoja naye."
John 3:3-6
Yesu alimwambia nini Nikodemo hata kumtatanisha na kumchanganya?
Yesu alimwambia Nikodemo kwamba ilimpasa mtu kuzaliwa upya ndipo auingie ufalme wa Mungu
Nikodemo aliuliza swali gani linalotufanya tujue kwamba kauli ya Yesu ilimchanganya na kumtatanisha Nikodemo?
Nikodemo alisema," Mtu anawezaje kuzaliwa akiwa mzee? Hawezi kuingia tumboni mwa mama yake mara ya pili na kuzaliwa, Je! Anaweza?"
John 3:7-8
Yesu alimwambia nini Nikodemo kilichomshangaza na kumchanganya?
Yesu alimwambia Nikodemo kwamba mmoja alikuwa na kuzaliwa tena, kwa asipozaliwa kwa maji na kwa roho ili kuingia ufalme wa Mungu.
John 3:9-11
Yesu alimkemeaje Nikodemo?
Alimkemea Nikodemo kwa kumwambia, "Wewe u mwalimu wa Israeli, hata huyaelewi mambo haya?
John 3:12-13
Ni nani alipanda mbinguni?
Hakuna aliyepanda mbinguni isipokuwa yeye aliyeshuka kutoka mbinguni, Mwana wa Adamu.
John 3:14-15
Kwa nini ni lazima Mwana wa Adamu ainuliwe juu?
Ni lazima Ainuliwa ili kwamba wote wanaoamini katika yeye wapate uzima wa milele.
John 3:16-18
Ni jinsi gani Mungu lionyesha kwamba aliupenda ulimwengu?
Alionyesha pendo Lake kwa kumtoa Mwanawe wa pekee ili kila mtu amwaminiye asipotee bali awe na uzima wa milele.
Je! Mungu alimtuma Mwanawe kuuhukumu ulimwengu?
Hapana.Mungu alimtuma Mwanawe ili kwamba ulimwengu uokolewa kwa kupitia Mwanawe.
John 3:19-28
Kwa nini watu huangukia hukumuni?
Watu kuanguka chini ya hukumu kwa sababu nuru imekuja ulimwenguni, na watu wakapenda giza kuliko kuipenda nuru, kwa sababu matendo yao ni maovu.
Kwani ni wale wanaofanya maovu hawataki kuja kwenye nuru?
Wanaofanya maovu huichukia nuru na hawataki kuja ndani yake kwa sababu hawataki matando yao yawekwe wazi.
Kwa nini waitendao kweli huja kwenye nuru?
Wanakuja kwenye nuru ili kwamba matendo yao yaonekane wazi na kuweka wazi kwamba matendo yao yametokana na utii kwa Mungu
John 3:29-30
Yohana alisema kingetokea nini kwa huduma ya Yesu, ukilinaganisha na huduma ya Yohana?
Yohana alisema, "Anapaswa kuzidi, nami napaswa kupungua."
John 3:31-33
Wale walioukubali ushuhuda wa Yeye atokaye juu, atokaye mbinguni, walithibitisha nini?
Walithibitisha kwamba Mungu ni mkweli.
John 3:34-36
Baba ameweka nini mkanoni mwa Mwana?
Ameweka vitu vyote mkononi mwa Mwana.
Wale wanaomini katika Mwana wana nini?
Wanauzima wa Milele.
Huwa kunatoea nini kwa wale wanaomwasi Mwana?
Hawatauona uzima, bali ghadhabu ya Mungu nashikamana juu yao.
John 4
John 4:1-3
Ni wakati gani Yesua alitoka Yudea na kwenda Galilaya?
Yesu alitoka Yudea kwa Galilaya baada ya yeye kujua Mafarisayo wamesikia ya kwamba yeye alikuwa anabatiza na kuwapata wanafunzi wengi kuliko Yohana.
John 4:4-5
Yesu alifika wapi alipokuwa njiani kwenda Galilaya?
alifika kwenye mji wa Samaria, unaoitwa Sikari,
John 4:6-8
Ni nani alikuja kwenye kisima cha Yakobo Yesu alipokuwa hapo?
Mwanamke Msamaria alikuja hapo kuteka maji,
Yesu alisema nini kwanza kwa mwanamke Msamaria?
alimwambia, "Nipe ya kunywe."
Wanafunzi wa Yesu walikuwa wapi?
Walikuwa wamekwenda zao mjini kununua chakula.
John 4:9-10
Kwa nini mwanamke Msamaria alishangaa kumwona Yesu anaongea naye?
Alishangazaa kwa sababu Wayahudi hawakujishughulisha na Wasamaria.
Yesu alisemaje ili kuulekaza mjadala kwa mambo ya Mungu?
Yesu anamwambia kwamba kama angelijua karama ya Mungu, na yule aliyekuwa akiongea naye ni nani agelimwomba maji na angekuwa amamishampa maji ya uzima."
John 4:11-14
Ni kauli gani ambayo mwanake anatoa kuashria kuwa hayaelewi asili ya kiroho ya maoni ya Yesu?
mwanamke akajibu, `Mheshimiwa, wewe huna ndoo, na kisima ni kirefu. ungeyapata wapi hayo maji yaliyo hai? '
John 4:15-16
Yesu anamwambia nini mwanamke kuhusu maji atakayompa?
Yesu anamwambia mwanamke wale wanaokunywa maji anatoa yeye wahataona kiu tena na kwamba maji hayo yatakuwa chemchemi ya maji, yakibubujikia uzima wa milele.
Kwa nini mwanamke anayataka maji ambayo Yesu anatoa?
Yeye anataka maji hayo ili asione kiu na asije tena kisimani kuteka maji.
Yesu anabadili somo la mazungumzo. Anamwambia nini Mwanamke?
Yesu anamwambia, "Nenda ukamwite mumeo, kisha urudi hapa."
John 4:17-18
Ni namna gani mwanamke anamjibu Yesu anapomwambia kumwita mume wake?
mwanamke anamwambia Yesu kuwa hana mume.
Yesu anamwambia nini mwanamkwa ambaye hakumjua asili ya maisha yake.
Anamwambia amekuwa na waume watano na mwanaume aliyenaye sasa siyo mumewe.
John 4:19-22
Mwanamke analeta mjadala gani kwa Yesu kuhusu ibada?
Anaibua mjadala juu ya mahali sahihi pa kuabudia.
John 4:23-24
Yesu anamwambia nini mwanamke kuhusu aina ya waabuduo ambao Baba anawatafuta?
Yesu anawaambia Mungu wake ni Roho na wale waabuduo kweli lazima wamwabudu Mungu katika roho na kweli.
John 4:25-27
Yesu anamwambia nini mwanamke alipomwambia kwamba wakati Masihi (Kristo), atakapokuja atawambia mambo yote?
Yesu anamwambia kwamba yeye ni Masihi (Kristo).
John 4:28-33
Mwanamke alifanya nini baada ya mazungumzo yake na Yesu?
mwanamke akauacha mtungi wake pale, akaenda mjini na kuwaambia watu, 'Njoo kuona mtu aliyeniambia mambo yote niliyotenda. Hii inaweza kuwa Kristo, au sivyo? '
John 4:34-38
Yesu anasema chakula chake ni nini?
Yesu alisema chakula chake ni kufanya mapenzi ya yule aliyemtuma, na kukamilisha kazi yake.
Ni nini faida ya mavuna?
Wavunaji hupokea ujira wao na kukusanya matunda kwa ajili ya uzima wa milele, ili kwamba yule anayepanda na anayevuna waweze kufurahi pamoja.
John 4:39-40
Ni kwa nini Wamaria wengi katika mji huo walimwamini katika Ysu?
Taarifa ya mwanamke ilisababisha Wasamaria wengi kumawamini Yesu katika mji huo
John 4:41-42
Wengi wa Wasamaria hao waliamini nini kuhusu Yesu?
Walisema kwamba sasa walijua kwamba Yesu alikuwa Mwokozi wa ulimwengu hasa.
John 4:43-45
Yesu alipoingia Galilaya, kwa nini Wagalilaya walimkaribisha?
walimkaribisha kwa sababu walikuwa wameona mambo aliyokuwa ametenda huko Yerusalemu kwenye sikukuu
John 4:46-47
Baada ya Yesu kutoka Yudea na kurudi Galilaya, nani alikuja kwa Yesu na alitaka nini?
ofisa aliyekuwa na mtoto mgonjwa alikuja kwa Yesu, kumwomba ashuke na kumponya mwanawe.
John 4:48-52
Yesu alimwambia nini yule ofisa kuhusu ishara na maajabu?
esu akamwambia, "Watu wasingeliamini mpaka waone ishara na miujiza.
Yule ofisa alifanya nini wakti Yesu hakwenda naye bali alimwambia,"Nenda; mwanao ni mzima?
Mtu huyo aliyaamini maneno ambayo Yesu alimwambia, na akaenda zake.
John 4:53-54
Ni nini kilichotokea baada ya baba wa mtoto wa mgonjwa alipoambiwa mtoto wake alikuwa mzima na kwamba homa ilimwacha saa saba siku moja kabla, na kwamba ni wakati ule ule alipoambiwa na Ysu, 'Mwana ni mzima"?
Matokeo yalikuwa kwamba yule ofisa pamoja na wa nyumbani mwake wote waliamini.
John 5
John 5:1-4
Bwawa katika mji wa Yeruslemu kwenye lango la kondoo ambalo lilikuwa na kumbi tano liliitwaje
Bwawa hilo liliitwa Bethesda
Nani alikuwako huko Bethesda?
Idadi kubwa ya wasiojiweza ilikuwemo, yaani vipofu, viwete, au waliopooza walikuwa wamelala katika kumbi hizo
John 5:5-6
Pale Bethesda ni nani aliyeambiwa naYesu , "Unataka kuwa mzima?
Yesu alimuuliza mtu fulani aliyekuwa mgonjwa kwa muda wa miaka thelathini na minane na ambaye alikuwa amelazwa huko kwa muda mrefu
John 5:7-8
Jibu la yule mtu lilikuwa lipi alipoulizwa, "Unataka kuwa mzima"?
mtu mgonjwa akajibu, `Mheshimiwa, mimi sina mtu yeyote wa kunitumbukiza bwawani maji yanapotibuliwa. Wakati Ninapojaribu kuingia, mtu mwingine hunitangulia kuingia.
John 5:9
Ni nini kilitokea wakati Yesu alipomwambia yule mtu mgonjwa, "Simama, chukua kitanda chako, na uende?
'Mara hiyo mtu huyo aliponywa, alichukua kitanda chake na kutembea'
John 5:10-13
Kwa nini liliwahuzunisha viongozi wa Kiyahudi walipomwona yule mtu aliyekuwa mgonjwa akitambea akiwa kitanda chake?
Liliwahuzunisha kwa sababu ilikuwa ni Sabato na wakasema mtu mtu huyo hakuruhusiwa kubeba kitanda chake siku ya Sabato.
John 5:14-15
Yesu alisema nini kwa yule mtu aliyemponya baada ya Yesu kumwaona hekaluni ?
Yesu alimwambia, "Tazama, umepona! "Usitende dhambi tena usije ukapatwa na jambo baya zaidi."
Yule mgonjwa aliyeponywa alifanya nini baada ya Yesu kumwambia kuacha kutenda dhambi?
Yule mtu alienda akawaambia viongozi wa Wayahudi kwamba alikuwa ni Yesu aliyemponya.
John 5:16-18
YEsu aliwajibuje viongozi wa Wayahudi ambao wamtesa kwa basababu alikuwa akifanya mambo haya (kupojanya) kwenye Sabato?
Yesu aliwaambia, " Baba yangu anafanya kazi hata sasa, na Mimi, pia, nafanya kazi."
Kwanini kauli ya Yesu kwa vingozi wa Wayahudi iliwafanya watake kumuua Yesu?
Ilitokea hivi kwa sababu yesu hakuwa tu anavunja Sabato (akilini mwao), bali pia alimwita Mungu Baba yake, akijifanya mwenyewe kuwa sawa na Mungu
John 5:19-20
Yesu alifanya nini?
Aliifanya kile alichomwona Baba akifanya.
Ni kitu gani Baba angefanya ili kwamba viongozi wa Wayahudi wangeshangazwa?
Baba angemwonyesha Mwana mambo makubwa zaidi ya haya hivyo viongozi wa Wayahudi wangeshangazwa.
John 5:21-23
Ni kwa nini Baba alimempa mwana hukumu yote?
Baba amempa Mwana hukumu yote ili kwamba wote wamuheshimu Mwana kama vile Mwana anavyomuheshimu Baba
HUtokea nini kama humheshi Mwana?
Kama humheshimu Mwana humheshimu Baba aliyemtuma.
John 5:24-25
Ni nini kinatokea kama ukiamini neno la Yesu na kumwamini Baba aliyemtuma?
Kama hivyo, una uzima wa milele na hutahukumiwa lakini utakuwa umepita mautini kuingia uzima.
John 5:26-27
Baba amempa nini Mwana kuhusu uzima?
Baba amempa Mwana kuwa na uzima ndani yake.
John 5:28-29
Nini kitatokea wote walio makaburini watakaposikia sauti ya Baba?
Nao watoka nje. Wale waliotenda mema kwa ufufuo wa uzima, na wale waliotenda maovu kwa fufuo wa hukumu.
John 5:30-35
Kwa nini hukumu ya Yesu ni ya haki?
Hukumu yake ni ya haki kwa sababu yeye hatafuti mapenzi yake mwenyewe bali mapenzi ya Baba aliyemtuma.
John 5:36-38
Ni ushuhuda gani mkuu kuliko wa Yohana alionao Yesu kuthibitisha kwamba alitumwa kutoka kwa Baba?
Kazi alizofanya Yesu zilishuhudia kuwa alitumwa kutoaka kwa Baba.
Ni nani ambaye alikuwa hata hajawahi kuisikia sauti ya Baba wala kuona umbo lake wakati wowote?
Viongozi wa Wayahudi hawakuahi hata kusikia sauti wala kuona umbo lake wakati wowote.
John 5:39-42
Kwa nini Wayahudi waliyachunguza maandiko?
Waliyachunguza kwa sababu walidhani kwamba ndani yake kulikuwa na uzima wa milele.
Maandiko yanamshuhudia nani?
Maandiko hushuhudia kuhusu Yesu.
John 5:43-44
Viongozi wa Wayahudi hawakutafuta sifa kutoka kwa nini?
Walikuwa hawatafuti sifa ambayo ilitoka kwa Mungu pekee.
John 5:45-47
Yesu alisema vinNi nani aliyekuwa akiwashitaki viongozi wa Wayahudi mbele za Baba?
Musa alikuwa anaenda kuwashitaki viongozi wa Wayahudi mbele ya Baba.
Yesu anasema viongozi wa Wayahudi wangefanya nini kama walimwamini Musa?
Anasema viongozi wa Wayahudi wangeamili katika Yesu kwama kweli alimwamini Musa kwa sababu Musa aliandika kuhusu Yesu.
John 6
John 6:1-3
Jina lingine la Bahari ya Galilaya iliitwaje?
Bahari ya Galilaya pia aliitwa bahari ya Tiberia.
Kwa nini kundi mkutano mkubwa ulimfuata Yesu?
Walimfuata kwa sababu walikuwa wakiziona ishara ambazo Yesu alikuwa akizifanya juu ya wale waliokuwa wagonjwa.
John 6:4-6
Yesu aliona nini baada ya kukaa mlimani akiwa na wanafunzi wake na kutazama juu?
Yeye akaona mkutano mkuu wanakuja kwake.
Kwa nini Yesu alimwuliza Filipo, "Tutakwenda wapi kununua mikate ili hawa waweze kula?"
Yesu alisema hili kumjaei Filipo.
John 6:7-9
Mwitikio wa Filipo ulikuwa ni upi kwa swali la Yesu, "Ni wapi tutakaponunua mikate ili watu hawa wote wale?"
Philipo alisema, "Hata mikate ya dinarimia mbili isingekuwa kutosha kwa ajili ya kila mmoja kuwa na hata kidogo."
Mwitikio wa Andrea kwa swali la Yesu, "Ni wapi tutakaponunua mikate ili watu hawa wote wale?
Andrea alisema,"Kuna mvulana hapa ana mikate mitano na samaki wawili, lakini hivi kitu gani kwa watu wengi namna hii?"
John 6:10-12
Ni wanaume wangapi waliokuwepo katika sehemu ile?
Kulikuwa na wanaume wapatao elfu tano huko.
Yesu alifanya aliifanyia nini mikate na hao samaki?
"Yesu alichukua ile mikate mitano akashukuru akawagawia wale waliokuwa wamekaa. Vivyo hivyo akawagawia samaki kwa kadiri ya vile walivyohitaji.
Watu walikula kiasia gani?
Walipata vingi kulingana na walivyotaka kula.
John 6:13-15
Ni kiasi gani cha mikate kilichookotwa baada ya kula mikate?
Wanafunzi wakajaza vikapu kumi na viwili vipande kutoka mikate mitano ya shayiri na vipande vya kushoto juu kutoka kwa wale waliokula.
Kwa nini Yesu alijitenga tena peke yake kwenda mlimani?
Yesu alijitenga kwa sababu aligundua kwamba , baada ya watu kuona muujiza alifanya (kuwalisha watu elfu tano), walikuwa karibu kuja na kumkata kwa nguvu na kumfanya mfalme.
John 6:16-18
Kulitokea nini kwa hali ya hewa baada ya wanafunzi kuingia kwenye mtumbwi na kuanza safari ya kwenda Kaprnaumu?
Upepo mkali ulianza kuvuma na Bahari ilianza kuchafuka.
John 6:19-25
Kwa nini wanafunzi wa Ysu walianza kuogopa?
Walikuwa na hofu kwa sababu walimwona Yesu akitembea juu ya maji anakaribia mashua.
Yesu aliwaambia nini wanafunzi wake ambacho kilichowafanya wakubali kumpokea kwenye mtubwi?
Yesu aliwaambia, "kawambia, "Ni mimi! Msiogope."
John 6:26-29
Yesu alisema sababu ya makutano kumtafuta ilikuwa ni ipi?
Yesu alisema walikuwa wanamtafuta Yeye si kwa sababu waliziona ishara, bali kwa sababu walikula baadhi ya mikate wakashiba.
Yesu aliwaambia makutano wafanye nini na wasifanye nini?
Yesu aliwambiaa waache kukifanyia kazi chakula chenye kuharibika, bali wafanyie kazi chakula kidumcho hata milele
John 6:30-34
Mkutano ulianza kumwomba Yesu kwa ajili ya ishara kama Manna, mkate kutoka mbinguni, baba zao waliapa ili wale, Ni mkate gani tena Yesu anauonglea?
Yesu anazungumza kuhusu mkate wa kweli kutoka mbinguni kwa Mungu ambao ni uhai kwa ulimwengu. kisha Yesu anawaambia yeye ni mkate wa uzima.
John 6:35-37
Ni mikate gani ambao Yesu anauongelea?
Yesu anasema kwamba yeye ndiye wmkate wa uzima.
Ni nani atakayekuja kwa Yesu?
Wote ambao Yesu amepewa na Baba watakuja kwake.
John 6:38-45
Mapenzi ya Baba aliyemtuma Yesu nini?
Mapenzi ya Baba ni kwamba Yesu asimpoteze hata mmoja wa wale wa aliompa Yeye na kwamba yeyote amtazamaye Mwana na kumwamini apate uzima wa milele; na Yesu atamfufua siku ya mwisho.
John 6:46-49
Ni nani aliyemwona Baba?
Ni yule tu aliyetoka kwa Mungu ndiye aliyemwona Baba.
John 6:50-51
Ni mkate gani Yesu ambao Yesu atautoa kwa ajili ya uzima wa ulimwengu?
Mkate atakaoutoa Yesu kwa ajili ya uzima wa ulimwangu ni mwili wake."
John 6:52-53
Unatakiwa kufamya nini ili kupata uzima ndani yako?
Ili kupata uzima ndani yako ni lasima uule mwili wa Mwana wa Adamu na kuinywa damu yake.
John 6:54-56
Tnawezaje kukaa ndani ya Yesu na Yesu kukaa ndani Yestu?
Kama tutakula mwili wake na kunywa damu yake tutakaa ndani ya Yesu na yeye ndani Yetu.
John 6:57-59
Ni kwa nini Yesu anaishi?
Yesu anaishi kwa sababu Baba.
John 6:60-63
wanafunzi wengi wa Yesu waliitikia namna gani baada ya kusikia mafundisho ya Yesu juu ya kula mwili wake na kuinywa damu yake?
Wanafunzi waliposikia haya mafundisho wengi wao wakasema, 'Hili fundisho gumu ni nani awezaye kulipokea?" Baada ya hayo, wengi wa wanafunzi wake walirudi nyuma wasiandamane naye.
John 6:64-65
Yesu alifahamu nini kuhusu watu tangu mwanzo?
"Yesu alijua tangu mwanzo yule ambaye asiyeweza kuamini na yeye ambaye angemsaliti".
John 6:66-69
Yesu alipowauliza wale kumi na wawili, "Ninyi hamtaki kuniacho pia, sivyo?, ni nani alijibu na alisema nini?
Simoni Petro alimjibu na alisema, Bwana, wende kwa nani kwani wewe unayo maneno ya uzima wa milele, na tumeamini na kujua kuwa wewe ni Mtakatifu wa Mungu."
John 6:70-71
Yesu alimaanisha nani aliposema mmoja wa wanafunzi wake, kumi na wawili alikuwa shetani?
Yesu alizumngumzia Yuda, mwana wa Simoni Iskarioti; maana yeye ingawaje alikuwa miongoni mwa wale kumi na wawili, alikuwa ndiye ambaye angemsaliti Yesu.
John 7
John 7:1-2
Kwa nini Yesu hakuwa tayari kwenda Uyahudi
Hakuwa tayari kwenda kule kwa sababu watu Wayahudi walitaka kumuua.
John 7:3-4
Kwa nini ndugu zake Yesu walimsihi aende Uyahudi kwenye Sikukuu ya Vibanda?
Walimsihi Yesu kwenda ili kwamba, wanafunzi wa wake wangeweza kuyaona matendo aliyokuwa akiyafanya na ili kwamba ulimwengu ungeweza kujua.
John 7:5-9
Ni sababu gani aliyoitoa Yesu kwa kutotaka kwenda kwenye sikukuu?
Yesu aliwaambia ndugu zake wakati wake ulikuwa haujafika bado na majira yake hayajatimiza bado.
Ni kwa nini ulimwengu humchukia Yesu.
Yesu alisema ulimwengu ulimchukia yeye kwa sababu huushuhudia ulimwengu kuwa matendo yake ni maovu.
John 7:10-11
Lini na jinsi gani Yesu alikwenda kwenye sikukuu?
Yesu alikwenda baada ya ndugu zake kuwa wamekwenda kwenye sikukuu lakini alienda kwa siri na sio hadharani.
John 7:12-13
Makutano ya watu walisemaje kumuhusu Yesu?
Baadhi yao walisema, "Ni mtu mzuri."Wengine walisema, "Hapana, anawapotosha makutano."
Kwa nini hakukuwa na yeyote aliyezungumza juu yake hadharani
Ilikuwa ni kutokana na hofu ya Wayahudi kwamba hakukuwa na mtu aliyezungumza hadhdrani kuhusu Yesu.
John 7:14-16
Ni lini Yesu alipanda kwenda hekaluni na kuanza kufundisha?
Wakati sikukuu ilipofika katikati, Yesu alipanda kwenda hekaluni na kuanza kufundisha
John 7:17-18
Yesu alisemaje ikiwa mmoja angelitaka kujua kama mafundisho yake yanatoka kwa Mungu, au kama Yesu alikuwa anaongea ya kwake mwenyewe?
Yesu alisema kama yeyote anapenda kufanya mapenzi ya mtu aliye mtuma Yesu, angelijua kuhusu mafundisho haya, kama yanatoka kwa Mungu au la.
Yesu alisemaje kuhusu mtu anayetafuta utukufu wa Yeye aliyemtuma?
Yesu alisema kwamba mtu huyo ni mkweli, na ndani yake hakuna kutotenda haki.
John 7:19-22
Kulingana na Yesu, nani anatenda shelia?
Yesu alisema hakuna atendaye sheria.
John 7:23-24
Hoja ya Yesu kwa kuponya katika Sabato ikoje?
Hoja ya Yesu ilikuwa: Nyinyi mtatahiri mtu katika Sabato ili kwamba sheria ya Musa isivujwe. Hivyo kwa nini mnanikasirikia kwa sababu nilimfanya mtu kuwa mzima kabisa katika Sabato.
Yesu aliwaambia watu namna gani?
Yesu aliwaambia wasihukumu kwa kuangalia mwonekano, bali wahukumu kwa haki.
John 7:25-29
Ni ipi mojawapo ya hoja walizozitoa watu kwa kutomwamini Yesu kwamba alikuwa Kristo
Watu walisema walijua Yesu anakotoka, lakini walisema Kristo atakapokuja, walisema hakuna atakayejua.
John 7:30-34
Ni nani aliyetuma maafisa kumkamata Yesu?
Wakuu wa Makuhani na Mafarisayo walituma maafisa kumkata Yesu.
John 7:35-38
Je Wayahudi walielewa kile Yesu alimaanisha aliposema, "Bado muda kidogo niko na ninyi, na kisha nitakwenda kwake aliyenituma. Mtanitafuta lakini hamtaniona; kule niendako hamuwezi kuja."?
Kwa mazungumzo kati yao wenyewe yalionesha kuwa hawakuielewa kauli ya Yesu.
John 7:39-44
Yesu alikuwa akirejea nini aliposema, ikiwa yeyote ana kiu, na aje kwangu na kunywa. Yeyote aniaminiye mimi, kama maadiko yalivyosema, ndani yake kutatoka mito ya maji ya uzima."
Yesu alisema hivi kuhusu Roho, ambaye wale walioamini katika Yeye wangempokea.
John 7:45-49
Maafisa waliwajibuje Makuhani wakuu na Mafarisayo ambao walisema kwao, "kwa nini hamkumleta(Yesu)?"
Maafisa walijibu, "Hakuna mtu ambaye amewahi kuzungumza kama huyu kabla."
John 7:50-53
Nikodemo aliwajibuje Mafarisayo wakati mafarisayo walipoagiza maafisa waliotumwa kumkamata Yesu, "Je ninyi pia mmepotoshwa? Je kuna mmoja kati yenu viongozi aliyemuamini, au mmoja wa Mafarisayo?"
Nikodemo akawaambia Mafarisayo, "Je sheria yetu humhukumu mtu isipokuwa imesikia kwanza kutoka kwake na imejua alichotenda?"
John 8
John 8:1-3
Yesu alipokuwa akifundisha watu hekalu kilitokea Waalimu wa Sheria na Mafarisayo walifanya nini?
Walimletea mwanamke aliyekamatwa katika kitendo cha kuzini. Wakamweka katikati yao na wakamuuliza Yesu alikuwa ana nini cha kusema kuhusu mwanamke huyo (kumhukumu yeye).
John 8:4-6
Kwa nini Waandishi na Mafarisayo hasa walimleta mwanamke huyu kwa Yesu?
Kwa kweli walimleta mwanamke huyu kwa Yesu ili kumtega Yesu ili kwamba wangeweza kuwa na jambo la kumshtaki.
John 8:7-8
Yesu aliwaambia nini Waandishi na Mafarisayo baada ya kuendelea kumuuliza kuhusu mwanamke aliyekamatwa katika uasherati?
Yesu aliwaambia, "Yeye ambaye hana dhambi kati yenu, na awe wa kwanza kutupa jiwe kwa mwanamke."
John 8:9-11
Watu walifanya nini baada ya Yesu kuongea nao kuhusu ambaye anapaswa kuwa wa kwanza kutupa jiwe kwa wanamke aliekamatwa katika uasherati?
Baada ya Yesu kuongea waliondoka mmoja baada ya mwingine, kuanzia mzee na kumalizia na yule wa mwisho.
Yesu alimwambia afane nini yule Mwanamke (aliyekamatwa katika uzinzi)>
Yesu alimwambia kwenda zake na kisha kutotenda dhambi kamwe.
John 8:12-16
Malalamiko ya Mafarisayo yalikuwa nini baada ya Yesu kusema,"Mimi ni nuru ya ulimwengu; yeye anifuataye mimi hatatembe gizani bali atakuwa na uru ya uzima?
Mafarisyo walilalamika kwamba Yesu alikuwa akijishuhudia mwenyewe na kwamba ushuhuda wake haukuwa wa kweli.
John 8:17-22
Yesu aliteteaje ushahidi wake kama kuwa ni mkweli?
Yesu alisema kwamba katika sheria zao imeandikwa kwamba ushuhuda wa watu waili ni kweli. Ndipo akaeleza kwamba yeye na Baba aliye mtuma wote wanashuhudia kuhusu Yesu
John 8:23-24
Ni katika msingi upi Yesu alijenga kauli yake kwamba Mafarisayo wangekufa katika dhambi zao?
Yesu alijenga kauli hiyo juu ya ufahamu wao, kwamba walitoka chini, yeye ametoka juu. walikuwa wa duniani na yeye hakuwa wa dunia hii.
Ni kwa jinsi gani Mafarisayo wangeweza kuepuka kufa katika dambi zao?
Yesu alisema kama hawataamini kuwa MIMI NDIYE wangekufa katika dhambi zao.
John 8:25-27
Yesu alisema nini kwa ulimwengu?
Yesu alima kwa ulimwengu mambo aliyoyasikia kutoka kwa Baba.
John 8:28-30
Kwa nini Baba aliyemtuma Yesu alikaa pamoja naye na asimwache peke yake?
Baba alikaa pamoja na Yesu na hakumwacha peke yake kwa sababu siku zote Yesu alifanya mambo yalikuwa yakimpendeza Baba.
John 8:31-33
Yesu alisemaje Wayahudi ambao waliokuwa wamemwamini wangejuaje walikuwa kweli wanafunzi wake?
Wangejua walikuwa wanafunzi wa Yesu kweli kwa kukaa katika neno lake.
John 8:34-36
Yesu alikuwa anamaanisha nini aliposema, "...na mtaijua kweli na hiyo kweli itawaweka huru?
Yesu alikuwa anamaanish kuwekwa huru kutoka katika kuwa watumwa wa dhambi.
John 8:37-38
Sababu ni ipi, kulingana na Yesu, iliyofanya Wayahudi watake kumuua Yesu?
Walitaka kumuua Yesu kwa kuwa hakuwa na nafasi ndani yao.
John 8:39-41
Kwa nini Yesu alisema hivi Wayahudi walikuwa sio watoto wa Abrahamu?
Yesu alisema walikuwa sio watoto wa Abrahamu kwa sababu hawakufanya kazi za Abrahamu. Badala yake walitaka kumuua Yesu.
John 8:42-44
Wakati hawa Wayahudi wanasema wana Baba mmoja, Mungu, Yesu aliwakanushaje?
Yesu aliwaambia, "Kama Mungu angekuwa Baba yenu, mngenipenda mimi, kwa kuwa nilikuja k na nimetoka kwa Mungu; kwa kuwa sikuja kwa ajili yangu mwenywe, bali alinituma."
Ni nani anayesemwa na Yesu kuwa ni baba wa Wayahudi hawa?
Yesu anasema baba yao ni shetani.
Yesualisema nini kuhusu shetani?
Yesu alisema shetani alikuwa mwuaji tangu mwanzo na hawezi kusimama katika kweli kwa sababu kweli haimo ndani yake. Anapoongea uongo, anaongea kutoka kwenye asili yake kwa sababu ni mwongo na baba wa uongo.
John 8:45-49
Ni nani husikia maneno Ya Mungu?
Yeye aliye wa Mungu husikia maneno ya Mungu.
John 8:50-51
Yesu nasema hutokea nini mtu anapoyashika neno la Yesu?
Iwapo yeyote anayshika maneno ya Yesu, hataona mauti.
John 8:52-56
Kwa nini Wayahudi walisema Yesu alikuwa na pepo?
Walisema hivi kwa sababu Yesu alisema, "Amini, amini, Nawaambia, kama yeyote anashika neno langu, hataonja mauti.
Kwa nini walifikiri kauli ya Yasu juu ya kutoonja mauti kabisa haikuwa ya kawaida?
Walifikiri hivi kwa sababu walifikiri juu ya mauti ya mwili. Hata Abrahanu na manabii walikufa (miili yao inayoonekana)
John 8:57-59
Yesu alieleza nini kusema kwamba alikuwako kabla ya Abrahamu?
Yesu alisema, "Amini, amini, nawaambia, kabla Abrahamu hajazaliwa, MIMI NIKO.
John 9
John 9:1-2
Ni dhana gani linaletwa na wanafunzi kwa swali la kwa nini mtu huyu alizaliwa kipofu?
Wanafunzi walikuwa wakisadi kwamba sababu ya mtu huyo kuzaliwa kipofu in kwa sababu ama mtu huo au wazazi wake walitenda dhambi.
John 9:3-5
Yesu alisema ni nini ilikuwa sababu ya mtu huyo kuzaliwa kipofu?
Yesu alisema mtu huyu alizaliwa kipofu ili kwamba kazi za Mungu ziweze kufunuliwa katika yeye.
John 9:6-7
Yesu alifanya nini na alisema nini kwa mtu kipofu?
Yesu alitema mate aridhini, akafinyanga tope kiasi na akayapaka macho ya mtu huyo kwa udongo. Ndipo Yesu akamwambia yule kipofu nenda ukanawe katika bwawa la Siloamu.
John 9:8-12
Alishuhudiaje yule mtu mabishano yalipozuka juu ya kama alizaliwa kipofu kweli au siyo yeye aliyezowea kuketi chini na kuomba?
Yule mtu alishuhuia ya kuwa alikuwa kipofu mwombaji.
Kilitokea nini baada ya yule mwanaume kipofu kunawa katika bwawa la Siloamu?
Alirudi akiona.
John 9:13-15
Watu waliokuwa na yule aliyakuwa kipofu mwaombaji walifanya nini?
Walimpeleka mtu huyo kwa mafarisayo..
Uponyaji ulitoka lini?
Upaonyaji huyo kipofu ulitokea kwenye Sabato.
Mafarisayo walimuuliza nini yule aliyekuwa kipofu?
Walimuuliza alivyopata kuona.
John 9:16-18
Mgawanyiko gani ambao ulitokea miongoni mwa Mafarisayo?
Baadhi ya Mafarisayo walisema, Yesu hakutoka kwa Mungu kwa sababu hakuitunza Sabato (aliponya siku ya Sabato) na baadhi ya Mafarisayo walisema inawezekanaje mtu ambaye ni mwenye dhambi kufanya ishara ya namna hiyo.
Je! Yule aliyekuwa kipofu alipoulizwa kuhusu Yesu alisemaje?
Mtu aliyekuwa kipofu alisema, "Ni nabii"
Kwa nini Wayahudi waliwaita wazazi wa kipofu ambaye alikuwa amepokea uponyaji?
Waliwaita wazazi wa kipofu kwa sababu bado walikuwa hawajamwamini kuwa yeye kwaeli alikuwa ni yule mtu aliyekuwa kipofu.
John 9:19-21
Wazazi wa yule aliyekuwa kipofu walishuhudiaje kuhusu mtoto wao?
Walishuhudia kwamba mtu huyo alikuwa mtoto wao kweli na kwamba alikuwa amezaliwa kipofu.
wazazi wa yule mtu, walisema hawakujua kitu gani?
Walima hawakujua jinsi gani sasa liweza kuona au macho yake yalifumbuliwaje.
John 9:22-23
Kwa nini wazazi wa mtu huyu walisema, "Yeye ni mtu mzima. Muulizeni."
Walisema hivi kwa sababu walikuwa wanawaogopa Wayahudi. Kwa kuwa Wayahudi walikuwa tayari wamekubaliana kuwa ikiwa mtu yeyote amtakiri Yesu kuwa ni Kristo, atatengwa na synagoge.
John 9:24-25
Mafarisayo walisema nini kwa mtu aliyekuwa kipofu walipomwita mara ya pili?
Walisema, "Mpe Mungu utukufu. Tunamjua mtu huyu (Yesu) ni mwenye dhambi."
Jibu la aliyekuwa kipofu kwa Mafarisaya walipomwita Yesu mwenye dhambi lilikuwaje?
Alijibu akasema, "Awe ni mwenye dhambi, mimi sijui. Kitu kimoja ninachokijua: nilikuwa kipofu, na sasa ninaona."
John 9:26-29
Yule aliyekuwa kipofu aliwauliza swali gani Mafarisayo?
Ayeyekuwa kipofu aliwauliza, "Kwa nini mnataka kusikia tena? Hamtaki kuwa wanafunzi wake pia, sivyo?"
John 9:30-31
Mafarisayo walipomtukana yule aliyekuwa kipofu, huyo aliyekuwa kipofu alisema nini ambacho kila mmoja alikijua?
Mtu aliyekuwa kipofu alisema kwamba kila mmoja alijua yakuwa Mungu hamsikilizi mwenye dhambi
John 9:32-34
Mafarisayo waliitikiaje kwa jibu la ukali l aliyekuwa kipo?
Walimwambia alizaliwa katika dhambi kabisa, na wewe unathubutu kutufundisha sisi. Ndipo walimwamru kutoka ndani ya sinagogi.
John 9:35-38
Yesu alifanya nini aliposikia aliyekuwa kipofu amefukuzwa kutoka kwenye sinagogi?
Yesu alikwenda kumtafuta mtu huyo na akampata.
Yesu alisema nini kwa aliyekuwa kipofu baada ya kumpata?
Yesu alimwambia mtu huyo kama amemwamini Mwana wa Mtu na kisha akamwambia aliyekuwa kipofu kuwa yeye (Yesu) ndiye Mwana wa Mtu.
Yule aliykuwa kipofu aliitikiaje kwa taarifa kwamba Yesu alikuwa Mwana wa Mtu?
Aliyekuwa kipofu alimwambia Yesu, "Naamini," ndipo akamwabudu Yesu.
John 9:39-41
Yesu alisema nini kuhusu dhambi za Mafarisayo?
Yesu aliwaambia, Kama mngelikuwa vipofu, msingelikuwa na dhambi. Hata hivyo, sasa mnasema, 'Tunaona,' dhambi yenu inakaa."
John 10
John 10:1-2
Kwa mjibu wa Yesu mwizi na mnyang'anyi ni nani?
Yeye asiyeingia kwenye nzizi la kondoo, bali anapanda juu kwa njia nyingine, mtu huyo ni mwizi na mnyang'anyi.
Ni nani anayeingia kwaenye zizi la Kondoo kwa kupitia langoni?
Yeye aingiaye mlangoni ni mchungaji wa kondoo.
John 10:3-4
Kwa nini kondoo wanamfuata mchungaji anapo waita?
Wanamfuata mchungaji kwa sababu wanaijua sauti yake.
John 10:5-6
Je! Kondoo watamfuata mgeni?
Hapana. Kondoo hawatamfuata mgeni.
John 10:7-8
Ni nani wale waliomtangulia Yesu?
Wale wote waliomtangulia walikuwa wezi na wanyang'anyi, na kondoo hawakuwasikiliza wao.
John 10:9-10
Yesu alisema alikuwa mlango. Nini hutokea kwa wale waingiao kwa kupitia huo mlango?
Wale waingiao kwa kupitia Yesu, ambaye ni mlango, wataokolewa; wataingia ndani na kutoka na watapata malisho.
John 10:11-13
Ni nini ambacho Yesu, mchungaji mwema, alikuwa tayari kufanya na alifanya nini kwa ajili ya kondoo?
Yesu, mchungaji mwema alikuwa tayari na aliutoa uhai wake kwa ajili ya kondoo.
John 10:14-16
Je! Yesu analo kundi jingine Kondoo divyo kutokee nini kwao.
Yesu alisema anao kondoo wengine ambao si wa zizi hilo. Hao pia, Alisema nilazima kuwaleta, nao wangesikia sauti yake ili kwamba pawepo na kundi moja na mchungaji mmoja.
John 10:17-18
Kwa nini Baba anampenda Yesu?
Baba anampenda Yesu kwa sababu aliutoa uhai wake kwamba aweze kuutwaa tena.
Kuna yeyote anayeweza kuutwaa uhai wa Yesu
Hapana. kama ni kuutoa huutoa mwenyewe.
Yesu alipata wapi mamlaka ya kuyatoa maisha yake na kuyatwaa tena
Yesu alilipokea agizo hilo kutoka kwa Baba yake.
John 10:19-21
Wayahudi walisema nini kwa sababu ya maneno ya Yesu?
Wengi walisema, "Ana pepo na amechanganyikiwa. Kwa nini mnamsikiliza? Wengine walisema, "Haya sio maelezo ya mtu aliyepagawa na pepo. Pepo anaweza kufumbua macho ya kipofu?"
John 10:22-24
Wayahudi walisemaje kwa Yesu walipomzunguka mle hekaluni katika ukumbi wa Selemani?
"Mpaka lini utatuweka katika mashaka? kama wewe ni Kristo, tuambie wazi.
John 10:25-26
Yesu aliwajibuje Wayahudi ndani ya ukumbi wa Sulemani?
Yesu alisema amekwisha waambia (kuwa alikuwa ni Kristo) na hawakumwamini kwa sababu hawakuwa kondoo wake.
John 10:27-28
Yesu anasemaje kuhusu uangalizi wake na ulinzi kwa Kondoo wake?
Yesu alisema huwapa Kondoo wake uzima wa milele; hawataangamia kamwe, na hakuna hata mmoja atakayewanyakuwa kutoka mkononi mwangu.
Kuana yeyote aliyekuu kuliko Baba?
Baba ni Mkuu kuliko wengine wote.
John 10:29-31
Ni nani aliyempa Yesu kondoo?
Baba alimpa Yesu kondoo.
Kuna yeyote aliye mkuu kuliko Baba?
Baba ni mkuu kuliko wengine wote.
John 10:32-33
Kwa nini Wayahudi waliokota mawe kumponda Yesu?
Ni kwa sababu waliamini kuwa Yesu alikuwa anakufuru na kujifanya mwenyewe Mungu ingawaje alikuwa mwanadamu.
John 10:34-36
Yesu alijiteteaje kuhusiana na tuhuma ya kukufuru?
Yesu anajitetea mwenyewe kwa kusema, "Je haikuandikwa katika sheria zenu, 'Nilisema "Ninyi
ni miungu"'? Kama aliwaita wao miungu, kwa yeye neno la Mungu lilikuja (na maandiko hayawezi kuvunjwa), Je mnasema kumuhusu yeye ambaye Baba alimtakasa na kumtuma katika ulimwengu, 'unakufuru,' kwa sababu nilisema, 'Mimi ni mwana wa Mungu'?.
John 10:37-39
Yesu anawaambia Wayahudi wafanye nini ili waweze kuamua kumwamini yeye au kutomwamini?
Yesu anawaambia Wayahudi kuziangalia kazi zake. Ikiwa Yesu hafanyi kazi ya Baba yake, wasimwamini. Ikiwa anafanya kazi ya Baba yake, wamini yeye.
Yesu anawaambia Wayahudi wangeliweza kujua na kuelewa nini kama wangeliiamini kazi aliyofanya Yesu?
Yalisema wangejua na kuelewa kwamba Baba yuko ndani ya Yesu na kwamba Yesu yuko ya Baba.
Itikio la Wayahudi kwa kauli ya Yesu juu ya Baba kuwa ndani ya Yesu na Yesu kuwa ndani Ya Baba lilikuwaje?
Wayahudi walijaribu tena kumkamata Yesu.
John 10:40-42
Yesu alienda wapi baada ya tukio hili?
Yesu alienda tena ng'ambo ya Yordani sehemu ambayo awali Yohana alikuwa akibatiza.
Wale watu wenu waliokuja kwa Yesu walisema nini na kufanya nini?
Waliendelea kusema , "Yohana kweli hakufanya ishara yoyote, lakini mambo yote aliyoyasema Yohana juu ya huyu mtu ni ya kweli." Watu wengi wakamwamini Yesu hapo.
John 11
John 11:1-2
Huyu Lazaro alikuwa ni nani?
Lazaro alikuwa mtu kutoka Bethania. Dada zake walikuwa Mariamu na Martha. Ni Mariamu yule yule atakayempaka Bwana Marhamu na kumfuta kwa nywele zake.
John 11:3-4
Yesu aliposikia kwamba Lazaro ni Mgonjwa alisema nini kuhusu Lazaro na ugonjwa wake?
Yesu alisema , "Ugonjwa huu si wa mauti, lakini, badala yake ni kwa ajili ya utukufu wa Mungu ili kwamba Mwana wa Mungu apate kutukuzwa katika huo Ugonjwa."
John 11:5-7
Yesu aliposikia kwamba Lazaro ni mgonjwa alifanya nini?
Yesu alibaki siku mbili zaidi mahali alipokuwa
John 11:8-9
Wanafunzi wa Yesu walisema nini alipowaambia, "twendeni Uyahudi tena?"
Wanafunzi walimwambia Yesu "Rabi, Wayahudi sasa walijaribu kukuponda mawe, na wewe unarudi tena huko?"
Yesu aliseama nini kuhusu kutembea katika nuru?
Yesu alisema kama mtu anatembea mchana hawezi kujikwaa, kwa sababu anaona kwa nuru ya mchana.
John 11:10-11
Yesu alisemaje kuhusu kutembea mchana na kutembea usiku?
Yesu alisema ikiwa mtu atatembea mchana hatajikwaa kwa sababu anaona kwa nuru ya mchana. Hata hivyo, ikiwa atatebea usiku, atajikwaa kwa sababu nuru haimo ndani yake.
John 11:12-14
Ni kwa namna gani wanafunzi walifikiri kwamba Lazaro amelala?
Wanafunzi wadhani anazungumza juu ya kulala usingizi.
Yesu alimaanisha nini aliposema Lazaro amelala?
Yesu aliposema Lazaro amelala alikuwa akiongelea kifo cha Lazaro.
John 11:15-16
Kwa nini Yesu alifurahi kwamba hakuwepo wakati Lazaro anakufa?
Yesu alisema, " Nina furaha kwa ajili yenu, kwamba sikuwepo pale ili kwamba mpate kuamini.
John 11:17-20
Lazaro alikuwa amekaa kaburini kwa muda gani Yesu alipokuja?
Lazaro alikuwa kaburini kwa siku nne.
Martha alifannya nini aliposikia kwamba Yesu alikuwa anakua?
Martha aliposikia Yesua anakuja alikwenda na kukutana naye.
John 11:21-23
Marthaalifikiri Mungu angefanya kwa ajili ya Yesu?
Martha alisema, "Hata sasa, najua ya kuwa lolote utakaloomba kutoka kwa Mungu, atakupatia".
John 11:24-26
Yesu aliposema kwa Martha, "Kaka yako atafufuka tena," jibu lake lilikuwaje kwa Yesu?
Alisema kwa Yesu, "Najua atafufuka tena wakati wa ufufuo siku ya mwisho."
Yesu alisema kungotokea nini kwa wale waaminio katika yeye?
Yesu alisema kwamba yeye aniaminiye katika Yseu, ingawa atakufa, hata hivyo atakuwa anaishi; na yeye aishiye na mwamini Yesu hatakufa
John 11:27-29
Ushuhuda wa Martha ni upi kuhusu Yesu ni nani?
Martha alimwambia Yesu, "Ndiyo, Bwana, naamini kwamba wewe ni Kristo, Mwana wa Mungu, yeye ajaye ulimwenguni"
Mariamu alikuwa anakwenda wapi?
Mariamu alikuwa anakwenda kukutana nna Yesu
John 11:30-32
Mariamu alipoinuka harakka na kwenda nje, Wayahudi aliokuwapo pale pamoja naye walifikiri nini na kufanya nini?
Wale Wayahudi waliokuwa na Mariamu nyumbani walidhani kuwa anaenda kaburini ili akalie huko kwa hiyo walimfuata.
John 11:33-35
Kinaonekana kilimsukuma Yesu kuhuzunika rohoni na kuhangaika na kulia?
Yesu alihuzunika rohoni na kuhangaika na kulia kwa sababu alimwona Mariamu pamoja na Wayahudi wakilia.
John 11:36-37
Wayahudi walisema nini cha mwisho walipomuona Yesu analia?
Walisema kuwa Yesu alimpenda Lazaro
John 11:38-40
Pingamili la Martht kwa Amri ya Yesu kulitoa jiwe kinywani mwa kaburi ambamo Lazaro alikuwa amelazwa lilikuwaje?
" Martha alisema, "Bwana, kwa muda huu, mwili utakuwa umeoza, kwa sababu amekwishakuwa maiti kwa siku nne."
Jibu la Yesu kwa pingamizi la Yesu kulitoa jiwe likoje?
Yesu alimwambia Martha, "Mimi sikukuwaambia ya kwamba, kama ukiamini, utauona utukufu wa Mungu?"
John 11:41-44
Yesu alifanya nini kwa haraka baada ya jiwe kuwa limeondolewa kutoka kwenye kaburi?
Yesu aliinua juu macho yake na kuomba kwa sauti kwa Baba yake.
John 11:45-48
Nini jibu la Wayahudi walipomwona Lazaro akitoka kaburini?
Wengi miongoni mwa Wayahudi walipoona alichokifanya Yesu walimwamini, lakini wengine wakaenda kwa Mafarisayo na kuwaambia kile alichokifanya Yesu.
John 11:49-50
Kwenye kikao cha Halmashari ya Kuhani Mkuu na Mafarisayo Kayafa alitabiri nini?
Kayafa alisema kwamba yafaa kwa ajili yao kwamba mtu mmoja yapasa kufa kwa ajili ya watu kuliko taifa lote kuangamia."
John 11:51-53
Tangu siku hiyo na kuendelea baraza lilipanga kufanya nini?
Walipanga jinsi ya kumuua Yesu
John 11:54-55
Yesu alifanya nini baada ya kumfufua Lazaro?
Hakutembea tena wazi wazi kati ya Wayahudi, bli aliondoka kutoka Bethania kwenda nchi iliyokuwa karibu na jangwa katika mji uitwao Efraimu. Huko alikaa na wanafunzi wake.
John 11:56-57
Je! Wakuu wa Makuhani na Mafarisyo walitoa amri gani?
Walitoa aamri kwamba mtu yeyote alipajua mahali alipokuwa Yesu, ilimpasa kutoa taarifa ili kwamba wangemkamata.
John 12
John 12:1-3
Ni lini Yesu alirudi Bethania?
Alikuja Bethania siku sita kabla ya Pasaka.
Mariamu alifanya nini kwenye chakula cha jioni kilichokuwa kimeandaliwa kwa ajili Yesu>
Mariamu alichukua ratli ya manukato yaliyotengenezwa kwa nardo safi, yenye thamani kubwa, akampaka Yesu miguuni, na kumfuta miguu kwa nywele zake;
John 12:4-6
Kwanini Yuda Iskariote alilalamika kwamba manukato yangeuzwa na fedha kupewa maskini?
Yuda alisema haya, sio kwasababu aliwahurumia maskini, bali kwasababu mwizi: Yeye ndiye aliyeshika mfuko wa fedha na alikuwa akichukua baadhi kwa ajili yake mwenyewe.
John 12:7-8
Jinsi gani Yesu amlitetea Mariamu alipotumia manukato ya Nardo?
Yesu alisema, "Mwache aweke alicho nancho kwa ajili ya siku ya maziko yangu. Maskini mnao siku zote; lakini hamtakuwa nami siku zote."
John 12:9-11
Kwanini umati mkubwa wa watu ulikusanyika kule Bethania?
Walikuja kwa ajili ya Yesu na pia kumuona Lazaro, ambaye Yesu alimfufua kutoka kwa wafu.
John 12:12-13
Makutano walifanya nini waliposikia kwamba Yesu alikuwa nakuja?
Walichukua matawi ya miti ya mitende na kutoka nje kwenda kumlaki na wakapiga kelele, "Hosana! Amebarikiwa yeye ajaye kwa jina la Bwana, Mfalme wa Israeli."
John 12:14-15
Ni unabii gani kumhusu Yesu ulitimizwa Yesu alipoingi mjini akiwajuu ya Punda?
Unabii kwamba usiogope, binti Sayuni; tazama, Mfalme wako anakuja, amepanda mwana-punda ulitimizwa."
John 12:16
Ni mambo gani ambayo wanafunzi wa Yesu hawakuyaelewa hapo awali lakini baada ya Yesu kutukuzwa walikumbuka ya kuwa walimtendea hayo?
Wanafunzi walikumbuka kuwa aliandikiwa Yesu, "Usiogope ewe binti Sayuni, tazama, mfalme wako anakuja, amekaa juu ya mwana punda."
John 12:17-22
Kwanini mkutano ule katika sikukuu ulitoka kwenda kumlaki Yesu?
Walienda kumlaki Yesu kwasababu walikuwa wamesikia kutoka kwa mashahidi wa macho kuwa Yesu alimuita Lazaro kutoka kaburini na ya kuwa alimfufua kutoka katika wafu.
John 12:23-24
Yesu alisema nini baada ya Andrea na Filipo kumwambia kuwa baadhi ya Wayunani wanataka kumuona?
Yesu aliwajibu na kusema, "Saa imefika kwa ajili ya Mwana wa Mtu kutukuzwa..."
Yesu alisema kungetokea nini kwa chembe ya ngani kama ikianguka katika nchi na kufa?
YEsu aalisema kwamba kama ikifa, ingezaa matunda mengi.
John 12:25-26
Ni kitu gani Yesu alisema kingetokea kwa mtu anayependa maisha yake hapa duniani na kwa yule ambaye anayachukia maisha yake?
Yseu alisema kuwa yule apendaye maisha yake atayapoteza, bali yeye achukiaye maisha yake hapa duniani atayasalimisha hata uzima wa milele.
Hutekea nini iwapo yeyote ananmtumikia Yesu?
Baba atamheshi yeye.
John 12:27-29
Kilitokea ni Yesu aliposema, Baba, ulitukuze lako?
Sauti ikaja kutoka mbinguni na kusema, "Nimelitukuza nami nitalitukuza tena."
John 12:30-31
Yesu alisema sauti kutoka mbinguni ilikuwa na sababu gani?
Yesu alisema, "Sauti haikuja kwa ajili yangu bali kwa ajili yenu (Wayahudi)."
Yesu alisema kulikuwa kunakwenda kutokea nini?
Yesu alijibu na kusema, "Sauti hii haikuja kwa ajili yangu, bali kwa ajili yenu. Sasa hukumu ya ulimwengu huu ipo: Sasa mkuu wa ulimwngu huu atatupwa nje.
John 12:32-33
Kwa nini Yesu alisema, Nami nikiinuliwa juu ya nchi, nitawavuta wote kwangu."
Aliyanena hayo akionesha ni mauti gani atakayokufa.
John 12:34-36
Makutano walipouliza, "Utaseamaje, ni lazima Mwana wa Mtu ainuliwe juu?" , Je! aliwajibu moja kwa moja?
Hapana halijibu swali lao moja kwa moja.
Yesu alisemaji kuhusu nuru?
Yesu alisema, "Nuru ingalipo pamoja nanyi muda kidogo. Enendeni maadamu mnayo nuru, ili kwamba giza lisije likawaweza. Yeye aendaye gizani hajui aendako. Mngali mnayo nuru, Iaminini nuru hiyo ili mpate kuwa wana wa nuru."
John 12:37-38
Kwanini watu hawakumwamini Yesu?
Hawakumwamini ili kwamba neno la nabii Isaya iliweze kutimizwa, linalosema: "Bwana, ni nani aliyesadiki habari zetu? Na mkono wa Bwana amefunuliwa nani?"
John 12:39-40
Kwanini watu wasingemwamini Yesu?
Wasingemwamini kwasababu kama Isaya alivyosema, "Amewapofusha macho yao, na ameifanya migumu mioyo yao; wasije wakaona kwa macho yao na wakafahamu kwa mioyo yao, na wakaongoka nami nikawaponya."
John 12:41-43
Kwanini Isaya aliyasema mambo haya?
Aliyasema mambo haya kwasababu aliuona utukufu wa Yesu.
Ni kwanini wakuu walioamini hamkiri
Hawakukiri ili wasije wakatengwa na sinagogi. Walipenda sifa za wanadamu kuliko sifa zitokazo kwa Mungu.
John 12:44-45
Yesu alisema maneno gani juu yake na Baba yake?
Yesu alisema, "Yeye aniaminiye mimi, haniamini mimi tu bali na yeye aliyenituma mimi, naye anionaye mimi anamuona yeye aliyenituma."
John 12:46-47
Yesu alisema alikuwaja ulimwenguni kufanya nini?
Yesu alisema alikuja kuuokoa ulimwengu
John 12:48-50
Ni nini kitawahukumu wale wote wanaomkataa Yesu na wasiopokea maneno yake?
Neno ambalo Yesu amelisema litawahukumu wale wote waliomkataa siku ya mwisho.
Je, Yesu alinena kwa nafsi yake mwenyewe?
Hapana. Baba aliyemtuma Yesu alimwagiza kuhusu yale atakayoyanena na atakayosema.
Ni kwanini Yesua aliwaambia watu "kama Baba alivyoniambia, ndivyo ninenavyo kwao?"
Yesu alisema hivi kwa sababu agizo la Baba yake ni uzima wa milele.
John 13
John 13:1-2
Ni kwa urefu gani Yesu aliwapenda watu wake?
Aliwapenda hata upeo.
Ibilisi alifanya nini kwa Yuda Iskariote?
Na ibilisi alikuwa ameweka katika moyo wa Yuda Isikariote, mwana wa simoni, kumsaliti Yesu.
John 13:3-5
Baba ameweka nini kwa Yesu?
Baba aliweka vitu vyote mikononi mwa Yesu.
Yesu alitok wapi na wapi alikokuwa anakwenda?
Yesu alikuwa alitoka kwa Mungu na likuwa nanakwenda Mungu.
Yesu alifanya nini alipoamka chakulani?
alikaweka chini vazi lake la nje. Kisha alichukua taulo na akajifunga mwenyewe.
John 13:6-9
Yesu alisema nini Petro alipokataa kuoshwa miguuu yake?
." Yesu alisema, "Ikiwa sitakuosha, hutakuwa na sehemu pamoja nami."
John 13:10-11
Ni kwa nini Yesu alisema kwa wanafunzi wake, "Mmekuwa safi, lakini si nyote."
Yesu aalisema hivi kwa sababu alijua ni nani angemsaliti yeye
John 13:12-15
Kwa nini Yesu alionysha miguu ya wanafunzu ?
Yesu aliosha miguu ya wanafunzi kwa sababu alitaka kuwapa mfano ili kwamba nao wafanye kama yeye alivyofanya kwao.
John 13:16-18
Je mtumwa ni mkuu kuliko bwana wake au yule aliyetumwa ni kuu kuliko yule aliyemtuma?
Mtumwa si mkuu kuliko bwana wake; wala yule ambaye ametumwa ni mkuu kuliko yule aliye mtuma.
Ni nani aliyeinua kisigino chale dhidi yake.
'Yeye aliyekula mkate wa Yesu aliinulia kisigino chake dhidi Yake.
John 13:19-22
Kwa nini Yesu aliwaambia wanafunzi wake, "Si wote mliosafi" na "Yeye alaye mkate wangu ameniinulia kisigino chake.'
Yesu aliwambia hili kabla halijatokea ili kwamba litakapotokea, wangeweze kuamini kuwa yeye ndiye yule MIMI NDIYE.
Ukimpokea Yesu kama utampokea Yesu?
KIpokea Yesu tampokea yeyote anayemtuma, na ukimpoke Yesu pia utampokea yule aliyemtuma Yesu."
John 13:23-25
Yesu alipowaambia wanafunzi wake kwamba mmoja wao angemsaliti yeye, Simoni Petro alifanya nini?
Simoni Petro alimuuliza mwanafunzi yule amabaye Yesu alimpenda na alisema, "Twambie ni yupi ambaye anazungumzia."
John 13:26-27
Yesu alijibuje mwanafunzi aliyempenda Yesu alipomuuliza Yesu ni nani aliyekuwa anataka kumsaliti Yesu?
Yesu alijibu, "Ni yule nitakaye chovya kipande cha mkate na kumpatia." Kisha Yesu alichovya mkate na alimpa Yuda mwana wa Simon Iskariote.
John 13:28-30
Kulitokea nini kwa Yuda na alifanya nini baada ya Yesu kumpa Yuda mkate?
Baada ya Yuda kuupokea mkate, alitoka nje haraka
John 13:31-33
Mungu alikuwa atukuzwaje?
Mungu alikuwa alikuwa anakwenda kutukzwa ndani ya Mwana wa Adamu. Mwana wa Adamu alipotukuzwa hilo lilimtukuza Mungu.
Je! Simoni Petro alielewa mahali Yesu alipokuwa akienda wakati Yesu alipowaambi. "Niendako Mimi hamwezi kuja?"
Hapana. Simoni hakuelewa kwa sababu alimwuliza Ysu, "Bwana,unakwenda wapi?"
John 13:34-35
Ni amri gani mpya Yesu aliyowapa wanafunzi wake?
Amri mpya ilikuwa kwamba wapate kupendana wao kwa wao kama vile Yesu amewapenda wao.
Yesu alisema kungetokea nini kama wanafunzi wangetii amri ya kupendana wao kwa wao?
Yesu alisema kwamba kutokana na kuitii amri hii, watu wote wangetambua ya kwamba walikuwa wanafunzi wake.
John 13:36-38
Yesu alimjibuje Simoni Petro aliposema, "Nitayatoa maisha yangu kwa ajili yako?
Yesu alijibu, "Je utayatoa maisha yako kwa ajili yangu? Amini amini nakwambia, jogoo hatawika kabla hujanikana mara tatu."
John 14
John 14:1-3
Ni kwa nini myoyo ya wanafunzi isiwe na mahangaiko?
Myoyo yawanafunzi isihangaike kwa sababu Yesu anakwenda kuwaandalia mahali na Yesu atakuja tena kuwakaribisha kwake mwenyewe ili kwamba Yesu alipo na wao wawepo pia.
Nyumbani kwa Baba kuna nini?
Nyumbani mwa Baba mna makazi mengi.
Yesu alikuwa anakwenda kufanya nini kwa ajili ya wanafuzi?
Yesu alikuwa anakwenda kuandaa mahali kwa ajili yao.
John 14:4-7
Njia pekee ya kuja kwa Baba ni ipi
Njia pekee ya kuja kwa Baba ni kwa kupitia Yesu.
John 14:8-9
Filipo alimwambia Yesu afanye nini ambacho kingetosha kwa ajili ya wanafunzi?
Filipo anamwambia Yesu, "Bwana, tuonyeshe Baba, na hivyo itakuwa imetutosha."
John 14:10-11
Je! Yesu anasema kwa wanafunzi juu yake mwenyewe?
Hapana Yesu hazungumzii habari zake mwenyewe, badala yake, ni Baba akaaye ndani Yake anayeifanya kazi ya Baba.
Kama siyo kwa sababu nyingine, kwa nini Yesu anawaambia wanafunzi yawapasa kuamini kwamba Yesu yumo ndani ya Baba na Baba yumo ndani ya Yesu?
Yesu alisema ni lazima waamini hivi kama siyo kwa sababu nyingine basi ni kwa sababuya kazi za Yseu hasa.
John 14:12-14
Ni kwa nini Yesu alisema wanafunzi wataweza kufanya hata kazi kuliko zile alizofanya yeye?
Yesu anasema wanafunzi watafanya kazi kubwa kwa sababu Yesu anakwenda kwa Baba>
Kwa nini Yesu atafanya lolote watakaloomba wanafunzi katika jina lake?
Yesu atafanya ili kwamba Baba aweze kutukuzwa katika Mwana.
John 14:15-20
Yesu anasema utafanya nini kama utazipenda amri zake?
Yesu anasema utazishika amri zake kama unampenda Yeye.
Ni nani Yesu anamwita mfariji mwingine ambaye Baba atawapa wanafunzi ili kuwa nao milele?
Yesu anamwita Roho wa Kweli
Kwani nini ulimwengu hauwezi kumpokea Roho wa Kweli?
Ulimwengu hauwezi kumpokea Roho wa Kweli kwa sababu haumwoni au kumjua yeye.
Ni wapi Yesu alisema atakuwa huyo Roho wa Kweli?
Yesu alisema Roho wa Kweli angekaa ndani ya wanafunzi.
John 14:21-24
Kutatokea nini kwa yeyote aliye na amari za Yesu na kuzishika?
Watu wale watapendwa na Yesu na Baba yake na Yesu mwanyewe atajifunua kwa watu hao.
John 14:25-27
Yule mfariji,Roho Mtakatifu atafanya nini atakapotumwa na Baba?
Mfariji, Roho Mtakatifu atawafundisha wanafunzi mambo yote na atawafanya wakumbuke yote ambayo Yesu aliyasema kwao.
John 14:28-31
Kwa nini ni lazima wafuzi wengefurahi kwamba Yesu alikuwa anaondoka?
Yesu alisema ilipasa wafurahi kwa sababu Yesu alikuwa anakwenda kwa Baba na kwamba Baba ni mkuu kuliko Yesu.
Ni sababu gani Yesu anatoa kwa kusema hatasema mengi na wanafunzi wake?
Sababu anayoita Ysu ni kwamba mkuu wa dunia hii anakuja.
John 15
John 15:1-2
Mzabibu wa kweli ni nini?
Yesu ndiye mzabibu wa kweli
Mkulima wa mzabibu ni nani?
Baba ndiye mkulima wa mzabibu.
Baba hufanya nini kwa matawi walio katika Yesu?
Baba huyaondoa matawi yasiyozaa matatunda na husafisha kila tawi lizaalo matunda ili lizidi kuzaa matunda zaidi.
John 15:3-4
Ni kwa nini wanafunzi wako safi?
Wako safi kwa sababu kwa sababu ya ujumbe ambao Yesu aliwaambia
John 15:5-7
Matawi ni nani?
Sisi tu matawi
Ni lazima tufanyanye nini ili kuzaa matunda?
Ili kuzaa matunda ni lazima ukae ndani ya Yesu.
Hutokea nini kama hukai ndani ya Yesu.
ikiwa yeyote hakai ndani ya yesu, huyo hutupwa kama tawi na hunyauka.
Ni lazima tufanye nini ili kwamba kila tuombalo lifanyike kwa ajili yetu?
inatupasa kukaa ndani ya Yesu na neno lake lazima likae ndani yetu. Baadaye tunaweza kuomba lolote tupendalo nalo litafanyika kwa ajili yetu.
John 15:8-9
Ni katika njia gani mbili amabazo Baba hutukuzwa?
Baba hutukuzwa tunapozaa matunda mengi na tupofnyika wanafunzi wa Yesu.
John 15:10-11
Ili tubaki katika pendo la Yesu itatupasa tufanyaje?
Ni lazima tuzishike amri zake.
John 15:12-13
Ni pendo gani kuu analoweza kuwa nalo mtu?
Hakuna mtu aliye na upendo mkuu kuliko huu, kwamba ayatoe maisha yake kwa ajiliya rafiki zake.
John 15:14-17
Tunapataje kutambua kama tu marafiki wa Yesu au la?
Sisi tu mafariki za Yesu kama tunafanya mambo aliyotuamru.
Kwa nini Yesu aliwaita wanafua rafiki zake?
Aliwaita rafiki, kwa sababu kwa sababu alifunua kwao mambo yote aliyoyasikia kutoka kwa Baba.
John 15:18-22
Ni kwa nini ulimwengu huwachukia wale wanaomfuata Yesu kwasababu?
Ulimwengu huwachukia wanaomfuata Yesu kwasababu wao sio wa ulimwengu huu na kwa sababu aliwachagua kutoka ulimwenguni.
John 15:23-25
Yesu alifanya nini kiasi kwamba ulimwengu hauna udhuru?
Ulimwengu hauna udhuru kwa dhambi yao kwa sababu Yesu alikuja na kuteda akazi miongoni mwao amabayo hapana hata mmoja wao aliyefanya pia.
John 15:26-27
Nani atakayemshuhudia Yesu?
Yule Mfariji, ambaye ni Roho wa Kwali, na wanafunzi wa Yesu watamshuhudia Yesu.
Kwa nini wanafunzi watamshuhudia Yesu?
Wangemshuhudia Yesu kwa sababu wamkuwa pamoja naye tangu mwanzo.
John 16
John 16:1-2
Kwa nini Yesu aliongea haya kwa wanafunzi wake?
Yesu aliongea haya kwao ili wasiwe na mashaka.
John 16:3-4
Kwa sababu gani watu watawato wanafunzi wa Yesu ndani ya masinagogi na kuwaua baadhi yao?
Watawafanyia haya kwa sababu hawamfahamu Baba wala Yesu.
Kwa nini basi Ysu hakuwaambia haya tangu mwanzo?
Yesu hakuwambia mwanzoni kwa sababu alikuwa pamoja nao.
John 16:5-7
Kwa nini ni vema Yesu aondoke?
Ni vema Yesu aondoke kwa sababu Mfariji hatakuja kwao isipokuwa Yesu Yesu ameondoka. Yesu atamtuma Mafariji kwao.
John 16:8-11
Kuhusu jambo gani mfariji atauhukumu ulimwengu?
Mfariji atauhukumu ulimwengu kutokana na dhambi, haki na hukumu.
John 16:12-14
Mfariji atakapokuja atafanya nini kwa wanafunzi?
Atawaongoza wanafunzi katiak kweli yote, kwa sababu hatanena kwa ajili yake; lakini yoyote atakayoyasikia, atayasema mambo hayo; na atayadhihirisha kwao mambo yatakayokuja.
Huyo Roha wa Kweli atamtukuza nani?
Atamtukuza Yesu kwa kuyachukua mambo ya Yesu na kuyatangaza kwa wanafunzi.
John 16:15-16
Ni mambo gani ya Yesu ambayo Roho wa kweli atayachukua?
Roho wa kweli atachukua mambo ya Baba. Yote aliyonayo Baba ni ya Yesu pia.
John 16:17-18
Ni misemo gani ya Yesu ambayo wanafunzi hawakuielewa
Hawakuelewa Yesu aliposema, "Bado muda mfupi, hamtaniona tena; na baada ya muda mfupi tena, mtaniona." Na aliposema, "kwa sababu naenda kwa Baba?"
John 16:19-21
Kitatokea nini kwa huzuni ya Wanafunzi?
Itageuzwa kuwa furaha
John 16:22-25
Kipi kitatokea na kuwasababisha wanafunzi wafurahie?
Watamuona tena Yesu na mioyo yao itafurahi.
John 16:26-31
Ni kwa sababu gani Baba aliwapenda wanafunzi wa Yesu?
Baba anawapenda wanafunzi wa Yesu kwa sababu wanafunzi walimpenda Yesu na waliamini kwamba ametoka kwa Baba.
Yesu alitoka wapi na alikuwa anakwenda wapi?
Yesu alikuja ulimwenguni kutka kwa Baba na alikuwa anaondoka ulimwenguni na kurudi kwa Baba.
John 16:32-33
Ni kitu gani Yesu aliwaambia wanafunzi wanapaswa kufanya kwa wakati huo?
Yesu aliwaambia wanafunzi wake kuwa watatawanyija, kila mtu na kwao, na watamuacha Yesu peke yake.
Nani atabaki na Yesu baada ya wanafunzi wake kumuacha?
Baba ataendelea kuwa na Yesu.
Kwa nini Yesu aliwaambia wanafunzi wake kujipa moyo hata kama wangekuwa na matatizo?
yesu aliwaambia wajipe moyo kwa sababu yeye ameushinda ulimwengu.
John 17
John 17:1-2
Kwa nin Baba alimpa Yesu mamlaka yote juu ya wot wenye mwili?
Baba alifanya hivi kwa ili kwamba awape uzima wa milele wale wote ambao umenipa.
John 17:3-5
Uzima wa milele ni nini?
Uzima wa milele ni kumjua Baba, Mungu pekee wa Kweli, na yeye uliye mtuma, Yesu Kristo.
Ni jinsi gani Jesu alimtukuza Mungu duniani?
Alifanya hivi kwa kukamilisha kazi ambayo Baba alimpa kuifanya.
Ni utukufu gani Yesu anaoutaka?
Hule utkufu anaoutaka ni ule ambao alikuwa nao alipokuwa na Baba kabla ya ulimwangu kuumbwa.
John 17:6-8
Yesu alaimfunulia nani jina la Baba?
Yesu aliwafunulia jina la Baba watu aliopewa na Mungu toka Ulimwenguni.
Wale watu ambao Baba amewabidhi kwa Yesu waliyaitikiaje maneno ya Yesu?
Waliyapokea maneno ya Yesu na habari za kweli kwamba Yesu alikuja kutoka kwa Baba na waliami kwamba Baba alimtuma Yesu.
John 17:9-11
Yesu alisema hawaombei watu gani?
Yesu alisema hauombei ulimwengu
Kwa kifupi Yesu anamwomba nini Baba kwa ajili ya wale ambao Baba alimkabidhi Yesu?
Yesu anamwomba Baba kuwatunza hao katika jina la Baba ili wawe mmoja, kuwalinda kutokana na yule mwovu, awaweke katika kweli, na kisha wawe katika Yesu na Baba na kuwa nao wale ambo Baba amempa kuwa nao mahali atakapokuwa.
John 17:12-14
Yesu alipokuwa ulimwenguni, aliwafanyia nini watu ambao baba alikuwa amempa?
Yesu aliwalinda
John 17:15-17
Kwa kifupi Yesu anamwomba nini Baba kwa ajili ya wale ambao Baba alimkabidhi Yesu?
Yesu anamwomba Baba kuwatunza hao katika jina la Baba ili wawe mmoja, kuwalinda kutokana na yule mwovu, awaweke katika kweli, na kisha wawe katika Yesu na Baba na kuwa nao wale ambo Baba amempa kuwa nao mahali atakapokuwa.
John 17:18-19
Kwa nini Yesu anajitoa kwa Mungu?
Yesu anajito mwenyewe ili kwamba wale ambao Baba ampa nao waweze kujitoa kwa kweli.
John 17:20-23
Yesu anawaombia watu gani tena?
Yesu anawaombea watu watakaomwamini kupitia neno la wale waliokuwa wamemfuata wakati huo.
Kwa kifupi Yesu anamwomba nini Baba kwa ajili ya wale ambao Baba alimkabidhi Yesu?
Yesu anamwomba Baba kuwatunza hao katika jina la Baba ili wawe mmoja, kuwalinda kutokana na yule mwovu, awaweke katika kweli, na kisha wawe katika Yesu na Baba na kuwa nao wale ambo Baba amempa kuwa nao mahali atakapokuwa.
John 17:24
Kwa kifupi Yesu anamwomba nini Baba kwa ajili ya wale ambao Baba alimkabidhi Yesu?
Yesu anamwomba Baba kuwatunza hao katika jina la Baba ili wawe mmoja, kuwalinda kutokana na yule mwovu, awaweke katika kweli, na kisha wawe katika Yesu na Baba na kuwa nao wale ambo Baba amempa kuwa nao mahali atakapokuwa.
John 17:25-26
Ni kwa nini Yesu alilifanya la Baba kujulikana na ataendele kulifanya lijulikane kwa wale ambao Baba amempa yeye?
Yesu alifanya hivyo na ataendelea kulifanya lijulikane ili kwamba lile pendo ambalo kwalo alimpenda Yesu liweze kuwa ndani yao, na Yesu aweze kuwa ndani yao.
John 18
John 18:1-3
Baada ya Yesu kusema maneno haya alikwenda wapi?
Aliondoka na wanafunzi wake kueleke Kidroni kwenye ile bustani na akaingia ndani yake.
Yuda alijuaje kuhusu bustani?
Alilijua eneo hilo, kwani Yesu alikuwa akienda hili eneo mara kadhaa akiwa na wanafunzi wake.
Nani mwingine alikuja pamoja na Yuda bustanini wakiwa na taa, mienge na silaha?
Yuda, kundi la maaskari na maofisa kutoka kwa wakuu wa makuhani wakuu, walikuja bustanini wakiwa na taa, mienge na silaha.
John 18:4-5
Yesu aliwaulizaje wale kundi la watu waliokuwa bustanini?
Ni nani mnayemtafuta?
John 18:6-7
Kilitokea nini wakati lile kundi la watu liliposema kuwa walikuwa wakimtafuta Yesu wa Nazareth na Yesu alipojibu, " Mimi ndiye."?
Wale askari na wale waliokuwa pamoja nao wlirudi kinyume na kuanguka chini.
John 18:8-9
Kwa nini Yesu alisema, "Nimewaambieni kuwa mimi ndiye; kwa hiyo kama mnanitafuta mimi waacheni hawa waende."?
Yesu alisema hivyo ili kwamba neno litimilike, lile neno lisemalo; "katika wale ulionipa, sikumpoteza hata mmoja,"
John 18:10-11
Yesu alimwambia nini Petro baada ya Petro kumkata sikio Malikusi, mtumish wa Kuhani Mkuu?
Yesu alimwambia Petro. "Rudisha upanga wako kwenye ala yake. Kwa nini nisikinywee kikombe kile alichonipa Baba?"
John 18:12-14
Baada ya lile kundi la askari na jemedari, na watumishi wa Wayahudi kukamata Yesu na kumfunga na walimpeleka wapi?
kwanza walimpeleka kwa Anasi
Anasi allikuwa nani?
Anasi alikuwa mkwewe Kayafa, ambaye alikuwa kuhani mwaka huo.
John 18:15-16
Je, Petro aliwezaje kuingia kwenye ukumbi wa Kuhani Mkuu?
Mwanafunzi aliyekuwa akifahamika kwa kuhani mkuu, alitoka nje akaenda kuongea na yule mwanamke mtumishi aliyekuwa akilinda mlango na kumwingiza Petro ndani.
John 18:17-18
Ni nani aliyemwuliza Petro kama naye alikuwa mwanafunzi wa Yesu au naye alikuwa na Yesu?
Yule mwanake kijakazi aliyekuwa akilinda mlango wa ukumbi, mmoja wa wale watu waliokuwa wamesimama kuuzunguka moto wa mkaa na mmoja wa watumishi wa kuhani mkuu, aliyekuwa ndugu wa yule mtu ambaye Petro alimkata sikio, wote walimwuliza Petro kama yeye naye alikuwa mwanafunzi wa Yesu au alikuwa na Yesu.
John 18:19-21
Kwa kifupi, Yesu alijibuje wakati Kuhani mkuu alipomwuliza Yesu juu ya wanafunzi wake na mafundisho yake?
Yesu alimjibu kuwa yeye aliufundisha ulimwengu waziwazi hadharani. Akamwambia Kuhani mkuu awaulize wale waliomsikia yeye juu ya kile alichosema
John 18:22-24
Baada ya Anasi kumuuliza Yesu maswali alimpeleka wapi
Anasi alimpeleka Yesu kwa Kayafa Kuhani Mkuu.
John 18:25-27
Baada ya Petro kukana kuhusishwa na Kristo mara tatu mara kukatokea nini?
Mara Jogoo akawika baada ya Petro kukana kuhusishwa na Kristo mara ya tatu .
John 18:28-30
Kwa nini wale waliompeleka Yesu kwenye Praitorio hawakuingia nadani yake?
Hawakuingia ndani ya Praitorio ili wasije wakanajisika kiasi cha kutoila Pasaka.
John 18:31-32
Kwa nini Wayahudi walimpeleka Yesu kwa Pilato badala ya wao wenyewe kumwadhibu?
Ni kwa sababu Wayahudi walitaka kumwua Yesu na wao hawakurusiwa kisheria kumuua mtu yeyote bila ruhusa toka mamlaka ya Kirumi
John 18:33-35
Pilato alimwuliza nini Yesu?
Pilato alimwuliza Yesu kama yeye alikuwa mfalme wa Wayahudi, pia alimwuliza Yesu alichokuwa amekifanya.
John 18:36-37
Yesu alimwambiaje Pilato juu ya Ufalme wa Yesu?
Yesu alimwambia Pilato kuwa Ufalme wake si sehemu ya ulimwengu huu na hautokani na Ulimwengu huu.
Ni kwa kusudi gani Yesu alizaliwa?
Yesu alizaliwa kuwa Mfalme
John 18:38-40
Hukumu ya Pilato juu ya Yesu baada ya kuongea naye ilikuwaje?
Pilato aliwaambia Wayahudi kuwa, "Sijaona Kosa lolote kwa mtu huyu"
Pilato alipopendekeza kumfungulia Yesu, Wayahudi walipiga kelele kusemaje kwa Pilato?
Wayahudi walipiga kelele tena wakisema, siyo huyu, tufungulie Baraba."
John 19
John 19:1-3
Askari walimtendea nini Yesu baada ya Pilato kumchapa mijeredi Yesu?
Wale maaskari walisokota miiba na kutengeneza taji. Wakaiweka juu ya kichwa cha Yesu na kumvalisha vazi la rangi ya zambarau. Wakamjia na kusema, "Wewe mfalme wa Wayahudi! na kisha kumpiga kwa mikono yao.
John 19:4-6
Kwa nini Pilato alimtoa Yesu nje kwa Wayahudi tena?
Pilato alimtoa Yesu nje kwa watu ili wajue kuwa Pilato hajaona kosa kwa Yesu.
Yesu alikuwa amevaa nini Palato alimrusha tena nje kwa watu?
Yesu alikuwa amevaa taji ya miiba na vazi la zambarau
Wakuu wa Makuhani wa Maofisa walisema nini Yesu?
Wlipiga kelele na wakasema., "Msurlibishe, Msulibishe!"
John 19:7-9
Wayahudi walisema kitu gani ambacho kilimfanya Pilato aogope zaidi?
Wayahudi walimwambia Pilato kuwa, "Sisi tunayo sheria, na kwa sheria hiyo inampas kufa kwa sababu yeye alijifanya mwenyewe Mwana wa Mungu."
Pilato alipomuuliza Yesu, "Wewe unatoka wapi?", Yesu alisemaje?
Yesu hakumjibu Pilato.
John 19:10-11
Yesu alisema ni nani yaliyempa Pilato mamlaka juu ya Yesu?
Yesu alisema, "Usingekuwa na uwezo dhidi yangu kama usingepewa toka juu.
John 19:12-13
Ijapokuwa Pilato alitaka kumwacha Yesu huru, Wayahudi walisema kitu gani kilchomzuia Pilato?
Wayahudi walipiga kelele wakisema, "Kama utamwacha huru, basi wewe si rafiki wa Kaisari: Kila ajifanyaye kuwa mfalme humnenea kinyume Kaisari."
John 19:14-16
Ni jambo gani la mwisho wakuu wa makuahani walisema kabla Pilato hamkabidhi kwao Yesu ili asulibiwe?
Makuu wa Makuhani walisema, "Sisi hatuna mfalme isipokuwa Kaisari."
John 19:17-18
Yesu walimsulibisha Wapi?
Yesu walimsulibisha Golgotha, maana yake fuvu la kichwa
Je! Ni yesu peke yake aliyesulibiwa siku hiyo?
Hapana. Kuna wanaume wengine wawili waliosulibiwa pamoja naye, mmoja upande huu na mwingine upande huu.
John 19:19-22
Pilato aliandika nini kwenye bango ambalo liliwekwa kwenye msalaba wa Yesu
Kwenye lile bango paliandikwa, "YESU MNAZARETI, MFALME WA WAYAHUDI."
Ni katika lugha gani lile bango kwenye Msalaba wa Yesu lilindikwa?
Bano lilikuwa limeandkwa katika Kiebrania, Kilatini na Kiyunani.
John 19:23-24
Je, askari walifanya nini juu ya mavazi ya Yesu
Askari waliyagawa mavazi ya Yesu katika mafungu manne, fungu moja kwa kila askari. Lakini walipigia kura ili kupata nani atachukua kanzu ya Yesu ambayo ilikuwa imefumwa pamoja bila mikunjo.
Kwa nini askari walifanya walivyofanya juu ya mavazi ya Yesu?
Hii lilitokea ili kwamba Maandiko yatimie yale yanayosema, "Waligawanya mavazi yangu na nguo yangu wakaipigia kura."
John 19:25-27
Ni nani alioyekuwa amesima karibu na msalaba wa Yesu?
Mama yake na Yesu, dada yake na mariamu mama wa Yesu, Mariam mke wa Kleopa, Mariamu Magdalene na mwanafunzi yule aliyependwa na Yesu. Hawa wote walikuwa wamesimama karibu na msalaba wa Yesu.
Yesu alimwambia nini mama yake alipomwona mama yake na mwanafunzi aliyempenda wamesima kariribu naye?
Yesu alimwambi "Mwanamke, tazama, huyu hapa ni mwanao!"
Yule mwanafunzi aliyependwa na Yesu alifanya nini baada ya kuambiwa na Yesu, "Huyu hapa ni mama yako?"
Tokea saa hiyo yule mwanafunzi akamchukua mama yake Yesu nyumbani kwake.
John 19:28-30
Kwa nini Yesu alisema, "naona kiu."
Yesu alisema hivyo ili kuuthibitisha ukweli wa Maandiko.
Yesu alifanya nini baada ya kuwa amekuywa siki kutoka kwenye sifongo iliyowekwa juu ya ufito na kuwekwa mdomoni mwake?
Naye Yesu alipoionja hiyo, akasema, "Imekwisha." Kisha akainamisha kichwa chake, akaikabidhi roho yake.
John 19:31-33
Kwa nini Wayahudi walimtaka Pilato avunje miguu ya wale wnume wliokuwa wamesulibishwa?
Kwa sababu ilikuwa ni maandalio, na kwa sababu miili haikutakiwa kubaki msalabani wakati wa Sabato ( na kwa sababu Sabato ilikuwa siku muhimu sana kwa Wayahudi), Wayahudi walimwomba Pilato kuwa miguu ya wahalifu ivunjwe na miili yao ishushwe.
Kwa nini Askari hawakuivunga miguu ya Yesu?
Hawakuivunja miguu ya Yesu kwa sababu walimwona tayari amekwisha kufa
John 19:34-35
Asakari walifanya nini baada ya kumkut Yesu kuwa tayari alikuwa amekufa?
Mmoja wa wale askari alimchoma Yesu ubavuni kwa mkuki.
Kwa nini aliyeona mambo haya yote kuhusiana na kusulibiwa kwa Yesu alitoa ushuhuda kwao?
Naye aliyeona matukio haya ametoa ushuhuda ili nanyi pia mweze kuamini.
John 19:36-37
Kwa nin miguu ya Yesu haikuvunjwa na kwa nini Yesu alichomwa kwa mkuki?
Haya mambo yalitokea ili kwamba maandiko yaweze kutimilika, "Hapana mfupa wake utakaovunjwa." na tena, "watamtazama yeye waliyemchoma."
John 19:38-39
Nani aliyekuja kuuomba mwili wa Yesu?
Yusufu wa Arimathaya alimwomba Pilato ili auchukue mwili wa Yesu
Ni nani aliyekuja pamoja na Yusufu wa Arimathea kuuchukua mwili wa Yesu
Nikodemo ndiye aliyekuja pamoja na Yusufu wa Arithea.
John 19:40-42
Yusufu wa Arimathea na Nikodemo waliufanyia nini mwili wa Yesu?
Waliufanga mwaili wa Yesu kwenye sanda ya kitani na pamoja na yale manukato. Kisha waliulaza mwili wa Yesu katika kaburi jipya ambalo lilikuwa bustanii
John 20
John 20:1-2
Ni wakati gani Mriamu Magdalena alikuja Kaburini?
Alikuja kaburini mapema siku ya kwanza ya juma
Mariamu Magdalena aliona nini alipofika kaburini?
Aliliona lile jiwe likiwa limevingirishwa toka kaburini
Mariamu alisema nini kwa wanafunzi wale wawili?
Aliwaambi, "wamemchukua Bwana kaburini, nasi hatujui kule walikomlaza."
John 20:3-5
Simon Petro na wanafunzi wengine walifanya nini waliposikia kile alichosema Mariamu Magdalena?
Wote walikimbia kuelekea kaburini.
John 20:6-7
Mle Kaburini, Petro aliona nini?
Petro aliiona ile sanda ya kitani imelala pale na ile leso iliyokuwa kichwani pake haikuwa imewekwa pamoja na zile sanda za kitani bali ilikuwa imewekwa pembeni peke yake.
John 20:8-10
Je, Mwitikio wa Yule mwanafunzi mwingine ulikuwaje juu ya kile alichokiona mle kaburini?
Aliona na kuamini
John 20:11-13
Mariamu aliona nini alipokuwa amesimmama na kutazama kaburuni?
Aliona malaika wawili wenye sura nyeupe wamekaa mmoja kichwani na mwingine miguuni mahali ambapo Yesu alikuwa amelala.
Malaika walimwambuia nini Mariamu?
Walimuuliza, "Mwanamke, kwa nini unalia?
John 20:14-15
Mariamu alipogeuka aliona nini'?
Alimwona Yesu akiwa amesimama pale, lakini hakujua kama huyo alikuwa Yesu.
Mariamu alifikiri Yesu alikuwa nani?
Alifikiri alikuwa mtunza bustani?
John 20:16-18
Ni wakati gani Mariamu alimtambua Yesu?
Alimtambua Yesu pale alipolimka jina lake, "Mariamu."
Ni kwa nini Yesu alimwambia Mariamu asimguse?
Yesu alimwambia asimguse kwa sababu bado alikuwa hajapaa kwenda kwa Baba.
Yesu alimwambia akawaambie nini ndugu Zake?
Yesu alimwambia akwambie ndugu Zake, kuwa Nitapaa kwa Baba na Baba yenu, na Mungu wangu na Mungu wenu.
John 20:19-20
Kilitokea nini kwa wanafunzi wakati wa jioni ya kwanza ya siku ya kwanza ya juma?
Yesu alikuja na kusimama katkati yao.
John 20:21-23
Yesu alisema alikuwa anafanya nini kwa wanafunzi?
Yesu alisema alikuwa akiwatuma wanafunzi kama vile Baba yake alivyomtuma yeye.
Yesu alisema nini kwa wanafunzi wake baada ya kuwavuvia?
Aliwaambia, "Pokeeni Roho Mtakatifu. Dhambi za yeyote mkizisamehewa, zitakuwa zimesamehewa kwa ajili yao, na dhambi za yeyote mtakazozifungia watakuwa zimefungiwa."
John 20:24-25
Ni mwanfunzi yupi ambaye hakuwa pamoja na wenzake walipomwona Yesu?
Thomaso, mmoja wa wale thenashara, aitwaye Pacha, hakuwa pamoja na wanafunzi wenzake wakati Yesu alipokuja.
Thomaso aliseaama ingemagharimu nini kuamini kwamba alikua hai?
Thomaso alisema, "Kama sitaona alama za misumari katika mikono yake, na kutia vidole vyangu kwenye hizo alama, na pia kutia mkono wangu kwenye ubavu wake sitaamini."
John 20:26-27
Thomaso alimwona Yesu wakati gani?
Baada ya siku nane, Thomaso alikuwa na wanafunzi wenzake na milango ilikuwa imefungwa na Yesu akasimama kati kati yao.
Yesu alimwambia nini Thomaso?
Yesu alimwambia Thomaso kumgusa kwa kidole chake na kuona tazama mikono ya Yesu na amgese kwa mkono wake kuutia ubavuni Mwake. Kisha Yesu alimwambia asiwe mwenye kupungukiwa na imani, bali mwenye kuamini.
John 20:28-29
Thomaso alimwambia nini Yesu?
Thomaso alimwambia, "Bwana wangu na Mungu wangu"
Yesu alimwambia nini Thomaso?
Yesu alisema, "Wamebarikiwa wao wanaoamini, pasipokuona."
John 20:30-31
Je, Yesu alifanya ishara nyingine ambazo hazikuandikwa kwenye kitabu?
Ndiyo, Yesu alifanya ishara nyingi mbele ya wanafunzi ambazo hazikuandikwa kwenye kitabu cha Yohana.
Ni kwa nini ishara ziliandikwa kitabuni?
Zimeandikwa ili kwamba muweze kuamini kwamba Yesu ndiye Kristo, mwana wa Mungu, na kwamba muaminipo muwe na uzima katika jina lake.
John 21
John 21:1-3
Wanafunzi walikuwa wapi wakati Yesu alipojionyesha kwao tena?
Wanafunzi walikuwa kwenye bahari ya Tiberia
Ni wanafunzi gani walikuwa kwenye bahari ya Tiberia?
Simon Petro, Thomaso aitwaye Didimo, Nathanaeli wa kana ya Galilaya, wana wa Zebedayo na wanafunzi wengine wawili wa Yesu walikuwa kwenye bahari ya Tiberia.
Wanafunzi walikuwa wakifanya nini?
Wanafunzi hawa walikuwa wamekwenda kuvua samaki lakini hawakupata cho chote usiku kucha.
John 21:4-6
Yesu aliwaambia wanafunzi kufanya nini?
Yesu aliwaambia wanafunzi kutupa nyavu zao upande wa kulia wa mtumbwi wao na wangeliweza kuvua sameki kiasi.
Kulitokea nini wanafunzi walipotupa nyavu zao?
Nao hawakuweza kuzivuta tena kwa sababu ya kulikuwa na samaki wengi ndani yake.
John 21:7-9
Je, Simon Petro alifanya nini pale mwanafunzi aliyependwa na Yesu aliposema, "Ndiye Bwana"
alaijifunga vazi lake kisha akajitupa baharini
Wale wanafunzi wengine walifanya nini?
Wale wanafunzi wengine walikuja kwenye mtumbwi wakikokota nyavu zikiwa zimejaa samaki.
John 21:10-11
Yesu aliwaambia kufanya nini na baadhi ya samaki waliokuwa wamewavua?
Yesu aliwaambia wanafunzi kuleta baadhi ya samaki waliokuwa wamewavua sasa hivi.
John 21:12-14
Hii ni mara ya ngapi sasa kwa Yesu kujidhihirisha kwa wanafunzi wake?
Hii ilikuwa mara ya tatu kwa Yesu kujidhihirisha kwa wanafunzi wake baada ya kufufuka toka wafu.
John 21:15-16
Baada ya kifungua kinywa Yesu alimuuliza Simon Petro jambo gani la kwanza?
Yesu alimuuliza Simoni Petro kama alimpenda Yesu kuliko hawa.
John 21:17-18
Je! Mara ya tatu Simon Petro alimjibu nini Yesu alipomwuliza Petro kama alimpenda Yesu?
Mara ya tatu Petro alipoulizwa alijibu, Bwana; wewe wajua yote, unajua kuwa nakupenda."
Mara ya tatu Petro anamjibu swali la Yesu. "Je!" Wanipenda?" Yesu alimwambia Petro kufanya nini?
Mara ya tatu Yesu alimwambia Petro, "Lisha wanakondoo wangu."
Yesu alimwambia nini Simoni Petro ambacho kilichokuwa kinakwenda kumtokea Simoni yatakapokuwa mzee?
Yesu alimwambia limwambia simoni Petrokuwa atakapokuwa mzee angenyosha mikono yake na mwingine angemfunga nguo na kumpeleka asikotaka kwenda.
John 21:19-21
Kwa nini Yesu alimwambia Petro kile kitakachompata Petro katika uzee wake?
Yesu aliyasema haya ili kuonyesha ni aina gani ya kifo ambacho Petro atakufa kwa ajili ya utukufu wa Mungu
John 21:22-23
Yesu alilijibuje swali la Petro, la, "Huyu mtu atafanya nini?"
Yesu alimwambia Petro. "nifuate"
John 21:24-25
Ni nani aliandika kitabu hiki na anatolea ushuhuda kwa jambo gani>
Mwanafunzi aliyependwa na Yesu ndiye aliyeandika kitabu na ndiye anayeshuhudia na ushuhudia kwamba kwamaba yanayoelezewa katika kitabu hiki ni kweli.