Kiswahili: translationQuestions

Updated ? hours ago # views See on DCS Draft Material

Acts

Acts 1

Acts 1:1-3

Ni kwa mtu yupi Luka alimwandikia kitabu hiki?

Luka alimwandikia kitabu hiki Theofilo.

Yesu alifanya nini siku arobaini baada ya mateso yake?

Yesu alijidhihirisha kwa mitume wake, akisema mambo yahusuyo ufalme wa Mungu.

Acts 1:4-5

Kwa vipi Yesu aliwaamuru mitume wake wasubiri?

Yesu aliwaambia mitume wake waisubiri ahadi ya Baba.

Kwa kitu gani mitume wangebatizwa katika sdiku chache?

Mitume wangebatizwa kwa Roho Mtakatifu

Acts 1:6-8

Lini mitume walitaka kujua muda wa kurudishiwa ufalme wao, na jinsi gani Yesu anawajibu?

Yesu aliwaambia kwamba si haja ya wao kujua muda.

Kitu gani Yesu aliwaambia mitume wangekipokea kutoka kwa Roho Mtakatifu?

Yesu aliwaambia wangepokea nguvu.

Ni wapi Yesu aliwaambia mitume wangekuwa mashahidi?

Yesu aliwaambia mitume wangekuwa mashahidi katika Yerusalemu, Yudea, Samaria na hata mwisho wa nchi.

Acts 1:9-11

Yesu alitowekaje kutoka kwa mitume wake?

Yesu aliinuliwa juu na wingu likamficha machoni pao.

Malaika walisemaje, kwamba Yesu angerudi tena ulimwenguni?

Malaika walisema kwamba Jesu angerudi kwa namna ile alivyonyakuliwa kwenda mbinguni.

Acts 1:12-14

Nini mitume, wanawake, Mariamu, na ndugu zake na Yesu walikuwa wakifanya katika chumba cha juu?

Walikuwa wakiomba kwa bidii.

Acts 1:15-16

Nini kilikuwa kimetimizwa katika maisha ya Yuda, aliyemsaliti Yesu?

Maandiko yalikuwa yametimizwa kupitia Yuda

Acts 1:17-19

Nini kilitokea kwa Yuda baada ya kupokea fedha kwa ajili ya kumsaliti Yesu?

Yuda alinunua shamba, kichwa chake kiliinama, mwili wake ulipasuka, na matumbo yake kumwagika nje.

Acts 1:20

Katika kitabu cha Zaburi, kinasema kitatokea nini kwa nafasi ya Yuda ya uongozi?

Zaburi yasema kwamba nafasi ya Yuda ya uongozi itajazwa na mtu mwingine.

Acts 1:21-23

Yalikuwepo matakwa gani kwaajili ya mtu ambaye angelichukua nafasi ya Yuda ya uongozi?

Mtu anayechukua nafasi hii lazima awe aliambatana na mitume kutoka wakati wa ubatizo wa Yohana, na lazima awe ameshuhudia kufufuka kwa Yesu.

Acts 1:24-26

Namna gani mitume walitambua yupi kati ya watahiniwa wawili atakayechukua nafasi ya Yuda?

Mitume waliomba kwamba Mungu afunue chaguo lake, na ndipo wakapiga kura.

Nani aliyejumuishwa na mitume kumi na moja?

Mathias alijumuishwa na mitume kumi na moja.

Acts 2

Acts 2:1-4

Katika sikukuu ipi ya Kiyahudi wanafunzi walikuwa pamoja?

Wanafunzi walikuwa pamoja kwenye sikukuu ya Pentekoste.

Lini Roho Mtakatifu alikuja ndani ya nyumba, wanafunzi walianza kufanya nini?

Wanafunzi walianza kusema kwa lugha nyingine.

Acts 2:5-7

Wakati huu Yerusalemu, walikuwepo wayahudi wacha Mungu kutoka wapi?

Pale walikuwepo Wayahudi wacha Mungu kutoka kila taifa chini ya mbingu.

Kwanini makutano ya watu walichanganyikiwa wakati waliposikia wanafunzi wakinena?

Makutano ya watu walichanganyikiwa kwasababu kila mmoja alisikia wakisema kila mmoja kwa lugha yake.

Acts 2:8-11

Kuhusu nini wanafunzi walikuwa wakinena?

Wanafunzi walikuwa wakisema habari za matendo makuu ya Mungu.

Acts 2:12-15

Baadhi ya wale waliokuwa wakiwadhihaki mitume walifikiri nini?

Baadhi waliwadhihaki wakifikiri wamelewa na mvinyo mpya.

Acts 2:16-19

Petro alisema nini kimetimizwa wakati huu?

Petro alisema unabii wa Yoeli ulikuwa umetimia ambapo Mungu angemwaga Roho wake juu ya miili yote.

Acts 2:20-21

Katika unabii ya Yoeli, Nani ambao wameokolewa?

Kila mtu aliitiae jina la Bwana ni moja ya waliookolewa

Acts 2:22-24

Namna gani huduma ya Yesu ilikuwa thabiti kwa Mungu?

Huduma ya Yesu ilikuwa thabiti kupitia kazi ya uweza na maajabu na ishara ambazo Mungu alifanya kupitia yeye.

Mipango wa nani uliomfanya Yesu asulibiwe?

Yesu alisulibiwa kupitia mpango wa mahususi wa Mungu.

Acts 2:25-26

Katika Agano la Kale, Mfalme Daudi alitoa unabii gani kuhusu Mungu aliye Mtakatifu?

Mfalme Daudi alisema kwamba hataruhusu Mtakatifu Wake kuona uharibifu.

Acts 2:27-28

Katika Agano la Kale, Mfalme Daudi alitoa unabii gani kuhusu Mungu aliye Mtakatifu?

Mfalme Daudi alisema kwamba Mungu hageruhusu Mtakatifu Wake kuona uharibifu.

Acts 2:29-31

Ni ahadi ipi Mungu aliifanya kwa Mfalme Daudi kuhusu uzao wake?

Mungu alimwahidi Mfalme Daudi kwamba mmoja wa uzao wake angeketi juu ya kiti cha enzi.

Katika Agano la Kale Nini Mfalme Daudi alitabiri kuhusu Mungu mtakatifu?

Mfalme Daudi alisema kwamba Mungu asingeruhusu Mtakatifu wake kuona uharibifu.

Acts 2:32-33

Nani aliyekuwa Mtakatifu wa Mungu ambaye hakuona uharibifu na angeketi kwenye kiti cha enzi?

Yesu alikuwa katabiriwa Aliye Mtakatifu na Mfalme.

Acts 2:34-36

Petro alihubiri kwamba Mungu amempa Yetu vyeo gani viwili?

Mungu alimfanya Yesu kuwa Kristo na Bwana

Acts 2:37-39

mkutano uliposikia mahubiri ya Petro, walipokeaje?

Mkutano uliuliza kile wanachopaswa kufanya.

Petro aliwaambia nini makutano cha kufanya?

Petro aliwaambia makutano kutubu na kubatizwa katika Jina la Yesu Kristo kwa ajili ya msamaha wa dhambi zao.

Kwa ajili ya nani Petro aliwaambia ilikuwa ahadi ya Mungu?

Petro alisema ahadi ya Mungu ilikuwa kwa ajili ya makutano, watoto wao na wote waliokuwa mbali.

Acts 2:40-42

Watu wangapi waliobatizwa siku hiyo?

Ilikuwa yapata watu elfu tatu waliobatizwa siku hiyo.

Watu waliobatizwa waliendelea na hatua gani?

Waliendelea katika mafundisho ya mitume na ushirika, na katika kuumega mkate na katika maombi.

Acts 2:43-45

Je! Wale walioamini walifanya nini kuwasaidia wale waliokuwa wahitaji?

Waliuza mali zao na vyote walivyomiliki na kuwagawia kila mmoja aliyekuwa na uhitaji.

Acts 2:46-47

Waumini walikuwa wanakutana wapi wakati huu?

Waumini walikutana kwenye Hekalu.

Nani waliokuwa wakiongezeka siku kwa siku kwa kundi la waumini?

Bwana aliwazidisha siku kwa siku wale waliokuwa wakiokolewa.

Acts 3

Acts 3:1-3

Petro na Yohana walimwona nani wakiwa wanakwenda hekaluni?

Petro na Yohana walimwona mtu mwenye kupooza toka azaliwe alikuwa akiomba kwenye mlango wa hekalu

Acts 3:4-6

Ni kitu gani Petro hakumpa yule mtu?

Petro hakumpa mtu yule fedha na dhahabu.

Acts 3:7-8

Petro alimpa nini mtu huyu?

Petro alimpa mtu huyu uwezo wa kutembea.

Yule mtu aliitikiaje kwa kile alichopewa na Petro?

Mtu yule aliingia hekaluni akitembea, kupiga makofi, na kumsifu Mungu.

Acts 3:9-14

Jinsi gani watu waliitikia walipomwona yule mtu ndani ya hekalu?

Watu walijawa na hofu na mshangao mkubwa

Acts 3:15-18

Petro aliwakumbusha watu nini ambacho walikifanya kwa Yesu?

Petro aliwakumbusha watu kwamba walimuua Yesu.

Petro alisema nini kutokana na mtu waliyekuwa wamemfanya kuwa mzima?

Petro waliwaambia ni imani katika jina la Yesu ndilo lililomfanya kuwa mzima.

Acts 3:19-20

Petro aliwaambia watu wafanye nini?

Petro aliwaambia watu watubu.

Acts 3:21-23

Petro alisema mbingu zingempokea Yesu hata wakati gani?

Petro alisema kwamba mpaka wakati wa urejesho wa vitu vyote, Yesu angelipokelewa mbinguni.

Nini Musa alishasema juu ya Yesu?

Musa alisema kwamaBwana Mungu angemwinua nabii kama yeye mwenyewe, kwa mtu huyu watu wangemsikia

Nini kitatokea kwa kila mtu ambaye hataki kumsikia Yesu?

Mtu ambaye asiyemsikiliza Yesu ataangamizwa kabisa.

Acts 3:24-26

Ni unabii gani wa Agano la Kale wa agano la ahadi ambao Petro aliwakumbusha watu?

Petro aliwakumbusha watu kwamba walikuwa watoto wa agano la Mungu uliofanywa na Abrahamu wakati Mungu alisema, "Katika uzao familia zote za duniani zitabarikiwa".

Jinsi gani Mungu alitamani kuwabariki Wayahudi?

Mungu alitamani sana kuwabariki wayahudi kwa kumtuma Yesu kwao ili kuwatoa kwenye uasi.

Acts 4

Acts 4:1-7

Petor na Yohana walikuwa wakifundisha nii kwa watu waliokuwa hekaluni?

Petro na Yohana walikuwa wakifundisha habari za Yesu na kufufuka kwake kutoka kwa wafu.

Kwa jinsi gani wakuu wa hekalu, makuhani na masadukayo waliitikia juu ya mafundisho ya Petro na Yohana?

Waliwakamata Petro na Yohana na kuwatupa kifungoni.

Kwa jinsi gani watu waliitikia juu ya mafundisho ya Petro na Yohana?

Watu wengi waliamini, yapata watu elfu tano.

Acts 4:8-10

Kwa nguvu gani au kwa Jina lipi ambalo Petro alisema kwamba lilimponya yule mtu katika hekalu?

Petro alisema kuwa ni katika Jina la Yesu Kristo lilimponya mtu aliyekuwa hekaluni.

Acts 4:11-12

Petro alisemaje nini juu ya njia moja ambayo tunaweza kuokolewa?

Petro alisema kwamba hakuna jina jingine isipokuwa la Yesu ambalo tunaweza kuokolewa

Acts 4:13-14

Kwanini viongozi wa kiyahudi wasingeweza kusema lolote dhidi ya Petro na Yohana?

Viongozi wasingeweza kusema lolote kwasababu yule mtu aliyekuwa ameponywa alikuwa amesimama pamoja na Petro na Yohana.

Acts 4:15-18

Viongozi wa kiyahudi waliwaamrisha Petro na Yohana wasifanye nini?

Viongozi wayahudi waliwaamrisha Petro na Yohana wasinene au kufundisha habari za Yesu.

Acts 4:19-28

Jinsi gani Petor na Yohana waliwajibu viongozi wa Kiyahudi?

Petro na Yohana walisema kuwa haitawasaidia isipokuwa kuzidi kunena habari za mambo waliyokwisha yaona na kuyasikia kutoka kwake.

Acts 4:29-31

Je waumini waliomba nini kwa Mungu katika kukabiliana na onyo kutoka kwa viongozi wa Kiyahudi?

Waumini waliomba ujasiri katika kusema neno, na kwa ishara na maajabu kufanywa katika jina la Yesu.

Nini kilitokea baada ya waumini kumaliza maombi yao?

Baada ya waumini kumaliza maombi yao, mahali walipokuwa wamekusanyika palitikisika, walijazwa na Roho Mtakatifu, na walinena neno kwa ujasiri.

Acts 4:32-33

Je! Kwa jinsi gani mahitaji ya waumini yaliweza kutimizwa?

waumini walikuwa na vitu vyote shirika, na wale ambao walimiliki mali waliziuza na kutoa pesa kugawanywa kulingana na uhitaji wa mtu.

Acts 4:34-35

Je! Kwa jinsi gani mahitaji ya waumini yaliweza kutimizwa?

waumini walikuwa na vitu vyote shirika, na wale ambao walimiliki mali waliziuza na kutoa pesa kugawanywa kulingana na uhitaji wa mtu.

Acts 4:36-37

Nini jina gani jipya, maana yake "mwenye kutia moyo," alilopewa mtu ambaye aliuza shamba lake na kutoa fedha kwa mitume?

Mtu mmoja aitwaye "mwenye kutia moyo" alikuwa Barnaba.

Acts 5

Acts 5:1-2

Nini dhambi gani Anania na Safira Walifanya?

Anania na Safira walidanganya, wakisema kwamba walikuwa wakitoa thamani yote ya kuuza mali zao, lakini kwa kweli tu walitoa sehemu ya fedha ya thamani iliyouzwa.

Acts 5:3-8

Kwa nani ambaye Petro alisema Anania na Safira walikuwa wamesema uongo?

Petro alisema kuwa Anania na Safira walikuwa wamesema uongo kwa Roho Mtakatifu.

Hukumu gani ya Mungu iliyompata Anania?

Mungu alimwua Anania.

Acts 5:9-13

Hukumu gani ya Mungu iliyompata Safira?

Mungu alimwua Safira.

Ni mwitikio gani kwa kanisa na kwa wote waliosikia habari za Anania na Safira?

Hofu kuu ilikuja juu ya kanisa na kwa wote kuhusu Anania na Safira.

Acts 5:14-16

Watu walikuwa wakifanyaje kupelekea wagonjwa kuponywa?

Baadhi yao walikuwa wakiwabeba wagonjwa na kuwaweka pembeni mwa barabara ili kivuli cha Petro kiweze kuwafikia, na wengine waliwaleta wagonjwa kutoka miji mingine mpaka Yerusalemu.

Acts 5:17-18

Mwitikio wa Masadukayo ulikuwaje kwa wale mgonjwa waliokuwa wakiponywa katika Yerusalemu?

Masadukayo walijaa wivu na kuwatupa mitume gerezani

Acts 5:19-21

Ni vipi Mitume walitoka nje ya jela?

Malaika wakaja na kufungua milango ya gereza na kuwaacha watoke nje.

Acts 5:22-25

Maafisa wa Kuhani Mkuu waliona nini walipokwenda eneo la jela?

Maafisa waliona jela imefungwa kwa usalama, lakini hapakuwa na hata mtu mmoja ndani.

Acts 5:26-28

Kwa nini maafisa waliwaleta Mitume kwa Kuhani Mkuu na baraza bila vurugu?

Maafisa walihofia kwamba watu watawapiga mawe.

Acts 5:29-32

Walipoulizwa kwa nini walikuwa wakifundisha kwa jina la Yesu wakati wao walikuwa wamewazuia, Je! mitume wajibu nini?

Mitume walisema, "Lazima tumtii Mungu kuliko wanadamu".

Mitume walisema ni nani alihusika katika kumwua Yesu?

Mitume walisema Kuhani Mkuu na wajumbe wa baraza walihusika katika kumwua Yesu.

Acts 5:33-37

Je wajumbe wa baraza waliitikiaje juu ya taarifa kwamba wao walihusika kumwua Yesu?

Wajumbe wa baraza walikuwa na hasira na walitaka kuwaua mitume.

Acts 5:38-39

Nini ambacho Gamalie alitoa ushauri kwa baraza?

Gamaliel alilishauri baraza kuwaachia mitume pekee.

Kitu gani Gamalieli aliwatahadhalisha baraza kuwa kitawapata kama watazidi kuwatesa mitume?

Gamalieli aliwatahadhalisha baraza kuwa wangeweza kuishia katika kupingana na Mungu.

Acts 5:40-42

Je! Baraza walifanya uamzi gani juu ya Mitume?

Baraza waliwacharaza viboko na wakawaamuru wasifundishe tena kwa jina la Yesu; kisha wakawaacha waende zao.

Je! Mitume waliitikiaje juu ya vitendo walichotendewa kutoka kwa baraza?

Mitume walifurahi kwamba walikuwa wamehesabiwa wa thamani kwa kudhalilishwa kwa ajili ya Jina la Yesu.

Mitume walifanya nini kila siku baada ya mkutano wano na baraza la wazee?

Mitume walizidi kuhubiri na kufundisha kila siku kwamba Yesu alikuwa ni Kristo.

Acts 6

Acts 6:1

Nini malalamiko yaliyozuka kwa Wayunani wa kiyahydi dhidi ya Waebrania?

Wayunani wa kiyahudi walilalamika kuwa wajane wao walikuwa wanasahauliwa katika ugawaji wa chakula wa kila siku.

Acts 6:2-4

Nani waliochagua wanaume saba ili kusimamia huduma ya kugawa chakula?

Wanafunzi (ndugu) waliwachagua wale wanaume saba.

Sifa za wale wanaume saba waliochaguliwa zilikuwa ni zipi?

Wanaume saba waliochaguliwa walikuwa na sifa nzuri, wamejawa na Roho Mtakatifu na hekima.

Je! Mitume waliamua kuendelea na nini?

Mitume waliendelea na maombi na huduma ya neno.

Acts 6:5-6

Mitume walifanya nini pale waumini walipowachagua hao wanaume saba?

Mitume waliwaombea na kuweka mikono juu yao.

Acts 6:7-9

Nini kilikuwa kinatokea kwa wanafunzi huko Yerusalemu?

Idadi ya wanafunzi ilikuwa inazidi kuongezeka sana, ikiwa ni pamoja na kundi kubwa la makuhani.

Acts 6:10-11

Nani ambaye alikuwa mshindi wa mijadala kati ya Wayahudi wasioamini na Stephano?

Wayahudi wasioamini hawakuweza kusimama dhidi ya hekima na Roho ambayo Stephen alikuwa akinena.

Acts 6:12-15

Ni mashitaka gani ya uongo yaliyoshuhudiwa mbele za baraza dhidi ya Stefano?

Mashahidi wa uongo walidai kwamba Stefano alisema Yesu angepaharibu mahali hapa na kuzibadili desturi za Musa.

Wajumbe wa baraza walipomtazama Stefani, ni kitu gani walikiona kwake?

Waliuona uso wake ulikuwa kama uso wa malaika.

Acts 7

Acts 7:1-3

Stefano alianzia kwa kina nani kuelezea historia ya ahadi ya Mungu kwa wayahudi?

Stefano alianza kutoa historia kwa kuzungumzia ahadi ya Mungu kwa Ibrahimu.

Acts 7:4-5

Ni ahadi gani Mungu alimwahidi Ibrahimu?

Mungu alimwahidi Ibrahimu kumpatia nchi yeye na uzao wake.

Kwanini ahadi ya Mungu kwa Ibrahimu ilionekana kutotimizwa?

Ahadi ya Mungu ilionekana kutokuwezekana kwasababu Ibrahimu hakuwa na mtoto.

Acts 7:6-8

Mungu alimwambia Abraham nini kingeweza kutokea kwanza kwa uzao wake kwa miaka mia nne?

Mungu alimwambia Abraham uzao wake ungekuwa mateka katika nchi ya ugeni kwa miaka mia nne

Ni agano lipi ambalo Mungu alimpa Ibrahimu?

Mungu alimpa Ibrahimu agano la tohara.

Acts 7:9-10

Ni kwa namna gani Yusufu alikuwa mtumwa katika nchi ya Misri?

Ndugu zake walimwonea wivu wakamuuza katika nchi ya Misri

Ni kwa namna gani Yusufu alikuwa mkuu nchi ya Misri?

Mungu alimpa Yusufu neema na hekima mbele ya uso wa Farao

Acts 7:11-13

Yakobo alifanya nini wakati njaa ilipoingia katika nchi ya Kanani?

Yakobo aliwatuma watoto wake wa kiume kwenda Misri kwasababu alisikia kule kulikuwa na nafaka.

Acts 7:14-16

Kwa nini Yakobo na jamaa yake walikwenda Misri?

Yusufu aliwatuma ndugu zake kumwambia baba yao kwenda Misri

Acts 7:17-19

Nini kilitokea katika idadi ya Israel huko Misri kama ahadi ya Mungu ilivyokuwa karibu

Idadi ya Waisraeli huko Misri ilikua na kuongezeka.

Kwa jinsi gani mfalme mpya wa Misri alijaribu kupunguza idadi ya Waisraeli.

Mfalme mpya aliwalazimisha Waisraeli kuwatupa watoto wachanga wa kiume ili wasiweze kuishi.

Acts 7:20-21

Jinsi gani Musa alipona ali hali naye alitupwa?

Binti wa Mfalme Farao alimwokota Musa na kumlea kama mtoto wake mwenyewe.

Acts 7:22-28

Jinsi gani Musa alipata elimu?

Musa alifundishwa mafunzo yote ya Kimisri

Alipofikisha umri wa miaka arobaini, Musa alifanya nini alipowaona wana wa Israeli kutendewa mabaya?

Musa aliwatetea waisraeli na hata kumpiga na kumwua Mmisri.

Acts 7:29-32

Musa alikimbilia wapi?

Musa alikimbilia Midiani

Wakati Musa alipotimiza umri wa miaka themanini, Je! Musa aliona nini?

Musa alimwona malaika ndani ya miali ya moto ukiwaka katika kichaka.

Acts 7:33-34

Bwana alimwagiza Musa kwenda wapi, na kitu gani Mungu alikuwa anakwenda kufanya kule?

Bwana alimwagiza Musa kwenda Misri, kwasababu Mungu alikuwa anakwenda kuwaokoa Waisraeli.

Acts 7:35-40

Ni kwa muda gani Musa aliwaongoza Waisraeli huko nyikani?

Musa aliwaongoza Waisraeli nyikani kwa muda wa miaka arobaini.

Musa alitabiri nini juu ya wana wa Israeli?

Musa alitabiri kwa Waisraeli kwamba Mungu angemwinua nabii kama yeye miongoni mwa ndugu zao.

Acts 7:41-42

Ni kwa jinsi gani Waisrael waliigeuza mioyo yao na kutamani kurudi Misri?

Waisraeli walitengeneza ndama wakaitolea sadaka kwa miungu.

Namna gani Mungu aliwajibu Waisraeli juu ya kumwacha Yeye?

Mungu aliwaacha Waisraeli na kuwaruhusu kutumikia viumbe wa mbinguni.

Acts 7:43

Ni wapi Mungu alisema angewapeleka Waisraeli?

Mungu alisema angewapeleka Waisraeli utumwani Babeli.

Acts 7:44-46

Katika jangwa, Mungu aliwaamuru Israeli kujenga nini, ambacho baadaye walikibeba kwenda katika nchi?

Katika jangwa Waisraeli walijenga hema la ushuhuda.

Nani aliyeyafukuza mataifa mbele ya Waisraeli?

Mungu aliwafukuza mataifa mbele ya Waisraeli.

Nani aliuliza kujenga mahali pa makao ya Mungu?

Daudi aliomba kumjengea Mungu mahali pa kukaa

Acts 7:47-50

Nani hasa aliyemjengea Mungu nyumba?

Sulemani alimjengea Mungu nyumba.

Mahali gani kilipo kiti cha Mungu aliye juu?

Mungu Mkuu anakiti chake juu mbinguni.

Acts 7:51-53

Ni kwa vipi Stefano aliwashtaki watu kwa yale waliyokuwa wakitenda ,kama baba zao walivyotenda?

Stefano aliwashtaki watu kwa kuendelea kumpinga Roho Mtakatifu.

Je Stefano alisema nini kwa walioasi juu ya mmoja mwenye haki?

Stefano alisema; watu walimsaliti na kumwua mmoja mwenye haki.

Acts 7:54-56

Ni kwa namna gani wajumbe wa baraza walliitikia kwa mashtaka ya Stefano?

Wajumbe wa baraza walichomwa mioyo yao na kumsagia meno Stefano.

Stefano alisema nini alipotazama macho yake juu?

Stefano alisema, alimwona Yesu amesimama mkono wa kuume wa Mungu

Acts 7:57-58

Wajumbe wa baraza walifanya nini kwa Stefano?

Wazee wa baraza walimwinukia, wakamtupa nje ya mji na kumpiga kwa mawe.

Waliokuwa wakimpiga kwa mawe, mavazi yao ya nje waliyaweka kwa nani aliyekuwa shuhuda wa kifo cha Stefano?

Walimpiga Stefano kwa mawe mavazi yao ya nje waliyaweka chini ya miguu ya Sauli aliyekuwa shuhuda wa kifo cha Stefano.

Acts 7:59-60

Jambo gani la mwisho Stefano aliomba kabla hajafa?

Stefano alimwomba Mungu asiiangalie dhambi ya watu hao kwa kile walichokitenda.

Acts 8

Acts 8:1-3

Sauli alifikiri nini kuhusu kupigwa mawe kwa Stefano?

Sauli alikuwa katika makubaliano juu ya kifo cha Stefano.

Nini kilianza siku Stefano alipopigwa mawe?

Siku Stefano alipopigwa mawe mateso makali yaliaanza dhidi ya kanisa la Yeruselemu

Waumini wa Yerusalem walifanya nini?

Waumini wa Yerusalemu walitawanyika katika majimbo ya Yuda na Samaria.

Acts 8:4-5

Waumini wa Yerusalemu walifanya nini?

Waumini wa Yerusalem walitawanyika katika majimbo ya Yuda na Samariana kwenda kuhubiri injili.

Acts 8:6-8

Kwa nini watu wa Samaria walikuwa makini kwa kile alichosema Philipo?

Watu walikuwa makini pale walipoona ishara alizofanya Philipo

Acts 8:9-11

Kwa nini watu Samaria walikuwa makini kwa Simoni?

Watu walikuwa makini walipoona uchawi wake.

Acts 8:12-13

Wakati Simoni alipousikia ujumbe wa Filipo, Je! Alifanya nini?

Simoni pia aliamini na akabatizwa.

Acts 8:14-17

Nini kilitokea wakati Petro na Yohana walipoweka mikono yao juu ya waumini wa Samaria?

Waumini wa Samaria walipokea Roho Mtakatifu.

Acts 8:18-19

Ni zawadi gani Simoni alifanya kwa mitume?

Simoni aliwapatia mitume fedha ili wabadilishane na nguvu ya Roho Mtakatifu kwa kuwekewa mikono

Acts 8:20-25

Baada ya Simoni kutoa zawadi hiyo kwa mitume, Petro alisema nini kuhusu maisha yake ya kiroho?

Petro alimwambia Simoni alikuwa na sumu ya uchungu na kifungo cha dhambi.

Acts 8:26-28

Malaika alimwambia Philipo nini cha kufanya?

Malaika alimwambia Philipo kwenda kusini mwa jangwa barabara iendayo Gaza.

Filipo alikutana na nani na mtu yule alikuwa anafanya nini?

Filipo alikutana na towashi mwenye mamlaka kutoka Ethiopia alikuwa amepanda kwenye mkokoteni akisoma kitabu cha nabii Isaya.

Acts 8:29-31

Filipo alimwuliza swali gani yule mtu?

Filipo alimwuliza yule mtu, "Je! Unayaelewa yale unayoyasoma?"

Mtu yule alimwomba nini Filipo?

Mtu yule alimwomba Filipo kupanda kwenye mkokoteni na kumwelezea alichokuwa anasoma.

Acts 8:32-33

Nini kilitokea kwa mtu aliyeelezwa ndani ya maandiko kutoka Isaya ambacho kilikwishasomwa?

Mtu huyo aliongozwa kama kondoo kwenda machinjoni ,lakini hakufungua kinywa chake.

Acts 8:34-35

Ni swali gani yule mtu alimwuliza Filipo kuhusu andiko alilosoma?

Huyo mtu alimwuliza Filipo kama nabii aliongea habari zake mwenyewe au habari za watu wengine.

Mtu yupi Filipo alimsema aliyetajwa na Nabii Isaya?

Filipo alielezea kwamba mtu huyo Isaya alimtaja katika maandiko alikuwa Yesu.

Acts 8:36-38

Filipo alimfanyia nini yule mtu?

Filipo na Towashi wote walikwenda kwenye maji na Filipo akambatiza.

Acts 8:39-40

Nini kilitokea wakati Filipo alipotoka nje ya maji?

Wakati Philipo alipotoka nje ya maji ,Roho wa Bwana alimtwaa Filipo.

Towashi alifanya nini alipotoka kwenye maji?

Wakati Towashi alipotoka majini aliendlea na safari yake kwa furaha nyingi.

Acts 9

Acts 9:1-2

Sauli aliomba kibali cha kufanya nini kwa kuhani mkuu wa Yerusalemu?

Sauli aliomba barua ili aweze kusafiri kwenda Dameski kumleta na kumfunga yeyote anayeifuata njia hiyo.

Acts 9:3-4

Sauli alipokaribia Dameski,aliona nini?

Sauli alipokaribia Dameski aliona nuru kutoka mbinguni.

Je! Sauti hiyo ilimwambiaje Sauli?

Sauti ilimwambia, "Sauli, Sauli kwanini unanitesa".

Acts 9:5-7

Wakati Sauli alipouliza sauti ya nani aliyekuwa akiongea, jibu lilikuwa nini?

Jibu lilikuwa, "Mimi ni Yesu ambaye ambaye unanitesa."

Acts 9:8-9

Mara Sauli alipoinuka kutoka katika nchi, kitu gani kilikuwa kimetokea kwake?

Wakati Sauli alipoinuka hakuweza kuona chochote.

Baadaye Sauli alienda wapi, na kufanya nini?

Sauli alikwenda Dameski na hakuweza kula wala kunywa kwa siku tatu mfurulizo.

Acts 9:10-12

Mungu alimwambia Anania kufanya nini?

Mungu alimwambia Anania kwenda na kuweka mikono juu ya Sauli ili Sauli angeweza kupokea kuona tena.

Acts 9:13-16

Ni wasiwasi gani Anania aliueleza kwa Bwana?

Anania alikuwa na wasiwasi kwa sababu alimjua Sauli akikuwa amekuja Dameski kumkamata kila mtu aliitiaye jina la Bwana

Ni huduma gani ya Bwana aliyokuwa amemjulisha juu ya Sauli kuwa chombo kiteule?

Bwana alimwambia Sauli angelichukua Jina la Bwana mbele ya mataifa, wafalme, na kwa watoto wa Israeli.

Je! Bwana alimwambia Sauli kuwa huduma yake itakuwa nyepesi au itakuwa ngumu?

Bwana alimwambia Sauli angeteswa kikubwa kwa ajili ya Jina la Bwana.

Acts 9:17-19

Baada ya Anania kuweka mikono yake juu ya Sauli, Nini kilitokea?

Baada ya Anania kuweka mikono juu ya Sauli, Sauli alipokea kuona, alibatizwa, na kula chakula.

Acts 9:20-22

Wakati huo huo Sauli alianza kufanya nini?

Wakati huo huo Sauli alianza kumtangaza Yesu katika masinagogi ,akisema kwamba Yesu ni Mwana wa Mungu

Acts 9:23-25

Wakati wayahudi waliponga na kutaka kumwua Sauli, Sauli alifanya nii?

Wakati wayahudi walipopanga kumwua Sauli, Sauli aliwakwepa kwa njia ya kushushwa chini kupitia ukutani akuwa ndani ya kikapu.

Acts 9:26-27

Mara Sauli alipofika Yerusalemu, ni kwa namna gani wanafunzi waliweza kumpokea?

Huko Yerusalemu, wanafunzi walimwogopa Sauli.

Nani aliyemleta Sauli kwa mitume na kuwaelezea kile kilichokuwa kimetokea kwa Sauli huko Dameski?

Barinaba alimleta Sauli kwa mitume na kuwaelezea kile kilichokuwa kimetokea kwa Sauli huko Dameski.

Acts 9:28-30

Sauli alifanya nini akiwa huko Yerusalemu?

Sauli alinena kwa ujasiri kupitia Jina la Bwana Yesu.

Acts 9:31-32

Baada ya Sauli kupelekwa Tarso,hali ya kanisa la Uyahudi, Galilaya na Samaria ilikuwaje?

Hali ya kanisa la Uyahudi, Galilaya na Samaria likawa na amani, na likajengwa na kukua kwa idadi.

Acts 9:33-39

Nini kilitokea LIda na kusababisha kila mmoja kumgeukia Bwana?

Huko Lida, Petro aliongea na mtu aliyepooza, mtu yule aliponywa na Yesu,

Acts 9:40-43

Nini kilitokea Yafa ambacho kilisababisha watu wengi kumwamini Bwana?

Petro aliomba kwa ajili ya mwanamke aliyefariki jina lake Thabitha,ambaye alifufuka.

Acts 10

Acts 10:1-2

Kornelio alikuwa mtu wa namna gani?

Kornelio alikuwa mtu maarufu mwenye hofu ya Mungu, mtoaji sadaka na akimwomba Mungu daima.

Acts 10:3-8

Malaika alisemaje kilichomfanya Mungu kukumbuka habari za Kornelio?

Malaika alisema Maombi ya Kornelio, na zawadi kusaidia maskini zilimkumbusha Mungu kuhusu Kornelio.

Malaika alimwambia Kornelio mambo gani ya kufanya?

Malaika alimwambia Kornelio kutuma watu mpaka Yopa kumwita Petro.

Acts 10:9-12

Siku iliyofuata, Petro aliona nini wakati alipokuwa akiomba kwenye chumba cha juu?

Petro aliona kitambaa kikubwa kimejaa kila aina ya wanyama, na viumbe vya kutambaa, na ndege.

Acts 10:13-18

Wakati Petro alipoona maono, Je! Sauti aliyoisikia ilisema nini kwake?

Sauti ilimwambia Petro, "Inuka, Petro, chinja na ule."

Mwitikio wa Petro juu ya sauti hiyo ulikuwaje?

Petro alikataa, akisema hajawahi kamwe kula kitu najisi na kichafu

Baadaye Petro alisikia sauti ikimwambiaje?

Sauti ilisikika kusema, "Kile Mungu amekitakasa, usikiite ni najisi".

Acts 10:19-21

Roho alimwambia nini Petro wakati wanaume kutoka kwa Kornelio walipofika kwenye nyumba alimokuwa Petro?

Roho alimwambia Petro kushuka chini na kwenda pamoja nao.

Acts 10:22-24

Je! Wanaume kutoka Kornelio walitarajia Petro kuja na kufanya ujumbe katika nyumba ya Kornelio?

Wanaume kutoka kwa Kornelio walimtarajia Petro kuja na kutoa ujumbe katika nyumba ya Kornelio.

Acts 10:25-26

Petro alisema nini wakati Kornelio alipoinama chini kwenye miguu ya Petro?

Petro alimwambia Kornelio kusimama kwa vile yeye naye alikuwa ni mwanadamu.

Acts 10:27-33

Petro alianza kufanya mambo gani ambayo tokea nyuma alikuwa hayafanyi?

Petro alianza kujichanganya na watu kutoka mataifa mengine, kwasababu Mungu alikuwa amemwonyesha kuwa asiwaite watu najisi na wasio safi.

Acts 10:34-35

Ni mtu yupi Petro anasema anayeweza kukubaliwa na Mungu?

Petro anasema kuwa kila mmoja aliye na hofu ya Mungu na anayetenda matendo ya haki huyo anakubaliwa na Mungu.

Acts 10:36-38

Ni ujumbe upi wa Yesu ambao ulikuwa umesikiwa na watu wa nyumba ya Kornelio?

Watu walikuwa wameshasikia kwamba Yesu alikuwa ametiwa mafuta na Roho Mtakatifu na kwa nguvu, na kwamba alikuwa akiwaponya wote waliokuwa wameonewa na nguvu za mwovu, kwa kuwa Mungu alikuwa pamoja naye.

Acts 10:39-41

Petro alitamka nini kile ambacho kilikuwa kimetokea kwa Yesu baada ya kifo chake na kwa jinsi gani Petro alijua hili?

Petro alitamka kwamba Mungu alikuwa amemfufua Yesu katika siku ya tatu, na kwamba Petro alikuwa amekula pamoja naye baada ya ufufuo wake.

Acts 10:42-43

Petro alisema nini juu ya Yesu aliyekuwa amewaamuru kuhubiri kwa watu"

Yesu aliwaagiza kuhubiri kwamba Yesu ndiye ambaye Mungu alimchagua kuwa mhukumu wa walio hai na waliokufa

Petro alisema, kwa yeyote anayemwamini Yesu atapokea kitu gani?

Petro alisema yeyote amwaminiye Yesu angepokea msamaha wa dhambi zake.

Acts 10:44-45

Nini kilitokea kwa watu waliokuwa wakimsikiliza Petro wakati akiendelea kuongea?

Roho Mtakatifu alishuka juu ya wote waliokuwa wakimsikiliza Petro.

Kwanini jamii ya waumini wa kundi la tohara walishangaa?

Maumini wa kungi la tohara walikumbwa na mshangao kwa sababu ile zawadi ya kipawa cha Roho Mtakatifu ilikuwa imemwagwa pia kwa watu wa mataifa.

Acts 10:46-48

Watu walikuwa wakifanya nini kilichoonyesha Roho Mtakatifu ameshuka juu yao?

Watu walikuwa wanongea kwa Lugha zingine na kumsifu Mungu ndicho kilichoonyesha kuwa Roho Mtakatifu ameshuka kwao.

Baada ya kuwaona watu walikuwa wamempokea Roho Mtakatifu, Je! Petro aliamru wafanyiwe nii?

Petro aliagiza watu wale wabatizwe katika Jina la Yesu Kristo.

Acts 11

Acts 11:1-3

Habari gani njema ambayo mitume na ndugu wa Yudea waliisikia?

Mitume na ndugu wa Yudea walisikia kuwa wamataifa wameokea pia neno la Mungu.

Ni upinzani gani uliotokea kwa Petro toka kwenye kundi la waumini wa tohara huko Yerusalemu?

Wale waumini wa kundi la tohara walimpinga Petro kwa vile alikula pamoja na wamataifa.

Acts 11:4-14

Jinsi gani Petro alijibu kutokana na upinzani kinyume chake?

Petro akajibu upinzani kwa kufafanua maono ya nguo na ubatizo wa Roho Mtakatifu wa wamataifa.

Acts 11:15-16

Ushahidi upi Petro aliuonyesha kwamba Mungu alikuwa amewakubali wamataifa?

Petro aliwasilisha uthibitisho wa hakika kuwa Roho Mtakatifu alikuwa ameshuka kwa mataifa.

Acts 11:17-18

Nini lilikuwa hitimisho la wale kundi la waumini wa tohara wakati walipomsikia Petro akielezea?

Walimtukuza Mungu na kuhitimisha kwa kusema Mungu alikuwa amewap wamataifa pia toba kwa ajili ya maisha yao.

Acts 11:19-21

Nini walichokuwa wakifanya baadhi ya waumini waliokuwa wametawanyika baada ya kifo cha Stefano?

Baadhi ya waumini waliotawanyika walinena ujumbe wa Kristo kwa Wayahudi pekee.

Kitu gani kilitokea kwa baadhi wa waumini waliokuwa wametawanyika walipohubiri habari za Yesu kwa Wayunani?

Wakati walipohubiri habari za Bwana Yesu kwa Wayunani idadi kubwa ya wati waliamini.

Acts 11:22-24

Nini ambacho Barnaba kutoka Yerusalemu aliwaambia Wagriki walioamini huko Antiokia?

Barnaba aliwatia Moyo Wagriki kubaki na Bwana kwa mioyo yao wote.

Acts 11:25-26

Nani alibaki muda wa mwaka mmoja katika kanisa la Antiokia?

Barnaba na Sauli walibaki mwaka mzima katika kanisa la Antiokia.

Jina gani wanafunzi walilipokea huko Antiokia?

Kwa mara ya kwanza wanafunzi waliitwa wakristo huko Antiokia.

Acts 11:27-28

Agabo Nabii alitabiri nini kilichokuwa kinakwenda kutokea?

Agabo Nabii alitabiri kutokea kwa njaa kuu ambayo ingetokea ulimwenguni kote.

Acts 11:29-30

Mitume waliupokeaje unabii wa Agabo?

Mitume walituma misaada kwa ndugu wa Yudea kwa mkono wa Barnaba na Sauli.

Acts 12

Acts 12:1-2

Herode Mfalme alimtendea nini Yakobo ndugu yake ya Yohana?

Herode Mfalme alimwua Yakobo ndugu yake Yohana kwa upanga.

Acts 12:3-4

Herode Mfalme alifanya nini kwa Petro?

Herode alimkamata na kumweka Petro gerezani akitarajia kumpeleka kwa watu baada ya pasaka.

Acts 12:5-6

Kusanyiko la wakristo lilikuwa likifanya nini kwa ajili ya Petro?

Kusanyiko la wakristo lilikuwa likiomba kwa bidii kwa ajili ya Petro.

Acts 12:7-8

Ni namna gani Petro alitoka Gerezani?

Malaika alijitokeza pembeni mwake, miyororo yake ikamwachia, na akamfuata malaika nje ya Gereza.

Acts 12:9-12

Jinsi gani Petro aliweza kuvuka lindo la kwanza na la pili la walinzi na kutoka kwenye lango la gereza?

Petro alimfuata malaika aliyemvusha kwa walinzi, na kisha lango kuu likajifungua lenyewe.

Acts 12:13-15

Wakati Petro alipofika kwenye nyumba pale waumini walikuwa wanaomba, Ni nani aliyejibu Petro alipogonga mlanga na alifanya nini?

Mtumishi wa kike Roda alijibu na kutoa taarifa kuwa Petro alikuwa amesimama kwenye mlango, lakini hakufungua mlango.

Jinsi gani waumini waliitikia mara tu walipoisikia taarifa ya Rhoda?

Mwanzoni walidhani Rhoda alikuwa ameehuka.

Acts 12:16-17

Baada ya kuwaambia waumini kile kilichokuwa kimetokea kwake, Je! Petro waliwaagiza wafanye nini?

Petro aliwaagiza watoe taarifa ya mambo hayo kwa Yakobo na ndugu wote.

Acts 12:18-21

Nini kilitokea kwa wanaume waliokuwa wakimlinda Petro?

Herode aliwahoji walinzi na kisha aliwachukua na kuwaua.

Acts 12:22-23

Watu walishangilia kitu gani wakati Herode alipokuwa akitoa hotuba?

Watu walishangilia wakisema , "Hii ni sauti ya mungu, na siyo ya mwanadamu"!

Nini kilitokea kwa Herode baada ya hotuba yake, na kwanini?

Kwasababu Herode hakumpa utukufu Mungu, Malaika alimpiga na akatafunwa na minyoo na kufa.

Acts 12:24-25

Nini kilikuwa kinatokea kwa neno la Mungu wakati huu?

Neno la Mungu likapata nguvu na kusambaa wakati huu.

Nani aliambatana na Barnaba na Sauli?

Barnaba na Sauli walimchukua Yohana Marko pamoja nao.

Acts 13

Acts 13:1-3

Kusanyiko la Antiokia lilikuwa kinafanya nini wakati Roho Mtakatifu alipozungumza nao?

Kusanyiko la Antiokia lilikuwa likimwabudu Bwana na kufunga wakati Roho Mtakatifu alipozungumza nao.

Roho Mtakatifu aliwaambia nini cha kufanya?

Roho Mtakatifu aliwaambia kuwaweka wakfu Barnaba na Sauli kufanya kazi ambayo Roho alikuwa amewaita kufanya.

Kusanyiko walifanya nini baada ya kumsikiliza Roho Mtakatifu?

Kusanyiko walifunga, waliomba, waliweka mikono juu ya Barnaba na Sauli na kuwatuma kwenda zao.

Acts 13:4-5

Wakati Barnaba na Sauli walipokwenda Kipro, ni nani aliambatana nao?

Huko Kipro, Yohana Marko aliambatana nao kama msaidizi wao.

Acts 13:6-8

Bar-Yesu alikuwa nani?

Bar-Yesu alikuwa ni nabii wa uongo wa kiyahudi alikuwa na uhusiano na mkuu wa jimbo hilo.

Kwanini mkuu wa jimbo aliwaita Barnaba na Sauli?

Mkuu wa jimbo aliwaita Barnaba na Sauli kwasababu alitaka kusikia neno la Mungu.

Acts 13:9-10

Jina gani jingine ambalo Sauli alijulikana?

Sauli pia alijulikana kama Paulo.

Acts 13:11-12

Paulo alisema nini ambacho kingetokea kwa Bar-Yesu kwasababu ya kujaribu kumgeuza imani mkuu wa jimbo?

Paulo alimwambia Bar-Yesu kwamba angekuwa kipofu kwa muda.

Mwitikio wa Mkuu wa Jimbo ulikuwaje wakati Bar-Yesu alipotokewa na tukio hilo?

Mkuu wa jimbo aliamini.

Acts 13:13-15

Yohana Marko alifanya nini wakati Paulo na rafiki zake waliposafiri majini kuelekea Perge?

Yohana Marko alimaacha Paulo na Rafiki zake na kurudi Jerusalem.

Ni mahali gani huko Antiokia ya Pisidia Paulo aliomwa kutoa hotuba?

Katika Antiokia Pisidia Paulo aliombwa kutoa hotuba ndani ya Sinagogi la Wayahudi.

Acts 13:16-22

Katika hotuba ya Paulo, Ni nani Paulo alimtaja kuwa Mungu alimchagua tangu zamani?

Katika hotuba ya Paulo, Paulo alisema Mungu alimchagua Israeli.

Acts 13:23-25

Ni kutoka kwa nani Mungu aliwaletea Israeli Mkombozi?

Kutoka kwa Mfalme Daudi Mungu aliwaletea Israeli Mkombozi.

Paulo alimsema nani aliyekuwa ameandaliwa kuandaa njia ya ujio wa Mwokozi?

Paulo alisema kwamba Yohana Mbatizaji alikuwa ameandaa njia kwa ujio wa Mwokozi.

Acts 13:26-29

Kwa jinsi gani watu na watawala katka Yerusalemu walitimiza ujumbe wa unabii?

Watu na watawala katikaYerusalemu walitimiza ujumbe wa manabii kwa kumhukumu Yesu hadi mauti.

Acts 13:30-31

Nani walikuwa mashahidi wa Yesu kwa watu?

Watu waliomwona Yesu baada ya kufufuka kwake kutoka wafu hao walikuwa mashahidi wake.

Acts 13:32-34

Kwa jinsi gani Mungu alidhihirisha kuwa alikuwa ameitunza ahadi aliyokuwa ameinena kwa Wayahudi?

Mungu aliidhihirisha kwamba alikuwa ameitunza ahadi kwa Wayahudi kwa njia ya kumfufua Yesu kutoka kwa wafu.

Acts 13:35-37

Ni nini Mungu aliwaahidi Watakatifu katika moja ya zaburi?

Mungu aliwaahidi kwamba Watakatifu wake wasingeuona uharibifu.

Acts 13:38-39

Paulo anahubiri nini kwa kila mmoja anayeamini katika Yesu?

Paulo alihubiri msamaha wa dhambi kwa kila mmoja aaminiye katika Yesu.

Acts 13:40-43

Ni onyo gani pia Paulo aliwapa wasikilizaji wake?

Paulo aliwaonya wasikilizaji wake wasiwe kama walionenwa kwenye unabii waliosikia tangazo la kazi ya Mungu lakini wasiliamini.

Acts 13:44-45

Huko Antiokia, ni nani alikuja kusikia neno la Bwana katika Sabato iliyofuata?

Karibia mji wote walikuja kusikia neno la Bwana Sabato iliyofuata.

Jinsi gani Wayahudi waliitikia walipoliona kundi kubwa likisikiliza?

Wayahudi walijawa na wivu nawakaanza kunena ujumbe kinyume na Paulo, na kumdhihaki.

Acts 13:46-47

Paulo alisema nini kuhusu Wayahudi walivyokuwa wakifanya kwa neno lililokuwa limesemwa na Mungu juu yao?

Paulo aliwaambia Wayahudi kwamba walikuwa wakilisukumia mbali neno la Mungu lililosemwa na Mungu juu yao.

Acts 13:48-49

Ni nini mwitikio wa Mataifa waliposikia kwamba Paulo anawageukia wao?

Mataifa walifurahi na kulisifu neno la Bwana.

Mataifa wangapi waliamini?

Wengi kama walivyokuwa wamechaguliwa kupata uzima wa milele waliamini.

Acts 13:50-52

Wayahudi waliwafanyia nini kwa Paulo na Barnaba?

Wayahudi walichochea mateso dhidi ya Paulo na Barnaba na kuwatupa nje ya mji.

Paulo na Barnaba walifanya nini kabla ya kwenda mji wa Ikonia?

Paulo na Barnaba walikung'uta mavumbi ya miguuni mwao dhidi ya waliokuwa kinyume chao katika mji wa Antioki waliokuwa wamewatupa nje.

Acts 14

Acts 14:1-2

Je, Wayahudi wasioamini katika Ikonio walifanya nini baada ya mkutano kuamini mahubiri ya Paulo na Barnaba

Wayahudi wasioamini walichochea akili za Mataifa na kuwafanya kuwa na uchungu dhidi ya ndugu.

Acts 14:3-4

Ni kwa namna gani Mungu anatoa uthibitisho kuhusu ujumbe wa neema yake?

Mungu alitoa uthibitisho kuhusu ujmbe wa neema yake kwa kutoa ishara na maajabu yaliyofanywa kwa mikono ya Paulo na Barnaba.

Acts 14:5-7

Kwanini Paulo na Barnaba waliondoka Ikonia?

Baadhi ya Wamataifa na Wayahudi kulijaribu kuwashawishi watawala wao kuwatenda vibaya na kuwaponda mawe Paulo na Barnaba.

Acts 14:8-13

Je, ni nini Paulo alifanya kilichosababisha vurugu huko Lystra?

Paulo alimponya mtu aliyekuwa kiwete kutoka tumboni mwa mama yake.

Acts 14:14-16

Jinsi gani Paulo na Barnaba waliitikia kwa kile watu walichotaka kuwafanyia?

Barnaba na Paulo walirarua mavazi yao, wakaenda kwenye kusanyiko, na kulia wakisema kwamba watu wageuke na kuacha vitu visivyofaa na kumwelekea Mungu.

Acts 14:17-18

Ni jinsi gani Mungu hakuruhusu asiwepo mtu wa kumshuhudia siku zilizopita?

Mungu aliwapa mataifa mvua na nyakati za mafanikio, akijaza mioyo yao kwa chakula na furaha.

Watu wa Listra walitaka kufanya nini juu ya Paulo na Barnaba?

Watu walitaka kutoa dhabihu kupitia kuhani wa mungu Zeusi kwa Paulo na Barnaba.

Acts 14:19-20

Jambo gani baadaye kusanyiko huko Listra walimfanyia kwa Paulo?

Kusanyiko huko Listra baadae walimponda mawe Paulo na kumvuta nje ya mji.

Paulo alifanya nini pale wanafunzi walipokuwa wamesimama wamemzunguka?

Paulo aliinuka na kuingia ndani ya mji.

Acts 14:21-22

Kupitia nini Paulo aliwaambia wanafunzi lazima kuingia katika ufalme wa Mungu?

Paulo aliwaambia wanafunzi lazima kuingia katika ufalme wa Mungu kwa njia ya mateso mengi.

Acts 14:23-26

Paulo na Barnaba walifanya nini katika kila kusanyiko la waamini kabla ya kuondoka kwao?

Katika kila kusanyiko, Paulo na Barnaba walichagua wazee, waliomba pamoja na kufunga, na kuwakabidhi waamini kwa Bwana.

Acts 14:27-28

Paulo na Barnaba walifanya nini wakati waliporudi Antiokia?

Waliporudi Antikia , walitoa taarifa kwa mambo yote ambayo Mungu aliwasaidia kuyafanya, na kwa namna alivyofungua mlango wa imani kwa Mataifa.

Acts 15

Acts 15:1-2

Ni watu gani walitoka Uyahudi na kwenda kuwafundisha Ndugu?

Watu fulani kutoka Uyahudi walifundisha kwamba ndugu wasipotahiriwa hawataokolewa.

Namna gani ndugu waliamua kuyashughulikia maswali yaliyokuwa yamejitokeza?

Ndugu waliamua kuwatuma Paulo na Barnaba na kundi jingine waende Yerusalemu wakawaone mitume na wazee wa baraza.

Acts 15:3-4

Kwa kupitia Foinike na Samaria, ni habari njema zipi Paulo na wenzake walizitangaza?

Paulo na wenzake walipota miji hiyo wakitangaza kuokolewa kwa Mataifa.

Acts 15:5-6

Ni kundi gani kati ya waamini walidhani kwamba Mataifa lazima watahiriwe na kuitunza sheria ya Musa?

Kundi la Mafarisayo waliamini kwamba Mataifa lazima watahiriwe na lazima waitunze sheria ya Musa.

Acts 15:7-9

Petro alisemaje kuhusu Mungu alichokuwa amefanya kwa ajili ya mataifa?

Petro aliwaambia, Mungu aliwapa mataifa Roho Mtakatifu na alikuwa ameifanya mioyo yao kuwa safi kwa imani.

Acts 15:10-11

Jinsi gani Petro alisema kuwa Wayahudi na Wayunani wote wanaokolewa?

Petro alisema wote Wayahudi na Wayunani wanaokolewa kupitia neema ya Bwana Yesu.

Acts 15:12

Je! Paulo na Barnaba walitoa ripoti kwa Kusanyiko?

Paulo na Barnaba walitoa taarifa kuwa ishara na maajabu ya Mungu yalikuwa yakitendeka kwa Mataifa.

Acts 15:13-14

Je ni unabii gani Yakobo aliunukuu ukisema kwamba Mungu atajenga, na ni pamoja na nani?

Unabii ulisema kwamba Mungu atajenga tena hakalu la Daudi lililoanguka, na kwamba itawajumisha Mataifa.

Acts 15:15-18

Unabii ule ambao Yakobo aliounukuu ulisema Mungu atalijenga tena, na angejumuisha nani?

Unabii ulisema kuwa Mungu angelijenga tena hema lililoanguka la Daudi, na kwamba angewaunganisha wamataifa.

Acts 15:19-26

Amri zipi Yakobo alipendekeza wapewe wakristo wamataifa?

Yakobo alipendendekeza amri kwa wakristo wamataifa kuwa, wajiepusha na sanamu, uasherati, wajiepushe na nyama za kusongolewa na wajiepushe na damu.

Acts 15:27-29

Barua iliyoandikwa kwa wamataifa, Nani amenenwa kuwa kwenye makubaliano ya kuwapatia wamataifa machache yaliyo ya muhimu?

Waandishi wa waraka na Roho Mtakatifu wametajwa kuwa wamepatana kuwaandikia hayo mambo machache muhimu.

Acts 15:30-32

Mwitikio wa watu wa mataifa ulikuwaje waliposikia maelezo ya waraka kutoka Yerusalemu?

Watu wa mataifa walifurahi kwasababu ya kutiwa moyo kwao na waraka huo.

Acts 15:33-35

Paulo na Barnaba walifanya nini walipokaa Antiokia?

Paulo na Barnaba walifundisha na kulihubiri neno la Bwana.

Acts 15:36-38

Paulo alimwambia nini Barnaba alichotaka kufanya?

Paulo alimwambia Barnaba kwamba alihitaji kurudi na kuwatembelea ndugu katika kila mji walikokuwa wamehubiri neno la Bwana.

Acts 15:39-41

Kwanini Paulo na Barnaba walitengana na kusafiri katika uelekeo tofauti?

Kulitokea hali ya kutokukubaliana kati yao, hivyo walitengana kila mmoja na safari yake.

Acts 16

Acts 16:1-3

Paulo alifanya nini kabla hawajasafiri na Timotheo na kwa nini?

Paulo alimtahiri Timotheo kwasababu ya Wayahudi kattika maeneo hayo walimjua baba yake Timotheo alikuwa Mgiriki.

Acts 16:4-8

Ni maagizo gani Paulo alitoa kwa Makanisa walipokua wakienda?

Paulo alitoa maagizo ambayo yaliandikwa na mitumi na wazee huko Yerusalemu.

Acts 16:9-10

Paulo alijuaje kuwa Mungu alikuwa anamwita kuihubiri injili huko Makedonia?

Paulo aliona maono ya mtu wa Makedonia akimwita avuke huko na kuwasaidia.

Acts 16:11-13

Siku ya sabato, Kwanini Paulo alikwenda mtoni nje ya lango la Filipi?

Paulo alidhani kungekuwa na eneo la utulivu kwa maombi.

Acts 16:14-15

Bwana alifanya nini kwa Lidia wakati Paulo akiongea?

Bwana alimfungua moyo wake na kuweka maanani maneno yaliyosemwa na Paulo.

Nani aliyebatizwa baada ya Paulo kumaliza hotuba yake huko mtoni?

Lidia pamoja na watu wa nyumba yake walibatizwa baada ya hotuba ya Paulo.

Acts 16:16-18

Ni kwa namna gani yule msichana mwenye pepo mbaya aliwapatia fedha mabwana zake?

Aliwapatia fedha mabwana zake kwa kubashiri

Paulo alimtendea nini yule msichana baada ya kumfuata fuata kwa siku nyingi?

Paulo alimgeukia na kumwamru yule roho kwa Jina la Yesu atoke ndani yake.

Acts 16:19-21

Ni mashitaka gani yaliyoletwa na mabwana wa yule msichana dhidi ya Paulo na Sila?

Waliwashitaki Paulo na Sila juu ya mambo waliyokuwa wanafundisha kuwa ni kinyume cha sheria kwa warumi kuyapokea au kuyatekeleza.

Acts 16:22-24

Ni adhabu gani Paulo na Sila walipata kutoka kwa mahakimu?

walichapwa kwa viboko, na kutupwa gerezani, na kuwekewa kwenye ulinzi imara.

Acts 16:25-28

Paulo na Sila walikuwa wakifanya nini wakati wa usiku wa manane?

Walikuwa wakiomba na kuimba nyimbo za kumsifu Mungu.

Nini kilitokea na kumfanya mlizi wa jera atafute kujiua mwenyewe?

Kulikuwa na tetemeko la ardhi, milango yote ya gereza ilifunguka, na minyororo ya kila mmoja ulilegezwa.

Acts 16:29-31

Ni swali gani bwana jela aliwauliza Paulo na Sila?

Aliuliza; "Bwana zangu lazima nifanye nini kupata kuokolewa"?

Ni jibu gani Paulo na Sila walimjibu Bwana Jela?

Paulo na Sila walimjibu, "Mwamini Bwana Yesu, na utaokolewa , wewe na nyumba yako yote".

Acts 16:32-34

Nani aliyebatizwa usiku huo?

Aliyebatiwa ni bwana Jela na watu wa nyumba yake wote walibatizwa usiku huo.

Acts 16:35-36

Nini kiliwafanya mahakimu waogope pale walipotuma ujumbe wa kuwaruhusu Pauolo na Sila kuondoka?

Mahakimu waliogopa kwasababu walijua kuwa waliwapiga hadharani kabla ya kuwahukumu watu ambao ni rai wa Rumi.

Acts 16:37-39

Kitu gani kilisababisha mahakimu waogope na kulazimu watume ujumbe kwa Paulo na Sila wa kuwaruhusu waondoke?

Mahakimu walikumbwa na hofu kwasababu walikuwa wamewaadhibu hadharani raia wawili wa kirumi wasio na hatia.

Acts 16:40

Baada ya Mahakimu kuwaambia waondoke katika mji huo, Paulo na Sila walifanya nini?

Paulo na Sila walienda nyumbani kwa Lidia, na kuwatia moyo ndugu , na kisha kuondoka Filipi.

Acts 17

Acts 17:1-2

Alipofika Thesalonike, ni wapi Paulo alikwenda kwanza kuzungumza kutoka kwenye maandiko habari za Yesu?

Paulo alikwenda kwenye sinagogi la Wayahudi kwanza kuongea kutoka kwenye maandiko habari za Yesu.

Acts 17:3-4

Paulo alionyesha nini kilicho kuwa muhimu kutoka kwenye maandiko?

Paulo alionyesha kuwa ilimpasa Kristo ateseke na kufufuka tena kufufuka kutoka kwa wafu.

Acts 17:5-9

Mashitaka gani yaliandaliwa dhidi ya Paulo na Sila mbele ya wakuu wa mji?

Paulo na Sila walishitakiwa kwa kwenda kinyume na sheria za Kaisari, wakisema kuna mfalme mwingine ambaye ni Yesu

Acts 17:10-12

Ni wapi Paulo na Sila walikwenda walipofika Beroya?

Paulo na Sila walikwenda kwenye Sinagogi la Wayahudi.

Waberoya walifanya nini wakati waliposikia ujumbe wa Paulo?

Waberoya walilipokea neno na kuyachunguza maandiko kuona kama Paulo alichofundisha kilikuwa hicho.

Acts 17:13-15

Kwanini Paulo aliondoka Beroya , na alikwenda wapi?

Ilimbidi Paulo aondoke Beroya kwasababu Wayahudi wa Thesalonike walisababisha ghasia katika umati huko Beroya, kwahiyo Paulo alikwenda Athene.

Acts 17:16-18

Paulo alikwenda wapi wakati alipofika Athene?

Paulo aliingia kwenye Sinagogi la Wayahudi na eneo la gulio kufanya mahojiano ya maandiko.

Acts 17:19-21

Ni wapi Paulo aliletwa ili azungumzie zaidi juu ya mafundisho yake?

Paulo aliletwa Areopago ili aelezee mafundisho yake zaidi.

Acts 17:22-23

Madhabahu ipi katika Athene Paulo aliiona, ambayo alitaka kuelezea kwa watu?

Paulo aliiona madhabahu yenye maneno, KWA MUNGU ASIYEJULIKANA, ambayo alitaka kutolea ufafanuzi kwa watu.

Acts 17:24-25

Paulo alisemaje juu ya Mungu aliyefanya kila kitu huwapa nini wanadamu?

Paulo alisema Mungu aliyeumba kila kitu huwapa wanadamu uzima, pumzi na kila kitu pia.

Acts 17:26-27

Kutokea kwenye nini Mungu alifanya mataifa yote ya watu?

Kutokea kwa Mtu mmoja Mungu alifanya mataifa yote ye watu.

Ni kwa jinsi gani Paulo anasema umbali wa Mungu kutoka kwa kila mmoja?

Paulo anasema Mungu hayuko mbali na kila mmoja wetu.

Acts 17:28-29

Paulo anasemaje kutokufikiri juu ya Mungu?

Paulo anasema tusifikiri kuwa Mungu ni mfano wa dhahabu, au mawe, vinavyofanywa na wanadamu.

Acts 17:30-31

Kwa sasa Mungu anawaitia nini watu wote kila mahali wafanye?

Mungu anaita watu wote kila mahali watubu.

Mungu ametenga siku maalumu ya nini?

Mungu ametenga siku maalumu wakati Yesu atauhukumu ulimwengu katika haki.

Ni uthibitisho upi aliouweka Mungu kwamba Yesu ndiye aliyemchagua kuuhukumu ulimwengu?

Mungu amemthibitisha Yesu kuwa ndiye aliyemchagua kuuhukumu ulimwengu kwa kumfufua kutoka kwa wafu.

Acts 17:32-34

Baadhi yao walifanya nini waliposikia habari ya kufufuliwa kwa watu?

Baadhi yao walimdhihaki Paulo walipomsikia akiongea kuhusu kufufuliwa kwa wafu.

Je! Kila mmoja aliamini kile alichosema Paulo?

Ndiyo, Baadhi ya wanaume walimwamini Paulo, na wengine pamoja nao.

Acts 18

Acts 18:1-3

Kazi gani Paulo aliyoifanya kuwezesha mahitaji yake mwenyewe?

Paulo alifanya kazi ya kushona mahema ili kuwezesha kupata mahitaji yake mwenyewe.

Acts 18:4-8

Paulo alishuhudia nini kwa Wayahudi huko Koritho?

Paulo aliwashuhudia Wayahudi huko Koritho kwamba Yesu ndiye alikuwa Kristo.

Wakati Wayahudi walipompinga Paulo, yeye alifanya nini?

Paulo aliwaambia Wayahudi damu yao ilikuwa juu ya vichwa vyao wenyewe, na kisha alikwenda kwa wamataifa.

Acts 18:9-11

Ni faraja gani Paulo alipokea kutoka kwa Bwana akiwa Korintho?

Bwana alimuambia Paulo aendelee kuongea., kwani hakuna atakaye mdhuru huko.

Acts 18:12-13

Ni mashtaka gani Wayahudi walimletea mtawala kuhusu Paulo?

Wayahudi walimshutumu Paulo kwa kuwafundisha watu kuabudu kinyume na sheria,.

Acts 18:14-17

Kwa jinsi gani mtawala aliyapokea mashtaka ya Wayahudi dhidi ya Paulo?

Mtawala aliwajibu kuwa asingetamani kuwa mhukumu wa matatizo yahusuyo sheria za Wayahudi.

Acts 18:18-21

Ni mme na mke yupi walisafiri pamoja na Paulo kwenda Efeso?

Akwila na Prisila walisafiri pamoja na Paulo kwenda Efeso.

Acts 18:22-23

Ni sehemu zipi mbili ambazo Paulo alikwenda kwanza baada ya kuondoka Efeso?

Baada ya kuondoka Efeso, Paulo alikwenda Yerusalemu na kisha akaenda Antiokia.

Acts 18:24-26

Ni mafundisho yapi Apolo aliyajua vizuri, na mafundisho yapi aliyokuwa anahitaji maelekezo zaidi?

Apolo alifahamu mafundisho kuhusu Yesu Kristo vizuri, lakini alijua pekee habari za ubatizo wa Yohana.

Prisila na Akwila walimsaidia mambo gani Apolo?

Prisila na Akwila walikuwa marafiki wa Apolo na wakamfafanulia vema njia ya Mungu kwa usahihi zaidi.

Acts 18:27-28

Uwezo wa Apolo ulikuwa upi katika kunena na katika ujuzi wa maandiko?

Uwezo wa Apolo ulikuwa katika eneo la kuwavuta Wayahudi huku akiwaonyeshaYesu alikuwa Kristo.

Acts 19

Acts 19:1-2

Ni fundisho gani wanafunzi waliokuwa wameamini huko Efeso walikuwa hawalijui wakati Paulo alipokutana nao?

Wanafunzi hao walikuwa hawajawahi kusikia habari za Roho Mtakatifu.

Acts 19:3-4

Ubatizo wa Yohana ulikuwa ubatizo wa nini?

Ubatizo wa Yohana ulikuwa ubatizo wa toba

Yohana aliwafundisha watu kumwamini nani?

Yohana aliwafundisha watu kumwamini mmoja yule angekuja baada yake.

Acts 19:5-7

Kwa jina gani Paulo aliwabatiza wale wanafunzi wa Efeso?

Paul akawabatiza katika jina la Bwana Yesu.

Nini kilitokea kwa watu baada ya paulo kuwabatiza na kuwawekea mikono?

Roho Mtakatifu alishuka kwao na wakaanza kunena kila mtu kwa lugha nyingine na kutoa unabii.

Acts 19:8-10

Paulo alifanya nini wakati Wayahudi huko Efeso walipoanza kunena uovu juu ya njia ya Kristo?

Paulo aliwatenga waamini na hao na kuanza kuwafundisha waamini katika ukumbi wa Tirano.

Acts 19:11-14

Miujiza ipi maalumu aliyoitenda Mungu kupitia mikono ya Paulo?

Vitambaa na vikoyi vilivyotoka kwa Paulo, viliweza kuponya wagonjwa na kufukuza roho wachafu.

Acts 19:15-17

Nini kilitokea wakati wayahudi saba wapunga mapepo walipojaribu kufukuza pepo wachafu kwa jina la Yesu?

Pepo wachafu waliwashinda wapunga pepo na kukimbia wakiwa uchi na wamejeruhiwa.

Acts 19:18-20

Katika Efeso, walifanya nini wale awali walikuwa wakifanya mambo ya kichawi?

Wengi waliokuwa wakifanya kazi za kichawi katika Efeso walivichoma vitabu vyao mbele ya macho ya kila mmoja.

Acts 19:21-25

Wapi ambapo Paulo alisema angependa kwenda baada ya kwenda Yerusalemu?

Paulo alisema angependa kwenda Rumi baada ya kwenda Yerusalemu.

Acts 19:26-27

Wasiwasi gani wa mfua fedha Demetrius alipokuwa akiwaeleza mafundi wengine?

Demetrio alikuwa na wasiwasi kwamba Paulo alikuwa akiwafundisha watu kuwa hakuna miungu ambayo inaweza kufanya kwa mikono, na kwamba mungu Diana anaweza kuchukuliwa kuwa hafai.

Acts 19:28-29

Jinsi gani watu walikabiliana na kusudio la Demetrio'?

Watu walijawa na hasira, wakalia kwa sauti wakisema kuwa Diana alikuwa mkuu sana, mji mzima ukajawa na machafuko.

Acts 19:30-37

Kwa nini Paulo hakushughulika na umati, hata kama alitaka?

Wanafunzi na baadhi ya maafisa wa serikali hawakuruhusu Paulo kuzungumza na umati wa watu.

Acts 19:38-41

Je karani wa mji aliwaambia nini watu cha kufanya badala ya maandamano?

Karani wa mji aliwaambia watu walete mashtaka yao mahakamani.

Watu wa mji walikuwa wanakabiliwa na hatari gani karani wa mji aliwaambia?

Karani wa mji aliwaambia watu walikuwa wanakabiliwa na kushitakiwa kwa kukosa utaratibu, na kwamba kulikuwa hakuna cha kuelezea.

Acts 20

Acts 20:1-6

Nini kilichomfanya Paulo kubadirisha mipango yake na kumlazimu kurudi kupitia Makedonia badala ya kusafiri kwa njia ya baharini kuelekea Shamu?

Paulo alibadirisha mipango yake kwasababu wWayahudi walikuwa wamepanga njama dhidi yake kama angesafiri kwa njia ya baharini kwenda Shamu.

Acts 20:7-8

Ni siku ipi ya juma ambayo Paulo na waumini hukusanya kumega mkate?

Siku ya kwanza ya juma Paulo na waumini walikutana pamoja kwa kumega mkate.

Acts 20:9-14

Ni nini kilichotokea kwa kijana ambaye alianguka nje ya dirisha wakati Paulo alikuwa akizungumza?

Kijana alianguka chini kutoka ghorofa ya tatu na alichukuliwa akiwa amekufa, lakini Paulo alimkumbatia na yeye akawa mzima tena

Acts 20:15-16

Kwanini Paulo alikuwa akiharakisha kwenda Yerusalemu?

Paulo alikuwa akiharakisha kwenda Yerusalemu apate kuwa huko katka siku ya Pentekoste.

Acts 20:17-21

Paulo alisema nini wakati akiwaonya Wayahudi na Wagiriki tangu alipoingia Asia?

Paulo aliwaonya wote Wayahudi na Wagiriki kuhusu toba kwa Mungu na Imani katika Bwana Yesu.

Acts 20:22-24

Kitu gani Roho Mtakatifu alikuwa akimshuhudia Paulo katika kila mji wakati akisafiri kwenda Yerusalemu?

Roho Mtakatifu alikuwa akimshuhudia Paulo kwamba kifungo na mateso yalikuwa yakimngoja.

Huduma gani Paulo alikuwa ameipokea kutoka kwa Bwana Yesu?

Huduma ya Paulo aliyokuwa ameipokea kutoka kwa Bwana Yesu ilikuwa ya kuishuhudia kwa mataifa Injili ya neema ya Mungu.

Acts 20:25-27

Kwanini Paulo alisema alikuwa hana hatia kwa damu ya kila mtu?

Paulo alisema hana hatia kwa damu yao kwasababu alikuwa amelitangaza kusudi zima la Mungu kwao.

Acts 20:28-30

Paulo aliwaagiza nini wazee wa Efeso kufanya kwa makini baada ya kuondoka kwake?

Paul aliwaagiza wazee kulichunga kundi kwa makini.

Acts 20:31-32

Paulo aliwakabidhi kwa nani wazee wa Efeso?

Paulo aliwakabidhi wazee wa Efeso kwa Mungu.

Acts 20:33-35

Mfano gani Paulo aliuweka kwa Waefeso kutokana na kazi yake?

Paulo alifanya kazi kwa mahitaji yake mwenyewe na kwa wale waliokuwa pamoja naye, na kuwasaidia waliokuwa hawana uwezo.

Acts 20:36-38

Ni kitu gani kilishowafanya wengi wa wazee wa Efeso kuonekana wenye huzuni?

Wazee wa Efeso wengi wao walijawa na huzuni kwasababu Paulo alikuwa amawaambia wasingeweza kumwona uso wake tena.

Acts 21

Acts 21:3-6

Wanafunzi huko Tiro kupitia Roho walimwambia nini Paulo?

Wanafunzi walimwambia Paulo wakisema Roho hatamruhusu kwenda Yerusalemu.

Acts 21:7-9

Tunawafahamuje watoto wa mhubiri Filipo?

Filipo alikuwa na mabinti bikira wanne waliokuwa wakitoa unabii.

Acts 21:10-11

Agabo nabii alisema nini juu ya Paulo?

Agabo alimwambia Paulo kuwa Wayahudi huko Yerusalemu wangemfunga mikono yake mbele ya wamataifa.

Acts 21:12-16

Paulo alisemaje wakati kila mtu akimwambia asipande kwenda Yerusalemu?

Paulo alisema, yey e alikuwa tayari kufungwa na hata kufa huko Yerusalemu kwa ajili ya Jina la Bwana Yesu.

Acts 21:17-19

Paulo alikutana na nani alipowasili huko Yerusalemu?

Paulo alikutana na Yakobo na wazee wote.

Acts 21:20-21

Mashitaka yapi yaliandaliwa na Wayahudi dhidi ya Paulo?

Wayahudi walikuwa wakimshitaki Paulo kuwa amewafundisha Wayahudi wanaokaa miongoni mwa wamataifa kuacha kumfuata Musa.

Acts 21:22-24

Kwanini Yakobo pamoja na Wazee walimtaka Paulo kujitakasa mwenyewe na wanaume wanne waliokuwa wamekula kiapo?

Walitaka kila mmoja kujua kuwa Paulo kama Myahudi pia aliishi kwa kuzitunza sheria.

Acts 21:25-26

Je, Yakobo alisemaje juu ya mataifa mengine ambao waliamini walipaswa kufanya nini?

Yakobo alisema watu wa mataifa wangejiepusha na vitu vilivyotolewa sadaka kwa sanamu, na damu, na wanyama walionyongwa, na kujiepusha na uasherati.

Acts 21:27-29

Mashitaka yapi yaliyoletwa na Wayahudi toka Asia dhidi ya Paulo ndani ya hekalu?

Wayahudi walimshitaki Paulo kwa kufundisha kinyume cha mafundisho ya sheria na kulinajisi hekalu kwa kuwaingiza Wagiriki ndani ya hekalu.

Acts 21:30-31

Baada ya kuandaliwa kwa mashitaka hayo , Wayahudi walimfanyia nini Paulo

Wayahudi walimwondoa Paulo na kumpeleka nje ya hekalu na wakajaribu kumwua.

Acts 21:32-33

Jemedari wa kikosi cha ulinzi walifanya nini aliposikia kuwa Yerusalemu ilikuwa imemwinukia Paulo?

Jemedari alimkaribia Paulo na kumshika na akaamuru afungwe minyororo miwili, akiuliza yeye ni nani na amefanya nini.

Acts 21:34-38

Kelele za umati zilikuwa zikisemaje wakati askari walipomchukua Paulo ndani ya ngome?

Umati ulikuwa ukipiga kelele, "Mwondoeni huyu!"

Acts 21:39-40

Ombi gani Paulo alilolituma kwa jemedari wa jeshi?

Paul aliomba kuwa aruhusiwe kuzungumza na watu.

Acts 22

Acts 22:1-2

Wakati umati ulipomsikia Paulo akiongea kwa Kiebrania, Je! Walifanya nini?

Umati uliposikia Paulo akiongea kwa Kiebrania, wote walinyamaza.

Acts 22:3-5

Paulo alikua amesoma wapi, na nani alikua mwalimu wake?

Paulo alikua amesoma Jerusalemu, na Gamalieli alikua mwalimu wake.

Paulo akuwa akiwatenda vipi wale waliokuwa wakiifuata njia ile?

Paulo aliwatesa na kuwaua wale wote waliokuwa wakiifuata njia ile, na kuwakokota hadi gerezani.

Acts 22:6-8

Sauti kutoka mbinguni ilisemaje wakati Paulo alipokaribia Dameski?

Sauti kutoka mbinguni ilisema, "Sauli, Sauli, kwanini unanitesa?"

Paulo alikuwa akimtesa nani?

Paulo alikuwa akimtesa Yesu wa Nazareti.

Acts 22:9-11

Kwanini Paulo hakuweza kuona?

Paulo hakuweza kuona kwasababu ya ule mwanga wa nuru aliouona alipokaribia Dameski.

Acts 22:12-13

Jinsi gani Paulo alirudishiwa uwezo wa kuona?

Mtu mwema aitwae Anania alikuja na kusimama mbele ya Paulo na kusema, "Ndugu yangu Sauli, pokea kuona kwako".

Acts 22:14-16

Anania alimwambia Paulo asimame na kufanya nini, na kwanini?

Anania alimwambia Paulo ainuke na kubatizwa ili kuziosha dhambi zake, akiliita jina lake.

Acts 22:17-18

Wakati Yesu alipoongea na Paulo hekaluni, alimwambia Wayahudi wataitikiaje juu ya ushuhuda wake?

Yesu alimwambia Wayahudi hawataukubali ushuhuda wa Paulo.

Acts 22:19-21

Yesu alimtuma Paulo kwa nani?

Yesu alimtuma Paulo kwa mataifa.

Acts 22:22-24

Wayahudi waliitikiaje walipomsikia Paulo akizungumzia habari za mataifa?

Wayahudi walipaza sauti na kuvuaa mavazi yao na kurusha mavumbi hewani.

Acts 22:25-26

Swali gani Paulo alimuuliza akida kabla hajapigwa?

Paulo aliuliza kama ni haki yeye kupigwa kama mtu wakirumi ambae bado hajahukumiwa.

Acts 22:27-29

jinsi gani Paulo alikuwa raia wa Kirumi?

Paulo alikuwa raia wa Kirumi kwa kuzaliwa.

Acts 22:30

Jemedari mkuu aliamua kufanya nini alipotambua kwamba Paulo alikuwa raia wa Kirumi?

Jemedari mkuu alimfungua Paulo na kuwaamuru wakuu wa makuhani na baraza lote wakutane, akamweka Paulo mbele yao.

Acts 23

Acts 23:1-5

Kwanini Kuhani mkuu aliamuru wale waliosimama karibu na Paulo wampige mdomo wake?

Kuhani mkuu alikua amechukia kwasababu Paulo alisema ameishi mbele za Mungu kwa dhamira nzuri.

Acts 23:6-8

Ni kwasababu gani Paulo alisema anahukumiwa mbele ya baraza?

Paulo alisema alikua anahukumiwa kwasababu ya ujasiri wake katika mambo ya ufufuo.

Kwanini mabishano yalianza kwenye baraza wakati Paulo alipoeleza sababu ya kuhukumiwa kwake?

Mabishano yalianza kwasababu Mafarisayo husema kuna uffuo, lakini Masadukayo husema hakuna ufufuo.

Acts 23:9-10

Kwanini Jemedari wa jeshi alimchukua Paulo kutoka mbele ya baraza na kumrudisha kwenye ngome?

Jemedari wa jeshi alihofia kwamba Paulo angekatwa vipande vipande na wajumbe wa baraza.

Acts 23:11

Ni ahadi gani Bwana alimpatia Paulo usiku uliofuata?

Bwana alimwambia Paulo asiogope kwasababu atabeba ushuhuda wake katika Jerusalemu na Rumi.

Acts 23:12-13

wanaume wa Kiyahudi waliweka agano gani kuhusiana na Paulo?

Takribani Wayahudi arobaini waliweka agano kwamba hawatakula wala kunywa mpaka watakapomwua Paulo.

Acts 23:14-15

Ni mpango upi wayahudi arobaini waliuwasilisha kwa wakuu wa makuhani na wazee?

Waliwaomba wakuu wa makuhani na wazee kwamba Paulo aletwe barazani ili wamwue kabla hajafika.

Acts 23:16-21

Jemedari mkuu alijuaje kuhusu mpango wa Wayahudi arobaini?

Mtoto wa dada yake Paulo alisikia mpango huo na kumwambia Paulo.

Acts 23:22-27

Jemedari mkuu alifanyaje alipoufahamu mpango wa Wayahudi arobaini kutaka kumwua Paulo?

Jemedari mkuu aliagiza kundu kubwa la walinzi la kumchukua Paulo kwa usalama mpaka kwa Gavana Feliki katika zamu ya tatu ya usiku.

Acts 23:28-33

Kwenye barua yake kwa Gavana Feliki Jemedari Mkuu alisemaje juu ya mashitaka dhidi ya Paulo?

Jemedari Mkuu alimwandikia kuwa Paulo hakutakiwa kuuawa wala kufungwa, bali mashitaka yote yalilenga maswala yahusuyo sheria ya Wayahudi.

Acts 23:34-35

Nu muda upi Gavana Feliki alipanga kusikiliza kesi ya Paulo?

Gavana Feliki alisema angeisikiliza kesi ya Paulo baada ya washitaki wake kuwasili.

Paulo alitunzwa wapi kusubiri mateso yake?

Paulo alitunzwa katika makao ya Herode mpaka wakati wa mateso yake.

Acts 24

Acts 24:4-9

Mashitak gani Tetulo aliyaleta dhidi ya Paulo?

Tetulo alimshitaki Paulo kwa kusababisha Wayahudi kuasi na kulinajisi hekalu.

Acts 24:10-13

Nini alichokuwa amefanya Paulo hekaluni, Masinagogi na mjini?

Paulo alisema alikuwa hajawahi kupingana na yeyote na alikuwa hajawahi kuhamasisha kundi lolote.

Acts 24:14-16

Paulo alisema yeye ni mwaminifu kwa yapi?

Paulo alisema alikua mwaminifu kwa yote yaliyo katika sheria na maandiko ya manabii.

Tumaini lipi alilolishirikisha kwa Wayahudi waliomshitaki Paulo?

Aliwashirikisha tumaini la Mungu kuja kuwafufua walio haki na wafu wasio haki.

Acts 24:17-21

Kwanini Paulo alikuwa amekwenda Yerusalemu?

Paulo alisema amekuja kuleta msaada kwa taifa lake na zawadi ya fedha.

Paulo alikuwa anafanya nini hekaluni alipoonekana na Wayahudi toka Asia?

Paulo alisema alikuwa katika taratibu za utakaso wakati alipoonekana na Wayahudi hao wa Asia.

Acts 24:22-23

Liwali Feliki alikuwa ametaarifiwa kuhusu nini?

Liwali Feliki alikua ametaarifiwa vizuri kuhusu njia.

Lini Feliki alisema ataamua kesi ya Paulo?

Feliki alisema ataamua kesi ya Paulo pindi Lisia jemedari atakapokuja kutoka Yerusalemu.

Acts 24:24-25

Baada ya siku kadha, Paulo alimwambia Feliki kuhusu nini?

Paulo alimwambia Feliki kuhusu imani ndani ya Kristo, utakatifu, kuwa na kiasi na hukumu itakayokuja.

Feliki aliitikiaje baada ya kumsikiliza Paulo?

Feliki alijawa na hofu na alimwomba aondoke mbele yake.

Acts 24:26-27

Baada ya miaka miwili, Kwanini Feliki alimwekea ulinzi Paulo wakati Gavana mpya alipokuja?

Feliki alimwacha Paulo chini ya ulinzi kwasababu alitaka kupata upendeleo kwa Wayahudi.

Acts 25

Acts 25:1-3

Ni upendeleo gani Kuhani Mkuu na Wayahudi mashuhuri waliuomba kwa Festo?

Walimwomba Festo kumwita Paulo kwenda Yerusalemu ili waweze kumwua akiwa njiani.

Acts 25:4-8

Festo aliwaambia nini cha kufasnya Kuhani Mkuu na Wayahudi mashuhuri?

Festo aliwambie waende kwa Kaisari , kule Festo alikuwa anaenda, ili wakaweze kumshitaki Paulo kule.

Acts 25:9-10

Alipokuwa akihukumu kesi ya Paulo huko Kaesaria ni swali gani Festo alimwuliza Paulo?

Festo alimwuliza Paulo kama alitaka kwenda Yerusalemu kuhukumiwa huko.

Kwa nini Festo alimuuliza Paulo swali hili?

Festo alimwuliza Paulo swali hilo ili ajipendekeze kwa wayahudi.

Jibu la Paulo lilikuwaje kuhusiana na swali la Festo?

Paulo alijibu alikuwa amesimama mbele ya kiti cha hukumu cha Kaisari mahali ambapo angepaswa kuhukumiwa.

Acts 25:11-12

Festo alikusudia kufanya nini katika kesi ya Paulo?

Festo alikusudia kwamba kwa vile Paulo alikuwa amemtaja Kaisari hivyo angemtuma kwenda kwa Kaisari

Acts 25:13-16

Festo alisema ni kitu gani kilikuwa halali kwa dwsturi ya warumi kwa watu waliotuhumiwa kwa uhalifu?

Festo alisema Warumi walitoa nafasi kwa mshitakiwa kwenda mbele ya washitaki wake na kujenga utetezi dhidi ya mashitaka yake.

Acts 25:17-24

Ni mashitaka yapi aliyoyasema Festo yaliyoletwa na Wayahudi dhidi ya Paulo?

Festo alisema Mashitaka yalikuwa juu ya dini yao, na yahusuyo madayi ya kusema Yesu aliyekuwa ameuawa, Paulo alidai kuwa alikuwa hai tena.

Acts 25:25-27

Kwanini Festo alimpeleka Paulo mbele ya Mfalme Agripa?

Festo alitaka Mfalme Agripa amsaidie kuandika hoja za msingi kuhusu kesi ya Paulo kwa Mfalme.

Kwanini Festo alisema isingefaa kwake kumtuma Paulo kwa Mfalme?

Festo alisema isingefaa kwake kumtuma Paulo kwa Mfalme bila ya kuelezea mashitaka dhidi ya Paulo.

Acts 26

Acts 26:1-3

Kwanini Paulo alikuwa na furaha kuweza kusimama na kujitetea mbele ya Mfalme Agripa?

Paulo alikuwa na furaha kuweza kujitetea mbele ya Mfalme Agripa kwasababu Agripa alikuwa na ujuzi wa desturi za Wayahudi na maswali.

Acts 26:4-5

Jinsi gani Paulo aliweza kuishi toka ujana wake huko Yerusalemu?

Paulo aliisha kama Farisayo, Kikundi chenye msimamo mkali katika dini ya kiyahudi.

Acts 26:6-8

Ni ahadi gani ya Mungu ambayo Paulo na Wayahudi wanatarajia kuifikia?

Paulo alisema kuwa yeye na wayahudi wanatarajia kuifikia ahadi ya ufufuo.

Acts 26:9-11

Kabla ya kuongoka kwake, Paulo alikuwa akifanya nini kulipinga jina la Yesu wa Nazareti?

Paulo alikuwa akiwafungia Watakatifu wengi gerezani, alikuwa akiidhinisha wakati wakiuawa, na alikuwa anawafukuza kwenda miji ya ugenini.

Acts 26:12-14

Paulo aliona nini wakati akienda Dameski?

Paulo aliona mwanga kutoka mbinguni uliong'aa kuliko jua.

Paulo alisikia nini wakati akienda Dameski?

Paulo alisikia sauti ikisema, "Sauli, Sauli, kwanini unanitesa?

Acts 26:15-18

Nani alikuwa akiongea na Paulo alipokuwa akielekea Damaskasi?

Yesu alikuwa akiongea na Paulo alipokuwa njiani kuelekea Damaskasi.

Yesu alimchagua Paulo kufanya nini?

Yesu alimchagua Paulo kuwa mtumishi wake na mwenye kupeleka ushuhuda kwa mataifa.

Yesu alitaka mataifa wapokee nini kupitia kwa Paulo?

Yesu alimwambia, alitaka mataifa kupokea msamaha wa dhambi zao na kupokea urithi kutoka kwa Mungu.

Acts 26:19-21

Mambo gani mawili Paulo aliyahubiri kila alipokwenda?

Paulo anasema, alihubiri watu wapate kutubu na kumgeukia Mungu, na pia watende matendo yakanayo na thamani ya toba yao.

Acts 26:22-23

Ni kitu gani manabii na Musa walisema kigetokea?

Manabii na Musa walisema kwamba Kristo atateseka, atafufuliwa kutoka kwa wafu, na kutangaza nuru kwa Wayahudi na kwa mataifa.

Acts 26:24-26

Je Festo alimfikiriaje Paulo baada ya kusikiliza utetezi wake?

Festo alidhani kuwa Paulo alikuwa mwendawazimu.

Acts 26:27-29

Tamaa ya Paulo ulikuwa nini kwa Mfalme Agripa?

Paulo alitamani Mfalme Agripa angekuwa mkristo.

Acts 26:30-32

Ni uamzi upi uliotolewa na Mfalme Agripa, Festo na Bernike kuhusu mashitaka dhidi ya Paulo?

Walikubaliana kusema Paulo hakutenda lolote lenye kustahili kifo ama kifungo, na kwamba angekuwa huru kama asingekuwa amekata rufaa kwa Kaisari.

Acts 27

Acts 27:3-6

Vipi ambavyo jemadari Julius alimtendea Paul katika mwanzo wa safari kuelekea Roma?

Julius alimtendea Paulo vizuri na kumruhusu kwenda kwa rafiki zake na kupokea huduma zao.

Acts 27:7-8

Ni kisiwa kipi meli ya Paulo ilipita kwa kuzunguka kwa shida?

Meli ilisafiri kuzunguka kisiwa cha Krete kwa shida.

Acts 27:9-13

Kwanini Julias hakukubali kufuata maonyo ya Paulo kuhusu hatari iliyokuwa inawakabiri wakiendelea na safari?

Julius hakutaka kufuata maonyo ya Paulo kwasababu alisikiliza zaidi maelekezo ya mmiliki wa meri.

Acts 27:14-18

Baada ya kuanza kwa safari, upepo gani ulianza kupiga chini ya meli?

Baada ya kuanza safari taratibu , upepo ulioitwa Kaskazi-mashariki ulianza kupiga chini ya meli.

Acts 27:19-22

Baada ya siku nyingi, Tumaini lipi lilikuwa limetoweka kwa watumishi wa meli?

Baada ya siku nyingi watumishi wa meli walikuwa wamepoteza tumaini la kuwa salama tema.

Acts 27:23-26

Ni ujumbe gani Paulo alipewa na malaika juu ya watu waliokuwa wakidsafiri pamoja naye?

Malaika alimwambia Paulo kwamba yeye na wote waliokuwa wakisafiri wangeweza kupona.

Acts 27:27-29

Wakati wa usiku wa manane katika usiku wa kumi na nne, mabaharia walifikiri nini kilichokuwa kinakwenda kutokea kwenye meli?

Mabaharia waliwazo meli ilikuwa inakaribia sehemu ya nchi kavu.

Acts 27:30-32

Mabaharia walikuwa wakitafuta jinsi gani ya kufanya?

Mabaharia walikawa wanatafuta njia kuiacha meli yao.

Paulo alimwambiaje Juluas na maaskari juu ya Mabaharia?

Paulo aliwaambia Julius na maaskari kuwa mabaharia wasipobaki kwenye meli, wote Julius na maaskari hakuna ambaye angepona.

Acts 27:33-38

Wakati wa mchana ulikuwa anakuja juu, nini Paulo aliwahimiza kila mmoja cha kufanya?

Paulo aliwahimiza wote wale chakula.

Acts 27:39-41

Kwa vipi wafanyakazi waliamua kuiegesha meli pwani, na nini kilitokea?

Wafanyakazi waliamua kuegesha meli pwani na kuipitisha moja kwa moja kuelekea pwani, lakini nanga ya meli ikawa imekwama ardhini na usukani ukavunjika .

Acts 27:42-44

Askari walitaka kuwatendea nini wafungwa wakati huu?

Askari walikuwa wanaenda kuwaua wafungwa ili hakuna hata mmoja ageweza kutoroka.

Kwanini askari wa kirumi aliuzuia mpango wa maaskari?

Askari aliuzuia mpango wa askari kuwaua wafungwa kwasababu alitaka kumwokoa Paulo.

Namna gani watu melini waliweza kufika salama katka nchi kavu?

Walioweza kuogelea waliruka kwanza na waliosalia walifuatia walitumia vipande vya mbao na wengine juu ya vitu vingine kutoka melini.

Acts 28

Acts 28:1-2

Wenyeji wa kisiwa cha Malta waliwahuhumiaje Paulo na watumishi wote wa meli?

Watu wale waliwahudumia kwa ukarimu zaidi

Acts 28:3-4

Watuwalifikiri nini walipomwona nyoka amening'inia katika mkono wa Paulo?

Watu walidhani alikuwa mwuuaji ambaye asingepaswa kuishi kwa haki.

Acts 28:5-6

Watu walifikiri nini walipomwona Paulo akiendelea kuishi bila kufa baada ya kung'atwa na nyoka?

Watu walidhani kuwa Paulo alikuwa miungu.

Acts 28:7-12

Nini kilitokea Baada ya Paulo kumponya baba yake na Pablio mkuu wa kisiwa kile?

Baadhi ya watu wa kisiwa waliokuwa wagonjwa pia walikuja kwake na wakaponywa.

Acts 28:13-15

Paulo alifanya nini alipowaona ndugu kutoka Rumi kukutana naye?

Wakati alipowaona ndugu hao , Paulo alimshukuru Mungu na ujasiri ukaongezeka.

Acts 28:16-18

Nini ilikuwa mipango ya maisha ya Paulo katika Rumi kama mfungwa?

Paulo aliruhusiwa kukaa peke yake pamoja na askari aliyekuwa mwenye kumlinda.

Acts 28:19-20

Kwasababa ipi Paulo aliwaambia Wayahudi viongovi waliokuwa Rumi kuwa amekuwa katika vifungo?

Paulo aliwaambia Wayahudi viongozi katika Rumi amekuwa kifungoni kwa tumaini la Israeli

Acts 28:21-22

Wayahudi viongozi katika Rumi walijuaje ukristo ni dini?

Wayahudi viongozi katika Rumi walijua ukristo ni dini kwa kuwa ilikuwa ikipingwa kila mahali.

Acts 28:23-24

Wakati viongozi wa Kiyahudi alipokuja tena kwa Paul katika makao yake, ni nini Paulo alijaribu kufanya tangu asubuhi hata jioni?

Paul alijaribu kuwashawishi kuhusu Yesu, kutoka katika sheria ya Musa na kutoka kwa manabii.

Mwitikio wa Wayahudi viongozi ulikuwaje katika hoja za Paulo?

Baadhi ya Wayahudi viongozi walishawishika, wakati wengine hawakuamini.

Acts 28:25-27

Nini ambacho maandiko ya mwisho yalinukuliwa na Paulo akisema kuhusu viongozi wa Wayahudi ambao hawakuamini?

Andiko la mwisho Paulo alinukuu aakisema kwamba wale ambao hawakuamini wasingeweza kufahamu walichokisikia wala kuona kwa macho yao.

Acts 28:28-29

Wapi ambapo Paulo alisema ujumbe wa Mungu wa wokovu aliokuwa ametumwa, na nini mwitikio wake?

Paul alisema kuwa ujumbe wa Mungu wa wokovu ulikuwa umetumwa kwa watu wa mataifa na wangeweza kusikiliza.

Acts 28:30-31

Paulo alifanya nini akiwa mfungwa huko Rumi?

Paulo alitangaza ufalme wa Mungu na kufundisha habari za Yesu Kristo kwa ujasiri wote.

Nani aliyemzuia Paulo kuhubiri na kufundisha wakati akiwa mfungwa huko Rumi kwa miaka miwili?

Hakuna yeyote aliyamzuia kuihubiri Injili.