Esther
Esther 1
Esther 1:1-2
Ahasuero alitawala hadi wapi
Ahasuero alitawala kutoka India hadi Ethiopia, juu ya majimbo 127.
Esther 1:3-4
Ni nani aliyekuwa katika uwepo wa mfalme?
Mfalme wa Uajemi na Umedi, na wasimamizi waheshimiwa na magavana wa majimbo walikuwa katika uwepo wake.
Esther 1:5-6
Karamu ambayo ilidumumu kwa siku saba ilikuwa kwa ajili ya nani?
Karamu ya siku ya saba ilikuwa kwa ajili ya watu wote katika ikulu ya Shushani, tangu mkuu hadi mdogo.
Mfalme alitoa karamu kwa ajili ya nani?
Karamuilikuwa kwa ajili ya watu wote katika ikulu ya Shushani, tangu mkuu hadi mdogo.
Esther 1:7-8
Ni kwa nini kulikuwa na divai nyingi ya kifalme?
kulikuwa na mvinyo nyingi ya kifalme kwa sababu ya ukarimu wa mfalme.
Maagizo ya mfalme yalikuwa ni nini kwa viongozi wote wa ikulu?
Mfalme alitoa maagizo kwa wahudumui wote wa ikulu yake kufanya kwa ajili yao chochote alichotamani mgeni.
Esther 1:9-12
Mfalme aliwambia nini maafisa saba waliotumika mbele zake?
Mfalme aliwambia maafisa saba waliotumika mbele zake kumleta Malkia Vashiti mbele zake akiwa katika mavazi yake ya kimalkia.
Esther 1:13-15
Mfalme aliwaendea wakina nani?
Mfalme aliwaendea wanaume ambao walijulikana kuwa wenye hekima, ambao walizijua nyakati?
Esther 1:16-18
Kulingana na maelezo ya Mekukani Vashiti alikuwakosea wakina nani?
Memukani akasema sio tu kwamba Vashiti amemkosea mfalme, bali kwa maafisa na watu wote walio katika majimbo yoteya Mfalem Ahusiero?
Memukani alisema wanawake wa wakuu wa Uajemi na Umedi hatimaye wangefanya nini kabla ya siku hiyo?
Alisema kwamba kabla ya siku hiyo wanawake wa wakuu wangewakataa/ kugomea maafisa wa mfalme.
Esther 1:19-20
Ni kwa nani ambaye mfalme angempa nafasi ya Vashiti kama malikia?
Mfalme angempa mtu nafasi ya Vashiti kama angekuwa bora kuliko Vashiti.
Esther 1:21-22
Mfalme aliamuru nini?
Mfalme aliamuru kwamba kila mme lazima awe bwana wa nyumba yake mwenyewe.
Esther 2
Esther 2:1-2
vijana wa mfalme walishauri nin?
Kisha vijana wa mfalme wakashauri kutafuta kufanyike kwa niaba ya mfalme kwa ajili ya mabikira warembo.
Esther 2:3-4
Mabikira waliwekwa chini ya uangalizi wa nani?
Mabikira waliwekwa chini ya uangalizi wa Hega, mtumishi, ambaye alikuwa msimamizi wa wanawake.
Esther 2:5-6
Ni nani aliyekuwa amechukua Modekai Yerusalemu?
Nebuakadreza mfalme wa Baberi alikuwa amemchukua Modekai kutoka Yerusalemu.
Esther 2:7
Jina jingine la Esta lilikuwa nani?
Jina jingine la Esta lilikuwa Hadasa
Esta alikuwa ana uhusiano gani na Modekai?
Esta alikuwa binti wa mjomba wake na Modekai.
Esther 2:8-9
Hegai alimpa na kitu gani Esta?
Hegai alimpa vipodozi na sehemu yake ya chakula na kumkabidhi watumishi saba wasichana kutoka katika ikulu ya mfalme.
Esther 2:10-11
Ni kwa nini Esta hakuwa amemwambia mtu kuhusu jamaa na ndugu zake walikuwa wakina nani?
Esta hakuwa amemwambia mtu yeyote watu wake na jamaa zake walikuwa wakinani, kwa maana Modekai alikuwa amwelekeza asiwaambie.
Esther 2:12-13
wakati msichana alipoenda kwa mfalme, alipewa nini?
Wakati msichana alipoenda kwa mfalme alipewa chochote alichopenda.
Esther 2:14
Ni lini msichana alipaswa kurudi kwa mfalme?
Msichana alsingeweza kurudi tene kwa mfalme isipokuwa amefurahisha na kumuita tena.
Esther 2:15-16
Esta aliomba kwa ajili ya nini?
Hakuomba kitu chochote isipokuwa vitu ambavyo Hegai mtumishi, aliyekuwa msimamizi wa wanawake alivipendekeza aende navyo.
Ni wakati gani Esta alipelekwa kwa Mfalme Ahusiero?
Esta alipelekwa kwa Mfalme Ahusiero mwezi wa wa kumi, ambao ni mwezi wa Tebethi katika mwaka wa saba wa utawala wake.
Esther 2:17-18
Kwa nini mfalme alimvika Esta taji ya kimalikia kichwani na kumfanya malkia?
Mfalme alimpenda zaidi Esta kuliko wanawake wote na alipata kibari na wema mbele zake, zaidi kuliko mabikira wengine, hivyo akamvika taji ya kimalkia juu ya kichwa chake na akamfanya malkia.
Esther 2:19-21
Ni kitu gani ambacho Bigthani na Tereshi walitafuta kwa Mfalme Ahusiero?
Bigtahni na Tereshi walihitaji kumdhuru Mfalme Ahusiero.
Esther 2:22-23
Ni kilitokea kwa Bigthani na Tershi?
Wanaume wawili walitundikwa juu ya mti.
Esther 3
Esther 3:1-2
Ni wakinani waliopiga magoti na kumwinamia Hamani?
Watumishi wote wa mfalme waliokuwa katika lango la mfalme mara zote walpiga magoti na kuinama mbele za Hamani.
Esther 3:3-4
Modekai alikataa kufanya nini?
Modekai alikataa kufuata matakwa ya watumishi wa mfalme.
Esther 3:5-7
Hamani alitaka kumuua nani?
Hamani alitaka kumuua Modekai na Wayahudi wote.
Esther 3:8-11
waliopiga kura, ni mwezi gani waliochagua?
walipopiga kura walichagua mwezi wa kumi na mbili (mwezi wa Adari).
Ni kiasi gani cha fedha ambacho Hamani alikuwa tayari kuweka katika hadina ya mfalme kama mfalme angetoa amri ya kuuwawa kwa Wayahudi.
Hamani alikuwa tayari kuweka talanta elfu kumi za fedha katika hazina ya mfalme kama mfalme angetoa amri ya kuuwawa Wayahudi.
Esther 3:12-13
Nyaraka zilifikishwaje katka majimbo yote ya mfalme?
Nyaraka zilikuwa zikipelekwa kwa mikono kwa wapelekaji katika majimbo yote ya mfalme.
Esther 3:14-15
Mji wa Shushani uliitikiaje juu ya mbiu?
Mji wa Shushani ulikuwa katika uangamivu.
Esther 4
Esther 4:1-3
Modekai alienda umbali gani? na kwa nini?
Alienda wa lango la mfalme, kwa sababu hakuna mtu aliye ruhusiwa kuingia akiwa amevaa magunia.
Esther 4:4-5
Modekai alijibu namna gani wakati Esta alipopeleka nguo ili Modekai avae?
Wakati Esta alipeleka nguo ili Modeka avikwe hakuzipokea.
Esther 4:6-8
Modekai alieleza nini kwa Hathaki?
Modekai alimweleza Hathaki yote ambayo yaliyotokea kwake,na jumla ya fedha ambayo Hamani alikuwa ameahidi kutoa na kuiweka katika mifuko ya mfalme ili kwamba kuwauwa Wayahudi.
Ni kwa nini Modekai alimpa Hathaki nakala ya mbiu ambayo ilikuwa imetolewa katika mji Shushani kwa ajili ya maangamizi ya Wayahudi?
Modekai alifanya hivi ili kwamba Hathaki amwonyeshe Esta, na ili kwamba Hathaki ampe jukumu la kwenda kwa mfalme kuomba kibali n kuomba pamoja naye kwa niaba ya watu wake.
Esther 4:9-12
Ni nini kilitokea kama mtu mme au mke alienda kwa mfalme ndani ya uwa wa ndani pasipo kuruhusiwa?
Kama mtu mme au mtu mke alienda ndani uwa pasipo ruhusa, kulikuwa na sheria moja tu: kwamba ni lazima auwawe-isipokuwa yeyote yule ambaye mfalme amemnyoshea fimbo ya dhahabu ili aishi.
Esther 4:13-14
Modekai alisema nini kingetokea kama Esta angeendelea kunyamaza kimya?
Kama Esta angeendelea kukaa kimya kwa wakati huo, msaada na wokovu kwa Wayahudi ungekuja kutoka sehemu nyingine, lakini Esta na nyumba ya baba yake wangeangamia.
Esther 4:15-17
Esta alimwambia Modekai kufanya nini?
Esta alimwambia Modekai kuwakusanya Wayahudi wote walioishi katika mji wa Shushani ngomeni, na kuwaambia kufunga kwa siku tatu kwa ajili yake.
Esther 5
Esther 5:1-2
uwa wa ndani wa ikulu ya mfalme ulikuwa wapi?
uwa wa ndani wa ikulu ya mfalme ulikuwa mbele ya nyumba ya mfalme.
Ni kwa nini mfalme wakati alipomwona malkia Esta amesimama ndani ya ua, alimnyoshea fimbo yake ya dhahabu katika mkono wake?
Esta alipata kibali katika uso mbele yake, hivyo aliinyosha fimbo yake ya dhahabu katika mikono yake.
Esther 5:3-6
Esta aliomba nini kutoka kwa mfalme?
Aliomba kwamba mfalme na Hamani wahudhurie kwenye karamu aliyokuwa ameiandaa kwa ajili ya mfalme.
Esther 5:7-8
Kwa mara ya pili Esta aliomba nini kutoka kwa mfalme?
Aliomba kwamba mfalme na Hamani wahudhurie kwenye karamu aliyokuwa ameiandaa kwa ajili yao.
Esther 5:9-11
Hamani aliisimlia nini familia yake?
Hamani aliwasimlia utukufu wa utajiri na idadi ya wana wake wengi, alivyo kuwa amepanda juu ya maafisa na watumishi wa mfalme.
Esther 5:12-13
Ni kwa nini Hamani alihisi kwamba kualikwa kwake katika karamu haikikuwa kitu cha thamani kwake?
Kualikwakatika karamu hakikuwa kitu kitu cha kufaa kama alimwona Modekai Myahudi akiwa ameketi kwenye lango la mfame.
Esther 5:14
Zereshi alimwambia Hamani atengeneze nini? Kwa nini?
Zereshi alimwambia kutengeneza mti wa futi hamsini kwenda juu ili kwamba amtundike Modekai juu yake.
Esther 6
Esther 6:1-3
Kwanini mfalme aliwaamuru watumishi kuleta vitabu vya kumbukumbu ya matukio wa utawala wake?
Usiku huo mfalme hakuweza kulala, hivyo akawaamuru watumishi walete vitabu vya kumbukumbu ya matukio ya utawala wake.
Ni kitu gani cha heshima alichokuwa amefanyiwa Modekai kwa kutambua kazi aliyoifanya ya kumwambia mfalme kuhusu Bghana na Tereshi?
Hakuna kilichokuwa kimefanyika cha kumpa heshima au kutambua kazi ya Modekai ya kumwambia mfalme kuhusu Bighana na Tereshi.
Esther 6:4-6
wakati mfalme alimuuliza Hamani nini afanyiwe mtu yule ambaye mfalme ampenda na kumheshimu, Hamani alifikiri mfalme alikuwa akiongea kumuhusu nani?
Wakati mfalme alipomuuliza Hamani nini afanyiwe nini mtu yule ambaye mfalme ampenda na kumuheshimu, Hamani akafikiri mfalme alikuwa akiongea kumuhusu yeye.
Esther 6:7-9
Nani angemvisha mtu ambaye mfalme ampenda na kumuheshimu, na wampandishe kumpitisha juu ya farasi na kumpitisha katika mitaa yote ya mji?
Mmoja wa maafisa wa mfalme angeweza kumvisha mtu yule ambaye mfalme ampenda na kumuheshimu akampandisha juu ya farasi na kumpitisha katika mitaa.
Esther 6:10-11
Ni nani aliyemvalisha Modekai na kumpitisha katika mitaa akiwa juu ya farasi?
Hamani alimvisha Modekai na kumpitisha katika mitaa akiwa juu ya farasi.
Esther 6:12-14
Mkewe Hamani na marafiki wa Hamani walimuunya kuhusu nini?
Mkewe na marafiki zake wenye hekima walisema, kama Modekai alikuwa ni Myahudi, Hamani asingeweza kumshinda badala yake angeweza kuanguka mbele zake.
Esther 7
Esther 7:3-5
Ombi la Esta lilikuwa nini?
Alitaka maisha yake na ya watu wake apewe.
Esta lisema angefanya nini kama watu wake wangekuwa wameuzwa utumwani?
Kama watu wake wangekuwa wameuzwa utumwani, alisema angekaa kimya.
Esther 7:6-7
Ni nani ambaye Esta alimuelezea kama 'Mtu mwovu, yule adui..."
Haya yalikuwa ni maelezo kuhusu Hamani.
Hamani alifanya nini wakati mfalme alipoinuka katika ghadhabu kutoka kwenye sehemu ya mvinyo?
Mfalme alipoamka katika ghadhabu kutoka kwenye sehemu ya kunywea mvinyo, Hamani alibaki kuomba usalama wa maisha yake kwa malkia Esta.
Esther 7:8
Baada ya Hamani kuanguka juu ya kochi mahali ambapo Esta alikuwa, mfalme alifikiri Hamani alikuwa anafanya nini?
Baada ya Hamani kuanguka juu ya kochi mahali ambapo Esta alipokuwa, alidhani alikuwa akimdharirisha malkia mbele ya uwepo wa mfalme.
Esther 7:9-10
Mfalme alisema Hamani atundikwe wapi?
Mfalme alisema Hamani na familia yake watundikwe katika miti ambayo Hamani alikuwa ameiandaa kwa ajili Modekai.
Esther 8
Esther 8:1-2
Kwa nini Modekai alianza kutumika mbele za mfalme?
Modekai alianza kutumika mbele ya mfalme, kwa maana Esta alimwambia mfalme jinsi ambavyo alikuwa na uhusiano wa kindugu na Modekai.
Kwa nini Modekai alikuwa msimamizi wa shamba la Hamani?
Esta alimuhidhinisha Modekai kuwa msimamizi wa shamba la Modekai.
Esther 8:3-4
Mfalme alifanya nini ili kwamba Esta angeweza inuka na kusimama mbele yake?
Mfalme alimnyoshea Esta fimbo ya dhahabu, hivyo aliinuka akasimama mbele ya mfalme.
Esther 8:5-6
Ni barua gani Hamani aliziandika?
Hamani aliandika kuhusu kuwaharibu Wayahudi ambao walikuwa katika majimbo yote ya mfalme.
Esther 8:7-8
Ni kwa nini Esta alipaswa kuandika mbiu nyingine kwa ajili ya Wayahudi kwa jina la mfalme?
Esta alihitaji kuandika mbiu nyingine kwa jina la mfalme, kwa kuwa mbiu ya kwanza iliyokuwa imeandikwa kwa jina la mfalme na kugongwa muhuri kwa pete ya mfalme isingeweza kubatilishwa.
Esther 8:9
Waandishi wa mfalme waliweza kuitwa lini?
Waandishi wa mfalme waliitwa mwezi wa tatu, ambao ni mwezi wa Sivani, siku ya ishirini na tatu ya mwezi.
Esther 8:10-14
Mfalme aliwapa ruhusa Wayahudi kufanya nini?
Mfalme aliwapa Wayahudi ruhusa ya kukusanyika kwa pamoja na kujilinda; kuua na kuharibu na kuharibu jeshi lolote au mtu yeyote kutoka jimbo lolote ambaye angeweza kuwashambulia, watoto na wanawake wakijumuishwa au kutaifisha mali zao.
Esther 8:15-17
Kwa nini wengi kutoka kwa watu mbalimbali wa nchi walikuwa Wayahudi?
Wengi kutoka miongoni mwa watu wengi wa nchi walikuwa Wayahudi, kwa sababu hofu ya Wayahudi ilikuwa imewaangukiwa.
Esther 9
Esther 9:1-2
Kwa nini hakuna hata mmoja angeweza kusimama kinyuma na Wayahudi?
Hakuna mmoja angeweza kinyume na Wayuhudi, kwa maana hofu yao ilikuwa juu ya watu.
Esther 9:3-10
Wayahudi waliwafanyia nini maadaui zao?
Wayahudi waliwashambulia maadui zao kwa upanga, wakiwauwa na kuwaharibu , na kufanya kama ilivyowapendeza kwa wale waliwachukia.
Esther 9:11-12
Wayahudi waliwaua watu gani?
Wayahudi waliwauwawatu mia tano katika mji wa Shushani ngomeni, pamoja na watoto kumi wa Hamani.
Esther 9:13-14
Ni nini kilitokea kwa miili ya watoto kumi wa Hamani?
Miili ya wana kumi wa Hamani ilitundikwa juu ya miti.
Esther 9:15-16
Ni wanaume wangapi ambao Wayahudi waliwauwa siku ya kumi na nne ya mwezi wa Adari?
Siku ya kumi na nne ya mwezi wa Adari, Wayahudi waliuwa wanaume mia tatu zaidi katika mji wa Shushani ngomeni.
Esther 9:17-19
Ni kwa nini Wayahudi wa vijijini waliadhimisha siku ya kumi na nne ya mwezi wa Adari kama siku ya furaha na ya sherehe?
Wayahudi wa vijijini waliadhimisha siku ya kumi na nne ya mwezi wa Adari kama siku ya furaha na sherehe kwa sababu waliacha kuua, na walipumzika na wakaifanya siku hiyo kuwa ya sherehe na furaha.
Esther 9:20-22
Ni mara ngapi Modekai aliwaamuru Wayahudi kuitunza siku ya kumi na nne na ya kumi na tano ya Adari.
Modekai aliwaamuru kutunza siku ya kumi na nne na ya kumi na tano ya Adari kila mwaka.
Esther 9:23-25
Puri ina maana gani?
Puri ina maana ya 'kura.'
Esther 9:26-32
Ni kwa nini Wayahudi na watoto wao hawakuacha kuwa waaminifu katika kuadhimisha siku hizi za Purimu?
Wayahudi na watoto wao wasingeweza kuazimisha kwa uaminifu siku hizi za Purimu, ili kwamba wasiwe kusahahau.
Esther 10
Esther 10:1-2
Ni wapi Mfalme Ahusiero aliweka kodi wapi?
Mfalme Ahusiro aliweka kodi juu ya nchi na nchi zote za mwambao wa bahari.
Mafanikio yote ya nguvu na ukuu wa Mfalme Ahusiero ulikuwa umeandikwa wapi?
Mafanikio na nguvu na ukuu vilikuwa vimeandikwa katika Kitabu cha kumbukumbu za Wafalme wa Wamedi na Waajemi.
Esther 10:3
Ni cheo gani ambacho Modekai Myahudi alikuwa nacho?
Modekai Myahudi alikuwa wa pili katika cheo kwa mfalme Ahusiero
Ni kwa niniModekai alikuwa mkuu na maarufu miongoni mwa Wayahudi na ndugu zake wengi Wayahudi?
Alikuwa mkuu na maarufu miongoni mwa ndugu zake Wayahudi, kwa maana alitafuta masirahi ya watu wake, na alitetea amani ya watu wake wote.