Habakkuk
Habakkuk 1
Habakkuk 1:1-2
Swali gani Habakuki anamuuliza Yahwe anapoanza kutangaza wazi?
Habakuki anauliza kwanini Yahwe hajasikia au hajamwokoa yeye, ingawaje amelia apate msaada.
Habakkuk 1:3-4
Nini ambacho amefanywa Habakuki aone?
Habakuki amefanywa aone dhambi, matendo maovu, uharibifu, uasi, migongano na ukinzani.
Aina gani ya haki inayoendelea?
Haki isiyo ya kweli inaendelea.
Habakkuk 1:5-7
Yahwe anamwambia nini Habakuki ambacho ataona nyakati zake?
Yahwe anasema kwamba Habakuki ataona Wakaldayo wanatembea kupitia ardhi kutwaa makao.
Wakaldayo ni watu wa namna gani?
Wakaldayo ni wakutetemesha na wakuogofya.
Habakkuk 1:8-9
Wakaldayo walikusanya nini kwa vurugu?
Wakaldayo walikusanya mateka kwa vurugu kama mchanga.
Habakkuk 1:10-11
Mtazamo wa Wakaldayo kuelekeawafalme na watawala wengine ulikuwa ni nini?
Wakaldayo walidhihaki wafalme na watawala wengine.
Habakkuk 1:12
Nani aliyeamuru kwamba Wakaldayo waje kuleta hukumu?
Yahwe ameamuru kwmba Wakaldayo waje na kuleta hukumu.
Ni vyeo gani Habakuki anatumia kwaajili ya Yahwe?
Habakuki anatumia vyeo "Mungu wangu," "aliye mtakatifu" na "Mwamba" kwaajili ya Yahwe.
Habakkuk 1:13-14
Swali au lawama ipi Habakuki anafanya kwa Yahwe?
Habakuki anamuuliza Yahwe kwanini yeye yuko kimya wakati uovu unawameza wale wenye haki zaidi.
Habakkuk 1:15-17
Wale ambao wanawachinja mataifa wanafurahia kuhusu nini?
Wanafurahia jinsi wanavyokusanya na kuwaburuta.
Kazi gani Habakuki anasema inafanana na kusanyiko la watu kwaajili ya hukumu?
Habakuki anasema kusanyiko la watu kwaajili ya hukumu ni kama nyavu za kutegea samaki.
Hisia gani wanakosa wale ambao wanachinja mataifa?
Wale wanaochinja mataifa wanapungukiwa huruma.
Habakkuk 2
Habakkuk 2:1
Habakuki aliangalia nini kwa makini?
Habakuki aliangalia kwa makini kuona ambacho Yahwe angesema kwake?
Habakkuk 2:2-3
Yahwe alimwambia nini Habakuki afanye kuhusu maono?
Yahwe alimwambia Habakuki ayaandike maono juu ya kibao.
Yahwe alimpa Habakuki uhakika gani kuhusiana na badaye?
Yahwe alimhakikishia kwamba maono haya yangenena hata kama yanachelewa.
Habakkuk 2:4-5
Yahwe alisema wenye haki wataishije?
Yahwe alisema wenye haki wataishi kwa imani.
Vitu gani vitatu Yahwe alisema haviridhiki?
Yahwe anasema kijana mwenye tamaa ya kiburi, kaburi na kifo huwa haviridhiki.
Habakkuk 2:6-8
Yahwe anasema kitatokea nini kwa kijana mwenye kiburi ambaye anateka mataifa mengi?
Yahwe anasema kijana mwenye kiburi atatekwa na mabaki ya watu.
Habakkuk 2:9-11
Yahwe anatangaza ole kwanza dhidi ya nani?
Yahwe anatangaza ole dhidi ya yule ambaye anafanyia juhudi mapato maovu kwaajili ya nyumba yake.
Yahwe anasema nini kitapaza sauti sababu ya aibu na dhambi?
Yahwe anasema mawe yatalia kwa sababu ya aibu na dhambi.
Habakkuk 2:12-14
Dhidi ya nani Yahwe anatangaza ole ya pili?
Yahwe anatangaza ole dhidi ya yule ambayeanajenga mji kwa damu na maovu.
Yahwe anaahidi nini kitatokea kwaajili ya nchi badaye?
Yahwe anaahidi kwamba nchi itajazwa maarifa ya utukufu wa Yahwe.
Habakkuk 2:15-17
Dhidi ya nani Yahwe anatangaza ole ya tatu?
Yahwe anatangaza ole dhidi ya yule anayemfanya jirani yake anywe sumu awaangalie uchi wao.
Nini kitakuja kiwe malipo kwa yule amfanyaye jirani yake anywe sumu?
Kikombe cha mkono wa kuume wa Yahwe kitakuja katika kumlipa yule amfanyaye jirani yake anywe sumu.
Habakkuk 2:18-20
Kwenye nini fundi amechonga sanamu akaweka imani yake?
Yeye ameweka imani yake kwenye kazi ya mikono yake anapotengeneza miungu hii isiyoongea.
Nini lazima kifanyike mbele ya Yahwe, ambaye yumo katika hekalu lake takatifu?
wote lazima wawe kimya mbele za Yahwe katika hekalu lake takatifu.
Habakkuk 3
Habakkuk 3:1-3
Kusikia taarifa ya Yahwe, jibu la kihisia la Habakuki lilikuwa nini?
Kusikia taarifa ya Yahwe, Habakuki kaogopa.
Habakuki alimwambia Yahwe akumbuke nini?
Habakuki alimwambia Yahwe akumbuke rehema katika ghadhabu yake.
Habakkuk 3:4-5
Mungu alipokuja, nini kilitangulia mbele na kumfuata?
Mungu alipokuja, madhara yalitangulia mbele yake na mapigo yakafuata.
Habakkuk 3:6-12
Yahwe alifanya nini kwa mataifa katika ghadhabu yake?
Yahwe aliyatikisa mataifa.
Habakkuk 3:13
Kwanini Yahwe alitangulia katikahasira yake?
Yahwe alitangulia katika hasira yake kwaajili ya wokovu wa watu wake na mteule wake.
Yahwe alimpondaponda nani katika hasira yake?
Yahwe anapondaponda kichwa cha nyumba ya mwovu.
Habakkuk 3:14-15
Wapiganaji waovu wanapokuja kutapanya watu wa Yahwe wanafanya nini?
Wapiganaji wanawaangalia kwa wivu watu wa Yahwe.
Habakkuk 3:16
Kwaajili ya nini Habakuki anasubiri kwa utulivu?
Habakuki anasubiri kwa utulivu siku ya huzuni ije juu ya watu waliowashambulia watu wa Yahwe.
Habakkuk 3:17
Magumu gani watu wa Yahwe yanawatesa?
Miti ya mtini na mizeituni haizai, mashamba hayatoi chakula na hakuna wanyama wa kufuga.
Habakkuk 3:18-19
Licha ya ugumu, Habakuki atafanya nini?
Licha ya ugumu Habakuki atafurahia katika Yahwe.