Kiswahili: translationQuestions

Updated ? hours ago # views See on DCS Draft Material

Hebrews

Hebrews 1

Hebrews 1:1-3

Namna gani Mungu alisema katika nyakati zilizopita?

Mungu alizungumza katika nyakati zilizopita kupitia manabii mara nyingi na kwa njia nyingi.

Ni kwa jinsi gani Mungu amezungumza katika siku hizi za karibuni?

Mungu amezungumza katika siku hizi za karibu kwa njia ya mwana wake

Kwa kupitia nani ulimwengu iliumbwa?

Ulimwengu uliumbwa kupitia mwana wa Mungu

Ni kwa jinsi gani vitu vyote vime tunzwa?

Vitu vyote vimetunzwa kwa njia ya neno la mwana wa Mungu mwenye uwezo.

Ni kwa jinsi gani mwana huonesha utukufu na uhalisia wa Mungu?

Mwana ni mn'gao wa utukufu wa Mungu, na tabia yake ya Ki Mungu.

Hebrews 1:4-5

Mwana wa Mungu analinganishwaje na malaika?

Mwana wa Mungu ni bora kuliko malaika.

Hebrews 1:6-7

Mungu aliwaamuru malaika kufanya nini wakati Mwana alipoletwa ulimwenguni?

Mungu aliwaamuru malaika kumwabudu Mwana wakati Mwana alipoletwa katika ulimwengu.

Hebrews 1:8-9

Ni kwa muda gani Mwana atatawala kama mfalme?

Mwana atatawala kama mfalme milele na milele.

Je mwana hupenda nini na huchukia nini?

Mwana hupenda haki na mwana huchukia kutotii sheria

Hebrews 1:10-12

Nini kitatokea kwa nchi na mbingu wakati huo?

Nchi na mbingu zitachakaa kama vazi na kuangamia.

Nini kitatokea kwa nchi na mbingu wakati huo?

Nchi na mbingu zitachakaa kama vazi na kuangamia.

Hebrews 1:13-14

Ni wapi Mungu alimwambia Mwana kuketi, na mpaka hapo nini kilitokea?

Mungu alimwambia Mwana kukaa mkono wake wa kulia mpaka Mungu atakapowafanya maadui wa Mwana kuwa kiti cha miguu ya Mwana.

Ni kwa ajili ya nani malaika wanahudumu?

Malaika huwahudumia wale amabao wanakaribia kurithi wokovu.

Hebrews 2

Hebrews 2:1

Kwa nini lazima waumini waweke kipaumbele zaidi kwa yale ambayo wamesikia?

Waumini lazima waweke kipaumbele kwa yale waliyosikia ili kwamba wasije wakatengwa mbali nayo.

Hebrews 2:2-4

Ni kitu gani ambacho kila kosa na uasi hupokea?

Kila kosa na uasi hupokea adhabu tu.

Ni kwajinsi gani Mungu hushuhudia ujumbe wa wokovu uliotangazwa na Bwana?

Mungu hushuhudia kwa njia ya ishara , maajabu, matendo ya nguvu, na kwa karama ya Roho Mtakatifu.

Hebrews 2:5-6

Je, ni kina nani hawatatawala ulimwengu ujao?

Malaika hawatatawala ulimwenge ujao?

Hebrews 2:7-8

Je, ni kina nani watatawala ulimwengu ujao?

Mwanadamu atatawala ulimwengu ujao.

Je, ni kina nani watatawala ulimwengu ujao?

Mwanadamu atatawala ulimwengu ujao.

Hebrews 2:9-10

Kwa nini Yesu alivikwa taji ya utukufu na heshima?

Yesu alivikwa taji ya utukufu na heshima kwa sababu ya mateso yake na kifo chake.

Je, Yesu alionja kifo kwa ajili ya nani?

Yesu alionja kifo kwa ajili ya kila mtu.

Ni nani Mungu anapanga kufikishia utukufu?

Mungu hupanga kuwafikishia utukufu watoto wengi.

Hebrews 2:11-12

Akina nani ambao wote wanatoka kwa mwenye asili moja, Mungu?

Wote wawili, yule anayetakasa na wale wanaotakaswa wanatoka kwenye asili moja, Mungu?

Hebrews 2:13-15

Nani alifanywa dhaifu kupitia kifo cha Yesu?

Shetani alifanywa dhaifu kupitia kifo cha Yesu

Ni kutoka katika utumwa wa nani watu huwekwa huru kupitia kifo cha Yesu?

Kwa kupitia kifo cha Yesu watu huwekwa huru kutoka katika hofu ya kifo.

Hebrews 2:16-18

Kwa nini ilikuwa ni muhimu kwa Yesu kufanyika kama ndugu zake katika njia nyingi?

Ilikuwa ni laziama ili kwamba afanyike wa Huruma na kuhani mkuu mwaminifu juu ya mambo ya Mungu, na pia ili afanikishe msamaha wa dhambi za watu.

Kwa nini Yesu anaweza kuwasaidia wale ambao wanajaribiwa?

Yesu anaweza kuwasaidia wale wanao jaribiwa kwa sababu alijaribiwa pia.

Hebrews 3

Hebrews 3:1-4

Ni vyeo gani viwili ambavyo mwandishi wa kitabu cha Waebrania anampatia Yesu?

Mwandishi anampatia Yesu vyeo vya, Mtume na pili Kuhani Mkuu

Kwa nini Yesu anahesabiwa kuwa na heshima kubwa ya utukufu kuliko Musa?

Yesu amehesabiwa kuwa na heshima na utukufu mkubwa kuliko Musa kwa sababuwakati Musa anafanyika mwaminifu katika nyumba yote ya Mungu, Yesu ndiye aliye jenga nyumba.

Kwa nini Yesu anahesabiwa kuwa na heshima kubwa ya utukufu kuliko Musa?

Yesu amehesabiwa kuwa na heshima na utukufu mkubwa kuliko Musa kwa sababuwakati Musa anafanyika mwaminifu katika nyumba yote ya Mungu, Yesu ndiye aliye jenga nyumba.

Hebrews 3:5-6

Nini ilikuwa kazi ya Musa katika nyumba ya Mungu?

Musa alikuwa mtumishi katika nyumba ya Mungu.

Musa alitoa ushuhuda kuhusu nini?

Musa alitoa ushuhuda kuhusu mambo yaliyopaswa kunenwa kwa baadaye.

Nafasi ya Yesu katika nyumba ya Mungu ni ipi?

Yesu ni mwana mkuu katika nyumba ya Mungu

Nani ni nyumba ya Mungu?

Waamini ni nyumba ya Mungu ikiwa watashikilia sana tumaini kwa ujasiri.

Hebrews 3:7-8

Ni nini walichokifanya Waisraeli walipokuwa nyikani pale waliposikia sauti ya Mungu?

Waisraeli waliifanya mioyo yao kuwa migumu.

Ni nini walichokifanya Waisraeli walipokuwa nyikani pale waliposikia sauti ya Mungu?

Waisraeli waliifanya mioyo yao kuwa migumu.

Hebrews 3:9-11

Mungu aliapa nini kuhusu waisraeli walio asi katika mioyo yao?

Mungu aliapa kuwa hawata ingia katika pumziko lake.

Mungu aliapa nini kuhusu waisraeli walio asi katika mioyo yao?

Mungu aliapa kuwa hawata ingia katika pumziko lake.

Hebrews 3:12-13

Ni nini ambacho ndugu walionywa kuwa makini?

Ndugu walionywa kuwa makini kwamba wasitoke kwenda mbali na Mungu aishie kwa kutoamini.

Ndugu wanapaswa kufanya nini kuzuia ugumu unaotokana na udanganyifu wa dhambi?

Ndugu wanapaswa kutiana moyo kila siku.

Hebrews 3:14-15

Kama washirika wa Kristo, ni nini waumini wanapaswa kufanya?

Kama washirika wa Kristo, waumini lazima wasimame imara ujasiri wao ndani yake kutoka mwanzo hadi mwisho.

Hebrews 3:16-19

Ni kwa ajili ya nani Mungu alikasirika kwa muda wa miaka arobaini?

Mungu alikasirika kwa ajili ya wale walio fanya dhambi jangwani.

Nini kilitokea kwa wale ambao Mungu aliwakasirikia?

Maiti zao zililala katika jangwa.

Kwa nini waisraeli wasio tii hawakuweza kuingia katika pumziko la Mungu?

Hawakuweza kuingia katika pumziko la Mungu kwa sababu ya kutoamini kwao.

Hebrews 4

Hebrews 4:1-2

Ni habari gani njema waisraeli pamoja na waamini walisikia?

Waamini na Waisraeli wote walisikia habari njema kuhusu pumziko la Mungu.

Kwa ni i habari njema hazikuwanufaisha waisraeli?

Habari njema hazikuwanufaisha waisrael kwa sababu hawakuiunganisha na imani

Hebrews 4:3-5

Ni nani ambaye ataingi katika pumziko la Mungu?

Wale wanao sikia habari njema na kuiamini ndio wataingia pumziko la Mungu.

Ni lini Mungu alimaliza kazi za kuumba na baadae kupumzika?

Mungu alimaliza uhumbaji wa kazi yake toka mwanzo wa ulimwengu na baadae alipumuzika siku ya saba.

Ni lini Mungu alimaliza kazi za kuumba na baadae kupumzika?

Mungu alimaliza uhumbaji wa kazi yake toka mwanzo wa ulimwengu na baadae alipumuzika siku ya saba.

Mungu alisema nini kuhusu waisraeli na pumziko lake?

Mungu alisema kwamba Waisraeli hawataingia katika pumziko lake

Hebrews 4:6-7

Ni siku gani ambayo Mungu ameipanga kwa ajili ya watu kuingia katika pumziko lake?

Mungu amepanga " leo" kama siku ya watu kuingia katika pumziko lake.

Ni jambo gani mtu anapaswa kufanya ili kuingia katika pumziko lake?

Mtu lazima asikilize sauti ya Mungu na asifanye moyo wake kuwa mgumu.

Hebrews 4:8-11

Ni kitu gani ambacho kimetunzwa kwa ajili ya watu wa Mungu?

Pumziko la sabato bado limetunzwa kwa ajili ya watu wa Mungu.

Mtu anaye ingia katika pumziko la Mungu pia hupumzika katika jambo gani?

Mtu anaye ingia katika pumziko la Mungu pia hupumzika katika matendo yake.

Kwa nini waaminiwanapaswa kupenda kuingia katika pumziko la Mungu?

Waamini wanapaswa kupenda kuingia katika pumziko la Mungu ili kwamba wasije wakawa kama waisraeli walivyofanya.

Hebrews 4:12-13

Neno la Mungu lina ukali kuliko nini?

Neno la Mungu lina ukali kuliko upanga wowote wenye makali kuwili.

Neno la Mungu linaweza kugawanya nini?

Neno la Mungu linaweza kugawanya nafsi na roho, na viungo kutoka kwa mafuta.

Neno la Mungu lina uwezo wa kupambanua nini?

Neno la Mungu linauwezo wa kupambanua fikira za moyo na nia.

Nani amefichwa katika uwepo wa Mungu?

Hakuna kiumbe ambacho kimefichika mbele ya uwepo wa Mungu.

Hebrews 4:14-16

Ni nani anatumika kama kuhani mkuu kwa waumini?

Yesu Mwana wa Mungu utumika kama kuhani mkuu kwa waumini.

Kwa nini Yesu anaona huruma kwa udhaifu wa waamini?

Yesu anaona huruma kwa udhaifu wa waamini kwa sababu alijaribiwa pia katika njia zote.

Ni mara ngapi Yesu alifanya dhambi?

Yesu hakuwa na dhambi.

Katika nyakati za kuhitaji waamini wanapaswa kufanya nini ili wapokee rehema na kuapata neema?

Katika nyakati za kuhitaji, waamini wanapaswa kutokea kwa ujasiri kwenye kiti cha neema.

Hebrews 5

Hebrews 5:1-3

Nini alichokuwa akifanya kuhani mkuu badala ya watu?

Kwa ajili ya watu , kila kuhani mkuu hutoa zawadi na dhabihu kwa ajili ya dhambi.

Zaidi ya watu je ni kwa ajili ya nani pia kuhani mkuu alitoa sadaka?

Kuhani mkuu pia hutoa sadaka kwa ajili ya dhambi

Hebrews 5:4-5

Ni kwa jinsi gani mtu hupokea heshima ya kuwa kuhani mkuu wa Mungu?

Lazima mtu aitwe na Mungu kuwa kuhani mkuu wa Mungu.

Nani alimtangaza Yesu kuwa kuhani mkuu

Mungu alimtangaza Kristo kuwa kuhani mkuu.

Hebrews 5:6

Ni kwa kipindi gani Kristo ni kuhani mkuu wa Mungu?

Kristo ni kuhani mkuu wa Mungu milele.

Ni kwa zamu ipi Kristo ni kuhani mkuu?

Kristo ni kuhani mkuu kwa zamu ya Melkizedeki.

Hebrews 5:7-8

Kwa nini Kristo alisikiwa na Mungu wakati alipoomba?

Kristo alisikiwa na Mungu kwa sababu alimuheshimu Mungu.

Ni kwa jinsi gani Kristo alijifunza utii?

Kristo alijifunza utii kutokana na mabo aliyo teswa nayo.

Hebrews 5:9-11

Ni kwa nani Kristo alifanyika sababu ya wokovu wa milele?

Ni kwa kila mtu atakayemtii, Kristo amefanyika sababu ya wokovu wao wa milele.

Hali ya kiroho ya wasomaji wa kwanza wa waraka huu ilikuwa je?

Wasomaji wa kwanza walikuwa wavivu wa kusikia

Hebrews 5:12-14

Ni kwa jinsi gani mwandishi wa waraka anasema kwamba waamini hukua kutoka uchanga wa kiroho na kufikia ukubwa?

Waamini wanakuwa kiroho kwa kutofautisha kati ya mema na mabaya, kupambanua wema na uovu.

Hebrews 6

Hebrews 6:1-3

Ni nini mwandishi wa Waebrania alitaka waamini waweze kushika?

Mwandishi wa Waebrania anataka waamini wakue katika imani.

Ni mafundisho gani mwandishi ametaja kama msingi wa ujumbe wa Kristo?

Mafundisho ya msingi ni toba kutoka kwenye kazi zilizo kufa, imani katika Mungu, mabatizo, kuweka mikono juu, ufufuo wa wafu, na hukumu ya milele.

Ni mafundisho gani mwandishi ametaja kama msingi wa ujumbe wa Kristo?

Mafundisho ya msingi ni toba kutoka kwenye kazi zilizo kufa, imani katika Mungu, mabatizo, kuweka mikono juu, ufufuo wa wafu, na hukumu ya milele.

Hebrews 6:4-6

Ni kitu gani hakiwezekani kwa wale ambao walikua washiriki wa Roho Mtakatifu wakaanguka?

Haiwezekani kwa wale ambao walikuwa washiriki katika Roho Mtakatifu, lakini wakaanguka, kuweza kurejeshwa tena katika toba

Ni kitu gani ambacho hawa wlio tiwa nuru wameonja?

Hawa waliotiwa nuru wameonja kipawa cha mbinguni, neno la Mungu, na uwezo wa ulimwengu ujao.

Ni kitu gani ambacho hawa wlio tiwa nuru wameonja?

Hawa waliotiwa nuru wameonja kipawa cha mbinguni, neno la Mungu, na uwezo wa ulimwengu ujao.

Ni kitu gani hakiwezekani kwa wale ambao walikua washiriki wa Roho Mtakatifu wakaanguka?

Haiwezekani kwa wale ambao walikuwa washiriki katika Roho Mtakatifu, lakini wakaanguka, kuweza kurejeshwa tena katika toba

Kwa nini watu hawa hawawezi kurejeshwa katika hali ya toba?

Hawezi kurejeshwa katika toba kwa sababu wamemsulibisha wao wenyewe mwana wa Mungu.

Hebrews 6:7-8

Katika ulinganisho wa mwandishi, nini kitatokea kwenye ardhi yenye kupokea mvua lakini huzaa miiba na magugu?

Ardhi yenye kupokea mvua lakini inazaa miiba na magugu, mwisho wake ni kuchomwa moto.

Katika ulinganisho wa mwandishi, nini kitatokea kwenye ardhi yenye kupokea mvua lakini huzaa miiba na magugu?

Ardhi yenye kupokea mvua lakini inazaa miiba na magugu, mwisho wake ni kuchomwa moto.

Hebrews 6:9-10

Nini matarajio ya mwandishi kuhusu waamini aliowaandikia?

Mwandishi alitarajia mambo bora juu ya waamini hao, juu ya mambo yahusuyo wokovu.

Mungu hatasahau nini kuhusu hwa waamini?

Mungu hatasahau kazi yao, upendo na huduma kwa watakatifu.

Hebrews 6:11-12

Waamini wana paswa kuiga nini kwa wale wanaorithi ahadi za Miungu?

Waamini lazima waige imani na uvumilivu wa wale ambao wanarithi ahadi za Mungu.

Hebrews 6:13-15

Ibrahimu alifanya nini ili kuweza kupokea ahadi alizohaidiwa na Mungu?

Ibrahimu alipaswa kusubiri kwa uvumilivu ili kuweza kupokea kile Mungu alichokua amemuahidi.

Ibrahimu alifanya nini ili kuweza kupokea ahadi alizohaidiwa na Mungu?

Ibrahimu alipaswa kusubiri kwa uvumilivu ili kuweza kupokea kile Mungu alichokua amemuahidi.

Hebrews 6:16-18

Kwa nini Mungu alihakikisha ahadi zake kwa kiapo?

Mungu alihakikisha ahadi zake kwa kiapo ili kuonesha wazi wazi sifa yake ya kutobadilika katika kusudi lake.

Ni jambo gani haiwezekani Mungu kulifanya?

Haiwezekani Mungu kudanganya.

Hebrews 6:19-20

Ujasiri wa waamini katika Mungu hufanya nini kwa roho yake?

Ujasiri wa waamini kwa Mungu ni Usalama na nanga ya kutegemewa ya roho yake.

Yesu aliingia wapi kama mtangulizi wa waamini?

Yesu aliingia katika sehemu za ndani nyuma ya pazia kama mtangulizi wa waamini.

Hebrews 7

Hebrews 7:1-3

Ni vyeo gani viwili ambavyo Melikizedeki alikuwa navyo?

Melikizedeki alikuwa mfalme wa Salemu na kuhani wa Mungu aliye juu.

Ibrahimu alimpatia nini Melkizedeki?

Ibrahimu alimpatia melkizedi moja kumi ya vitu vyote alivyokuwa amejipatia.

Jina ili Melkizedeki lina maana ganai?

Jina Melkizedeki maana yake ni "Mfalme wa haki" na "Mfalme wa amani.

Nani walikuwa wazazi wa Melkizedeki, na alikufa lini?

Melkizedeki alikuwa hana wazazi na alikuwa hana mwisho wa maisha.

Hebrews 7:4-6

Je ni kwa watu gani makuhani walitokea ambao ni makuhani kwa mijibu wa sheria, na nani alipokea zaka kutoka kwa watu?

Makuhani wa sheria wanatokea kwa Lawi na Ibrahimu.

Hebrews 7:7-10

Ni nani aliyekuwa mtu mkubwa, Ibrahimu au Melikizedeki?

Melikizedeki alikuwa mtu mkubwa kwa sababu alimbariki Ibrahimu.

Ni kwa njia ipi Lawi pia alitoa zaka kwa Melkizedeki?

Lawi pia alitoa zaka kwa Melkizedeki kwa sababu Lawi alikuwa katika uzao wa Ibrahimu wakati Ibrahimu anatoa zaka kwa Melkizedeki.

Ni kwa njia ipi Lawi pia alitoa zaka kwa Melkizedeki?

Lawi pia alitoa zaka kwa Melkizedeki kwa sababu Lawi alikuwa katika uzao wa Ibrahimu wakati Ibrahimu anatoa zaka kwa Melkizedeki.

Hebrews 7:11-12

Kwa ni i ilikuwa ni hitaji kwa kuhani mwingine kuinuka baada ya mpangilio wa Melikizedeki?

Kulikuwa na hitaji la kuhani mwingine kuinuka baada ya mpangilio wa Melikizedeki kwa sababu ukamilifu haukuwezekana kupitia ukuhani wa Kilawi.

Kitu gani ambazcho lazima kibadilike wakati ukuhani unabadilika?

Sheria lazima ibadilike wakati ukuhani unabadilika

Hebrews 7:13-14

Je kutoka kabila ipi Yesu alishuka, na kufanya kabila hii ihudumu katika madhabahu kama makuhani?

Yesu alishuka kutoka kabila ya Yuda, ambaya haikuwahi kuhudumu madhabahuni kama makuhani.

Hebrews 7:15-17

Ni kwa kigezo kipi Yesu alifanyika kuhani baada ya mpango wa Melkizedeki?

Yesu alifanyika kuhani baada ya mpangilio wa Melkizedeki kwa msingi wa uwezo wa maisha yasiyo haribika.

Hebrews 7:18-19

Ni nini kilichowekwa kando kwa sababu kilikuwa dhaifu na hakifai?

Amri za zamani, sheria, ziliwekwa kando kwa sababu ni dhaifu na hazifai.

Ni nini kilichowekwa kando kwa sababu kilikuwa dhaifu na hakifai?

Amri za zamani, sheria, ziliwekwa kando kwa sababu ni dhaifu na hazifai.

Hebrews 7:20-21

Je ni kiapo gani ambacho Mungu aliapa kuhusiana na Yesu?

Mungu aliapa kuwa Yesu atakuwa kuhani milele

Hebrews 7:22-24

Kwa jinsi gani Yesu ni dhamana?

Yesu ni dhamana ya agano bora.

Hebrews 7:25-26

Kwa nini Yesu anaweza kukamilisha kuwaokoa wale wanaosogea karibu na Mungu kupitia kwake?

Yesu anaweza kukamilisha kuwaokoa wale wanaosogea karibu na Mungu kupitia kwake kwa sababu siku zote anaishi kuomba kwa ajili yao.

Ni sifa gani nne alizo nazo Yesu kuwa kuhani sahihi kwa waamini?

Yesu hana dhambi, hana lawama, safi, na amejitenganisha na wenye dhambi.

Ni matoleo gani Yesu alihitaji kufanya kwa ajili ya dhambi zake

Yesu hakuhitaji kufanya matoleo yoyote kwa ajili ya dhambi zake kwa sababu hana dhambi.

Hebrews 7:27-28

Ni sadaka gani ambayo Yesu aliifanya kwa ajili dhambi za watu?

Yesu alijitoa yeye mwenyewe mara moja kwa ajili ya dhambi za watu.

Yesu anatofautianaje na makuhani waliochaguliwa kwa mujibu wa sheria?

Makuhani walio chaguliwa kwa mujibu wa sheria walikuwa dhaifu, lakini Yesu amefanyika mkamilifu milele

Hebrews 8

Hebrews 8:1-2

Kuhani mkuu wa waumini amekaa wapi?

Kunani mkuu wa waumini amekaa mkono wa kulia wa kiti cha enzi mbinguni.

Hema ya kweli iko wapi?

Hema ya kweli iko mbinguni.

Hebrews 8:3-5

Kwa kila kuhani alipaswa kuwa na nini cha muhimu?

Kila kuhani ni lazima awe na chochote cha kutoa.

Walikuwa wapi makuhani ambao walitoa zawdi kulingana na sheria?

Makuhani ambao walitoa zawadi kwa mujibu wa sheria wako duniani.

Makuhani wa duniani walitumikia nini?

Makuhani wa duniani walitumikia nakala na kivuli mambo ya mbinguni.

Kwa mfumo upi hema ya dunia ilijengwa?

Hema ya dunia ilijengwa kw amujibu wa mfumo ambao Mungu alimuonesha Musa juu ya mlima.

Hebrews 8:6-7

Kwa nini Kristo alikuwa na huduma ya ukuhani iliyo bora?

Kristo alikuwa na huduma ya ukuhani bora kwa sababu ni mpatanishi wa agano bora, limeanzishwa na ahadi bora.

Hebrews 8:8-9

Mungu aliahidi nini lilipopatikana kosa kwa watu waliokuwa chini ya agano la kwanza?

Mungu aliahidi kufanya agano jjipya kwa nyumba ya Israeli na kwa nyumba ya Yuda.

Hebrews 8:10

Mungu alisema atafanya nini ndani ya agano jipya?

Mungu alisema ataweka sheria katika akili za watu, na ataziandika mioyoni mwao.

Hebrews 8:11-12

Ndani ya agano jipya, ni nani atakayemjua Bwana?

Ndani ya agano jipya, wote watamjua Bwana, kutoka mdogo hadi mkubwa zaidi.

Mungu alisema atawafanya na dhambi za watu katika agano jipya?

Mungu alisema hatakumbuka dhambi za watu tena.

Hebrews 8:13

Kwa kulitangaza agano jipya, Mungu alilifanya nini agano la kwanza?

Kwa kulitangaza agano jipya, Mungu alilifanya agano la kwanza kuukuu na tayari kupotea.

Hebrews 9

Hebrews 9:1-2

Ilikuwa mahali gani pa ibada katika agano la kwanza?

Sehemu ya ibada katika agano la kwanza ilikuwa katika hema hapa duniani.

Ilikuwa mahali gani pa ibada katika agano la kwanza?

Sehemu ya ibada katika agano la kwanza ilikuwa katika hema hapa duniani.

Mahali patakatifu paliwekwa wapi katika hema ya duniani?

Katika patakatifu kwenye hema kulikuwa na kinara cha taa, meza, na mkate wa wonyesho.

Hebrews 9:3-5

Mahali patakatifu paliwekwa nini katika hema ya duniani?

Paliwekwa madhabahu kwa ajili ya ubani au uvumba sanduku la agano

Hebrews 9:6-7

Ni mara ngapi kuhani mkuu aliingia patakatifu pa patakatifu na alifanya nini kabla ya kwenda huko?

Kuhani mkuu aliingia mara moja kwa mwaka , baada ya kufanya sadaka ya dhambi zake mwenyewe na kwa ajili ya watu.

Hebrews 9:8-10

Nini kilitumika kama mfano kwa wasomaji wa waraka huu

Hema ya duniani na sadaka zawadi vilitumika kama mfano wakati huo

Matoleo katika hema ya duniani hayakuweza kufanya nini?

Matoleo hayakuweza kuwatakasa fikra za waabuduo

Lini amri ya hema ya kidunia ilitolewa?

Amri ya hema ya kidunia ilitolewa adi taratibu mpya iwekwe katika sehemu yake.

Hebrews 9:11-12

Nini tofauti kuhusu hema takatifu ambalo Kristo alihudumu?

Hema takatifu ambalo Kristo alihudumu ni kamilifu zaidi, halikutengenezwa kwa mikono ya wanadamu, na halimilikiwi katika ulimwengu huu ulioumbwa.

kristo alitoa sadaka gani, ambayo aliingia kwayo katika patakatifu?

Kristo alitoa sadaka ya mwili wake ambayo kwayo aliingia patakatifu.

Sadaka ya Kristo ilikamilisha nini?

Sadaka ya Kristo ilikamilisha uzima wa milele kwa kila mmoja.

Hebrews 9:13-15

Damu ya Kristo ya fanya nini kwa kila mwamini?

Damu ya Kristo ya takasa dhamira ya kila mwamini kutoka katika matendo ya liyo kufa ili kumtumikia Mungu aliye hai.

Kristo ni mpatanishi wa nini?

kristo ni mpatanishi wa agano jipya.

Hebrews 9:16-17

Nni kina itajika kwa urithi kuwezeshwa?

KIfo lazima kitokee kwa urithi kuwezeshwa.

Hebrews 9:18-20

Kifo gani kilikuwa kinatakiwa katika agano la kwanza?

Kuuawa kwa ndama Mbuzi ni kifo kilichokuwa kinatakiwa katika agano la kwanza.

Hebrews 9:21-22

Nini kinweza tokea pasipo kumwaga damu?

Pasipo kumwaga damu hakuna msamaha wa dhambi.

Hebrews 9:23-24

Kristo anatokea wapi sasa kwa niaba yetu?

Kristo anatokea mbinguni yenyewe, katika uwepo wa Mungu, kwa niaba yetu.

Hebrews 9:25-26

Kristo anahitaji kujitoa sadaka mara ngapi ili kuondoa dhambi?

Kristo anaitaji kujitoa sadaka mara moja.

Hebrews 9:27-28

Kwa kila mtu, nini kinatokea baada ya vifo vyao?

baada ya kila mtu kufa, wanakutana na hukumu.

Kwa kusudi lipi Kristo atakuja kwa mara ya pili?

Kristo atakuja mara ya pili kwa ajili ya wokovu wa wao wanao msubiri kwa subira.

Hebrews 10

Hebrews 10:1-4

Kwa namna gani sheria inalinganishwa na ukweli katika Kristo?

Sheria ni kivuli pekee cha ukweli katika Kristo.

Sadaka iliyo tolewa tena katika sheria ya wakumbusha nini waabudu?

Sadaka iliyo tolewa tena katika sheria inawakumbusha waabudu dhambi zao za kila mwaka.

Damu ya ng'ombe na mbuzi yaweza fanya nini?

Damu ya ng'ombe na mbuzi haiwezi kuondoa dhambi.

Hebrews 10:5-7

Mungu alitayarisha nini kwa Kristo wakati Kristo alipokuja duniani?

Mungu aliandaa mwili kwa ajili ya Kristo.

Hebrews 10:8-10

Ni taratibu gani Mungu aliziweka pembeni wakati Kristo alipokuja duniani?

Mungu aliziweka pembeni zile taratibu za dhabihu zilizokuwa zinatolewa kwa mujibu wa sheria.

Hebrews 10:11-16

Kristo anasubiri nini anapoketi mkono wakuume wa Mungu?

Kristo anasubiri mpaka maadui zake watakapo shushwa na kufanywa stuli ya miguu yake

Kristo anasubiri nini anapoketi mkono wakuume wa Mungu?

Kristo anasubiri mpaka maadui zake watakapo shushwa na kufanywa stuli ya miguu yake

Kristo amewafanyia nini wao wanao takaswa kwa sadaka yake?

Kristo amewakamilisha wao wanao takaswa na damu yake.

Hebrews 10:17-18

Nini kisicho itajika palipo na masaha wa dhambi?

Sadaka za ziada haziitajiki palipo na msamaha wa dhambi.

Hebrews 10:19-22

Katika eneo gani waamini wanaweza sasa kuingia kwa damu ya Yesu?

Waamini wanaweza sasa kuingia mahali patakatifu zaidi kwa damu ya Yesu.

Ni nini imenyunyiziwa na ni nini imeosha kwa mwamini?

Moyo wa mwamini umenyunyiziwa kutoka katika dhamiri mbaya, na mwili wake umeoshwa na maji safi

Hebrews 10:23-25

Katika yapi lazima waamini washikilie kwa uimara?

Waamini lazima washikilie kwa uimara katika ungamo la tumaini lao la uhakika.

Ni nini lazima waamini wafanye waonapo siku inakaribia?

Waamini lazima watiane moyo zaidi na zaidi waonapo siku inakaribia.

Hebrews 10:26-27

Nini matarajio yao ambao kwa kusudi wameendelea kufanya dhambi baada ya kuipokea elimu ya ukweli?

Tarajio la wale ambao kwa kusudi wanaendelea kutenda dhambi baada ya kuipokea elimu ya ukweli ni hukumu na moto ambao huteketeza maadui wa Mungu.

Hebrews 10:28-29

Anajitakia nini mtu ambaye anaitendea damu ya Kristo ambayo alitengwa kwayo kama kitu kisicho kitakatifu?

Mtu anayeitendea damu ya Kristo ambayo kwayo alitengwa kama kitu kisicho kitakatifu ajitakia hukumu bila ya rehema zaidi ya hukumu iliyotolewa chini ya sheria ya Musa.

Hebrews 10:30-31

Ni kwa nani kisasi kinamilikiwa?

Kisasi kinamilikiwa na Bwana

Hebrews 10:32-34

Waamini walio pokea hii barau waliitikaje kitendo kukamatwa kwa malizao?

Waamini walikubali kwa furaha kukamatwa kwa malizao, wakijua kwamba wanamiliki ya milele.

Hebrews 10:35-37

Muumini anahitaji nini ili aweze kupokea kile Mungu ameahidi?

Muumini anahitaji uhakika na uvumilivu ili aweze kupokea kile Mungu ameahidi.

Hebrews 10:38-39

Jinsi gani mwenye haki waishi?

Mwenye haki ataishi kwa imani.

Mungu anawaza nini kwa wao ambao hurudi nyuma?

Mungu hapendezwi na hao ambao hurudi nyuma.

Ni nini matarajio ya mwandishi kwa walio pokea hii barua?

Matarijio ya mwanidshi ni kwamba hao walio pokea hii barau watakuwa na imani ya kuhifadhi roho zao.

Hebrews 11

Hebrews 11:1-3

Ni mtazamo gani ambao mtu wa imani huwa nao juu ya ahadi za Mungu ambazo hazijatimilika?

Mtu wa imani hutegemea kwa hakika na ana uhakika juu ya ahadi za Mungu ambazo bado hazijatimilika.

Vitu vinavyo onekana vya ulimwengu viliumbwa na nini?

Vitu vinavyo onekana vya ulimwengu havikuumbwa na vitu vinavyo onekana.

Hebrews 11:4

Kwa nini Mungu alimsifu Habili kuwa mwenye haki?

Mungu alimsifu Habili kwa sababu kwa njia ya imani Habili alitoa sadaka iliyokubalika zaidi ya ile ya Kaini.

Hebrews 11:5-6

Mtu anaye kuja kwa Mungu anatakiwa kuamini nini kuhusu Mungu?

Mtu anaye kuja kwa Mungu ana paswa kuamini Mungu yupo na kuwa anatoa thawabu kwa wanao mtafuta.

Hebrews 11:7-10

Ni kwa namnagani Nuhu alionesha imani yake?

Nuhu alionesha imani yake kwa kujenga safina ya kuokolea familia yake kama onyo la Mungu lilivyokuwa.

Hebrews 11:11-12

Ni ahadi zipi ambazo Ibrahim na Sara walipokea kwa njia ya imani?

Ibrahim na Sara walipokea kwa imani uwezo wa kubeba mimba ingawa walikuwa wazee sana.

Hebrews 11:13-14

Je mababu wa imani waliona nini tokea mbali?

Mababu wa imani waliona na kuzikaribisha ahadi za Mungu kutokea mbali.

Je mababu wa imani walijionaje wenyewe katika dunia?

Mababu wa imani walijiona kuwa wageni na wapitaji katika dunia.

Hebrews 11:15-16

Mungu ameandaa nini kwa wao wa imani?

Mungu ameandaa mji wa kimbingu kwa wao wa imani.

Hebrews 11:17-19

Je Ibrahimu aliamini nini ambacho Mungu anaweza kufanya hata alipo mtoa mwanawe wa pekee Isaka?

Ibrahimu aliamini kuwa Mungu angeweza kumfufua Isaka.

Hebrews 11:20-22

Yusufu alitabiri nini kwa imani mwisho wake ulipo fika?

Yusufu alitabiri kuondoka kwa wana wa Israeli kutoka Misri mwisho wake ulipo fika.

Hebrews 11:23-26

Musa alichagua kufanya nini kwa imani alipo kuwa mtu mzima?

Musa alichagua kushiriki mateso na watu wa Mungu, akiona aibu ya kumfuata Kristo kuwa utajiri mkuu.

Hebrews 11:27-28

Ni nini Musa alishika nini kwa imani ili kuwaokoa wazaliwa wa kwanza?

Musa alishika pasaka na kwa imani akanyunyiza damu ili kuwaokoa wazaliwa wa kwanza.

Hebrews 11:29-31

Rahabu alifanya nini kwa imani ili kujiepusha na kuangamia?

Rahabu kwa imani aliwapokea wapelelezi kwa usalama jambo ambalo lilimuondolea kuangamia.

Hebrews 11:32-34

Baadhi ya mababu wa imani walikamilisha nini katika vita?

Baadhi ya mababu wa imani walizishinda falme, walikwepa ncha ya upanga, walikuwa mashujaa vitani, na walisabisha majeshi wageni kukimbia.

Hebrews 11:35-38

Je mababu wa imani walipitia mateso gani?

Baadhi ya mababu wa imani walipitia mateso ya maumivu, dhihaka, mapigo , minyororo, vifungo, kupondwa mawe, kukatwa na misumeno vipande viwili, vifo, kupungukiwa.

Hebrews 11:39-40

Licha ya imani ya hawa mababu wa imani, je ni mambo gani hawakuyapokea katika dunia?

Licha ya imani ya hawa mababu wa imani, katika maisha yao ya duniani hawakupokea kile ambacho Mungu aliwaahidia.

pamoja na kina nani mababu wa imani watapokea ahadi ya Mungu na kukamilishwa?

Mababu wa imani watapokea ahadi za Mungu na kukamilishwa pamoja na waamini wa agano jipya katika Kristo.

Hebrews 12

Hebrews 12:1-6

Kwa nini mwamini anapaswa kutupa mbali dhambi inayo mzingira?

Kwa sababu ya kuzungukwa na kundi kubwa la mashahidi, mwamini anapaswa kutupa mbali dhambi imzingayo.

Kwa nini Yesu alivumilia msalaba na kudharau aibu ya msalaba?

Yesu alivumilia msalaba na kudharau aibu yake kwa sababu ya furaha iliyokuwa imewekwa mbele yake

Ni kwa namna gani mwamini anaweza kuzuia kuchoka au kukata tamaa?

Kwa kutazama Yesu ambaye alivumilia hotuba za chuki kutoka kwa wenye dhambi, mwamini anaweza kuzuia kuchoka au kukata tamaa.

Hebrews 12:7-8

Mtu asiye na marudi ya Bwana ni mtu wa namna gani?

Mtu asiye na marudi ya Bwana ni mtoto haramu na si mtoto wa Mungu.

Hebrews 12:9-13

Nidhamu huzaa nini?

Nidhamu huzaa tunda la amani ya haki.

Hebrews 12:14-17

Je wamini Wanapaswa kufanya nini pamoja na watu wote?

Waamini wanapaswa kutafuta amani na watu wote.

Ni kitu gani kisicho stahili kukua na kusababisha matatizo na kunajisi wengi?

Shina la uchungu halipaswi kukua na kusababisha matatizo na kunajisi wengi

Nini kilitokea kwa Hesau alipotamani kurithi baraka kwa machozi baada ya kuuza haki yake ya kuzaliwa?

Hesau alikataliwa alipotamani kurithi barakakwa machozi baada ya kuuza haki yake ya kuzaliwa.

Hebrews 12:18-21

Kwa ajili gani waisraeli waliomba mlimani ambapo Mungu alizungumza?

Waisraeli waliomba kwamba neno lingine lisizungumzwe kwao.

Hebrews 12:22-24

Je waamini wa Kristo huenda wapi badala ya kwenda mlimani mahali ambapo waisraeli walienda kusikia sauti ya Mungu?

Waamini katika Kristo waje mlima Sayuni na katika mji wa Mungu aliye hai.

Ni katika kusanyiko gani waamini wa Kristo huja?

Waamini katika Kristo huja katika kusanyiko la wazaliwawa kwanza wote waliosajiliwa mbinguni.

Ni kwa nani waamini katika Kristo huja?

Waamini katika Kristo huja kwa Mungu muhukumu wa wote, kwa roho za haki na kwa Yesu.

Ni kwa nani waamini katika Kristo huja?

Waamini katika Kristo huja kwa Mungu muhukumu wa wote, kwa roho za haki na kwa Yesu.

Hebrews 12:25-26

Je kitatokea nini kwa wale ambao wanageuka kutoka kwa yule awaonyae toka mbinguni?

Wale wanao geuka hawatamuepuka Mungu.

Mungu ameahidi kutikisa nini?

Mungu ameahidi kutikisa dunia pamoja na mbingu.

Hebrews 12:27-29

Waamini watapokea nini badala ya vitu ambavyo vitatikiswa?

Waamini watapokea ufalme ambao hautatikiswa.

Ni kwa namna gani waamini watamwabudu Mungu?

Waamini wanapaswa kumwabudu Mugu kwa kunyenyekea na katika kicho.

Kwa nini waamini wanapaswa kumwabudu Mungu kwa jinsi hii?

Waamini wanapaswa kumwabidu Mungu kwa jinsi hii kwa sababu ni moto ulao.

Hebrews 13

Hebrews 13:1-2

Je wengine wamefanya nini kwa kuwakaribisha wageni?

Wengine wamewakaribisha malaika bila kufahamu

Hebrews 13:3-4

Ni kwa namna gani waamini wanaweza kuwakumbuka walioko gerezani?

Waumini wanapaswa kuwakumba kana kwamba walikuwa nao gerezani pia, na kama miili yenu ilitendewa kama wao pia.

Nini kinapaswa kupatiwa utii na wote?

Ndoa lazima ieshimiwe na watu wote.

Mungu hufanya nini na waasherati na wazinzi

Mungu huwahukumu waasherati na wazinzi.

Hebrews 13:5-6

Ni kwa namna gani mwamini anaweza kushinda tamaa ya kupenda pesa?

Mwamini anaweza kuwa huru kushinda tamaa ya kupenda fedha kwa sabaubu Mungu aliisha sema sitamuacha wala kumtelekeza mtu.

Hebrews 13:7-8

Ni imani ya nani waamini wanapaswa kuiga?

Waumini wanapaswa kuiga imani ya wale walio waongoza na walioongea neno la Mungu kwao.

Hebrews 13:9-11

Ni kuhusu aina gani ya mafundisho ya kigeni ambayo mwandishi anawaonya waamini?

Mwandishi anawaonya waumini kuhusu mafundisho ya kigeni yanayo husisha sheria ihusuyo chakula.

Miili ya wanyama iliyotumika kutoa sadaka katika mahali patakatifu ilichomewa wapi?

Miili ya wanyama ilichomewanje ya kambi.

Hebrews 13:12-14

Yesu aliteseka wapi?

Yesu aliteseka nje ya mlango wa mji.

Waamini wanapaswa kwenda wapi na kwa nini?

Waamini wanapaswa kwenda kwa Yesu nje ya kambi wakibeba fedheha yake.

Je ni mji gani wa kudumu ambao waamini wanao hapa duniani?

Waamini hawana mji wa kudumu hapa duniani.

Ni mji gani waamini hutafuta badala yake?

Badala yake waamini hutafuta mji ujao.

Hebrews 13:15-19

Ni sadaka ya aina gani waamini wanatakiwa kuitoa mara kwa mara kwa Mungu?

Waamini wanapaswa mara kwa mara kumutolea Mungu sadaka ya kumutukuza.

Je ni mtazamo gani waamini wanapaswa kuwa nao juu ya viongozi wao?

Waamini wanapaswa kuwatii na kunyenyekea kwa viongozi wao.

Hebrews 13:20-21

Nini ambacho Mungu hufanya katika maisha ya mwamini?

Mungu hufanya mema yanayofaa machoni pa Mungu katika maisha ya mwamini.

Hebrews 13:22-25

Mwandishi atakuja na nani atakapo watembelea waamini?

Mwandishi atakuja na Timotheo wakati atakapo watembelea waamini.