2 Kings
2 Kings 1
2 Kings 1:1-2
Je! Ahazia aliumiaje?
Ahazi alianguka chini kwenye kiunzi cha fito katika chumba chake cha juu katika Samaria, na aliumia.
2 Kings 1:3-6
Kwa nini Ahazi anaenda kufa hakika?
Ahazi alikuwa akienda kushauriana na Baal Zebubu, mungu wa Ekron; kwa hiyo, angekufa hakika.
2 Kings 1:7-8
Je! Eliya alivaa nini?
Eliya alivaa vazi lililotengenezwa kwa nywele, na kulikuwa na mkanda wa ngozi uliofungwa kuzunguka kiuno chake.
2 Kings 1:9-12
Je! Nini kilimla nahodha na watu wake hamsini?
Moto ulishuka kutoka mbinguni na kumla nahodha na watu wake hamsini.
2 Kings 1:13-16
Je! yule nahodha wa tatu alimshawishije Eliya?
Yule nahodha wa tatu alipanda, akaanguka kwenye miguu ya Eliya, na kumuomba.
2 Kings 1:17-18
Kwa nini Yoramu alianza jutawala katika eneo la Ahazia?
Yoramu alianza kutawala mahali pake kwa sababu Ahazi hakuwa na mwana.
2 Kings 2
2 Kings 2:1-2
Lini Eliya aliondoka pamoja na Elisha kutoka Giligali?
Wakati Yahwe alipokuwa akienda kumchukua Eliya kw akimbunga kwenda mbinguni, Eliya alibaki na Elisha kutoka Giligali.
2 Kings 2:3-6
Je! Eliya alijibu vipi wakati wana wa manabii walipomwambia kwamba Yahwe angemchukua bwana wake kutoka kwake?
Elisha alijibu, "Ndio, nalijua hilo, lakini usiongee kuhusu hilo."
2 Kings 2:7-8
Kwa nini mto uligawanyika pande zote?
Kwa sababu Eliya alichukua vazi lake, kulizungusha, akalipigia maji, mto ukagawanyika pande zote.
2 Kings 2:9-10
Kwa ajili gani Elisha aliuliza?
Elisha aliuliza kwa ajili ya sehemu mbili ya roho ya Eliya kuja juu yake.
2 Kings 2:11-12
Je! Elia ailpandaje mbinguni?
Eliya walipanda juu kwa kimbunga kwenda mbinguni.
2 Kings 2:13-14
Nini kilitokea wakati Elisha alipoyapiga maji kwa vazi la Eliya?
Wakti Eliya alipoyapiga maji, yaligawanyika sehemu mbili na Elisha akapita.
2 Kings 2:15-16
Je! wana wa manabii waliwataka wale watu hamsini wafanye nini?
Waliwataka watu hamsini hodari kwenda na kumwangalia bwana wa Elisha, ikitokea Roho wa Yahwe alimchukua juu na kumtupa kwenye baadhi ya milima au au kwenye bonde.
2 Kings 2:17-18
Je! Ni kwa mda gani wale watu hamsini walimtafuta Eliya?
Wale watu hamsini walmtafuta kwa siku tatu.
2 Kings 2:19-20
Je! Yeriko kulikuwa na tatizo gani?
Maji yalikuwa mabaya na nchi inazaa matunda.
2 Kings 2:21-22
Je! maji yaliponyaje?
Elisha alitoka nje kwenye chimchem ya maji na kurusha chumvi katika hiyo.
2 Kings 2:23-25
Wakati baadhi ya vijana walipomtania Elisha, ni laana gani iliwatokea?
Wakati baadhi ya vijana walipomtania Elisha, dubu wawili majike walitoka kwenye miti na kujeruhi vijana arobaini na mbili.
2 Kings 3
2 Kings 3:1-3
Je! utofauti wa uovu wa Yoramu ulikuwaje tofauti na uovu wa baba yake na mama yake?
Uovu wa Yoramu haukuwa kama wa baba yake na mama yake, kwa kuwa aliliondoa nguzo ya jiwe takatifu la Baali ambalo baba yake alilitengeneza.
2 Kings 3:4-8
Kwa nini Mfalme Yoramu aliondoka Samaria?
Mfalme Yoramu aliondoka Samaria kuwashawishi Israeli yote kwa ajili ya vita.
2 Kings 3:9-10
Ni majeshi gani matatu yamekuja katika nusu duara kwa mda wa siku saba?
Israeli, Yuda, na Edomu walikuja katika nusu duara kwa mda wa siku saba.
2 Kings 3:11-12
Je! Elisha alifanya nini kwa ajili ya Eliya?
Elisha alimwaga maji juu ya mikono (msaidizi) waEliya.
2 Kings 3:13-14
Kwa nini Elisha alivuta usikivu kwa mfalme wa Israeli?
Elisha alivuta usikivu kwa mfalme wa israeli kwa sababu Elisha aliheshimu uwepo wa Yehoshafati mfalme wa Yuda.
2 Kings 3:15-19
Je! Ni lini mkono wa Yahwe ulikuja juu ya Elisha?
Wakati mpiga kinubi alipopiga, mkono wa Yahwe ukaja juu ya Elisha.
2 Kings 3:20
Je! Ni lini nchi ilijazwa kwa maji?
Katika asubuhi karibu na mda wa kutoa sadaka, maji yakaja kutoka mwelekeo wa Edomu, na nchi ikajaa maji.
2 Kings 3:21-25
Je! Ni akina nani kutoa Wamoabu walikusanyika wenyewe pamoja kupigana?
Wote waliokuwa wanaweza kuweka juu silaha walikusanyika wenyewe pamoja.
Je! Wamoabu walitafakari nini walipoyaona maji?
Wakati Wamoabu walipoyaona maji, walifikiri wafalme watatu walikuwa wameangamizwa, na walikuwa wameuana kila mmoja.
2 Kings 3:26-27
Je! Mfalme wa Moabu alifanya nini kwa mwana wake wa kwanza?
Alimchukua mwana wake wa kwanza na kumtoa kama sadaka juu ya ukuta.
2 Kings 4
2 Kings 4:1-2
Je! Ni nini kilichokuwa kinaenda kutokea kwa watoto wa mke wa mmoja wa wana wa manabii?
Wawia walikuwa wakienda kuwachukua watoto wake wawili kuwa watumwa wake.
2 Kings 4:3-4
Kutoka wapi yule mwanamke aliazima vyombo?
Yule mwanamke aliazima vyombo kutoa kwa majirani zake.
2 Kings 4:5-9
Je! Ni lini mafuta yalianza kumwagika?
Baada ya mwana wake kusema hapakuwa na vyombo zaidi, mafuta yaliacha kumwagika.
2 Kings 4:10-13
Nini mwanamke muhimu kutoka Shunemu na mume walitengeza kwa ajili ya Elisha?
Walitengeneza chumba kidogo juu ya paa kwa ajili ya Elisha, pamoja na kitanda, meza, na taa.
2 Kings 4:14-16
Mwanamke alipaswa kushikilia nini kwa muda wa mwaka mmoja?
Alipaswa kumshikilia mtoto wa kiume
2 Kings 4:17-24
Lini mtoto alijiumiza kichwa chake?
Wakati mtoto alipoenda siku moja kwa baba yake, ambaye alikuwa pamoja na wavunaji, akajiumizi kichwa chake.
Je! Yule mtoto aliketi wapi hadi alipokufa?
Mtoto aliketi juu ya magoti ya mama yake hadi alipokufa.
2 Kings 4:25-26
Je! Mtu wa Mungu alikuwa wapi?
Mtu wa Mungu alikuwa Mlima Karmeli.
Wakati Gehazi alipomuuliza yule mwanamke kama kila kitu kilikuwa sawa, je alijibu nini?
Wakati Gehazi alipomuuliza yule mwanamke kama kila kitu kilikuwa sawa, alijibu, "kiko sawa."
2 Kings 4:27
Je! Yule mwanamke alifanya nini wakati alipokuja kwa yule mtu wa Mungu kwenye mlima?
Wakati alipokuja kwa mtu wa Mungu kwenye mlima, alimkumbatia miguu yake.
2 Kings 4:28-29
Je! Geahazi angefanya nini kama angekutana na mtu yeyote au kama yeyote aliyemsalimia?
Kama Gehazi angekutana na mtu yeyote au kama yeyote angemsalimia, asingemjibu.
2 Kings 4:30-31
Je! Gehazi alilalia nini juu ya uso wa mtoto?
Alilalia fimbo juu ya uso wa mtoto.
2 Kings 4:32-34
Je! Mwili wa mvulana ulipataje na joto?
Elisha alijinyoosha kuelekea juu ya mwili, na mwili wa kijana ukapata na joto.
2 Kings 4:35-37
Je! Yule mtoto alifanya nini kabla ya kufungua macho yake?
Yule mtoto alipiga chafya mara saba na kisha kufungua macho yake.
2 Kings 4:38-39
Je! Ni nani alikusanya matunda pori?
Mmoja wa wana wa manabii walikusanya matunda pori.
2 Kings 4:40-41
Je! Elisha aliondoaje kifo kutoka kwenye sufuria?
Elisha alirusha unga kwenye sufuria.
2 Kings 4:42-44
Je! Ni watu wangapi walikula boflo ishirini ya mikate ya shayiri?
Watu mia moja walikula maboflo ishirini ya mikate ya Shayiri.
2 Kings 5
2 Kings 5:1-2
Je! Yahwe alimpatia nini Aramu kupitia Naamani?
Yahwe alimpatia ushindi Aramu.
2 Kings 5:3-4
Je! Ni nani ambaye msichana mdogo alisema angemponya bwana wake?
Msichana alisema nabii aliyekuwa Samaria angemponya bwana wake.
2 Kings 5:5-6
Je! Naamani alichukua barua kwa nani ambayo ilitoka kwa mfalme Aramu?
Naamani alichukua barua kupeleka kwa mfalme wa Israeli.
2 Kings 5:7
Je! Mfalme wa Israeli alifikiria nini ilikuwa sababu ya Naamani kuja kwake kwa ajili ya tiba?
Mfalme wa Israeli alifikiri Naamani alikuwa akitafuta kuanza majadiliano pamoja naye.
2 Kings 5:8-10
Je! Naamani aliambiwa kufanya nini ili awe msafi?
Naamani aliambiwa kwenda na kuzama mwenyewe kwenye Yordani mara saba kuwa msafi.
2 Kings 5:11-12
Je! Naamani alifikiri Elisha angempnyaje?
Naamani alifikiri Elisha angekuja kwake na kusimama na kuitia juu ya jina la Yahwe Mungu wake, na kupunga mkono juu ya mahali na kuponya ukoma.
2 Kings 5:13-14
Je! Nyama ya mwili wa Naamani ilirudi kama nini?
Nyama ya mwili wa Naamani ilirudi tena kama nyama ya mtoto mdogo.
2 Kings 5:15-16
Baada ya Naamana kuponywa, alifahamu nini?
Baada ya Naamani kuponywa, alifahamu kwamba hapakuwa na Mungu katika dunia yote isipokuwa katika Israeli.
2 Kings 5:17-19
Kwa ajili gani Naamani alimuuliza Yahwe kumsamehe?
Naamani alimuomba Yahwe kumsamehe wakati alipopiga magoti mwenyewe katika nyumba ya Rimoni.
2 Kings 5:20-22
Kutokana na Gehazi, nani alikuja kutoka nchi ya mlima wa Efraimu?
Kutokana na Gehazi, vijana wawili wa wana wa manbii walikuja kutoka nchi ya mlima wa Efraimu.
2 Kings 5:23-25
Gehazi alificha nini katika nyumba?
Alificha mifuko ya fedha katika nyumba.
2 Kings 5:26-27
Nini kilitokea kwa sababu ya Gehazi kudanganya?
Kwa sababu Gehazi alidanganya, akawa na ukoma.
2 Kings 6
2 Kings 6:1-3
Kwa nini wana wa manabii wanataka kujenga mahali pa kuishi?
Mahali ambapo waliishi pamoja na Elisha palikuwa padogo, hivyo walitaka kujenga mahali pa kuishi.
2 Kings 6:4-5
Kwa nini yule mtu aliyepoteza kichwa cha shoka walipatwa na wasiwasi?
Aliogopa kwa sabau shoka ilikuwa imeazimwa.
2 Kings 6:6-11
Je! Elisha alifanyaje shoka kuelea?
Alikata fimbo, akuitupa kwenye maji, na kuifanya shoka kuelea.
2 Kings 6:12-13
Nani alimwambia mfalme wa Israeli maneno ya mfalme wa Aramu?
Elisha alimwambia mfalme wa israeli maneno ya mfalme wa Aramu.
2 Kings 6:14-16
Kwa nini mtumishi wa Elisha alipatwa na wasiwasi?
Alipatwa na wasiwasi kwa sababu aliona jeshi kubwa pamoja na farasi na magari ya farasi yamezunguka mji.
2 Kings 6:17-19
Ni jinsi gani Elisha aliongoza Washami kwenda Samaria?
Elisha alimwomba Yahwe awapofushe, na kisha Elisha akawaambia kumfuata.
2 Kings 6:20-21
Je! Washami walikuwa wapi wakati Yahwe alipofungua macho yao?
Washami walikuwa katikati ya mji wa Samaria wakati Yahwe alipofungua macho yao.
2 Kings 6:22-23
Mfalme wa Israeli alifanya nini kwa Washami?
aliweka mkate na maji mbele yao, na aliwatuma mbali.
2 Kings 6:24-26
Kwa nini kichwa cha punda kiliuzwa kwa vipande themanini vya fedha?
Kulikuwa na njaa kubwa katika Samaria, hivyo kichwa cha punda kiluzwa kwa vipande themanini vya fedha.
2 Kings 6:27-29
Yule mwanamke alimwambia mfalme nini kilikuwa kinamsumbua?
Alijibu, "Huyu mwanamke amenambia, 'Mtoe mwana wako ili kwamba tuweze kumla leo, na tutamla mwanangu kesho,' " Hivyo tukamchemsha mwanangu na kumla, na nikamwambia siku ya pili yake, "Mtoe mwanao ambaye tunaweza kumla, lakini alikuwa amemficha mwanaye."
2 Kings 6:30-31
Nani alimlaumu mfalme alaumu kwa ajili ya njaa?
Alimlaumu Elisha.
2 Kings 6:32-33
Lini mjumbe alikuja kwa Elisha, aliwaambia wazee wafanye nini?
Wakati wajumbe walipokuja kwa Elisha, kuwaambia wazee kufunga mlango, na kushika mlango kuufunga juu yao.
2 Kings 7
2 Kings 7:1-2
Elisha alisema nini kingetokea kwa nahodha ambaye hakumwamini?
Elisha alimwambia asingekula unga wowote wala shayiri.
2 Kings 7:3-4
Kwa nini wale watu wanne wenye ukoma walienda kwenye jeshi la Washami?
Walienda kwenye jeshi la Washami kwa sababu walisema wangeweza kufa kama wataenda kwenye mji, kusimama mahali walipokuwa, au kwenda kwa jeshi la Washami.
2 Kings 7:5-8
Kwa nini jeshi la Washami walifikiri mfalme wa Israeli aliwakodi wafalme wa Wahiti na Wamisri kuja dhidi ya Washami?
Jeshi la Shamu kupitia mfalme wa israeli aliwakodi wafalme wa Wahiti na Wamisri kuja dhidi ya Washami kwa sababu walisikia sauti za magari ya farasi, na sauti za farasi-suti ya jeshi jingine kubwa.
2 Kings 7:9-11
Je! Mabawabu walifanya nini baada ya kuambiwa kwamba Washami walikuwa wametoka kambini kwao?
Mabawabu walipiga kelele kwa sauti habari kwamba Washami walitoka kwenye kambi yao.
2 Kings 7:12-13
Mfalime alifikiria nini ilikuwa sababu ya Washami kuondoka kwenye kambi yao?
Mfalme alifikiri waliondoka nje ya kambi kujificha katika mashamba. Kisha wakati Waisraeli walipotoka kwenye mji, Washami wangewachuka wakiwa hai, na kuingia kwenye mji.
2 Kings 7:14-17
Barabara ilikuwa imejaa nini?
Barabara ilikuwa imejaa nguo na vifaa vya Washami walivitupa mbali wapate kukimbia upesi.
2 Kings 7:18-20
Je! Nahodha alisema nini wakati Elisha alipomwambia, "Kuhusu huu mda katika lango la Samaria, vipimo viwili vya shayiri vitapatikana kwa shekeli moja, na kipimo kimoja cha unga mzuri kwa shekeli moja."?
Nahodha alimwambia Elisha, "Tazama, hata kama Yahwe ataweka madirisha mbinguni, je hili jambo linaweza kutokea?".
2 Kings 8
2 Kings 8:1-2
Kwa nini yule mwanamke ambaye mtoto wake Elisha alimfufua katika nchi ya Wafilisti miaka saba?
Yule mwanamke ambaye mtoto wake Elisha alimfufua katika nchi ya Wafilisti miaka saba kwa sababu Elisha alimwambia Yahwe alimuita kwa ajili ya njaa.
2 Kings 8:3-4
Kwa nini yule mwanamke alienda kwa mfalme?
Yule mwanamke alienda kwa mfalme kumuomba kwa ajili ya nyumba yake na kwa ajili ya nchi yake.
2 Kings 8:5-6
Je! Gehazi alikuwa akimwambia nini mfalme wakati yule mwanamke mwenye mtoto ambaye Elisha alimfufua?
Gehazi alikuwa akimwambia mfalme jinsi Elisha alivyomfufua yule mtoto aliyekuwa amekufa.
2 Kings 8:7-9
Hazaeli alichukua nini pamoja naye kumpatia Elisha?
Hazaeli alichukua zawadi za kila kitu kizuri pamoja naye za Damaskasi, zilibebwa kwa ngamia arobaini.
2 Kings 8:10-12
Kwa nini mtu wa Mungu aliomboleza?
Mtu wa Mungu aliomboleza kwa sababu alijua uovu ambao Hazaeli aliufanya kwa watu wa Israeli.
2 Kings 8:13-17
Baada ya Hazaeli kumwambia mfalme wa Shamu kwamba atapona, atapona, je! alifanya nini kwa Mfalme Ben Hadadi?
Baada ya Hazaeli kumwambia Mfalme Ben Hadadi kwamba atapona, alichukua blanketi na kulizamisha kwenye maji, na kulisambaza juu ya uso wa Ben Hadadiili hivyo basi akafa.
2 Kings 8:18-19
Mke wa Yoramu alikuwa nani?
Mke wa Yoramu alikuwa binti wa Ahabu.
Kwa nini Yahwe hataki kwenda kuiharibu Yuda?
yahwe hakutaka kwenda kuiharibu Yuda tangu alipomwambia mtumishi wake Daudi kwamba angempatia uzao.
2 Kings 8:20-24
Wakati Edomu alipoasi chini ya mkono wa Yuda?
Katika siku za Yoramu, Edomu aliasi chini ya mkono wa Yuda.
2 Kings 8:25-27
Kwa nini Ahazi alifanya kilicho kiovu katika uso wa Yahwe?
Ahazi alifanya kilicho kiovu katika uso wa Yahwe, kwa kuwa Ahazi alikuwa mtoto wa kambo kwenye nyumba ya Ahabu.
2 Kings 8:28-29
Mfalme Yoramu alirudi wapi kuponywa majeraha ambayo Washami walimpa huko Rama?
Mfalme Yoramu alirudi kuponywa katika Yezreeli.
2 Kings 9
2 Kings 9:1-3
Kwa nini mmoja wa wana wa manabii walichukua chopa ndogo ya mafuta katika mkono wake na kwenda Ramath Geliadi?
Alichukua chupa ya mafuta na kwenda Giliadi kumpaka Yehu.
2 Kings 9:4-6
Nani alimwagiwa mafuta juu ya kichwa cha Yehu?
Nabii alimwaga mafuta juu ya kichwa cha Yehu.
2 Kings 9:7-8
Je! Yahwe alilipizaje kisasi cha damu ya watumishi wake?
Kama Yehu aliiua familia ya Ahabu, Yahwe angelipiza kisasi cha damu ya watumishi wake.
2 Kings 9:9-10
Nini kilikuwa kinaenda kutokea kwa Yezebeli?
Mbwa wangemla Yezebeli katika Yezreeli, na huko pasingekuwa na mtu wa kumzika.
2 Kings 9:11-13
Watumishi wa bwana wa Yehu walifanya nini baada ya Yehu kusema alimpaka mafuta kama mfalme?
Baada ya Yehu kusema alikuwa amepakwa mafuta kama mfalme, kila mmoja wa watumishi alichukua haraka vazi lake la nje na kuliweka juu ya Yehu juu ya ngazi. Walipigatarumbeta na kusema, "Yehu ndiye mfalme."
2 Kings 9:14-16
Kwa nini Mfalme Yoramu alirudi Yezreeli?
Mfalme Yoramu alirudi Yezreeli kuponywa majeraha ambayo Washami walikuwa wamempatia.
2 Kings 9:17-18
Je! Mlinzi alimuona mlinzi anafanya nini?
Mlinzi alimuona mjumbe akiendesha pamoja na Yehu.
2 Kings 9:19-20
Je! Mlinzi alijuaje Yehu alikuwa akiendesha gari la farasi?
Mlinzi alijua Yehu alikuwa akiendesha gari la farasi, kwa kuwa kwa nguvu sana.
2 Kings 9:21-22
Je! Yoramu mfalme wa Israeli alijinasua kuonana na Yehu?
Yoramu mfalme wa Israeli alijinasua pamoja na Ahazia mfalme wa Yuda, kila mmoja katika gari lake la farasi, kumlaki Yehu.
2 Kings 9:23-24
Nini kilitokea baada ya Yehu kumpiga Yoramu kati ya mabega yake?
Baada ya Yehu kumpiga Yoramu kati ya mabega yake, mshale ulipita kwenye moyo wa Yoramu, na akaanguka chini katika gari lake la farasi.
2 Kings 9:25-26
Ni kitu gani kingetimiza mambo yaliyokuwa yamesemwa kuwa yatatimia kwa neno la Yahwe?
Kumchukua Yoramu na kumtupia kwenye lile shamba kungetimiza mambo ambayo yailikuwa yamesemwa yangetokea kwa neno la yahwe.
2 Kings 9:27-29
Ni nani alizikwa katika kaburi lake pamoja na baba yake katika mji wa Daudi?
Ahazia alizikwa katika kaburi lake pamoja na baba yake katika mji wa daudi.
2 Kings 9:30-32
Nini kilitokea wakati Yehu alipokuja kwa Yezreeli?
Wakati yehu alipokuja kwa Yezreeli, Yezebeli alisikia kuhusu hili, alichora macho yake, akapanga nywele zake, na kutazama kwenye dirisha.
2 Kings 9:33-34
Nani alimtupa Yezreeli chini?
Baadhi ya matowashi walimtupa Yezebeli chini.
2 Kings 9:35-37
Kwa nini hapakuwa na mtu wa kumzika Yezebeli?
wakati walipoenda kumzika, hawakukuta chochote zaidi ya fuvu, miguu, na viganja vya mikono mikono yake.
2 Kings 10
2 Kings 10:1-3
Barua ya Yehu ilikuwa inawaambia kufanya nini wazee na walezi wa ukoo wa ahabu?
Iliwaambia wazee na walezi wa ukoo wa Ahabu kuchagua koo za bwana wao nzuri zinazostahili na kumuweka kwenye kiti cha enzi cha baba yake.
2 Kings 10:4-5
Kwa nini wazee na walinzi wa koo za Ahabu hawajfanya mtu yeyote mfalme?
Hawakumfanya mtu yeyote kuwa mfalme kwa sababu walitambua kwamba isingewezekana wafalme wawili waweze kusimama mbele ya mfalme Yehu.
2 Kings 10:6-9
wazee na walezi wa koo za Ahab walifanya nini kwa wana wa mfalme?
Waliwachukua wana wa mfalme na kuwauua, watu sabini, wakaviweka vichwa vyao katika vikapu, na kuvipeleka kwa Yehu katika Yezreeli.
2 Kings 10:10-11
Kwa nini Yehu alisema kwamba hakuna sehemu ya neno la Yahwe, lile neno ambalo linalohusu familia ya Ahabu, lingeanguka chini?
Yehu alisema kwamba hakuna sehemu ya neno la Yahwe, lile neno lililonenwa kuhusu familia ya Habu, lingeanguka chini, kwa kuwa Yahwe alifanya kile alichokinena kupitia mtumishi wake Eliya.
2 Kings 10:12-14
Yehu aliwalaki na kuwaua ndugu wa Ahazia wangapi?
Aliwalaki na kuwaua arobaini na mbili.
2 Kings 10:15-17
Kwa nini Yehu alimchukua Yehonadabu kwenye gari la farasi?
Yehu walimchukua Yehonadabu kwenye gari la farasi kwa sababu Yehonadabu alisema moyo wake ulikuwa na Yehu na alimpa Yehu mkono wake.
2 Kings 10:18-20
Kwa nini Yehu aliwakusanya manabii wote wa Baali, waja wake wote, na makuhani wake wote?
Aliwakusanya kwa hila, kwa dhamira ya kuwaua waja wa Baali.
2 Kings 10:21-22
Wamwabuduo Baali walikuja wapi?
Walikuja kwenye hekalu la Baanali.
2 Kings 10:23-24
Nini kingetokea kama yeyote kati ya wamwabuduo Baali angetoroka?
Kama yeyote kati ya wamwabuduo Baali angetoroka, yeyote aliyemwacha huyo mtu akatoroka, mke wake angechukuliwa kwa ajili ya uzima wa abaye aliyetoroka.
2 Kings 10:25-28
Walezi na manahodha walitengeneza nyumba ya Baali kwenye nini?
Walitengeneza nyumba ya Baali kwenye choo.
2 Kings 10:29-33
Yehu alishindwaje kucha dhambi za Yeroboamu?
Yehu hakuacha dhambi za Yeroboamu kwa sababu aliabudu ndama wa dhahabu katika Betheli na Dani.
Kwa nini ukoo wa Yehu ungekaa kwenye kiti cha enzi cha Israeli hata kizazi cha nne?
Kwa sababu Yehu alifanya vizuri katika kutekeleza kile kilicho haki katika macho ya Yahwe, na kufanya kwenye nyumba ya ukoo ungekaa juu ya kiti cha enzi cha Israeli hata kizazi cha nne.
2 Kings 10:34-36
Je! Mambo mengine yaliyokuwa yanamuhusu Yehu yaliandikwa wapi?
Mambo mengine yanayomuhusu Yehu, na yote aliyoyafanya, na uweza wake wote, yalikuwa yameandikwa katika kitabu cha matukio ya Mfalme wa Israeli.
2 Kings 11
2 Kings 11:1-3
Je! Athalia hakumuua nani?
Athalia hakumuua Yashi.
2 Kings 11:4-6
Je! Mamia ya makamanda wa magari ya farasi na wa walinzi walitakiwa kufanya nini kabla ya kumuona mwana wa mfalme?
Mamia ya makamanda ya Wakri na walinzi walifanya agano pamoja na Yehoyada na kuapa kiapa katika nyumba ya Yahwe. Kisha akawaonyesha mwana wa mfalme.
2 Kings 11:7-8
Makundi mawili ambayo hayakuwa yanatumika katika Sabato yalikuwa yakifanya nini?
Makundi mawili ambayo hayakuwa yakitumika katika Sabato yalikuwa yakitunza mda juu ya nyumba ya Yahwe kwa ajili ya mfalme.
2 Kings 11:9-12
Yehoyada alipeleka nini kwa makamanda?
Yehoyada alipeleka mikuki na ngao iliyokuwa ya Mfalme Daudi, ambayo ilikuwa katika nyumba ya Yahwe.
2 Kings 11:13-14
Kwa nini Athalia alichana mavazi yake na kupiga kelele?
Athalia alichana mavazi yake na kupiga kelele kwa sababu alimuona Mfalme Yoashi amesimama karibu na nguzo.
2 Kings 11:15-16
Kwa nini Athalia aliuawa kwenye nyumba ya mfalme?
Athalia aliuawa kwenye nyumba ya mfalme, kwa kuwa kuhani alisema, "Msimwache auawe kwenye nyumba ya Yahnwe."
2 Kings 11:17-18
Baada ya Yehoyada kufanya agano, je!watu walifanya nini?
Baada ya Yehoyada kufanya agano, watu waliirarua chini nyumba ya Baali, kupiga madhabahu ya Baali na picha za sanamu zake kuwa vipande vipande, na kumuua Matani, kuhani wa Baali.
2 Kings 11:19-21
Wakti Yoashi alipokaa juu ya kiti cha enzi cha wafalme, je! watu waliitikiaje?
Wakati Yoashi alipokalia kiti cha enzi cha wafalme, watu wote wa nchi walifurahi.
2 Kings 12
2 Kings 12:1-3
Kwa nini Yoashi alifanya kile kilicho sahihi katika macho ya Yahwe siku zote?
Yoashi alifanya kile kilichokuwa sahihi katika macho kwa Yahwe siku zote, kwa sababu Yehoyada kuhani alikuwa akiwa akimfundisha.
2 Kings 12:4-5
Ni kwa namna gani watu walitiwa hamasa kutoa pesa kwa ajili ya hekalu?
Watu walitiwa hamasa na Yahwe katika mioyo kutoa.
2 Kings 12:6-8
Kwa nini Yoashi aliwaambia makuhani wasichukue pesa tena kutoka kwa walipa kodi?
Yoashi alimwambia makuhani hivi kwa sababu hawakuwa wamekatarabati chochote katika hekalu.
2 Kings 12:9-10
Je! Nani aliweka pesa kwenye kifua?
Makuhani waliokuwa wakilinda mlango wa kuingia kwenye hekalu na kuweka kwenye kifua pesa zote ambazo zililetwa kwenye nyumba ya Yahwe.
2 Kings 12:11-14
Watenda kazi walitumia pesa kwa ajili ya nini?
Watenda kazi walitumia pesa kwa ajili ya kununua mbao na kukata mawe kwa ajili ya kukarabati hekalu la Yahwe, na kwa yote yaliyokuwa yanahitajika kwa ajili ya kulikarabati.
2 Kings 12:15-16
Kwa nini pesa ya sadaka za hatia na pesa za sadaka za dhambi hazikuletwa kwenye hekalu la Yahwe?
Pesa za sadaka za hatia na pesa za sadaka za dhambi hazikuletwa kwenye hekalu la Yahwe, kwa sababu zilikuwa mali ya makuhani.
2 Kings 12:17-18
Je! Mfalme Yoashi alimzuiaje Mfalme Hazaeli kutoka kuishambulia Yerusalemu
Yoashi alichukua vitu vyote vitakatifu ambavyo Yehoshafati na Yehoramu na Ahazia waliviweka wakfu kwa ajili ya Yahwe, vitu vyake vitakatifu, na dhahabu yote iliyokuwa imepatikana katika chumba cha kuhifadhi cha nyumba za Yahwe na za mfalme, na aliwatuma kwa Ahazaeli, mfalme wa Aramu. Kisha Hazaeli akaenda mbali na Yerusalimu.
2 Kings 12:19-21
Nani alimshambulia Yoashi?
Yozakari, mwana wa Shimeathi, na Yehozabadi, mwana wa Shomeri, watumishi wake, walimshambulia Yoashi.
2 Kings 13
2 Kings 13:3-5
Kwa nini Yahwe aliwapatia ulinzi Israeli?
Yehoahazi alimsihi Yahwe, hivyo Yahwe akawapatia Israeli ulinzi.
2 Kings 13:6-13
Mfalme wa Aramu aliliharibu jeshi la Israeli na kuwafanya kama nini?
Mfalme wa Aramu aliliharibu jeshi la Israeli na kuwafanya kama nyasi ziliyopurwa.
2 Kings 13:14-16
Wakati Elisha alipokuwa anaumwa, Je! Alimwambia Yoashi achukue nini?
Alimwambia Yoashi kuchukua upinde na mishale.
2 Kings 13:17-19
Nini kilitokea kwa sababu Yoashi alipiga ardhi mata tatu tu?
Kwa sababu alipiga ardhi mara tatu tu, angeweza kuishambulia Aramu mara tatu tu.
2 Kings 13:20-21
Nini kilitikea kwa yule mtu ambaye alikuwa amezikwa katika kaburi la Elisha?
Yule mtu ambaye aliyezikwa katika kaburi la Elisha alifufuka na kusimama kwa miguu yake mwenyewe mapema kama yule mtu aliyegusa mifupa ya Elisha.
2 Kings 13:22-25
Kwa nini Yahwe hakuipeleka Israeli mbali na uwepo wake?
Yahwe aliwafadhili Israeli, na alikuwa na huruma juu yao na uhusiano nao, kwa sababu ya agano lake na Ibrahimu, Isaka, na Yakobo. Hivyo Yahwe hakuwaangamiza, na hakuwapeleka mbali na uwepo wake.
2 Kings 14
2 Kings 14:4-5
Ahazia alifanya nini mapema utawala ulivyokuwa umeimarika vizuri?
Mapema wakti utawala wake ulipokuwa umeimarika vizuri, Amazia aliwaua watumishi waliokuwa wamuua baba yake, mfalme.
2 Kings 14:6-7
Kwa nini Ahazia hakuwaua wana wa wauaji?
Amazia hakuwaua wana wa wauaji kwa sababu Yahwe alimwamuru, kusema, "Mababa wasiuawe kwa ajili ya wana wao, wala mtoto asiuawe kwa ajili ya wazazi wake. Badala yake, kila mtu atauawa kwa ajili ya dhambi zake mwenyewe."
2 Kings 14:8-12
Nini kiliangusha chini ule mbaruti?
Hayawani aliyekuwa Lebanoni aliuangusha chini.
2 Kings 14:13-16
Yoashi alichukua nini kutoka Yerusalemu?
Alichukua dhahabu na fedha zote, vitu vyote vilivyokuwa vimepatikana katika nyumba ya Yahwe, na vile vitu vya thamani katika nyumba ya mfalme, pamoja na mateka pia.
2 Kings 14:17-19
Je! Amzia alikufaje?
Njama iliundwa na Amazia katika Yerusalemu, na kukimbilia Lakishi na walimuulia huko.
2 Kings 14:20-22
Je! Uzia alifanya nini kwa Elathi?
Uzia aliijenga upya Elathi na kuirejesha kwa Yuda.
2 Kings 14:23-25
Kupitia nani Yeroboamu alisikia kwamba arudishe mpaka wa Israeli kutoka Lebo Hamathi hata bahari ya Araba?
Yeroboamu alisikia kupitia Yona mwana na Amitai, nabii, kwamba ataurudisha mpaka wa Israeli kutoka Lebo Hamathi hata bahari ya Araba.
2 Kings 14:26-29
Kwa sababu Yahwe aliona hapakuwa na ulinzi kwa ajili ya Israeli, je aliwaokoaje?
Kwa sababu Yahwe aliona hakuna ulinzi kwa ajili ya Israeli, Yahwe aliwaokoa kwa mkono wa Yeroboamu mwana wa Yehoashi.
2 Kings 15
2 Kings 15:4-5
Je! Yahwe alimtesaje mfalme Uzia?
Yahwe alimtesa mfalme kwa ukoma katika siku za kufa kwake na kuishi katika nyumba iliyojitenga.
2 Kings 15:6-9
Nani alikuwa mfalme katika nyumba kifalme ya Uzia?
Yothamu, mwana wake, akawa mfalme katika nyumba ya kifalme.
2 Kings 15:10-12
Je! Shalumu alimuulia wapi Zekaria?
Shalumu alimua Zekaria mbele ya watu.
Uzao wa Yehu ungekalia kiti cha Israeli kwa mda gani?
Uzao wa Yehu ungekalia kiti cha Israeli hata kizazi cha nne.
2 Kings 15:13-18
Kwa nini Shalumu alitawala mwaka mmoja pekee katika Samaria?
Shalumu alitawala mwaka mmoja pekee katika Samaria kwa sababu Menahemu mwana wa Gadi alimuua.
2 Kings 15:19-24
Menahemu alikusanyaje vipaji elfu moja vya fedha kutoa Pulu?
Menahemu alikusanya vipaji elfu moja vya fedha kwa kumtaka kila mtu tajiri alipe shekeli hamsini za fedha kwake.
2 Kings 15:25-28
Nani alimuua Pekahia?
Peka alimuua Pekahia.
2 Kings 15:29-33
Kwa nini Hoshea aliandaa mateso juu ya Peka?
Hosehea aliandaa mateso juu ya Peka kwa sababu Tiglath Pileseri mfalme wa Ashuru alikuja na kuchukua miji mingi.
2 Kings 15:34-38
Yothamu alifuata mfano wa nani?
Yothamu alifwata mfano wa baba yake Uzia.
2 Kings 16
2 Kings 16:3-4
Ahazi alifanya nini kwa mtoto wake?
Ahazi alimuweka mtoto wake kwenye moto kama sadaka ya kuteketeza, kufuata mazoea ya mataifa
2 Kings 16:5-6
Reseni hakufanya nini wakati alipoiteka Yerusalemu?
Wakati Reseni alipoishambulia Yerusalemu, hakuweza kumshinda Ahazi.
2 Kings 16:7-9
Ahazi alimpatia zawadi gani mfalme wa Ashuru?
Ahazi alichukua fedha na dhahabu zilizokuwa zimepatikana katika nyumba ya Yahwe na miongoni mwa hazina za nyumba ya mfalme, na kuituma kama zawadi kwa mfalme wa Ashuru.
2 Kings 16:10-12
Ni madhabahu ipi Ahazi alitaka Uria aifufue?
Ahazi alitaka kufufua madhabahu huku Damaskasi.
2 Kings 16:13-14
Nani alitengeza sadaka yake ya kuteketeza na sadaka yake ya mazao?
Mfalme alitengeneza sadaka yake ya kuteketeza na sadaka yake ya mazao.
2 Kings 16:15-16
Dhumuni la madhabahu ya shaba lilikuwa nini?
Madhabahu ya shaba ilikuwa kwa ajili ya Ahazi kwa ajili ya kuuliza msaada wa Mungu.
2 Kings 16:17-20
Kwana nini Ahazi aliondoa njia iliyokuwa imefunika kwa ajili ya Sabato ambayo walikuwa wameijenga kwenye hekalu, karibu na mlango wa mfalme wa kuingia nje ya hekalu la Yahwe?
Ahazia aliondoa njia iliyokuwa imefunika kwa ajili yha Sabato walikuwa wameijenga kwenye hekalu, karibu na mlango wa kuingia wa mfalme nje ya hekalu la Yahwe, kwa sababu ya mfalme wa Ashuru.
2 Kings 17
2 Kings 17:1-3
Hoshea alifanya nini wakati alipokuwa mtumishi wa Shalmanesa?
Hoshea alikuwa mtumishi wa wake na alimletea kodi.
2 Kings 17:4-6
Hoshea alikuwa anapangaje njama juu ya Shalmanesa?
Hoshea alikuwa akipanga njama juu ya Shalmanesa, kwa ajili ya Hoshea alikuwa akituma ujumbe kwa So, mfalme wa Misri.
2 Kings 17:7-10
Kwa nini utumwa umetokea?
Utumwa ulitokea kwa sababu watu wa Israeli walitenda dhambi juu ya Yahwe Mungu wao.
2 Kings 17:11-12
Yahwe alisema Waisraeli wasifanye nini?
Yahwe alisema wasiabudu sanamu.
2 Kings 17:13
Yahwe alishuhudia na nani kwa Israeli na Yuda?
Yahwe alishuhudiwa kwa Israeli na kwa Yuda kwa kila nabii na kila mwonaji.
2 Kings 17:14-15
Waisraili walikuwa wakaidi kama nani?
Waisraeli walikuwa wakaidi kama baba zao ambao hawakumwamini Yahwe Mungu wao.
2 Kings 17:16-20
Waisraeli walijiuzaje wenyewe?
Waisraeli walijiuza wenyewe kufanya kile ambacho ni uovu katika usu wa Yahwe.
2 Kings 17:21-23
Kwa nini Yahwe aliwaondoa Israeli katika uso wake?
Watu wa Israeli walifuata dhambi zote za Yeroboamu na hawakuondoka kutoka kwao hivyo Yahwe aliwaondoa Israeli kutoka usoni mwake.
2 Kings 17:24-26
Kwa nini Yahwe alipeleka simba kati ya mataifa mapya katika Samaria?
Mataifa katika Samaria hawakumheshimu Yahwe, hivyo alipeleka simba kati ya yao.
2 Kings 17:27-28
Kuhani aliwafundisha nini watu wapya katika Betheli?
Kuhani aliwafundisha jinsi wanavyotakiwa kumheshimu Yahwe.
2 Kings 17:29-31
Je! kundi la kila kabila liliweka wapi miungu waliyoitengeneza?
Kila kundi la kabila lilifanyah miungu yao wenyewe, na kuiweka katika madhabahu ambayo Wasamaria walikuwa wamezifanya.
2 Kings 17:32-33
Badala ya miungu yao, mataifa mapya yamuheshimu nani katika Israeli?
Mataifa mapya pia yalimwabudu Yahwe.
2 Kings 17:34-38
Je! Watu wapya katika Israeli hawakumuheshimuje Yahwe?
Watu wapya hawakumuheshimu Yahwe, kwa sababu aliwaamuru kwamba wasiwaogope miungu wengine.
2 Kings 17:39-41
Je! Mataifa mapya katika Israeli hayakusikilizaje?
Hayakusikiliza kwa sababu waliendelea kufanya waliyokuwa wameyafanya siku za nyuma.
2 Kings 18
2 Kings 18:4-8
Watu wa Israeli walikuwa wakifanya nini kwenye nyoka wa shaba Musa aliyokuwa ameitengeneza?
Watu wa Isaraeli walikuwa wakichoma ubani kwenye nyoka wa shaba aliyekuwa ametengenezwa na Musa.
2 Kings 18:9-10
Ni kwa mda gani Shalmanesa aliiteka Samaria?
Shalmanesa mfalme wa Ashuru aliiteka Samaria kwa miaka mitatu.
2 Kings 18:11-12
Kwa nini mfalme wa Ashuru aliichukua Israeli mateka kwenda Ashuru?
Mfalme wa Ashuru aliwachukua mateka kwenda Ashuru kwa sababu hawakutii sauti ya Yahwe Mungu wao.
2 Kings 18:13-15
Hezekia alipata fedha kutoka wapi kumpatia mfalme wa Ashuru?
Hezekia alipata fedha zilizokuwa zimepatikana katika nyumba ya Yahwe na katika hazina za eneo la mfalme.
2 Kings 18:16-18
Kutokaa wapi Tartani na Rabsarisi na kamanda mkuu waliitwa na mfalme Hezekia?
Waliitwa kwa Mfalme Hezekia kutoka kwenye mfereji wa kisima cha kuogelea cha juu, juu ya barabara kuu ya uwanja wa dodi.
2 Kings 18:19-21
Nini kingetokea kama huyo mtu angeegemea juu ya Misri?
Kama huyo mtu angeegemea juu ya Misri, ingempiga kwenye mkono wake na kuichoma.
2 Kings 18:22-23
Ni kitu gani ambacho mfalme wa Ashuru alijitolea kufanya?
Mfalme wa Ashuru alijitolea kutoa farasi elfu mbili, kama Ahazi angeweza kuwapata waendeshaji kwa ajili yao.
2 Kings 18:24-25
Yahwe alimwambia nini mfalme wa Ashuru kufanya?
Yahwe alimwambia mfalme wa Ashuru kuishambulika Yuda na kuiharibu.
2 Kings 18:26-27
Ni katika lugha gani Eliakimu, Shebna, na Joa walimuuliza amiri jeshi mkuu kuzungumza?
Eliakimu, Shebna, na Joa walimuuliza amiri jeshi mkuu kuzungumza kiaramaiki.
2 Kings 18:28-30
Amiri jeshi mkuu alipiga kelele kwa lugha gani?
Amiri jeshi mkuu alipiga kelele kwa lugha ya Kiyahudi.
2 Kings 18:31-35
Je! Mfalme wa Ashuru angewaacha wale wafanyao amani pamojam naye wafanye nini?
Angewaacha wale kutoka mzabibu wao wenyewe na kutoka kwenye mtini wao wenyewe, na kunywa kutoka kwenye maji katika chemichemi zao wenyewe.
2 Kings 18:36-37
Mfalme Ahazi alimwamuru nani?
Mfalme Ahazi aliwaamuru watu wasimjibu amiri jeshi mkuu.
2 Kings 19
2 Kings 19:1-2
Mfalme Hezekia alifanya nini baada ya kusikia taarifa?
Wakati mfalme Hezekia aliposikia taarifa, alirarua mavazi yake, na kujifunika kwa magunia na kwenda kwenye nyumba ya Yahwe.
2 Kings 19:3-4
Hezekia alisema Yahwe angefanya nini?
Hezekia alisema Yahwe atasikia maneno yote ya Rabshake na na kuweza kumuonya maneno ambayo Yahwe aliyoyasikia.
2 Kings 19:5-9
Yahwe angefanya nini kumsitisha mfalme wa Ashuri?
Yahwe angeweka roho katika yeye, na mfalme angesikia taarifa nyingine na kurudi katika nchi yake mwenyewe.
2 Kings 19:10-13
Kutokana na Senakeribu, ni kwa njia gani Mungu alimdanganya Hezekia?
Kutokana na Senakeribu, Mungu alimdanganya Hezekia kwa kusema Yerusalemu haitapatiwa juu ya mkono wa mfalme wa Ashujru.
2 Kings 19:14-18
Hezekia alisambaza wapi barua kutoka wajumbe?
Hezekia alisambaza barua kutoka wajumbe katika nyumba ya Yahwe.
2 Kings 19:19
Kwa nini Yahwe atawaokoa watu wa Yuda?
Yahwe atawaokoa watu wa Yuda ili kwamba falme zote za dunia wajue kwamba Yahwe ni Mungu pekee.
2 Kings 19:20-22
Mfalme wa Ashuru aliinua saujti juu ya nani?
Mfalme wa Ashuru aliinua saujti yake juu ya Mtakatifu Mmoja wa Israeli!
2 Kings 19:23-24
Nani alisema alijaribu mito yote ya Misri chini ya nyayo za miguu yake?
Senakeribu alisema alijaribu mito yote ya Misri chini ya nyayo za miguu yake.
2 Kings 19:25-26
Nani alibainisha zamani kwamba miji isiyoingilika itapunguzwa kwenye fungu la uharibifu?
Yahwe alibainisha zamani kwamba miji isiyoingilika ingepunguzwa kwanye fungu la uharibifu.
2 Kings 19:27-28
Yahwe angeweka nini katika pua ya Senakeribu?
Yahwe angeweka ndoana yake katika pua ya Senakeribu.
2 Kings 19:29-31
Ishara ya Hezekia itakuwa kwa ajili ya nini?
Ishara itakuwa kwamba watu wa Yuda watakula vimeavyo porini, na katika mwaka wa pili vile vimeavyo kutoka hapo.
2 Kings 19:32-34
Kwa nini Yahwe aliilinda Yerusalemu?
Yahwe aliilinda Yerusalemu kwa ajili yake mwenyewe na kwa ajili ya mtumishi wake Daudi.
2 Kings 19:35-37
Je! Yahwe aliilindaje Yerusalemu?
Yahwe alienda na kuishambulia kambi ya Waashuru, kuwaua maaskari 185,000.
2 Kings 20
2 Kings 20:1-3
Je! Yahwe alimwambia Hezekia afanye nini kwa sababu angekufa?
Yahwe alimwambia Hezekia kuweka nyumba yake katika hali nzuri kwa kuwa angbekufa.
2 Kings 20:4-5
Kwa nini Yahwe alitaka kumponya Hezekia?
Kwa sababu Yahwe alisikia maombi ya Hezekia na kuona machozi yake, alitaka kumponya.
2 Kings 20:6-9
Hezekia aliponaje?
Mkate wa mtini uliwekwa juu ya jipu lake, na alipona.
2 Kings 20:10-11
Je! Yahwe alibadilishaje kivuli?
Yahwe alileta kivuli hatua kumi nyuma, kutoka mahali kilipokuwa kimehamia hata kwenye ngazi ya Ahazi.
2 Kings 20:12-15
Hezekia aliwaonyesha nini wajumbe kutoka kwa mfalme wa Babeli?
Hezekia aliwaonyesha kila kitu katika nyumba ya utawala.
2 Kings 20:16-18
Nini kitatokea kwa wana waliozaliwa kutoka Hezekia?
Watu wa Babeli watawachukua wana waliozaliwa kutokana na yeye, na watakuwa matowashi kwenye nyumba ya kifalme ya mfalme wa Babeli.
2 Kings 20:19-21
Kwa nini Hezekia alidhani kwamba neno la Yahwe lilikuwa jema?
Hezekia alidhani kwamba kwamba neno la Yahwe lilikuwa jema kwa sababu kungukuwa na amani na uthabiti katika siku zake.
2 Kings 21
2 Kings 21:1-3
Manase alijenga nini tena?
Manase alipajenga tena mahala pa juu ambapo Hezekia baba yake, alipaharibu.
2 Kings 21:4-6
Pamoja na nani Manase alipajenga?
Manase alipajenga pamoja na wale waliokuwa wamenena na wale waliukufa pamoja na wale walionena na roho.
2 Kings 21:7-9
Manase aliweka nini katika nyumba ya Yahwe?
Manase aliweka picha ya ndama ya Ashera ambayo alikuwa ameitengeneza katika nyumba ya Yahwe.
2 Kings 21:10-12
Nani Manase alifanya maovu zaidi kuliko?
Manase alifanya maovu zaidi kuliko Waamori mbele yake.
2 Kings 21:13-15
Kwa nini masalia majanga na nyara kwa ajili ya adui zao?
Masalia yalikuwa majanga na nyara kwa ajili ya adui zao kwa sababu walifanya yaliyo uovu katika uso wa Yahwe, kuchochea hasira yake.
2 Kings 21:16-20
Je! Ni kiasi gani cha damu isiyokuwa na hatia alizimwaga?
Manase alizimwaga damu nyingi sizokuwa na hatia ambazo alizijaza Yerusalemu kutoka upande huu hata mwingine kwa kifo.
2 Kings 21:21-23
Je! Amoni alikufaje?
Watumishi wa Amoni wakafanya njama dhidi yake na kumuua mfalme kwenye nyumba yake mwenyewe.
2 Kings 21:24-26
Amoni alizikwa wapi?
Watu walimzika Amoni katika kaburi lake katika bustani ya Uza.
2 Kings 22
2 Kings 22:1-2
Je! Yosia alitembeaje?
Yosia alitembea katika njia zote za Daudi babu yake, na hakugeuka wala kulia au kushoto.
2 Kings 22:3-5
Yosia alitaka Hilkia atoe nini kwa wafanya kazi ambao walikuwa katika nyumba ya Yahwe?
Yosia alimtaka Hilkia atoe fedha zilizokuwa zimeletwa kwenye nyumba ya Yahwe kwa wafanyakazi waliokuwa katika nyumba ya Yahwe.
2 Kings 22:6-7
Kwa nini hazikutakiwa kuhesabiwa wakati walipokuwa wanapewa wafanyakazi?
hazikutakiwa kuhesabiwa wakati walipokuwa wanapewa, kwa sababu waliimudu ile kazi kwa uaminifu
2 Kings 22:8-10
Hilkia alikuta nini katika nyumba ya Yahwe?
Hilkia alikuta kitabu cha sheria katika nyumba ya Yahwe.
2 Kings 22:11-13
Wakati mfalme aliposikia maneno ya sheria, alifanya nini?
Wakati mfalme aliposikia maneno ya sheria, alirarua mavazi yake.
2 Kings 22:14-16
Hulda aliishi wapi?
Hulda aliishi katika Yerusalemu katika mtaa wa pili.
2 Kings 22:17-19
Kwa nini Yahwe alimsikiliza mfalme wa Yuda?
Yahwe alisikiliza mfale wa Yuda kwa sababu moyo wako ulikuwa mlaini, na kwa sababu umejinyenyekesha mwenyewe mbele ya Yahwe, na kwa sababu alirarua mavazi yake na kuomboleza mbele za Yahwe.
2 Kings 22:20
Macho ya mfalme wa Yuda hayakuona nini?
Macho yake hayakuona maafa yoyote ambayo Yahwe angeyaleta juu ya mahali na wenyeji wake.
2 Kings 23
2 Kings 23:1-2
Alisoma katika masikioni kwao maneno yote ya kitabu cha agano?
Mfalme alisoma maneno yote ya kitabu cha agano katika usikivu wa watu wote wa Yuda na wenyeji wote wa Yerusalemu, na makuhani, manabii, na watu wote, kuanzia wadogo hata wakubwa.
2 Kings 23:3
Je! Watu wote walikubaliana kufanya nini?
Watu wote walikubaliana kusimama kwenye agano.
2 Kings 23:4-5
Je! Mfalme alichoma nini nje ya Yerusalemu katika nyanda katika bonde la Kidroni?
Mfalme alichoma vyombo vyote ambavyo vilitengenezwa na Ashera, kwa ajili ya njota zote za mbinguni nje ya Yerusalemu katika mashamba katika bonde la Kidroni.
2 Kings 23:6-7
Ni vyumba gani mfalme alivisafisha?
Mfalme alivisafisha vyumba vya wanaume makahaba ambao walikuwa katika hekalu la Yahwe.
2 Kings 23:8-9
Makuhani wa hayo madhabahu ambapo walipokuwa wanachomea ubani walirusiwa kula mikate isiyotiwa chachu?
Makuhani wa hayo madhabahu ambapo ubani ulichomwa waliruhusiwa kula mkate usiotiwa chachu katika Yerusalemu.
2 Kings 23:10-11
Farasi wa wafalime waliokuwa wametolewa kwa ajili ya jua walikuwa wapi?
Farasi ambao walikuwa wametolewa kwa jua na wafalme wa Yuda walikuwa katika eneo la lango la kuingia hadi kwenye hekalu la Yahwe, karibu na chumba cha Nathani Meleko.
2 Kings 23:12-14
Nani alijenga mlima wa uharibisfu?
Sulemani mfalme wa Israeli alijenga mlima wa uharibifu.
2 Kings 23:15-16
Kwa nini Yosia aliiteketeza mifupa juu ya madhabahu ilikuwa Betheli?
Aliichoma mifupa juu ya madhabahu ili kuinajisi.
2 Kings 23:17-20
Mifupa ya nani haikuhamishwa na Yosia?
Yosia hakuhamisha mifupa ya mtu wa Mungu aliyekuja kutoka Yuda na yule nabii aliyekuwa amekuja kutoka Samaria.
2 Kings 23:21-23
Ni kwa mda gani aina hiyo ya sikukuu ya Pasaka haijawahi kufanyika?
Aina hiyo ya sikuu ya Pasaka haijawahi kufanyika kutoka siku za waamuzi waliotawala Israeli, wala katika siku zote za wafalme wa Israeli au Yuda.
2 Kings 23:24-25
Je! Yosia alimrudiaje Yahwe?
Yosia alimrudia Yahwe kwa moyo wake wote, roho yake yote, na nguvu zake zote.
2 Kings 23:26-27
Yahwe hakugeuka kutoka wapi?
Yahwe hakugeuka kutoka kwenye ukali wa ghadhabu yake.
2 Kings 23:28-30
Nani alienda kupigana juu ya mfalme wa Ashuru huko mto Frati?
Farao Neko, mfalme wa Misri, alienda kupigana juu ya mfalme wa Ashuru katika mto Frati
2 Kings 23:31-33
Kwa nini Farao Neko alimuweka Yehoahazi gerezani huko Ribla katika nchi ya Hamathi?
Farao Neko alimuweka gerezani huko Ribla katika nchi ya Hamathi, ili asiweze kutawala katika Yerusalemu.
2 Kings 23:34-37
Je! Yehoyakimu alipataje pesa ya kumlipa Farao?
Yehoyakimu aliitoza nchi kulipa pesa, kwa ajili ya kumlipa Farao.
2 Kings 24
2 Kings 24:1-2
Yahwe aliongea nini kupitia watumishi wake manabii?
Yahwe aliongea kupitia watumishi wake manabii ukanda wa Wakaldayo, Washami, Wamoabu, na Waamoni angeiharibu Yuda.
2 Kings 24:3-6
Ni kitu gani ambacho Yahwe hakuwa tayari kusamehe?
Yahwe hakuwa tayari kumsamehe kwamba Manase aliijaza Yerusalemu kwa damu isiyokuwa na hatia.
2 Kings 24:7-9
Kwa nini mfalme wa Misri hakumshambulia tena nje ya nchi yake?
Mfalme wa Misri hakushambulia tena nje ya nchi yake, kwa sababu mfalme wa Babeli alakuwa amezishinda nchi zote ambazo zilikuwa zikitawaliwa na mfalme wa Misri.
2 Kings 24:10-12
Nebukadreza alimteka Yekonia lini?
Nebukadreza alimteka Yekonia katika mwaka wa nane wa utawala Nebukadreza.
2 Kings 24:13-14
Nani aliondoka katika nchi?
Watu maskini pekee waliondoka katika nchi.
2 Kings 24:15-20
Ni kwa jina gani mfalme wa Babeli alimbadilisha Matania?
Mfalme wa Babeli alibadilisha jina la Matanika kuwa Zedekia.
2 Kings 25
2 Kings 25:1-3
Kwa nini hapakuwa na chakula kwa ajili ya watu wa nchi?
Njaa ilikuwa kali sana katika mji ambao haukuwa na chakula kwa ajili ya watu wa nchi.
2 Kings 25:4-5
Wapiganaji wote walikimbia?
Wapiganaji wote walikimbia usiku kwa njia ya lango katika ya kuta mbili, karibu na bustani ya mfalme.
2 Kings 25:6-7
Nini kilitokea kwa Zedekia baada ya wana wake kuchinjwa?
Baasa ya wana wa Zedekia kuchinjwa, Wakaldayo walitolewa macho yao, wakamfunga pingu, na kumpeleja Babeli.
2 Kings 25:8-10
Nani aliziharibu kuta zote kuzunguka Yerusalemu?
Jeshi lote la Wababeli waliokuwa chini ya kamanda wa mlinzi waliziharibu kuta zote kuizunguka Yerusalemu.
2 Kings 25:11-15
Kwa nini mlinzi aliwaacha baadhi ya maskini wa nchi?
Mlinzi aliwaacha baadhi ya mskini wa nchi kufanya kazi kwenye mizabibu na mashamba.
2 Kings 25:16-19
Ni kiasi gani cha shaba kilichukua kwa nguzo mbili?
Zile ngunzo mbili zilichukua shaba zaidi kuliko kuwa na uzani.
2 Kings 25:20-21
Mfalme wa Babeli alifanya nini kwa watu waliokuwa wamechuliwa mateka na kamanda wa mlinzi?
Mfalme wa Babeli aliwaua.
2 Kings 25:22-24
Nebukadreza alimuweka nani kuwa msimamizi wa watu waliobaki katika nchi ya Yuda?
Nebukadreza alimuweka Gedalia msimamizi wao.
2 Kings 25:25-26
Kwa nini watu wote na makamanda wa maaskari walienda Misri?
Watu wote na makamanda wa maaskari walikwenda Misri, kwa sababu waliwaogopa Wababeli.
2 Kings 25:27
Yekonia alitolewa lini kutoka gerezani?
Yekonia altolewa kutoka gerezani katika mwaka wa thelathini na saba wa uhamisho wa Yekonia, katika mwaka huo Evil-Merodaki alianza kutawala.
2 Kings 25:28-30
Yekonia alikula chakula gani?
Yekinia akala siku zote kwenye meza ya mfalme katika maisha yake yote yaliyokuwa yamebakia. Na chakula cha kawaida cha ruzuku kilitolewa kwa ajili yake kila siku kwa ajili ya maisha yake yote.