2 Peter
2 Peter 1
2 Peter 1:1-2
Ni nani alyeandika warakawa pili wa Petro?
Ni Simon Petro, mtumwa na mtume wa Yesu Kristo.
Petro alimwandikia nani?
Petro aliwaandikia wale waliokuwa wameipokea ile imani ya thamani
2 Peter 1:3-4
Je, hali ya nguvu ya Mungu na utauwa ilikuwaje kwa Petro na kwa wale walioipokea imani?
Wlipew kwa njia ya maarifa ya Mungu
Kwa nini Mugu alimpatia Petro na wale walioipokea imani mambo yote ya nguvu ya Mungu katika maisha na utauwa, pamoja na ahadi kubwa na za thamani?
Alifanya hivyo ili waweze kuwa wamilika wa asili ya Mungu
2 Peter 1:5-7
Ni kitu gani kikubwa ambacho wale walioipokea imani walitaiwa kukipata kwa njia ya imani?
Walikusudiwa kupata upendo kwa njia ya imani yao.
Ni kitu gani kikubwa ambacho wale walioipokea imani walitaiwa kukipata kwa njia ya imani?
Walikusudiwa kupata upendo kwa njia ya imani yao.
2 Peter 1:8-9
Ni kitu gani ambacho kipofu wa rohoni amesahau?
Amesahau kusafishwa kwa dhambi zake za zamani.
2 Peter 1:10-11
Kama ndugu wangefanya juhudi ili kujithibitishia wito na uteule wao kingetokea nini?
Wasingejikwaa, na wangelipewa lango la kuingia kwenye ufalme wa milele wa Bwana na mwokozi Yesu Kristo.
2 Peter 1:12-15
Kwa nini Petro alifikiri ilikuwa sahihi kuwakumbusha ndugu mambo haya?
Kwa sababu Bwana wao Yesu Kristo karibu ataondoa hema lake.
2 Peter 1:16-18
Ni kitu gani ambacho wale waliokuwa mashahidi wa Yesu kristo waliona?
Waliona kuwa Yesu alipokea toka kwa Mungu Baba heshima na utukufu
2 Peter 1:19-21
Twawezaje kuwa na uhakika ya kwamba maneno ya unabii ni ya kweli?
Kwa sababu unabii ulioandikwa hautokani na uwezo wa manabii wa kufikria, wala hapana unabii uliopatikana kwa utashi wa mtu, isipokuwa wanadamu waliwezeshwa na Roho Mtakatifu aliyeongea toka kwa Mungu.
2 Peter 2
2 Peter 2:1-3
Kitu gani ambacho waalimu wa uongo watakileta kwa waumini kwa siri?
Walimu wa uongo wataleta mafundisho ya uongo yaharibuyo na kumkana Bwana aliyewanunua.
Kitu gani kitatokea kutokana na waalimu wa uongo?
Kuharibiwa na na hukumu vitakuja haraka kwa sababu ya waalimu wa uongo
Walimu wa uongo watayatumiaje maneno ya uongo?
Watayatumia maneno ya uongo kwa kujipatia faida kutoka kwa wenzao.
2 Peter 2:4-6
Ni viumbe gani ambavyo Mungu hakuviachilia?
Mungu hakuwaachilia Malaika waliokengeuka, ulimwengu wa zamani na pia Sodoma na Gomora.
Mungu alimuokoa nani katika gharika?
Mungu alimuokoa Nuhu na wengine saba.
2 Peter 2:7-9
Mungu alionesha nini kwa kuwaokoa wengine na kuwaangamiza wengine?
Kitendo hiki cha Mungu kinaonesha kuwa Mungu anajua kuwaokoa watu wake.
2 Peter 2:10-11
Hao watukufu ni akina nani ambao watu wasiomwabudu Mungu hawaogopi kuwakufuru?
Hao watukufu ni malaika, ambao hawawezi kuleta hukumu juu ya watu wa Bwana.
2 Peter 2:12-14
Waalimu wa uongo waliwashawishi watu gani.
Waalimu wa uongo waliwashawishi watu wasio imara kiimani.
2 Peter 2:15-16
Nani aliyezuiua wazimu wa balaam?
Punda bubu aliongea katika sauti ya binadamu.
2 Peter 2:17-19
Ni kwa namna gani mwanadamu anaweza kuwa mtumwa?
mwanadamu anaweza kuwa mtumwa kwa chochote kinachomtawala.
2 Peter 2:20-22
Wana uheri upi? wale wajiepushao na uchafu wa ulimwengu kwa kutumia maarifa ya Yesu Kristo na kisha kuyarudia uchafu huo?
Ingekuwa heri kwao kama wasingeijua njia ya haki.
2 Peter 3
2 Peter 3:1-2
Kwa nini Peter kuandika barua ya pili?
Aliandika barua hii ili kukumbuka maneno yaliyosemwa na manabii na juu ya amri ya Bwana na Mwokozi wao.
2 Peter 3:3-4
Je wenye mzaha watasema nini katika siku ya mwisho?
Wenye mzaha watauliza swali juu ya ahadi ya kurudi kwa Yesu na kusema kuwa mambo yote yatabaki kama yalivyokuwa kama mwanzo wa uumbaji.
2 Peter 3:5-7
Mbingu na nchi vimetengenezwaje na ni jinsi gani vimewekwa akiba kwa ajili ya moto katika siku ya hukumu na uharibifu wa watu waovu?
Vilianzishwa na kuwekwa akiba kwa neno la Mungu.
2 Peter 3:8-9
Kwa nini Bwana anawavumilia watu anaowapenda?
Kwa sababu hawastahili kuangamia na wana muda wakutubu.
2 Peter 3:10
Siku ya Bwana itakuja kwa namna gani?
Siku ya Bwana itakuja kama mwizi.
2 Peter 3:11-13
Kwa nini Petro aliwauliza wapendwa kuhusu aina ya watu ambao walipaswa kuwa katika mambo yahusuyo maisha matakatifu na utaua?
Kwa sababi mbingu na nchi zitaharibiwa na kwa sababu wanatarajia haki iwepo katika mbingu mpya na nchi mpya.
2 Peter 3:14-16
Nini kitatokea kwa watu wasio na nidhamu ambao wameharibu hekima waliyopewa na Paulo?
Matendo yao yatasababisha kuangamia kwao.
2 Peter 3:17-18
Tofauti na suala la kupotoshwa na udanganyifu na kupoteza uaminifu, Petro aliwaamuru wapendwa wafanye nini?
Aliwaamuru wakue katika neema na ufahamu wa Bwana na Mwokozi Yesu Kristo