2 John
2 John 1
2 John 1:1-3
Katika barua hii Yohana ambaye ni mwandishi anajitamburisha kwa cheo gani?
Yohana anajitamburisha kama Mzee.
Barua hii iliandikwa kwa nani?
Barua iliandikwa kwa mama mteule na watoto wake.
Yohana anasema amani, rehema na neema hutoka kwa nani?
Yohana anasema amani, rehema na neema zinatoka kwa Mungu Baba na kwa Yesu Kristo mwana wake.
2 John 1:4-6
Kwa nini Yohana anafurahi?
Yohana anafurahi kwa sababu amefahamu kuwa baadhi ya watoto wa mwanamke wanatembea nuruni.
Yohana anasema ni amri gani wamekuwa nayo tangu mwanzo?
Yohana anasema kwamba wamekuwa na amri ya kupendana tangu mwanzo.
Yohana anasema upendo ni nini?
Yohana anasema upendo ni kuenenda kulingana na amri za Mungu.
2 John 1:7-8
Yohana anawaitaje wale wasio kiri kuwa Yesu Kristo alikuja katika mwili?
Yohana anawaita wale wasio kiri kuwa Yesu Kristo alikuja katika mwili wadanganyifu na wapinga Kristo.
Yohana anawaambia waumini wawe waangalifu kufanya nini?
ohana anawaambia waumini wawe waangalifu wasipoteze mambo waliyokwisha kuyafanya.
2 John 1:9-11
ohana anawaambia waumini wamfanye nini mtu anayeleta mafundisho yasiyo ya kweli kuhusu Kristo?
Yohana anawaambia waumini wasimpokee mtu yeyote asiyeleta mafundisho ya kweli kuhusu Kristo.
Muumini anahatia gani kama atampokea mtu ambaye haleti mafundisho ya kweli kuhusu Kristo?
Muumini anahatia ya kushiriki katika matendo maovu ya mtu ambaye haleti mafundisho ya kweli kuhusu Kristo.
2 John 1:12-13
Yohana anatumaini kufanya nini wakati ujao?
Yohana anatumaini kuja na kuongea uso kwa uso na mwanamke mteule.