Kiswahili: translationQuestions

Updated ? hours ago # views See on DCS Draft Material

Galatians

Galatians 1

Galatians 1:1-2

Ni kwa jinsi gani Paulo alikuwa ni mtume?

Paulo alikuwa mtume kupitia kwa Yesu Kristo na Mungu baba.

Galatians 1:3-5

Waumini ndani ya Yesu Kristo wameololewa kutoka wapi?

Waumini ndani ya Yesu Kristo wameokolea kutoka katika nyakati hizi za uovu

Galatians 1:6-7

Paulo anashangazwa na jambo gani katika kanisa la Galatia?

Paulo anashangazwa na jinsi watu walivyogeukia haraka injili nyingine

kuna injili ngapi za kweli?

kuna injili moja tu ya kweli, ya Yesu Kristo

Galatians 1:8-10

Paulo anasema kutatokea nini kwa mtu anayetangaza injili nyingine tofauti na injili ya Kristo?

Paulo anasema mtu yeyote anayehubiri injili nyingine lazima alaaniwe.

Je watumishi wa Mungu wanatakiwa kutafuta uthibitisho kwa nani kwanza?

Watumishi wa Mungu wanapaswa kutafuta uthibitisho wa Mungu kwanza.

Galatians 1:11-12

Je ni kwa namna gani Paulo alipokea ufahamu of Injili ya Kristo?

Paulo aliipokea injili ya Kristo kwa ufunuo kutoka kwa Yesu Kristo moja kwa moja

Galatians 1:13-14

Paulo alikuwa akifanya nini katika maisha yake kabla ya kuupoke ufunuo wa injili ya Kristo?

Paulo alikuwa akifuata dini ya Kiyahudi kwa juhudi sana na kulitesa kanisa la Mungu.

Galatians 1:15-17

Mungu alimchagua Paulo lini awe Mtume wake?

Ilimpendeza Mungu kumchagua Paulo awe mtume wakati akali katika tumbo la mama yake

Kwa kusudi gani Mungu alimchagua Paulo awe mtume wake?

Mungu alimchagua Paulo kama mtume wake ili aweze kumtangaza Kristo kwa watu wa mataifa.

Galatians 1:18-20

Je, hatimaye Paulo alikutana wapi na mitume wengine?

Hatimaye Paulo alikutana na Petro na Yakobo baada ya kuwa amekwenda Yerusalem

Galatians 1:21-24

Je makanisa ya uyahudi yalikuwa yanasikia nini kuhusu Paulo?

Makanisa ya uyahudi yalikuwa yakisikia kwamba Paulo aliyekuwa akilitesa kanisa hapo mwanzo, sasa anaitangaza imani.

Galatians 2

Galatians 2:1-2

Je Paulo alifanya nini alipoenda Yerusalemu baada ya miaka kumi na minne?

Paulo aliongea na viongozi kwa siri, akiwaeleza injili aliyokuwa akiihubiri/kuitangaza.

Galatians 2:3-5

kitu gani ambacho Tito, mtu wa mataifa, hakutakiwa kufanya?

Tito hakutakiwa kutahiriwa

Galatians 2:6-8

Je viongozi wa kanisa huko Yerusalemu waliubadili ujumbe wa Paulo?

Hapana, hawakuchangia chochote kwa ujumbe wa Paulo.

Je kimsingi Paulo alikuwa ametumwa kwa watu gani kutangaza injili?

Paulo alikuwa ametumwa kuwatangazia injili watu wasiotahiriwa

Je, kimsingi Petro alikuwa ametumwa kutangaza injili kwa watu gani?

Petro alikuwa ametumwa kutangaza injili kwa watu waliotahiriwa.

Galatians 2:9-10

Je ni kwa namna gani viongozi wa Yerusalemu walionesha kuikubali huduma ya Paulo?

Viongozi wa Yerusalemu waliwapa mkono wa kulia Paulo na Barnaba kuonesha kuwapokea na kuwakubali katika ushirika.

Galatians 2:11-12

Ni kosa gani Petro alifanya alipoenda Antiokia?

Petro alikataa kula na watu wa mataifa kwasababu aliwaogopa watu wale waliotahiriwa.

Galatians 2:13-14

Paulo alimwuliza nini Kefa ( Petro) mbele za watu?

Paulo alimwuliza Kefa ni kwa jinsi gani anaweza kuwaamuru watu wa mataifa kuishi kama wayahudi wakati Kefa alikuwa akiishi kama mtu wa mataifa.

Galatians 2:15-16

Paulo alisema mtu hawezi kuhesabiwa haki kwa kitu gani?

Paulo alisema kwamba hakuna mtu awezaye kuhesabiwa haki kwa matendo ya sheria.

Je mtu anaweza kuhesabiwa haki mbele za Mungu kwa namna gani?

Mtu huhesabiwa haki kwa njia ya Imani katika Kristo Yesu.

Galatians 2:17-19

Paulo anasema atakuwaje mtu yule ambaye amekwisha mwamini Yesu, kisha akarudi na kufuata sheria?

Paulo anasema kuwa mtu huyo anajionesha kuwa yeye ni mwasi.

Galatians 2:20-21

Paulo alisema ni nani anayeishi ndani yake?

Paulo anasema kwamba Kristo anaishi ndani yake sasa.

Paulo anasemaje juu ya kile Kristo alichokifanya ndani yake?

Paulo anasema Mwana wa Mungu anampenda na amejitoa kwa ajili ya Paulo

Galatians 3

Galatians 3:6-9

Jinsi gani Ibrahimu alihesabiwa haki mbele za Mungu?

Ibrahimu alimwamini Mungu ikahesabiwa kwake kuwa haki.

Watoto wa Ibrahimu ni akina nani?

Watu wale wanaomwamini Mungu ni watoto wa Ibrahimu.

Je maandiko yalitabiri nini juu ya watu wa mataifa wangehesabiwa haki kwa njia gani?

Maandiko yalitabiri kwamba watu wa mataifa wangehesabiwa haki kwa njia ya imani.

Galatians 3:10-12

Je watu wale wanaotegemea matendo ya sheria wapate kuhesabiwa haki wako chini ya nini?

Wanaotegemea matendo ya sheria wapate kuhesabiwa haki wako chini ya laana.

Ni watu wangapi wamehesabiwa haki na Mungu kupitia matendo ya sheria?

Hakuna mtu yeyote aliyekwisha hesabiwa haki kwa matendo ya sheria.

Galatians 3:13-14

Kwanini Kristo alifanyika laana ili alitukomboe?

Kristo alitukomboa kwa kufanyika laana kwa ajili yetu ili baraka za Ibrahimu ziwe ya watu wa mataifa.

Galatians 3:15-16

Ni "uzao" wa nani unaozungumziwa katika ahadi ya Ibrahimu.

Uzao unaongelewa katika ahadi ya Ibrahimu ni Kristo

Galatians 3:17-18

Je Kuja kwa sheria ya wayahudi miaka 430 baada ya Ibrahimu kunazuia ahadi za Mungu kwa Ibrahimu?

Hapana, sheria hazikuweza kuzuia ahadi alizofanya Mungu kwa Ibrahimu.

Galatians 3:19-20

Kwa nini basi tena kukawa na sheria?

Sheria ilikuja kwa sababu ya uasi mpaka uzao wa Ibrahimu (Yesu) ulipokuja.

Galatians 3:21-22

Ni kitu gani ambacho sheria ya maandiko humfunga mtu nacho?

Sheria za maandiko humfunga mtu chini ya dhambi.

Galatians 3:23-26

Jinsi gani tunawekwa huru kutoka katika kifungo cha sheria?

Tunawekwa huru kutoka kifungo cha sheria kwa imani katika Kristo Yesu.

Galatians 3:27-29

Nani amekwisha kujivika katika Kristo?

Wote waliokwisha kubatizwa katika Kristo wamekwisha kujivika katika Kristo.

Ni watu wa aina gani waliofanywa kuwa mmoja katika Kristo?

Wayahudi, Wagriki, watumwa, walio huru, wanaume, na wanawake wote hufanya kuwa mmoja katika Kristo Yesu.

Galatians 4

Galatians 4:1-2

Kwa jinsi gani mrithi huishi akiwa yungali mtoto mdogo?

Mrithi huishi chini ya msimamizi na mdhamini akiwa bado mdogo mpaka muda uliokusudiwa na baba yake kutimia wa kupokea uruthi wake.

Galatians 4:3-5

Mungu alifanya nini ulipofika wakati sahihi katika historia?

Ulipotimia wakati sahihi Mungu alimmtuma Mwana wake kuja kuwakomboa wale walikuwa chini ya sheria.

Je ni kwa namna gani Mungu aliweza kuwatoa watoto walikuwa chini ya sheria na kuwaleta kwenye familia yake?

Mungu aliwapokea na kuwafanya kuwa wana wale waliokuwa chini ya sheria.

Galatians 4:6-7

Ni kitu gani ambacho Mungu ameweka ndani ya watoto wake?

Mungu alimtuma Roho wa Mwanawe Yesu Kristo kuingia na kukaa ndani ya mioyo ya wauasi wake (Wakristo).

Galatians 4:8-11

Kabla ya kumjua Mungu tulikuwa chini ya ya utumwa wa nani?

Kabla ya kumjua Mungu wa kweli tulikuwa chini ya utumwa wa roho za dunia hii ambazo si miungu kamwe.

Ni jambo gani ambalo Wagalatia walikuwa wanalirudia kias cha Paulo kumtatiza Paulo?

Paulo alishangazwa na kitendo cha Wagalatia kurudi tena kwenye utawala wa roho za dunia hii.

Ni kitu gani ambacho Paulo alikiogopa baada ya kuona Wagalatia wakirudi nyuma?

Paulo aliogopa kuwa Wagalatia wangekuwa watumwa tena, na kwamba kazi yake itakuwa bure juu yao.

Galatians 4:12-16

Tatizo gani alilokutana nalo Paulo baada ya kufika Galatia kwa mara ya kwanza?

Paulo alipofika Galatia kwa mara ya kwanza aliugua/ alikuwa mgonjwa.

Pamoja na tatizo alilokuwa nalo Paulo, Wagalatia walimpokeaje?

Pamoja na tatizo la Paulo, Wagalatia walimpokea Paulo kama ni malaika wa Mungu, kama Yesu Kristo.

Galatians 4:17-20

Ni nani waliokuwa walimu wa uongo waliotaka kuwatenga Wagalatia ?

Ni wale walimu wa Uongo waliokuwa wakiwafundisha Wagalatia ili kuwatenga na Paulo

Galatians 4:21-25

Walimu wa uongo walikuwa wakitafuta kuwatia Wagalatia chini ya nini?

Walimu wa uongo walikuwa wakijaribu kuwatia Wagalatia chini ya sheria.

Ni aina gani ya wanawake ambao kutoka kwao Ibrahimu alipata wana?

Ibrahimu alikuwa na wana wawili , mmoja kutoka kwa mtumwa na mmoja kutoka kwa mwanamke huru.

Galatians 4:26-27

Nani ni Mama wa mfano wa Paulo na waumini wa Galatia?

Yerusalemu, Mwanamke aliye huru, ndiye mama wa mfano wa Paulo na waumini wa Galatia.

Galatians 4:28-29

Je! Waumini ndani ya Kristo ni watoto wa mwili ama wa ahadi?

Wakristo wote katika Kristo ni watoto wa Ahadi.

Nani huwatesa watoto wa ahadi?

Watoto wa mwili huwatesa watoto wa ahadi.

Galatians 4:30-31

Ni kitu gani wanachorithi watoto wa mwanamke mtumwa?

Watoto wa mwanamke mtumwa hawatarithi pamoja na watoto wa mwanamke huru.

Je waumini ndani ya Yesu Kristo ni watoto wa mwanamke mtumwa au wa mwanamke huru?

Waumini ndani ya Kristo ni watoto wa mwanamke huru.

Galatians 5

Galatians 5:1-2

Kristo ametuweka huru kwa kusudi gani ?

Kristo ametuweka huru ili tuwe huru

Paulo aliwaonya Wagalatia kuwa kitu gani kingetokea kama Wagalatia wangetahiriwa?

Paulo alisema kwamba kama Wagalatia wangetahiriwa, wasingepata faida yoyote katika Kristo.

Galatians 5:3-4

Ni kitu gani ambacho Paulo aliwaonya Wayahudi kuwa kingetokea kama wangetafuta kuhesabiwa haki kwa kushika sheria?

Paulo aliwaonya Wagalatia ambao kama wangetafuta kuhesabiwa haki kwa kushika sheria wangetengwa na Kristo na wangekatiliwa mbali na neema ya Mungu.

Galatians 5:5-8

Tofauti na hali ya kutahiriwa na kutotahiriwa, kuna jambo gani pekee lenye maana ndani ya Yesu?

Imani inayotenda kazi katika upendo katika Kristo ndiyo kitu chenye maana sana.

Galatians 5:9-10

Ni jambo gani ambalo Paulo alikuwa nalo uhakika kuhusu mtu yule ambaye angewapotosha Wagalatia kuhusu injili?

Paulo ana uhakika kuwa mtu yule atakayewapotosha Wagalatia kuhusu injili atahukumiwa na Mungu.

Galatians 5:11-12

Paulo anasema kunafanyika nini kama tohara itatangazwa ?

Paulo anasema kwamba kwa kutangaza tohara kikwazo cha msalaba kingeweza kuharibiwa.

Galatians 5:13-15

Namna gani waumini hawapaswi kutumia uhuru wao katika Kristo?

Waumini hawapaswi kutumia uhuru wao katika kama fursa kwa kutimizia matakwa ya mwili.

Namna gani waumini wanapaswa kutumia uhuru wao katika Kristo?

Waumini wanapaswa kutumia uhuru wao katika Kristo kutumikiana kwa upendo wao kwa wao.

Ni amri gani ambayo hukamilisha sheria yote?

Sheria yote hutimilizwa katika amri moja " Mpende jirani yako kama wewe mwenyewe"

Galatians 5:16-18

Namna gani waumini hawawezi kutimiza tamaa mbaya za mwili?

Waumini wanaweza kuishi kwa Roho ili wasitimize tamaa mbaya za mwili.

Ni mambo gani mawili yanayokinzana ndani ya Muumini?

Roho na mwili hupingana ndani ya muumini.

Galatians 5:19-21

Ni mifano gani mitatu ya matendo ya mwili?

Mifano mitatu ya matendo ya mwili ni moja wapo ya yafuatayo: uasherati, tamaa mbaya, kuabudu sanamu, uchawi, wivu, ulevi, .....

Ni kitu gani ambacho watu wanatenda matendo ya mwili hawatakipokea?

Wale wenye kutenda matendo ya mwili hawataurith ufalme wa Mungu.

Galatians 5:22-26

Tunda la Roho ni nini?

Tunda la Roho ni upendo, furaha, amani, uvumilivu, utu wema, fadhili, uaminifu, upole na kiasi.

Watu walio wa Kristo wamefanya jambo gani katika mwili na tamaa zake?

Watu wa Yesu Kristo wameusulubisha mwili pamoja na tamaa zake.

Galatians 6

Galatians 6:1-2

Wale ambao ni wa kiroho wanapaswa kufanya nini ikiwa mtu amenaswa katika baadhi ya maovu?

Wale ambao ni wa kiroho wanapaswa kumrejesha mtu huyo kwa roho ya upole.

Ni hatari gani ambayo wale walio wa kiroho wanapaswa kujihadhari nayo?

Wale walio wa kiroho lazima wajihadhari kwamba wasije nao wakajaribiwa!

Ni kwa jinsi gani waumini wanaweza kutimiza sheria ya Kristo?

Wakristo wanaweza kutimiza sheria ya Kristo kwa kuchukuliana mizigo.

Galatians 6:3-5

Ni kwa namna gani mtu anaweza akawa na kitu cha kujivunia kuhusu kazi yake?

Mtu anaweza kuwa na kitu ndani yake cha kujivunia kwa kupima kazi yake mwenyewe bila kujilinganisha na wengine.

Galatians 6:6-8

Ni nini ambacho mtu ambaye amefundishwa Neno anapaswa kumfanyia mwalimu wake?

Yule ambaye amefundishwa Neno lazima amshirikishe mwalimu wake vitu vizuri.

Kitatokea nini kwa mtu aliyepanda chochote kiroho?

Chochote anachopanda mtu kiroho atakivuna.

Atavuna nini mtu aliyepanda katika mwili ?

Mtu yule apandaye katika mwili wake atavuna uharibifu katika mwili wake.

Atavuna nini mtu apandaye katika Roho?

Mtu yule apandaye katika Roho atavuna uzima wa milele.

Galatians 6:9-10

Muumini atapata nini kama hatakata tamaa na kuendelea kutenda mema?

Muumini atakayeendelea kutenda mema atavuna mavuno.

Waumini wanatakiwa kutenda mema kwa nani?

Waumini wanatakiwa kutenda mema kwa hao walio wa nyumba ya imani.

Galatians 6:11-13

Ni msukumo gani walio nao watu wale wanaoshurutisha waumini kutahiriwa?

Wale wanaotaka kuwalazimisha waumini kutahiriwa hawaki kuteswa kwa ajili ya msalaba wa Kristo.

Galatians 6:14-16

Paulo alikuwa anajivunia nini?

Paulo alisema kwamba alikuwa anajivunia msalaba wa Bwana wetu Yesu Kristo.

Ni gani cha muhimu tofauti na kutahiriwa au kutotahiriwa?

kitu cha muhimu ni kuwa kiumbe kipya au uzao mpya.

Ni watu gani Paulo alikuwa akiwatakia amani na rehema?

Paulo anawatakia amani na rehema wale wanaoishi kwa kufuata kanuni za utu mpya na pamoja na Israeli ya Mungu.

Galatians 6:17-18

Paulo amebeba nini katika mwili wake?

Paulo amebeba chapa za Yesu katika mwili wake.