Ecclesiastes
Ecclesiastes 1
Ecclesiastes 1:1-3
Mwalimu alikuwa uzao wa nani?
Mwalimu alikuwa uzao wa Daudi, mfalme Yerusalemu.
Ecclesiastes 1:4-6
Nini kinabaki milele?
Dunia inabaki milele.
Ecclesiastes 1:7-8
Jicho haliridhiki na nini?
Jicho haliridhiki na kile inachokiona.
Ecclesiastes 1:9-11
Nini kitafanyika?
Chochote kilichofanyika kitafanyika tena.
Ecclesiastes 1:12-15
Mwalimu alitia akili yake kwa kitu gani?
Mwalimu alitia akili yake kusoma na kutafuta kwa hekima kila kitu kilichofanyika chini ya mbingu.
Matendo yote yanayofanyika chini ya jua yanaambulia nini?
Matendo yote yanaoyofanyika chini ya jua ni mvuke na jaribio la kuuongoza upepo.
Ecclesiastes 1:16-18
Wapi kuna kusumbuka kwingi?
Kwenye wingi wa hekima kuna kusumbuka kwingi.
Ecclesiastes 2
Ecclesiastes 2:1-2
Nini kilikuwa upepo wa muda?
Anasa zilikuwa upepo wa muda.
Ecclesiastes 2:3
Mwalimu alitaka kugundua nini?
Mwalimu alitaka kugundua ni ktiu gani kilifaa kwa watu kufanya chini ya mbingu wakati wa siku zao za maisha.
Ecclesiastes 2:4-6
Kwa nini Mwalimu alitengeneza mabwawa wa maji?
Mwalimu alitengeneza mabwawa ya maji kumwagilia msitu ambapo miti ilipandwa.
Ecclesiastes 2:7-8
Mwalimu alifanyaje vitu ambavyo vingempa furaha mwanamme yeyote duniani?
Kwa njia ya wake wake na masuria, alifanya vitu ambavyo vingempa furaha mwanamme yeyote duniani.
Ecclesiastes 2:9-10
Moyo wa Mwalimu ulifurahia nini?
Moyo wa Mwalimu ulifurahia kazi zake zote.
Ecclesiastes 2:11-12
Wapi hapakuwa na faida?
Hapakuwa na faida chini ya jua.
Ecclesiastes 2:13-14
Nini kinamsubiri kila mtu?
Mwisho mmoja unamsubiri kila mtu.
Ecclesiastes 2:15-16
Nani hakumbukwi kwa muda mrefu?
Mtu mwenye hekima, kama mpumbavu, hakumbukwi kwa muda mrefu.
Ecclesiastes 2:17-18
Kwa nini Mwalimu alichukia mafanikio yake yote?
Mwalimu alichukia mafanikio yake yote kwa sababu ilimbidi kuyaacha yote nyuma kwa mtu atakayemfuata.
Ecclesiastes 2:19-20
Moyo wa Mwalimu ulijisikia aje kuhusu kazi zake?
Moyo wa mwalimu ulianza kuhuzunika juu ya kazi zake zote alizofanya.
Ecclesiastes 2:21-23
Kwa nini roho ya aliyefanya kazi kwa bidii haikupumziki usiku?
Kila siku kazi yake inaumiza na kuchosha, kwa hiyo usiku roho yake haipati kupumzika.
Ecclesiastes 2:24-25
Kuna nini kinachofaa kuliko kwa kila mtu?
Hakuna kinachofaa kwa kila mtu kuliko kula na kunywa na kuridhika na kile kilicho kizuri katika kazi yake.
Ecclesiastes 2:26
Mungu anampa nini mtenda dhambi?
Kwa mtenda dhambi, Mungu anampa kazi ya kukusanya na kutunza ili ampe mtu anayempendeza Mungu.
Ecclesiastes 3
Ecclesiastes 3:1-7
Kuna msimu wa vitu gani?
Kuna msimu wa kila jambo chini ya mbingu.
Ecclesiastes 3:8-10
Mwalimu aliona nini?
Mwalimu aliona kazi ambayo Mungu aliwapa binadamu kukamilisha.
Ecclesiastes 3:11
Mungu aliweka nini mioyoni mwa watu?
Mungu aliweka umilele katika mioyo yao.
Ecclesiastes 3:12-13
Nini ni zawadi kutoka kwa Mungu?
Kizuri kitokacho kwenye kazi ya mtu ni zawadi kutoka kwa Mungu.
Ecclesiastes 3:14-15
Kwa nini hakuna kitu kinachoweza kuongezwa au kupunguzwa kutoka katika kitu chochote afanyacho Mungu?
Hakuna kitu kinachoweza kuongezwa au kupunguzwa kwa sababu ni Mungu ndiye aliyekifanya.
Ecclesiastes 3:16-18
Nini hupatikana katika sehemu ya haki?
Mahali pa haki uovu kawaida upo.
Ecclesiastes 3:19-20
Watu wakoje kama wanyama?
Kama wanyama, wote wanakufa. Wote lazima wapumue hewa moja. Kila kitu kinatoka kwenye mavumbi na kila kitu kinarudi kwenye mavumbi.
Ecclesiastes 3:21-22
Ni nini jukumu la kila mtu?
Jukumu la kila mtu ni kufurahia kazi yake.
Ecclesiastes 4
Ecclesiastes 4:1
Ni kitu gani hakina mfariji?
Hakuna mfariji wa machozi ya wanyonge.
Ecclesiastes 4:2-4
Nani ana bahati zaidi ya walio hai na wafu?
Aliye na bahati zaidi kuliko walio hai na wafu ni yule ambaye bado hajaishi.
Ecclesiastes 4:5-8
Ni nini kilicho bora zaidi ya mikono miwili yenye kazi ya kujaribu kuchunga upepo?
Bora mkono wa faida na kazi ya utulivu kulko mikono miwili yenye kazi ya kujaribu kuuchunga upepo.
Ecclesiastes 4:9-11
Kwa nini watu wawili ni bora kuliko mmoja pale ambapo mmoja ataanguka?
Watu wawili ni bora kuliko mmoja kwa sababu kama mmoja akianguka, yule mwingine atamuinua rafiki yake.
Ecclesiastes 4:12
Nini hakikatiki kwa urahishi?
Kamba yenye nyuzi tatu haikatiki kwa urahisi.
Ecclesiastes 4:13-14
Ni nini bora kuliko kuwa mfalme mzee aliye mpumbavu?
Ni bora kuwa masikini mwenye hekima kuliko kuwa mfalme mzee mpumbavu.
Ecclesiastes 4:15-16
Watu wanataka kufanya nini kwa mfalme mpya?
Watu wanataka kumtii mfalme mpya.
Ecclesiastes 5
Ecclesiastes 5:1
Kwa nini watu wanapaswa kwenda kwenye nyumba ya Mungu?
Watu wanapaswa kwenda kwenye nyumba ya Mungu kusikiliza.
Ecclesiastes 5:2-3
Kwa nini watu wanapaswa kufanya maneno yao yawe machache?
Mungu yuko mbinguni, lakini watu wako duniani, kwa hiyo wanapaswa kufanya maneno yao yawe machache.
Ecclesiastes 5:4-7
Ni nini kilicho bora kwa mtu kufanya kuliko kuweka madhiri na kushindwa kuitekeleza?
Ni bora kwa mtu kutokuweka nadhiri kuliko kuweka nadhiri ambayo anashindwa kutekeleza
Ecclesiastes 5:8-9
Wakati mtu akiona masikini akiteswa na kunyimwa haki na matendo mema, kwa nini mtu yeyote asishangae kana kwamba hakuna ajuaye?
Mtu akiona masikini anateswa na kunyimwa haki na matendo mema, hapaswi kushangaa kwa sababu kuna watu katika madaraka wanao watazama walio chini yao, na hata wapo walio juu zaidi yao.
Ecclesiastes 5:10-11
Ni hutokea mafanikio yanapoongezeka?
Mafanikio yanapoongezeka, watu wanaotumia pia wanaongezeka.
Ecclesiastes 5:12
Ni hakimruhusu tajiri kulala vizuri?
Mali za mtu tajiri hazimruhusu kulala vizuri.
Ecclesiastes 5:13-14
Nini hutokea wakati mtu tajiri anapopoteza utajiri wake kwa bahati mbaya?
Mtu tajiri anapopoteza utajiri wake kwa bahati mbaya, mwana wake, yule aliye mlea, anaachwa bila kitu mikononi mwake.
Ecclesiastes 5:15-18
Mtu anazaliwaje na ataundokaje katika haya maisha?
Mtu anazaliwa uchi kutoka tumboni mwa mama yake, vivyo hivyo utaondoka katika haya maisha akiwa uchi.
Ecclesiastes 5:19-20
Kwa nini mtu hakumbuki mara kwa mara siku za maisha yake?
Mtu hakumbuki mara kwa mara siku za maisha yake kwa sababu Mungu anamfanya kuhangaika na vitu anavyofurahi kufanya.
Ecclesiastes 6
Ecclesiastes 6:1-2
Mwalimu aliona uovu gani?
Mwalimu aliona kuwa Mungu anaweza kugawa utajiri, mali, na heshima kwa mtu ili asipongukiwe kitu chochote anachotamani, lakini Mungu anamnyima uwezo wa kufurahia. Badala yake, mtu mwingine anatumia vitu vyake.
Ecclesiastes 6:3-4
Kama moyo wa mtu hauridhiki na mema na hazikwi kwa heshima, nani yu bora zaidi yake?
Kama moyo wa mtu hauridhiki na mema na hazikwi kwa heshima, basi mtoto aliyezaliwa mfu ni bora zaidi yake.
Ecclesiastes 6:5-6
Kama mtu akiishi miaka elfu mbili na hajifunzi kufurahia vitu vizuri, anaenda wapi?
Hata kama mtu aishi miaka elfu mbili lakini hajifunzi kufurahia vitu vizuri, yeye huenda sehemu sawa na wengine wote.
Ecclesiastes 6:7-8
Ingawa kazi yote ya binadamu ni kujaza mdoma wake, nini hutokea?
Ingawa kazi yote ya binadamu ni kujaza mdoma wake, lakini hamu yake haishibi.
Ecclesiastes 6:9-12
Nini hutokea pale ambapo maneno zaidi yakizungumzwa?
Maneno zaidi yakizungumzwa, ndivyo ubatili huongezeka.
Ecclesiastes 7
Ecclesiastes 7:1-2
Kwa nini ni bora kwenda kwenye nyumba ya maombolezo kuliko nyumba ya karamu?
Ni bora kwenda kwenye nyumba ya maombolezo kuliko nyumba ya karamu kwa sababu maombolezo yanakuja kwa kila mtu mwisho wa maisha.
Ecclesiastes 7:3-4
Moyo wa myenye hekima uko wapi?
Moyo wa myenye hekima uko katika nyumba ya maombolezo.
Ecclesiastes 7:5-6
Kicheko cha wapumbavu ni kama nini?
Ni kama mlio wa miiba chini ya chungu, ndivyo kilivyo kicheko cha wapumbavu.
Ecclesiastes 7:7
Nini humfanya mtu mwenye hekima kuwa mpumbavu?
Unyang'anyi humfanya mtu mwenye hekima kuwa mpumbavu.
Ecclesiastes 7:8-10
Kwa nini watu wasiwe na haraka ya kukasirika kwenye nafsi zao?
Watu hawapaswi kuwa na haraka ya kukasirika katika nafsi zao kwa sababu hasira hukaa katika mioyo ya wapumbavu.
Ecclesiastes 7:11-13
Kwa nini hekima ni bora kuliko fedha?
Hekima hutoa ulinzi kama fedha inavyoweza kutoa ulinzi, lakini faidi ya maarifa ni kwamba hekima humpa uhai yeyote aliye nayo.
Ecclesiastes 7:14
Wakati nyakati ni nzuri, watu wanapaswa kuishije?
Wakati nyakati ni nzuri, wanapaswa kuishi kwa furaha katika uzuri huo.
Ecclesiastes 7:15-16
Nini kilitokea kwa watu waovu kulinga na Mwalimu alivyoona?
Mwalimu aliona watu waovu wakiishi maisha marefu licha ya uovu wao.
Ecclesiastes 7:17-20
Nini kitatokea kwa mtu amchaye Mungu?
Mtu amchaye Mungu anakutana na wajibu wake wote.
Ecclesiastes 7:21-22
Kwa nini watu hawapaswi kusikiliza kila neno linalo zungumzwa?
Watu hawapaswi kusikiliza kila neno linalo zungumzwa kwa sababu wanaweza kusikia watumishi wao wakiwalaani.
Ecclesiastes 7:23-25
Iko wapi hekima?
Hekima iko mbali.
Ecclesiastes 7:26
Mwenye dhambi atachukuliwa na nani?
Mwenye dhambi atachukuliwa na mwanamke ambaye moyo wake umejaamitego na nyavu, na ambaye mikono yake ni minyororo.
Ecclesiastes 7:27-29
Ingawa Mwalimu alipata mwanamme mmoja mwenye haki kati ya watu elfu moja, ni kitu gani ambacho hakupata?
Ingawa Mwalimu alipata mwanamme mmoja mwenye haki kati ya wanaume elfu moja, hakupata mwanamke miongoni mwao.
Ecclesiastes 8
Ecclesiastes 8:1
Mtu mwenye hekima ni nani?
Mtu mwenye hekima ni yule anayejua maana ya matukio maishani.
Ecclesiastes 8:2-4
Kwa nini watu hawapaswi kuharikisha kutoka katika uwepo wa mfalme, na kutotetea jambo lisilofaa?
Watu hawapaswi kuharikisha kutoka katika uwepo wa mfalme, na kutotete jambo lisilofaa kwa sababu mfalme anafanya kila anachotamani.
Ecclesiastes 8:5-7
Nani hukwepa madhara?
Yule anayetii amri ya mfalme anayekwepa madhara.
Ecclesiastes 8:8-9
Ni kitu gani ambacho hakuna aliye na mamlaka?
Hakuna aliye na mamlaka juu ya pumzi ya uhai kuizuia kupumua, na hakuna aliye na mamlaka juu ya siku yake ya kufa.
Ecclesiastes 8:10-11
Waovu walisifiwa na nani?
waovu walisifiwa na watu katika mji ambapo walifanya maovu yao.
Ecclesiastes 8:12-13
Kama mwenye dhambi akifanya uovu mara mia na bado akaishi muda mrefu, nini kitatokea kwa wale wanaomheshimu Mungu?
Kama mwenye dhambi akifanya uovu mara mia na bado akaishi muda mrefu, itakuwa vyema na wale wanaomheshimu Mungu, wanaoheshimu uwepo wake pamoja nao.
Ecclesiastes 8:14-15
Kwa nini Mwalimu anapendekeza furaha?
Malimu anapendekeza furaha kwa sababu mtu hana kilicho bora chini ya jua zaidi ya kula na kunywa na kuwa na furaha.
Ecclesiastes 8:16-17
Mtu hawezi kuelewa nini?
Mtu hawezi kuelewa kazi inayofanyika chini ya jua.
Ecclesiastes 9
Ecclesiastes 9:1
Nani yuko katika mikono ya Mungu?
Watu wenye haki na hekima wote wamo mikononi mwa Mungu.
Ecclesiastes 9:2
Ni kiko sawa kwa kila mtu.
Kila mtu ana uhakika mmoja.
Ecclesiastes 9:3
Mioyo ya binadamu imejaa nini?
Mioyo ya binadamu imejaa uovu.
Ecclesiastes 9:4-5
Kwa nini wafu hawana tena dhawabu?
Hawana tena dhawabu kwa sababu kumbukumbu yao imesahaulika.
Ecclesiastes 9:6-8
Nini kilipotea zamani?
Upendo,chukina wivu wa walio kufa umepotea zamani.
Ecclesiastes 9:9-10
Watu wafanye nini na kila ambacho mikono yao itapata kufanya?
Kile ambacho mikono yao itapata kufanya, wanapaswa kufanya kwa nguvu zao zote.
Ecclesiastes 9:11-12
Binadamu wamefungwa na nini?
Binadamu wamefungwa na nyakati za uovu ambazo zinawakuta ghafla.
Ecclesiastes 9:13-16
Nini kilitokea kwa mtu masikini mwenye hekima ambaye kwa hekima yake aliuokoa mji?
Hakuna aliyemkumbuka mtu masikini mwenye hekima ambaye kwa hekima yake aliuokoa mji.
Ecclesiastes 9:17-18
Ni nini bora zaidi ya silaha za vita?
hekima ni bora kuliko silaha za vita.
Ecclesiastes 10
Ecclesiastes 10:1-4
Nini hudhibitisha kwa kila mmoja kuwa mtu ni mpumbavu?
Pale ambapo kufikiri kwa mtu kuna upungufu, hii inadhibitisha kwa kila mtu kuwa ni mpumbavu.
Ecclesiastes 10:5-7
Mwalimu aliona watumwa akifanya nini?
Mwalimu aliona watumwa wakipanda farasi.
Ecclesiastes 10:8-9
Nini huweza kutokea wakati mtu akivunja ukuta?
Pale mtu anapovunja ukuta,nyoka anaweza kumng'ata.
Ecclesiastes 10:10-12
Nini hutokea kama mtu hanoi bapa la chuma butu?
Kama mtu hanoi bapa butu la chuma, basi lazima atumie nguvu zaidi.
Ecclesiastes 10:13-15
Mwishoni, mdomo wa mpumbavu unatiririka nini?
Mwishoni, mdomo wampumbavu unatiririka uovu na wazimu.
Ecclesiastes 10:16-17
Ni lini kuna tabu katika nchi?
Kuna tabu katika nchi kama mfalme ni kijana na viongozi wakianza karamu asubuhi!
Ecclesiastes 10:18-19
Kwa nini nyumba inavuja?
Kwa sababu ya mikono isiyo fanya kazi nyumba huvuja.
Ecclesiastes 10:20
Kwa nini watu hawapaswi kumlaani mfalme?
Watu hawapaswi kumlaani mfalme kwa sababu ndege wa angani anaweza kubeba maneno yao.
Ecclesiastes 11
Ecclesiastes 11:1-5
Kwa nini watu wanapaswa kugawana mkate na watu saba, hata watu wanane.
Watu wanapaswa kugawana na watu saba, hata watu wanane kwa kuwa hawajui ni majanga gani yanakuja duniani.
Ecclesiastes 11:6-8
Watu wanatakiwa kupanda mbegu kwa muda gani?
Watu wanapaswa kupanda mbegu asubuhi hadi jioni.
Ecclesiastes 11:9-10
Watu wanapaswa kuondoa nini mioyoni mwao?
Watu wanapaswa kuondoa hasira mioyoni mwao.
Ecclesiastes 12
Ecclesiastes 12:1-2
Watu wanatakiwa kumkumbuka Muumbaji wao wakati gani?
Watu wanatakiwa kumkumbuka Muumbaji wao katika siku za ujana wao.
Ecclesiastes 12:3
Kwa nini wanawake wanao saga watakoma?
Wanawake wanao saga watakoma kwa sababu watakuwa wachache.
Ecclesiastes 12:4-5
Wanaume watashtuliwa na nini?
Wanaume watashtuliwa na sauti ya ndege.
Ecclesiastes 12:6-7
Vumbi itarudi wapi?
Vumbi itarudi ardhini ambapo imetokea.
Ecclesiastes 12:8-9
Mwalimu aliwafundisha nini watu?
Mwalimu aliwafundisha watu maarifa.
Ecclesiastes 12:10-11
Maneno ya mwenye hekima ni kama nini?
Maneno yamwenye hekima ni kama fimbo ya kuchungia ng'ombe.
Ecclesiastes 12:12
Kusoma kwingi kunaleta nini?
Kusoma kwingi kunaleta uchovu mwilini.
Ecclesiastes 12:13-14
Ni nini mwisho wa jambo?
Mwisho wa jambo ni kwamba watu wanatakiwa kumcha Mungu na kutunza amri zake.