Kiswahili: translationQuestions

Updated ? hours ago # views See on DCS Draft Material

Lamentations

Lamentations 1

Lamentations 1:1-2

Mji wa Yerusalemu umekuwa kuwa kama nini japo awali ailkuwa mji wenye nguvu?

Amekuwa kama mjane.

Lamentations 1:3

Yuda ana shindwa kupata nini japo anaishi miongoni mwa mataifa?

Yuda hapati pumziko japo anaishi miongoni mwa mataifa.

Lamentations 1:4-5

Kwanini Yahweh ameuadhibu mji wa Yerusalemu?

Yahweh ameudhabibu mji wa Yerusalemu kwasababu ya dhambi zake nyingi.

Lamentations 1:6

Nini kilicho mwacha binti wa Sayuni?

Uzuri umemwacha binti wa Sayuni

Lamentations 1:7

Nini ambacho Yerusalemu alikuwa nacho siku za awali ambacho sasa ana kumbuka?

Yerusalemu inakumbuka hazina zake za dhamani alizo kuwa nazo awali

Lamentations 1:8-9

Kwasababu Yerusalemu ili tenda dhambi vikubwa, amakuwa kama nini?

Yerusalemu amedhalillika kama kitu kichafu.

Lamentations 1:10

Nini Yerusalemu imeona ikiingia pahali pa takatifu japo Yahweh aliamuru kisiingie?

Ameona mataifa yakiingia sehemu yake takatifu

Lamentations 1:11-12

Watu wanafanya nini wanapo tafuta mkate?

Watu wote wana sononeka wanapo tafuta mkate.

Lamentations 1:13-14

Yahweh ametandaza nini mbele ya miguu ya Yerusalemu ili kumgeuza?

Ametanda nyavu kwa miguu ya Yerusalemu.

Nini kimeshindikana kwasababu ya nira ya makosa ya Yerusalemu ambayo vimefungwa pamoja shingoni mwake?

Uweza wa Yerusalemu umeshindwa kwasababu ya nira ya makosa ya Yerusalemu ambayo vimefungwa pamoja shingoni mwake.

Lamentations 1:15

Bwana amemganyaga bikra wa binti wa Yerusalemu kama nini?

Bwana amewakanyaga binti bikra wa Yuda kwenye chombo cha kusagia mvinyo

Lamentations 1:16-17

Kwanini watoto wa Yerusalemu wamekuwa ukiwa?

Watoto wa Yerusalemu wamekuwa ukiwa kwasababu adui ameshinda.

Lamentations 1:18-19

Nani ameenda matekani kwasababu Yerusalemu imeasi dhidi ya amri za Yahweh?

Mabikra na wanaume imara wa Yerusalemu wameenda matekani.

Nani aliye anguka katika mji walipo kuwa wakitafuta chakula kurjesha uhai wao?

Makuhani na wazee wa Yerusalemu waliangamia kwenye mji.

Lamentations 1:20

Nini kimegeuzwa ndani ya Yerusalemu kwasababu ameasi vikubwa?

Moyo wa Yerusalemu umegeuzwa ndani yake.

Lamentations 1:21-22

Nini maadui wa Yerusalemu wanafanya wanapo sikia majanga?

Maadui wa Yerusalemu wana furahia.

Yerusalemu ina muomba Yahweh afanye nini kwa maadui zake wanapo kwa Yahweh?

Yerusalemu anaomba kwamba Yahweh awaadhibu maadui zake kama Yahweh alivyo muadhibu kwa makosa yake yote.

Lamentations 2

Lamentations 2:1-2

Bwana anaonyeshaje hasira yake kwasababu ya uasi wa Yeremia?

Ametupa utukufu wa Israeli, hajawa na huruma kwa miji yote ya Yakobo, ameangusha miji imara ya binti wa Yuda.

Lamentations 2:3-4

Jinsi gani hasira yake inadhuru Israeli na Sayuni?

Bwana ameondoa uweza wote wa Israeli na kumwaga gadhabu yake kwa Sayuni.

Lamentations 2:5-6

Hasira ya Bwana inaonyeshwaje?

Bwana amekuwa kama adui, Ameharibu sehemu ya kukusanyikia, amemdharau mfalme na kuhani.

Lamentations 2:7

Kwanini adui anaonekana mshindi?

Wana jisikia washindi kwasababu Bwana amekataa madhabahu yake na kuwapa kuta za majumba maadui.

Lamentations 2:8-9

Nini kimetokea kwa malango na nguzo za Sayuni?

Malango yake yameanguka chini, ameharibu na kuvunja chuma za ukuta.

Lamentations 2:10

Wazee na mabikra wanonyeshaje wana uzuni?

Wazee wameketi chini, Wamerusha vumbi kichwani mwao na kuvaa magunia. Mabikra wameinamisha vichwa vyao chini.

Lamentations 2:11-14

Kwanini Yeremia anaomboleza?

Kwasababu hakuna kitu kwa watu wake cha kula au kunywa.

Lamentations 2:15-17

Wadhihaki wanafanya nini wanapo pita kwenye mji?

Wana piga makofi kwako, wanaguna na kutikisa vichwa vyao, wanapiga mruzi na kusaga meno yao.

Lamentations 2:18-19

Watu wanaonyeshaje toba yao?

Wanalia kwa Bwana na kuinua mikono yao kwake kwa ajili ya watoto wao.

Lamentations 2:20

Kwanini watu wanaomba rehema za Yahweh?

Kwa kuwa amewatendea kwa ukali sana, wana njaa, wana wasiwasi juu ya makuhani wao kuchinjwa.

Lamentations 2:21-22

Yeremia anaelezeaje siku ya gadhabu ya Yahweh?

Siku ya gadhabu ya Yahweh, Yahweh aliua wadogo kwa wakubwa, hakuna aliye pona, na hakuonyesha huruma.

Lamentations 3

Lamentations 3:1-4

Mwandishi anasema Yahweh amemgeuzia nini siku nzima?

Mkono wa Yahweh umegeuzwa dhidi yake siku nzima.

Lamentations 3:5-8

Mwandishi anasema Yahweh amejenga nini kumzunguka ili asitoroke?

Yahweh amejenga ukuta.

Lamentations 3:9-11

Mnyama gani ambaye mwandishi anamlinganisha na Yahweh na kusema anasubiri amshambulie?

Mwandishi anaelezea Yahweh kama dubu anaye subiri kumshambulia.

Lamentations 3:12-15

Mwandishi amekuwa nini kwa watu wake?

Mwandishi amekuwa kichekesho kwa watu wake wote.

Lamentations 3:16-18

Mwandishi hawezi kukumbuka nini tena tangu Yahweh ameondoa amani kutoka maishani mwake?

Mwandishi hakumbuki furaha tena.

Lamentations 3:19-21

Hali ya mwandishi ikoje anapo kumbuka mateso yake?

Hali ya mwandishi haina matumaini tena anapo kumbuka mateso.

Lamentations 3:22-24

Mwandishi anasema nini kinatokea kila asubui?

Mwandishi anasema matendo ya rehema yanatokea kila asubui.

Lamentations 3:25-29

Yahweh yupo kama nani kwa yeye anaye msubiri na kwe yeye anaye subiri taratibu wakovu wa Yahweh?

Yahweh ni mwema kwao wanao msubiri, na kusubiri taratibu wakovu wa Yahweh.

Mtu anapaswa kuketije kwasababu Yahweh amemuekea juu yake?

Mtu aketi peke yake na kusubiri kwasababu Yahweh ameweka juu yake.

Lamentations 3:30-36

Yahweh anaonyesha nini, japo analeta uzuni?

Yahweh anaonyesha huruma japo analeta uzuni.

Kutoka wapi ambapo Yahweh hawaadhibu au kuwatesa watoto wa wanadamu?

Yahweh hatesi kutoka moyoni mwake au kuwaadhibu watoto wa wanadamu.

Lamentations 3:37-39

Vitu gani viwili vinatoka kwenye kinywa cha Yahweh?

majanga na mazuri yanakuja kutoka kwenye kinywa chake Aliye Juu.

Lamentations 3:40-43

Watu wainue nini kwa Mungu aliye mbinguni wanapo pima na kujaribu njia zao na kugeuka kwa Yahweh?

Watu wanyanyue mioyo yao na mikono yao kwa Mungu mbinguni.

Watu wakiri nini wamefanya dhidi ya Yahweh wanapo omba?

Wakiri wametenda dhambi na kuasi dhidi ya Yahweh.

Lamentations 3:44-47

Mwandishi anasema Yahweh amewafanya kuwa miongoni mwa watu?

Yahweh amewafanya wawe uchafu miongoni mwa watu.

Lamentations 3:48-50

Mwandishi anaelezeaje machozi yanayo toka machoni mwake?

Machozi yake ni mifereji ya maji yanayo toka machoni mwake.

Lamentations 3:51-54

Jinsi gani mwandishi anasema maadui zake wanapo mtafuta na kuharibu maisha yake katika kisima na kuweka jiwe juu yake?

Anasema, "Nimekatwa mbali"

Lamentations 3:55-57

Yahweh alimwambiaje mwandishi alipo liitijia jina la Yahweh na kumuomba Yahweh kusikia kilio chake?

Yahweh alimwambia, "Usiogope"

Lamentations 3:58-61

Mwanishi anamuombaje Yahweh ahukumu kesi yake?

Anamuomba Yahweh ahukumu kesi yake kwa haki.

Lamentations 3:62-63

Mwandishi ni kitu gani kwa maadui wake, katika kuketi kwao au kuinuka kwao?

Ni kitu cha nyimbo yao dhihaka.

Lamentations 3:64-66

Mwandishi anamuomba Yahweh afanye nini kwa maadui zake?

Anamuomba Yahweh alipize kwa kadiri ya waliyo fanya kama mikono yao ilivyo fanya.

Lamentations 4

Lamentations 4:1-2

Nini kimekuwa kwa dhahabu na mawe matakatifu?

Dhahabu imechakaa, dhahabu safi imebadilika na mawe matakatifu yamezagaa katika kila njia ya mtaa.

Wana wa Sayuni walikuwa ni nani, na sasa wana thaminiwaje?

Wana wa Sayuni walikuwa na thamani, walikuwa na thamani ya uzito wa dhahabu safi, akini sasa hawana thamani zaidi ya majagi ya udogo, kazi ya mikono ya mfinyazi.

Lamentations 4:3

Mabinti wa watu wake wana tendaje?

Wamekuwa wa katili, kama mbuni katika jangwa.

Lamentations 4:4-5

Nini kinatokea kwa ulimi wa mtoto anaye nyonya na watoto wanaomba nini?

Ulimi wa mtoto mchanga anaye nyonya unagota juu mdomo wake kwa kiu na watoto wanaomba mkate, lakini hakuna kwa ajili yao.

Nini kimewatokea wao walio kuwa wana kula chakula cha gharama na wao walio vaa nguo za gharama?

Wao walizoea kula chakula cha gharama sasa wana shinda njaa mitaani; wao walio lelewa kwa kuvaa nguo za zambarau, sasa wamelala katika majalala.

Lamentations 4:6

Jinsi gani dhambi ilivyo kubwa ya binti wa watu wake?

Dhambi ya binti wa watu wangu ni kubwa kuliko hiyo ya Sodoma.

Lamentations 4:7-8

Viongozi walikuwaje awali, na sasa wakoje?

Viongozi wake walikuwa wasafi kuliko theluji, weupe kuliko maziwa; miili yao ilikuwa imara kuliko jiwe, mwili wao ulikuwa kama yakuti samawi. 8Muonekano wao umekuwa mweusi kama giza; hawatambuliki mitaani. Ngozi zao zimesinya kwenye mifupa yao; imekuwa kavu kama kuni.

Lamentations 4:9-10

Yeremia anasema nini kuhusu hao waliyo uliwa kwa njaa ukilinganisha na hao waliyo uliwa kwa upanga?

Yeremia hao waliyo uliwa kwa upanga ni bora kuliko hao waliyo uliwa kwa njaa.

Wanawake wenye huruma walifanya nini kwa watoto wao?

Waliwachemsha watoto wao na watoto wakawa chakula chao.

Lamentations 4:11

Yahweh aliridhishaje hasira yake?

Yahweh alionyesha gadhabu yake yote; alimwaga hasira yake kali, aliwasha moto Sayuni uliteketeza misingi yake.

Lamentations 4:12-13

Wafalme na wakazi wa ulimwengu hawaku amini nini kingeweza kutokea kwa Yerusalemu?

Hawaku amini kuwa adui angeweza kuingia malangoni mwa Yerusalemu.

Nini adui alifanya kwasababu ya dhambi za manabii na makosa ya makuhani?

Adui aliingia malangoni mwa Yerusalemu.

Lamentations 4:14-15

Nini kiliwatokea manabii na makuhani?

Walitanga, kwa upofu, mitaani. Walikuwa wamejitia unajisi kwa damu hiyo ambapo hakuna aliye ruhusiwa kushika nguo zao.

Nini manabii na makuhani alikililia kwa sauti?

Manabii na makuhani walilia na kusema wakimbie na wasiwaguse.

Wapi manabii na makuhani walienda?

Walitanga kwenye nchi ambazo mataifa walisema hawawezi ishi tena hapo.

Lamentations 4:16

Nini Yahweh alifanya kwa manabii na makuhani?

Yahweh mwenyewe akawatawanyisha manabii na makuhani na hawaonyeshi upendeleo kwa wazee.

Makuhani wanapokelewaje na wazee wanapokelewaje?

Makuhani hawaheshimu tena na wazee hawaonyeshwi kujaliwa.

Lamentations 4:17-18

Nini kilikosa kupata msaada?

Macho yao yalikwama kupata msaada.

Adui aliwafanya nini?

Walifuata hatua zao walipo enda mitaani.

Nini watu walisema kuhusu mwisho wao?

Mwisho wO ulikuwa karibu na siku zo zilihesabiwa, mwisho wetu ulifika.

Lamentations 4:19-20

Jinsi gani watu walielezea waliyo wakimbiza, na waliyo wakimbiza waliwafanyaje?

Walio wakimbiza walikuwa wepesi kuliko tai na kuwa kimbiza kwenye milima na kutuwinda nyikani.

Nini kilitokea kwa mfalme wao?

Mfalme alikamatwa katika shimo la adui.

Lamentations 4:21-22

Kwanini binti wa Edomu aliambiwa afurahi?

Aliambiwa kikombe kitapitishwa; utalewa na kuvua nguo.

Nini binti wa Sayuni aliambiwa?

Aliambiwa hukumu yake imefika mwisho na Yahweh na Yahweh atamuacha matekani.

Nini aliambiwa binti wa Edomu?

Binti wa Edomu aliambiwa Yahweh ata muadhibu hatia yake na kufunika dhambi zake.

Lamentations 5

Lamentations 5:1-4

Nini Yeremia anamuomba Yahweh afanye?

Yeremia anamuomba Yahweh kukumbuka kilicho watokea na kuona aibu yao.

Nini Yeremia ana muambia Yahweh kimetokea kwa urithi wao?

Yeremia ana mwambia Yahweh kwamba umegeuziwa kwa wageni, na nyumba zao kwa mataifa.

Lamentations 5:5-7

Jinsi gani Yeremia anavyo eleza kinacho watokea?

Maadui wao wana wakimbiza, wamechoka, na wamewaomba Wamisri na Waasiria kwa ajili ya chakula.

Watu wanasemaje kuhusu dhambi?

Wanasema baba zao wametenda dhambi na wanabeba dhambi za baba zao.

Lamentations 5:8-10

Watu wanasemaje kuhusu watumwa?

Watu wanasema watumwa wana watawala na hakuna wakuwaokoa.

Wana jielezeaje wanapo enda nje kuchukuwa mkate?

Wana pata mkate wanapo hatarisha maisha katika uso wa upanga wa nyikani.

Wanaelezeaje ngozi yao?

Ngozi yao ni kama jiko limechomeka kwa ukame.

Lamentations 5:11-12

Nini kimewatokea wanawake na mabikra?

Wanawake wanabakwa Sayuni, na mabikra katika mji wa Yuda.

Nini kimewatokea watoto wa wafalme na wazee?

Watoto wa mfalme wamenyongwa na mikono yao, na hakuna heshima inayoonyeshwa kwa wazee.

Lamentations 5:13-14

Nini kimewatokea wanaume imara na wanaume vijana?

Wanaume imara waliletwa kusaga mbegu kwa jiwe la kusagia, na wavulana wanajikwa chini ya vifurushi vya kuni.

Nini kiliwatokea wazee na wanaume imara?

Wazee wameacha lango la mji, na vijana wameacha miziki.

Lamentations 5:15-16

Jinsi gani wanaelezea furaha ya moyo wao, michezo yao, na taji lao?

Furaha ya moyo imekoma na kucheza kwetu kumegeuka kilio, na taji limeanguka kutoka kichwani mwao.

Lamentations 5:17-18

Wanasema nini kuhusu mioyo na macho yao?

Mioyo yao imekuwa ikiumwa na macho yao yamefifia.

Lamentations 5:19-22

Wanasemaje kuhusu utawala wa Yahweh na kiti chake cha enzi?

Yahweh anatawala milele na kiti chake cha enzi ni cha vizazi na vizazi.

Nini wanamuomba Yahweh afanye?

Wanamuomba Yahweh kama ana wasahau milele, na kama watamrudia.