Kiswahili: translationQuestions

Updated ? hours ago # views See on DCS Draft Material

Jonah

Jonah 1

Jonah 1:1-3

Bwana alimuamulu nini Yona kwenda na kufanya?

Bwana akamwamuru Yona kwenda Ninawi na kusema juu yake.

Yona alifanya nini baasa ya kusikia amri ya Bwana?

Yona alikimbia mbali na uwepo wa Bwana na kwenda Tarshishi

Jonah 1:4-5

Bwana aliifanya nini Meli aliyokuwa amepanda Yona?

Bwana alituma mawimbi makubwa baharini na ikaonekana kwamba meli ilitaka kuvunjika.

Mabaharia walifanya nini katikati ya upepo mkali?

baharini waliogopa sana na kila mtu alilia kwa mungu wake mwenyewe.

Jonah 1:6-7

Mabaharia walifanya nini kumtambua aliyekuwa sababu ya uovu, na matokeo yake ilikuwa nini?

Mabaharia walipiga kura ili kuamua nani ndiye sababu, na kura hiyo ilimuonyesha Yona.

Jonah 1:8-10

Yona alisema nini ilikuwa sababu ya uovu uliokuwa unawatokea?

Yona akawaambia watu kwamba alikuwa akikimbia kutoka mbele ya Bwana.

Jonah 1:11-13

Yona aliwaambia watu wafanye nini ili kuzuia dhoruba?

Yona akawaambia watu wamtupe baharini ili kuzuia dhoruba.

Jonah 1:14-16

Je, ni maombi gani mawili waliyoomba mabaharia kwa Bwana?

Walimwomba Bwana asiwaache waangamie, na kuwashtaki kwa sababu ya kifo cha Yona.

Nini kilichotokea wakati mabahari walipomtupa Yona ndani ya bahari?

Walipomtupa Yona ndani ya baharini, bahari iliacha ukali.

Jonah 1:17

Nini kilitokea baada ya Yona kutupwa baharini?

Samaki mkubwa alimmeza Yona, na alikuwa ndani ya tumbo la samaki kwa siku tatu.

Jonah 2

Jonah 2:1-2

Yona alifanya nini akiwa tumboni mwa samaki?

Yona alimuita Bwana amsaidie?

Jonah 2:3-4

Yona alifikiri kuwa hawezi kufanya nini tena?

Yona alidhani hawezi kamwe kuona hekalu takatifu la Bwana tena.

Jonah 2:5-6

Bwana alileta uhai wa Yona kutoka wapi?

Bwana akauleta uhai wa Yona kutoka shimoni.

Jonah 2:7-8

Ni nini kinachotokea kwa wale wanaozingatia miungu isiyofaa

Wale wanaozingatia miungu isiyofaa hukataa uaminifu wa Bwana kwao.

Jonah 2:9-10

Yona alifanya ahadi gani kutoka tumbo la samaki?

Yona aliahidi kutimiza yale aliyoahidi.

Kutoka wapi Yona alisema kuwa wokovu unakuja?

Yona alisema kwamba wokovu unakuja kutoka kwa Bwana.

Bwana alimuambia samaki kufanya nini?

Bwana aliwaambia samaki kumtapika Yona juu ya nchi kavu.

Jonah 3

Jonah 3:1-3

Ni amri gani ambayo Bwana alimpa Yona kwa mara ya pili?

Bwana alimuamuru Yona kwenda Ninawi na kuhubiri ujumbe wa Bwana.

Kwa namna gani Yona alikubari amri ya Bwana wakati huu?

Yona alitii na kwenda Ninawi.

Jonah 3:4-7

Ni ujumbe gani ambao Yona aliuhubiri Ninawi?

Yona alihubiri kwamba katika siku arobaini Ninawi itakuwa kwenye matatizo

Jonah 3:8-9

Watu wa Ninawi waliitikiaje ujumbe wa Bwana ambao Yona alihubiri?

Watu wa Ninawi walifunga na kuvaa magunia, wakageuka njia zao mbaya, wakalia kwa Mungu.

Ni matumaini gani mfalme wa Ninive alivyokuwa nayo kwa ajili ya watu na mji?

Mfalme wa Ninive bado alikuwa na matumaini ya kwamba Mungu anaweza kuacha ghadhabu yake kali.

Jonah 3:10

Kwa jinsi gani Mungu alikubali toba ya watu wa Ninawi?

Mungu alibadili mawazo yake juu ya adhabu ambayo alikuwa amesema angewafanyia na hakufanya hivyo.

Jonah 4

Jonah 4:1-3

Ni nini kilichoonekana kibaya sana kwa Yona?

Ilionekana kuwa mbaya kwa Yona kwamba Bwana alibadili mawazo yake na hakuwaadhibu watu wa Ninawi.

Kwa nini Yona alisema kuwa alikuwa amejaribu kukimbilia Tarshishi?

Yona alisema alijua kwamba Bwana alikuwa mwenye huruma, mwenye huruma, asi mwepesi wa hasira, mwingi wa fadhili, na anayemkabiliana na kutuma maafa.

Nini ambacho Yona alitaka Bwana amtendee?

Yona alitaka Bwana achukue uhai wake.

Jonah 4:4-5

Swali gani Bwana alimwuliza Yona?

Bwana akamwuliza Yona ikiwa ni vizuri kwamba alikuwa mwenye hasira.

Kwa nini Yona alienda nje ya mji na kukaa chini?

Yona alitaka kuona nini kitatokea kwa mji.

Jonah 4:6-7

Nini ambacho Bwana alifanya kwa Yona alipotoka nje ya mji?

Bwana aliandaa kivuli cha mti kwaajiri yake, kisha mdudu akauangamiza siku ya pili, na kisha akandaa upepo mkali wa mashariki kumfanya Yona aanguke.

Jonah 4:8-9

Swali gani ambalo Bwana alimuuliza Yona?

Bwana alimuuliza Yona kama ni vema yeye kuwa na hasira juu ya mmea.

Jonah 4:10-11

Yona alihisije juu ya kivuli cha mmea ?

Yona aliuhurumia mmea.

Kwa nini Bwana aliwahurumia?

Bwana alikuwa na huruma kwa watu wa Ninawi na ng'ombe.