Kiswahili: translationQuestions

Updated ? hours ago # views See on DCS Draft Material

Micah

Micah 1

Micah 1:1

Ni akina nani walikuwa wafalme wa Yuda wakati neno la Yahwe lilipomjia Mika?

Yotahamu, Ahazi, na Hezekia walikuwa wafalme wa Yuda wakati neno la Yahwe lilipomjia Mika.

Micah 1:2-4

Kwa namna gani Yahwe atashuka na kupakanyaga?

Yahwe atashuka chini na kukanyaga kwenye madhabahu ya wapagani juu ya nchi.

Micah 1:5

Kwa nini Yahwe ataileta hii hukumu?

Yahwe ataileta hii hukumu kwa sababu ya uasi wa Yakobo, na kwa sababu ya dhambi za nyumba ya Israeli

Micah 1:6-7

Je! Ni jinsi gani Samaria ilivyokusanya picha zilizochongwa, zawadi, na sanamu?

Samaria ilikusanya picha za kuchongwa, zawadi, na sanamu kutoka zawadi kwenda kwa ukahaba wake.

Micah 1:8-10

Je! ni jinsi gani Mika anaeleza huzuni juu ya dhambi ya Israeli na Yakobo?

Mika alilia na kuomboleza, na kwenda peku na uchi.

Micah 1:11-12

Kwa nini Beth Ezeli aliomboleza?

Beth ezeli aliomboleza, kwa ajili ya ulinzi wao ulikuwa umechukuliwa.

Micah 1:13-14

Ni Mji gani ulikuwa chanzo cha dhambi kwa ya binti wa Sayuni?

Lakishi ulikuwa chanzo cha dhambi kwa binti wa Sayuni.

Micah 1:15-16

Kwa nini Waisraeli walitakiwa kunyoa vichwa vyao?

Walitakiwa kunyoa vichwa vyao, kwa ajili ya watoto wao watakaokwenda utumwani kutoka kwao.

Micah 2

Micah 2:1-2

Ni wapi watu wanapanga kufanya uovu?

Wanapanga kufanya uovu juu ya vitanda vyao.

Micah 2:3-5

Kwa nini watu matajiri hawana ukoo kugawanya eneo?

Yahwe atalibadilisha eneo la watu, na kuliondoa kutoka kwao. Hivyo watu matajiri hawatakuwa na ukoo kuligawanya eneo.

Micah 2:6-8

Je! Ni kutoka kwa nani watu wa Yahwe watavua joho?

Wamelivua vazi kutoka wale ambao wapitao karibu na wasioshutumiwa.

Micah 2:9-11

Kwa nini watu wa Yahwe watainuka na kuondoka?

Watainuka na kuondoka kwa kuwa hii haikuwa sehemu ambayo wangeweza kuishi, kwa sababu ya unajisi wake.

Micah 2:12-13

Je! Ni nani atawakusanya mabaki ya Israeli?

Yahwe atawakusanya mabaki ya Israeli.

Micah 3

Micah 3:1-3

Je! Ni nani alaye nyama ya watu wa Yahwe?

Wakuu wa Yakobo hula nyama ya watu wa Yahwe.

Micah 3:4

Kwa nini Yahwe atauficha uso wake kutoka kwa wakuu wa yakobo?

Yahwe atauficha uso wake kutoka kwa wakuu wa Yakobo kwa sababu wamefanya matendo maovu.

Micah 3:5-8

Je! Kwa nini manabii hawawezi kubashiri?

Itakuwa giza ili kwamba manabii wafanye utabiri

Micah 3:9-12

Je! Kwa ajili gani wakuu wanahukumu?

Wakuu wanahukumu kwa ajili ya rushwa.

Micah 4

Micah 4:1

Ni lini mlima wa nyumba ya Yahwe utaimarishwa juu ya milima?

Katika siku za mwisho mlima wa Yahwe utaimarishwa juu ya milima mingine.

Micah 4:2-3

Kwa nini mataifa mengi yatataka kwenda kwenye mlima wa Yahwe?

Mataifa mengi yatataka kwenda kwenye mlima wa Yahwe, hivyo atawafundisha njia zake, na watatembea katika njia zake.

Micah 4:4-5

Ni katika nini wote hutembea?

Watu wote hutembea katika jina la mungu wao

Micah 4:6-8

Yahwe asema atamkusanya nani?

Yahwe atamkusanya achechemeaye na kumkusanya aliyefukuzwa, wale ambao aliyekuwa amefukuzwa.

Micah 4:9-10

Binti Sayuni ataokoka wapi?

Binti Sayuni ataokoka katika Babeli.

Micah 4:11-12

Kutokana na nabii, ni nani ambaye hayajui mawazo ya Yahwe?

Mataifa hawayajui mawazo ya Yahwe

Micah 4:13

Kwa nani Yahwe atawaweka wakfu milki za watu wengi?

Yahwe ataziweka milki zao kwake mwenyewe.

Micah 5

Micah 5:1

Maaskari watampiga mkuu wa Israeli kwa nini?

Watampiga mkuu wa Israeli kwa fimbo kwenye shavu.

Micah 5:2-3

Je! Ni kwa mda gani Mungu ataziacha koo za Yuda?

Mungu atawaacha, hadi mda wakati yeye ambaye aliye na uchungu atakapozaa mtoto.

Micah 5:4-5

Ni nani atakaye chunga kundi lake kwa nguvu ya Yahwe?

Mwana atachunga kundi lake katika nguvu ya Yahwe.

Micah 5:6-7

Kwa ajili gani mabaki ya Yakobo hatasubiri?

Mabaki ya Yakobo hayamsubiri mtu.

Micah 5:8-11

Nini kitatokea wakati mkono wa Waisraeli utakapobakia juu ya adui zao?

Wakati mkono wa Waisraeli utakapobakia juu ya maadui zao, utawaharibu.

Micah 5:12-15

Ni juu ya nani Yahwe atalipiza kisasi?

Yahwe atalipiza kisasi juu ya mataifa ambao hakusikiliza.

Micah 6

Micah 6:1-2

Je! Yahwe atafanya nini juu ya Israeli?

Yahwe atapigana katika mahakama juu ya Israeli.

Micah 6:3-5

Yahwe aliwaamuru watu wake kufanya nini juu yake?

Aliwaamuru kushuhudia juu yake.

Micah 6:6-10

Je! Yahwe alitaka nini kutoka kwa watu wake?

Yahwe aliwataka watu wake kutenda haki, upendo, ukarimu, na kuenenda kwa unyenyekevu pamoja na Mungu wao.

Micah 6:11-12

Je! Ni ulimi wa nani mdanganyifu?

Ulimi wa wenyeji ndio umenena mdanganyifu.

Micah 6:13-15

Je! Kwa nini Yahwe ameuharibu mji?

Yahwe aliuharibika kwa sababu ya dhambi zao.

Micah 6:16

Je! Ni kwa ushauri wa nani mji ulitembea?

Mji ulitembea kwa ushauri wa Omri na Ahabu.

Micah 7

Micah 7:1-2

Je! Ni nani aliangamizwa kutoka kwenye dunia?

Mcha Mungu ameangamizwa kutoka kwenye dunia.

Micah 7:3-4

Je! ni nani aliyewajulisha siku ya Hukumu ya watu waliosalia?

Walinzi waliwaajulisha siku ya Hukumu ya watu waliobakia.

Micah 7:5-6

Je! Ni nani maaadui wa mtu?

Maadui wa mtu ni watu wa nyumba yake mwenyewe.

Micah 7:7-8

Ji! Ni nini kitatokea baada ya Mika kuanguka?

Baada ya Mika kuanguka, atainuka.

Micah 7:9

Je! Ni kwa mda gani Mika atabeba ghadhabu ya Yahwe?

Mika atabeba ghadhabu ya Yahwe hadi Yahwe atakapotoa maelezo ya kosa lake, na kutoa hukumu kwa Mika.

Micah 7:10

Je! Macho ya Mika yatatazama kwa nani?

Macho ya Mika yatatazama kwa adui yake.

Micah 7:11-13

Je! Nini kitatokea wakati siku ya itakapokuja kuzijenga kuta?

Wakati siku itakapofika ya kuzijenga kuta, mipaka itanyooshwa mbali sana.

Micah 7:14-15

Je! Mika alimuulizaje Yahwe jinsi ya kuwachunga watu wake?

Mika alimuuliza Yahwe kuwachunga watu wake kwa fimbo yake.

Je! Yahwe atawaonyesha watu wake kufanya nini?

Yahwe atawaonyesha miujiza.

Micah 7:16-17

Je! Mataifa yataona nini na kuonea aibu?

Wataona na kuonea aibu nguvu zake zote.

Je! Mataifa watakuja kwa nani na kumhofia?

Mataifa watakuja kwa Yahwe na kuogopa kwa sababu yake.

Micah 7:18

Kwa nini Yahwe hataweza kutunza hasira yake milele?

Yahwe hataweza kutunza hasira yake milele, kwa sababu anapenda kuonyesha agano lake amanifu.

Micah 7:19-20

Je! Yahwe atazitupa dhambi za watu wa Israeli kwenye nini?

Yahwe atazitupa dhambi zao kwenye vilindi vya bahari.