Nahum
Nahum 1
Nahum 1:2-3
Yahwe amejaa kitu gani?
Yahwe amejaa ghadhabu.
Yahwe atalipiza kisasi kwa nani?
Yahwe atalipiza kisasi kwa adui zake
Yahwe huifanya njia yake kwa namna gani?
Yahwe hufanya njia yake kwenye upepo wa kisulisuli na dhoruba.
Nahum 1:4-6
Nini kinatokea kwenye maua ya Lebanoni?
Maua ya Lebanoni ni dhaifu.
Nini hutokea katika dunia kwenye uwepo wa Yahwe?
Dunia huanguka mbele zake
Nahum 1:7-11
Yahwe tunaweza kumlinganisha na kitu gani katika siku ya taabu?
Yahwe ni boma katika siku ya taabu.
Yahwe atawawinda adui zake kwenye nini?
Yahwe atawawinda adui zake kwenye giza.
Nahum 1:12-13
Yahwe atafanya nini kwenye nira ya watu?
Ataivunja nira ya watu kutoka kwao.
Nahum 1:14
Kwa nini Yahwe atachimba makaburi kwa ajili ya watu wa Ninawi?
Atachimba makaburi yao kwa kuwa wao ni waovu.
Nahum 1:15
Iko wapi miguu yake ambaye analeta habari njema?
Miguu yake ambaye analeta habari njema ipo juu ya milima.
Kwa nini Yuda anapaswa kusherehekea sikukuu na kutunza nadhiri zake?
Yuda anapaswa kusherehekea sikukuu na kutunza nadhiri zake, kwa maana mwovu hatawavamia tena.
Nahum 2
Nahum 2:1-2
Yahwe anarejesha nini?
Yahwe anayarejesha majeshi ya Yakobo.
Nahum 2:3-5
Ngao za watu hodari zinarangi gani?
Ngao za watu hodari ni nyekundu.
Kuna mwendo wa namna gani katika mitaa?
Magari ya vita yanamwendo wa kasi kwenye mitaa.
Nahum 2:6-7
Agizo gani limetolewa?
Imekwisha kuagizwa: malkia amevuliwa mavazia yake na amaechukiliwa; watumishi wake wa kike wanaomboleza kama njiwa, wanavipiga vifua vyao.
Nahum 2:8-10
Watu wa Ninawi watafanya nini?
Watakimbia kama maji yanayotiririka.
Nahum 2:11-12
Simba waliogopa kitu gani?
Hawakuogopa kitu chochote.
Simba alijaza nini kwenye pango na makazi yake?
Simba lijaza pango lake mawindo na makao yake kwa mizoga.
Nahum 2:13
Yahwe atafanya nini katika Ninawi?
Yahwe tayachoma magari yao ya vita katika moshi, na upanga utateketeza simba wao vijana, na kuyaondoa mawindo yao katika nchi.
Nahum 3
Nahum 3:1-2
Mji umejaa nini?
mji umejaa damu, uongo na mali za wizi.
Nahum 3:3-4
Watu wangapi watauwawa kwa shambulio la wapanda farasi?
Kutakuwa na marundo ya maiti, mafungu makubwa ya miili ambapo hakuna ukomo wa miili.
Kwa nini mambo haya yanatokea?
Hii inatokea kwa sababu ya matendo ya tamaa ya kahaba mzuri.
Nahum 3:5-7
Yahwe wa majeshi atafanya nini dhidi ya kahaba kwa sababu yupo kinyume naye?
Yahwe ataiinua sketi yake juu ya uso wake na kuzionyesha sehemu zake za siri kwa mataifa, aibu yake kwa falme. Atarusha uchafu wa kuchukiza juu yake na kumfanya awe mbaya sana; atamfanya awe mtu wa kutazamwa na kila mmoja.
Nahum 3:8-9
Nani ambaye ukuta wake ulikuwa bahari?
Noamoni ukuta wake ulikuwa bahari.
Nahum 3:10-11
Nani alipiga kura kwa ajli ya watu wa Noamoni wenye heshima?
Maadui wa Noamoni walipiga kura kwa watu wake wenye heshima.
Nahum 3:12-15
Ni nini kitatokea kama ngome za Ninawi zitatikiswa?
Kama ngome za Ninawi zitatikiswa zitaangukia kwenye mdomo wa mlaji.
Nahum 3:16-17
Ni wafalme wangapi wapo pale?
Wafalme waliopo pale ni wengi kama nzige.
Nahum 3:18-19
Kila mtu atakayesikia habari juu yako atafanya nini?
Kila mtu atakayesikia habari juu yako atapiga makofi kwa furaha.