2 Timothy
2 Timothy 1
2 Timothy 1:1-2
Ni kwa namna gani Paulo alikuwa mtume wa Kristo?
Paulo alikuwa mtume wa Kristo kwa mapenzi ya Mungu.
Kuna uhusiano gani kati ya Paulo na Timotheo?
Timotheo ni mtoto wa kiroho wa Paulo.
2 Timothy 1:3-5
Paulo alipomkumbuka Timotheo katika maombi, Paulo alipanga kufanya nini?
Paulo alipanga kwenda kumuona Timotheo.
Nani mwingine alikuwa na imani halisi katika familia ya Timotheo kabla ya Timotheo?
Bibi yake na Timotheo pamoja na mama yake.
2 Timothy 1:6-7
Ni roho gani Mungu alimpa Timotheo?
Mungu alimpa Timotheo roho ya nguvu na upendo na nidhamu.
2 Timothy 1:8-11
Paulo alimwambia Timotheo asifanye nini?
Paulo alimwambia Timotheo asiuonee haya ushuhuda wa Bwana
Paulo alimwambia Timotheo afanye nini?
Paulo alimwambia Timotheo ashiriki mateso kwa ajili ya Injili.
Ni kipindi gani tulipewa mipango na rehema za Mungu?
Mipango ya Mungu na rehema zake tulipewa kabla ya nyakati kuanza.
Ni kwa namna gani Mungu alithibitisha mpango wake wa ukombozi?
Mpango wa Mungu wa ukombozi ulidhihirika kwa kuja kwa mkombozi wetu Kristo Yesu.
Yesu alipokuja alifanya nini kuhusu mauti na uzima?
Yesu aliondoa mauti na kuleta uzima usio na mwisho.
2 Timothy 1:12-14
Paulo hakuionea haya injili kwa kuwa alikua na ujasiri kuwa Mungu anaweza kufanya nini kwake?
Paulo ana ujasiri kuwa Mungu anaweza kuweka yale aliyokabidhi kwa Mungu hata siku ile.
Timotheo anapaswa kufanya nini na kitu kizuri alivyopewa na Mungu?
Timotheo anatakiwa akitunze kitu kizuri alichokabidhiwa na Mungu kupitia roho mtakatifu.
2 Timothy 1:15-18
Ni nini ambacho watu wa Asia walimfanyia Paulo?
Wote waliopo Asia walimuacha.
Kwa nini Paulo alimuomba Bwana airehemu nyumba ya Onesiforo?
Paulo alimuomba Bwana airehemu nyumba ya Onesiforo kwa sababu Onesiforo alimsaidia Paulo kwa njia nyingi.
2 Timothy 2
2 Timothy 2:1-2
nini uhusiano kati ya Paulo na Timotheo?
Timothy ni mwana wa kiroho wa Paulo.
Timotheo anapaswa akabidhi ujumbe aliopewa na Paulo kwa akina nani?
Timotheo anatakiwa akabidhi ujumbe kwa watu waaminifu watakaokuwa tayari kuwafundisha wengine.
2 Timothy 2:3-7
Paulo alisema askari mzuri hatakiwi kujishughulisha na nini?
Askari mzuri hajishughulishi na shughuli za kawaida za maisha haya.
2 Timothy 2:8-10
Alipokuwa akimwandikia Timotheo, Paulo alikuwa katika hali gani ya mateso katika kuhubiri neno la Mungu?
Paulo anateseka kwa kufungwa minyororo kama mkosaji.
Ni kitu gani Paulo amesema hakifungwi minyororo?
Neno la Mungu halifungwi minyororo.
Kwa nini Paulo alivumilia haya yote?
Paulo alivumilia haya yote kwa ajili ya waliochaguliwa na Mungu ili wapate wokovi ulio katika Kristo Yesu.
2 Timothy 2:11-13
Kristo anaahidi nini kwa watakaovumilia?
Watakaovumilia watamiliki pamoja na Kristo.
Kristo anawaonya nini wale wanaomkataa?
Wale wanaomkataa Kristo, Kristo atawakataa.
2 Timothy 2:14-15
Kuhusu nini kile lazima Timothy kuwaonya watu wasiwe wagomvi?
Timothy lazima kuwaonya watu wasiwe wagomvi juu ya maneno, ambayo hayana faida yoyote
2 Timothy 2:16-18
Watu wawili waliukosa ukweli, walifundisha mafundisho yapi ya uongo?
Walifundisha kuwa ufufuo tayari umeshatokea.
2 Timothy 2:19-21
Ni kwa namna gani waamini wanapaswa kujiandaa kwa kila kazi njema?
Waamini wanapaswa kujitakasa toka kwenye matumizi yasiyo na heshima, kujiweka wakfu kwa kila kazi njema.
2 Timothy 2:22-23
Kutokana na nini Timotheo kukimbia
Timotheo ni kukimbia tamaa za ujana.
2 Timothy 2:24-26
Ni aina gani ya tabia lazima mtumishi wa Bwana awenazo
Mtumishi wa Bwana lazima kuwa mpole, na uwezo wa kufundisha, mvumilivu kwa upole kuwaelimisha wale wanaopinga yake.
Ibilisi amewafanya nini wale wasioamini?
Ibilisi amewafunga na kuwateka wale wasioamini.
2 Timothy 3
2 Timothy 3:1-4
Nini ambacho Paulo anasema kitakuja siku za mwisho?
Paulo anasema ya kuwa katika siku za mwisho kutakuwa na nyakati hatari.
Katika siku za mwisho ni vitu gani vitatu watu watavipenda kuliko kumpenda Mungu?
Siku za mwisho watu watajipenda wenyewe, kupenda pesa na kupenda anasa kuliko kumpenda Mungu.
2 Timothy 3:5-7
Nini Paulo anamwambia Timotheo kufanya kwa watu wanaoonekana kama wacha Mungu kumbe sio?
Paulo anamwambia Timotheo kujitenga mbali na watu wanaoonekana kama wacha Mungu
Ni jambo gani ambalo hufanywa na watu wasio na Mungu?
Baadhi ya watu wasio na Mungu huingia kwenye nyumba za watu na kuwashawishi wanawake wanaoongozwa na tamaa zao.
2 Timothy 3:8-9
Ni watu wa namna gani wasiomcha Mungu kama Yanne na Yambre katika agano la kale?
Hawa watu wasiomcha Mungu ni Walimu wa uongo wanasimama kuipinga kweri kama Yanne na Yambre.
2 Timothy 3:10-13
Badala ya Walimu wa uongo ni nani ambaye Timotheo amamfuata?
Timotheo alimfuata Paulo
Bwana alikuokoa Paulo kutoka kwenye nini?
Bwana alimuokoa Paulo kutoka kwenye mateso yake yote.
Ni mambo gani Paulo anasema yatatokea kwa wote walioamua kuishi maisha ya kumcha Mungu?
Paulo anasema walioamua kuishi maisha ya kumcha Mungu watateswa.
Ni mambo gani yatakuwa mabaya zaidi siku za mwisho?
Watu waovu na wadanganyifu watazidi kuwa waovu zaidi siku za mwisho.
2 Timothy 3:14-15
Ni katika kipindi gani cha maisha ya Timotheo alifahamu juu ya maandiko matakatifu?
Timotheo alifahamu juu ya maandiko matakatifu tangu alipokuwa mtoto.
2 Timothy 3:16-17
Ni kwa namna gani andiko lote limepewa kwa mwanadamu?
Kila andiko limepewa pumuzi ya uhai na Mungu
Ni kwa namna gani andiko lafaa?
Kila andiko lafaa kwa mafundisho, kuonya, kurekebisha makosa na kufundisha katika haki.
Ni nini madhumuni ya kuwafundisha watu mafundisho?
Mtu anapewa mafundisho ili awe kamili na kupewa nyenzo kwa ajili ya kutenda kazi njema.
2 Timothy 4
2 Timothy 4:1-2
Yesu Kristo atamuhukumu nani?
Yesu Kristo ni muhukumu wa walio hai na waliokufa.
Ni agizo gani lenye uzito Paulo alimpa Timotheo?
Paulo alimuagizo Timotheo ahubiri neno.
2 Timothy 4:3-5
Paulo alionya kuwa muda utakuja ambao watu watafanya nini?
Watu hawatachukuliana na mafundisho ya kweli, badala yake watasikiliza mafundisho yanayokubaliana na tamaa zao.
Ni kazi gani na huduma ambayo Timotheo alipewa kufanya?
Timotheo alipewa kazi na huduma ya uinjilisti.
2 Timothy 4:6-8
Ni muda gani katika maisha yake Paulo anasema imewadia?
Paulo anasema muda wake wa kuondoka imewadia.
Ni zawadi gani ambayo Paulo anawaambia watapewa wale wote wanaompenda Kristo?
Paulo anasema kwamba wote wanaompenda Kristo watapokea taji ya haki.
2 Timothy 4:9-10
Kwa nini Dema alimuacha Paulo?
Dema alimuacha Paulo kwa sababu aliupenda ulimwengu huu.
2 Timothy 4:11-13
Ni nani aliyekuwa mshirika wa Paulo ambaye yeye peke yake ndiye aliyebaki naye?
Ni Luka peke yake alikuwa bado yuko pamoja na Paulo.
2 Timothy 4:14-22
Paulo alisema kuwa mtu yule aliympinga yeye atalipwa kulingana na nini?
Paulo alisema kwamba mtu yule ambaye aliyekuwa akimpinga atalipwa kwa kadiri ya matendo yake.
Nani alisimama na Paulo kwa ule utetezi wake wa kwanza?
Kwa utetezi wa kwanza wa Paulo, Bwana alisimama pamoja na Paulo.